"Uamuzi wangu wa kuachia nafasi zangu zote za uongozi nilizopata kwa tiketi ya CCM haukutokana na wala haumaanishi kukubaliana na shinikizo lililopotoshwa kuhusu azma ya utekelezaji wa dhana ya kujivua gamba, la hasha, bali dhamira ya dhati ya kuachana na siasa hizi uchwara (gutter politics) na kutumia muda wangu kushughulika na biashara zangu."
"Katika ulimwengu wa kibiashara wa leo, vita hivi ambavyo vinaweza kuonekana kuwa ni vidogo tu vyenye malengo ya kuchafuana kisiasa, vinakuwa na athari kubwa katika uhusiano wa kibiashara kuliko hata wale wasioelewa wanavyoweza kukadiria"
"mimi ni mfanyabiashara wa kimataifa."
"Baada ya kukaa na wanafamilia yangu, marafiki na washirika wangu wa kibiashara niliona halitakuwa jambo la busara hata kidogo kuendelea kuvutana na viongozi wa chama changu na wanachama wenzangu wa CCM katika mambo ambayo yanaweza kumalizwa kwa njia muafaka"Rostam Aziz kwa mujibu wa Fikira Pevu (13 july011)
Tujiulize huyu mtu kweli alikuwa kwenye siasa kwa lengo la kusaidia jamii au kulinda biashara zake ! kwani baada kashfa na tuhuma alizonazo zinaweza kuathiri biashara zake ameamua kuachia ngazi haraka ili kuendeleza michakato yake ya kibiashara.
Ushauri kwa watz na viongozi , uongozi ni kujitoa na kujitolea kwa watu walio kupa dhamana na sio eneo la kujinufaisha!
Mwisho haitoshi kujiuzulu kama kuna chochote cha Wtz alichochukua arudishe ili aende kwa amani hata akibadili uraia ni sawa 2!