Sababu kuu zenye Mantiki zilizowafanya na zinazowafanya Wayahudi wengi Wasimuamini Yesu Kristo

kiila mtu na tafsiri yake mkuu huo n mtazamo wako masela wala hatujengi chuki na imani yako itakuponya.hv ushawahi kujiuliza tunaishi kwa imani?ushawahi kumwona mungu?au kuona roho? je ushawahi kuuona upepo upepo una rangi gani?au umeme uko vp.japo hvyo vitu vipo c unaamini hvyo vitu vipo japo hujaona bac ishi kwa kuamini mzee baba narudia tena tunaishi kwa imani na kila mtu na tafsiri yake.cjui kaka yangu na mtani wangu anasemaje wajuzi wa mambo watakutafsiria
 
Vizuri ngoja tuone kati yangu na wewe nani mwenye ndogo. Usije kukimbia hoja.

Uyahudi ni dini, hapa tuko sawa. Hakuna taifa lililo itwa Uyahudi. Taifa lipo lililo itwa "Israili". Kwa mara ya kwanza liliundwa na wale ndugu wawili, mmoja akiwa mtoto wa nabii Suleyman mwisho likaja kupotea.

Kisha baadae wakaja Waka Wazayuni kwa msaada wa Waingereza wakaunda Taifa hili liitwalo Israeli Leo hii.

Unaongelea Historia ya kidato Cha nne, historian ambayo haina "Chain" ulivyo anza kwa mbwembwe nikajua walau unaweza kunusa historian kumbe marejeo yako ni Historian ya kidato cha nne. Kijana hata balehe ya kwanza ya elimu huja balehe.

Safi kabisa, unaweza kunithibitishia ya kuwa hapa andiko lako limemaanisha dini au taifa ? Kama dini ushahidi uko wapi na kama taifa kadhalika ushahidi uko wapi ? Yaani andiko lako haliko wazi.

Unaona ulivyopopoma.

Suleiman hakuwa na watoto Wawili, Suleiman mwenyewe ni Myahudi.

Pili, usiongee mambo usiyoyajua, Uzayuni sio utaifa wala sio udini, Uzayuni ni Movements/vuguvugu lenye sera za kurudisha mamlaka na utawala wa Kiyahudi.
Zionism sio utaifa wala sio Dini.

Israel ni taifa na utaifa.
Uyahudi ni taifa na ni Dini.

Kama hujui Historia ya Waisrael ukae chonjo.
Elewa kuwa Israel ilikuwa imegawanyika, kulikuwa na utawala wa Kaskazin, na utawala wa kusini.
Lakini sina haja kukuelezea mambo hayo Kwa sababu hata chimbuko la Wayahudi hulijui.

Hapohapo Kwa Wayahudi kuna taifa lilizaliwa linaitwa Wasamaria, lakini Kwa vile huna ujualo utasema usamaria sio taifa.

Esta 2:5
5. Mjini Susa, palikuwa na mtu mmoja Myahudi, jina lake Mordekai, mwana wa Yairi mwana wa Shimei, mwana wa Kishi wa kabila la Benyamini.

Esta 3
4Kila siku walimshauri aache tabia hiyo, lakini Mordekai hakukubaliana nao. Alikataa kufanya hivyo kwa madai kwamba yeye ni Myahudi na kwa hiyo hawezi kumsujudia Hamani. Basi, wakamwarifu Hamani ili waone kama ataivumilia tabia ya Mordekai. 5Hamani aliwaka hasira alipojua kwamba Mordekai hamwinamii wala hamsujudii. 6Tena alipogundua kuwa Mordekai alikuwa Myahudi, aliamua kwamba kumwadhibu peke yake haitoshi. Basi akala njama kuwaangamiza Wayahudi wote, watu wa ukoo wa Mordekai, katika utawala wa mfalme Ahasuero.

7Katika mwaka wa kumi na mbili wa utawala wa mfalme Ahasuero, mnamo mwezi wa kwanza uitwao Nisani, Hamani aliagiza kura (yaani Purimu) ifanywe kupata siku na mwezi ambapo angetekeleza njama zake. Basi, kura ikaangukia siku ya kumi na nne ya mwezi wa kumi na mbili uitwao Adari.
8Basi, Hamani akamwambia mfalme: “Wapo watu wa taifa fulani walioko kila mahali katika utawala wako, nao wako katika kila mkoa. Watu hao wana sheria zilizo tofauti kabisa na za watu wengine. Isitoshe, wao hawazitii sheria zako, kwa hiyo haikufaidi chochote kuwavumilia.

9“Ukipenda, ewe mfalme, amri na itolewe, watu hawa waangamizwe. Nami naahidi, kama utaamuru hivyo, nitatoa kiasi cha kilo 10,000 za fedha ziwekwe katika hazina ya mfalme.”
10Mfalme akaivua pete yake, ambayo ilitumiwa kupigia mhuri matangazo, akampa adui wa Wayahudi Hamani mwana wa Hamedatha wa uzao wa Agagi. 11Ndipo mfalme akamwambia Hamani, “Umepewa watu wote na hizo fedha, tumia upendavyo.”

12Basi, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza, Hamani aliwaita makatibu wote wa mfalme, akawapa tangazo ambalo alitaka litafsiriwe kwa kila lugha na kila namna ya maandishi katika utawala huo, halafu nakala zisambazwe kwa watawala wote, wakuu wa mikoa yote, na viongozi wa makabila – kufuatana na lugha zinazotumika kwao. Tangazo hilo lilitolewa kwa jina la mfalme Ahasuero, na kupigwa mhuri kwa pete yake. 13Matarishi walizipeleka nyaraka hizo kwa kila mkoa katika utawala huo. Tangazo hilo lilisema kwamba kwa siku moja tu, yaani siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili uitwao Adari, Wayahudi wote – vijana kwa wazee, wanawake kwa watoto, wote lazima wauawe, waangamizwe na kufutiliwa mbali, na mali zao zote zichukuliwe. 14Taarifa hiyo ilitakiwa iandikwe hadharani katika kila mkoa, ili kila mtu ajiandae kwa ajili ya siku hiyo.

15Kwa amri ya mfalme, tangazo hili lilitolewa katika mji mkuu wa Susa, nao matarishi wakalitangaza katika mikoa yote. Mfalme na Hamani walikaa chini kunywa wakati watu mjini Susa wanafadhaika.

Kabla hujaanza kuropoka vitu unapaswa kufanya uchunguzi wako VIZURI.

Nitakupa mfano mdogo, katika kabila la Wapare, wapare kama Wapare wao hujijua kama Waasuu"Vaasu" Lugha ya ni "Chasu"
Ila Kwa sasa wanaitwa "Wapare" Kutokana na matukio ya kihistoria.

Sasa nakuuliza, MTU akikuambia Wapare ni kabila wewe utakataaa Kwa sababu unajua jina lao jingine waitwalo Vaasu?

Au hao waisrael wakiitwa Wayakobo utasema hakuna taifa kama Hilo Wakati Kwa jina jingine Waisrael ndio haohao Wayakobo?

Elimu ni kitu muhimu Sana
 
Utamjua Yesu kuliko Wayahudi?
Utaijua Bible kuliko walioiandika na inayowazungumzia?

Hizo hoja niza Wayahudi, hivyo ukija ujibu hoja moja Baada ya nyingine.
Mimi nitakuwa upande wa Wayahudi katika Mjadala
Utamjua Yesu kuliko Wayahudi?
Utaijua Bible kuliko walioiandika na inayowazungumzia?

Hizo hoja niza Wayahudi, hivyo ukija ujibu hoja moja Baada ya nyingine.
Mimi nitakuwa upande wa Wayahudi katika Mjadala huu

Anaandika, Robert Heriel
Kuhani.

Leo Taikon atajadili sababu zinazopelekea wayahudi wengi kutokumuamini Yesu Kristo Kama Masihi wao na waulimwengu.

Andiko hili lijadiliwe Kwa Hoja zisizo na mihemko ya kidini. Kama unajijua Akili yako imefungwa fungwa hii mada haitakuhusu.

Hivi uliwahi kujiuliza ni Kwa nini Wayahudi hawamuamini Yesu Kristo? Yaani Kwa nini wamuamini Musa, Daudi, yona, Daniel, Isaya, Ezra, Joshua, n.k lakini Kwa nini hawataki kumuamini Yesu Kristo?

Embu nawe Fikiria hapo. Kumbuka hata huyo Yesu naye NI Myahudi.

