Rwanda yatishia kuishambulia kijeshi DRC

Rwanda yatishia kuishambulia kijeshi DRC

Lol,hao France walipigwa wakimsaidia Habyarima wakati kina Kagame wakiwa gorrilas,sipendi vita lakini usitegemee France or UN wafe kwa ajiri ya Congo
France walipigwa???hivi una uhakika na unaloongea au unaota ndoto za mchana...subiri muziki mukubwa utaanza then ndo utajua kachumbari ni mboga au chachandu...PK ataisoma number soon!! Haya ni maandalizi ya muda mrefu sio kwamba wamekurupuka.
 
Hapa umenifikisha Bukya. Napenda watu wanaoandika na sense. Ushauri wangu kwa Tanzania kabla janga halijaifikia: acheni kufurahia kupita kiasi kwa kuchukua ngome ya M23. PK sasa ameamua kulipiza kwa niaba ya M23. Pia huenda wakashirikiana na UGANDA iliyoko Kisangani na kuwazingira. Ni nyie tu ndio Kagame ana dukuduku nanyi, si majeshi mengine ya UN. Hivi sasa ni wakati wa kuchemsha na kupanga mbinu zenye ubunifu mkubwa, zikiwemo pre emptive strikes. Ni vizuri kummwajiri Mbusa Nyamwasa kwani yeye bado anajua mbinu nyingi za PK. Huyu jamaa ni tactician mkubwa na ameiva kwa vita na Watutsi si watu wa kuchezea inapokuja kwenye vita!

Mkuu huyo Bukya ndo Nyamwasa mwenyewe...hapa ni JF tu lakini hivi vinavyoongelewa hivi unafikiri JWTZ hawavijui????Hivi unafikiri hawajui UG na Rwanda lao ni moja???subiri muziki munene unakuja athubutu kuingiza majeshi yake Congo ndo utajua what I'm saying'.....muhimu for nw TISS waanze kuinvestigate commuinications za watz wenye asili ya Rwanda maana hawa jamaa kuuza timu hawatokawia kutuuza kwa PK...nawakilisha!
 
kuna mdau kadokeza ati Urusi na China zipo nyuma ya Rwanda na m23,
 
Hii vita niliitegemea sana tangu siku lilipoundwa jeshi la umoja wa mataifa kulinda amani huko Kongo, jkwani Kagame alichukizwa sana na kitendo cha Tanzania kupeleka huko asikari kwenda kuwabana watu wake wa M23. Ndio wakati huo huo Kagame alipofanya mabadiliko ghafla sana ya viongozi wa kijeshi na kumpandisha cheo General mmoja ambaye alikuwa ametoka vitani huko Darfur kwa kujua kuwa huyu alikuwa bado ni active sana kivita. Umepita muda mrefu Kagame hajapigana vita, jambo ambalo linakuwa haliendani na tabia yake kwa vile maisha yake yote amekuwa katika vita tu. Amani siyo kitu anachopenda au alichozowea. Katika miaka minane iliyopita, jamaa huyu alijilimbikizia silaha sana kiasi kuwa huko nyuma nilitoa wasiwasi wangu hapa forum kuhusu lengo la kiongozi huyo kwa siku za mbele kwani kazi ya silaha za kivita ni kupigana vita. Nadhani nilitoa tahadhari hapa lakini watu walinipoza kuwa hakuna tatizo. Vita inayokuja siyo ya Rwanda na Kongo tu, bali itakuwa na nia ya kuhamishiwa kuwa ya Rwanda na Tanzania; time will tell.

Tulijidai tunajua amani, sasa tunalazimishwa kuvunja amani. Kuna makosa makubwa Tanzania tumeshayafanya huko nyuma kuhusu vyombo vyetu vya usalama wa taifa kwa vile vina mapandikizi wengi sana wa kutokea Rwanda. Kuna wanyarwanda wengi sana nilisoma nao pale Dar wakapata kazi serikalini lakini baada ya Kagame kuingia madarakani baadhi yao wakarudi huko kwao hadi leo na wengine bado wakabakia hapo Dar.

