Rungwe Wamshukuru Rais Samia Kwa Huduma za Afya

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
WILAYA ya Rungwe mkoani Mbeya, imemshukuru Dk. Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kufanikisha mapambano dhidi ya vifo vitokanavyo na uzazi pingamizi. Kutokana na maboresho makubwa yaliyofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Rungwe, zaidi ya wanawake 350 wanajifungua wakiwa salama na watoto wao kwa mwezi.

Akizungumza jana katika Hospitali ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, Mbunge wa Viti Maalumu
(CCM), Suma Fyandomo, alimshukuru Rais Dk. Samia kwa kuendelea kufanikisha mapambano dhidi ya vifo vitokanavyo na uzazi pingamizi. Suma alisema katika mapambano hayo, wanamtambua Rais Dk. Samia kama shujaa na askari namba moja aliyedhamiria kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi nchini.

"Mkoa huu ni kati ya mikoa ambayo watu wanazaliana kwa wingi, hapo awali huduma za afya hususan za uzazi zilikuwa changamoto katika vituo vya afya na hospitali zetu, kwa sasa hususan katika miaka miwili hi ya Rais Dk. Samia tumeona uthubutu na uchungu alionao kwa wanawake ambapo vifaa tiba na mazingira wezeshi ya kujifungulia yanatupa uhakika wa uzazi salama," alisema.

Alieleza kuwa, katikahospitali hiyo wanajifungua wanawake zaidi ya 350 kwa mwezi huku wote wakiwa salama na watoto. Mbunge Suma alisema kwa namna ambavyo uongozi wa Rais Dk. Samia unamjali mama na mtoto; maboresho ya wodi za kujifungulia yamezingatia upatikanaji wa vifaa vote vya afya vya kisasa kutoka Bohari ya Dawa (MSD), katika vituo vote hadi vya pembezoni ambavyo sasa vinafanya upasuaji.

"Kuanzia Kyela, Chunya, Mbarali, Mbeya mjini na vijijini hakuna mahali kuna malalamiko ya kukosa dawa na vifaa tiba hadi ngazi ya zahanati, kuna majengo kisasa na huduma mbalimbali, ikiwemo ya dharura ambapo ujenzi unaendelea kila sehemu, nami katika kuunga mkono jitihada hizo nimenunua shuka, viti mwendo kutoka MSD" alisema.​
 
Back
Top Bottom