Askofu Gwajima: Zaidi ya wanachama 500 wapya wajiunga CCM Jimbo la Kawe

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
Mbunge wa Jimbo la Kawe Askofu Dkt. Josephat Gwajima (MNEC) ameandikisha zaidi ya wanachama 500 Wapya wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Bunju Mtaa wa Boko Chama 02-07-2023

 

Attachments

  • 343247A6-E52E-48B9-8B65-7EEDBC6D6CD8.jpeg
    343247A6-E52E-48B9-8B65-7EEDBC6D6CD8.jpeg
    24.4 KB · Views: 5
  • 7E1D868E-B324-4473-8DFB-68012F06CD94.jpeg
    7E1D868E-B324-4473-8DFB-68012F06CD94.jpeg
    58 KB · Views: 4
  • 8A1AE1BB-C5A4-4252-814A-5285BFB72379.jpeg
    8A1AE1BB-C5A4-4252-814A-5285BFB72379.jpeg
    79.5 KB · Views: 5
  • 2EB7BEBB-17BA-41F6-BEBD-9A3A7F2CC790.jpeg
    2EB7BEBB-17BA-41F6-BEBD-9A3A7F2CC790.jpeg
    32 KB · Views: 5
  • 79BF2FF4-015A-4458-A2E8-E1C0366B506B.jpeg
    79BF2FF4-015A-4458-A2E8-E1C0366B506B.jpeg
    55.3 KB · Views: 4
  • 66378CB0-C277-472D-A008-F927D71C14CA.jpeg
    66378CB0-C277-472D-A008-F927D71C14CA.jpeg
    131.1 KB · Views: 4
  • FABEC48E-B2A0-49C7-8888-DC784E92CE7D.jpeg
    FABEC48E-B2A0-49C7-8888-DC784E92CE7D.jpeg
    150.5 KB · Views: 5
  • 44CE837E-0120-46F8-8AB0-6151A41F6659.jpeg
    44CE837E-0120-46F8-8AB0-6151A41F6659.jpeg
    75.7 KB · Views: 5
  • D7429672-DECD-4779-AC3C-C134038CEEA7.jpeg
    D7429672-DECD-4779-AC3C-C134038CEEA7.jpeg
    55.1 KB · Views: 4
ASKOFU KANISA KATOLIKI AIBUA TUHUMA KUWA MCHANGA UNACHIMBWA BONDE LA MTO MSIMBAZI NA KUPELEKWA VISIWANI!

Mhashamu Baba Askofu Severine Niwemugizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge-Ngara, Kagera ameibua tuhuma kuhusu uharibifu wa mazingira eneo la Segerea kando kando ya Mto Msimbazi, Dar es Salaam. Anasema kuwa kuna taarifa mchanga unachimbwa pale unapelekwa Visiwani. Anasema kuwa Mkuu wa Seminary ya Segerea alipofuatilia ili kukomesha zoezi hilo alipatiwa vitisho. Anasema kuwa hata Polisi wa Staki Shari wana taarifa lakini wanaogopa shari wamekaa kimya kwani mamlaka za juu zinajua na zimeruhusu. Je, mamlaka gani zilizoruhusu uharibifu huo? Sisi Askofu Mwamakula tuko na na Askofu Niwemugizi kupazia sauti jambo hili. Soma ujumbe wake hapa chini kisha sambaza:

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.
Dar es Salaam, 3 Julai 2013; 13:30 pm.

"Hiyo picha chini inaonyesha janga la uharibifu wa mazingira eneo la Segerea, mto Msimbazi! Miaka 27 iliyopita mto huu haukuwa mpana hivi. Palikuwa na daraja unavuka toka pale seminari kuja Sitakishari. Daraja halikuzidi mita kumi na tano. Nimerudi kuona leo hali nikakuta panatisha. Daraja liliondoshwa na maji na mto umepanuka vya kutisha.

Mmomonyoko umeshika kasi. Lakini ungekuwa huo tu ingekuwa nafuu. Lakini sasa kuna uchimbaji wa kutisha wa mchanga. Nimekuta mashine ziko pale na magari ya kuusomba. Nilipouliza kulikoni nikaambiwa ni kazi ya kusafisha kingo za mto! Na mamlaka za juu kabisa zimeruhusu. Lakini za ndani zaidi zinasema mchanga huo unachimbwa kwenye huo mto na kusafirishwa hadi visiwa vya Karafuu! Hakuna wa kuzuia kazi hiyo, asiyejipenda tu ndiye atajaribu kupiga kelele za kuzuia.

Kumbe mamlaka ya Seminari Kuu ya Segerea yamejitahidi bila mafanikio kuzuia uharibifu huo. Na hata vitisho vimekwisha tolewa kwa Mkuu wa seminari alipojaribu kufuatilia ili uharibifu huo ukomeshwe. Polisi Sitakishari wakataarifiwa juu ya vitisho na sasa ni kimya lakini uharibifu unaendelea!

Hapa kuna utata kidogo. Huu usafishaji wa kingo za mto unafanyika eneo moja tu la Segerea? Viongozi wetu wanazungumza sana juu ya utunzaji wa mazingira, lakini kwa pale sauti hizo zinanyamaa!! Kuna ruhusa rasmi ya kuharibu, kwa nini? Wanaharakati wa mazingira hapo mmeishapaona? Kama bado nendeni mjionee na mfanye kitu tafadhali."

Na Askofu Severine Niwemugizi. 3 Julai 2023.
 

Attachments

  • 3A08E490-E262-4A55-9972-080A4E72A809.jpeg
    3A08E490-E262-4A55-9972-080A4E72A809.jpeg
    52 KB · Views: 4

Similar Discussions

Back
Top Bottom