Rostam, Msabaha, Kikwete and Richmond - Yes I said it again!

Kama Kikwete alihusika katika haya yote inakuwaje huyu mtu anajitenga kama vile hakushiriki kwenye kitu chochote?Hivi Tanzania hii kweli hamna vitu kama Orange Revolution ya Ukraine iliyomuondoa madarakani Victor Yanukovich alipoiba kura na kukaa madarakani.Yaani hamna mtu influential wa kuinfluence such a revolution?

Siyo wajibu wa mtu bali ni wa watu!! Mtu mmoja hawezi kufanya yote hayo. Kinachohitajika ni jitihada za pamoja.
 
Kama Kikwete alihusika katika haya yote inakuwaje huyu mtu anajitenga kama vile hakushiriki kwenye kitu chochote?Hivi Tanzania hii kweli hamna vitu kama Orange Revolution ya Ukraine iliyomuondoa madarakani Victor Yanukovich alipoiba kura na kukaa madarakani.Yaani hamna mtu influential wa kuinfluence such a revolution?

.....hahaa ahaha aha,acha mchezo wewe,leo mafisadi wakienda kugombea ubunge kuanzia Lowassa,chenge,Rostam aziz,Mgonja,msabaha,Karamagi etc watashinda in a landslide,hiyo ndio version yetu ya Orange revolution mkuu.
 
MKJJ: Sasa utaona ni wapi Rostam anapata nguvu.

Mimi hoja yangu imekuwa kwa nini tumekuwa tukiwakwepa wengine, na hasa JK, kwenye hili sakata la Richomond? Au ndio tunasubiri atoke madaraka ndio tumbebee bango kama tunavyofanya sasa kwa Mkapa? Huoni kama huu utamaduni hautasaidii sana kwenye haya mapambano yetu?

Kitila is a man!! Tutasema mpaka tutachoka mafisadi wa aina ya Rostam wako wengi hapa nchini, na hatutaweza kuwafanya lolote mpaka Kikwete aamua kufanya jambo.NAONA TATIZO NI RAIS TU HUYU NDIYO ABANWE MPAKA BASI, HAWA WENGINE, HATA ROSTAM AU EL N.K WAKIFUNGWA LEO NA BADO WAKABAKI WENGINE HATUJAFANYA KITU. NAONA KAMA INTELLECTUALS, TUANGALIE SOURCE-MZIZI WA TATIZO TATIZO NI KIKWETEE

Kalenge
 
kamati ya mwakyembe ingewahoji hao watu wawili, nafikiri ingeweza kuthibitisha bila doubt nani mmiliki wa richmond na dowans....
lakini kwa vile serkali haikutaka watu hao wahojiwe, ndio ukakuta "wakaenda nje ya nchi" na hawakulazimishwa kutoa ushahidi wowote baadae...

Alipokuwa anafungua hotuba yake mbele ya Bunge, na katika aya za kwanza za Ripoti yake, Mwakyembe anamshukuru Spika kwa kumpa nguvu za 'summons.'

Rostam alitumiwa summons haku show up.

Summons maana yake usipo show up unatumiwa onyo la dharau, au contempt of authority.

Ukidharau onyo la contempt, unatumiwa barua ya tatu ya 'arrest warrant.'

Kwanini Mwakyembe, anaefundisha hivi vitu Chuo kikuu, hakufanya hayo?

Nani alimzuia asitumie nguvu za summons kama ameshatuambia anamshukuru Spika kwa kumpa full force of the law?
 
