Royal Tour: Rais Samia asimama Jimbo la Kawe na kusikiliza wananchi kupitia Mbunge wao, Askofu Gwajima

Mama anampiga kijembe cha haja "Gwajiboy" kwa kuuliza kwa kusanifu...."Kawe tunachanja ama hatuchanji"...naona Gwajiboy ameshikwa na kidaka...."Ana-smile" Ni hakika Moyoni ananajua mtihani huo:) teh teh teh...Anaikwepa kuijbu kistaaarabu kauli hiyo ya Mama anabakia kusema... "Mama watu wa Kawe wana mahaba na wewe...:)

Kweli..."Siasa si hasa" Period!
 
Watu wa maadili pale mjengoni watanuna!

Mh Rais wa JMT kaustukia mchezo wa Kiongozi wa Bunge alikuwa hamsaidii bali alitaka kuonesha IGP/CPL kakosea na kuonesha dharau. Pia ni kama kutaka kuonesha anasimama na Mh Rais kuliko hao wa wizara ya mambo ya ndani na ile ya sheria/ Mwanasheria Mkuu wa Serikali .

Mh Rais kafanya vizuri kuongea kwa kusisitiza kwamba chanjo ni hiari na mtu mzima mwenye akili timamu hatakiwi kupangiwa afanye maamuzi gani juu ya chanjo. Kwa kweli hili na apongezwe sana sana na ndicho wengine tulichokitaka. Lakini asiishie hapo ajipange atafanya nini kama mkuu wa nchi kuwalinda walio amua kuchagua hiari ya kuto chanja, pale wenye chanjo watakapoanza kuleta masharti ya kibaguzi na ukandamizaji. USA watu wanafukuzwa kutoka kwenye ajira zao kwa vile wamekataa kuchanjwa.
 
Hayo ma helkopta yanayodhurula angani ni kufuja pesa tu.
Ni nani anampango na nyie wadhulumati?
Au mnamwogopa Hamza?
 
Tukio liko mubashara ITV

Rais Samia akiwa na mbunge wa Kawe wanahutubia wananchi wa jimbo la Kawe eneo la Tegeta manispaa ya Kinondoni.

Kwa sasa askofu Gwajima amepanda kwenye gari ya Ikulu na anatoa salamu za shukrani kwa Rais Samia kwa niaba ya wananchi.

Gwajima anasema wananchi wa Kawe siyo tu Wanampenda mama Samia bali wana mahaba naye.

Helicopter za polisi zinavinjari juu ya anga kuulinda mkutano huu mtakatifu.

Rais Samia amewataka wananchi waendelee kulipa kodi kwani kodi ni kwa maendeleo ya taifa.

Rais Samia amesema anaelekea Bagamoyo katika mtiririko wa uchukuaji picha ya filamu ya vivutio vya utalii wa Tanzania itakayozinduliwa nchini Marekani na kuonyeshwa dunia nzima.

Karibu

========

Katika ziara hiyo Rais Samia pia amekutana na Mbunge wa Kawe Askofu Gwajima, ambapo Rais ameuhoji umma: “Tunachanja, hatuchanji?” Huku wananchi wakijibu “Tunachanja!”

Askofu Gwajima pia ameshukuru kwa kupata Bilioni 8 kwa ajili ya kurekebisha mitaro ya Kata ya Mbweni ili kudhibiti mafuriko kipindi cha mvua.

“Jambo lingine, ulitupa kila jimbo milioni 500 kwa ajili ya barabara lakini kwenye Jimbo la Kawe ukatupa bilioni 14, ambazo tunatengeneza barabara 115 za jimbo la Kawe za naani kwa mkono wa TARURA.”,

“Shida ya maji iliyokuwepo Nakasangwe, iliyokuwepo Kisanga, tayari matenki yameshajengwa katika maeneo mbalimbali na sasa kuanzia mwezi wa 10 tarehe 15 mradi wa maji yanayotokea Ruvu Chini utakuwa umeshafika Kawe.”
Gwajima,
Amepanda mapa ya mwisho,mwezi ujao anavuliwa uanachama na maccm .
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom