Rungwe -Tukuyu pazuri kuishi 100%

Rungwe -Tukuyu pazuri kuishi 100%

Nialishi Tukuyu kama miezi mi5 hivi. Nilikuwa napata shida sana ya kupata mgahawa mzuri wa kula sehemu pekee ni Lax na Kivanga. Nikasema nitafungua mgahawa mmoja classic sema ndio kilichonipeleka kikaisha kabla ya muda tarajiwa.

Nakubali gharama za maisha zipo chini sana. Ila zile mvua dah ni kisanga. Kuna muda wa miezi ya 4,5 ilinibidi kufua nguo Tukuyu tunaenda kuanika Kyela.
 
Hyo ya hali ya hewa mimi ndio inanikwaza
 
Nialishi Tukuyu kama miezi mi5 hivi. Nilikuwa napata shida sana ya kupata mgahawa mzuri wa kula sehemu pekee ni Lax na Kivanga. Nikasema nitafungua mgahawa mmoja classic sema ndio kilichonipeleka kikaisha kabla ya muda tarajiwa.

Nakubali gharama za maisha zipo chini sana. Ila zile mvua dah ni kisanga. Kuna muda wa miezi ya 4,5 ilinibidi kufua nguo Tukuyu tunaenda kuanika Kyela.
kuna sehem nilikula supu flani iv kwa 1500 **** ndiz ndan pemben chapat moja ndim pemben kwanza inakarot sijui pilpil hoho mixaer viaz mviringo n htr.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eneo la rungwe ni linasifika kwa unafuu wa maisha na mzunguko mzuri wa pesa
hapa tanzania.

Tuangalie sifa zake :

-Rungwe ni sehem nzuri kwa kilimo mfano ndizi, viaz mahind,maharage njugu,karanga nk

-Kiukweli Rungwe biashara yoyote inalipa we anzisha tu chochote utaona mafanikio.

-Watu wake ni wakarimu sana ila hawapend dharau.
-Hali ya hewa ni nzuri muda wote kutokana na miti ya matunda na mazao ya kilimo eneo zima la hapo.

-Rungwe hakuna kunyimana misosi ukimtembelea mtu kwake unapewa kamzigo

-Usafiri upo wa kumwaga noah,coster pamoja na hiace.

-Huduma za afya zipo za kutosha

-Ukiwa mtumishi wa umma unaweza ukajisahau hata kujenga maana vyumba ni bei chee sana. Mfano mji wa kibiashara wa Kiwira nyumba nzima elfu 70 kwa mwezi.

-Nauli mpaka Mbeya mjini ni buku 3 gari zake dk 45 tu umeingia mjini zinapaa mwendokasi.

-Wadada wa hapo ni kitonga sana hawaogopi kutoa mzigo nadhan ni kwasababu ya baridi ya kule lakini ukimkuta mlokole inabidi uokoke kwanza then ukajitambulishe kwa wazazi na mahali utoe ndio utakula mzigo.

-Ni vizuri uwe umeoa maana ukimwi upo nje nje.
-Watumishi wa Serikali mfano walimu walioanza kazi kule hawatakagi kuhama hiyo ni kutokana na unafuu wa maisha ukiwa na elfu kumi ukiingia sokoni unarudi na kiloba cha mazaga zaga.
-Ni sehemu ambayo watu wake jioni wanapiga pamba kali lakini asubuhi unawakuta mashambani wanachezea udongo.
-Watu wake wapo smart sana wanajua kuvaa
-Watu wake wanapenda sana dini, elimu na kilimo.
-Kama unapenda pombe hapa ndio penyewe
-Kama umeolewa halafu umehamia Rungwe unashinda ndani tu hujishughulishi na chochote utakoma na maneno ya wamama wa kinyakyusa sifa ya mwanamke wanajua ni kupiga kazi kusaidia familia.
-Watu wake wamechangamka muda wote

Mwisho::,,,,, kupanga ni kuchagua.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kabisa kabisa ni pazuri sana sana na wenyeji sio wabaguzi
 
Alfajiri utaona wamama wakienda shambani, sijui WANAUME wa Tukuyu walikufa wote au ni vipi SIJUI. Sioni wanaume mashambani.

Hapana Mkuu, huelewi culture ya watu wa Tukuyu. Hii kitu ofisi yetu ilifanyia research - magawanyo wa kazi wa Wanyakyusa kati ya wanaume, wanawake na watoto. Ni kwamba ule ukulima mkubwa wa kuandaa mashamba kwa ajili ya kupanda nafaka au kutengeneza matuta ya kupanda viazi hufanywa na wanaume, sio wanawake. Wanawake wanaingia kazini wakati wa kupanda na palizi. Palizi za mashamba ya ndizi hufanywa na wanaume.

Lakini wanaume hata siku moja hawafanyi kazi ya palizi kama mahindi au maharage au kuchimba viazi nk. Hizo ni strictly kazi za wanawake. Kumkuta mwanaume kainama anapalilia mahidi, maharage au anachimba viazi sio rahisi.

Kwa hiyo wewe unaweza uliwaona wanawake wakienda shambani wakati wa palizi za mahindi au maharage, na hukuona wanaume wakiwa wamefuatana nayo. Hilo ni kawaida.

Wanaume wa Tukuyu wakikuona mwanaume unapalilia shamba la maharage au karanga hawakuelewi. Wewe unatakiwa ulime kishe unamkabidhi mama apande, kupalilia na kuvuna.

By the way, hata size na aina ya majembe ya wanawake na wanaume ni tofauti. Majembe ya wanaume ni makubwa sana yametengenezwa kwa ajili ya kazi kubwa (ploughing)

1588924568625.png
 
Atlest mnagawana majukumu...sio mbaya inavutia...ingawa mwanamke majukumu yanamzidia kwa hizo kazi..!
 