................ Rostam alikuwa na hisa kwenye RDC... he knows it na mtu yeyote ambaye angeamua kufuatilia suala hili lilipoanza 2006 angeona hivyo. Wengine tulishafanya uchunguzi mapema sana na kuestablish the following facts. (tafuta maswali yangu 10 kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU kuhusu Richmond - 2006).

a. RDC iliingia nchini kwa ushirika wa Mhe. Msabaha (Mbunge - Waziri wa Madini)
b. RDC iliingia nchini kwa ushirika wa Jakaya Kikwete (Mbunge)
c. RDC (USA) wametoa mchango mkubwa katika kampeni ya Kikwete na Msabaha
d. Rostam Aziz ndiye mfanyabiashara aliyetengeneza mazingira ya wao RDC kujikita kwenye biashara hiyo ya energy. Yeye mwenyewe akiwa ni shemeji ya Kikwete.
e. Naeem Gire waliingia na asilimia 75 ya RDC (tanzania) na asilimia 25 zilizobakia zikigawanywa miongoni mwa wahusika wakuu.

yes I said it! RDC inahusiana na Msabaha, Kikwete, Rostam na familia ya kina Gire ambao ni wachangiaji wa kampeni za uchaguzi CCM (2005). Kupewa kwa mradi wa bomba la mafuta 2005 na miezi michache baadaye mradi wa majenereta ilikuwa ni shukrani ya CCM kwa michango ya kina Gire katika kampeni za Msabaha na Kikwete na pia kama nafasi ya kuvuna walipopanda hasa baada ya JK alipoingia madarakani kumchukua Msabaha na kumuweka kuwa Waziri wa Nishati na Madini.

so, now you know.

Hiyo niliyoweka alama nyekundu inanishangaza kidogo.

Kuna kila sababu ya kuamini kuwa RA ndiye mshiriki mkubwa wa Richmond. Na vile vile nakubaliana nawe kuhusu uhusika kwa Richmond na kampeini za uchaguzi wa mwaka 2005 kwa vile Gire mwenyewe aliwahi kusema kuwa watu waliokuwa wanapiga kelele kuhusu mradi huo wana wivu wa kisiasa kwa sababu walishindwa uchaguzi mwaka 2005.

MKJJ: Sasa utaona ni wapi Rostam anapata nguvu.

Mimi hoja yangu imekuwa kwa nini tumekuwa tukiwakwepa wengine, na hasa JK, kwenye hili sakata la Richomond? Au ndio tunasubiri atoke madaraka ndio tumbebee bango kama tunavyofanya sasa kwa Mkapa?Huoni kama huu utamaduni hautasaidii sana kwenye haya mapambano yetu?

Nakubaliana nawe kabisa kuhusu utamaduni huu wa kuogopa kusema makosa ya viongozi wakiwa madarakani. Tukimsubiri Kikwete amalize kipindi chake itakuwa ni miaka saba ijayo na ushahidi utakuwa umepotea, au statue of limitations itatuzuia kumshitaki kwa kosa hilo kwa vile itakuwa imeshapita miaka karibuni 10 hivi tangu kosa lifanyike.
 
.....hahaa ahaha aha,acha mchezo wewe,leo mafisadi wakienda kugombea ubunge kuanzia Lowassa,chenge,Rostam aziz,Mgonja,msabaha,Karamagi etc watashinda in a landslide,hiyo ndio version yetu ya Orange revolution mkuu.

Hata siku moja tena nitake radhi mara moja.Hiyo ni ignorance ya watu wachache ambao wamenyimwa elimu na hawa mafisadi ila mtu kama wewe na mimi ndio tuwaeleze wale ambao ni ignorant kufanya yaliyo sahihi kwa kuwanyima kura.
 
Hiyo niliyoweka alama nyekundu inanishangaza kidogo.

Kuna kila sababu ya kuamini kuwa RA ndiye mshiriki mkubwa wa Richmond. Na vile vile nakubaliana nawe kuhusu uhusika kwa Richmond na kampeini za uchaguzi wa mwaka 2005 kwa vile Gire mwenyewe aliwahi kusema kuwa watu waliokuwa wanapiga kelele kuhusu mradi huo wana wivu wa kisiasa kwa sababu walishindwa uchaguzi mwaka 2005.

