Rufaa dhidi ya Sabaya ngoma ngumu bado

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,370
8,107
Rufaa ya kupinga kuachiwa huru kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya imeahirishwa hadi kesho Jumanne Desember 13, 2022.

Rufaa hiyo ilikatwa na Serikali ikipinga hukumu ya kuwaachia Sabaya na wenzake watano iliyotolewa Juni 10,2022.

Juni 10,2022 Sabaya na wenzake sita walishinda kesi ya uhujumu uchumi na kuachiwa huru baada ya mahakama hiyo kubaini ushahidi uliotolewa na Jamhuri ulighubikwa na utata hivyo kushindwa kuthibitisha mashitaka yaliyokuwa yanawakabili na kuwatia hatiani.

Sabaya ambaye leo pia alikuwa na kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, ameomba kuahirisha kwa kesi hiyo kwa sababu hakuwa na uwakilishi wa mawakili mahakamani hapo.

Leo Jumatatu Desemba 12 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilipanga kuanza kusikiliza rufaa hiyo iliyokatwa na upande wa Jamhuri dhidi ya Hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Mbali na Sabaya wajibu rufaa wengine ni Enock Mnkeni, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Aidha katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27/2021 iliyotolewa uamuzi na mahakama hiyo aliyekuwa mshitakiwa wa tatu katika kesi hiyo (Watson Mwahomange) hajajumuishwa katika rufaa hiyo.

Mbele ya Jaji Salma Maghimbi, Sabaya alifikishwa mahakamani hapo huku Serikali ikiwakilishwa na mawakili wa Serikali waandamizi Patrick Mwita, Abdallah Chavula, Hebel Kihaka, Felix Kwetukia na Timotheo Mmari.

Kwa upande wake Sabaya, aliieleza mahakama kuwa hana mwakilishi na kuwa amepata wito wa mahakama leo na hakujua anakuja kufanya nini mahakamani hapo.

"Hata sasa hivi sijafahamu nipo hapa kwa sababu gani? Hivyo sijatafuta wakili na nimetoka Moshi chini ya uangalizi wa daktari naumwa,"ameeleza Sabaya

Sabaya ameiomba mahakama hiyo wiki mbili ili aweze kujiandaa na kufanya mawasiliano na mawakili wake pamoja na familia yake.

"Mheshimiwa naomba unitendee haki nahitaji wiki mbili kujiandaa kwani nina appointment na madaktari KCMC tarehe 15, na kuna mipangilio ya malipo kwa mawakili naomba unipe muda ili haki itendwe kikamilifu," Sabaya.

Baada ya maelezo hayo Jaji huyo alimweleza Sabaya kuwa rekodi zinaonyesha aliachiwa huru na Jamhuri imekata rufaa.

Kwa upande wake wakili Mwita, ameieleza mahakama kuwa kesi imepangwa kwa ajili ya kusikilizwa na hati ya wito mahakamani ilitolewa Desemba Mosi mwaka huu.

"Mheshimiwa tuna taarifa kwamba wito kwa ajili ya mjibu rufaa wa kwanza na wengine ziliwasilishwa kwa mawakili wao na mpaka tunaingia mahakamani leo asubuhi tulimuona wakili wake (Sabaya), angekuwa hana nia ya kumwakilisha angeleta notisi ya kuiarifu mahakama kuwa hamwakilishi mjibu rufaa.

"Lakini pia mjibu rufaa anaposema hajui mahakamani amefata nini inashangaza kidogo kwani baada ya kuachiwa huru upande wa mashitaka uliwasilisha mahakamani nia ya kukata rufaa na nakala ilitolewa kwa wakili wake Juni 24,2022 hivyo tunapinga ahirisho leo," Mwita.

Akiahirisha rufaa hiyo Jaji Maghimbi amesema rufaa imepangwa kusikilizwa mfululizo kwa muda wa siku tano na wakili wa Sabaya hajatoa taarifa yoyote kwa mahakama hivyo rufaa hiyo kuanza kusikilizwa kesho Desemba 13.

MWANANCHI
 
Mpka sasa gharama alizotumia ni kubwa sana kuendesha hizo kesi mbaya zaidi anatumia tu haingizi kitu siku akirudi kitaa amepukutika ameisha na yeyealizoea kula vya bure serikalini kuapmbna mtaani sio mchezo lazima adate
Alipokuwa uraiani alipora, alidhulumu majasho ya watu na kuwaonea sana wafanyabiashara sasa malipo hapa hapa acha apuluswe mpk abaki na hyo suruali aliyovaa tu
 
Back
Top Bottom