Mkuu haya makosa ya kuwaingiza hawa watutsi yalifanywa na baba wa taifa yy si imani yake ilikua afrika ni moja .....but usiwe na wasi hata wahutu tunao wengi pia ambao wako against na hio serikali ya PK na wanazijua hizo siri zake na wao vile vile walikua huko na sasa wamo pia huku Tz..kwa hio hapo ni ngoma drooo..hii ni mikakati ya muda mrefu ilikuwa inasubiri proper time kwani Idd Amin ilikuwaje???alipangiwa timing na yy akajiingiza kichwa kichwa haahaahaaa....unakumbuka kilichotokea atiii.
 
kuna mdau kadokeza ati Urusi na China zipo nyuma ya Rwanda na m23,

China??? labda urusi naweza nikasema yes but sio China...sasa hivi muhimu kuifuatilia mizigo yao itakayopitia mombasa ili kuua logistics kabisa...ile ni landlocked country haiwezi shindana na Tz yenye bandari kubwa 3..tukizima mizigo yao hapo mombasa hakuna kitu kwenda kwao tumemaliza mchezo..Hivyo vifaru vyao vitatembelea maji??tunahujumu kila kitu!!chezea nchi yenye bandari weye!!!
 
Mbona majeshi yatanzania ndio yanatumia mizinga congo! hiyo inajulikana,subirini jamaa wakizama congo mtausikia mziki wao,mnasema m 23 inasaidiwa na rwanda,hamujui mziki wao,mkisikia wameingia hakutakua cha angola,zimbabwe,drc,fdlr,tz yani ni kiboko mbele kwa mbele,waache waendelee kuchokoza.

Sasa kuna kila dalili kwamba vita ya Tanzania na Rwanda itapiganiwa DRC, sio kati ya mpaka wa Tanzania na Rwanda.
 
rwanda wana Apache , sijui kama kuna nchi nyine hapa afrika mashariki na kati wanazo.

Rwanda haitapigana na nchi yoyote ile ila itapigana na UN, South wapo tayari kutoa hata mabomu yao kuilinda DRC. kuna uzi flani unaongelea jinsi South walivyo tayari kuisaidia DRC. Kama Kagame akithubutu kuishambulia DRC basi atafutika hata kwa wiki moja.
 
impregnable
Mkuu huyo Bukya ndo Nyamwasa mwenyewe...hapa ni JF tu lakini hivi vinavyoongelewa hivi unafikiri JWTZ hawavijui????Hivi unafikiri hawajui UG na Rwanda lao ni moja???subiri muziki munene unakuja athubutu kuingiza majeshi yake Congo ndo utajua what I'm saying'.....muhimu for nw TISS waanze kuinvestigate commuinications za watz wenye asili ya Rwanda maana hawa jamaa kuuza timu hawatokawia kutuuza kwa PK...nawakilisha!
Mkuu Mauza uza, kuhusu communication - mimi nimeshangaa sana kuona majeshi ya DRC yanatumia SSB radios (VHF/UHF) ku-communicate yaani wanaleta mambo ya ndombolo ya solo kwenye warfront! PK was right - jamaa hawa hawako serious kujikomboa hata Che Guevara aliwahi kuhoji attitude za Wakongomani katika medani za vita/kujikomboa - Che alisema Wacongo wako interested kwenye mambo ya miziki na wanawake na pombe (Primus bila shaka) na sijui kupiga PAMBA! Yaani hawana habari kwamba PK anaweza kutumia a radio scanner na ku-sweep frequencies zote wanazo tumia na kujua kila kitu kinacho endelea kimawasiliano, actually attitude za majeshi ya Congo yanaweza kuhatarisha majeshi yetu. Juzi juzi niliona kwenye an International media fulani makamanda wa jeshi la DRC wanashangilia tuu kwamba M23 wamekimbia! Hawajiulizi - Je, kweli wamekimbia kutokana na woga/kipigo au ni mbinu zao ya kutaka kuwavuta wa Congo ili wajisahau waingie mtegoni alafu baadae PK awageuzie kibao wajute kuzaliwa. I hope jeshi la UN lina means of communication other than SSB, jeshi letu lisitumie GSM/LTE/CDMA kuwasiliana - anyway jeshi letu sina shaka lina an impregnable means of communication in case of worst case scenario wanaweza kutumia Satellite Phones. Wanajeshi wetu wanapashwa kuwaelemisha wanajeshi wa DRC kwamba mambo ya vodafasta na SSB hazifahi kwenye mazingira ya vita. Mambo mengine uliyo pendekeza nayo yanapashwa kuzingatiwa na wana usalama wetu ambao najuwa wako mahili sana, CHEERS.
 
