Sababu gani hupelekea watu kununua vitu vya watu maarufu waliokufa kwa pesa nyingi?

a45

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
1,325
1,403
Ndugu WanaJF,

Habari za muda huu twende kwenye mada Moja kwa Moja.

Nimeona mara kadhaa vitu vilivyokuwa vinamilikiwa/ kutumiwa na watu maarufu kuuzwa Kwa pesa nyingi na kimsingi sio kwamba vitu hivyo ni ghari hapana bali ni vitu vya kawaida sana mfano nimeona kofia ya Michael Jackson aliyoivaa kwenye tamasha Moja inauzwa kwa bei kubwa kabisa na Tena nikasikia koti (jacket) la huyu huyu Michael Jackson likiuzwa Kwa mamilion ya shilingi.

Pia Kama mnakumbuka kifo cha mcheza kikapu Kobe Bryant baadae Jessy aliyokuwa anavaa nayo iliuzwa Kwa pesa nyingi kuliko kawaida.

Sasa Mimi swali langu ni kwanini vitu hivyo viuzwe Kwa bei kubwa hivyo? Au tusene Wanunuzi wa vitu hivyo hupendea Nini au wanatafuta Nini kutoka kwenye hivyo vitu kiasi cha watu kuwa tayari kutoa pesa nyingi kiasi hicho?
 
..
IMG_20231109_173348.jpg
 
mshana njoo utoe maelezo kutoka angle ya kilozi na kishirikina kwanini watu wananunua vitu vilivyo milikiwa na wafu Kwa pesa nyingib
 
Ni kama wewe unavyoenda Makkah au Jerusalem kuzulu makaburi ya watu waliokufa unaita kuhiji, basi na wao hujisikia furaha na faraja kumiliki vitu vya wapendwa wao maarufu waliokufa.
Asante Kwa maelezo
 
Back
Top Bottom