Rostam abonga na Hichilema kuzalisha umeme nchini Zambia. Pia aangazia usambazaji wa gesi

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,446
7,822
Rostam Aziz amekutana na Rais wa Zambia, Haikande Hichilema mjini Lusaka na wamejadiliana kuhusu uwekezaji kwenye sekta ya nishati na madini.

Taifa group kupitia kampuni yake tanzu ya Taifa Gas tayari imeingia ubia na kampuni ya Delta Marimba ya Zambia kuzalisha megawat 100 kwa kutumia gesi. Uwekezeji wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 100.

Screenshots_2023-10-23-10-09-36.png

Karibuni pia Rostam amewekeza nchini Kenya na Rwanda kwa kujenga sehemu za kuhifadhi gesi ya LPG zenye uwezo wa kuhifadhi tani 30,000 na 25,000. Taifa Gas inaangalia fursa kama hiyo nchini Zambia.

Citizen
 
naona deal la umeme Zambia limezinguliwa ili mwamba apate nafasi na hpa ni Rostam na Abdul bila shaka
 
Watu kama kina Rostam Aziz ma local na international lobbyists wanahitajika sana, naamini mbali ya gesi pia amechomekea suala la malori ya Tanzania pia reli ya TAZARA intermodal transportation kutafutiwa ufumbuzi biashara ya usafirishwaji kuvuka mipaka changamoto zipungue nchi zizidi kufunguka kivitendo badala ya siasa za kishamba za uzalendo uchwara.

Wizara za mambo ya nje, biashara na viwanda wawe wanakaa naye wapewe madini kwa ajili ya kupika mabalozi ambao wanauwezo wa kushawishi na kuingia popote kusawazisha mambo biashara za kuvuka mipaka ya kikanda na hata bahari na makontineti za watanzania zizidi kusambaa na pia kuvutia uwekezaji pale mtaji wetu unapokuwa mdogo.

Fikiria dizaini ya wafanyabiashara kina Rostam na rais William Ruto hustler rais Uhuru Kenyatta, rais Freeman Mbowe na rais Hichilema wote hawa wenye background ya biashara nchi hizi zingechangamka vizuri kibiashara maana wanaelewana lugha na mikiki ya biashara za kuvuka mipaka
 
Back
Top Bottom