Rudi Nyumbani! Mama Watoto

Rudi Nyumbani! Mama Watoto

Mzee

Platinum Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
13,620
Reaction score
5,868
Rudi nyumbani mama watoto, wewe ni mke wangu. Toka uondoke nyumba naiona kubwa. Wewe ni pumzi zangu, wewe ni sehemu ya maisha yangu. Nini na kipi kilichokubadili ghafla?

Kuchelewa kurudi nyumbani?. Mama watoto si unajua tunatakiwa kula, kunywa, kuvaa n.k??? Ninapochelewa si kwamba nipo nyumba ndogo mama. Natafuta pesa. Vumilia ipo siku nitawahi nawe utafurahi.

Kufanya outing mara moja moja kwa bahati???. Elewa ni ugumu wa maisha mama. Wapo wanaotamani kupata outing moja kwa mwaka wanaikosa, bado wanavumilia. Rudi nyumbani. Ipo siku tutaenda Dubai outing.

Kula mlo mmoja kwa siku?. Kumbuka kuna wanaotamani hata huo mlo mmoja wanauokosa. Please rudi nyumbani. Ipo siku nitazinyaka, utasahau yote yaliyopita.

Ama ni Hidaya??. Yule nimeshaachana naye mke wangu. Ni shetani tu alinipitia. Nakuahidi sitarudia tena.

Ama ni hizo nguo za mtumba? Usihofu mama watoto. Si unawaona wanawake wengine wanatembea uchi?

Hizo zote ni changamoto mke wangu. Maisha yangu bila wewe yamepoteza Thamani. Nakusihi rudi nyumbani. Mimi ni binadamu nina mapungufu yangu.

am just a man, am just a man.
 
Shemeji popote ulipo tafadhali rudi home Mzee wako anakuita.
 
Last edited by a moderator:
huyu si ndo aliyekuwa ana5ilia penzi la Zahra White
 
Last edited by a moderator:
Unatafuta hela usiku? Utatia akili sasa!
Weka hausigelo ili umlipe kuhalalisha matumizi ya hela.
 
Unatafuta hela usiku? Utatia akili sasa!
Weka hausigelo ili umlipe kuhalalisha matumizi ya hela.

King'asti hakuna muda myafaka wa kutafuta pesa. Niombee msamaha.

Hausigelo tena??
 
Last edited by a moderator:
Sasa kama muda muafaka wako wa kutafuta pesa ni usiku, unataka mke wa kukuchungia nyumba ama? Mi nataka uweke hausigelo ili ukirudi unakuta msosi na nguo zako zimefuliwa. No demands. Au unaonaje baba?
King'asti hakuna muda myafaka wa kutafuta pesa. Niombee msamaha.

Hausigelo tena??
 
Last edited by a moderator:
genye mbaya sana maana kama sio hizo sasa hivi umetulia tuli..
 
Sasa kama muda muafaka wako wa kutafuta pesa ni usiku, unataka mke wa kukuchungia nyumba ama? Mi nataka uweke hausigelo ili ukirudi unakuta msosi na nguo zako zimefuliwa. No demands. Au unaonaje baba?

King'asti kutafuta kwangu usiku hakuniondolei haki yangu ya "kuoa".

Kurudi asbuhi, mchana, jioni ama usiku ni swala tu la ratiba.
 
Last edited by a moderator:
Sasa kilichomuondoa kwako hakirekebishiki. Unamtaka arudi ili akubaliane na hali ama? Let her go, atapata asieyetafuta hela gizani. Na wewe tafuta asiejali kulinda fenicha zako. Simple!

King'asti!!! Wahenga walinena

Mvumilivu hula mbivu. Kwanini asizisubiri mbivu

Mchumia juani hulia kivulini. Kwanini asikisubiri kivuli. Machungu yote yatakwisha.

Kila mwenye mafanikio, kuna magumu aliyoyapitia.

Rudi nyumbani mama. Hizo no changamoto tu.
 
Last edited by a moderator:
Hahaha weeh hizo chai za 19kweusi usimuuzie dada wa watu! Nuie mkikamata mkwanja mnashikika sasa? Atakaa hapo juani na wewe ukichuma, saa ya kuvuna unatafuta wasio na sunburn wenye ngozi mororo wa kula nao vinono hehehe. lara 1 njoo umueleweshe huyu.

King'asti!!!

Nipo tayari kula kiapo mbele ya mahakama tukufu.
 
Last edited by a moderator:
Mzee ndo ujiongeze bi mkubwa arudi
 
Last edited by a moderator:
Hapa naona kama kuna mtu anacheza kombolela...
 
Back
Top Bottom