Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,672
- 40,549
Mwanakijiji,
1. Kuhusu Richmond na Dowans, Bunge lenu lilichunguza likasema hakuna sehemu walipoona kwamba Mh. Rostam Aziz anahusika... sasa nini kifanyike tena...
Hicho ndicho nilichosema nimenotice katika maelezo ya Rostam. Siyo kwamba hakuhusika, na hajawahi kukanusha hicho. Yeye anasema walichunguza na hawakuona jina lake. Vitu hivi ni viwili tofauti. Rostam hajawahi kukana kuhusika na Richmond na Dowans. Sikiliza tena majibu yake alipoulizwa hata jana.
2. Mamlaka za kuchunguza zinachunguza kukiwa na hoja,,, sio kila anachosema mwanakijiji kichunguzwe... wanapoona unaongea utumbo wanakuacha na utumbo wako.
Sasa, kama anachosema "mwanakijiji" ni utumbo kwanini watake ushahidi tena? Hivi nani mmiliki wa Richmond au Dowans? Kuna mtu anajua. Kamati ya Bunge ilishindwa kuonesha ni nani hasa mmiliki wa Richmond. Hebu nikukumbushishe kilichosemwa kuhusu Rostam kwenye ripoti ya Mwakyembe:
Mashahidi wawili, Ndugu Daniel Yona na Mhe. Rostam Aziz, (Mb) walipelekewa hati za kuitwa mbele ya Kamati Teule lakini hawakufika kwa maelezo kwamba walikuwa nje ya nchi.....
Mhe. Rostam Aziz alitakiwa atoe maelezo kuhusu uhusiano wake na Kampuni za Richmond Development Company LLC na Dowans Holdings S.A baada ya mashahidi zaidi ya watano kumtaja kuwa ana uhusiano nazo. Aidha, alitakiwa na Kamati Teule aeleze kwanini anwani ya posta na anwani ya barua pepe ya kampuni yake ya Caspian Construction Company Ltd inatumiwa na Dowans Holdings S.A. Kamati Teule ilipata majina ya baadhi ya wafanyakazi wa Caspian ambao pia wanaitumikia Dowans Holdings S.A.
Na kamati hiyo hiyo teule inasema hivi:
Pamoja na juhudi hizo za wamiliki wa kampuni ya Richmond Development Company LLC, Kamati Teule ilibaini kutokana na ushauri mbalimbali iliopata wa kisheria, kuwa tatizo la uhalali wa Richmond ya Tanzania lilikuwa palepale kwani kifungu cha 3(1) cha Sheria ya Makampuni kinataka watu wawili au zaidi kuwa na uwezo wa kufungua kampuni. Kwa kuwa mmoja wa wanahisa waliofungua kampuni hiyo ya Richmond ya Tanzania ni Richmond Development Company LLC ya Marekani (yenye asilimia 75 ya hisa zote za kampuni hiyo iliyosajiliwa Tanzania) na kwa kuwa kampuni hiyo ya kimarekani haijasajiliwa Marekani wala hapa Tanzania kwa mujibu wa kifungu cha 434 cha Sheria ya Makampuni na kwa kuwa, kutokana na hiyo sababu, kampuni hiyo ya kimarekani haina nguvu wala mamlaka stahili ya kikampuni, Richmond Development Company (T) Limited ina mwanahisa mmoja tu kwa jina Naeem Gire, hali ambayo haikubaliki kisheria.
Ni wazi kuwa picha iliyojengwa kwenye mkataba tunaouongelea hapa kuhusu hadhi na uhalali wa Richmond Development Company LLC nchini Tanzania ilikuwa ya kisanii, ya uongo na isiyo na msingi wowote kisheria.
Sasa kwa mfanyabiashara mzuri na msafi kama Rostam ambaye anasingiziwa tu mambo ya ufisadi, kufanya kazi na biashara na hata kushirikiana anuani na kampuni ya kifisadi ambayo ilishajulikana ni ya kifisadi hakumfanyi yeye fisadi? Inakuwaje kwa mfanyabiashara "msafi" ambaye familia yake imefanya biashara kuanzia 1852 kushindwa kuangalia uhalali wa kampuni anazofanya nazo biashara?
Je kweli Rostam hakuijua kabisa hii kampuni? Kwa ukaribu aliokuwa nao inapita akili kufikiria kuwa alikuwa hajui RDC ni nini au kuhusika na mambo yao.
3. Mpaka sasa ni Mambo ya Umbea tu... hakuna kitu Tangible hata kimoja... umaskini wenu tu... kila mkimuona mtu tajiri mnadhani ameiba...
Hakuna umbeya, Rostam alikuwa anahusika na Richmond, that is an established fact. Suala pekee ambalo halikuweza kuonekana (siyo kwamba halipo) ni kuwa halionekani.
4. Narudia... tunaomba kuona -ushare-holding wa Rostam Aziz, kwenye hizo kampuni mnazozungumzia kama hamna... acheni mambo ya kitoto hapa!
sawa kama ni utoto, lakini kwa kutuita watoto hakufanyi hoja zako kuwa na nguvu kama yule ndugu mwingine ambaye asipokubaliana na wengine anawaita wapumbavu! Rostam alikuwa na hisa kwenye RDC... he knows it na mtu yeyote ambaye angeamua kufuatilia suala hili lilipoanza 2006 angeona hivyo. Wengine tulishafanya uchunguzi mapema sana na kuestablish the following facts. (tafuta maswali yangu 10 kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU kuhusu Richmond - 2006).
a. RDC iliingia nchini kwa ushirika wa Mhe. Msabaha (Mbunge - Waziri wa Madini)
b. RDC iliingia nchini kwa ushirika wa Jakaya Kikwete (Mbunge)
c. RDC (USA) wametoa mchango mkubwa katika kampeni ya Kikwete na Msabaha
d. Rostam Aziz ndiye mfanyabiashara aliyetengeneza mazingira ya wao RDC kujikita kwenye biashara hiyo ya energy. Yeye mwenyewe akiwa ni shemeji ya Kikwete.
e. Naeem Gire waliingia na asilimia 75 ya RDC (tanzania) na asilimia 25 zilizobakia zikigawanywa miongoni mwa wahusika wakuu.
yes I said it! RDC inahusiana na Msabaha, Kikwete, Rostam na familia ya kina Gire ambao ni wachangiaji wa kampeni za uchaguzi CCM (2005). Kupewa kwa mradi wa bomba la mafuta 2005 na miezi michache baadaye mradi wa majenereta ilikuwa ni shukrani ya CCM kwa michango ya kina Gire katika kampeni za Msabaha na Kikwete na pia kama nafasi ya kuvuna walipopanda hasa baada ya JK alipoingia madarakani kumchukua Msabaha na kumuweka kuwa Waziri wa Nishati na Madini.
so, now you know.