RPC Arusha na ulinganishi wa vyeo JWTZ na PT

RPC Arusha na ulinganishi wa vyeo JWTZ na PT

Kiitifaki ya kupigiwa saluti,Commisioned officer (CP) wa polisi ni sawa na commisioned officer (2lt wa nyota moja) wa Jwtz.

Chini ya Commisioned rank, vyeo hivyo huitwa other ranks.

Kwa hiyo kwa cheo chake cha ACP ukilinganisha na Jwtz ni cheo cha pili kurudi chini ya commisioned officer ambacho ni Warrant officer class2 na hata mishahara ukiichunguza inalingana.

Asijikweze, sababu hata vita vikizuka, akishikizwa jeshini, lazima atapewa mafunzo (refresher) wakufunzi wakiwa ni hao other ranks na atakasimiwa na kuvishwa vyeo vya other ranks na hilo halina ubishi ni kanuni.

Halafu tukija kwenye sheria za kijeshi (military defence act) hao civilian police ni idara za kiraia zinazofanya kazi zinazofanana na za kijeshi, wakiwemo magereza na zimamoto.
Hivyo Jwtz hawaruhusiwi kumkamata raia na kumuweka rumande za jeshi akiwemo yeye, kwa sababu anahesabika kuwa ni raia kwenye vitabu vya sheria za majeshi.
Mbona wanakamataga raia na kuwatesa humo makambini mwao?
Kifupi ni kwamba wanajeshi wanajiona wapo juu ya sheria hata ikitokea amekosea basi anatetewa na wenzake asikamatwe.
 
Mwanajeshi kuua ni suala la mtu binafsi halihusiani na kulichafua jeshi zima kama unavyotaka kuaminisha watu.

Utovu wa utu na unyama hauegemei kada ya mtu ni sawa na kuongelea mchawi.

Unapokaa nyuma ya keyboard usijisahau sana na kuanza kupakaza chuki zako binafsi kwa taasisi zenye kuheshimika na taifa.

Raia yeyote wa Tz akiwemo mwanajeshi, akitenda jinai atawajibika kwa makosa yake mwenyewe binafsi na si taasisi nzima.

Hapa mada imeanzishwa kupima ulinganifu wa vyeo, badala yake wewe unaigeuza na kuipeleka kwenye mauaji na chuki zako, what for?
Mada hii imekuja kutokana na tukio la mwanajeshi kudaiwa kumuua mkewe sasa kinachokupandisha mori nini kamanda?
Wanajeshi wengi wanazingua sana inapotokea wamegombana na raia wa kawaida na wanapata msaada jeshini inapotokea anatakiwa kuadhibiwa na taasisi za kiraia tofauti na polisi.
Ni rahisi sana mwanajeshi kugoma kukamatwa na askari polisi kisa amemzidi cheo ilhali ipo wazi kukamatwa kwake ni kutokana na yeye kutenda kosa.
Kama mnataka kujisagisha badilikeni kimtazamo.
 
Naona wanapolisi na wanajeshi wanatoana jasho.....vipi na sisi makuruta tunapiga saluti au tunasema tu jambo afande!!!
 
Katika tukio la kifo lililotokea majuzi kule Arusha likimuhusisha mwanamke(marehemu)na askari wa JWTZ. Wakati RPC wa Arusha anaongea na waandishi wa habari alitoa kauli ambayo alisema kuwa ktk vyeo vya JWTZ anayemzidi kwa cheo ni Brigedia Jenerali kwenda juu!! Najiuliza ulinganifu huu amezingatia vigezo/muongozo upi?! RPC yeye ni Assistant Commissioner of Police(ACP). Wajuzi wa haya mambo ya vyeo naomba ufafanuzi plz.
Mara kadhaa nimekuwa nikiona askari wakigombana na kutunishiana misuri na mmoja kujiona bora zaidi kuliko mwenzake tena askari wa JWTZ wamekuwa Mara kwa Mara wakiwashambulia askari hasa wa Usala barabarani mbaya zaidi wao wapo Lori moja traffic mmoja haaaaaa.Kichekesho kwenye vyeo yule wa nyota moja Jwtz anajiona bora kuliko yule wa polisi nyota moja.Haaaaaa umbumbumbu in mzigo ssna.Sheria tu ndiyo inaweza kuwapima kulingana na vyeo vyenu si kingine .Je sheria inasema nini?
SURA YA TISA KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAJESHI YA ULINZI
Ibara ya
147.-(1) Ni marufuku kwa mtu yoyote au shirika lolote au
kikundi chochote cha watu, isipokuwa Serikali kuunda au
kuweka Tanzania jeshi la aina yoyote.
(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano yaweza, kwa mujibu
wa sheria, kuunda na kuweka Tanzania majeshi ya aina
mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi
wa Tanzania.
(3) Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na
chama chohote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki
ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.
(4) Kwa madhumuni ya ibara hii, "mwanajeshi" maana yake
ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumu
katika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza au Jeshi
la Kujenga Taifa.
Madaraka ya
Amiri Jeshi Mkuu
Sheria ya 1984
Na.15 ib.49
148.-(1) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria
yoyote iliyotungwa na Bunge, miongoni mwa madaraka ya Rais
akiwa kama Amiri Jeshi Mkuu ni kuyaamuru majeshi ya nchi
yatende mambo yanayohusika na vita vya ulinzi wa Jamhuri ya
Muungano, mambo ya kuokoa maisha na mali ya watu katika
hali ya hatari na mambo mengineyo ambayo Amiri Jeshi Mkuu
ataona yahitajika, na kwa ajili hiyo Amiri Jeshi Mkuu aweza
kuyaamuru hayo majeshi yatende mambo hayo ama ndani au
nje ya Tanzania.
(2) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria
iliyotungwa na Bunge, madaraka juu ya mambo yafuatayo
yatakuwa mikononi mwa Amiri Jeshi Mkuu, yaani-
(a) madaraka ya kuwateua viongozi katika majeshi ya
ulinzi ya Jamhuri ya Muungano;
(b) madaraka ya kuwateua watu watakaojiunga na
majeshi ya ulinzi na madaraka ya kuwaondoa jeshini
wanajeshi;
(c) madaraka ya kuwateua wanajeshi watakaoongoza
Kuna mambo mengine ya kiutendaji yanawalinganisha katika sheria mfano kwenye kutuliza Fujo na kutawanya maandamano sheria inasema hivi
PENAL CODE (CAP. 16)

