Nikifufukammekwisha
JF-Expert Member
- Aug 17, 2007
- 260
- 6
Tuliombee Taifa Rostam Aziz
Sunday, July 6, 2008
Asema watu wanachukiana na kuombeana vifo
Adai wanazushiana uchawi, anapakaziwa fisadi
Aomba kanisa litumike kurejesha taifa katika mstari
Dar es Salaam, Julai 6, 2008
MBUNGE wa Igunga, Bw. Rostam Aziz amesema taifa liko katika wakati mgumu kisiasa na kijamii na ameomba watu watumie makanisa kulirejesha katika mstari ulio sahihi.
FMES... utazua kasheshe... nani kawaambia mwili wa Ballali ulichomwa..?
Tuliombee Taifa – Rostam Aziz
Sunday, July 6, 2008
Asema watu wanachukiana na kuombeana vifo
Adai wanazushiana uchawi, anapakaziwa fisadi
Aomba kanisa litumike kurejesha taifa katika mstari
Dar es Salaam, Julai 6, 2008
MBUNGE wa Igunga, Bw. Rostam Aziz amesema taifa liko katika wakati mgumu kisiasa na kijamii na ameomba watu watumie makanisa kulirejesha katika mstari ulio sahihi.
Bw. Rostam ametoa mwito huo leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi na kuweka wakfu albamu ya kwaya ya Amkeni ya Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kinondoni, iliyofanyika katika viwanja vya kanisa hilo ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Amesema waumini wa dini hawamtuhumu mtu, hawamshutumu, hawapendi wenye wivu na wenye chuki bali wanapenda haki, na kwamba licha ya kashfa za ufisadi anazozushiwa, wamepuuza hilo na wamejenga imani kwake.
"Nawashukuru kwa kuamua kunialika kuwa mgeni rasmi… ni ishara kwamba mmeamua kupuuza maneno na upuuzi wa vijiweni. Nafurahi kuwa miongoni mwenu…. hamtuhumu, hamshutumu, hampendi wenye wivu na wenye chuki, mnapenda haki. Ninao watoto watatu na nataka niwalee katika misingi hii," alisema Rostam huku akishangiliwa na umati wa watu waliofurika katika hafla hiyo.
Mwaka 2005, Rostam pia alishiriki katika harambee ya ujenzi wa jengo la Kanisa la KKKT Kinondoni ambalo kwa sasa linatumika kama Chuo Kikuu cha Tumaini.
Balali huko aliko akiskia story kua inadhaniwa alichomwa moto basi lazma mwili umsisimke kwa hisia za kiberiti..
FMES... utazua kasheshe... nani kawaambia mwili wa Ballali ulichomwa..?
Ni lile anaposali Spika Samwel Sitta... (KKKT Kinondoni).
Aichangia kwaya Tshs Milioni 7...
Amalizia na kuwaomba waumini kuiombea nchi kwani iko kwenye kipindi kibaya cha watu kutafutana uchawi na kuonesha hali si shwari nchini.
Zaidi tusubiri kutoka vyombo vya nyumbani kwani walikuwepo wengi. Wasipoandika tutaandika!
By the way, according to the dataz ni kwamba hivi karibuni watoto wawili wa Balali, walikwenda Iringa huko nyumbani kijijini na ki-box kidogo kinachosadikiwa kuwa na mabaki ya mwili uliochomwa wa Balali na kufanyika maombolezo rasmi kwa wanafamilia huko Iringa, shughuli hiyo pia ilihudhuriwa na waziri mmoja wa serikali ya sasa,
Wanafamilia wamekasirika sana kuona mjane hakutokea na watoto na mabaki ya mwili, samahani wakuu nilitaka kuhabarisha tu the up-to-dates.
Ahsante Wakuu!
JMushi.
Salama mkuu. Mie siamini RA kwenda kanisani anakosali Sitta ni makosa ya Sitta. Siamini kama kweli Sitta anajaribu kumsafisha RA. Tusijeanza kupandikiza chuki dhidi ya Sitta kisa RA kaenda pale na kuchangia Kwaya. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko wazi linapokuja suala la dini. Mtu anaweza kwenda kuabudu mahala popote bila kuvunja sheria.
Mtu yeyote naamini alikuwa ana uwezo wa kuchangia pale awe mkatoliki au muislamu. Mie nilipokuwa huko niliwahi kwenda msikitini mara kadha nikiwa ni aliyekuwa boss wangu (Marehemu) ambaye pia alikuwa msaidizi wa Rais. Lakini mie nimezaliwa, nikakulia na nitazikwa kama mkristo.
Naamini tatizo tulilonalo hapa si RA kwenda kanisani bali hizo fedha alizochangia tunaamini ni fedha chafu. Na fedha chafu haziwezi kupelekwa kanisani au msikitini. Watu wengine wanaweza kuamini pesa hizo ni safi kutokana na shida zetu watanzania lakini ukweli hizo pesa ni chafu. Hakuna anayemdanganya Mungu bali tunajidanganya sisi wenyewe,
Hivyo ningependa uondoe hiyo dhana kuwa Sitta anajaribu kumsafisha Rostam. Hili ni ombi na wala si lazima. Ombi laweza kukubaliwa au kukataliwa, naogopa kuwa watu wanaweza kujenga dhana kulingana na maneno hayo kuwa Sitta anamsafisha RA halafu wakajenga chuki dhidi yake kwa kitu ambacho hatuna ushahidi. Siko hapa kumtetea RA. Hata Makamba (akiwa Mkuu wa Mkoa Dar )alipokuwa anachangisha harambee kwa ajili ya shughuli za KKKT kule Arusha siamini kama alikuwa anajisafisha lakini twende KULIA, KUSHOTO, NYUMA na MBELE ukweli ni kwamba Pesa za RA ZINANUKA but but..... Siamini kama Sitta anajaribu kumsafisha tena kanisani.
...Sasa ni Mchungaji,wanakwaya ama Six mwenyewe ndiye aliyemwalika?
Kwa mtizamo wangu ni WOTE WALIOMWALIKA! Na wala hakujialika mwenyewe!
some reasoning is not just flawed but extremely unreasonable..!
Rostam alisema watu wanachukiana mpaka kufikia hatua ya kuzushiana uchawi na kuombeana vifo. "Tutumie makanisa kukemea vitu hivi ili kurejesha taifa katika mstari ulio sahihi," alisema