Atlest mnagawana majukumu...sio mbaya inavutia...ingawa mwanamke majukumu yanamzidia kwa hizo kazi..!
Mkuu, usisahau kazi ya palizi ya mashamba ya migomba kwa wanaume wa Tukuyu ni full time job. Yaani wanakuwa na mashamba makubwa, kwa hiyo akimaliza shamba, alikoanza magugu yanakuwa yameota. Ndio maana wanawake wanapewa kazi za palizi na kuvuna ambazo ni za msimu. Mwanaume yeyote wa Tukuyu mwenye shamba ni kwamba kila siku asubuhi ataenda kwenye kupalilia shamba la migomba, ambalo mara nyingi liko hapohapo nyumbani. Atafanya kazi hiyo hadi saa sita. Kisha anaenda kuoga mtoni. Hawana tabia ya kuoga maji ya moto pamoja na baridi ile. Ila baada ya kazi za shambani asubuhi, jioni kwenda kupiga ulabu ni kawaida!
 
Kaka sio kesi, hamna anayesema kijijini kwenye hamna rutuba, ni suala tu la kutumia akili utaelewa kinazungumzwa nini. Mdau kasema, ukiwa na 10,000 ukaenda sokoni unarudi na kiroba cha mazagazaga. Hiyo ni indication kuwa thamani ya mazao ya shambani iko chini, kwa hiyo mkulima wa mdogo wa Tukuyu financially hawezi kuwa fit. Sasa sijaona sababu ya kutokwa misuli ya koo kutetea kijiji.

Tarehe 28 nilikuwa Tukuyu. Tumepita pale Kiwira wamama wanalia na mabeseni ya maparachichi kila mmoja analia akuuzie angalau ya 500. Ukianza kuilinganisha Tukuyu na Dar nakuona mwehu sababu wamama wa Dar watakwambia parachichi moja ni 800 na kama hutaki SEPA kwa kuwa wana uhakika wa kuyauza.

Kwa kifupi Tukuyu imebarikiwa ardhi. Mgomba ni mgomba kweli na ndizi imesimama hasa, lakini ni neema ya chakula. Alfajiri utaona wamama wakienda shambani, sijui WANAUME wa Tukuyu walikufa wote au ni vipi SIJUI. Sioni wanaume mashambani.

Kuhusu Tukuyu kuwa na wafanyabiashara na wasomi hiyo nayo ni ligi ya kijinga. Hamna mkoa ulioshindwa kuregister wasomi wawili watatu na wafanyabiashara hapa Dar. Hata watu wa Dodoma tu wana wasomi wao. Nenda pale stendi ya mkoa Ubungo ukahesabu watu wangapi wa Tukuyu wapo Dar wakiuza Power Bank za Kichina kwenye mabasi, wauza Flash Disk, Boda boda na pia tembelea soko la Njegere pale Kigogo uone ndugu zako wanavyoshindana na Waluguru, wao na karoti, Waluguru na Njegere halafu uje utetee kijiji

Ila ujumbe wangu kwa watu wa Tukuyu, wanaume acheni umwinyi. Amkeni na wamama asubuhi kwenda shambani. Sio picha nzuri kukutana wa wamama kwenye ukungu huku vidume vimejifungia ndani vinasubiri kupambazuke vikanywe komoni na makoti yao kama tai

View attachment 1439418

huku vidume vimejifungia ndani vinasubiri kupambazuke vikanywe komoni na makoti yao kama tai

hahhaha mkuu umeua...
 
Mkuu, usisahau kazi ya palizi ya mashamba ya migomba kwa wanaume wa Tukuyu ni full time job. Yaani wanakuwa na mashamba makubwa, kwa hiyo akimaliza shamba, alikoanza magugu yanakuwa yameota. Ndio maana wanawake wanapewa kazi za palizi na kuvuna ambazo ni za msimu. Mwanaume yeyote wa Tukuyu mwenye shamba ni kwamba kila siku asubuhi ataenda kwenye kupalilia shamba la migomba, ambalo mara nyingi liko hapohapo nyumbani. Atafanya kazi hiyo hadi saa sita. Kisha anaenda kuoga mtoni. Hawana tabia ya kuoga maji ya moto pamoja na baridi ile. Ila baada ya kazi za shambani asubuhi, jioni kwenda kupiga ulabu ni kawaida!

Hahhhaa hahhhaa..i like it..kumbe hizo species za kiume huko ndo zimebaki??..lol...yaan mwanaume ukimchek unasema kwel huyu ni mwanaume..kisigino kimechanika balaa...mkono mgumuuu😅😅😅! Haelew masuala ya deodorant wala nives spray! Ohh i love that!
 
Mjini mbalizi, Mbeya, mahindi nmenunua jana ni 5000 kwa debe,
IKUTI mbeya mjini, mahindi ni tsh 6000,
Kuna utofauti mkubwa sana kati ya mahindi ya Rungwe na sehemu nyingine ya mkoa wa Mbeya na SONGWE, walaji wa ugali tunajua.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sembe la morogoro na sembe la iringa ni mbingu na ardhi..la Iringa zuri linaste poa mdomon..la moro kama limepoa..same na sembe ya songea na iringa zinapishana..songea nzuri zaidi...nadhan na ph za udongo
 
Achaga ubinafsi ndo maana wilaya haiendelei sababu ya kuwa na watu wenye mawazo finyu kama yako wageni wakija kwa wingi ndipo huwa tunapata maendeleo
Na mfumo wa maisha hubadirika jamani wageni karibu Tukuyu kupo kama Europe
Wewe bila shaka haujaishi uchagani
 
Back
Top Bottom