Je, ni Yesu pekeake aliyekataliwa na Wayahudi au kuna manabii Masihi wengine waliokataliwa n mayahudi?
Ikiwa wapo je nini sababu ya wao kukataliwa? Nisirefushe andiko.

Twende sasa!

Wayahudi wanasababu kadhaa za kutokumzingatia Yesu kama Masihi au Nabii aliyetabiriwa katika maandiko kaa sababu kuu zifuatazo;

1. Yesu Mnazareth Hakutimiza Unabii hivyo anakosa vigezo vya kuwa Masihi mtabiriwa.
Hapa kuna mambo ambayo Masihi aliyetabiriwa alipaswa kuyatimiza Siku atakapokuja. Mambo hayo ni pamoja na;

a). KUSHUSHA UTAWALA WA MUNGU NA KUKOMBOA WANADAMU
Masihi aliyetabiriwa moja ya majukumu yake akija ni kukomboa Wanadamu na kushusha utawala wa Mungu. Wayahudi hawamuamini Yesu Wa Nazareth Kwa sababu hakutimiza Jambo Hilo. Hakuushusha utawala wa Mungu na wala hakumkomboa Mwanadamu.

Hii ni Kwa sababu mpaka hapa tunapozungumza Bado Dunia haijakombolewa, madhambi ni mengi, na utawala wa Shetani ndio umetamalaki.

Soma utabiri wa Isaya juu ya Masihi atakayekuja kisha linganisha, je Yesu Mnazareth analingana na utabiri huo;

Isaya 9:6
6 . Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto wa kiume;
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu,
Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.

Ukichambua Unabii huo sentensi Kwa sentensi, je Yesu Mnazareth anatimiza Unabii huo. Embu tuone, "Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;"
Je Yesu alikuwa na uwezo wa kifalme began mwake? Je alitimiza vigezo vya kuitwa Mfalme? Labda Kwa vile hapa Tanzania kizazi cha sasa hakijaongozwa na wafalme. Lakini tunaweza kuchukulia mfano WA mamlaka ya Rais.

Je Yesu Mnazareth alikuwa anauwezo wa kirais, yaani mamlaka kama tuyaonayo Kwa Rais? Zingatia Mfalme ni zaidi ya Rais Kwa mambo mengi.

Ukisoma maandiko Yesu hakuwa na uwezo wowote wa Kifalme, alikuwa ni nabii kama walivyomanabii wengine.
Hivyo Sifa hii hakuwa nayo.
"Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu,
Baba wa Milele, Mfalme wa Amani
"

Je, Yesu Mnazareth alitimiza Unabii wa kuwa na Sifa ya kuitwa Mungu mwenye nguvu? Je Yesu alileta Amani? Maana Unabii unasema ataitwa Mfalme wa Amani.

Je ni kweli Yesu alileta Amani Duniani? Jibu ni Hapana, Yesu Mnazareth hakuleta Amani. Msikilize Yesu mwenyewe;

Mathayo 10:34 BHN​

“Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga.​

Yesu hakuleta Amani Duniani isipokuwa Upanga. Hivyo anakosa kigezo cha Nabii aliyetabiriwa na manabii wa zamani.

Kwa tuliosoma Histori ya Ulimwengu. Ukristo ndio dini pekee iliyoua Watu wengi Duniani katika kuueneza.
Watu wengi wameuawa Kwa sababu ya Kristo au Kwa jina la Kristo. Hivyo hakuwa Mfalme wa Amani Bali alikuwa Mfalme wa machafuko.

Ukombozi uliolengwa na manabii waliotabiri Ujio wa Masihi ulikuwa ukombozi wa Kimwili. Lakini Yesu hakuja kukomboa yeyote Kimwili. Hiyo ni hoja inayofuata baadaye

b) MASIHI LAZIMA AZALIWE KATIKA UKOO WA DAUDI LAKINI YESU HAKUZALIWA KATIKA UKOO WA DAUDI.

Wayahudi wanamkataa Yesu Kwa sababu yupo Kinyume na Unabii wa Masihi aliyetabiriwa. Ndio maana wao wanamsubiri huyo Masihi Kwa jinsi vitabu vyao vinavyoeleza.

Maandiko yanaonyesha kuwa Yesu hakuwa Uzao wa DAUDI. Hii ni Kutokana na sababu zifuatazo;

I) Yesu alizaliwa pasipo na Baba.
Maandiko yanaeleza kuwa Yesu alizaliwa Kwa Njia ya Roho mtakatifu. Hana Baba wa kibinadamu. Jambo ambalo linampotezea Sifa ya kuwa Masihi aliyetabiriwa.

Wayahudi wanaeleza kuwa Masihi aliyetabiriwa angezaliwa kikawaida kama binadamu wengine tena angetoka katika Uzao WA Daudi. Yaani Baba yake lazima awe katika ukoo wa Daudi (Daudi mtoto wa Year).

Mwanzo 49:10 BHN​

“Fimbo ya kifalme haitatoka kwa Yuda, wala bakora ya utawala miguuni pake, mpaka atakapofika yule ambaye ni yake; ambaye mataifa yatamtii.​

Soma Unabii wa Isaya;
ISAYA 11
1 Kutatokea chipukizi katika kisiki cha Yese,
tawi litachipua mizizini mwake.
2Roho ya Mwenyezi-Mungu itakaa kwake,
roho ya hekima na maarifa,
roho ya shauri jema na nguvu,
roho ya ujuzi na ya kumcha Mwenyezi-Mungu.
3Atafurahia kumcha Mwenyezi-Mungu.
Hatahukumu kadiri ya mambo ya njenje,
wala kuamua kufuatana na yale anayosikia.
4 Atawapatia haki watu maskini,
atawaamulia sawasawa wanyonge nchini.
Kwa neno lake ataiadhibu dunia,
kwa tamko lake atawaua waovu.
5 Haki itakuwa kama mkanda wa kujifunga,
uaminifu utakaa naye kama mkanda kiunoni.
6 Mbwamwitu ataishi pamoja na mwanakondoo,
chui watapumzika pamoja na mwanambuzi.
Ndama na wanasimba watakula pamoja,
na mtoto mdogo atawaongoza.
7Ngombe na dubu watakula pamoja,
ndama wao watapumzika pamoja;
na simba atakula majani kama ng'ombe.
8Mtoto mchanga atacheza kwenye shimo la nyoka
mtoto ataweza kutia mkono shimoni mwa nyoka wa sumu.
9 Katika mlima mtakatifu wa Mungu
hakutakuwa na madhara wala uharibifu.
Maana kumjua Mwenyezi-Mungu kutaenea pote nchini,
kama vile maji yajaavyo baharini.
10 Siku ile chipukizi wa Yese atakuwa ishara kwa mataifa; mataifa yatamtafuta na makazi yake yatatukuka.
11Siku hiyo, Bwana ataunyosha mkono wake tena kuwarejesha watu wake waliosalia huko Ashuru, Misri, Pathrosi, Kushi, Elamu, Shinari, Hamathi na sehemu za pwani

Unabii huu unaeleza Sifa za Masihi atakayekuja, yaani sharti atokee Katika ukoo wa Daudi. Jambo ambalo Yesu Mnazareth maandiko yanaeleza kuwa hajatokea kwani hakuwa na Baba.

Hata Mariam mamaye Yesu angetokea ukoo wa Daudi bado isingemsaidia lolote Yesu kwani kiunabii au kimaandiko Uzao unatoka Kwa Baba.

Hoja hii inaungwa mkono na Wayahudi wengi na kufikia hitimisho kuwa Yesu sio Masihi aliyetabiriwa. Yesu hakuwa na Baba, huyo Yusufu ambaye ukoo wake umetajwa kwenye Biblia hakuwa Baba mzazi wa Yesu. Ndio maana alitaka kumkimbia Mariam.

Wayahudi wanadai kuwa Masihi angezaliwa kikawaida, Kwa kuwa Na Baba mzazi na Mama mzazi na sio kutumia njia ya miungu kutunga mimba. Jambo ambalo Wayahudi wanaliita ni dhana ya upagani wa Kirumi.

C) MASIHI LAZIMA AWARUDISHE WAYAHUDI WOTE WALIOTAWANYIKA DUNIANI WARUDI ISRAEL.
Yesu Mnazareth hakutimiza hilo. Wayahudi walichukuliwa uhamishoni huku na Huko. Na wapo wengine waliobakizwa Uyahudini.

Masihi aliyetabiriwa moja y majukumu yake ilikuwa kuwakusanya na kuwarejesha waisrael wote waliotawanyika warudi nyumbani Yesu hakufanya hilo. Hivyo anakosa Sifa za kinabii za Masihi aliyetabiriwa

ISAYA 11:
10 Siku ile chipukizi wa Yese atakuwa ishara kwa mataifa; mataifa yatamtafuta na makazi yake yatatukuka.
11. Siku hiyo, Bwana ataunyosha mkono wake tena kuwarejesha watu wake waliosalia huko Ashuru, Misri, Pathrosi, Kushi, Elamu, Shinari, Hamathi na sehemu za pwani.

Yesu Mnazareth hakumrejesha hata myahudi mmoja Israel. Hivyo anakosa Sifa za kinabii za Masihi.

Wakristo wanadai Yesu Mnazareth atatimiza hayo kwenye Ujio wa Pili Wakati upande Kwa Wayahudi na vyanzo vya Kiyahudi vinaonyesha kuwa MASIHI atatimiza utume wake Moja Kwa Moja. Katika Biblia hasa ya Unabii wa Masihi aliyetabiriwa hakuna dhana "Masihi Kurudi/kuja Mara yapili.

d) MASIHI ATAKUJA KUKOMESHA MAGONJWA, VITA, TAABU, NJAA N.K
Masihi aliyetabiriwa na manabii moja ya Kazi yake akija atakomesha magonjwa, Vita, Taabu, njaa na majanga mengine. Lakini Yesu Mnazareth hakukomesha chochote Kati ya hivyo kwani mpaka hivi leo, Mambo hayo yapo.
Hivyo anakosa Sifa za Masihi aliyetabiriwa.

Hoja ya kusema kuwa Yesu Mnazareth alikuja Kwa mambo ya ufalme wa Kiroho inazidi kumuondoa Yesu kwenye Sifa za Masihi aliyetabiriwa.

Labda tuseme, Yule Aliyetabiriwa na Yesu Mnazareth kuwa atakuja ambaye Wakristo wanamuita Roho mtakatifu ndiye Masihi ambaye kwa HAKIKA bado hajaja.

E) Masihi hataleta mambo ya utatu mtakatifu ambayo Kwa Torati ni Shirki, ibada za Sanamu.
Masihi ataleta ufalme wa Mungu, Haki yake, na utawala wake. Ataleta Amani Duniani. Hatakuwa sehemu ya Mungu, Ila atakuwa ni sehemu ya Uzao wa DAUDI. Utatu mtakatifu pekee yake unamuondoa Yesu Mnazareth katika Sifa za Masihi aliyetabiriwa na vitabu vya Kale.

Hao ni Wayahudi wanavyomchukulia Myahudi mwenzao yaani Yesu Kristo.

Maswali ambayo tunatakiwa tujiulize;

1. Ikiwa Yesu alitoka mbinguni, Kwa nini hakuandaa makao ya Watu wake Kabla hajaja Duniani kuwakomboa?
Badala yake Akaja Duniani kwanza ndipo akaenda kuandaa Makao. Hii maana yake ni nini?

Mungu aliumba makazi, Dunia ndipo akaumba MTU. Nuhu alijenga Safina ndipo akawakomboa Watu wake. Iweje Yesu aanze na ukombozi kwanz alafu ndio akaandae Makao?

2. Je Yesu na Ukristo, Yesu kama mwenye uwezo na Nabii. Kabla hajaja hakuona hatari ya Ujio wake kuwa mamilioni ya Watu watauawa kisa jina lake.

Yaani watalazimishwa kukubali jina lake kilazima hata kama hawataki? Kwa maana mpaka sasa jina la Yesu ndio linashikilia nafasi ya Kwanza Kwa Watu kuuawa ili tuu Watu waupokee Ukristo au waukatae Ukristo.

3. Iweje Yesu Mnazareth alishindwa kutimiza kazi yake Kwa miaka 33 aliyokaa Duniani mpaka awape majukumu Wanafunzi wake?

Je, hakuona kuwa kuna upotoshaji ungeweza kujitokeza Wakati ambapo hatokuwepo?
Ikiwa alilisha Watu zaidi ya elfu tano Kwa mikate mifano na samaki Wawili, akafufua Watu, na miujiza mingine, kumaanisha alikuwa na uwezo.

Ni kipi alishindwa kuhakikisha kila binadamu anayezaliwa automatically, amjue Mungu na habari zake pasipo kufundishwa na yeyote, ili kuepusha kile kiitwacho uongo na habari zake kuingiziwa hadithi za Uongo. Huo ungekuwa muujiza mzuri na wala asingewapa Wanafunzi wake kazi ya Kutangaza habari zake na habari za Mungu.

4. Yesu aliwaagiza Wanafunzi wake kuhubiri Injili. Je hakujua kuwa Miaka na miaka itapita, Vizazi na Vizazi vitapita.

Je, Vizazi ambavyo havikuwepo Wakati wake(Wakati WA Yesu) Sisi tukiwa miongoni mwa Vizazi hivyo, tunapata mamlaka ipi na uthibitisho upi kuwa Injili tuliyonayo ndio Ile aliyoitoa Yesu? Je, tutatumia kipimo kipi kuthibitisha ukweli WA kile tukisemacho?

5. Ikiwa lengo la Kufa Kwa Kristo ni kuwakomboa wanadamu na kuifia dhambi. Je kama dhambi ilikomeshwa na Kifo cha Yesu, ni kwanini Watu wanaendelea kutenda dhambi?

6. Swali la mwisho, ni Jambo Gani linalopelekea Wakristo kuamini Yesu Mnazareth ndiye Kristo/Masihi ilhali hajatimiza robo tatu ya Masihi aliyetabiriwa na manabii?

Kwa mfano, swali alilouliza Yohana Mbatizaji kuwatuma Wanafunzi wake wakamuulize Yesu kuhusu, Je Ni yeye Masihi au wamsubiri mwingine na jibu la Yesu kuwa viwete wanapona, vipofu wanatembea, viziwi wanasikia, na wafu wanafufuliwa. Je hiyo ndio ilikuwa misheni kuu ya Yesu?

Vipi kuhusu kuwarejesha Wayahudi Israel, vipi kuhusu yeye kuwa Mfalme na kuleta Amani na Haki Duniani, vipi kuhusu kuadhibu na kuhukumu?

7. Je Yesu anapowaambia Wanafunzi wake kuwa atarudi tena, je anaongea hayo Kwa kutimiza Unabii upi wa Masihi?

Maana hakuna sehemu Huko Nyuma ambayo ilitabiriwa ataondoka kisha atarudi tena. Ikiwa ndiye aliyetabiriwa, hiyo dhana aliitolea wapi?

Karibuni kwenye mjadala.
Mihemko hapa haitakuwa sehemu yake.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Myahudi ni mtu yeyote ambaye mama yake alikuwa Myahudi mfano Mariam kwa mwanae Yesu,japokuwa Biblia ya Kiebrania haitaji kwa wazi mahali popote kwamba asili ya uzazi inapaswa kutumiwa
Au Myahudi ni mtu yeyote ambaye amepitia mchakato rasmi wa kubadili kuenda Uyahudi,Je! Yesu alikuwa Myahudi kwa kikabila, au mamake alikuwa Myahudi? Yesu aliweka wazi kwa Wayahudi wa siku Zake, watu wake wa kimwili na kabila na dini yao.

Agano Jipya hutangaza waziwazi ukabila wa Kiyahudi wa Yesu. "Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu" (Mathayo 1: 1). Ni dhahiri kutoka vifungu kama Waebrania 7:14, "Kwa maana ni wazi kwamba Bwana wetu alitoka kwa Yuda," kwamba Yesu alitoka kwa kabila la Yuda, ambalo tunapata jina "Myahudi." Na nini kuhusu Maria, mama ya Yesu? Katika ukoo wa kizazi katika Luka sura ya 3, tunaona wazi kwamba Maria(mariam) alikuwa kizazi cha moja kwa moja cha Mfalme Daudi ambacho kilimpa Yesu haki ya kisheria ya kuinua kiti cha enzi cha Kiyahudi na hamna shaka kwamba Yesu alikuwa Myahudi kwa kikabila.
UNAPOSEMA 1. Yesu Mnazareth Hakutimiza Unabii hivyo anakosa vigezo vya kuwa Masihi mtabiriwa.

Kwanza Masihi inatoka kwa neno la Kiebrania mashiach na inamaanisha "aliyetiwa Wakfu" ama "mteule."
Neno sawia la Kigiriki ni Christos ama kwa Kiingereza, Christ. Jina "Yesu Kristo" ni sawa na "Yesu Masihi." Katika nyakati za Biblia, kupaka mtu mafuta ilikuwa ishara kuwa Mungu alikuwa akimtakasa ama kumtenga mtu huyo kwa ajili ya kutekeleza jukumu fulani. Kwa hivyo, "aliyetiwa wakfu" alikuwa mtu aliyekuwa na kusudi maalum, kusudi lililoamuriwa na Mungu.

Katika Agano la Kale, watu walitiwa wakfu kwa majukumu ya nabii, kuhani na mfalme. Mungu alimwambia Elia amtie mafuta Elisha ili awe nabii wa Isreaeli ( I Wafalme 19:16). Haruni aliwekwa wakfu kama kuhani mkuu wa kwanza wa Israeli ( Mambo ya Walawi 8:12). Samweli aliweka wakfu Sauli na Daudi kuwa Wafalme wa Israeli (I Samweli 10:1; 16:13). Wanaume hawa wote walikuwa na majukumu yaliyo "tiwa wakfu." Lakini Agano la Kale lilitabiri kuwa Mkombozi ajaye, aliyechaguliwa na Mungu kukomboa Israeli (Isaya 42:1; 61:1-3). Mkombozi huyu alijulikana na Wayahudi kama Masihi.

DAI LA a). HAKUSHUSHA UTAWALA WA MUNGU NA KUKOMBOA WANADAMU si kweli
Bwana Yesu aliwajibu wayahudi kwamba(luka 17:20-21) "20 Siku moja, Mafarisayo walipomwuliza Yesu Ufalme wa Mungu utakuja lini, aliwajibu hivi: “Ufalme wa Mungu hauji kwa kuone kana, 21 wala watu hawatasema, ‘Huu hapa’ au ‘Ule kule’ kwa maana Ufalme wa Mungu umo ndani yenu.”

Kupitia jibu la Yesu kwa mafarisayo ni kwamba ufalme wa Mungu upo kati yao lkn hawakuuona bali walizidi kusubiri mbeleni,na katika mawazo yao walidhani ufalme wa Mungu ni kuifanya Izrael kuwa taifa kubwa duniani,na walikuwa na mioyo migumu na Yesu aliongea nao kwa Mifano lkn bado hawakuelewa.Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwamba(luka 8:10)“Ninyi mmejaliwa kufahamu siri za Ufalme wa Mungu, lakini kwa wengine nazungumza kwa mifano ili, ‘Kuangalia waangalie lakini wasione, kusikia wasikie, lakini wasielewe.’
Hapa Yesu alikuwa anajiongelea yeye mwenyewe kwamba yupo kati yao akizifanya kazi za ufalme wa Mungu ambao yeye (Yesu) kauleta huku wakiangalia lkn hawaoni na wanamskia sauti yake lkn hawamwelewi,tena wakawa wanamshtumu kuwa anatumia nguvu za giza akawajibu kwamba (mathayo 12:28)

"Lakini kama ninatoa pepo kwa nguvu za Roho wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umekwisha kuwafikia" Hivyo nguvu za roho mtakatifu na kazi zake za kutoa maradhi na mapepo nguvu hizo zilijidhihirisha kwa Yesu na zilibainisha kuwa ufalme wa Mungu umekuja na wenye nguvu ndio watakaouteka(mathayo 11:12)Na hapo Yesu hakumaanisha nguvu za mwili bali nguvu ya nia na Imani; Lakini Wayahudi walidumu kutoamini na kumkataa Yesu, na Bwana Yesu akwaambia Neno gumu sana. “Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake. [Mathayo 21:43].”

Hilo taifa lingine, ni taifa la waaminio, wale ambao wana nguvu ya nia na Imani katika Kristo Yesu Mwana wa Mun

Agano Jipya hutangaza waziwazi ukabila wa Kiyahudi wa Yesu. "Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu" (Mathayo 1: 1). Ni dhahiri kutoka vifungu kama Waebrania 7:14, "Kwa maana ni wazi kwamba Bwana wetu alitoka kwa Yuda," kwamba Yesu alitoka kwa kabila la Yuda, ambalo tunapata jina "Myahudi." Na nini kuhusu Maria, mama ya Yesu?

Katika ukoo wa kizazi katika Luka sura ya 3, tunaona wazi kwamba Maria(mariam) alikuwa kizazi cha moja kwa moja cha Mfalme Daudi ambacho kilimpa Yesu haki ya kisheria ya kuinua kiti cha enzi cha Kiyahudi na hamna shaka kwamba Yesu alikuwa Myahudi kwa kikabila.

UNAPOSEMA 1. Yesu Mnazareth Hakutimiza Unabii hivyo anakosa vigezo vya kuwa Masihi mtabiriwa.
Kwanza Masihi inatoka kwa neno la Kiebrania mashiach na inamaanisha "aliyetiwa Wakfu" ama "mteule."
Neno sawia la Kigiriki ni Christos ama kwa Kiingereza, Christ. Jina "Yesu Kristo" ni sawa na "Yesu Masihi." Katika nyakati za Biblia, kupaka mtu mafuta ilikuwa ishara kuwa Mungu alikuwa akimtakasa ama kumtenga mtu huyo kwa ajili ya kutekeleza jukumu fulani. Kwa hivyo, "aliyetiwa wakfu" alikuwa mtu aliyekuwa na kusudi maalum, kusudi lililoamuriwa na Mungu.Katika Agano la Kale, watu walitiwa wakfu kwa majukumu ya nabii, kuhani na mfalme. Mungu alimwambia Elia amtie mafuta Elisha ili awe nabii wa Isreaeli ( I Wafalme 19:16).

Haruni aliwekwa wakfu kama kuhani mkuu wa kwanza wa Israeli ( Mambo ya Walawi 8:12). Samweli aliweka wakfu Sauli na Daudi kuwa Wafalme wa Israeli (I Samweli 10:1; 16:13). Wanaume hawa wote walikuwa na majukumu yaliyo "tiwa wakfu." Lakini Agano la Kale lilitabiri kuwa Mkombozi ajaye, aliyechaguliwa na Mungu kukomboa Israeli (Isaya 42:1; 61:1-3). Mkombozi huyu alijulikana na Wayahudi kama Masihi.
DAI LA a). HAKUSHUSHA UTAWALA WA MUNGU NA KUKOMBOA WANADAMU si kweli
Bwana Yesu aliwajibu wayahudi kwamba(luka 17:20-21) "20 Siku moja, Mafarisayo walipomwuliza Yesu Ufalme wa Mungu utakuja lini, aliwajibu hivi: “Ufalme wa Mungu hauji kwa kuone kana, 21 wala watu hawatasema, ‘Huu hapa’ au ‘Ule kule’ kwa maana Ufalme wa Mungu umo ndani yenu.”

Kupitia jibu la Yesu kwa mafarisayo ni kwamba ufalme wa Mungu upo kati yao lkn hawakuuona bali walizidi kusubiri mbeleni,na katika mawazo yao walidhani ufalme wa Mungu ni kuifanya Izrael kuwa taifa kubwa duniani,na walikuwa na mioyo migumu na Yesu aliongea nao kwa Mifano lkn bado hawakuelewa.Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwamba(luka 8:10)“Ninyi mmejaliwa kufahamu siri za Ufalme wa Mungu, lakini kwa wengine nazungumza kwa mifano ili, ‘Kuangalia waangalie lakini wasione, kusikia wasikie, lakini wasielewe.’
Hapa Yesu alikuwa anajiongelea yeye mwenyewe kwamba yupo kati yao akizifanya kazi za ufalme wa Mungu ambao yeye (Yesu) kauleta huku wakiangalia lkn hawaoni na wanamskia sauti yake lkn hawamwelewi,tena wakawa wanamshtumu kuwa anatumia nguvu za giza akawajibu kwamba (mathayo 12:28)

"Lakini kama ninatoa pepo kwa nguvu za Roho wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umekwisha kuwafikia" Hivyo nguvu za roho mtakatifu na kazi zake za kutoa maradhi na mapepo nguvu hizo zilijidhihirisha kwa Yesu na zilibainisha kuwa ufalme wa Mungu umekuja na wenye nguvu ndio watakaouteka(mathayo 11:12)Na hapo Yesu hakumaanisha nguvu za mwili bali nguvu ya nia na Imani; Lakini Wayahudi walidumu kutoamini na kumkataa Yesu, na Bwana Yesu akwaambia Neno gumu sana. “Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake. [Mathayo 21:43].”

