Unahitaji kujua zaidi ya hizo propaganda za mabomu kurushwa ndani ya Rwanda. Moja sehemu wanayopigania ni mpakani kabisa mwa Rwanda. Mji wa Goma (Kongo) na Gisenyi (Rwanda) ni mmoja uliotenganishwa na mpaka tu. Kwa hiyo ni ngumu kupigana Goma na Gisenyi isidhurike. Lakini kubwa ni kuwa kuna uthibitisho kuwa M23 ni kikosi cha Rwanda. Umoja wa mataifa wanasema mabomu hayo yanarushwa na wao M23, pengine kutafuta sababu ya kulalamika au kuingia ndani ya Kongo.Unapotoa hoja kuwa na fikra kidogo hivi kama ni kweli mabomu yamerushwa ndani ya ardhi ya Rwanda kutoka DRC hapo mchokozi ni nani? na tukumbuke Idd amin alianza kuishambulia Tanzania kwa mbinu za kichokozi kama hizo mwisho wa siku akaingiza majeshi kabisa na kuua watanzania wengi kule Kagera kama ni kweli wamerusha mabomu ni vema Rwanda nayo ikajihami na uvamizi huo.