Royal Tour: Rais Samia asimama Jimbo la Kawe na kusikiliza wananchi kupitia Mbunge wao, Askofu Gwajima

Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
7,687
2,000
kweli kabisa. Maana kwa fikra za kawaida hii nchi inavyokwenda ni kama haina mwenyewe. Leo linaamuliwa jambo na kutangazwa, kesho linafutwa na mbaya zaidi anaepaswa kutoa kauli hata hajui kinachoendelea. Ni kama vile na yeye anagundua mambo mengi baada ya kutangazwa. Ni wazi hayupo sehemu ya maamuzi aidha kwa kuogopa majukumu ama kwa kusudio la waliomuweka

as long as zanzibar is progressing under hussein mwinyi. she doesnt care about Tanganyika. atakula bata kwenda mbele. Akina majaliwa wasiposhtuka wakafanya kazi na kusimamia wizara na idara kwa umakini 2025 watapata shida sana ilhali yeye atakuwa on her way to Makunduchi for retirement
 

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
1,703
2,000
Shida za wananchi zimeisha maza yupo busy na filamu
Mtaelewa tu, mtake msitake. Anachonifurahisha huyu mama ni huu mwendo wake mdogo mdogo na kimya kimya.....kama haoni au hataki vileeee kumbe anaupiga mwingi hatari. Kabla ya kuzungumza kidhihaka kuhusu hiyo filamu, yapaswa kuielewa kwanza; hii si filamu ya kina wema sepetu ya kuonyesha uzuri na uzungu!
 

ruaharuaha

JF-Expert Member
Feb 14, 2018
2,009
2,000
Tukio liko mubashara ITV

Rais Samia akiwa na mbunge wa Kawe wanahutubia wananchi wa jimbo la Kawe eneo la Tegeta manispaa ya Kinondoni.

Kwa sasa askofu Gwajima amepanda kwenye gari ya Ikulu na anatoa salamu za shukrani kwa Rais Samia kwa niaba ya wananchi.

Gwajima anasema wananchi wa Kawe siyo tu Wanampenda mama Samia bali wana mahaba naye.

Helicopter za polisi zinavinjari juu ya anga kuulinda mkutano huu mtakatifu.

Rais Samia amewataka wananchi waendelee kulipa kodi kwani kodi ni kwa maendeleo ya taifa.

Rais Samia amesema anaelekea Bagamoyo katika mtiririko wa uchukuaji picha ya filamu ya vivutio vya utalii wa Tanzania itakayozinduliwa nchini Marekani na kuonyeshwa dunia nzima.

Karibu

========

Katika ziara hiyo Rais Samia pia amekutana na Mbunge wa Kawe Askofu Gwajima, ambapo Rais ameuhoji umma: “Tunachanja, hatuchanji?” Huku wananchi wakijibu “Tunachanja!”

Askofu Gwajima pia ameshukuru kwa kupata Bilioni 8 kwa ajili ya kurekebisha mitaro ya Kata ya Mbweni ili kudhibiti mafuriko kipindi cha mvua.

“Jambo lingine, ulitupa kila jimbo milioni 500 kwa ajili ya barabara lakini kwenye Jimbo la Kawe ukatupa bilioni 14, ambazo tunatengeneza barabara 115 za jimbo la Kawe za naani kwa mkono wa TARURA.”,

“Shida ya maji iliyokuwepo Nakasangwe, iliyokuwepo Kisanga, tayari matenki yameshajengwa katika maeneo mbalimbali na sasa kuanzia mwezi wa 10 tarehe 15 mradi wa maji yanayotokea Ruvu Chini utakuwa umeshafika Kawe.”

Hii Royal Tour ni wazo zuri sana, apite na kwenye mbuga, beach, kusini, Tanga, bila kuisahau Ruaha
 

ruaharuaha

JF-Expert Member
Feb 14, 2018
2,009
2,000
Kuna baadhi ya mambo yanafikirisha sana awamu hii. Sasa kama Raisi anazunguka kupiga picha za utalii, Waziri wa maliasili anafanya nini?
Hili linadhihirisha kuwa kuna driving force nyuma ya tunaemuona raisi, kwa maana ana Job Description katengenezewa na kuna anao report kwao na kumwambia cha kufanya. In other words yeye ni sura tu ya uraisi.
Sikuwahi mpenda Magufuli mpaka anakufa ila Magufuli alikuwa shujaa katika kusimama na maamuzi na kujua hasa nguvu yake kama raisi. Mpaka 2025 ambapo nina hakika ndio ukomo wa mtangaza utalii, tutaona mengi sana

Kutangaza utalii ni jambo jema sana, nguvu kubwa ni vizuri imekweze hapo na kwenye miundombinu ta utalii, huduma nzuri, first class service kuanzia website, airport, barabara, ndege, hoteli, usafiri.

Akikomaa vizuri na utalii, kilimo, madini atatoboa. Nguvu hiyo hiyo iwekweze kwenye kilimo na kutafuta masoko nje kutangaza mazao / bidhaa zetu na ubora wake.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
50,077
2,000
Mtaelewa tu, mtake msitake. Anachonifurahisha huyu mama ni huu mwendo wake mdogo mdogo na kimya kimya.....kama haoni au hataki vileeee kumbe anaupiga mwingi hatari. Kabla ya kuzungumza kidhihaka kuhusu hiyo filamu, yapaswa kuielewa kwanza; hii si filamu ya kina wema sepetu ya kuonyesha uzuri na uzungu!
Shirikiana naye sasa
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
6,918
2,000
Waulize Dr Slaa na Dr Mashinji.

Labda kama huyo J J Mnyika mnamdhulumu!
Hao si wako kwenu? Na kama imeandikwa kwenya Katiba kuna haja gani ya kuwauliza wakati unaweza kutaja tu kifungu kinacho husika?
Katiba ya Chadema hii hapa. Taja kifungu kinachosema Katibu Mkuu wa Chadema atalipwa mshahara unaolingana na mbunge. Mimi sijakiona.


Tabia ya uongo sio nzuri hata kidogo.

Amandla...
 

Otterhound

JF-Expert Member
Sep 10, 2016
2,555
2,000
Huyu mama anaakili mingi mno,,hatumii pawa ni akili tuuu. Miaka miwili inamtosha mno mpinga chanjo na yule anaetembea na furushi la vitabu/bibilia utazani anaenda kuhubili 🤣
 

Katavi yetu

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
1,129
2,000
Kwani gwajima si atawajibishwa na chama kupitia kamati za maadili za chama na mikutano mikuu ya halmashauri kuu ya chama n.k,hata Kama mama anamchukia hawezi kumuoneshea pale pale hadharani,Kama kweli anamakosa lazima atawajibishwa tu ndani ya chama.

Lakini pia mama si alishaliambia bunge kwamba linademuka na mambo ya kwenye mitandao,ngoma zinapigwa mitandao wanaodemuka ni wabunge wakiwa bungeni.
 

Shehullohi

JF-Expert Member
Jul 21, 2020
2,432
2,000
Kama yule Kingu ndio bure kabisa!

Watu kama hawa ndio viongozi tena Waheshimiwa wabunge ambao uwezo, Hekima na Busara zitokazo kwa Mungu wa Mbinguni ni zina walakini.

Ndio sababu wakati mwengine unamsikitia Mh Rais anapoongea kwa lugha ya kama kukashifu ama tuseme mipasho eti " kelele za mitandaoni hazimpi shida na mombo kama hayo." Unabakia ukistaajabu tu.

Ajiongeze na ajue faida ya hii mitandao na yanayo ongelewa humu. Wako watu wenye uwezo mkubwa kiAkili , Kibusara na Hekima ambao kimsingi ni karama walizojaliwa na Mungu wao. Tuna soma humuhumu mitandaoni hoja za nguvu kubwa za kiuongozi na ufumbuzi wa mambo muhimu ya nchi. Wako watu humu wenye uwezo mzuri sana kuliko baadhi ya watu wanao msaidia kazi na kumzunguka Mh Rais.

Ingekuwa busara kwa Mh Rais akaona ni muhimu kuchukua na kuyafanyia kazi yale mazuri na muhimu yanayoongelewa mitandaoni kuliko kuongea kijumlajumla tu kuwa kelele za mlangoni hazimnyimi mwenye nyumba kulala usingizi wake. Hata asipokubali huu ukweli mambo ya msingi yanayo ongelewa mitandaoni hatimaye yatamnyima usingizi tu ama angalau kulala usingizi wa mangamungamu asipochukua hatua sahihi na kuyafanyia kazi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom