Royal Tour: Rais Samia asimama Jimbo la Kawe na kusikiliza wananchi kupitia Mbunge wao, Askofu Gwajima

mjusilizard

JF-Expert Member
Nov 7, 2019
761
1,000
Mnyama sana huyu jamaa. Ila gwaji Yuko Vizuri Sana Yani anajuwa kula na kipofu .
Namkubali sana huyu mwamba
 
AGITATOR

JF-Expert Member
Apr 7, 2019
1,972
2,000
Tukio liko mubashara ITV

Rais Samia akiwa na mbunge wa Kawe wanahutubia wananchi wa jimbo la Kawe eneo la Tegeta manispaa ya Kinondoni.

Kwa sasa askofu Gwajima amepanda kwenye gari ya Ikulu na anatoa salamu za shukrani kwa Rais Samia kwa niaba ya wananchi.

Gwajima anasema wananchi wa Kawe siyo tu Wanampenda mama Samia bali wana mahaba naye.

Helicopter za polisi zinavinjari juu ya anga kuulinda mkutano huu mtakatifu.

Rais Samia amewataka wananchi waendelee kulipa kodi kwani kodi ni kwa maendeleo ya taifa.

Rais Samia amesema anaelekea Bagamoyo katika mtiririko wa uchukuaji picha ya filamu ya vivutio vya utalii wa Tanzania itakayozinduliwa nchini Marekani na kuonyeshwa dunia nzima.

Karibu

========

Katika ziara hiyo Rais Samia pia amekutana na Mbunge wa Kawe Askofu Gwajima, ambapo Rais ameuhoji umma: “Tunachanja, hatuchanji?” Huku wananchi wakijibu “Tunachanja!”

Askofu Gwajima pia ameshukuru kwa kupata Bilioni 8 kwa ajili ya kurekebisha mitaro ya Kata ya Mbweni ili kudhibiti mafuriko kipindi cha mvua.

“Jambo lingine, ulitupa kila jimbo milioni 500 kwa ajili ya barabara lakini kwenye Jimbo la Kawe ukatupa bilioni 14, ambazo tunatengeneza barabara 115 za jimbo la Kawe za naani kwa mkono wa TARURA.”,

“Shida ya maji iliyokuwepo Nakasangwe, iliyokuwepo Kisanga, tayari matenki yameshajengwa katika maeneo mbalimbali na sasa kuanzia mwezi wa 10 tarehe 15 mradi wa maji yanayotokea Ruvu Chini utakuwa umeshafika Kawe.”

Acha unafiki, wananchi tulijibu HATUCHANJI.
 
magu2016

JF-Expert Member
Oct 8, 2017
6,529
2,000
Mimi nangoja ibada ya Jumapili ijayo kwenye Kanisa la Ufufuo na Uzima nisikie Gwaji atasema nini tena!
Tusijekushangaa amefanya U-turn!
Kutokana na Viongozi wa dini kujiingiza kwenye siasa za nchi hii,hawaaminiki tena!
 
bulabo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
443
500
RAIS nimesikia ujenzi wa barabara za Jimbo la KAWE inafurahisha kwa kweli. Na sisi RAIS tunaomba utukumbuke watu wa UKONGA barabara zetu mashimo makubwa sana.

Mbunge wetu sina hakika kama anapambana. Nimemsikia GWAJIMA alivyosema Jimbo limepewa bil14 kwa ajili ya barabara 114 za mtaa inafurahisha sana. Sisi Ukonga tumrogwa na nani??
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
23,870
2,000
..hivi Maza ataweza kushawishi Wamarekani waje kutembelea vivutio vya utalii hapa Tanzania?

..Yaani tangazo la utalii kwa Wamarekani tunamuweka Maza mbele na tukitarajia muitikio mzuri?

..Je, tumejaribu kuwa-study watalii wa Marekani ni watu wa aina gani, umri, tamaduni zao, silka zao, n.k?

Cc Chige, Kamundu, Geza Ulole
 
Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
4,720

Hii program ambayo Raisi ana rekodi sio kwa utalii pekee lengo kubwa ni kubadilisha fikra za watu wa nje kuhusu Tanzania hivyo kuongeza utalii, uwekezaji, na kuangaliwa tofauti. Hii walifanya Rwanda na sasa wanajulikana kwa vitu vingine zaidi ya kuuwana wenyewe kwa wenyewe.

Kuhusu Utalii wa US.

US kuna watalii wa aina nyingi sana

1. Watalii wa uwindaji hawa ni matajiri wanaopenda kuwinda na wanapewa vitalu. Wengi wanataoka hapa Texas matajiri wa mafuta. Hawa ni matajiri sana na wanakuja na ndege zao na kutua viwanja vya Arusha wengi hawa hawatabadilika maana wanajua Tanzania
2. Watalii wa vikundi vya elimu, Afya na dini hawa wataongezeka. Hawa ni wale wanaokuja kwa makundi na wanapenda kwenda sehemu yenye usalama maana wengi ni vijana wa vyuo au makundi ya kidini. Tanzania ilishaanza kuonekana kama nchi ya unyanyasaji kwenye vyombo na hii itabadilisha hilo
3. Watalii wa kawaida wa mbuga. Mtalii mmoja inakugarimu sio chini ya $10,000 kwa safari ya siku saba tu. Hivyo ni lazima tuelewe ni gharama kubwa sana kwenda Tanzania na kuna watu wengi wanataka kwenda lakini hawana uwezo huo. Mfano familia ya watoto wawili na watu wanne wanatumia $30,000-$40,000 kwa wiki tu. Hii wengi hawajui hivyo tatizo la kwanza ni gharama kubwa. Tanzania kwa sasa hasa Zanzibar imepata umashuhuri sana miaka ya karibuni na kitu ambacho Raisi atasaidia ni kuongeza sehemu za watalii kwenda zaidi ya mbuga zetu lakini inabidi gharama ziwe rafiki.
4. Wawekezaji kwenye wawekezaji hii program ndiyo itasaidia zaidi. Uwekezaji hasa kwenye utalii kama ujenzi wa hoteli sehemu mbalimbali utaongezeka. Vilevile kama Rwanda tutaweza ku brand vitu vyetu kama Rwanda kwenye kahawa au kutengeneza magari n.k. Hivyo ni kubadilisha ule woga Magufuli aliyouweka kwa wawekezaji kufikiri wanaweza kufilisiwa tu bila sababu. Hii ni kama kampeni ya kujisafisha na kuongeza uwekezaji.
 
Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
43,833

kwa Wamarekani na general western culture kuvaa ushungi ni sign against women emancipation! Refer Burka views in the West!
 
..mtalii wa kimarekani sio rahisi kushawishiwa na mama mtu mzima aliyevaa ushungi kuja kutembelea fukwe za bahari za tanzania.

..namheshimu rais samia na naamini ana nia njema, but she can not do everything, pia siyo mjumbe sahihi kwa hadhira wanayotaka kuishawishi.

..tatizo la Tanzania ni kwamba Raisi ndio kila kitu. Hata kutangaza utalii tunataka afanye Raisi.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
23,870
2,000
kwa Wamerekani na general western culture kuvaa ushungi ni sign against women emancipation! Refer Burka views in the West!

..exactly.

..wakaangalie Wamarekani wanavyovaa, na wanapenda nini wanapotembelea fukwe za bahari, halafu wajiulize kama Maza ni mtu sahihi kuwavutia waje Tz.

..program yao ina malengo mazuri, lakini siamini kama wanatumia watu sahihi ktk kufikisha ujumbe wanaoukusudia.
 
Niza doyi

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
1,509
2,000
Mnyama sana huyu jamaa. Ila gwaji Yuko Vizuri Sana Yani anajuwa kula na kipofu .
Namkubali sana huyu mwamba
Duniani Kuna maajabu mengi, Ndugai alisema hata wasikanyage eneo la bunge halafu Gwajiboy anakuja kukutana na rais uso kwa uso na kupewa nafasi ya kueleza shida za wananchi.
 
Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
16,388
2,000
Hii inaandaliwa na wataalamu wa kimataifa bwashee!
Watanzania hawawezi kufanya vizuri zaidi? Matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi, tunao vijana wengi tu wana fanya kazi (wanaweza) kwa nini anawathamini wageni zaidi kuliko wazawa? Au ndio ile gia ya kuwapa permit in days mtandaoni?
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
47,840
2,000
Watanzania hawawezi kufanya vizuri zaidi? Matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi, tunao vijana wengi tu wana fanya kazi (wanaweza) kwa nini anawathamini wageni zaidi kuliko wazawa? Au ndio ile gia ya kuwapa permit in days mtandaoni?
Hii kitu ni ya kimataifa bwashee!
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,352
2,000
Tanzania ilikataa habari za Ufalme na Uchifu.

Kwa kwenda na imani kuwa watu wote ni sawa.

Zanzibar walipindua royal family wakaanzisha Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Sasa hii Royal Tour Tanzania inakuja vipi?

Which royalty are we talking about here?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom