elimukwanza
Senior Member
- Dec 27, 2010
- 169
- 23
Nimeisoma Hotuba ya Rostam na kuitafakari vizuri sana hatma ya maamuzi yake...
Bila shaka yaonyesha kazi nzuri imefanywa na Uongozi mpya ambao kwa mchezo wa Kibongo wamemzunguka Rostam na wenzake. Hongera Chiligati na Nnauye, hakika leo nimewaaminia kwa kazi yenu kutokana na kauli za Rostam kushangazwa na maamuzi ya uongozi mpya wa chama.
Sina uhakika kama aloyasema yote ni ya kweli lakini kama kweli amejiuzuru bila kupenda na kamalizia kwa maneno haya:- Napenda kuliweka hili sawa sawa. Uamuzi wangu wa kuachia nafasi zangu zote za uongozi nilizopata kwa tiketi ya CCM haukutokana na wala haumaanishi kukubaliana na shinikizo lililopotoshwa kuhusu azma ya utekelezaji wa dhana ya kujivua gamba, la hasha, bali dhamira ya dhati ya kuachana na siasa hizi uchwara (gutter politics) na kutumia muda wangu kushughulika na biashara zangu.
Hapa ndipo napomalizia na kusema JK kweli msanii maana kawazunguka Boyz 2Men, na mwisho wa siku kawaondoa wote na kabakia pekee mjengoni. Lakini kwa kumtahadharisha tu afahamu kwamba kazi ya kummaliza yeye kama wale waliotangulia na kuandika historia mpya nchini NDIO INAANZA RASMI!. Nyoka kujivua gamba sii hoja, sumu yake inabakia palepale. Hivyo, ukitaka kumuua nyoka lenga kichwa! na waganga wa kienyeji wanasema - Sumu ya nyoka hutibiwa na magamba yake!.
What next! yangu machoo....
Mkandara maneno hayo mazito na hakika yanakuja ila unapoyatoatoa hapa jf unayakwamisha maana yana maslahi kwa taifa.