kweli aisee ni makosa tena makubwa ila sasa hapa tatizo ni kwamba huyu jamaa(PK) haaminiki tena uwezekano mkubwa wa kuwatumia m23 kurusha mabomu ni mkubwa ili kusudi yeye apate sababu ya kuingia DRC kuwasaidia watu wake wa M23 baada ya kuona wamezidiwa

nakuunga mkono na hata BBC wamesema hivyo, na JWTZ wanatuhakikishia ila swali linabaki kwa kina P. Kagame na MUKAMASIMBA km m23 sio wanyarwanda basi wasaidie kuwanyanganya hizo silaha maana wamejificha kwao, hayo mazungumzo ya meza moja Museveni na JK hatutaki PK alimfanya vibaya Habyarimana

Jeshi la Wananchi Tz ‏@JW_TZ 30 Aug Puuzeni taarifa ya M23 kuwa wamesitisha mapigano na kurudi nyuma kupisha mazungumzo, Tumewadhibiti wakalikimbia eneo lao la Kibati

Waasi wa M23 kusitisha mapigano DRC - BBC Swahili - Habari
Waasi wa M23 kusitisha mapigano DRC

Msaidizi wa katibu huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa, amenukuliwa akiiambia Umoja wa Mataifa kuwa wapiganaji wa kundi la waasi wa M23, wameonekana wakirusha makombora wakilenga Rwanda.Serikali ya Rwanda imesema jeshi la Congo lilirusha makombora hayo, madai ambayo yamekanusha na serikali ya Congo.
Wengi wa wapiganaji wa M23 ni wanajeshi walioasi jeshi la serikali, wengi wao wakiwa wa kibila la Kitutsi sawa na uongozi wa Rwanda.
Serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa zimeishutumu serikali ya Rwanda kwa kuwaunga mkono wapiganaji wa kundi hilo la M23, tuhuma ambazo zimekanushwa na utawala wa Kigali.
Awali, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa rais wa Rwanda, kuwa mvumilivu huku

.Tulishasema humu ndani na tutaendelea kusema kuwa mwisho wa Kagame na kagenge chake unahesabika.......maji sasa yamefika shingoni
..Majuzi baada ya M23 kuelemewa walijaribu kupeleka toka Rwanda reinforcement ambayo pia kikosi cha Afrika Kusini kilidhibidi kwa kutumia helcopter gunships
...Hatimaye makao yao makuu pale Kibati yametekwa na wanaume wa shoka
...Tunasuburi M23 wote kuvuka mpaka kukimbilia Rwanda, huko tutahitaji wakamatwe warudishwe Congo, la sivyo naiona Gisenyi kuwa next step..!
...Update toka twitter ya JW inathibitisha utekwaji wa Kibati
Jeshi la Wananchi Tz ‏@JW_TZ 31m Mapigano yaliyodumu saa 24 tangu 28/8/2013 tumefanikiwa kuichukua ngome kuu ya waasi wa M23 ya Kibati (Nyirangongo Territory - Goma, E- DRC)
 
Last edited by a moderator:
Bukyanagandi Mkuu wangu wala usihofu Batallion inayopigana ni yetu hao watu wa mayenu wacha wakae nyuma wakishangilia, ndio maana nakubaliana na Mauza uza anaposema ...subiri muziki mukubwa ...PK ataisoma number soon!! Haya ni maandalizi ya muda mrefu sio kwamba wamekurupuka.
Mkuu Mauza uza, kuhusu communication - mimi nimeshangaa sana kuona majeshi ya DRC yanatumia SSB radios (VHF/UHF) ku-communicate yaani wanaleta mambo ya ndombolo ya solo kwenye warfront! PK was right - jamaa hawa hawako serious kujikomboa hata Che Guevara aliwahi kuhoji attitude za Wakongomani katika medani za vita/kujikomboa - Che alisema Wacongo wako interested kwenye mambo ya miziki na wanawake na pombe (Primus bila shaka) na sijui kupiga PAMBA! Yaani hawana habari kwamba PK anaweza kutumia a radio scanner na ku-sweep frequencies zote
ingawa ni twitter ya JWTZ ingia tu Mkuu ujue updates kuwa hu JF kuna vibaraka wa PK wanatutibua lkn kwao kimenuka
Jeshi la Wananchi Tz ‏@JW_TZ 31 Aug Katika umoja huu JWTZ ndio yenye wanajeshi wengi, tuna Bataliani moja, hivyo tumepewa nafasi adhimu na ya heshima kuongoza mipango ya vita
 
