Mtego wa Noti
JF-Expert Member
- Nov 27, 2010
- 2,591
- 1,599
sasa nimeanza kuelewa...ningeshangaa mtu aliyechoka anavyoweza kujizimisha ati kwa sababu rostam kaachia ubunge......!!!!!waliozomia ni mabalozi na watu wake wa karibu waliokuwa wananyonya mirija na kununuliwa visimu vya sh 45,000/=
Wildcard,Pengine atakapofariki dunia ndipo mazuri yake yatasemwa. Kwa vyovyote vile mazuri yapo hata kama ni kwa mtu mmojammoja. Kuna mkoa nchi hii ulikuwa na Rais kwa zaidi ya miaka 20 lakini wana barabara moja tu ya lami na kauwanja ka ndege ni ka vumbi na tope!
Sasa hii inanipasua kichwa mpaka nachanganyikiwa kila ninapotafakari. Miezi kadhaa kabla ya Rostam kuachia siasa uchwara, tuliambiwa kuwa, wana-Igunga jamaa aliwakatia bima ya afya ili wasipate tabu mara waendapo hospitali kupata huduma za afya. Sasa nachanganyikiwa nisikiapo kuwa eti watu wa igunga wamechoka na wengine wanasema eti Rostam alaaniwe kwa sababu Igunga ni moja za wilaya zinazoongoza kwa umaskini huko Tabora, sasa hizi kitihada tulizokuwa tunazisikia kuwa Igunga ni kama Newyok ilikuwa ni uzushi? Je hakuna ukweli wowote katika hili suala la kila mwana-Igunga kuwa na bima ya afya? Sasa ilikuwaje baadhi ya watu wa Igunga wakazimia mara baada ya Rostam kutangaa kuwa ameachana na siasa uchwara?
Nawasilisha wanaJF........................
Mura unadharau sana,nikisema la moyoni mwangu najuwa ntakula ban.Pengine atakapofariki dunia ndipo mazuri yake yatasemwa. Kwa vyovyote vile mazuri yapo hata kama ni kwa mtu mmojammoja. Kuna mkoa nchi hii ulikuwa na Rais kwa zaidi ya miaka 20 lakini wana barabara moja tu ya lami na kauwanja ka ndege ni ka vumbi na tope!