Rombo Green View Hotel na huduma tata ya massage

Rombo Green View Hotel na huduma tata ya massage

Siku nyingine ukitaka kuja mjini hakikisha unapata semina elekezi kwanza.
 
Karibu Dar es Salaam wa Mkoani
Huku Zanzibar naona ndio ungeshangaa kabisaaa,maana zipi Za Kumwaga
hizo massage parlour zipo kibao sana,halafu faham kuwa ni Treatment na kuna ma therapists kwenye Parlour hizo.

Ungenza kushangaa kwenye Salon za kiume ambazo zinatoa huduma kama hiyo.Ila umevyoanza kushangaa kwenye Hotel,aisee unatia aibu sana.
 
Mbona kwenye hiyo lift kuna tangazo la m pesa na la shoe shine, mbona hujaliongelea? Una pepo wa ngono wewe.
 
Its obviuos muanzisha thread hajui maana ya massage ,,kwanza massage parlors in a way zinaongeza hadhi ya hoteli!!!
 
Kwa wingi wenu kuwa na mtazamo huo, baasi tena , niwape pole watumishi wa mungu maana muu waumini ninyi.
Nilichosema ni kuwepo kwa massage tata, shetani kawatoa mapovu kwa kuingilia anga zenu
Astakafiri wengine eti mmefunga mnavuta vuta muda wa kufuturu
 
Kwa posts nilizopitia kuhusu mada hii hapa jamvini nadhani mleta mada husika atakuwa amejifunza kitu. Kama hakujifunza basi alitakiwa awe amejiunga na ile kozi maalumu ya Diploma ya ualimu pale UDOM.
Nimejifunza aise ubongo wenu umejazwa na mambo ya ibilisi maana nimeshambuliwa kwa na kuonekana mshamba kwa kuona pale pana zaidi ya massage
Any way Mungu bariki Tanzania
 
Jana nilibahatika kulala Rombo, nikapewa chumba cha juu kabisa. Sasa kwenye lift wakati napanda ghorofani, nikaona tangazo kwenye lift, "Huduma ya massage".

Nikachukua simu kutaka kujua ni nini hii, na ni shilingi ngapi? Kupiga akapokea mdada akanambia Massage 40,000/=. Nikamwambia Nina 10,000/= naweza pata kila kitu? Akashangaa elfu 10 kila kitu? Ongeza utapata.

Sikutegemea kuwepo kwa Huduma hii haswa hotel hii ambayo hata mwenye hotel atakuwa ameidhinisha kuwepo na kuruhusu no za simu zikawekwa kwa lift ili kujitangaza.

Nilikueshimu sana Rombo. Ntatafakari tena heshima yangu kwako baada ya kupata mawazo yenu wadau.

Karibuni..

Ni bei gani kulala rombo? Tuanzie hapo!!!! We Kama uliulizia kila kitu ulitaka ujibiweje? Na kila kitu maana yake Ni nini? Mawazo yako negative yatakuponza.
 
Wewe ndo ulianza kuwauliza "kila kitu utapata???"....ila wenyewe walisema Massage tu...sasa wao na wewe yupi mwenye maovu???????????????? [emoji22][emoji22][emoji58][emoji51][emoji28][emoji5]
 
hongera kulala Rombo chumba cha juu kabisa
 
Wewe ulipouliza huduma ya ziada ulimaanisha nini?
Je, ni jibu gani walikupati?
Je, uliridhika na hilo jibu?
Je, hiyo huduma ulikuwa unaihitaji?
Je, ulijuaje kwenye massage huwa kuna huduma za ziada?
Je, ni roho gani alikuongoza kuulizia hiyo huduma?

Hebu tuanze na hapo kwanza, ukinipa majibu tutaendelea.

Nimeona shetani asivyo na huruma
 
Back
Top Bottom