Mkuu not assumptions kwenye uongozi na hizi kazi za madaraka you need to be squeaky clean.., harufu yoyote ya rushwa na ufisadi he/she needs to step down na akajaribu kazi nyingine..., try umachinga, barmaid au biashara for all I care. Hapa hatutaki tukushike na ngozi ndio tujue umeiba.., !!!!
if one person calls you a chicken you say maybe they are crazy,
if two people calls you a chicken you start wondering, maybe am a chicken...
if 3 people say you are a chicken you better start laying some eggs...
Kama kila mtu anasema wewe ni Fisadi.... Sure as Hell wewe ni Fisadi
Huu ni ushindi kwa wapambanaji dhidi ya UFISADI (bila kujali chama). Hakuna cha mahakama wala cha nini, mtindo ni mmoja wa magamba kujidondosha yenyewe. Huyu bwana alikuwa ni chief architect wa EPA pamoja na wajukuu zake: KAGODA na MEREMETA ambao walichangia ushindi wa kishindo wa Mhe Dkt Dkt Dkt JK wa 2005. Baadaye akawa chie engineer wa DOWANS binti RICHMOND ambayo imechangia hiki KIZA tunachokishuhudia leo hii. Huyu bwana atapata jahanamu yake hapa hapa duniani!!!
Kujiuzulu haitoshi, na pesa yetu arudishe!
Hii sinema ndio kwanza inaanza; cdm kaeni mkao wa kula mfadhili anakuja huyo! Najua baada ya hapa ni kufanyiziana mbele kwa mbele, wale waheshimiwa wabunge waliofika hapo walipo kwa msaada wa huyu bwana mkubwa, jitukezeni mhesabiwe ili tumpeleke huyu bepari mbele ya sheria.
Ha ha! You say so because you know (CCM) as the accuser have no guts of taking him to court. Your doing good job defending him legally, but you can not change his image (especially politically) to the society, unless he put his effort to do so. If what your saying was applicable in Tanzania no one would bother to burn those vibakas in the street (take matters on their hand). So, although your trying hard to defend him legally here, I doubt if it is worth the effort. I should also remind you; you are in "Jukwaa la Siasa" and not "Jukwaa la Sheria" so that being said your playing soccer in a basketball field.
Yeah, quite true bcoz hakuna mwanaume katika serikali mwenye balls za kumpeleka mahakamani. serekali yote iko fukoni!!!
Hizo ni Gutter politics kama za NapeMwanangu Azizi we Jembe nimekukubali, uamuzi wako unaonyesha kweli we ni dume, wasikutishe hao wahuni na Mafisad wa Kichaga wa Chadema wamejaa maneno mengi ukiwachunguza zaidi utagundua fikra na matendo yao yapo kujinufaisha wao kama wachaga na sio jamii ya Tz. Wanaigunga tutakukumbuka sana kwa michango yako ndani na nnje ya Igunga. We gona mic u R Azizi.
Lakini, si angeweza kuyasema haya katika paragraph tatu tu. Nimejitahidi kusoma risala nzima naona zimejaa sifa tu za mazuri aliyowafanyia watu wa Igunga, na Watanzania kwa ujumla, lakini hajasema mabaya yeyote aliyoyafanya.
mkuu wewe uko nchi gani? habari ipo humu tangu kumekucha wewe ndiyo unakurupuka saa hizi!! ajabu sana,,, japo ungesoma vichwa tu vya habari hapa usingeandika hii.Naangalia saivi usiku wa habari, tbc bila chenga, rostam aziz ametangaza kujvua gamba
nawakilisha
Jamani mmeona sasa maneno hayo.Nape uliaswa usiwe mropokaji!Bado mzee wa rada,richmond,Wasaliti walioanzisha CCJ!kama kina Nape,Sitta(mnafiki mkubwa)Hiyo bado haitamtakasa. Haachie na ubunge.
Rostam Aziz said:Mara tu baada ya kumalizika kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ambacho kilichagua wajumbe wapya wa Kamati Kuu na kuidhinisha uundwaji wa Sekretarieti mpya, dhana ya kujivua gamba ambayo naamini Mwenyekiti wetu aliianzisha kwa nia njema ilianza kuenezwa ikichukua tafsiri na mwelekeo tofauti na ule wa awali.
Wajumbe wawili wa Sekretarieti, Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Bara), Mhe. John Chiligati, na Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Mhe. Nape Nnauye, walisikika wakitangaza kwamba Halmashauri Kuu ya Taifa ilikuwa imefikia uamuzi wa kuwapa siku tisini wale walioitwa watuhumiwa wanaokabiliwa na tuhuma za ufisadi ndani ya chama kujitoa katika nafasi zao za uongozi vinginevyo watafukuzwa na chama.
Wazee wangu, baada ya kushinikizwa sana na vyombo vya habari wawataje kwa majina wanasiasa waliokuwa wakituhumiwa kwa ufisadi ambao ni wajumbe wa NEC na ambao wanapaswa kujiuzulu nyadhifa zao, wajumbe hao wa Sekretarieti walikwenda mbele zaidi.
Baada ya awali kuwaeleza waandishi wa habari kwamba majina ya watuhumiwa hao yalikuwa yakifahamika kutokana na kuhusishwa katika kashfa tofauti kama zile za Richmond, EPA na ununuzi wa rada, mwishoni viongozi hao walikaririwa wakiyataja majina ya wanasiasa watatu kuwa ndiyo ambao walikuwa wakilengwa na maamuzi hayo.
Wazee wangu, nilishangazwa na kushitushwa na namna porojo na fitina za kisiasa zilivyofinyangwa kwa mara nyingine tena baada ya kusikia jina la mbunge wenu ambaye ni mimi, likitajwa kuwa miongoni mwa yale matatu ya viongozi waliokuwa wakitakiwa eti kupima wenyewe na kisha kuchukua uamuzi wa kujiuzulu nafasi zao za uongozi ndani ya NEC katika kipindi cha siku tisini.
Niliseme hili mapema. Mshangao na mshituko wangu haukusababishwa na kutajwa kwa jina langu, la hasha, bali namna uamuzi halisi wa NEC na hususani dhana nzima ya kujivua gamba ilivyoweza kupindishwa na wajanja wachache na kisha kuendeshwa kwa maslahi binafsi ya kikundi fulani cha watu.