Ruth H Mollel aliingia lini CHADEMA?

Ruth H Mollel aliingia lini CHADEMA?

kwa safari hii viti maalumu cdm wamejitaidi sana kuliko mwaka 2010. viti maalumu ccm wamejaa watoto wa vigogo tupu...
 
Kaka usihangaike. Hiyo ni ngoma ya Lowasa tangu akiwa katibu mkuu utumishi. Ameziba nafasi ya Regina. Ndo mapendekezo ya mzee Lowasa hayo. Yaani badala ya kwenda bibi mkubwa, kachukuliwa bibi mdogo

Toto la kiume kuwa mbeya namna hii mbona wantia wasi mie mzima kweli weye:what::banghead:
 
Wabunge wa viti maalumu CCM WANAPATIKANA KWA KUPIGIWA KURA HUKO MAJIMBONI,BAADAE MAJINA YAYOSHINNDA NDO WANAKAA WASUBIRI SASA UWINGI WA WABUNGE WA CCM,ILA CHADEMA MBOWE NDO ANAECHAGUA ANAOWATAKA YEYE

kiujumla mwaka huu wabunge wa viti maalumu ccm ni kichefuchefu yaani ni full undugunization sina hamu...
 
Wasalaam !

Kweli sasa nimeanza kuzeeka na kupitwa na matukio ya kisiasa na kijamii.

Nina swali la msingi kwa wadau makini hasa wana chadema asilia.

HIVI HUYU Ruth H Mollel ambaye kama sikosei(nitaomba kusahihishwa) alikuwa ni mtu mnene na msomi kwenye serikali kwa miongo kadhaa alihamia lini chadema?

Kwenye list ya wabunge wa viti maalum wa chadema nimeliona jina lake nikashtuka kidogo kwa maana ya kushangazwa.

Hivi mama huyu alianza harakati ndani ya chadema lini kiasi cha kuukwaa ubunge wa viti maalum?

Hivi Chadema ilikuwa inahubiri mabadiliko ya namna gani hasa kama kikundi chote cha waliokuwa madarakani wamehamia huko?

Kama ni yeye kweli ...kupata ubunge viti maalum kupitia chadema huku ukiwaacha vijana waliojaribu kuwekeza katika chadema kwa kukimbia mfumo wa kiccm inatoa picha gani?

Hebu wasemaji wa chadema asilia njooni mjadili hoja hii.

SAMAHANI:Kama huyu Ruth H Mollel sio yule aliyekuwa ofisi ya makamu wa Rais mazingira na CV zake lukuki.

OMBI:Mada ijikite katika mchakato wa kumpatia ubunge Ruth Mollel!

Kwa wale ambao ni kizazi cha bodi ya mikopo kaeni kando

Cc:
Pasco
Crashwise
Molemo
Mungi

Ni AMRI ya mwekezaji /Investor, EDO, DIRECTIVES PERIOD.
 
huu umbea si utakumaliza kwa style hizi?

ben mdogo wangu, wambea wako mahakamani, but i comend your stand for your party, i was really looking at chadema nominating younger generation with people like yourself who have given their lives in building the party. Anyway life is not fair. I still do believe that you will one day soon achieve your ambition to become a great politician.
Please don't fall in the trap of becoming the fodder for the party internal struggle on the way in chadema.
 
Ungesubiri uone na picha kama unayemsema ndiye huyo.

Nina mchepuko wangu naye anaitwa Ruth Mollel, huenda majina tu yamegongana
 
alijiunga mwaka 2013/05/27 akabaki CCM Kwa kazi maalum

Kazi maalumu imekamillika kwa mafanikio ya kumuwezesha kuukwaa ubunge...Nice try!!

By the way mkuu umepotea sana jamvini nilidhani umedakwa kati ya wale 190!
 
Ungesubiri uone na picha kama unayemsema ndiye huyo.

Nina mchepuko wangu naye anaitwa Ruth Mollel, huenda majina tu yamegongana

wadau wameshazirusha picha mkuu labda nitaconfirm siku ya kuapishwa!!Ruth Mollel wako wengi kweli hata mimi nina mchepuko wa jina hilo hilo
 
Meningitis ninaona kama umejawa na hasira ambayo inaelekea kwenye chuki. Hivi kweli wote walioko serikalini basi hawastahili kuwa wana chadema au una tatizo lingine. Kwa sababu tu hajaandikwa katika magazeti au hujamsikia majukwaaani badi kwako unafikiri si 'mwana mageuzi'...kama unavyowaita. Wote hawa ni watanzania na wana stahili zao katika siasa ndani ya vyama vyovyote vile vilivyopo kwa mujibu wa sheria. Je hata hivyo vyama pinzani vingeshinda una maana watendaji wote wa serikalini wangefukuzwa ili kuleta hao vijana wana mageuzi unaowasema. Ndiyo maana ninasema hasira zako zinaelekea kwenye chuki. Kumbuka hata Dr Slaa wenginewengi walioijenga CHADEMA walitokea CCM. Cha msingi ninkuingiza wabunge who will make a different and bring the required changes. Na kwa hili si mbaya kuwatumia watu wenye uzoefu ndani ya mfumo unaopigana nao.

Jamani si kila mtu anayeiunga mkono cdm lazima ajitangaze. Wapo wanachama wanao iunga mkono cdm kwa nguvu, akili na mali zao bila kupigiwa mizinga na tarumbeta. Wapo wengi tuu! Kwa hiyo msishangazwe kama kuna watu wameanza kujulikana sasa. Hurrah!!!
 
Kazi maalumu imekamillika kwa mafanikio ya kumuwezesha kuukwaa ubunge...Nice try!!

By the way mkuu umepotea sana jamvini nilidhani umedakwa kati ya wale 190!

nani alikwambia tumekamatwa wote...
 
juliana shonza mbona kpata ubunge huulizi aliwekeza nin ccm?
 
Ungesubiri uone na picha kama unayemsema ndiye huyo.

Nina mchepuko wangu naye anaitwa Ruth Mollel, huenda majina tu yamegongana
Mkuu pole sana....ikulu pamekuwa pagumu kufika
 
Tumia akili wewe,hivi siri za serikali nani anazipeleka chadema?Tambua kuna watu ni wafanyakazi wa serikali lakini huchangia harakati za siasa za upinzani kwa siri sana.Namaanisha wanaofanya kazi nyeti za chama huwa hawajionyeshi hadharani.Acha ujinga wewe!!wa ni mtu mnene na msomi kwenye serikali kwa miongo kadhaa alihamia lini chadema?

Kwenye list ya wabunge wa viti maalum wa chadema nimeliona jina lake nikashtuka kidogo kwa maana ya kushangazwa.

Hivi mama huyu alianza harakati ndani ya chadema lini kiasi cha kuukwaa ubunge wa viti maalum?

Hivi Chadema ilikuwa inahubiri mabadiliko ya namna gani hasa kama kikundi chote cha waliokuwa madarakani wamehamia huko?

Kama ni yeye kweli ...kupata ubunge viti maalum kupitia chadema huku ukiwaacha vijana waliojaribu kuwekeza katika chadema kwa kukimbia mfumo wa kiccm inatoa picha gani?

Hebu wasemaji wa chadema asilia njooni mjadili hoja hii.

SAMAHANI:Kama huyu Ruth H Mollel sio yule aliyekuwa ofisi ya makamu wa Rais mazingira na CV zake lukuki.

OMBI:Mada ijiki
 
Back
Top Bottom