Rushwa ya Ngono na Fedha zilitawala katika Idara za Uhamisho na Upangaji vituo vya kazi katika Halmashauri za Dodoma mwaka 2022

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Matukio ya Rushwa za Ngono na Fedha bado yanaendelea kuwa kikwazo cha upatikanaji wa Haki katika huduma ikiwemo kuwakosesha Watumishi wenye Sifa fursa za kupata Uhamisho wa Idara au Vituo vya Kazi kutokana na kukataa au kutoridhia masharti ya kutoa Rushwa.

Ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), iliyoangazia masuala ya Rushwa katika Halmashauri za Jiji la Dodoma katika Sekta ya Elimu mwaka 2022 ilibaini kuna Rushwa ya Ngono kwa 72% katika Idara za Upangaji Vituo vya Kazi 63% katika Idara za Uhamisho wa Watumishi ndani ya Halmashauri.

Mdau, umewahi kutakiwa kutoa au Kupokea Rushwa ya Ngono au Fedha ili upate Uhamisho, na ulichukua hatua gani?
============

1698470111052.png
 

Attachments

  • TAARIFA-KWA-UMMA-UTENDAJI-DODOMA.pdf
    572.3 KB · Views: 6
Hapo ndio sijawaelewa hao TAKUKURU. Wao wanatoa ripoti kuwa kuna rushwa katika taasisi, je sio kazi yao kuchunguza na kuhakikisha wahusika na rushwa wanafikushwa mahakamani?
 
Back
Top Bottom