Ruth H Mollel aliingia lini CHADEMA?

Ruth H Mollel aliingia lini CHADEMA?

Si Mlisema Jamaa Anakuja CHADEMA Na Mtaji Gani? Huyo Ndiyo Mmoja Wa MTAJI Wenyewe Ukiachilia Mbali Ule Ambao Mzee Mtei Na Mtoto Wa Mjini Mbowe Walioupata Pale Sea Cliff Hotel Kutoka Kwa Mr. WAKUCHINJWA CHINJWA KILA WAKATI.

hii ni kuonyesha kuwa asilimia kubwa ya kura za wagombea wa UKAWA wengi walichaguliwa na wana-CCM.

Wanaendelea kujitokeza - m/kiti UVCCM kapewa Viti maalum, M/hazina Iringa kapewa viti maalum.

Na bado wapo wengi ni mitaji hiyo waache kulialia NDOROBO hao!!!!!!
 
Kwani ni vigezo gani vilitumika kumpa huyo mama ubunge? Au mchakato ulikuwaje? Hii itasaidia kuondoa doubts kuhusu ukanda na kujua na.

Na wewe jiunge na wana mabadiliko UKAWA utajua jinsi wanavyochaguliwa.

Lakini ukiwa nje ya nyumba huwezi kuelewa yaliyo ndani ya nyumba.

Mpo wengi mnatamani kujiunga na CHADEMA / UKAWA karibuni sana msione aibu ni mambo ya kawaida
 
Tarehe ya kuingia ipo kwenye kadi yake ya chama.Na siyo mchoyo nadhani ukimuomba akuonyeshe atafanya hivyo.
BTW itakusaidia nini katika shughuli zako za kujenga nchi.
 
wewe ni nani katika chama?? Unataka kila mmoja apate ubunge wa viti maalum?? Mbona hujashtuka juliana shonza kupewa ubunge?? Kuhama ni kuhama tu siasa ni kazi by the way mbowe alisema wanagawana majukumu na sio kugawana ulaji.

sio jibu kaa kando wenye uwezo wa kujibu wajibu.ww ni walewale wakaskazini
 
Kaka usihangaike. Hiyo ni ngoma ya Lowasa tangu akiwa katibu mkuu utumishi. Ameziba nafasi ya Regina. Ndo mapendekezo ya mzee Lowasa hayo. Yaani badala ya kwenda bibi mkubwa, kachukuliwa bibi mdogo

Kwani mzee El nino yule muimba mapambio aliachana nae?au nae yupo kwenye list ya wabunge(another list of shame)
 
Naona efforts zimehamia kuiua chadema kwa nguvu zote
 
Kaka usihangaike. Hiyo ni ngoma ya Lowasa tangu akiwa katibu mkuu utumishi. Ameziba nafasi ya Regina. Ndo mapendekezo ya mzee Lowasa hayo. Yaani badala ya kwenda bibi mkubwa, kachukuliwa bibi mdogo
Du kweli nimeamini msemi wa wahenga kuwa mwenye pesa ndio mchagua wimbo kwa mpiga zumari.
 
Wajinga ndo waliwao!! Hamkujua kama CDMA ni NGO?!! Subirini mpaka miaka mitano iishe ndo majibu yatapatikana!!
 
Lowasa ni mutu wa misheni sana, sıjuı hali ingekuwaje km angeshinda!AHASANTE KWA KUTUEPUSHA BALAA HII.
 
Hizo ni mojawapo za Nafasi 4 alizopewa Mtukufu Rais Edward Lowasa na kamati Kuu ya CHADEMA ndio kawapendekeza hao mwingine ni yule mweka hazina wa CCM kule Iringa. Alibaki CCM kwa kazi maalumu.
chanzo: Salum Mwalim kupitia gazeti la Nipashe
 
Watanzania wanapaswa kujua kuwa vyama vya siasa siyo kampuni. Kampuni ndiko unawekeza kwa makusudi ya kuvuna au kupata mgawa faida inapopatikana. CDM ni chama cha siasa na kimeangalia mchango wa mtu katika siasa cha chama siyo hoja ya kusema watu wamewekeza ili kujipatia manufaa fulani. Chama cha siasa ni kama yule mtu aliyeajiri watu kwenye shamba aliyeanza kazi asubuhi na aliyeanza kazi saa tisa wote walilipwa dinari. Mama huyo japo alianza kazi jioni amefanya kazi yake vizuri na amelipwa dinari. Watu wanashangaa nini?
 
Hizo ni mojawapo za Nafasi 4 alizopewa Mtukufu Rais Edward Lowasa na kamati Kuu ya CHADEMA ndio kawapendekeza hao mwingine ni yule mweka hazina wa CCM kule Iringa. Alibaki CCM kwa kazi maalumu.
chanzo: Salum Mwalim kupitia gazeti la Nipashe

Katiba ya Chadema inasemaje kujusu hili...yaani mwanachama kugombea urais au kujiunga na chama anatoa masharti?
 
Tuondoke kwenye makoti ya kampeni na tuendelee kujadili kwa utashi wa akili zetu.

bensaanane

Kungekukua na kipimo cha utashi wa akili wewe ungekuwa huna kabisa huo utashi. Ni wazi una mgandamizo nje ya utashi wa akili yapo. Inakuwaje akili ni yako lakini utashi wako ni kuwatakia mabaya majirani tena bila aibu?
 
Katiba ya Chadema inasemaje kujusu hili...yaani mwanachama kugombea urais au kujiunga na chama anatoa masharti?
Nani katoa Masharti? Na ni masharti gani? Kumbukumbu nzuri la Tukio la Lowasa kuja CHADEMA kaliongea Vizuri Dr.Slaa tafuta Youtube video Ipo Tusiwe wavivu na watu wa kuhisi/kufikirika.
 
Chadema wakianza kujibu hili nitaanza kuzomea
 
Back
Top Bottom