Royal Tour: Rais Samia asimama Jimbo la Kawe na kusikiliza wananchi kupitia Mbunge wao, Askofu Gwajima

Ni kweli na pia uchepushaji/rushwa. Inabidi alikemee na hilo. Pia amtaje Mungu kuwa ndiye muweza wa yote. Ajikite kuwa mtoa matumaini maana watanzania wanahitaji kiongozi anayebeba maono. Mama anafaa sana kuendelea kwa jinsi nilivyomsikiliza leo.
Hafai hata kidogo ni mtu wa hovyo sn
 
mkuu usijihangaishe. ni ishara ya kukwepa majukumu mazito, na ni wazi anakimbilia mambo mepesi mepesi.
kweli kabisa. Maana kwa fikra za kawaida hii nchi inavyokwenda ni kama haina mwenyewe. Leo linaamuliwa jambo na kutangazwa, kesho linafutwa na mbaya zaidi anaepaswa kutoa kauli hata hajui kinachoendelea. Ni kama vile na yeye anagundua mambo mengi baada ya kutangazwa. Ni wazi hayupo sehemu ya maamuzi aidha kwa kuogopa majukumu ama kwa kusudio la waliomuweka.
 
Tukio liko mubashara ITV

Rais Samia akiwa na mbunge wa Kawe wanahutubia wananchi wa jimbo la Kawe eneo la Tegeta manispaa ya Kinondoni.

Kwa sasa askofu Gwajima amepanda kwenye gari ya Ikulu na anatoa salamu za shukrani kwa Rais Samia kwa niaba ya wananchi.

Gwajima anasema wananchi wa Kawe siyo tu Wanampenda mama Samia bali wana mahaba naye.

Helicopter za polisi zinavinjari juu ya anga kuulinda mkutano huu mtakatifu.

Rais Samia amewataka wananchi waendelee kulipa kodi kwani kodi ni kwa maendeleo ya taifa.

Rais Samia amesema anaelekea Bagamoyo katika mtiririko wa uchukuaji picha ya filamu ya vivutio vya utalii wa Tanzania itakayozinduliwa nchini Marekani na kuonyeshwa dunia nzima.

Karibu
 
Back
Top Bottom