Nakubaliana nawe kabisa kuhusu utamaduni huu wa kuogopa kusema makosa ya viongozi wakiwa madarakani. Tukimsubiri Kikwete amalize kipindi chake itakuwa ni miaka saba ijayo na ushahidi utakuwa umepotea, au statue of limitations itatuzuia kumshitaki kwa kosa hilo kwa vile itakuwa imeshapita miaka karibuni 10 hivi tangu kosa lifanyike.

Kichuguu.. hilo la red uliloliweka nimelichomekea kuongeza kisa cha kwanini RA ana uthubutu wa kufanya anachofanya. JK hawezi kamwe kuona baya linamkuta RA. Hilo halitatokea as long as JK is the president.
 
MKJJ: Sasa utaona ni wapi Rostam anapata nguvu.

Mimi hoja yangu imekuwa kwa nini tumekuwa tukiwakwepa wengine, na hasa JK, kwenye hili sakata la Richomond? Au ndio tunasubiri atoke madaraka ndio tumbebee bango kama tunavyofanya sasa kwa Mkapa? Huoni kama huu utamaduni hautasaidii sana kwenye haya mapambano yetu?

Tunaweza kuanza sasa kumbebea mabango
113817680_f26542874b.jpg
 
Kama Kikwete anahusika kwa namna moja ama nyingine basi tunawaonea kila Rostam na Msabaha na Karamagi na hata Lowassa kuwang'ang'ania wenyewe. Kikwete si ndio babalao?

Kama ambavyo tunamuonea Chenge na Mgonja na Yona na Marehemu na Vithlani na mafisadi wenzao wa Mkapa administration iwapo babaloa, Benjamin Mkapa, hayuko in trouble.

Tanzania kuna heshima isiyovunjwa ya mkubwa wa kazi hata kama inavunja utaratibu. Lowassa akimwambia Msabaha, Msabaha kachukue faili la Richmond kutoka Tanesco na shughulikia hii tenda, hata kama sheria inasema ni TANESCO ndio wanatakiwa ku process zabuni na mikataba yao, ni vigumu mno kwa Msabaha kukataa.

Kama Mkapa na Kiwete wako scotch free, basi na wengine wote hawa tuwaache wapumzike.
 
Kuhani.. you are reasoning is flawed... kwanini isiwe kama hawa wengine wanaandamwa na kutajwa na kuhusishwa na ufisadi kwanini tusiwafuatilie na wakubwa zao? Hakuna sababu ya kuwaachia wengine bali kuwajumuisha wote... I think that is what I have just done.
 
Kama Kikwete alihusika katika haya yote inakuwaje huyu mtu anajitenga kama vile hakushiriki kwenye kitu chochote?

Sio kwamba anajitenga; ni kwamba sisi hatumhoji na haiwezekani ajihoji mwenyewe! Tumewakazania mawakala waufisadi na kuacha mafisadi wenyewe. Tunasubiri watoke madarakani ndipo tuanze kuwachimba. Tujirekebishe!
 
Kuhani.. you are reasoning is flawed... kwanini isiwe kama hawa wengine wanaandamwa na kutajwa na kuhusishwa na ufisadi kwanini tusiwafuatilie na wakubwa zao? Hakuna sababu ya kuwaachia wengine bali kuwajumuisha wote... I think that is what I have just done.

Wote wako sawa na wote wanastahili wanayostahili kulingana na ushiriki wao...
 
Alipokuwa anafungua hotuba yake mbele ya Bunge, na katika aya za kwanza za Ripoti yake, Mwakyembe anamshukuru Spika kwa kumpa nguvu za 'summons.'

Rostam alitumiwa summons haku show up.

Summons maana yake usipo show up unatumiwa onyo la dharau, au contempt of authority.

Ukidharau onyo la contempt, unatumiwa barua ya tatu ya 'arrest warrant.'

Kwanini Mwakyembe, anaefundisha hivi vitu Chuo kikuu, hakufanya hayo?

Nani alimzuia asitumie nguvu za summons kama ameshatuambia anamshukuru Spika kwa kumpa full force of the law?

Kuna maswali ya msingi sana ya kumuuliza Mwakyembe ambayo hayakuulizwa, likiwemo hilo hapo juu kwa sababu watu walipagaishwa na hoja yake iliyomfanya Lowasa ajiuzulu.

Kwa kuwa sasa mpagaisho huo pengine umeisha tunahitahi kurudi kwenye hali yetu ya kawaida na ku-reflect tena more critically kwenye report ya Mwakyembe na kuona kama alijibu maswali ya msingi yaliyofanya kamati iundwe.

Binafsi sijawahi kuridhika na maelezo yake juu ya kwa nini hakumhoji Lowasa, ambaye at the end of the day ndiye alikuja kuonekana kwamba ndiye aliyekuwa player mkubwa na ultimate casuality kwenye sakata zima la Richmond. Mwakyembe anapaswa pia atueleze nafasi ya Rais Kikwete kwenye Richmond hasa kwa kuzingatia utetezi mzito ambao Rais Kikwete amewahi kuujenga juu ya kampuni hii ya kitapeli. Rais Kikwete aliwahi kututhibitishia watanzania, zaidi ya mara moja, kuwa kampuni ya Richmond ilikuwa ya uhakika na kwamba ingefanya kazi yake vizuri ndani ya muda uliopangwa. Sasa ilikuwaje maelezo muhimu kama haya hayakujikeza kwenye report ya Mwakyembe?

Ni kwa sababu ya hoja hizi mimi mwenzenu hushawishika kuamini kwamba report ya Mwakyembe ilitumika kama silaha ya kumalizana na kujengana kisiasa na wala haikuwa na lengo la kutafuta ukweli kuhusu kampuni Richmond. At the end of the day, ukweli utajulikana maana hata Mtikila amejificha miaka yote hii lakini leo hii shetani amemuumbua kweupe!
 
... you are reasoning is flawed... kwanini isiwe kama hawa wengine wanaandamwa na kutajwa na kuhusishwa na ufisadi kwanini tusiwafuatilie na wakubwa zao? Hakuna sababu ya kuwaachia wengine bali kuwajumuisha wote... I think that is what I have just done.

Kwa sababu Marais Tanzania hawawezi kushitakiwa.

Kwa jinai yeyote ambayo Rais amei mastermind ni kuwaonea wa chini yake kama kinara wa crime hayuko matatizoni.

Huwa unapenda kuongelea swala la kutoa immunity. Sasa ingekuwa nchi za watu, waendesha mashitaka wangewapa immunity hawa makatibu wakuu kina Mgonja na kina Rutabanzibwa na Makada wa Chama, kina Rostam, ili kukamata Mawaziri na Marais.

Huwezi ukamshitaki Rostam ukamuacha Lowassa na Karamagi, kama ambavyo huwezi kumfunga Daniel Yona ukamuacha Benjamin Mkapa.

Mmoja kachora dili, mwingine katekeleza, mwingine kasema waachwe wapumzike, mwingine kakamatwa kaficha hela, mwingine kakubali alishiriki akajiuzulu.

Kwa nini wote wasiachwe wapumzike?
 
Kama Kikwete anahusika kwa namna moja ama nyingine basi tunawaonea kila Rostam na Msabaha na Karamagi na hata Lowassa kuwang'ang'ania wenyewe. Kikwete si ndio babalao?

Kama ambavyo tunamuonea Chenge na Mgonja na Yona na Marehemu na Vithlani na mafisadi wenzao wa Mkapa administration iwapo babaloa, Benjamin Mkapa, hayuko in trouble.

Tanzania kuna heshima isiyovunjwa ya mkubwa wa kazi hata kama inavunja utaratibu. Lowassa akimwambia Msabaha, Msabaha kachukue faili la Richmond kutoka Tanesco na shughulikia hii tenda, hata kama sheria inasema ni TANESCO ndio wanatakiwa ku process zabuni na mikataba yao, ni vigumu mno kwa Msabaha kukataa.

Kama Mkapa na Kiwete wako scotch free, basi na wengine wote hawa tuwaache wapumzike.

Wote wako KAPU MOJA NA HAKUNA WA KUETETEWA WALA ANAYEONEWA!

Kila mtu ali play PART YAKE...NA MWANASHERIA MKUU NAYE ASILAUMIWE?

NANI KASEMA?

Kuwa hao watu eti wana IMMUNITY NA MWENYE KOSA NI JK MWENYEWE?

Nani mshauri wa RAIS?

Acheni hizo bana!

HAKUNA ANAYEONEWA NA HAKUNA WA KUSAFISHWA!

Na kusema eti mafisadi wapumzike kwa kunyonya DAMU ZETU NI KAULI ISIYOVUMILIKA!

Kwanza mimi ningekuwa JK ningewageuka na kusema hawa ni washauri wabaya!

Bado ana nafasi ya kurudi ULINGONI KAMA AKIKUBALI KUYATEMA MASLAHI NA USHAURI WA KIMAFIA!

Na pia kujitoa kwenye UMAFIA!

Kama amekula kiapo ni shauri yake!
Tutamuonyesha kuwa TZ NI YA WATANZANIA NA SI YA MAFIOSOS

AGEUKE NA ATAKUWA SHUJAA!

Zaidi ya HAPO...NARUDIA TENA...SAFARI YA WASHINGTON AITAFAKARI SANA.
 
Kuna mtu mmoja muhimu ambaye angeweza kutusaidia sana kwenye hili jambo na sina hakika sana kama alihojiwa na Kamati ya Mwakyembe. Huyu ni aliyekuwa Balozi wetu Marekani naye si mwingine ila ni Balozi Andrew Daraja. Nakumbuka jinsi nyakati hizo mkurugenzi wa RDC alijitapa sana kwenye tovuti yake alivyoweza kum'host' Balozi wetu ikiwa ni pamoja na kumtembeza, kumtambulisha na kumfanyia tafrija ya mwaka.

Kama sijakosea sana baadaye Mzee wa Kaya alitembelea Marekani na sehemu mojawapo aliyohakikisha amefika ni Houston, Texas. Haukupita sana muda na RDC wakapewa tenda. Sikumbuki vizuri mtiririko wa mambo na niko kwenye harakati kuzitafuta data lakini sidhani niko mbali na ukweli hata kidogo.

Hata hivyo kwenye tovuti ya RDC mpaka elo wanasema hivi:

RECENT PROJECTS

In 2006, we completed the Ubungo Emergency Supply Power Plant Project in Dar es Salaam, Tanzania. We provided full project development and engineering, procurement and commissioning (EPC) for the first 25MW, and all preparatory work for the second phase, of a 100MW ISO gas-based generation plant.

Sasa, kuliko wakati wowote ule, kuna ulazima mkubwa wa kumbebesha mzigo wa RDC mhusika mkuu na sio mabungusilo.

EVENTS

Richmond Development Company of Houston (RDEVCO) which is developing several projects in the East African nation of Tanzania hosted The Tanzanian Ambassador to USA, The Honorable Andrew M. Daraja to Houston, Texas, from July 20 through to July 22, 2003.

During his visit, Ambassador Daraja was introduced to the leaders of the business community of Houston, which also included alliance partner companies of RDEVCO.

Ambassador Daraja acknowledged that the African region is becoming prominent with regard to the economic and strategic interests of United States as evidenced by President Bush's recent trip to the region.

"With some of our Tanzanian projects approaching financial close, RDEVCO will add new high caliber jobs in Houston" said Dr. Huque, a principal at RDEVCO.

