Rostam na Bima ya afya kwa wana-Igunga!

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
2,592
1,599
Sasa hii inanipasua kichwa mpaka nachanganyikiwa kila ninapotafakari. Miezi kadhaa kabla ya Rostam kuachia siasa uchwara, tuliambiwa kuwa, wana-Igunga jamaa aliwakatia bima ya afya ili wasipate tabu mara waendapo hospitali kupata huduma za afya. Sasa nachanganyikiwa nisikiapo kuwa eti watu wa igunga wamechoka na wengine wanasema eti Rostam alaaniwe kwa sababu Igunga ni moja za wilaya zinazoongoza kwa umaskini huko Tabora, sasa hizi kitihada tulizokuwa tunazisikia kuwa Igunga ni kama Newyok ilikuwa ni uzushi? Je hakuna ukweli wowote katika hili suala la kila mwana-Igunga kuwa na bima ya afya? Sasa ilikuwaje baadhi ya watu wa Igunga wakazimia mara baada ya Rostam kutangaa kuwa ameachana na siasa uchwara?
Nawasilisha wanaJF........................
 
waliozomia ni mabalozi na watu wake wa karibu waliokuwa wananyonya mirija na kununuliwa visimu vya sh 45,000/=
sasa nimeanza kuelewa...ningeshangaa mtu aliyechoka anavyoweza kujizimisha ati kwa sababu rostam kaachia ubunge......!!!!!
 
Pengine atakapofariki dunia ndipo mazuri yake yatasemwa. Kwa vyovyote vile mazuri yapo hata kama ni kwa mtu mmojammoja. Kuna mkoa nchi hii ulikuwa na Rais kwa zaidi ya miaka 20 lakini wana barabara moja tu ya lami na kauwanja ka ndege ni ka vumbi na tope!
 
WildCard : Comment zako huwa siku zote zimeenda shule tatizo ni moja to achana na Magwanda
 
mimi sina mchango kwa hasira zangu nitapigwa ban, napita tu hapa mwaya.
 
Rostam amekuwa bize kufuatialia hukumu ya kesi yake kule Ikulu alipo ona JK anacheza karata 3 akaamua kuachia ngazio nyie mnasemaje eti Nape .Ulizei tuwap siri iko nje sasa kwa nini alijiondoa si Nape ngoma nzito hii .
 
Walilia kwa sababu walijua atakayekuja hatogawa pesa na huo ndo mwisho wao.
 
Kukatia bima wananchi unafikiri jambo la mchezo?hayo anayaweza mr gadafi my best president ever in africa
 
Pengine atakapofariki dunia ndipo mazuri yake yatasemwa. Kwa vyovyote vile mazuri yapo hata kama ni kwa mtu mmojammoja. Kuna mkoa nchi hii ulikuwa na Rais kwa zaidi ya miaka 20 lakini wana barabara moja tu ya lami na kauwanja ka ndege ni ka vumbi na tope!
Wildcard,
Naona unatupiga vijembe sisi watu wa Mara. Nyerere was not for Mara. He was for Tanzania na hilo tulilijua na tulishamsamehe. Tusaidieni basi angalau tupate kauwanja ka ndege kapya kama kale ka Mbeya.
 
when u read the history of community health fund (chf) wanasema ilianzia igunga mwaka 1996 (nakumbuka notes zangu za community medicine miaka hiyo). Sasa sijui,alianzisha ra? Ipo kweli mpaka sasa?Ni kweli ilianzia huko? Au walikuwa wanawapigia chapuo magamba,maana mkuu wa chuo ni magamba pure!
 
Sasa hii inanipasua kichwa mpaka nachanganyikiwa kila ninapotafakari. Miezi kadhaa kabla ya Rostam kuachia siasa uchwara, tuliambiwa kuwa, wana-Igunga jamaa aliwakatia bima ya afya ili wasipate tabu mara waendapo hospitali kupata huduma za afya. Sasa nachanganyikiwa nisikiapo kuwa eti watu wa igunga wamechoka na wengine wanasema eti Rostam alaaniwe kwa sababu Igunga ni moja za wilaya zinazoongoza kwa umaskini huko Tabora, sasa hizi kitihada tulizokuwa tunazisikia kuwa Igunga ni kama Newyok ilikuwa ni uzushi? Je hakuna ukweli wowote katika hili suala la kila mwana-Igunga kuwa na bima ya afya? Sasa ilikuwaje baadhi ya watu wa Igunga wakazimia mara baada ya Rostam kutangaa kuwa ameachana na siasa uchwara?
Nawasilisha wanaJF........................

Aliyeyasema hayo Maneno ni Mwanadada 1 anaitwa FAIZA FOXY kuwa wana-Igunga wote wanabima za Afya, sasa sijui Bima ipi aliyokuwa anatuambia na kumsifia yule mdoezi wa Iran. Aje hapa ajibu hii Hoja huyu Mwanadada
 
Hata mimi nilizi[ata news kuwa asilimia kubwa wana huduma ya afya ya CHF........

Cha kufurashisha na kuwa una membership card ya CHF ila facilities za kupata hiyo huduma ya CHF ndo kasheshe.......Unapewa nyama halafu unang'olewa meno yote.........

Ka udaku kidogo: Hivi hizi CHF si huwa wanalipa kwa fee ya annual kwa maana ya ukiishailipa once you have done it kwa mwaka? Nina wasiwasi kuwa aliwanunulia membership kama ka rushwa ka ubunge ndo maana wengi wanavyo maana hainiingii akilini kuwa wote walilipia fedha ya kununua....lazima kuna ka mkono ka mtu hapo...........natania tu jamani!!!
 
Pengine atakapofariki dunia ndipo mazuri yake yatasemwa. Kwa vyovyote vile mazuri yapo hata kama ni kwa mtu mmojammoja. Kuna mkoa nchi hii ulikuwa na Rais kwa zaidi ya miaka 20 lakini wana barabara moja tu ya lami na kauwanja ka ndege ni ka vumbi na tope!
Mura unadharau sana,nikisema la moyoni mwangu najuwa ntakula ban.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom