Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,244
- 113,628
Kama Kikwete alihusika katika haya yote inakuwaje huyu mtu anajitenga kama vile hakushiriki kwenye kitu chochote?Hivi Tanzania hii kweli hamna vitu kama Orange Revolution ya Ukraine iliyomuondoa madarakani Victor Yanukovich alipoiba kura na kukaa madarakani.Yaani hamna mtu influential wa kuinfluence such a revolution?
Kama Kikwete alihusika katika haya yote inakuwaje huyu mtu anajitenga kama vile hakushiriki kwenye kitu chochote?Hivi Tanzania hii kweli hamna vitu kama Orange Revolution ya Ukraine iliyomuondoa madarakani Victor Yanukovich alipoiba kura na kukaa madarakani.Yaani hamna mtu influential wa kuinfluence such a revolution?
MKJJ: Sasa utaona ni wapi Rostam anapata nguvu.
Mimi hoja yangu imekuwa kwa nini tumekuwa tukiwakwepa wengine, na hasa JK, kwenye hili sakata la Richomond? Au ndio tunasubiri atoke madaraka ndio tumbebee bango kama tunavyofanya sasa kwa Mkapa? Huoni kama huu utamaduni hautasaidii sana kwenye haya mapambano yetu?
kamati ya mwakyembe ingewahoji hao watu wawili, nafikiri ingeweza kuthibitisha bila doubt nani mmiliki wa richmond na dowans....
lakini kwa vile serkali haikutaka watu hao wahojiwe, ndio ukakuta "wakaenda nje ya nchi" na hawakulazimishwa kutoa ushahidi wowote baadae...
................ Rostam alikuwa na hisa kwenye RDC... he knows it na mtu yeyote ambaye angeamua kufuatilia suala hili lilipoanza 2006 angeona hivyo. Wengine tulishafanya uchunguzi mapema sana na kuestablish the following facts. (tafuta maswali yangu 10 kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU kuhusu Richmond - 2006).
a. RDC iliingia nchini kwa ushirika wa Mhe. Msabaha (Mbunge - Waziri wa Madini)
b. RDC iliingia nchini kwa ushirika wa Jakaya Kikwete (Mbunge)
c. RDC (USA) wametoa mchango mkubwa katika kampeni ya Kikwete na Msabaha
d. Rostam Aziz ndiye mfanyabiashara aliyetengeneza mazingira ya wao RDC kujikita kwenye biashara hiyo ya energy. Yeye mwenyewe akiwa ni shemeji ya Kikwete.
e. Naeem Gire waliingia na asilimia 75 ya RDC (tanzania) na asilimia 25 zilizobakia zikigawanywa miongoni mwa wahusika wakuu.
yes I said it! RDC inahusiana na Msabaha, Kikwete, Rostam na familia ya kina Gire ambao ni wachangiaji wa kampeni za uchaguzi CCM (2005). Kupewa kwa mradi wa bomba la mafuta 2005 na miezi michache baadaye mradi wa majenereta ilikuwa ni shukrani ya CCM kwa michango ya kina Gire katika kampeni za Msabaha na Kikwete na pia kama nafasi ya kuvuna walipopanda hasa baada ya JK alipoingia madarakani kumchukua Msabaha na kumuweka kuwa Waziri wa Nishati na Madini.
so, now you know.
MKJJ: Sasa utaona ni wapi Rostam anapata nguvu.
Mimi hoja yangu imekuwa kwa nini tumekuwa tukiwakwepa wengine, na hasa JK, kwenye hili sakata la Richomond? Au ndio tunasubiri atoke madaraka ndio tumbebee bango kama tunavyofanya sasa kwa Mkapa?Huoni kama huu utamaduni hautasaidii sana kwenye haya mapambano yetu?
.....hahaa ahaha aha,acha mchezo wewe,leo mafisadi wakienda kugombea ubunge kuanzia Lowassa,chenge,Rostam aziz,Mgonja,msabaha,Karamagi etc watashinda in a landslide,hiyo ndio version yetu ya Orange revolution mkuu.
Siyo wajibu wa mtu bali ni wa watu!! Mtu mmoja hawezi kufanya yote hayo. Kinachohitajika ni jitihada za pamoja.
Hiyo niliyoweka alama nyekundu inanishangaza kidogo.
Kuna kila sababu ya kuamini kuwa RA ndiye mshiriki mkubwa wa Richmond. Na vile vile nakubaliana nawe kuhusu uhusika kwa Richmond na kampeini za uchaguzi wa mwaka 2005 kwa vile Gire mwenyewe aliwahi kusema kuwa watu waliokuwa wanapiga kelele kuhusu mradi huo wana wivu wa kisiasa kwa sababu walishindwa uchaguzi mwaka 2005.
Nakubaliana nawe kabisa kuhusu utamaduni huu wa kuogopa kusema makosa ya viongozi wakiwa madarakani. Tukimsubiri Kikwete amalize kipindi chake itakuwa ni miaka saba ijayo na ushahidi utakuwa umepotea, au statue of limitations itatuzuia kumshitaki kwa kosa hilo kwa vile itakuwa imeshapita miaka karibuni 10 hivi tangu kosa lifanyike.
MKJJ: Sasa utaona ni wapi Rostam anapata nguvu.
Mimi hoja yangu imekuwa kwa nini tumekuwa tukiwakwepa wengine, na hasa JK, kwenye hili sakata la Richomond? Au ndio tunasubiri atoke madaraka ndio tumbebee bango kama tunavyofanya sasa kwa Mkapa? Huoni kama huu utamaduni hautasaidii sana kwenye haya mapambano yetu?
Kama Kikwete alihusika katika haya yote inakuwaje huyu mtu anajitenga kama vile hakushiriki kwenye kitu chochote?
Kuhani.. you are reasoning is flawed... kwanini isiwe kama hawa wengine wanaandamwa na kutajwa na kuhusishwa na ufisadi kwanini tusiwafuatilie na wakubwa zao? Hakuna sababu ya kuwaachia wengine bali kuwajumuisha wote... I think that is what I have just done.
Alipokuwa anafungua hotuba yake mbele ya Bunge, na katika aya za kwanza za Ripoti yake, Mwakyembe anamshukuru Spika kwa kumpa nguvu za 'summons.'
Rostam alitumiwa summons haku show up.
Summons maana yake usipo show up unatumiwa onyo la dharau, au contempt of authority.
Ukidharau onyo la contempt, unatumiwa barua ya tatu ya 'arrest warrant.'
Kwanini Mwakyembe, anaefundisha hivi vitu Chuo kikuu, hakufanya hayo?
Nani alimzuia asitumie nguvu za summons kama ameshatuambia anamshukuru Spika kwa kumpa full force of the law?
... you are reasoning is flawed... kwanini isiwe kama hawa wengine wanaandamwa na kutajwa na kuhusishwa na ufisadi kwanini tusiwafuatilie na wakubwa zao? Hakuna sababu ya kuwaachia wengine bali kuwajumuisha wote... I think that is what I have just done.
Kama Kikwete anahusika kwa namna moja ama nyingine basi tunawaonea kila Rostam na Msabaha na Karamagi na hata Lowassa kuwang'ang'ania wenyewe. Kikwete si ndio babalao?
Kama ambavyo tunamuonea Chenge na Mgonja na Yona na Marehemu na Vithlani na mafisadi wenzao wa Mkapa administration iwapo babaloa, Benjamin Mkapa, hayuko in trouble.
Tanzania kuna heshima isiyovunjwa ya mkubwa wa kazi hata kama inavunja utaratibu. Lowassa akimwambia Msabaha, Msabaha kachukue faili la Richmond kutoka Tanesco na shughulikia hii tenda, hata kama sheria inasema ni TANESCO ndio wanatakiwa ku process zabuni na mikataba yao, ni vigumu mno kwa Msabaha kukataa.
Kama Mkapa na Kiwete wako scotch free, basi na wengine wote hawa tuwaache wapumzike.
Kuna maswali ya msingi sana ya kumuuliza Mwakyembe ambayo hayakuulizwa, likiwemo hilo hapo juu kwa sababu watu walipagaishwa na hoja yake iliyomfanya Lowasa ajiuzulu.
Kwa kuwa sasa mpagaisho huo pengine umeisha tunahitahi kurudi kwenye hali yetu ya kawaida na ku-reflect tena more critically kwenye report ya Mwakyembe na kuona kama alijibu maswali ya msingi yaliyofanya kamati iundwe.
Binafsi sijawahi kuridhika na maelezo yake juu ya kwa nini hakumhoji Lowasa, ambaye at the end of the day ndiye alikuja kuonekana kwamba ndiye aliyekuwa player mkubwa na ultimate casuality kwenye sakata zima la Richmond. Mwakyembe anapaswa pia atueleze nafasi ya Rais Kikwete kwenye Richmond hasa kwa kuzingatia utetezi mzito ambao Rais Kikwete amewahi kuujenga juu ya kampuni hii ya kitapeli. Rais Kikwete aliwahi kututhibitishia watanzania, zaidi ya mara moja, kuwa kampuni ya Richmond ilikuwa ya uhakika na kwamba ingefanya kazi yake vizuri ndani ya muda uliopangwa. Sasa ilikuwaje maelezo muhimu kama haya hayakujikeza kwenye report ya Mwakyembe?
Ni kwa sababu ya hoja hizi mimi mwenzenu hushawishika kuamini kwamba report ya Mwakyembe ilitumika kama silaha ya kumalizana na kujengana kisiasa na wala haikuwa na lengo la kutafuta ukweli kuhusu kampuni Richmond. At the end of the day, ukweli utajulikana maana hata Mtikila amejificha miaka yote hii lakini leo hii shetani amemuumbua kweupe!
Huyu ni aliyekuwa Balozi wetu Marekani naye si mwingine ila ni Balozi Andrew Daraja. Nakumbuka jinsi nyakati hizo mkurugenzi wa RDC alijitapa sana kwenye tovuti yake alivyoweza kum'host' Balozi wetu ikiwa ni pamoja na kumtembeza, kumtambulisha na kumfanyia tafrija ya mwaka.