"The fact that Ambassador Daraja came to Houston demonstrates the commitment of The Government of Tanzania to extend business cooperation of Houston based companies" added Mr. Gire, another principal at RDEVCO.

The highlight of The Ambassador's visit to Houston was a Gala Dinner attended by Dr. Lee P. Brown, Mayor of Houston.

The Mayor awarded an honoree citizenship to The Ambassador.

Je,na mkono wa Mkapa upo hapa
 
Kuna maswali ya msingi sana ya kumuuliza Mwakyembe ambayo hayakuulizwa, likiwemo hilo hapo juu kwa sababu watu walipagaishwa na hoja yake iliyomfanya Lowasa ajiuzulu.

Kwa kuwa sasa mpagaisho huo pengine umeisha tunahitahi kurudi kwenye hali yetu ya kawaida na ku-reflect tena more critically kwenye report ya Mwakyembe na kuona kama alijibu maswali ya msingi yaliyofanya kamati iundwe.

Binafsi sijawahi kuridhika na maelezo yake juu ya kwa nini hakumhoji Lowasa, ambaye at the end of the day ndiye alikuja kuonekana kwamba ndiye aliyekuwa player mkubwa na ultimate casuality kwenye sakata zima la Richmond. Mwakyembe anapaswa pia atueleze nafasi ya Rais Kikwete kwenye Richmond hasa kwa kuzingatia utetezi mzito ambao Rais Kikwete amewahi kuujenga juu ya kampuni hii ya kitapeli. Rais Kikwete aliwahi kututhibitishia watanzania, zaidi ya mara moja, kuwa kampuni ya Richmond ilikuwa ya uhakika na kwamba ingefanya kazi yake vizuri ndani ya muda uliopangwa. Sasa ilikuwaje maelezo muhimu kama haya hayakujikeza kwenye report ya Mwakyembe?

Ni kwa sababu ya hoja hizi mimi mwenzenu hushawishika kuamini kwamba report ya Mwakyembe ilitumika kama silaha ya kumalizana na kujengana kisiasa na wala haikuwa na lengo la kutafuta ukweli kuhusu kampuni Richmond. At the end of the day, ukweli utajulikana maana hata Mtikila amejificha miaka yote hii lakini leo hii shetani amemuumbua kweupe!

Kama ripoti imemaliza baadhi ya watu kisiasa, hiyo ni collateral tu mzee. Bado ninadhani lengo nikutafuta ukweli katika mazingira magumu. Ugumu wa mazingira usikuvunje moyo, kwa kuwa ushindi kwenye haya mazingira ni mtamu zaidi.
 
Huyu ni aliyekuwa Balozi wetu Marekani naye si mwingine ila ni Balozi Andrew Daraja. Nakumbuka jinsi nyakati hizo mkurugenzi wa RDC alijitapa sana kwenye tovuti yake alivyoweza kum'host' Balozi wetu ikiwa ni pamoja na kumtembeza, kumtambulisha na kumfanyia tafrija ya mwaka.

Kwa kweli ni vigumu kuona wapi JK anaingia kwenye hili la RDC moja kwa moja, maana mtiririko wa matukio ulikuwa unaonyesha kama vile na yeye alikuwa hapewi habari zilizokamilika, kitu ambacho share holder angetakiwa awe anajua mapema zaidi.

Lakini labda hii ziara ya Balozi Andrew Daraja, kule Houston, ni ya kudadisi zaidi maana bosi wake wakati ule alikuwa JK. Kwa mtazamo wangu ni kuwa, labda JK alifahamu yote kuhusu RDC kwa kupitia kwa best wake, Lowassa, lakini hakuwa among the key players.

Balozi Daraja kauli yake kwenye hili suala kama angehojiwa ingekuwa ni muhimu sana ili kuelezea huyo aliyemtuma kwenda kuipandisha chati RDC.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom