Toto Afya: Waraka mfupi kwa Rais Samia

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
680
1,338
Rais awali ya yote natumai, natumaini na ni matumaini yangu umzima wa Afya,

Mwaka jana Wananchi hasa Sisi wenye watoto wadogo tilipata mshituko kidogo kusikia NHIF wametoa Kifurushi cha Toto Afya na kuweka utaratibu mpya

Utaratibu mpya wa sasa wa"Toto Afya"unapatikana kupitia mashuleni tu, Na Kule Shuleni NHIF imeweka utaratibu wa Idadi maalumu itimie ndo wapate hiyo "Toto Afya "

Kama hiyo Idadi ya watoto 100 isipotimia kwa shule basi mtoto hawezi kupata hiyo Huduma ya Toto afya

Mpaka Sasa shule nyingi zimekwama hicho kigezo ikiwepo shule wanayosoma Watoto wangu

Maana yake Sasa hivi watoto wengi Ambao wazazi wao sio waajiliwa wa Serikali wanakosa hii Huduma ya msingi ya Bima ya Afya kwa Watoto wao

MH Rais Samia:Chonde Chonde ingilia hili Kati NHIF warudishe ule Utaratibu wa awali hata ikibidi waongeze kiwango cha kulipia

Rais Samia 80% ya Watanzania ni (Sector Binafsi) kwahiyo utaona tatizo kubwa na Zaidi mamilioni ya watoto kukosa Huduma hii

Lakini pia Rais Serikali inaweza kubana matumizi mengi na pesa zingie kusadia au kutatua Hili tatizo na watoto wote waweze kupata haki zao za matibabu (Toto Afya)

MH Rais Naamini unaongozwa na jopo la washauri wenye Hekima,Walione hili kwa Jicho la Tai na kupatiwa Ufumbuzi wa haraka kuokoa vifo kwa watoto

Asante naomba kuwakilisha na nikutakie Majukumu Mema ya kuongoza Taifa letu

Alex
+255 655 308494
 
Suala la toto afya kadi,
Kisiasa Serikali imezingua ,
Kibiashara NHIF wapo sahihi, wabongo tulikuwa tunakatia watoto wagonjwa tu
 
Wabunge wakuteuliwa yaani wasio na majimbo wanalipiwa bima ya 200b pamoja na kwamba Wana mishahara minono.

Watoto wa wapiga kura wakiumwa wazazi wanakwenda moja kwa moja kwenye maduka ya dawa. Wauza maduka ya madawa ndio wanaouza dawa na kuamua ni dawa gani mgonjwa atumie.

Ikumbukwe maduka mengi ya madawa hayana qualified personnel (Kuna mmoja namjua alipata D ya chemistry na F nyingi , kaenda kusoma vyuo vya uchochoroni leo hii anauza dawa) Hii Ni kuepuka gharama za kumuona daktari.

Now you know.
 
Rais awali ya yote natumai, natumaini na ni matumaini yangu umzima wa Afya,

Mwaka jana Wananchi hasa Sisi wenye watoto wadogo tilipata mshituko kidogo kusikia NHIF wametoa Kifurushi cha Toto Afya na kuweka utaratibu mpya

Utaratibu mpya wa sasa wa"Toto Afya"unapatikana kupitia mashuleni tu, Na Kule Shuleni NHIF imeweka utaratibu wa Idadi maalumu itimie ndo wapate hiyo "Toto Afya "

Kama hiyo Idadi ya watoto 100 isipotimia kwa shule basi mtoto hawezi kupata hiyo Huduma ya Toto afya

Mpaka Sasa shule nyingi zimekwama hicho kigezo ikiwepo shule wanayosoma Watoto wangu

Maana yake Sasa hivi watoto wengi Ambao wazazi wao sio waajiliwa wa Serikali wanakosa hii Huduma ya msingi ya Bima ya Afya kwa Watoto wao

MH Rais Samia:Chonde Chonde ingilia hili Kati NHIF warudishe ule Utaratibu wa awali hata ikibidi waongeze kiwango cha kulipia

Rais Samia 80% ya Watanzania ni (Sector Binafsi) kwahiyo utaona tatizo kubwa na Zaidi mamilioni ya watoto kukosa Huduma hii

Lakini pia Rais Serikali inaweza kubana matumizi mengi na pesa zingie kusadia au kutatua Hili tatizo na watoto wote waweze kupata haki zao za matibabu (Toto Afya)

MH Rais Naamini unaongozwa na jopo la washauri wenye Hekima,Walione hili kwa Jicho la Tai na kupatiwa Ufumbuzi wa haraka kuokoa vifo kwa watoto

Asante naomba kuwakilisha na nikutakie Majukumu Mema ya kuongoza Taifa letu

Alex
+255 655 308494
Una hoja ya msingi sana,,

Kweli bima ya afya (NHIF)ni janga kubwa sana kwa kwl.
 
Back
Top Bottom