Rudi Nyumbani! Mama Watoto

Rudi Nyumbani! Mama Watoto

Last edited by a moderator:
Rudi nyumbani mama watoto, wewe ni mke wangu. Toka uondoke nyumba naiona kubwa. Wewe ni pumzi zangu, wewe ni sehemu ya maisha yangu. Nini na kipi kilichokubadili ghafla?

Kuchelewa kurudi nyumbani?. Mama watoto si unajua tunatakiwa kula, kunywa, kuvaa n.k??? Ninapochelewa si kwamba nipo nyumba ndogo mama. Natafuta pesa. Vumilia ipo siku nitawahi nawe utafurahi.

Kufanya outing mara moja moja kwa bahati???. Elewa ni ugumu wa maisha mama. Wapo wanaotamani kupata outing moja kwa mwaka wanaikosa, bado wanavumilia. Rudi nyumbani. Ipo siku tutaenda Dubai outing.

Kula mlo mmoja kwa siku?. Kumbuka kuna wanaotamani hata huo mlo mmoja wanauokosa. Please rudi nyumbani. Ipo siku nitazinyaka, utasahau yote yaliyopita.

Ama ni Hidaya??. Yule nimeshaachana naye mke wangu. Ni shetani tu alinipitia. Nakuahidi sitarudia tena.


Ama ni hizo nguo za mtumba? Usihofu mama watoto. Si unawaona wanawake wengine wanatembea uchi?

Hizo zote ni changamoto mke wangu. Maisha yangu bila wewe yamepoteza Thamani. Nakusihi rudi nyumbani. Mimi ni binadamu nina mapungufu yangu.

am just a man, am just a man.

pole kumbe haya mambo ni two way traffic yanakula kote kote
 
Back
Top Bottom