RPC Arusha na ulinganishi wa vyeo JWTZ na PT

RPC Arusha na ulinganishi wa vyeo JWTZ na PT

Tafsiri ya Jeshi ni: Jumla ya watu wanaopewa mamlaka ya kutumia nguvu ya silaha kutetea nchi kwa niaba ya Dola dhidi ya maadui wa nje.

Niambie wewe ni wapi Duniani idara ya Polisi ikaitwa Jeshi?
Tanzania
 
Mkuu hivi vyeo vya JW ulivoviweka ni vya kitambo sana havipo kwa sasa! Utaratibu uliopo ni

Brigedia General hana nyota tatu,ana nyota moja pamoja nembo ya taifa na mkasi!

Hakuna cheo cha Brigedia ila Brigedia General baada ya hapo ni Meja General.

Meja General ana nyota mbili na nembo ya taifa pamoja na mkasi.

Luteni General na nyota tatu nembo na mkasi

General ni nyota tano na baadhi vitu vyake nimesahau kidogo
Ahsante Mkuu kwa kunisahihisha....
 
Mara kadhaa nimekuwa nikiona askari wakigombana na kutunishiana misuri na mmoja kujiona bora zaidi kuliko mwenzake tena askari wa JWTZ wamekuwa Mara kwa Mara wakiwashambulia askari hasa wa Usala barabarani mbaya zaidi wao wapo Lori moja traffic mmoja haaaaaa.Kichekesho kwenye vyeo yule wa nyota moja Jwtz anajiona bora kuliko yule wa polisi nyota moja.Haaaaaa umbumbumbu in mzigo ssna.Sheria tu ndiyo inaweza kuwapima kulingana na vyeo vyenu si kingine .Je sheria inasema nini?
SURA YA TISA KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAJESHI YA ULINZI
Ibara ya
147.-(1) Ni marufuku kwa mtu yoyote au shirika lolote au
kikundi chochote cha watu, isipokuwa Serikali kuunda au
kuweka Tanzania jeshi la aina yoyote.
(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano yaweza, kwa mujibu
wa sheria, kuunda na kuweka Tanzania majeshi ya aina
mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi
wa Tanzania.
(3) Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na
chama chohote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki
ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.
(4) Kwa madhumuni ya ibara hii, "mwanajeshi" maana yake
ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumu
katika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza au Jeshi
la Kujenga Taifa.
Madaraka ya
Amiri Jeshi Mkuu
Sheria ya 1984
Na.15 ib.49
148.-(1) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria
yoyote iliyotungwa na Bunge, miongoni mwa madaraka ya Rais
akiwa kama Amiri Jeshi Mkuu ni kuyaamuru majeshi ya nchi
yatende mambo yanayohusika na vita vya ulinzi wa Jamhuri ya
Muungano, mambo ya kuokoa maisha na mali ya watu katika
hali ya hatari na mambo mengineyo ambayo Amiri Jeshi Mkuu
ataona yahitajika, na kwa ajili hiyo Amiri Jeshi Mkuu aweza
kuyaamuru hayo majeshi yatende mambo hayo ama ndani au
nje ya Tanzania.
(2) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria
iliyotungwa na Bunge, madaraka juu ya mambo yafuatayo
yatakuwa mikononi mwa Amiri Jeshi Mkuu, yaani-
(a) madaraka ya kuwateua viongozi katika majeshi ya
ulinzi ya Jamhuri ya Muungano;
(b) madaraka ya kuwateua watu watakaojiunga na
majeshi ya ulinzi na madaraka ya kuwaondoa jeshini
wanajeshi;
(c) madaraka ya kuwateua wanajeshi watakaoongoza
Kuna mambo mengine ya kiutendaji yanawalinganisha katika sheria mfano kwenye kutuliza Fujo na kutawanya maandamano sheria inasema hivi
PENAL CODE (CAP. 16)

77. Any magistrate or, in his absence, any
police officer of or above the rank of
inspector» or any commissioned officer in
the military forces of the United Republic,
in whose view twelve ormore persons are
riotously assembled, or who apprehends
that a riot is about to be committed by
twelve or more persons assembled within his
view, may make or cause to be made a
proclamationin the president's name, in
such form as he thinks fit, commanding the
rioters or persons so assembled to disperse
peaceably.
Making
rioters todisperse
.pia askari safi kutoka jeshi LA wananchi kuwa mkuu wa wilaya no kamishina lakini hawezi kumuamrisha kamishina msaidizi wa polisi anayeongoza mkoa. Hivyo kulinganisha neno kamisha kwa maana ya nyota moja jw saw a na RPC no utoto uliopitiliza sana Saimon Siro aliongoza vikosi vya operesheni tokomeza akiwa kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi kukiwa na mameja wengi wa jwtz wakipokea maelekezo.waza kifaida nyie askari.
Ahksnte kwa kuweka Walau hoja zenye mashiko
 
Vyeo vya Polisi
1.Constable =Plain uniform (Hana nembo yyte)
2.Coplo =V 1
3.Sajent =V 2
4.Sajent staff =V 2+ ngao
5.inspector msaidizi =Nyota 1
5.Inspector =Nyota 2
6.Sajent Meja =Ngao 1
7.S.A.C.P (kamishina msaidizi mwandamizi)=Nyota 2+ngao 1+nembo ya Taifa.
8.A.C.P(kamishina msaidizi)=kamishina msaidizi =nyota 1+nembo ya Taifa
9.S.S.P(Mkaribu mwandamizi)=Nyota 1+ngao moja.
10.A.S.P(mkaribu msaidizi)=nyota 3.
11.S.P(mkaribu )=ngao+nembo ya Taifa
12.D.C.P(Naibu kamishina)=Mkuki + nyota
13.C.P(kamishina)=Mkuki na nembo ya Taifa
14.I.G.P=mkuki+ngao +nembo ya Taifa

JWTZ
1.Private =Plain uniform
2.koplo mdogo =V1
3.koplo =v2
4.Sajent =V 3
5.Sajent mtumish=V 2+nembo ya Taifa
6.maafisa wateule II=nembo ya taifa
7.maafisa wateule I=alama ya taifa+ngao
8.Luten I= Nyota 1
9.Luten II= Nyota 2
10.captain =Nyota 3
11.Meja = alama ya Taifa
12.Luten canal = Nyota na alama ya Taifa
13.kanali =Nyota 2 na alama ya Taifa
14.Brigedia general =nyota 3 na nembo ya Taifa
15.Brigedia =Nyota 3 ,nembo ya Taifa na ngao
16.Meja general = Mkuki + nembo ya Taifa
17.Luten general = Mkuki na nyota + nembo ya Taifa
18.General =mkuki +nyota mbili +nembo ya Taifa.
Huu ulioandika ni uongo mtupu, hivi kuna koplo mwenye v1 au sajenti mwenye v2?? Acha uongo
 
Ujue kutofautisha kati ya cheo na madaraka ndugu
Cheo kijeshi, kinaendana na madaraka kijana! Wewe unadhani anaweza kuwepo CDF ambaye cheo chake ni Kanali wakati huo huo Luteni Generali yupo, na major generali yupo??
 
Kulinganisha vyeo vya Jeshi na vyeo vya Polisi ni ujuha uliopitiliza kwasababu ya tofauti kubwa ya mafunzo yao aidha kumlinganisha Commision officer na Gazetted officer siyo sahihi ni muhimu polisi na jeshi kuheshimiana na kupendana bila kujilinganisha
 
Nimeshangaa Coplo V moja[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Sir mejaa jee..[emoji15][emoji15]
Huyu jamaa muongo sana, nimesoma post yake kisha nikasema khaa! [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2445][emoji2445][emoji2445][emoji377][emoji377][emoji377]
 
Asante sana kamanda kwa elimu sasa hii Luteni Usu inaingia wapi hapo au kitu ksma Sir Major au ni maneno ya mitaani ?

Luten USU _ofisa wa jeshi wa cheo cha kwanza chini ya luteni.
Sir major ni vyeo vya kikolon...ni sawa na major tu ....na hawa ni wale waliokuwa wanaongoza vikos vya kijeshi nje ya Taifa la muingereza....hivo anatunukiwa heshima ya sir na Malkia...nimesema kwa hofu hivo sina hakika sana 100%
 
Tafsiri ya Jeshi ni: Jumla ya watu wanaopewa mamlaka ya kutumia nguvu ya silaha kutetea nchi kwa niaba ya Dola dhidi ya maadui wa nje.

Niambie wewe ni wapi Duniani idara ya Polisi ikaitwa Jeshi?
ni tanzania.

unataka kuiga mpaka uone kitu kwa watu kwanza,nikuulize.

ni nchi gani mwanajeshi anapanga uraiani?
 
Back
Top Bottom