Bukyanagandi Mkuu wangu wala usihofu Batallion inayopigana ni yetu hao watu wa mayenu wacha wakae nyuma wakishangilia, ndio maana nakubaliana na Mauza uza anaposema ...subiri muziki mukubwa ...PK ataisoma number soon!! Haya ni maandalizi ya muda mrefu sio kwamba wamekurupuka.

ingawa ni twitter ya JWTZ ingia tu Mkuu ujue updates kuwa hu JF kuna vibaraka wa PK wanatutibua lkn kwao kimenuka
Jeshi la Wananchi Tz ‏@JW_TZ 31 Aug Katika umoja huu JWTZ ndio yenye wanajeshi wengi, tuna Bataliani moja, hivyo tumepewa nafasi adhimu na ya heshima kuongoza mipango ya vita

Kuna sehemu nimesoma kuwa Rwanda imepelea division 10 yaani division division 6 za infantry na division 4 za vifaru. Kwa hali hiyo ni wazi kuwa Batallion moja ya TPDF haitafanya kitu chochote kuwazuia, na huenda wakawateketeza wote. JWTZ mnatakiwa kujibu mapigo hayo kwa division 10 vivyo hivyo. Kwa kiwango ambacho Rwanda imepeleka jeshi ni kama imepelaka jeshi lake lote huko Kongo, maana division kumi ni nyingi sana unless jeshi lao lina division 20 ambalo litakuwa ni jeshi kubwa sana kwa nchi ndogo. Hata hivyo sishangai kabisa kuona ukubwa wa jeshi la Rwanda kwa vile kwa muda mrefu Kagame amekuwa anajenga nchi pamoja na jeshi kwa kasi sana.
 
Kichuguu nikuhakikishie tu kuwa katika taasisi imara nchi hii limebaki jeshi tu....! Hayo yote unayoyasema naimani walishayafanyia kazi kitambo sana...! Tulishazungumza humu ndani kwanini JK aliteua majenerali 30 mwishoni mwa mwaka jana.....unafikiri ilikuwa ni kuwapa watu vyeo wakafurahie na familia zao au ulikuwa mkakati wa muda mrefu kijeshi......?

Pili, nikuhakikishie pia kuwa ingawa mimi ni raia wa kawaida lakini naelewa FIB haipo North Kivu kizembe zembe, nchi husika zilishapambanua jinsi ya kufanya reinforcement pindi nchi jirani kama Rwanda na Uganda zitasaidia M23....!

Tulishasema siku nyingi humu JF kuwa tunasubiri Rwanda washambulie FIB uone mziki wake utakavyochezwa.....!

Inshallah.....kwa pamoja na JWTZ tutakunywa chai Kigali
 
Nafahamu kuwa class mate wangu wawili wameteuliwa pia kuwa majenerali (brigadier generals); wote ni wasomi sana ila mmoja wao ndiye mtemi sana wa mambo ya vita. Ana Masters ya mipango ya vita, na kasomea mambo ya vita ya ardhi kutoka tasisi mbalimbali duniani huko, Egypt, Israel, UK, USA, South Africa na Canada.

Mimi ni shabiki sana wa vita za nchi nyingine ila huwa sipendi vita uhusishe nchi yangu.
 
Ulianza vizuri ila umemaliza vibaya😀
 
Katika shule za kijeshi pia kuna mafunzo ya kujua mwenendo wa kistrategia wa kiusalama....! Hili la Congo sio la JK bali ni mkakati ambao JW walishaona lisipotatuliwa sasa, hata sisi litatuletea shida baadae.....!

Usihofu na hao majenerali unaowasikia Rwanda na proxy forces zao huko Kivu......maanake kwao mtu akiingia msituni leo kama private baada ya miezi sita anatoka akiwa 'General'. Hata Kagame alikuwa just Captain mwaka 1986 akiwa failure from secondary school education, hakumaliza mafunzo ya kijeshi USA, lakini alipoingia msituni baada ya kufa Rwigyema, through Arusha Accord wakajipandisha vyeo kuwa Major General.......na sio kwa sababu ya mafunzo bali kisiasa!
 
Ulianza vizuri ila umemaliza vibaya😀
Huenda umenielewa vibaya au sikujieleza vizuri; ni shabiki sana wa kujua mipango ya kivita ikiwa imeshatokea, siyo kuwa ni shabiki wa kutaka wengine wapigane. Kwa mfano huwa ninasoma sana rekodi mbalimbali za kivita kutoka kwenye rekodi za vita mbalimbali ziliyokuwa declassified.
 
Katika shule za kijeshi pia kuna mafunzo ya kujua mwenendo wa kistrategia wa kiusalama....! Hili la Congo sio la JK bali ni mkakati ambao JW walishaona lisipotatuliwa sasa, hata sisi litatuletea shida baadae.....!

Usihofu na hao majenerali unaowasikia Rwanda na proxy forces zao huko Kivu......maanake kwao mtu akiingia msituni leo kama private baada ya miezi sita anatoka akiwa 'General'. Hata Kagame alikuwa just Captain mwaka 1986 akiwa failure from secondary school education, hakumaliza mafunzo ya kijeshi USA, lakini alipoingia msituni baada ya kufa Rwigyema, through Arusha Accord wakajipandisha vyeo kuwa Major General.......na sio kwa sababu ya mafunzo bali kisiasa!

Aisee ndugu yangu inaelekea unajua mengi sana kwa hiyo nitakuamini kwa kila utakaloandika kuhusiana na mgogoro huu kwa sababu ulilosema linagusa jambo moja ambapo mmoja wa hao majenerali class mate wangu alilisomea katika masters yake ya pili ya international relations na ulinzi wa amani akiwa anaachambua mgogoro wa Kongo na implications zake kwenye amani ya Tanzania. Mwingine ambaye nilimfahamu kupitia huyo mate wangu naye alikuwa anasoma pia international relations chuo hicho cha kijeshi kuhusu migogoro ya mipaka katika Afrika akiwa anafanya case study yake kuhusu mgogoro wa mpaka wa Tanzania na Malawi na implication zake katika amani ya Tanzania. Jamaa hawa wote wawili walipata masters zao mwaka 2006 wakti wakiwa makanali wa JWTZ wakati ambaao hata migogoro ya mpaka wa Malawi na huu wa Kongo haijaanza kuihusisha sana Tanzania. Inaeleka JW jamaa wanaona mbali.
 
mkuu Kwetunikwetu mwaga vitu mkuu, hivi kwa uchumi tulionao tunashindwa kununua vifaa vya kisasa kabisa kushinda nchi zote za EAC?
 
mabomu kuangukia nchi ya mwenzako huo ni uchokozi! Ni vema kuheshimu mipaka ya mwenzako labda kama ni sababu ya kutaka kupima maamuzi ya Rwanda!

Tatizo ni kwamba vita havina macho, inawezekana pia ni mabomu ya hao M23, unless bomu lililotumika linajulikana kuwa ni la fulani....

Yaani huku Congo sijui kutatulia lini......
 
Kagame kaamu kujitoa mhanga, kwa hiyo huko anaenda kupigana na UN.!

Sizani Kama yeye atakua wa kwanza kushambulia majeshi ya Un! Ila alichokifanya kusogeza majeshi yake mpakani ni mfumo olio Sawa wa kulinda nchi ambao kila nchi hufanya hivyo pindi ionapo hali kwa jirani mambo Sio mazuri! Anachotakiwa kufanya ni kuwapokonya hao waasi wa M23 silaha ili jamii ya kimataifa iweze kumuelewa na pia hatakiwi kwa namna yoyote ile kuwasapoti hao M23 na pia ikiwezekana awakamate hao Makamanda wa M23 na kutoishambulia Congo! Hapo jamii ya kimataifa itamuelewa! Kwakua hajiamini na utawala wake inawezekana atakua amepeleka vikosi vyake mpakani kwa Malengo yasiofaa! Tunaomba Amani Africa na Tanzania na East Africa! Mungu ibariki Tanzania!
 
Back
Top Bottom