Mkuu ku deal na Battle Tanks ni kazi ndogo ukiwa na ......, alafu vifaru avitumiki kulinda mipaka labda kama una mpango wa kuvamia majirani, inavyo onekena PK yuko determined kuvamia tena DRC na si ajabu , ndiye aliwahamuru M23 wafanye tactical withdrawal baada ya M23 kurusha makombora huko Rwanda ili PK apate kisingizio cha kuivamia DRC kwa mara nyingine tena. Hivi sasa PK anajipanga vizuri kuzingira majeshi ya UN na DRC ili afanye mashambulizi ya kushtukiza - tusisahau PK ana usongo mkubwa na jeshi letu, anatafuta kila mbinu kusababisha a maximum damages kwa majeshi ya Tanzania na South Africa, anataka wakate tamaa. PK na makamanda wake wako obsessed na majeshi ya nchi hizi mbili ndio maana anaya sema sema sana kwenye media as if majeshi ya UN huko DRC ni predominantly Tanzainan/South Africans.
Binafsi naona akifanya makosa ya kushambulia majeshi yetu kimakusudi basi tutakuwa hatuna sababu ya kuishia kurudisha majeshi yake mipakani tu. Jacob Zuma amekwisha muonya na Tanzania vile vile alitoa onyo kali, sasa mwenye mahamuzi ya mwisho ya hatima yake ni yeye mwenywe asuke au anyoe. Majeshi yetu yanapashwa kuwa makini sana wasiwe wamewekewa mtego wa kuzungukwa pande zote kwa Artillary za PK, kumbuka M23 ilikuwa kwenye sehemu hiyo kwa muda mrefu, hatuwezi kujua walikuwa wanafanya mbinu gani/wanajitayarisha kivipi kufanya mashambulizi ya kushtukiza under command ya Rwandan Army, don't underrate PK the guy is a tactician par excellence!
Sasa nini cha kufanya the soonest ili tu pre-empty mipango yake ya aidha kuvamia DRC au majeshi yetu: La kwanza - UN iombe NATO ianzishe kurusha DRONES 24/7 kwenye mipaka ya Rwanda/DRC na Uganda/DRC ku-track movement ya jeshi la Rwanda na la Uganda jamaa hawa lao moja, wakumbuke vile vile kwamba majeshi ya Rwanda yana kawaida ya kuvuaa nguo za kike ili wasitambulike kirahisi: La pili - UN iombe NATO/Merikani iwapatie ndege nne za kivita aina ya A-10 Warthong Tank Busters ku-deals na vifaru/magari ya deraya/Artillery piece na munitions dump za Rwandan Army kama PK athubutu kuvamia DRC au majeshi yetu.
Kwa upande wa ku-deal na Infantry watumie Helicopter Gunships aina ya Denel AH-2 Rooivalk kutoka South Africa na Hind Mi-24 kutoka Urusi, nataka nieleweke sio kwamba nashabikia mambo ya vita, lakini tunapokuwa na Kiongozi ambaye anatishia AMANI kwenye maeneo ya Great Lakes, mtu anapigaa vita mfurururizo takribani miaka ishirini bila ya kurudisha amani ya kudumu, hataki kushauliwa, yuko bellicose muda wote, uwezi kujua kesho atamuka na directive gani kwa makamanda wake - kama anaweza kutishia maisha ya Rais mwenzake openly, Je Watanzania/Wacongo na sisi raia tunaotoka mipakani tutaishi na roho juu mpaka lini?