Rostam awaparamia CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam awaparamia CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fangfangjt, Mar 15, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  RA amesema yeye ni mwanasiasa makini na kamwe hababaishwi na wanasiasa uchwara.

  Amesema maisha magumu kwa watanzania hayatokani na CCM, bali mfumo wa kidunia unaoendana na hali halisi ya sasa.

  SOURCE: MWANANCHI PG2

  Complete article.

  MBUNGE wa Igunga,mkoani Tabora, Rostam Aziz amesema yeye ni mwanasiasa makini na kamwe hababaishwi na wanasiasa uchwara , ambao wamekua wakieneza maneno ya uongo na uzushi dhidi yake.

  Akizungumza na wananchi wa mjini Igunga katika Viwanja vya CCM mjini Igunga jana, Rostam alisema kuna wanasiasa ambao kila kukicha, wamekuwa wakitoa maneno ya kuchafuana na kupakana matope.


  Alisema hata hivyo , wanasiasa hao hawambabaishi.


  Alisema mwanasiasa makini ni yule anayetoa hoja za ukweli na si anayetoa maneno ya kuhamashisha wananchi wafanye vurugu.


  Aliwata wananchi wa jimbo hilo kuwaepuka watu hao kwa kuwa ni hatari kwa nchi.


  "Hivi karibuni kumekuwa na chama cha siasa kinachoendesha propaganda na kupiga domo kwa kuwahadaa wananchi kwamba maisha magumu yanatokana na wao kuichagua CCM," alisema Rostam.


  Aliongeza "watu hao ni waongo kwani maisha magumu hayatokani na CCM, bali mfumo wa kidunia unaoendana na hali halisi ya sasa."


  Alisema kupanda kwa bei ya sukari na mafuta nchini, hakutokani na CCM na kwamba chama hicho hakina kiwanda cha sukari wala hakiagizi mafuta kutoka nje ya nchi.

  Alisema hata nchi jirani Kenya na Uganda, nazo zimekumbwa na mfumuko wa bei ya bidhaa hizo ambapo bei ya sukari katika nchi hizo ni Sh2,000 kwa kilo sawa na Tanzania.

  Alisema propaganda za kisiasa zinazoendeshwa na chama hicho ambacho hakukitaja kwa jina, zinalenga katika kuwapotosha watu.


  Hata hivyo aliwataka wananchi kuyapuuzia maneno ya wanasiasa wa chama hicho kwa madai kuwa ni uongo.


  Alisisitiza kuwa viongozi wa chama hicho ni waongo kuhusu madai wanayoyatoa.


  "Nilikutana na Dk Wilibrod Slaa katika uwanja wa ndege wa Mwanza nikamuuliza kuwa nilisikia wakati ukihutubia wananchi wa Musoma kwamba Chadema mkichukua nchi mfuko mmoja wa saruji utauzwa Sh5,000 tu, lakini hakujibu," alisema Rostam.


  Alisema kwa mtazamo huo aligundua kwamba maneno wanayozungumza Chadema ni ya kudanganya wananchi ili wawape ridhaa ya kuongoza nchi na si kuwaletea maendeleo kama walivyokuwa wakijinadi.


  Alisema katika kipindi hiki kigumu, amegundua kwamba wananchi wa Igunga wana hali mbaya ya chakula na kwamba atahakikisha kuwa hawafi kwa njaa. Mbunge huyo aliwaomba wananchi wa Igunga kumuunga mkono ili afanikishe malengo yake ya kuwaletea maendeleo.
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kakakuona kazungumza!
  mwanasiasa makini asiweza kuchangia mijadala mjengoni
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280

  mwizi makini.
   
 4. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  MWANASIASA MAKINI NDANI YA CCM,KAMA ANAWEZA KUONGOZA NCHI ILHALI YEYE SIO RAISI WALA WAZIRI MKUU

  he is the best among FOOLS
   
 5. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  best among STUPIDS
   
 6. M

  Marytina JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  king maker RA,hawa ni wale CCM wa kweli, ufisadi mbele.
  RA anafaa sana kwenye mfumo wa CCM.
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  alibaba and forty thieves
   
 8. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Siku zake zinahesabika bora azungumze sasa maana muda utakapowadia hatapata hiyo nafasi. Achague uraia mmojawapo kati ya alizonazo. Hawezi kutufanya mazuzu.
   
 9. k

  kisyesye New Member

  #9
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  RA, pamoja na kujigamba kuwa yeye ni mwanasiasa, lakini bado siasa zake ni za kinyonyaji kwa walipa kodi wa kitanzania. Nasema hivi kwa sababu yeye ndiye mkwapuaji wa mabillion ya shilingi za EPA, pili yeye ndiye mmiliki wa mitambo ya DOWANS, na ndiye anaidai fidia nchi yetu yenye umaskini mkubwa bilioni 94. Je, halioni hilo kuwa ni kati ya vitu vinavyomuongozea mtanzania ugumu wa maisha?

  Kimsingi RA aachane na siasa na pia kutaifishwa mali zake kwani mtu huyu ni hatari kwani amefikia hatua ya kuendesha nchi hii na kuimiliki dola ya Tanzania, hivyo yeye kuwa ndiye Amiri jeshi mkuu wa nchi hii.
   
 10. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Amesema wapi hayo maneno?source plz
   
 11. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Atarukaruka sana lakini kuna mwisho wake..
   
 12. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Source: Mwananchi pg2
   
 13. J

  Japhet Mosi JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 207
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanzilishi wa Richmond na mfuatiliaji HAZINA wa malipo ya TZS 152m kila siku hadi mkataba unavunjika na sasa hivi anasubiri TZS 95billion kisha atuuzie mitambo kwa USD 60m. Ndiye aliyemweka kijana wake William Ngeleja alipo ili madili yote yafanikiwe. Ndiye anayeitaka roho ya Mwakyembe na wenzake ili madili yatiki na mambo yake yaende vizuri. Kama ng'ombe anayetoa maziwa mpaka damu itoke kisha ahamie either Kanada au arudi kwao Uajemi (Persia) a.k.a Iran
   
 14. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Ni mara ya pili kuongea ndani na nje ya bunge kwa miaka 6. Kweli uyu mwanasiasa!
   
 15. U

  Upanga Senior Member

  #15
  Mar 15, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 135
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  AMA KWELI SISI NI MAZUZUUUUU! Anaongea tena kwa Jeuri huku wa Tanzania tunaangalia,angekuwa KIBAKA kaiba simu ya Mkononi sasa hivi kasha chomwa moto.
  Inafikia sehemu anasema yeye ni mwana siasa makini
   
 16. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Sasa kama yeye ndo mwendesha Nchi, nani atathubutu kuzisogelea mali na kumfilisi! Mwakyembe alimtaja tu kuwa RA ndo dowans angalia matokeo yake! RA anataka Kumsaidi israel kuondoa roho ya mwakyembe. CCM kwame hawawezi kumsogelea RA, nguvu ya umma ndiyo iliyobaki, lazima tuwang'oe wote waliomkumbatia huyu bigwa wa kuwatesa watanzania
   
 17. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Alikuwa anaongea na muadishi au ni Tangazo la biashara kwenye gazeti?

  Kwa nini huyo muandishi asimuulize kama dowans ni mfano mmoja wa mifumo hiyo ya kinyonyaji ya kidunia sawa na WB,IMF, EPA, KAGODA etc.
   
 18. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #18
  Mar 15, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Anajua Chadema wakishika nchi atakuwa mfungwa no 1 wa serikali ya Chadema
   
 19. C

  Chesty JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,350
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Adui wa masikini wa Tanzania, ipo siku tu, nayo yaja upesi. Haiwezekani watu wateseke ndani ya nchi yao kwa ajili yake halafu yeye aendelee tu kupeta.

  Ipo siku watanzania watasherehekea kutokuwepo kwa nyang'au huyu kama babu zetu walivyosherehekea kumng'oa mkoloni.
   
 20. T

  Tiote Senior Member

  #20
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pamoja na uchanga wako kwenye JF lakini umenena kitu ambacho wengi humu wamekuwa waoga kukizungumzia. Huyu bwana ana bahati kwamba yuko Tanzania na ndiyo maana anaweza kuongea maneno ya kejeli na dharau iliyopitiliza kama anavyofanya sasa. Lakini kila mwizi ana arobaini zake na yeye asubiri zake zitafika tu! Asijione mjanja!
   
Loading...