Mkuu ku deal na Battle Tanks ni kazi ndogo ukiwa na ......, alafu vifaru havitumiki kulinda mipaka labda kama una mpango wa kuvamia majirani, inavyo onekena PK yuko determined kuvamia tena DRC na si ajabu akawa ndiye aliwahamuru M23 wafanye tactical withdrawal baada ya M23 kurusha makombora huko Rwanda ili PK apate kisingizio cha kuvamia DRC kwa mara nyingine tena. Sasa hivi anajipanga vizuri kuzingira majeshi ya UN na DRC na kufanya mashambulizi ya kushtukiza - tusisahau PK ana usongo mkubwa na jeshi letu anatafuta kila mbinu kufanya a maximum damages kwa majeshi ya Tanzania na South Africa ili wakate tamaa ndio maana anaya sema sema sana kwenye media as if majeshi ya UN huko DRC ni predominantly Tanzainan/South Africans. Binafsi naona akifanya makosa ya kushambulia majeshi yetu kimakusudi basi tutakuwa hatuna sababu ya kuishia kurudisha majeshi yake mipakani tu. Jacob Zuma amekwisha muonya na Tanzania vile vile alitoa onyo kali, sasa mwenye mahamuzi ya mwisho ya hatima yake ni yeye mwenywe hasuke au anyoe. Majeshi yetu yanapashwa kuwa makini sana wasiwe wamewekewa mtego wa kuzungukwa pande zote na Artillary, kumbuka M23 ilikuwa kwenye sehemu hiyo kwa muda mrefu hatuwezi kujua walikuwa wanafanya mbinu gani/wanajitayarisha kivipi kufanya mashambulizi ya kushtukiza under Rwandan Army, don't underrate PK the guy is a tactician par excellence! Sasa nini cha kufanya the soonest, UN iombe NATO ianzishe kurusha DRONES 24/7 kwenye mipaka ya Rwanda/DRC na Uganda/DRC ku-track movement ya jeshi la Rwanda na la Uganda jamaa hawa lao moja, wakumbuke vile vile kwamba majeshi ya Rwanda yana kawaida ya kuvulia nguo za wanawake ili wasitambulike kirahisi, UN iombe NATO/Merikani iwapatie ndege nne za kivita aina ya A-10 Warthong Tank Busters ku-deals na vifaru/magari ya deraya/Artillery piece na munitions dump za Rwandan Army kama litathubutu kuvamia DRC au majeshi yetu. Kwa upande wa ku-deal na Infantry watumie Helicopter Gunships aina ya Denel AH-2 Rooivalk kutoka South Africa na Hind Mi-24 kutoka Urusi, nataka nieleweke hapa kwamba sio kwamba nashabikia mambo ya vita lakini tunapokuwa na Kiongozi ambaye anatishia AMANI kwenye maeneo ya Great Lakes, mtu anapigana vita mfurururizo takribani miaka ishirini bila ya kupata amani ya kudumu, hataki kushauliwa, yuko bellicose muda wote, uwezi kujua kesho atahamuka na directive gani kwa makamanda wake - kama anaweza kutishia maisha ya Rais mwenzake openly Je, Watanzania/Wacongo na sisi raia tunaotoka mipakani tutaishi na roho juu mpaka lini?