ThnkingAloud
JF-Expert Member
- Sep 13, 2017
- 606
- 621
Wataalamu wa sheria wanatueleza kuwa Quasi-Judicial Bodies kama Mabaraza ya Ardhi, Tume ya Ajira, n.k. siyo MAHAKAMA. Lakini tangu serikali (iliyokuwepo wakati huo - siyo hii ya sasa) ilipoamua kuwa mashauri kama ya Ardhi, Ajira, Kodi, n.k. kusikilizwa na Quasi-Judicial Bodies hizi kabla ya kupelekwa mahakamani, kuna mashauri yamaeamuliwa na Mabaraza ya Ardhi au Tume ya Ajira n.k. lakini maamuzi yao kutupiliwa mbali na Mahakama Kuu pale ambapo aliyeshindwa anapokata rufaa au kuomba mapitio ya Mahakama Kuu.
Cha ajabu ni kuwa kuna mashauri yaliyotupwa na Mahakama Kuu yamewahi kusikilizwa na Mahakama ya Rufaa baada ya kukatiwa rufaa na Mahakama ya Rufaa kuamua kuwa uamuzi uliotolewa na Quasi-Judicial Body husika ulikuwa ni sahihi na hivyo Mahakama ya Rufaa KU-RESTORE uamuzi ule wa Quasi-Judicial Body husika na kwa hiyo kutupilia mbali maamuzi ya Mahakama Kuu.
Hii inatokana na nini? Je ni weledi mdogo wa Jaji wa Mahakama Kuu aliyehusika kuyatupilia mbali maamuzi hayo au ni kutokana na kutawala kwa rushwa kwenye Mahakama Kuu. Yote kwa yote ni AIBU KUBWA kwa Jaji husika na uongozi mzima wa Mahakama Kuu.
Mifano iko mingi tu sina haja ya kutoa mfano.
Hongera sana Quasi-Judicial Bodies
Wakatabahu