Hilo taifa lingine, ni taifa la waaminio, wale ambao wana nguvu ya nia na Imani katika Kristo Yesu Mwana wa Munngu. [1 Petro 2:9,10]. Ambao ni wazao halisi wa Ibrahimu kwa njia ya Imani ambao ni Wakristo walio warithi sawasawa na ahadi. [Wagalatia 3:29]. Wayahudi wenye mioyo migumu yenye kutoamini walikatwa katika ufalme na mahali pao ikachukuliwa na wamataifa wenye kuamini, hivyo na wewe uliye katika ufalme usijivune pia usije katwa kama wao. [Warumi 11:20].

Yesu aliwaagiza wanafunzi wake wautangaze ufalme wa Mungu, kuutangaza ufalme wa Mungu ni kumtangaza Yesu kwa nguvu za Roho Mtakatifu na kupooza watu maradhi yao. [Luka 9:2]. Na Mitume waliutangaza ufalme wa Mungu kwa nguvu na kuponywa maradhi kiasi cha Wayahudi na Serikali ya Herode ikatetemeka na Herode akatafuta kumwona Yesu. [aya 7-9]. Na kutangaza ufalme wa Mungu ni kuhubiri Injili. [Luka 9:6]. Ambayo inawapa watu toba na msamaha wa dhambi. [Marko 1:15; Mdo 5:31].

Yesu alisema, “Akawaambia, Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia; maana kwa sababu hiyo nalitumwa. [Luka 4:43].” Mitume walimshuhudia pia kwamba. “habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye. [Matendo ya Mitume 10:38].”

Habari njema ya Ufalme maana yake ni INJILI YA UFALME, na Biblia inasema, “Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.” [Warumi 1:16]. Hivyo Injili inahusika na kila nafsi kuanzia Myahudi na Mmataifa, hakuna injili mbili, ni ile ile habari njema ambayo ilitufanya wawili kuwa umoja kwa kubomoa kiambaza cha kati kinachotutenga. [Waefeso 2:14].” Ni uweza wa Mungu huletao wokovu na uponyaji, na tunaupata uwezo huo ndani yetu kwa njia ya IMANI, maana pasipo Imani haiwezakani kumpendeza Mungu. [Waebrania 11:6].

Mitume baada ya Yesu kuondoka walihubiri sana ufalme huu, maandiko yafuatayo yanashuhudia hilo. “Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake. [Matendo ya Mitume 8:12].” “Wakiisha kuagana naye siku, wakamjia katika nyumba aliyokaa, watu wengi sana, akawaeleza kwa taratibu na KUUSHUHUDIA UFALME WA MUNGU, akiwaonya MAMBO YAKE YESU, kwa maneno ya sheria ya Musa na ya manabii, tangu asubuhi hata jioni. AKIHUBIRI HABARI ZA UFALME WA MUNGU, NA KUYAFUNDISHA MAMBO YA BWANA YESU KRISTO, kwa ujasiri mwingi, asikatazwe na mtu. [Matendo ya Mitume 28:23,31].

Hivyo kuhubiri Ufalme wa Mungu bila mambo yake Yesu ni kuhubiri Injili tupu isiyo okoa, maana hakuna wokovu katika mwingine isipo kuwa Bwana Yesu. [Mdo 4:12]. Maana Yesu ndiye asili yote ya ufalme wa Mungu. Kwahiyo ukihubiri fundisho lolote lisilo kwa jinsi ya Kristo hiyo itakuwa ni Injili nyingine, na mwisho ni kujipatia laana. [Wagalatia 1:8,9].

Na Ufalme wa Mungu umegawanyika mara mbili ingawa ni mmoja, ambao ni.
1. Ufalme wa neema
2. Ufalme wa utukufu

Ufalme wa Neema.

Ni utawala wa Neema katika mioyo ya waumini kwa njia ya Imani, utawala huu upo duniani ndani ya watu kwa njia ya Imani na ujazo wa Roho.[1 Yohana 3:24,4:13]. Na kiti cha enzi cha Mungu, kiti cha neema kimeondolewa pazia la kutukinga, hivyo wote wanaweza kumwendea Mungu moja kwa moja kwa ujasiri kwa damu ya Yesu mpatanishi ili wapate neema na rehema kwa mahitaji. [Waebrania 4:16]. Ufalme huu unapaswa kutangazwa kwa nguvu zote, kwa sauti kuu, maana ndio Injili ya Milele. [Ufunuo 14:6,7]. Na siri ya kuingia katika ufalme wa Neema ni kumwamini Yesu na kuzaliwa mara ya pili kwa maji na Roho. Yesu anasema,Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. [Yohana 3:5].

Na Ufalme huu watu wanapaswa kuufurahia kuanzia sasa, Mtume anasema, “Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.[ Warumi 14:17].” Haki, Amani na furaha katika Roho Mtakatifu, hayo mambo si ya baadae, yaani ‘ya wakati ujao’ ni mammbo tunayopaswa kuwa nayo sasa. Haki tayari tunayo kwa njia ya Imani, Amani tayari tumeshaachiwa, na furaha tunayo tayari kwa njia ya ujazo wa Roho Mtakatifu ndani yetu. [Tazama, Warumi 3:24, Yohana 14:27; Mdo 9:31]. Kama hujisikii kuwa na vitu hivi sasa, jipeleleze na fanya matengenezo.

Ufalme wa Utukufu

Huu utawala bado hujafunuliwa, na utakapofunuliwa kwa utukufu waaminio ndio watakao ng’aa kwa utukufu na kubadilishwa kuwa kama Yesu, [1 Yohana 3:2], ila wale walio upuuza ufalme wa Neema, watakuwa na kilio na kusaga meno na maangamizo. Biblia inasema, “Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele. [Ufunuo 11:15]. Ufalme huu utaziondoa falme zote za dunia hii na kuziangamiza kabisa na kusimama waziwazi. Biblia inasema hivi.

Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele. “Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii. [Dan 2:44; 7:27].

Je waovu watapata nafasi ya pili?
Biblia inasema hakuna kitu kama hicho, wasio mkubali Yesu wote wataangamizwa kwa maangamizo ya milele. “Kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi;na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu; watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake;yeye atakapokuja ili kutukuzwa katika watakatifu wake, na kustaajabiwa katika wote waliosadiki katika siku ile, (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu). [2 Wathesaloniki 1:7-10].”

Mungu akubariki sana unapofanya maamuzi ya kumpokea huyu Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako, maana wakati huu karibu. Wito ni kuamini Injili. [Marko 1:15].KUHUSU UWEZO WA KIFALME MABEGANI

Yesu ANAO UWEZO WA KIFALME MABEGANI MWAKE (Isaya 9:7).
Na Wakati Yesu Anakwenda KUSULUBIWA Baada Ya Kuchapwa Mijeledi, kuvishwa taji la miiba,Kutemewa Mate Na Kufanyiwa Kila Dhihaka, Bado Pia ALIBEBESHWA MSALABA MABEGANI MWAKE na kupigiliwa misumari.. Na Ni Mabega Hayo Hayo YALIYO NA UWEZO WA KIFALME!

kwa hiyo kuwa mfalme halikuwa jambo rahisi, ilikuwa ni lazima uwe na uwezo wa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili watu,ikiwemo kuponya wagonjwa,viwete,viziwi,kulisha kundi kubwa la watu(kumbuka samaki na mikato),kufufua,n.k n.k,(rejea maandiko yapo mengi tu agano jipya)hata leo viongozi wakubwa wanapotembelea maeneo mbali mbali huzomewa risala na kuelezwa changamoto kubwa mbalimbali zinazowakabili wananchi na wanatakiwa kuzitatua, hapo moja ya wafalme alishindwa kutatua changamoto na kuamua kufunga na kuomba kwa kuvaa magunia maana yake tatizo lilikuwa kubwa sana

Mungu alizungumza na manabii kuwa atakuja kiongozi mkubwa sana atakayetatua changamoto mbali mbali za watu wake sio katika Israel tu bali dunia nzima huyu ndiye masihi, tunapoadhimisha kuzaliwa kwake leo tunapaswa kukumbuka kuwa Mungu ametupa kiongozi mwenye uwezo wa kutatua changamoto za aina mbalimbali ulimwenguni na kwa wanadamu wote na huyu si mwingine ni Yesu Kristo.