77. Any magistrate or, in his absence, any
police officer of or above the rank of
inspector» or any commissioned officer in
the military forces of the United Republic,
in whose view twelve ormore persons are
riotously assembled, or who apprehends
that a riot is about to be committed by
twelve or more persons assembled within his
view, may make or cause to be made a
proclamationin the president's name, in
such form as he thinks fit, commanding the
rioters or persons so assembled to disperse
peaceably.
Making
rioters todisperse
.pia askari safi kutoka jeshi LA wananchi kuwa mkuu wa wilaya no kamishina lakini hawezi kumuamrisha kamishina msaidizi wa polisi anayeongoza mkoa. Hivyo kulinganisha neno kamisha kwa maana ya nyota moja jw saw a na RPC no utoto uliopitiliza sana Saimon Siro aliongoza vikosi vya operesheni tokomeza akiwa kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi kukiwa na mameja wengi wa jwtz wakipokea maelekezo.waza kifaida nyie askari.
 
JWTZ ____polisi
Lt usu = assistance inspector
LT. = inspector
Captain =ASP
MEJA =SP
LT. COLONEL =SSP
COLONEL =ACP
BRIGEDIA GENERAL. =SACAP
MEJA GENERAL. =DCP
LT GENERAL =CP
GENERAL. =IGP

Note: wakikutana afisa wa jwtz na afisa wa polisi wanao lingana vyeo, afisa wa polisi atampigia saluti afisa wa jwtz kwa sababu JWTZ ndio jeshi SNR. But wakikutana mmoja anamzidi mwingine cheo, protoco za kijeshi lazima zifuatwe mdogo kumsalimia mkubwa.
100%....
Nimekugongea na LIKE....
 
Nachojua kwenye Vita ya Kagera askari Polisi na Magereza walikuwa wanalia wakiitwa kwenda kwenye mapambano. Unatambua utofauti wa JWTZ na idara nyingine pale nchini inapokuwa vitani au mapinduzi.
 
Kwa tpdf huu ni mfumo wa zamani, Kuanzia brigadier general format imebadilika
Vyeo vya Polisi
1.Constable =Plain uniform (Hana nembo yyte)
2.Coplo =V 1
3.Sajent =V 2
4.Sajent staff =V 2+ ngao
5.inspector msaidizi =Nyota 1
5.Inspector =Nyota 2
6.Sajent Meja =Ngao 1
7.S.A.C.P (kamishina msaidizi mwandamizi)=Nyota 2+ngao 1+nembo ya Taifa.
8.A.C.P(kamishina msaidizi)=kamishina msaidizi =nyota 1+nembo ya Taifa
9.S.S.P(Mkaribu mwandamizi)=Nyota 1+ngao moja.
10.A.S.P(mkaribu msaidizi)=nyota 3.
11.S.P(mkaribu )=ngao+nembo ya Taifa
12.D.C.P(Naibu kamishina)=Mkuki + nyota
13.C.P(kamishina)=Mkuki na nembo ya Taifa
14.I.G.P=mkuki+ngao +nembo ya Taifa

JWTZ
1.Private =Plain uniform
2.koplo mdogo =V1
3.koplo =v2
4.Sajent =V 3
5.Sajent mtumish=V 2+nembo ya Taifa
6.maafisa wateule II=nembo ya taifa
7.maafisa wateule I=alama ya taifa+ngao
8.Luten I= Nyota 1
9.Luten II= Nyota 2
10.captain =Nyota 3
11.Meja = alama ya Taifa
12.Luten canal = Nyota na alama ya Taifa
13.kanali =Nyota 2 na alama ya Taifa
14.Brigedia general =nyota 3 na nembo ya Taifa
15.Brigedia =Nyota 3 ,nembo ya Taifa na ngao
16.Meja general = Mkuki + nembo ya Taifa
17.Luten general = Mkuki na nyota + nembo ya Taifa
18.General =mkuki +nyota mbili +nembo ya Taifa.
 
Nachojua kwenye Vita ya Kagera askari Polisi na Magereza walikuwa wanalia wakiitwa kwenda kwenye mapambano.
Lakini Mgambo na wale walopitia JKT walikwenda tena front line....
Nakumbuka kipindi hicho cha vita ya Kagera Niko std 3 na Mwl wangu mmoja alikwenda pigana vita hiyo...
 
Nakuelewesha! Brigedia Generali pale takukuru yupo chini ya Kamishna wa Polisi! Usiwakuze sana hao JWTZ as if they are so special compared to others! Everyone is special in his or her field!
Ujue kutofautisha kati ya cheo na madaraka ndugu
 
IGP( inspector general of police), CDF( chief of defence forces). Siro ni mkuu wa police Tanzania na mabeyo ni mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ndani ya Tanzania. Kiprotocal ACP( assistant commissioner ) hawezi kuwa sawa na colonel
 
Back
Top Bottom