Rostam awaparamia CHADEMA

Rostam awaparamia CHADEMA

Unahitaji kuwa makini kidogo! Source imeelezwa kuwa ni gazeti la mwananchi tena umewekewa hadi ukurasa (2). Alikuwa akiwahutubia wapiga kura wake kule Igunga. Unaweza kuchangia sasa...........
 
RA...Amesema maisha magumu kwa watanzania hayatokani na CCM, bali mfumo wa kidunia unaoendana na hali halisi ya sasa.
SOURCE: MWANANCHI PG2
Complete article.
.

hapa anajaribu kusema nini, kwamba na yeye maisha yake ni magumu? au ye sio mtanzania?
 
RA amesema yeye ni mwanasiasa makini na kamwe hababaishwi na wanasiasa uchwara.

Amesema maisha magumu kwa watanzania hayatokani na CCM, bali mfumo wa kidunia unaoendana na hali halisi ya sasa.

SOURCE: MWANANCHI PG2
Complete article.

MBUNGE wa Igunga,mkoani Tabora, Rostam Aziz amesema yeye ni mwanasiasa makini na kamwe hababaishwi na wanasiasa uchwara , ambao wamekua wakieneza maneno ya uongo na uzushi dhidi yake.

Akizungumza na wananchi wa mjini Igunga katika Viwanja vya CCM mjini Igunga jana, Rostam alisema kuna wanasiasa ambao kila kukicha, wamekuwa wakitoa maneno ya kuchafuana na kupakana matope.

Alisema hata hivyo , wanasiasa hao hawambabaishi.

Alisema mwanasiasa makini ni yule anayetoa hoja za ukweli na si anayetoa maneno ya kuhamashisha wananchi wafanye vurugu.

Aliwata wananchi wa jimbo hilo kuwaepuka watu hao kwa kuwa ni hatari kwa nchi.

"Hivi karibuni kumekuwa na chama cha siasga kinachoendesha propaganda na kupiga domo kwa kuwahadaa wananchi kwamba maisha magumu yanatokana na wao kuichagua CCM," alisema Rostam.

Aliongeza "watu hao ni waongo kwani maisha magumu hayatokani na CCM, bali mfumo wa kidunia unaoendana na hali halisi ya sasa."

Alisema kupanda kwa bei ya sukari na mafuta nchini, hakutokani na CCM na kwamba chama hicho hakina kiwanda cha sukari wala hakiagizi mafuta kutoka nje ya nchi.
Alisema hata nchi jirani Kenya na Uganda, nazo zimekumbwa na mfumuko wa bei ya bidhaa hizo ambapo bei ya sukari katika nchi hizo ni Sh2,000 kwa kilo sawa na Tanzania.

Alisema propaganda za kisiasa zinazoendeshwa na chama hicho ambacho hakukitaja kwa jina, zinalenga katika kuwapotosha watu.

Hata hivyo aliwataka wananchi kuyapuuzia maneno ya wanasiasa wa chama hicho kwa madai kuwa ni uongo.

Alisisitiza kuwa viongozi wa chama hicho ni waongo kuhusu madai wanayoyatoa.

"Nilikutana na Dk Wilibrod Slaa katika uwanja wa ndege wa Mwanza nikamuuliza kuwa nilisikia wakati ukihutubia wananchi wa Musoma kwamba Chadema mkichukua nchi mfuko mmoja wa saruji utauzwa Sh5,000 tu, lakini hakujibu," alisema Rostam.

Alisema kwa mtazamo huo aligundua kwamba maneno wanayozungumza Chadema ni ya kudanganya wananchi ili wawape ridhaa ya kuongoza nchi na si kuwaletea maendeleo kama walivyokuwa wakijinadi.

Alisema katika kipindi hiki kigumu, amegundua kwamba wananchi wa Igunga wana hali mbaya ya chakula na kwamba atahakikisha kuwa hawafi kwa njaa. Mbunge huyo aliwaomba wananchi wa Igunga kumuunga mkono ili afanikishe malengo yake ya kuwaletea maendeleo.