Isaya anamuelezea kiongozi huyu kuwa ni mwenye uwezo na mamlaka kubwa na kuwa atatua changamoto nyingi zinazowakabili wanadamu na moja ya changamoto kubwa inayowakabili wanadamu ni kukosekana kwa amani na utulivu mioyoni mwao na ndio maana Yesu anaitwa Mfalme wa Amani, kwanini mfalme wa amani

Ni muhimu kufahamu kuwa tunapozungumzia amani hii inayozingumziwa katika maandiko;-

Tunazungumziia ustawi, utulivu starehe amani na mafanikio makubwa ya mwanadamu ambayo asili yake ni Mungu, Amani hii ilikuwepo katika bustani ya Eden kabla ya anguko la mwanadamu, lakini baada ya anguko la mwanadamu amani hii ilitoweka Neno linalotumiska kuielezea amani hii katika lugha ya kiebrania ni SHALOM, neno shalom maana yake ni amani na ustawi na mafanikio ya kiunghu katika Nyanja zote, Waaarabu wanatumia neno SALAM, kwa kiaramu linatumika neno SALEMI, ni maneno yanayofanana sana katika lugha ya kiebrania, kiarabu na Kiswahili, kwa Kiswahili tunalo neno SALAMA ni hali ya amani, ni hali ya kuwa mbakli na masumbufu, ni hali ya kuwa na utulivu, Daudi alipigana sana vita katika maisha yake yote mpaka Mungu akamuita mtu wa Damu, Lakini mwanaye Suleimani hakukuwa na vita wakati wake, SULEMANI, SOLOMON maana yake ni utulivu na ustawi, Yerusalem maana yake ni mji
wa amani, Dar es Salaam maana yake

ni bandari ya amani, jina la mji wa mzizima Dare s Salaam lilitolewa na sultan Baraghash aliyekuwa anatawala Zanzibar na pwani na alitoa jina hilo kwa mji wa mzuizima kwa sababu aliamini badari hii ni mahali salama mno na patulivuIsaya anazungumzia kuwa masihi anazaliwa duniani kwa kusudi na malengo ya kuleta utulivu kwa wanadamu, utulivu huu ni ustawi wa mwanadamu katika Nyanja zote na ndio maana siku Yesu alipozaliwa malaika waliimba wimbo huu kuonyesha kuwa kiongozi mkubwa mwokozi wa ulimwengu atakayetatua matatizo na kuleta majibu na ufumbuzi wote wa mwanadamu amezaliwa na atatoa amani kwa watu wote atakaowakubali

Luka 2:8-18 “Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku. Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu. Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana. Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng'ombe. Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema, Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia. Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika, alilotujulisha Bwana. Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini. Walipomwona wakatoa habari waliyoambiwa juu ya huyo mtoto. Wote waliosikia wakastaajabu kwa hayo waliyoambiwa na wachungaji.”
YEYE NDIYE NI MSHAURI WA AJABU: Biblia inasema; “Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.” ZAB. 32:8 SUV

Hii ina maana kuwa nafasi ya ushauri ni ya Mungu mwenyewe katika maisha yetu. Kazi ya ushauri ni kukurahisishia kufanya maamuzi sahihi ya wapi uende wapi usiende, kipi ufanye na lipi usifanye.

Na Zaburi 119 anasema Neno lako ni taa ya miguu yangu …huniongoza popote niendapoHii inamaana kuwa Mungu anapoachilia ushauri analenga kukuongoza na anapokuongoza anatumia neno lake.akisema dunia inaitikia inafuataisha asemacho, ni kweli umetishwa kwaajili ya fedha mali na nguvu za watu, Yeye ndiye mshauri wa ajabu. Umekosa faraja, umekosa ushauri, umehangaika kwa washauri wameshindwa, leo kumbuka Yeye aliyezaliwa leo ni mshauri wa mambo yote, Yeye nimshauri wa ndoa, mshauri wa elimu ukiona mambo hayaendi inuka uombe mwite Yesu atakuja kwako na ataanza kukushauri. Ukiona biashara haiendi, ukiona kazi imegoma mwite atakupa ushauri unaofaa. Pokea ushauri kwa jina la Yesu. Mshauri wa ajabu anajua kulingana na chanzo cha tatizo, inawezekana ukipata shida unakimbilia kwa kaka, au shoga kimbila kwa mshauri wa ajabu Yesu Kristo.

Kila mtu anayemwamini Yesu anapewa amani hii moyoni mwake ni amani ambayo hata upatwe na changamoto ya aina gani wewe unakuwa na imani kuwa nitatoka nitatoboa kwa sababu ninaye mfalme
KUHUSU ETI YESU HANA NGUVU la hasha:

Bwana YESU alisema ‘Kwa kutumia Jina langu watatoa pepo,watasema kwa lugha mpya,watashika nyoka,hata wakinywa kitu cha kufisha hakitawadhuru kabisa,wataweka mikono yao juu ya wagonjwa nao watapata afya’Ndugu napenda ufahamu kuwa Jina la YESU lina nguvu inayotuwezesha kumtumikia Mungu kwa kulitumia jina hilo na kazi ya Mungu ikafanyika.Ni muhimu basi kuomba nguvu ya Jina la YESU kabla ya kwenda kuombea wagonjwa au kukemea pepo au kufanya huduma ya ukombozi au huduma yoyote ile.
LINAMLETA YESU PALE TULIPO.

YESU mwenyewe alisema katika Matayo 18 :20 : ‘Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa Jina langu,nami nipo papo hapo katikati yao’Hii ina maana kuwa popote pale tunapokusanyika halafu tukalitaja Jina la YESU,yeye mwenyewe YESU anashuka na kuwa pamoja nasi hata kama hatumwoni kwa macho yetu.Basi hii ni nguvu nyingine ambayo Mungu ameiweka kwenye Jina la YESU.
NGUVU ZA KIVITA :

Watu wengi hawategemei kuwa Jina la YESU lina nguvu ya kutusaidia katika vita tulivyonavyo hapa duniani.Ni rahisi kwao kuamini kuwa Jina hili lina nguvu kutushindia vita vya kiroho lakini si vya majeshi ya wanadamu.Kama umeingia vitani kwa kibali cha Mungu,basi Jina la YESU lina uwezo wa kukusaidia ushinde hivyo vita.Mkumbuke Mfalme Daudi wakati alipomwua Goliathi kwa kombeo la jiwe,hebu tusome Biblia 1Samweli 17 :45 : ‘Daudi akamwambia....lakini mimi nakujia kwa Jina la BWANA(Jina la YESU) wa majeshi,Mungu wa majeshi ya Israeli..’Ni wazi kuwa yule Goliathi alikuwa amejiandaa kuingia vitani hii ikiwa ni pamoja na kuvaa mavazi ya kuulinda mwili wake,na kwasababu hiyo ilikuwa si rahisi kwa nguvu za kibinadamu kumuua Golithi kwa jiwe la kombeo,lakini yeye Daudi hakuingia vitani kwa nguvu zake bali aliingia kwa nguvu za Jina la YESU,alipoingia vitani kwa Jina hilo,YESU aliteremsha msaada na nguvu zake kwa Daudi ndio maana akamwua Goliathi kwa jiwe la kombeo.Soma pia Zaburi 44 :5b,na Zaburi 20 :7 : ‘Hawa wanataja magari,hawa farasi lakini mimi nitalitaja Jina la Bwana Mungu wangu(Jina la YESU)’
KUAMURU UNACHOTAKA KITOKEE KUTOKEA.

Kwa kutumia jina la YESU tunaweza kuamuru chochote ambacho ni chema mbele za Mungu kitokee kikatokea kweli.
ITUMIE HIYO NGUVU
Natumaini kuwa umejifunza na kufahamu baadhi ya nguvu zilizomo kwenye Jina hili la ajabu,Jina la YESU Kristo.Sasa unachotakiwa kufanya ni wewe kuitumia hiyo nguvu iliyopo kwenye Jina hilo.
Ili uweze kulitumia Jina la YESU ni muhimu kumuomba Mungu mambo yafuatayo .

YEYE NI MFALME WA AMANI:
Katika ulimwengu uliojaa vita na vurugu, ni vigumu kuona jinsi Yesu angeweza kuwa Mungu mwenye nguvu zote ambaye anafanya katika historia ya binadamu na kuwa mfano wa amani. Lakini usalama wa kimwili na maelewano ya kisiasa haionyeshi aina ya amani Yeye anaongea kuhusu (Yohana 14:27).

Neno la Kiebrania la "amani," shalom, hutumiwa mara nyingi kwa kutaja utulivu na ustarehe wa watu binafsi, makundi, na mataifa. Neno la Kigiriki eirene lina maana "umoja na kuafikiana"; Paulo anatumia eirene kuelezea lengo la kanisa la Agano Jipya. Lakini maana pana na ya msingi, zaidi ya msingi maana ya amani ni "umoja wa kiroho unaoletwa na kurejeshwa kwa mtu binafsi na Mungu."

Katika hali yetu ya dhambi, sisi ni adui na Mungu (Warumi 5:10). "Lakini Mungu amethibitisha kwamba anatupenda ,maana wakati tulipokuwa bado wenye dhambi ,Kristo alikufa kwa ajili yetu" (Warumi 5: 8). Kwa sababu ya dhabihu ya Kristo, tunarudi kwenye uhusiano wa amani na Mungu (Warumi 5: 1). Hii ni amani ya kina, milele miongoni mwa mioyo yetu na Muumba wetu ambayo haiwezi kuchukuliwa (Yohana 10: 27-28) na utimilifu kamili wa kazi ya Kristo kama "Mkuu wa Amani."

Lakini dhabihu ya Kristo inatupa zaidi kuliko amani ya milele; pia inatuwezesha kuwa na uhusiano na Roho Mtakatifu, Msaidizi ambaye anaahidi kutuongoza (Yohana 16: 7, 13). Zaidi ya hayo, Roho Mtakatifu atajidhihirisha ndani yetu kwa kutupatia kuishi kwa njia ambazo hatuwezi kuishi kwa sisi wenyewe, ikiwa ni pamoja na kujaza maisha yetu kwa upendo, furaha, na amani (Wagalatia 5: 22-23). Upendo huu, furaha, na amani ni matokeo yote ya Roho Mtakatifu anayefanya kazi katika maisha ya mwamini. Wao ni tafakari ya uwepo Wake ndani yetu. Na, ingawa matokeo yao muhimu zaidi, ni muhimu kutupatia kuishi katika upendo, furaha, na amani na Mungu, hawawezi kusaidia tu kuingia katika mahusiano yetu na watu.Na tunahitaji sana-hasa kutokana na kwamba Mungu anatuita tuishi na ushirikifu wa kusudi na waamini wengine, kwa unyenyekevu, upole, na uvumilivu, "kuwa na bidii kulinda umoja wa Roho katika kifungo cha amani" (Waefeso 4: 1) -3). Umoja huu kwa madhumuni na upole haukuwezekana bila kazi ya Roho Mtakatifu ndani yetu na amani tunaye na Mungu kutokana na dhabihu ya Mwanawe.

Kwa kushangaza, ufafanuzi mwepesi zaidi wa amani, ule wa kuonekana kwa utulivu ndani ya mtu, unaweza kuwa vigumu sana kuelewa na kudumisha. Hatuna chochote cha kupata au kudumisha amani yetu ya kiroho na Mungu (Waefeso 2: 8-9). Na, wakati tunapoishi katika umoja na waumini wengine tunaweza kuwa vigumu sana, kuishi kwa amani katika maisha yetu inaweza mara nyingi kuwa ngumu.

Kumbuka kuwa amani haimaanishi "rahisi." Yesu hakuahidi kamwe rahisi; Aliahidi tu msaada. Kwa kweli, alituambia kutarajia dhiki (Yohana 16:33) na majaribu (Yakobo 1: 2). Lakini pia alisema kwamba, ikiwa tulimwita, angeweza kutupa "amani ya Mungu, ambayo hupita ufahamu wote" (Wafilipi 4: 6-7). Haijalishi matatizo gani tunayokabiliwa nao, tunaweza kuomba amani inayotoka kwa upendo wenye nguvu wa Mungu ambao hauna tegemezi kwa nguvu zetu au hali yetu.

KUHUSU UMILELE WAKE:
YEYE NI BABA WA MILELE; jana tulimwita baba, leo tunamwita Baba, alikuwapo, yupo na ataendelea kuwako milele. Uweza wake na mamlaka yake ni ya daima.

b) MASIHI LAZIMA AZALIWE KATIKA UKOO WA DAUDI LAKINI YESU HAKUZALIWA KATIKA UKOO WA DAUDI.
Alizaliwa ktk ukoo wa daudi rejea
Agano Jipya hutangaza waziwazi ukabila wa Kiyahudi wa Yesu. "Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu" (Mathayo 1: 1). Ni dhahiri kutoka vifungu kama Waebrania 7:14, "Kwa maana ni wazi kwamba Bwana wetu alitoka kwa Yuda," kwamba Yesu alitoka kwa kabila la Yuda, ambalo tunapata jina "Myahudi." Na nini kuhusu Maria, mama ya Yesu? Katika ukoo wa kizazi katika Luka sura ya 3, tunaona wazi kwamba Maria(mariam) alikuwa kizazi cha moja kwa moja cha Mfalme Daudi ambacho kilimpa Yesu haki ya kisheria ya kuinua kiti cha enzi cha Kiyahudi na hamna shaka kwamba Yesu alikuwa Myahudi kwa kikabila.
DAI LA YESU KUKOSA BABA HAKUMFANYI KUTOKUWA MASIHI.

kila mmoja wetu ana baba wawili: baba wa duniani na Baba wa Mbinguni. Baba wa duniani ni baba wa miili yetu. Baba wa Mbinguni ni baba wa roho zilizo ndani ya miili yetu. Yesu ana baba mmoja tu, kwa sababu Baba wa Mbinguni ndiye baba wa roho, na wa mwili wake. Hiyo ndiyo sababu Yesu anaitwa Mwana wa Mungu.
Kutokana na kuzaliwa kwa Yesu kwa njia ya Roho Mtakatifu ndani ya tumbo la Maria bikira (Luka 1: 26-38), utambulisho halisi wa Yesu Kristo daima umeulizwa na wasiwasi. Ilianza na mpenzi wa Maria, Yusufu, ambaye alikuwa na hofu ya kumuoa wakati alifunua kuwa alikuwa na ujauzito (Mathayo 1: 18-24).

Alimchukua kama mkewe tu baada ya malaika kumhakikishia kwamba mtoto aliyembeba alikuwa Mwana wa Mungu.Mamia ya miaka kabla ya kuzaliwa kwa Kristo, nabii Isaya alitabiri kuja kwa Mwana wa Mungu: "Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanaume, na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake. Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu,Mungu mwenye nguvu,Baba wa milele,Mfalme wa amani "(Isaya 9: 6). Malaika alipozungumza na Yusufu na kutangaza kuzaliwa kwa Yesu, alielezea unabii wa Isaya: "Tazama,bikira atachukua mimba,Naye atazaa mwana;Não watamwita jina lake Imanueli (maana yake ni 'Mungu pamoja nasi')" (Mathayo 1:23). Hii haikumaanisha kwamba watamwiita mtoto Imanueli; inamaanisha kuwa "Mungu pamoja nasi" ilikuwa utambulisho wa mtoto. Yesu alikuwa Mungu akija katika mwili kukaa na mwanadamu.

Yesu mwenyewe alielewa mawazo juu ya utambulisho wake. Aliwauliza wanafunzi wake, "Watu wanasema mimi ni nani?" (Mathayo 16:13; Marko 8:27). Majibu yalitofautiana, kama yanavyofanya leo. Kisha Yesu aliuliza swali la kusumbua zaidi: "Je, wewe unasema mimi ni nani?" (Mathayo 16:15). Petro alijibu jibu sahihi: "Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai" (Mathayo 16:16). Yesu alithibitisha ukweli wa jibu la Petro na aliahidi kwamba, juu ya ukweli huo, angejenga kanisa lake (Mathayo 16:18).

Asili ya kweli na utambulisho wa Yesu Kristo ina umuhimu wa milele. Kila mtu lazima ajibu swali ambalo Yesu aliwauliza wanafunzi wake: "Mnasema mimi ni nani?"

Alitupa jibu sahihi kwa njia nyingi. Katika Yohana 14: 9-10, Yesu alisema, "Yeyote ambaye ameniona amemwona Baba, unawezaje kusema, 'Tuonyeshe Baba'? Je, huamini kwamba mimi niko ndani ya Baba, na kwamba Baba ako ndani yangu? Maneno ambayo nawaambia siongei kwa uwezo wangu na mamlaka yangu, bali ni Baba, anayeishi ndani yangu, ambaye anafanya kazi yake. "

Biblia iko wazi juu ya asili ya utakatifu wa Bwana Yesu Kristo (angalia Yohana 1: 1-14). Wafilipi 2: 6-7 inasema kwamba, ingawa Yesu alikuwa "Yeye, kwa asili akikuwa daima Mungu;lakini hakufikiri kwamba kule kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kungangania kwa nguvu,bali, kwa hiari yake mwenyewe,aliachilia hayo yote akajitwalia hali ya mtumishi akawa sawa na mwanadamu akaonekana kama mwanadamu. " Wakolosai 2: 9 inasema, "Maana ndani yake Kristo katika ubinadamu Wake,umo ukamilifu wote wa Mungu."

Yesu ni Mungu kikamilifu na mwanadamu kamili, na ukweli wa mwili wake ni muhimu sana. Aliishi maisha ya kibinadamu lakini hakuwa na asili ya dhambi kama sisi. Alijaribiwa lakini hakufanya dhambi (Waebrania 2: 14-18; 4:15). Dhambi iliingia ulimwenguni kupitia Adamu, na asili ya dhambi ya Adamu imetumwa kwa kila mtoto aliyezaliwa ulimwenguni (Warumi 5:12) — isipokuwa kwa Yesu. Kwa sababu Yesu hakuwa na baba wa kibinadamu, hakuwa na urithi wa dhambi. Alikuwa na asili ya kimungu kutoka kwa Baba yake wa Mbinguni.Yesu alipaswa kukidhi mahitaji yote ya Mungu mtakatifu kabla ya kuwa dhabihu iliyokubaliwa kwa dhambi zetu (Yohana 8:29; Waebrania 9:14). Alipaswa kutimiza unabii zaidi ya mia tatu juu ya Masihi kwamba Mungu, kupitia manabii, Alitabiri (Mathayo 4: 13-14, Luka 22:37, Isaya 53, Mika 5: 2).

Tangu kuanguka kwa mwanadamu (Mwanzo 3: 21-23), njia pekee ya kufanywa wa kweli na Mungu imekuwa damu ya dhabihu isiyo na hatia (Mambo ya Walawi 9: 2, Hesabu 28:19, Kumbukumbu la Torati 15:21, Waebrania 9: 22). Yesu alikuwa dhabihu ya mwisho, kamilifu ambayo imeridhisha milele ghadhabu ya Mungu dhidi ya dhambi (Waebrania 10:14). Hali yake ya kimungu ilimfanya awe mzuri kwa kazi ya Mkombozi; Mwili wake wa kibinadamu ulimruhusu kumwaga damu muhimu ili kukomboa. Hakuna mwanadamu aliye na asili ya dhambi anaweza kulipa deni hilo. Hakuna mtu mwingine aliyeweza kukidhi mahit
KUHUSU "kiunabii au kimaandiko Uzao unatoka Kwa Baba."

Nipatie maandiko, na ukweli yesu hakuwa na baba hivo lazima kabila lake achukua kwa mamake.
Na ni kweli yusuph alimkimbia mariam kwa sababu tayr alimuona ana ujauzito. We myahudi huwezi kumwelewa Yesu mpaka ujue mambo ya roho mtakatifu na akusaidie.

C) MASIHI LAZIMA AWARUDISHE WAYAHUDI WOTE WALIOTAWANYIKA DUNIANI WARUDI ISRAEL. Si kweli maana limejibiwa vizuri hapo juu kwenye "katika mawazo yao walidhani ufalme wa Mungu ni kuifanya Izrael kuwa taifa kubwa duniani,na walikuwa na mioyo migumu na Yesu aliongea nao kwa Mifano lkn bado hawakuelewa.Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwamba(luka 8:10)“Ninyi mmejaliwa kufahamu siri za Ufalme wa Mungu, lakini kwa wengine nazungumza kwa mifano ili, ‘Kuangalia waangalie lakini wasione, kusikia wasikie, lakini wasielewe.’"
KUHUSU HILI LA "Masihi aliyetabiriwa moja y majukumu yake ilikuwa kuwakusanya na kuwarejesha waisrael wote waliotawanyika warudi nyumbani Yesu hakufanya hilo. Hivyo anakosa Sifa za kinabii za Masihi aliyetabiriwa"HAPA YEYE YESU ALIMAANISHA KUWAHUBIRI HABARI NJEMA ZA UFALME WA MUNGU ILI WAO WAYAHUDI NA MATAIFA MENGINE WAACHE MAOVU WAMRUDIE BWANA MUNGU "Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake. [Mathayo 21:43].” kuzaa matunda kwa maana waokoke waache maasi,watii sheria za bwana.
Maswali ambayo tunatakiwa tujiulize;

1. Ikiwa Yesu alitoka mbinguni, Kwa nini hakuandaa makao ya Watu wake Kabla hajaja Duniani kuwakomboa?
Badala yake Akaja Duniani kwanza ndipo akaenda kuandaa Makao. Hii maana yake ni nini? HII MAANA YAKE YOTE YANAWEZEKANA MAANA AMESHASEMA KWA NENO LAKE ""Yohana 14:1-25 SRUV
Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo. Nami niendako mwaijua njia. Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi tunaijuaje njia? Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. Filipo akamwambia, Bwana, utuoneshe Baba, yatutosha. Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo?

Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuoneshe Baba? Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe. Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lolote kwa jina langu, nitalifanya. Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu. Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona.

Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai. Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu. Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake. Yuda (siye Iskarioti), akamwambia, Bwana, imekuwaje ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu? Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenituma. Hayo ndiyo niliyowaambia wakati nilipokuwa nikikaa kwenu.""
Hayo maswali mengine wadai watanisaidia kujibu maana majibu yote baibo imeyabeba.
 
Unaona ulivyopopoma.

Suleiman hakuwa na watoto Wawili, Suleiman mwenyewe ni Myahudi.
Sasa kijana hata kusoma nilichokoandika unashindwa. Wapi nimeandika Suleyman alikuwa na watoto wawili ?

Naona kijana Uyahudi huujui, unajua kwanza maana ya Uyahudi ? Suleyman hakuwa Myahudi.
 
Hata Mungu anadhaniwa yupo kwanza.

Unajadili matawi ya mti wakati hata mzizi haupo?
Aliueumba limwengu(universe) na vilivyomo nani!?..yaani aliyemuumba wewe nani!?..ilikuaje ukawepo ikiwa unaasadiki hukuumbwa!?
 
Ukiwa na Akili ndogo jitahidi uzifiche.

Uyahudi ni Dini
Uyahudi ni taifa/utaifa.

Kama hujui Historia hata ya Kidato cha nne ni Bora ufiche ujinga wako.

7 Mama mmoja Msamaria akaja kuteka maji na Yesu akamwambia, “Naomba maji ya kunywa.” 8 Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula. 9 Yule mama akamjibu, “Wewe ni Myahudi na mimi ni Msamaria. Yawezekanaje uniombe nikupe maji ya kunywa?” -Wayahudi walikuwa hawashirikiani kabisa na Wasamaria.10 Yesu akamjibu, “Kama ungelifahamu Mungu anataka kukupa nini, na mimi ninayekuomba maji ya kunywa ni nani, ungeliniomba nikupe maji ya uzima
Hiyo biblia ya mfalme James ni ya mchongo,siyo reliable source,uyahudi ni dini siyo race
 
Hizo Takwimu ( 80%) ni kwa mujibu wa Nini?

Ingia kwenye worldometer population Angalia Nchi ya Israel, kipengele cha religion ni asilimia 4% ya Wayahudi wanaoamini Ukristo.
Huku 16 wakimuamini Muhammad. Wengine waliobaki ni Wayahudi (dini ya kiyahudi)
 
Kwani Israel wanaishi Wayahudi pekee?

Maana sijaelewa, unazungumzia Israel au Wayahudi?
 
Ingia kwenye worldometer population Angalia Nchi ya Israel, kipengele cha religion ni asilimia 4% ya Wayahudi wanaoamini Ukristo.
Huku 16 wakimuamini Muhammad. Wengine waliobaki ni Wayahudi (dini ya kiyahudi)
Hao ni waisrael mzee,huwezi sema hao waislam 16% ni wayahudi,huwezi kuwa myahudi na muislam,uislam unatambua dini tatu yaani ukiristo (naswara),uyahudi na uislam
 
Back
Top Bottom