Rostam Aziz awaomba radhi majaji, asema ULIMI ULITELEZA

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
430
623
Rostam Aziz ameomba radhi kwa majaji akisema ulimi uliteleza na hakumaanisha ambacho alikisema kuhusu majaji kuhongwa. Nadhani amefanya jambo la kiungwana sana.

===

Leo Jumanne July 4, 2023 mfanyabiashara mashuhuri nchini, Rostam Aziz ameongea na vyombo vya habari, pamoja na mambo mengine ameomba radhi na kusema hakukusudia kudharau mahakama.

Rostam Aziz: Baada ya kuona tamko la chama cha majaji na mahakimu kuhusiana na kauli niliyoitoa Jumatatu iliyopita wakati nikiongea kuhusiana na uwekezaji wa kampuni yetu kule Zambia.

Nimesoma taarifa ya chama, kwasababu ya kutambua na kuheshimu dhima, hadhi na wajibu wa kikatiba wa mahakama, ningependa kusema yafuatayo

Ningependa kuuhakikishia umma kwamba wakati nikizungumzia kuhusu uwekezaji, halikuwa kusudio langu kudharau mahakama zetu. Kama nilisema hivyo ilikuwa ni kuteleza kwa ulimi maana kusudio langu lilikuwa likilenga kuhusu uwekezaji nchini na maana yangu ilikuwa ni kwamba ili tuweze kupata uwekezaji nchini mwetu hatuna budi kuendana na taratibu zinazoongoza uwekezaji Duniani.

===

Kauli ya Rostam Azizi kujusu Majaji na Mahakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu: Rostam Aziz: Hakuna mwekezaji atakubali kuwekeza halafu umwambie aende Mahakama ya Kisutu ambapo Majaji wanaweza kupigiwa simu na watu wa Serikali



Tamko la kumtaka athibitishe kauli yake: Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania chamtaka Rostam Aziz kuthibitisha tuhuma alizotoa dhidi ya Majaji na Mahakama ya Kisutu
 
Nilijua tu, lazima angelegea na kuomba radhi, kutoa shutuma bila kuwa na ushahidi wa kutosha wa shutuma dhidi ya wale unaowalalamikia ni udhaifu, lakini pia, tena zaidi, kama wale unaowalalamikia ni wenzako - CCM.

Sasa matokeo yake Rostam kwa sababu ya kutokuchagua cha kuzungumza, na wapi akizungumze, amejikuta ameenda kutengeneza maadui zaidi ya yule Dr. Slaa aliyemdhamiria, hapo sasa kwa msamaha wake, amejikuta amejichafua yeye mwenyewe, na kuwasafisha wachafu - CCM na mahakama zake.
 
Rostam hofu yake ni biashara zake ndo imemfanya aombe msamaha.
Mahakama haiwezi kuingilia biashara zake, kuiponda kwake CCM na kutoa siri za yale wanayofanya hata nae akiwa mnufaika, ndiko kumemfanya ajikute anaenda kutengeneza matatizo mengine na asiowatarajia.

Rostam ameonesha udhaifu wake binafsi kwenye mambo kadhaa, kwanza hajiamini- hajui kusimamia anachokisema, pili hajui kuchagua aseme nini na wapi, na tatu, ni muongo na asiyeaminika - kwa kukiri kwake amekosea na kuomba msamaha.
 
Nilijua tu, lazima angelegea na kuomba radhi, kutoa shutuma bila kuwa na ushahidi wa kutosha wa shutuma dhidi ya wale unaowalalamikia ni udhaifu.
Kauli ya Rostam Aziz ilikuwa ni "wake up call" kwa mahakama za tanzania kujitathmini ktk utoaji haki na utendaji kazi wake na siyo mahakama ya kisutu peke yake. Watanzania wengi tulio na kesi mahakamani tungetamani mahakama zetu ziwe truly independent, fair and adhere to the rule of law. Kumlalamikia na kumtisha Rostam haisaidii. Kwanini mathlani Wakili Fatma Karume azuiwe kufanya kazi ya uwakili?? Why??
 
Majaji na Hongo ni kama Uji na Mgonjwa.
Tukisema mahakama zinahongwa sana na kila mmoja wetu ana ushahidi wa hilo, halafu ajabu, msemaji akose hata tukio/mfano mmoja wa kuthibitisha madai yake, kwangu naona ni jambo la ajabu sana.

Huu msamaha wa Rostam ni janja ya kuisafisha CCM, na mahakama, hapo Rostam ameamua kujichafua yeye kwa kukiri kusema uongo, na kuwasafisha CCM na mahakama.
 
danimutta

Rostam halalamikiwi wala kutishwa, hapo nimeandika tabia zake zilizomfanya akajifunga mwenyewe, kama angekuwa anajielewa na wewe unaamini alichokisema mwanzo.

Mlitakiwa/alitakiwa kupeleka ushahidi mahakamani kwamba mahakama hazipo huru, lakini kuomba radhi maana yake Rostam amekiri alisema uongo, kwamba hana ushahidi wa kile alichokizungumza, hapo sijamtisha yeyote.

Nikwambie kitu, huu msamaha Rostam alioomba, ukiutazama kwa undani kabisa utauona una manufaa kwa CCM yake, ni kama amekisafisha chama chake kijanja bika nyie wengine kujua hilo, msimtetee mtu anayeijua dhambi, akaisema, lakini ajabu mwisho wa siku akaamua kuomba radhi kwa kuisema kwake.
 
Mfanyabiashara, Rostam Aziz amekiangukia Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT), akiomba radhi kutokana na kauli aliyoitoa dhidi ya Mahakama nchini.

Rostam ameomba radhi saa chache baada ya JMAT kutoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari, kikimtaka mfanyabiashara huyo athibitishe tuhuma alizotoa dhidi ya Mahakama au aombe radhi hadharani.

Rostam, Juni 26, mwaka huu mbele ya waandishi wa habari alisema, "Hakuna mwekezaji atawekeza kwenye nchi ambayo kesi ikipelekwa hapo Kisutu kiongozi yoyote anaweza kupiga simu akaielekeza mahakama nini cha kufanya.”

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Rostam alizungumzia faida za uwekezaji wa sekta binafsi katika uendeshaji wa bandari, akirejea mkataba wa ushirikiano uliosainiwa na Serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu uwekezaji na uendelezaji wa bandari nchini.

Hata hivyo, sakata hilo limeibua hisia tofauti za wananchi, wengine wakikosoa kutokana na kile wanachoeleza kuwa, baadhi ya vifungu vya mkataba huo vina kasoro na hatari kwa masilahi ya nchi.

JMAT ilitangaza kusikitishwa na kauli hiyo ikisema, "Anapaswa athibitishe kauli yake akibainisha jina la Jaji na lini alipewa maagizo na Serikali kutoa maamuzi kinyume na taratibu zilizopo. Akishindwa kutoa uthibitisho, tunamtaka atumie jukwaa lile lile kuomba radhi kwa uzito ule ule.”

Baada ya taarifa hiyo, Rostam leo Jumanne, Julai 4, 2023 amezungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, akieleza alichokizungumza siyo kusudio lake ni kuteleza kwa ulimi.

"Kwa sababu ya kutambua na kuheshimu dhima, hadhi na wajibu wa kikatiba wa Mahakama, ningependa kusema yafuatayo.

"Ningependa kuuhakikishia umma, kwamba wakati nikizungumzia uwekezaji halikuwa kusudio langu kuidharau Mahakama," amesema.

Alichokizungumza, amesema ameteleza ulimi na si kusudiolake.

"Niliteleza ulimi, maana kusudio langu lilikuwa ni kueleza kuhusu uwekezaji nchini na maana yangu ilikuwa ni kwamba, ili tupate uwekezaji nchini hatuna budi kuendana na taratibu," amesema.

MWANANCHI
 
Mahakama haiwezi kuingilia biashara zake, kuiponda kwake CCM na kutoa siri za yale wanayofanya hata nae akiwa mnufaika, ndiko kumemfanya ajikute anaenda kutengeneza matatizo mengine na asiowatarajia.

Rostam ameonesha udhaifu wake binafsi kwenye mambo kadhaa, kwanza hajiamini- hajui kusimamia anachokisema, pili hajui kuchagua aseme nini na wapi, na tatu, ni muongo na asiyeaminika - kwa kukiri kwake amekosea na kuomba msamaha.
Ndiyo imefanya waarabu waombe sheria za uingereza, walijua wa Tanzania ni manguli wa sheria, rostam wangemfilisi
 
Back
Top Bottom