Kumbe RA naye ni kilaza! Hiyo ilikuwa statement, na siyo swali! alitegemea kupata jibu kwa swali lipi?
TAPELI WA KIHINDI AKIDHIHAKI VILAZA WA KIBONGO!
 
mwizi makini.
Ana makampuni yafuatayo yanayojulikana kwa sasa:
Richmond Dev Co
Dowans Costa Rica
Dowans Holdings
Dowans SA
Caspian
Mwananchi Communications
Trade Development Group(Tz)-(which own Morogoro and Mwanza Tannerries by majority shares)
Wembere Hunting Safaris(acquired and lent to his brother Akram Aziz)
Vodacom Tanzania
There are many more

Hivi TRA wanaweza kutuambia kodi anayolipa? huyu mwanasiasa "makini".
Nashawishika kukubaliana na hoja hapo juu kuwa si makini sana kama anavyo jigamba but a common economic criminal.
 
Waswahili walisema: Zimwi likujualo halikuli likakwisha!

Wengine kufeni tu!
 
Ana makampuni yafuatayo yanayojulikana kwa sasa:
Richmond Dev Co
Dowans Costa Rica
Dowans Holdings
Dowans SA
Caspian
T-tech
Mwananchi Communications
Trade Development Group(Tz)-(which own Morogoro and Mwanza Tannerries by majority shares)
Wembere Hunting Safaris(acquired and lent to his brother Akram Aziz)
Vodacom Tanzania
There are many more

Hivi TRA wanaweza kutuambia kodi anayolipa? huyu mwanasiasa "makini".
Nashawishika kukubaliana na hoja hapo juu kuwa si makini sana kama anavyo jigamba but a common economic criminal.

Duh,kweli makini
 
Alisema mwanasiasa makini ni yule anayetoa hoja za ukweli ......

Alisema kupanda kwa bei ya sukari na mafuta nchini, hakutokani na CCM na kwamba chama hicho hakina kiwanda cha sukari wala hakiagizi mafuta kutoka nje ya nchi.

KWELI ROSTAM NI MWANA SIASA MAKINI ANAE JUA KUJIBU KWA KUTOA HOJAAAAA...
 
Ana role kubwa sana kwenye vital sectors za Taifa letu and hence the well being of it,ameinvest kwenye infrastructures ie kampuni ya simu kama vodacom ambayo ni kwenye sector ya mawasiliano,construction company ,Kilimo ie Kagoda,madini,energy ie Dowans AKA Richmond,education,Real Estate,exportation of raw resouces ie Wembere Hunting and Trade Development Group(Tz) nk....Yuko everwhere na nchi iko mikononi mwake technically.
Kazi ipo.
 
Duh bata bubu naye kaongea leo. Hakika sinema limeanza kunoga, sijui wapiga kura wake wanategemea nini!
 
Jamani tumesema sana tumuache Mungu amushughurikie, yatupasa kuanza kumshukuru Mungu kwa kujibu maombi yetu.
 
ni kweli yeye (RA) ni mwanasiasa makini, unadhani ilikuwa kazi rahisi kumweka jk mikononi mwake! hata jimboni kwake amewageuza wananchi kuwa kama vimbola hata akiwatukana wanamshangilia na kumuabudu kuliko hata jk. umakimi wake ni katika kuwarubuni watu na kuiibia nchi bila jasho:smash:
 
Tangu lini RA akawa mbunge makini?? Grrrrrrrrhh. Yeye ni mwizi makini, siasa haiwezi. Tangu amechaguliwa kuingia bungeni vipindi vyote hajawahi kuuliza swali, sasa huyo utamwita mbunge makini. Cha kusikitisha na huko Igunga walikuwepo watu wanamsikiliza huyo MWIZI MAKINI. Siku yaja na wala haiko mbali ambayo hutakuwa na Makende ya kuwachezea watanzania.
 
Hajui kuwa viwanda vingi vya Sukari vilikuwa Mali ya Serikali na Vina Zalisha Sukari lakini Kiwanda Kama Cha Kagera Sugar wanaona ni bora kuuza nje ya nchi kuliko kusaidia soko la ndani ya Nchi.

Kama anashambulia matatizo ya kiuchumi Duniani; Tanzania haikupata na hilo tatizo as our Economy is not as Capitalist Money Economy as the Rich Nations.
 
Back
Top Bottom