Full Text: Hotuba ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mapato na Matumizi 2015/2016

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI, MHESHIMIWA WILLIAM V. LUKUVI (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2015/16

A. UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, kutokana na Taarifa iliyowasilishwa leo ndani ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa kazi za Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka wa fedha 2014/15 na malengo ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2015/16. Aidha, naliomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2015/16. Pamoja na hotuba hii nimewasilisha kitabu kinachoonesha taarifa ya utekelezaji wa kazi mbalimbali za Wizara pamoja na taasisi zake ikiwa ni sehemu ya hotuba yangu. Naomba Bunge lipokee taarifa hiyo na ijumuishwe kwenye Hansard.

2. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kuwapongeza Mawaziri na Naibu Mawaziri walioteuliwa na Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuingia katika Baraza la Mawaziri kufuatia mabadiliko aliyoyafanya mwezi Januari, 2015. Mawaziri hao ni Mhe. Dkt. Mary Michael Nagu, (Mb.), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu; Mhe. Jenister Joakim Mhagama, (Mb.), Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge; Mhe. Christopher Kajoro Chiza (Mb.), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji na Uwekezaji; Mhe. Steven Masatu Wassira (Mb.), Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika; Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb.), Waziri wa Nishati na Madini; Mhe. Dkt. Harrison George Mwakyembe, (Mb.), Waziri wa Afrika Mashariki na Mhe. Samuel John Sitta (Mb.), Waziri wa Uchukuzi. Aidha, nawapongeza Mhe. Angellah Jasmine Kairuki (Mb.), Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. Steven Julius Masele (Mb.), Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais; Mhe. Charles John Mwijage (Mb.), Naibu Waziri, Nishati na Madini na Mhe. Anne Kilango Malecela (Mb.), Naibu Waziri, Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Vilevile, nampongeza Mhe. George Masaju kwa kuteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Mhe. Dkt. Grace Khwaya Puja na Mhe. Innocent Rwabushaija Sebba kwa kuteuliwa kuwa Wabunge. Nawatakia wote kila la heri katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

3. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kumshukuru Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuniteua kuiongoza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Aidha, nampongeza yeye binafsi pamoja na Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri


ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mpanda Mashariki, kwa jitihada zao za kuongoza, kusimamia na kuendeleza amani, utulivu na maendeleo ya nchi yetu. Nawashukuru kwa ushauri, maelekezo na ushirikiano wanaonipa ambao unaniwezesha kutekeleza majukumu niliyokabidhiwa ya kuongoza sekta hii mtambuka na muhimu katika maendeleo ya Taifa letu. Nawapongeza kwa dhati Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi; Mhe. Maalim Seif Shariff Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar; na Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mbunge wa Kitope, kwa mafanikio makubwa yanayoendelea kupatikana katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

]Mheshimiwa Spika, naomba pia kuwashukuru Mhe. Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka (Mb.), aliyeongoza Wizara kabla yangu; Mhe. Goodluck Ole Medeye (Mb.) na Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb.)

4 waliokuwa Manaibu Waziri kwa kuweka misingi imara ya kusimamia sekta ya ardhi.

5. Mheshimiwa Spika, naomba kuchukua fursa hii kumpongeza Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Peter Pinda, Mbunge wa Mpanda Mashariki kwa hotuba yake iliyoeleza malengo ya Serikali na mwelekeo wa utendaji wa sekta mbalimbali pamoja na kazi za Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/16. Naahidi kwamba Wizara yangu itayafanyia kazi yale yote yanayoihusu sekta ya ardhi.

6. Mheshimiwa Spika, nakupongeza wewe kwa kuongoza shughuli za Bunge kwa ufanisi. Pia, nampongeza Mhe. Job Yustino Ndugai, Mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa Bunge letu kwa utendaji mzuri katika uendeshaji wa shughuli za Bunge. Vilevile, ninawapongeza Wenyeviti wa Bunge ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakiongoza shughuli za Bunge. Ni ukweli usiofichika kwamba wamemudu vema jukumu hili la kuongoza Bunge lako Tukufu kwa ufanisi

mkubwa. Mwenyezi Mungu aendelee kuwaongoza na kuwapa nguvu, afya na hekima za kumudu zaidi majukumu yao.

7. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee natoa shukrani zangu za dhati kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira inayoongozwa na Mwenyekiti Mhe. James Daudi Lembeli (Mb.) na Makamu Mwenyekiti Mhe. Abdulkarim Hassan Shah (Mb.) kwa ushirikiano mkubwa na ushauri wao ambao unaiwezesha Wizara kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Ushauri wao utaendelea kuzingatiwa wakati wote wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara hii. Vilevile, natoa shukrani za pekee kwa Naibu Waziri, Mhe. Angellah Jasmine Kairuki (Mb.), kwa ushirikiano na msaada mkubwa anaonipatia wakati wa kutekeleza majukumu ya sekta ya ardhi. Pia, ninawashukuru Katibu Mkuu Bw. Alphayo Japani Kidata; Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Selassie David Mayunga; Wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi zilizo chini ya

Wizara yangu pamoja na watumishi wote wa sekta ya ardhi katika ngazi zote kwa kutekeleza majukumu yao.

8. Mheshimiwa Spika, nilipokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mhe. Kapteni John Damiano Komba aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi. Naungana na Waheshimiwa Wabunge wenzangu kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu, ndugu na wananchi wa Jimbo la Mbinga Magharibi pamoja na wale wote walioguswa na msiba huo. Kadhalika, wapo wananchi waliofariki katika maafa na ajali mbalimbali nchini na wengine kujeruhiwa. Nachukua fursa hii kutoa pole kwa wafiwa wote Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi, Amina. Aidha, nawatakia afya njema waliojeruhiwa.

B. MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2014/15 NA MALENGO YA MWAKA WA FEDHA 2015/16

9. Mheshimiwa Spika, naomba nieleze kwa kifupi utekelezaji wa bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2014/15 na malengo kwa mwaka wa fedha 2015/16. Napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa taarifa za utekelezaji zinaishia mwezi Aprili, 2015.

Ukusanyaji wa Mapato

10. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara ilipanga kukusanya shilingi bilioni 61.32 kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato yanayotokana na kodi, ada na tozo mbalimbali za ardhi. Hadi Aprili, 2015, Wizara imekusanya shilingi bilioni 47.0 sawa na asilimia 76.6 ya lengo na ikiwa ni ongezeko la shilingi bilioni
3.8 ikilinganishwa na shilingi bilioni 43.2 zilizokusanywa mwaka 2013/14. Aidha, katika mwaka wa fedha 2014/15, Wizara iliendelea kuhimiza wamiliki wa ardhi

kulipa kodi ya ardhi, ada na tozo mbalimbali kupitia benki. Hatua hii inalenga kuongeza ukusanyaji wa maduhuli na kudhibiti uvujaji wa mapato.

11. Mheshimiwa Spika katika mwaka wa fedha, 2014/15 Wizara iliahidi kuhuisha viwango vya kodi, ada na tozo mbalimbali za ardhí ambavyo vilionekana kuwa kikwazo kwa wananchi wanaohitaji huduma za ardhi. Uhuishaji huu wa viwango vya kodi, tozo na ada za ardhi umelenga kupata viwango vinavyopangika, kukubalika na kulipika. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba kazi hiyo imekamilika.

12. Mheshimiwa Spika, baada ya kuhuisha viwango hivyo, wananchi wa kipato cha chini watamudu kulipa kodi, tozo na ada hizo. Kodi ya pango la ardhi imepungua kwa wastani wa asilimia 30 na viwango vingine vinavyomgusa mwananchi wa kawaida vimepungua kwa asilimia
50 au zaidi. Kwa mfano, kodi ya kupima mashamba imepunguzwa kwa asilimia 60 kutoka shilingi 1,000 hadi shilingi 400 na mashamba ya biashara imepunguzwa kwa asilimia 50 kutoka shilingi 10,000 hadi shilingi 5,000 kwa ekari; ada ya upimaji ardhi imepunguzwa kwa asilimia
62.5 kutoka shilingi 800,000 hadi shilingi 300,000 kwa hekta; nyaraka za tahadhari na vizuizi (Caveat) vimepunguzwa kwa asilimia
66.7 kutoka shilingi 120,000 hadi shilingi
40,000, nyaraka za ubadilishaji wa majina (Deed Poll) zimepungwa kwa asilimia 62.5 kutoka shilingi 80,000 hadi shilingi 30,000, usajili wa nyaraka nyinginezo zimepunguzwa kwa asilimia 50 kutoka shilingi 80,000 hadi shilingi 40,000. Vilevile gharama za kupata nakala ya hukumu kwenye Mabaraza ya Ardhi zimepunguzwa kwa asilimia 62.5 kutoka shilingi 16,000 hadi shilingi 6,000, ada ya maombi ya kumiliki ardhi imepunguzwa kwa asilimia 75 kutoka shilingi 80,000 hadi shilingi 20,000, na ada za maandalizi ya hati imepunguzwa kwa asilimia 68.8 kutoka shilingi 160,000 hadi shilingi 50,000. Viwango hivi vitaanza kutumika tarehe 1 Julai, 2015 na vipo katika kitabu cha kodi, ada na tozo mbalimbali za sekta ya ardhi ambacho kimesambazwa pamoja na hotuba hii.

13. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa viwango vya tozo ya mbele (premium), kuanzia mwaka wa fedha 2015/16 tozo hii itapunguzwa kwa asilimia 50 kutoka asilimia 15 ya sasa hadi asilimia 7.5 ya thamani ya ardhi na kiwango hiki ndicho kitakacholipwa kwa mashamba na viwanja wakati wa kumilikishwa. Kama ilivyo kwa marejesho ya ada, kodi na tozo nyingine za sekta ya ardhi, asilimia 30 ya maduhuli yote yatakayokusanywa kutokana na tozo hii yatarudishwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na matumizi yake yataelekezwa katika kuboresha sekta ya ardhi. Kwa kuwa viwango vya kodi za ardhi sasa ni rafiki, natoa rai kwa wamiliki wote wa ardhi kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati.

14. Mheshimiwa Spika, baada ya marekebisho ya viwango vya kodi kufanyika, katika mwaka wa fedha 2015/16, Wizara inatarajia kukusanya shilingi bilioni 70. Lengo hili litafikiwa kwa kutekeleza mikakati ifuatayo:-

a) Kutumia njia ya kielektroniki kukusanya kodi ya pango la ardhi, ada na tozo mbalimbali;

b) Wamiliki wa mashamba na viwanja kulipa kodi ya ardhi kupitia Benki;

c) Kushirikiana na Wizara ya Fedha kurejesha asilimia 30 ya makusanyo kwa wakati kwenye Halmashauri kwa lengo la kuchochea ukusanyaji wa kodi ya ardhi;

d) Kuhamasisha wamiliki wa ardhi kwa njia ya matangazo kwenye magazeti, redio, luninga na vipeperushi kulipa kodi kwa wakati; na

e) Kufuta milki za wamiliki wanaokiuka masharti ya umiliki ikiwemo kutokulipa kodi ya ardhi kwa wakati.

15. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2015/16, Wizara yangu itaboresha ukusanyaji wa kodi, ada na tozo mbalimbali za sekta ya ardhi kwa kuanzisha mfumo wa kielektroniki wa ulipaji utakaotumia simu za viganjani. Mfumo huu unatarajiwa kuanza kutumika tarehe 1 Julai, 2015 na utarahisisha ulipaji wa maduhuli, kupungaza adha ya msongamano na kupoteza muda kwenye vituo vya malipo. Aidha, huduma ya ukadiriaji wa pango la ardhi na uboreshaji wa taarifa za wamiliki wa viwanja na mashamba itapatikana kupitia simu ya kiganjani. Natoa wito kwa wananchi nchini kuupokea na kuutumia mfumo huo wa kulipa maduhuli yatokanayo na sekta ya ardhi kwa njia ya kielektroniki.

Matumizi

16. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara iliidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 85.74 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo shilingi bilioni
11.54 zilitengwa kwa ajili ya Mishahara; shilingi bilioni 40.05 kwa ajili ya Matumizi Mengineyo na shilingi bilioni 34.15 kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Kati ya fedha za miradi ya maendeleo, shilingi bilioni 13.3 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 20.85 ni fedha za nje. Hadi Aprili 2015, jumla ya shilingi bilioni 32.2 zilipokelewa, sawa na asilimia 37.6 ya fedha zilizoidhinishwa katika mwaka wa fedha 2014/15. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 10.38 ni mishahara na shilingi bilioni 21.82 ni matumizi mengineyo (OC). Aidha, hadi Aprili, 2015 Wizara haikupokea fedha za kutekeleza miradi (Jedwali Na. 1).

UTAWALA WA ARDHI

17. Mheshimiwa Spika, Tanzania imejaliwa kuwa na ardhi kubwa na ya kutosha kwa kila mwananchi kuweza kumiliki kipande cha ardhi kwa ajili ya shughuli za kiuchumi na kijamii. Kwa ukubwa wa nchi unaokadiriwa kuwa kilomita za mraba 947,000, kila Mtanzania anaweza kumiliki takribani ekari tatu. Ni jambo la kujivunia kuwa Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995, Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya mwaka 1999 zinatoa haki sawa kwa raia wote kumiliki ardhi sehemu yoyote ya nchi bila kujali jinsia wala sehemu mwananchi alikozaliwa. Changamoto iliyopo ni kuhakikisha kuwa ardhi yote inapangwa, kupimwa na kumilikishwa kisheria. Ili kukabiliana na changamoto hii, Serikali itaongeza kasi ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi kwa wananchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii na hivyo, kuongeza fursa za ajira, kupunguza umaskini na pia kukuza Pato la Taifa. yanayohusisha mamlaka za Halmashauri za Vijiji, Halmashauri za Wilaya na Miji. Majukumu na mamlaka za usimamizi yameainishwa vema katika Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995, Sheria ya Ardhi Na.4 ya mwaka 1999 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na.5 ya mwaka 1999. Lengo ni kuhakikisha kuwa wananchi wanashirikishwa ipasavyo katika suala zima la usimamizi wa rasilimali ardhi kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Taifa.

19. Mheshimiwa Spika, dhamira ya Serikali ni kuifanya ardhi kuwa kichocheo cha maendeleo na nyenzo muhimu katika kupambana na umaskini. Hivyo ni wajibu wetu kusogeza huduma za ardhi kwa wananchi na kutoa elimu kwa umma kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo ili wananchi waweze kuitumia ardhi ipasavyo kama mtaji hai kwa ajili ya kuanzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.

20. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara iliahidi kuigawa Kanda ya Mashariki kuwa kanda mbili, Kanda ya Dar es Salaam na Kanda ya Mashariki. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa Kanda ya Dar es Salaam imeanzishwa na inahudumia Manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni na Kanda ya Mashariki inahudumia mikoa ya Pwani na Morogoro. Hadi sasa Wizara ina Ofisi za Kanda nane ambazo ni Dar es Salaam, Mashariki, Kati, Ziwa, Kaskazini, Kusini, Nyanda za Juu Kusini na Magharibi.

21. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara yangu imeandaa rasimu ya mwongozo wa utaratibu wa kupanga, kuhakiki, kupima, kumilikisha na kusajili kila kipande cha ardhi. Hatua hii inalenga kuwaongezea watendaji wa sekta ya ardhi na wananchi kwa ujumla, uelewa wa pamoja kuhusu masuala ya ardhi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu. Aidha, Wizara imeandaa kitabu kwa lugha

rahisi kinachoelezea hatua mbalimbali zinazopaswa kufuatwa na wananchi ili kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na sekta ya ardhi.

22. Mheshimiwa Spika, Wizara inalo jukumu la kuteua wajumbe wa Kamati za Ugawaji Ardhi kulingana na Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 (Fungu
12) katika ngazi ya Taifa, Miji na Wilaya baada ya kupendekezwa na Halmashauri husika. Hadi sasa Halmashauri 119 kati ya Halmashauri 168 zina Kamati za Ugawaji Ardhi. Kamati hizi ni muhimu katika kushughulikia ugawaji ardhi nchini. Katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara imefanya uteuzi wa Wajumbe wa Kamati za Ugawaji Ardhi kwa Halmashauri za Wilaya zifuatazo: Mkuranga, Kibaha, Mlele, Uvinza, Musoma, Nzega, Ikungi, Mufindi, Kaliua, Busega, Kakonko, Biharamulo, Sikonge, Nsimbo na Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara/ Mikindani.

23. Mheshimiwa Spika, Kamati ya Taifa ya Ugawaji Ardhi pamoja na majukumu mengine, inalo jukumu la kupitia maombi ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji. Katika mwaka wa fedha 2014/15, Kamati hii ilipitia maombi 148 na kutoa ushauri wa kumilikisha viwanja 100 na mashamba 9 kwa ajili ya uwekezaji nchini. Natoa rai kwa Halmashauri zote ziwe na Kamati za Kugawa Ardhi ili kuongeza uwazi katika kugawa ardhi.

Hazina ya Ardhi (Land Bank)

24. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2015/16 Wizara imejiwekea lengo la kutambua maeneo ya ardhi yenye ukubwa wa ekari takriban 200,000 nchini na kuwa sehemu ya Hazina ya Ardhi kwa ajili ya uwekezaji na matumizi ya umma. Kwa kuzingatia mahitaji ya fidia kwa ajili ya utwaaji wa maeneo hayo, Serikali imetenga shilingi bilioni 5 katika Mfuko wa Fidia ya Ardhi (Land Compensation Fund) kwa ajili ya kulipa fidia ya maeneo yatakayotwaliwa. Aidha, hadi Aprili 2015, Serikali imebatilisha milki za mashamba mawili (Ufyome katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati katika mkoa wa Manyara na Fort Ikoma mkoani Mara) na viwanja 67 nchini kote. Vilevile, uhakiki na ukaguzi wa mashamba pori yaliyotelekezwa na wamiliki utaendelea kufanyika ili kuitwaa au kubatilisha na kuihifadhi kwenye Hazina ya Ardhi.

Utekelezaji wa Sheria za Ardhi

25. Mheshimiwa Spika, Wizara inashughulikia utoaji wa Hati, Vyeti vya Ardhi ya Vijiji na Hati za Hakimiliki ya Kimila. Katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara iliahidi kutayarisha na kutoa Hati Miliki 40,000. Hadi kufikia Aprili 2015, Wizara iliandaa na kusaini Hati Miliki 20,189 sawa na asilimia 50.5 ya lengo (Jedwali Na. 2). Kanda iliyoongoza kuandaa hati nyingi zaidi ni Dar es Salaam (hati 4,491) ikifuatiwa na Kanda ya Kusini Magharibi (hati 3,516). Kanda iliyoandaa hati chache zaidi ni Kati (hati 680). Aidha, Halmashauri iliyoongoza kuandaa hati nyingi zaidi ni Temeke (hati

1,959). Hata hivyo, Halmashauri ambazo hazikuandaahatiaukuwamilikishawananchi ardhi ni Iramba, Singida (W), Mkalama, Masasi (W), Lindi (W), Nyang'wale, Butiama, Mpanda (W), Nsimbo, Mlele, Kaliua, Ushetu, Msalala, Buhigwe, Kigoma(W), Kibondo, Kilindi, Momba na Busokelo. Katika mwaka wa fedha 2015/16 lengo la Wizara ni kuandaa na kutoa Hati Miliki 40,000. Napenda kurudia wito wangu kwa Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinamilikisha viwanja vyote vilivyopimwa na kuandaa Hati ili wananchi waweze kuwa na milki salama za ardhi na kila mwaka ziwe zinaweka malengo makubwa ya upimaji na umilikishaji wa viwanja na mashamba nchini. Aidha, wananchi na viongozi wa Serikali za Mitaa wanahimizwa kuheshimu na kulinda miliki zilizotolewa kisheria na maeneo yaliyotengwa kwa matumizi ya umma. Hatua za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya wavamizi wa maeneo ambayo yamemilikishwa kisheria.

26. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Wizara iliahidi kushughulikia maombi ya kibali cha uhamisho wa milki 3,500. Hadi kufikia Aprili 2015, maombi 4,540 yameshughulikiwa. Vilevile, Wizara itaendelea na jukumu lake la msingi la kusimamia masharti ya umiliki wa ardhi kwa kuhakikisha kuwa miliki zinaendelezwa ipasavyo. Ili kuhakikisha masharti ya uendelezaji ardhi yanazingatiwa, Wizara ilitoa ilani 3,823 (Jedwali Na. 2) za ubatilisho kwa wamiliki waliokiuka masharti wakiwemo wamiliki wa mashamba yasiyoendelezwa katika mikoa ya Morogoro, Pwani na Rukwa. Katika mwaka wa fedha 2015/16, Wizara itaendelea kushughulikia ubatilisho wa milki zote zinazokiuka masharti ya uendelezaji wa viwanja na mashamba. Natoa rai kwa Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatuma Ilani za ubatilisho wa milki kabla ya kuwasilisha mapendekezo hayo Wizarani.

Usimamizi wa Ardhi ya Vijiji

27. Mheshimiwa Spika, katika kuratibu usimamizi wa ardhi ya vijiji, Wizara itaendelea kutoa elimu kwa wananchi, kuhakiki mashamba, kuratibu utoaji vyeti vya ardhi ya kijiji na hati za hakimiliki ya kimila. Utoaji wa vyeti vya ardhi ya kijiji unaziwezesha Halmashauri za vijiji kutambua mipaka ya kijiji na kusimamia matumizi ya ardhi yao na hivyo kuepuka migogoro ya matumizi ya ardhi.

28. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili, 2015 Wizara imetoa Vyeti vya Ardhi ya Kijiji 988. Aidha, katika kipindi hicho, Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya, Ofisi ya Rais kupitia Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) na wadau mbalimbali imeratibu na kutoa Hati za Hakimiliki za Kimila 25,897 (Jedwali Na. 2) ikilinganishwa na lengo la kutoa Hatimilki za Kimila 70,000. Wizara itaendelea kushirikiana na Halmashauri za

Wilaya nchini pamoja na wadau mbalimbali kuhakikisha kwamba zoezi la utoaji wa Hati za Hakimiliki ya Kimila linakuwa endelevu na linafanyika kwa kasi zaidi. Hatua hii inalenga kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kutumia hati hizo kama dhamana kupata mikopo kwenye taasisi za fedha na pia kudhibiti migogoro ya matumizi ya ardhi ambayo inaendelea kujitokeza katika baadhi ya maeneo nchini.

29. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kuzishukuru taasisi za fedha ambazo zimetambua na kukubali kupokea hati milki za kimila kama dhamana ya kupata mikopo. Taasisi hizo ni pamoja na NMB, CRDB Bank, PSPF, SIDO, Meru
Community Bank na Agricultural Trust Fund Bank kwa kutoa mikopo ya jumla ya Shilingi bilioni 49.2 katika mwaka wa fedha 2014/15. Aidha, ninahimiza benki na taasisi zingine za fedha wazitambue na kuzikubali hatimiliki za kimila kutumika kama dhamana ya kupatia mikopo kwa kuwa zina nguvu sawa ya kisheria kama ilivyo kwa
hati miliki za kawaida.

Udhibiti wa Ardhi ya Vijiji

30. Mheshimiwa Spika, miaka ya hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la uporaji wa ardhi vijijini. Hili linafanywa na watu wachache wenye uwezo kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji wasio waadilifu. Kwa kiasi kikubwa ardhi inayoporwa inaachwa bila kuendelezwa na nyingine huhawilishwa, kupimwa na kuombewa hatimiliki za kawaida. Hali hii ikiachwa kuna hatari ya wananchi wa vijijini kugeuka wapangaji wa ardhi za vijiji vyao. Ili kuhakikisha kuwa miamala ya ardhi vijijini inafanyika kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za uhawilishaji wa ardhi ya vijiji utafanyiwa tathmini kuanzia mwaka wa fedha 2015/16 ili kujua ukubwa wa tatizo na kuzuia mianya ya ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu na ikibidi kuweka ukomo wa kiasi cha ardhi (land ceiling) ambacho mtu mmoja anaweza kumiliki kijijini. Azma hii inalenga kuyalinda makundi mbalimbali ya jamii wakiwemo wakulima na wafugaji kumiliki ardhi.

31. Mheshimiwa Spika, ili kusimamia kwa ufanisi ardhi ya vijiji iweze kuwanufaisha wananchi wote, napenda kutoa agizo kwa watendaji wa vijiji wote nchini kuandaa orodha ya walionunua ardhi katika vijiji vyao wakionesha majina na kiasi cha ardhi kilichonunuliwa. Taarifa hizi ziwasilishwe kwa Afisa Ardhi Mteule katika Halmashauri husika kwa uhakiki. Vilevile natoa rai kwa wananchi wote waishio vijijini kufuatilia kwa karibu uuzaji wa ardhi kiholela ili kuhakikisha kuwa unafanywa kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na.5 ya mwaka 1999.

Udhibiti wa Migogoro ya Matumizi ya Ardhi

32. Mheshimiwa Spika, karibu kila nchi duniani inakabiliwa na aina fulani ya migogoro ya matumizi ya ardhi. Nchini Tanzania kuna aina kuu tatu za migogoro

ambayo ni kati ya wakulima na wafugaji; wakulima/wafugaji na hifadhi; na wanavijiji na wawekezaji. Wizara imedhamiria kudhibiti migogoro hiyo ambayo inasababisha uvunjifu wa amani na vifo katika baadhi ya maeneo yenye migogoro kwa kutekeleza Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Sheria za Ardhi uliohuishwa mwaka 2013 (Strategic Plan for Implimentation of Land Laws - SPILL 2013), Mpango wa Matumizi ya Ardhi (2013- 2033) na Mpango Mkakati wa Wizara wa miaka mitano (2012/13 - 2016/17). Baadhi ya hatua zilizochukuliwa ili kupunguza migogoro ya ardhi katika Halmashauri nchini ni pamoja na kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji 1,560, kuandaa mipangokina ya miji na majiji na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo. Dawa pekee ya kudhibiti migogoro ya matumizi ya ardhi nchini ni kupanga na kupima kila kipande cha ardhi na kuwamilikisha wananchi na taasisi kisheria kwa kuwapatia hatimiliki. Pamoja na jitihada za jumla, Wizara imeendelea

kutafuta ufumbuzi wa mgogoro kwa mgogoro kwa kuwaita mezani pande husika na kukaa nao katika meza ya majadiliano ili kupata ufumbuzi na udhibiti wa migogoro.

33. Mheshimiwa Spika, hatua ya kukaa mezani na pande husika zimeanza kuleta mafanikio na kupata ufumbuzi katika mgogoro wa mashamba kati ya Mwekezaji (Tanzania Plantation Ltd.) na wananchi wanaozunguka mashamba yake na mgogoro kati ya mwekezaji wa shamba la Noor Farm lililopo Oljoro katika Wilaya ya Arumeru. Kutokana na makubaliano na wawekezaji. Serikali imepata jumla ya ekari 7,236.5 kwa ajili ya wananchi wasio na ardhi ndani ya migogoro husika.Aidha, Wizara imeunda timu ikijumuisha wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Arusha na Meru ambayo inaendelea na kazi ya uhakiki wa wananchi wasio na ardhi katika eneo husika, uthamini, upimaji na umilikishaji wa ekari zilizopatikana. Mgawanyo huo utazingatia pia kipaumbele cha Serikali kuwa na

akiba ya ardhi (Land Bank) kwa matumizi ya baadaye. Napenda kusisitiza kwamba, wakati wa ugawaji wa ardhi hii Halmashauri husika zizingatie mahitaji halisi ya wanakijiji na kuwapa kipaumbele kaya zilizo ndani ya kijiji ambazo hazina ardhi kabisa na kutoa hati za umilikaji ardhi mara tu mwanakijiji anapomilikishwa. Aidha, nawaasa wananchi wa maeneo husika kuwa watulivu na wenye subira ili zoezi liweze kukamilika kwa amani na mafanikio makubwa.

34. Mheshimiwa Spika, Wizara pia imefanikiwa kumaliza mgogoro kati ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na vijiji vya Ayamango, Gedamar na Gijedabung Wilayani Babati ambapo Mhe. Rais amefuta shamba la Ufyomi Galapo Estate. Kazi inayoendelea ni kuhakiki, kupima na kumilikisha ardhi ili wananchi walio katika hifadhi waweze kuhamishwa na kupatiwa ardhi katika shamba hilo. Vilevile, Wizara ya Ardhi kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii inaendelea na uhakiki wa mipaka ya

Hifadhi ya Tarangire na kuweka alama zenye kuonekana ili kuzuia kujitokeza migogoro mingine.

35. Mheshimiwa Spika, kuhusu mgogoro wa shamba la Malonje, Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga wameanza taratibu za kisheria za kufuta miliki ya shamba hilo kwa kutoa Ilani ya siku 90 kwa mmiliki.Taratibu za kisheria zitafuatwa mara baada ya siku hizo kufikia tamati. Kadhalika, shamba la Utumaini lililopo Halmashauri ya Mafia lipo katika hatua za mwisho za ufutaji. Kiambatisho Na.1 kinaonesha chimbuko la migogoro nchini, aina ya migogoro na hatua zilizotekelezwa/zinazotekelezwa na Wizara.

Utatuzi wa Kero na Malalamiko ya Wananchi Kuhusu Huduma ya Ardhi

36. Mheshimiwa Spika, ukweli ni kwamba kero na malalamiko ya wananchi yasiposikilizwa na kupatiwa ufumbuzi husababisha migogoro, wananchi kuichukia Serikali yao na kutotii sheria hivyo amani ya

nchi huwa hatarini kutoweka. Kwa kutambua hili, Wizara imedhamiria kuwa na utaratibu maalum wa kutembelea kila Halmashauri nchinikujadilikeronamalalamikombalimbali ya wananchi na kuzipatia ufumbuzi. Ili kutekeleza azma hii, nimetembelea Halmashauri ya Wilaya ya Arusha,Meru, Jiji la Mwanza(Nyamagana), Ilemela, Mji wa Kahama, Manispaa ya Tabora, Manispaa ya Sumbawanga na Morogoro kuzungumza na uongozi wa mikoa husika kuhusu migogoro ya ardhi, kukusanya kero za wananchi na kuunda kikosi cha kushughulikia kero na malalamiko hayo. Kwa Mkoa wa Mwanza nilipokea jumla ya malalamiko 280 ambapo 81 yametoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na 199 kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza(Nyamagana). Katika uchambuzi wa kina, masuala 395 yalijitokeza kama malalamiko zaidi ya yaliyokusanywa awali. Pia, katika Halmashauri ya Manipaa ya Sumbawanga nilikusanya malalamiko 91, Halmashauri ya Mji wa Kahama 86, Halmashauri ya Mji wa Babati na


na Halmashauri ya Wilaya ya Arusha na Meru malalamiko102, na Halmashauri ya Manispaa ya Tabora 215.Kwa upande wa Dar es Salaam madawati ya malalamiko yamefunguliwa katika Manispaa ya Temeke, Ilala na Kinondoni. Uchambuzi umeonesha kuwa malalamiko mengi yanatokana na fidia kutolipwa, kuwa pungufu, kucheleweshwa au ukadiriaji usiofuata taratibu, yakifuatiwa na uelewa mdogo wa Kanuni, Taratibu na Sheria kwa watendaji na wananchi, na yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na uadilifu na utendaji usiyoridhisha wa watumishi wa sekta ya ardhi. Napenda kutoa taarifa kwamba malalamiko haya yanashughulikiwa na zoezi hili ni endelevu. Aidha, kila mwananchi aliyewasilisha malalamiko atajibiwa na asiyewasilisha atafikiwa na kusikilizwa. Natoa wito kwa Halmashauri zote nchini kuanzisha dawati maalum la kushughulikia kero na malalamiko ya wananchi yanayohusu masuala ya ardhi na

kuwasilisha taarifa za utatuzi wa migogoro katika ofisi za kanda kwa uchambuzi. Taarifa hizo ziwe zinawasilishwa Wizarani kila mwezi kwa hatua stahiki.

Usajili wa Hati na Nyaraka za Kisheria
37. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara ilikuwa na lengo la kusajili Hati za kumiliki ardhi na Nyaraka za Kisheria zipatazo 87,000, kati ya hizo Hati za kumiliki ardhi ni 42,000 na Nyaraka za Kisheria ni 45,000. Hadi Aprili 2015, Hatimiliki na Nyaraka za Kisheria 69,063 zilisajiliwa sawa na asilimia 79.4 ya lengo lililokusudiwa. Kati ya hizo Hatimiliki ni 23,554, hati za sehemu ya jengo/eneo (Unit Titles) ni 1,005 na Nyaraka 33,058 zilisajiliwa chini ya Sheria ya Usajili wa Ardhi Sura 334 (Jedwali Na. 3A). Aidha, nyaraka 9,937 zilisajiliwa chini ya Sheria ya Usajili wa Nyaraka Sura 117 (Jedwali Na. 3B). Pia, rehani ya mali zinazohamishika zipatazo 2,506 zilisajiliwa chini ya Sheria ya Usajili wa Rehani ya Mali Zinazohamishika Sura 210 (Jedwali Na. 3C).
38. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2015/16, Wizara inakusudia kusajili Hatimiliki na Nyaraka za Kisheria 88,000. Kati ya hizi, Hati za kumiliki ardhi ni 38,000, hati za kumiliki sehemu ya jengo/ eneo 2,000 na Nyaraka za Kisheria 48,000.

39. Mheshimiwa Spika, katika kulinda hakizakumilikiardhi,wadauwaSektayaArdhi wanahimizwa kuzifahamu sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza Sekta hii. Kila mdau akiwa na ufahamu huo na akitambua wajibu wake, kwa kiasi kikubwa utapeli wa ardhi na migogoro inaweza kupungua kwa kiasi kikubwa. Wananchi wanaofanya miamala mbalimbali ya ardhi wanashauriwa kupata taarifa sahihi za kiwanja au shamba kutoka ofisi za ardhi. Nawahimiza wananchi/wadau wenye milki za ardhi kuhakikisha kuwa wanasajili mihamala yao yote inayohusu milki zilizosajiliwa. Usajili wa miamala hii utawawezesha kuwa na kumbukumbu sahihi na usalama wa milki.

TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO

40. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeendelea kujenga, kuimarisha na kusimamia mifumo ya kielektroniki kwa ajili ya kutunza kumbukumbu za ardhi. Mifumo hiyo ni: Mfumo wa Kusimamia Utawala wa Kumbukumbu za Ardhi (Management of Land Information System- MOLIS) na Mfumo wa Kutunza Kumbukumbu na Kukadiria Kodi ya Ardhi (Land Rent Management System - LRMS).

41. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara iliahidi kuanza ujenzi wa Mfumo Unganishi wa Kuhifadhi Kumbukumbu za Ardhi (Integrated Land Management Information System - ILMIS) ambao ni mfumo mpana zaidi ikilinganishwa na mifumo iliyopo. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba kazi ya ujenzi wa Mfumo huo imeanza Mei, 2015 na imekadiriwa kukamilika mwaka wa fedha 2019/20. Katika Awamu ya kwanza, Serikali

itakamilisha ujenzi wa Mfumo ambao utafungwa katika Makao Makuu ya Wizara na katika Ofisi za Kanda nane. Awamu hiyo ya kwanza inatarajiwa kukamilika mwaka wa fedha 2016/17. Awamu ya pili itahusisha kufunga Mfumo katika Ofisi za Ardhi katika Halmashauri zote nchini. Baada ya mfumo huu kufungwa, huduma za Upangaji, Upimaji na Umilikishaji ardhi zitakuwa zinatolewa kwa kutumia mfumo wa kielektroniki. Chini ya mfumo huu waombaji wa huduma hizo watakuwa na fursa ya kutuma maombi na kupata majibu kwa njia ya kielektroniki. Aidha, hatua hizo zitasaidia kurahisisha utunzaji wa kumbukumbu za ardhi, kurahisisha utoaji wa hatimiliki, udhibiti wa makusanyo ya kodi za ardhi, kudhibiti utoaji wa milki juu ya milki, kuzuia wizi, udanganyifu na ulaghai.

42. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara iliahidi kusimika mfumo wa kielektroniki wa kuhifadhi

Kumbukumbu na Kukadiria Kodi ya Ardhi katika Ofisi za Ardhi za Halmashauri 30. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba, hadi kufikia Aprili, 2015, Mfumo huu umeunganishwa katika ofisi za ardhi za Halmashauri 70 na kuzidi lengo zaidi ya mara mbili hivyo kuwa na jumla ya ofisi za ardhi 145 pamoja na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) Dodoma zinazotumia mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu (Jedwali Na. 4), na Ofisi za Halmashauri 23 zilizobaki zitafungiwa Mfumo huu kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha 2014/15. Natoa wito kwa watendaji wa sekta ya ardhi katika Halmashauri zote kuingiza taarifa sahihi na kamilifu ili kuboresha utendaji wa kazi na hivyo kuongeza ukusanyaji wa kodi za ardhi.

43. Mheshimiwa Spika, Wizara imeboresha Mfumo wa Kutunza Kumbukumbu za Ardhi (Management of Land Information System – MOLIS) kuwa na uwezo wa kuhifadhi taarifa za miamala inayofanyika katika Ofisi za Ardhi za Kanda na Msajili wa Hati. Kazi ya kufunga mfumo huu katika Ofisi za Kanda inaendelea na itakamilika katika mwaka wa fedha 2015/16.


Utunzaji wa Kumbukumbu zingine za Sekta ya Ardhi

44. Mheshimiwa Spika, ili kuwawezesha wadau mbalimbali wa sekta ya ardhi wakiwemo Waheshimiwa Wabunge kupata taarifa mbalimbali zinazohusiana na sekta ya ardhi, Wizara yangu imeziweka taarifa hizo katika mfumo wa kielektroniki. Taarifa hizo zinapatikana kwenye "app store" inayoitwa "ardhí tza" inayopatikana kwenye programu za simu. Aidha, hatua hii itasadia kupatikana kwa taarifa hizo kwa urahisi na mahali popote mhitaji atakapokuwepo. Miongoni mwa taarifa zilizowekwa katika mfumo huu ni pamoja na Sera, Sheria, kanuni, miongozo na machapisho mbalimbali yanayohusiana na sekta ya ardhi. Pia, Wizara imetayarisha Mfumo unaowawezesha wananchi kupata taarifa za umiliki wa viwanja na mashamba 38 yao kwa kutuma ujumbe mfupi kwa kutumia simu za mkononi kwa kuandika neno MOL kwenda namba 15404. Azma hii inalenga kuwapa elimu ya kutosha wananchi kwa njia ya mtandao kuhusu sera na sheria zilizopo za ardhi na hivyo kutambua haki na wajibu wao hususan katika ulipaji wa kodi ya ardhi.

UTHAMINI WA MALI
45. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutoa huduma za uthamini wa mali. Huduma hii ina lengo la kuishauri Serikali na Taasisi zake kuhusu bei na fidia za miamala ya ardhi kama vile kuuza, kununua na kutwaa mali zisizohamishika. Aidha, Wizara iliendelea na jukumu la kukagua na kuidhinisha taarifa za uthamini zilizoandaliwa na kuwasilishwa na Wathamini wa Halmashauri mbalimbali nchini na Makampuni Binafsi ya Uthamini. Wizara pia inasimamia uthamini nchini kwa kutoa miongozo, kodi ya pango la ardhi na viwango ashiria vya thamani ya ardhi na mazao.

46. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Wizara ilipanga kuandaa na kuidhinisha taarifa 10,000 za uthamini wa mali kwa matumizi mbalimbali. Matumizi haya ni pamoja na utozaji ada na ushuru wa Serikali unaotokana na miamala ya ardhi, vibali vya uhamisho wa milki za ardhi na utozaji malipo ya awali (premium) wakati wa utoaji milki mpya za ardhi, kuweka mali rehani, uhuishaji wa muda milki za ardhi na dhamana za mahakama. Vilevile taarifa hizo hutumika katika mgawanyo wa mali za wanandoa, mirathi, kinga za bima, mizania na ushauri wa thamani katika kutatua migogoro ya ardhi.

47.Mheshimiwa Spika, hadi Aprili, 2015, Wizara iliidhinisha taarifa 10,507 za uthamini wa mali. Huduma hii ya uthamini ilitolewa sawia na utozaji ada ya uthamini ambapo shilingi 637,114,010 zilikusanywa (Jedwali 5A). Katika mwaka wa fedha 2015/16, Wizara imepanga kuandaa na kuidhinisha taarifa 12,000 za uthamini wa nyumba na mali. 40 48. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Wizara ilipanga kufanya na kuidhinisha taarifa za uthamini wa fidia wa mali za wananchi 30,000 ambao mali zao zitaguswa na miradi ya maendeleo ya umma. Hadi Aprili, 2015 Wizara iliidhinisha taarifa 138 za uthamini kwa ajili ya ulipaji fidia stahiki kwa wamiliki wa asili 23,107 wa ardhi. Mali zilizofanyiwa uthamini zilikuwa na thamani ya jumla ya shilingi bilioni 150.06. Miradi ya uwekezaji iliyohusika ilikuwa ya migodi, miundombinu, kilimo, ujenzi wa barabara, upanuzi wa bandari, huduma za jamii na utekelezaji mipango ya miji na upimaji viwanja kwa matumizi mbalimbali (Jedwali Na. 5B). Katika mwaka wa fedha 2015/16, Wizara itafanya uthamini wa mali kwa ajili ya ulipaji fidia kwa wananchi 35,000 katika Halmashauri mbalimbali nchini.

Viwango vya Thamani

49. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuhakikisha uwepo wa viwango sahihi vya ukadiriaji thamani ya ardhi na
mazao. Katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara ilihuisha viwango vya thamani ya ardhi na mazao katika mikoa ya Mtwara na Lindi. Zoezi hili ni endelevu na hufanyika kila mwaka kwa vile thamani ya ardhi hubadilika kwa mujibu wa nguvu na mwenendo wa soko. Katika mwaka wa fedha 2015/16 kazi hii itaendelea katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Kigoma na Tabora.

50. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara iliahidi kusambaza miongozo kwa wataalam na wadau wa uthamini nchini. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa Mwongozo wa Utaratibu wa Uthamini wa Fidia na Mwongozo wa Uchambuzi na uwekaji viwango vya thamani ya soko la ardhi, majengo na mazao imesambazwa.

51.Mheshimiwa Spika, Ibara ya 24 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaelekeza kwamba hakuna mali ya mwananchi itakayochukuliwa bila fidia. Kifungu cha 11(i) cha Sheria ya Utwaaji kinaelekeza kuwa pale ardhi 42 inapotwaliwa mnufaika na utwaaji huo anawajibika kulipa fidia kwa mmiliki wa asili anayeondolewa kwenye ardhi hiyo. Aidha, Kifungu cha 3(1)(g) cha Sheria za Ardhi (Sura 113) na (Sura 114) kinaelekeza kuwa fidia hiyo ni lazima iwe kamilifu, ya haki na ilipwe kwa wakati (full, fair and prompt compensation). Ili kuhakikisha matakwa ya Sheria husika yanazingatiwa kabla ya kutwaa eneo, tarehe 21 Mei, 2015 Wizara imetoa Waraka Na. 1 wa mwaka 2015 ambao unatoa mwongozo wa masuala yanayopaswa kuzingatiwa wakati wa kufanya uthamini kwa ajili ya kulipa fidia.Waraka huo umesambazwa kwa Wizara, Mikoa, Wilaya, Taasisi za Umma na binafsi, Mashirika ya Umma, Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa na Halmashauri za Miji na Wilaya kwa utekelezaji. Kwa sasa, utaratibu ufuatao unapaswa kuzingatiwa:-

a) Wizara, Mamlaka za Mikoa, Wilaya, Taasisi za Umma, Taasisi Binafsi, Mashirika ya Umma, Mamlaka ya Halmashauri za Miji, Wilaya na Vijiji, inayohusika na kulipa fidia, itapaswa kuwasilisha uthibitisho wa uwepo wa fedha za kulipa fidia kwa mamlaka ya Halmshauri ambapo ardhí inatwaliwa na pia uthibitisho huo uwasilishwe kwa Mthamini Mkuu wa Serikali kabla ya utwaaji wa ardhí ya mwananchi;

b) Zoezi la fidia lazima lizingatie ushirikishwaji wa kutosha wa wadau wote muhimu wakiwemo Viongozi wa Kata, Serikali za Mitaa au Vijiji na Wananchi;

Uthamini isiyokuwa na kiambatisho
cha uthibitisho wa uhakika wa uwepo wa fedha iliyotengwa kwa ajili ya kulipa fidia;

d) Zoezi la uthamini lifanyike kwa uwazi, uadilifu na kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Taaluma ya Uthamini; na

e) Wakati wa kufanya malipo ya fidia ni lazima kuwe na mwakilishi wa Mthamini Mkuu wa Serikali.

Natoa rai kwa Halmashauri zote nchini na taasisi mbalimbali kutenga fedha za fidia kabla ya kutwaa maeneo.

MABARAZA YA ARDHI NA NYUMBA YA WILAYA

52. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara iliahidi kuimarisha Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kwa kuyapatia vitendea kazi na kushughulikia mashauri 18,444 yaliyokuwepo hadi Aprili, 2014 na mengine yatakayofunguliwa. Napenda kuliariafu Bunge lako Tukufu kwamba Mabaraza matano (Mpanda, Kyela, Ngara, Karagwe, na Ngorongoro) yaliyoundwa mwaka 2013/14 yameanza kufanya kazi. Hadi Aprili, 2015 jumla ya mashauri mapya 13,338 yalifunguliwa na hivyo kuwa na jumla ya mashauri 31,782. Kati ya mashauri hayo, mashauri 13,749 yaliamuliwa. Mashauri 18,033 yaliyobaki na yatakayofunguliwa yataendelea kushughulikiwa katika mwaka wa fedha 2015/16 (Jedwali Na. 6).

53. Mheshimiwa Spika, Wizara imekuwa ikiunda Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kutegemea upatikanaji wa fedha. Katika mwaka wa fedha 2015/16 Wizara itaendelea kuboresha Mabaraza yaliyopo kwa kuyapatia watumishi na vitendea kazi muhimu na kuanzisha mapya katika wilaya za Kahama, Kilindi na Mbulu. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa itaendelea kutoa elimu kwa Wajumbe wa Mabaraza ya Ardhi kwa lengo la kuimarisha utendaji wa kazi katika Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji na Kata. Uimarishaji wa mabaraza hayo utapunguza mlundikano wa mashauri katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kwa kuwa migogoro isiyo ya lazima kwenda ngazi ya Wilaya itasuluhishwa katika ngazi ya Kijji au Kata.

54. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2015/16 Wizara kwa kushirikiana na wadau itafanya tathmini ya miaka 12 ya Sheria ya Mahakama za Ardhi, Sura 216. Matokeo ya tathmini hiyo yatasaidia kupima 46 utendaji kazi katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya pamoja na vyombo vingine vya utatuzi wa migogoro ya ardhi. Aidha, kutokana na matokeo hayo, Serikali itachukua hatua stahiki ili kuboresha utendaji kazi katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya na mfumo wa utatuzi wa migogoro kwa ujumla.

HUDUMA ZA UPIMAJI NA RAMANI

55. Mheshimiwa Spika, Wizara iliendelea kusimamia upimaji ardhi na utayarishaji ramani za msingi kwa nchi nzima. Upimaji ardhi huwezesha kupata vipimo, ukubwa na mipaka ya vipande vya ardhi, taarifa na takwimu ambazo ni msingi wa usimamizi wa ardhi katika sekta zote. Katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara ilifanya kazi za kutayarisha ramani, kuhakiki mipaka ya ndani na ya kimataifa, kupima mipaka ya vijiji, kutafsiri Matangazo ya Serikali kuhusu mipaka ya hifadhi mbalimbali na kuidhinisha ramani za upimaji zenye viwanja na mashamba.

Utayarishaji Ramani

56. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara ilipanga kujenga na kuimarisha kanzi ya taarifa za kijiografia (geo-database) katika wilaya 19. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa hadi Aprili, 2015, Wizara imejenga na kuimarisha kanzi za wilaya 8 katika mikoa ya Shinyanga na Mwanza ambazo ni Shinyanga, Kahama, Kishapu, Kwimba, Magu, Ilemela, Ukerewe na Nyamagana. Katika mwaka wa fedha 2015/16 Wizara itaendelea kukamilisha kanzi za wilaya 8 za Kaliua, Urambo, Ikungi, Mkalama, Kalambo, Kasulu, Uvinza na Mbozi, pamoja na kujenga kanzi katika mikoa ya Kigoma, Tabora na Rukwa.

57. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara iliahidi kuchapa ramani za uwiano wa 1:2,500 za Jiji la Dar es Salaam, ramani elekezi ya Jiji la Dar es Salaam (City Guide map) pamoja na ramani za kuonesha maeneo ya utalii katika mbuga za wanyama za Serengeti na Mikumi. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba, hadi Aprili, 2015 ramani elekezi za Dar es Salaam za uwiano wa 1:2,500 zilichapishwa na kazi za uhakiki uwandani zinatarajia kukamilika Juni, 2015. Pia, uandaaji wa ramani zinazoonesha maeneo ya utalii kwenye mbuga za wanyama za Mikumi na Serengeti umekamilika. Kazi za uhakiki uwandani zitafanyika katika mwaka wa fedha 2015/16.

Mipaka ya Ndani ya Nchi

58. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara iliahidi kupima mipaka kati ya Hifadhi ya Serengeti na vijiji inavyopakana navyo pamoja na kutafsiri Tangazo la Serikali (Government Notice) Namba 358 la mwaka 1968. Aidha, Wizara iliahidi kuhakiki na kupima mipaka ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi za Wanyama za Taifa (TANAPA), wanavijiji na wadau wengine. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa kazi ya upimaji na uhakiki wa mpaka wa Hifadhi ya Serengeti na vijiji inavyopakana haijakamilika kwa sababu ya kesi iliyofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza na vijiji vya Mbochugu, Bisarara, Nyambuli, Mbalibali, Nyamakendo, Machochwe na Merenga vilivyoko katika wilaya ya Serengeti. Kazi ya kuhakiki mpaka wa Hifadhi ya Serengeti katika vijiji visivyo husika na kesi hii inaendelea uwandani. Katika mwaka wa fedha 2015/16, Wizara itaendelea kukamilisha uhakiki wa mipaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kushirikiana na wadau wengine iwapo yatakuwepo makubaliano kati ya Hifadhi na wananchi wanaopakana na Hifadhi hiyo.

59. Mheshimiwa Spika, Wizara imekuwa ikiendelea na upimaji wa mipaka ya vijiji vinavyoendelea kuanzishwa katika Halmashauri mbalimbali nchini. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa hadi Aprili, 2015 jumla ya vijiji 133 vilihakikiwa na kupimwa katika wilaya za Kiteto (45) na Bagamoyo (88). Katika mwaka wa fedha 2015/16 Wizara yangu itaendelea na upimaji wa vijiji 100.

50 Mipaka ya Kimataifa

60. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara iliahidi kukamilisha upimaji wa mpaka kati ya Tanzania na nchi za Kenya, Burundi, Zambia, Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) pamoja na kuandaa kanzi ya mipaka hiyo. Uhakiki wa mpaka kati ya Tanzania na Burundi wenye urefu wa kilomita 450 ulipangwa kufanyika katika awamu tatu. Awamu ya kwanza imefanyika katika Wilaya ya Ngara ambapo kilomita 135.8 zilihakikiwa na alama za mpaka 365 zilisimikwa na kupimwa. Awamu ya pili na tatu zitafanyika katika Wilaya za Kibondo na Kasulu mkoani Kigoma katika mwaka wa fedha 2015/16. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunzinza kwa pamoja walizindua rasmi uhakiki na uimarishaji wa mpaka huo katika kijiji cha Mugikomero wilayani Ngara mnamo tarehe 28 Agosti, 2014.
61. Mheshimiwa Spika, kazi ya upimaji picha ili kutengeneza ramani za msingi katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji inaendelea. Kati ya kilomita 671, kilomita 51 ambazo ni sehemu ya nchi kavu zimeimarishwa na kupimwa. Kilomita 620 ambazo ni sehemu ya majini (Mto Ruvuma) zitafanyiwa kazi mara baada ya kukamilisha uandaaji wa kanzi (database) na ramani za msingi sehemu ya nchi kavu. Kuhusu mpaka kati ya Tanzania na Malawi katika Ziwa Nyasa, mazungumzo ya usuluhishi chini ya jopo la Marais wastaafu Mhe. Joachim Chisano (Mwenyekiti), Mhe. Thabo Mbeki na Mhe. Festus Mogae yanaendelea. Aidha, katika mwaka wa fedha 2015/16, Wizara itaendelea na uhakiki na uimarishaji wa mipaka kati ya Tanzania na Kenya, na Tanzania na Zambia.

Upimaji wa Viwanja na Mashamba

62. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara yangu iliahidi kuidhinisha ramani za upimaji zenye viwanja 70,000 na mashamba 500. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa hadi Aprili 2015, ramani zenye viwanja 83,502 na mashamba 290 zimeidhinishwa (Jedwali Na. 7). Katika mwaka wa fedha 2015/16 Wizara itaidhinisha ramani za upimaji zenye viwanja 90,000 na mashamba 300.

63. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara iliahidi kukamilisha usimikaji wa alama za msingi (Control Points) 240 katika miji 38. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa ili kurahisisha upimaji ardhi mijini, jumla ya alama za msingi 80 zimesimikwa katika miji ya Kibaha (25), Bagamoyo (30) na Mkuranga (25). Katika mwaka wa fedha 2015/16 Wizara itaendelea kusimika na kupima alama za msingi 160 katika miji 35.

Upelekaji Huduma za Upimaji Kwenye Kanda

64. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imesogeza huduma za upimaji ardhi kwenye kanda ili kuwezesha wananchi kupatiwa huduma za upimaji katika maeneo yao. Aidha, Wizara itaanzisha vikosi maalum vya upimaji ardhi vitakavyokuwa na vifaa vyote vinavyohitajika pamoja na vyombo vya usafiri ili kufanikisha kazi za upimaji. Hatua hii ni muhimu kwa kuwa migogoro ya mipaka kati ya wilaya na wilaya au kijiji na kijiji sasa itatatuliwa kwenye kanda na hivyo, kurahisisha na kuharakisha utatuzi wa migogoro nchini. Vilevile upimaji ardhi ya wananchi utakuwa rahisi na hivyo kuharakisha azma ya kupima kila kipande cha ardhi nchini na kuwa na kumbukumbu sahihi zinazohusu miliki. Natoa wito kwa Halmashauri zote nchini kutumia huduma zitakazotolewa na vikosi hivi mara tu vitakavyokamilika ili kupunguza gharama za upimaji na pia kupunguza migogoro ya ardhi inayotokana na upimaji usiozingatia sheria.

Upimaji wa Ardhi chini ya Maji

65. Mheshimiwa Spika, jukumu mojawapo la Wizara ni upimaji wa ardhi chini ya maji na kutayarisha ramani zinazoonesha umbile la ardhi chini ya maji hususan milima, mabonde, miinuko na kina cha maji. Katika mwaka wa fedha 2015/16 Wizara imepanga kukusanya taarifa za upimaji chini ya maji kutoka kwenye taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi ili kuandaa kanzi ya taarifa za umbile la ardhi chini ya maji.

MIPANGOMIJI NA VIJIJI

66. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu ina jukumu la kusimamia upangaji na uendelezaji wa miji na vijiji ili wananchi wawe na makazi yaliyopangwa. Majukumu hayo yanaratibiwa na kutekelezwa kwa mujibu wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali na taratibu za uendelezaji Miji na Vijiji.

Uandaaji na Utekelezaji wa Mipango ya Jumla ya Uendelezaji Miji (Master Plans)

67. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara iliahidi kushirikiana na wadau mbalimbali kukamilisha Mipango ya Jumla ya Halmashauri za Manispaa ya Sumbawanga, Wilaya ya Mafia, Miji Midogo ya Bagamoyo na Bariadi. Rasimu ya Mipango ya Miji ya Bagamoyo na Kilindoni ilikamilika na itawasilishwa kwa wadau ili kupata ridhaa. Rasimu ya Mpango wa Manispaa ya Sumbawanga iko katika hatua ya kupata maoni na mapendekezo ya wadau.

68. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri iliahidi kuanza utayarishaji wa Mpango Kabambe wa Mji wa Mtwara ambao unajumuisha Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara/Mikindani na sehemu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara katika kata sita za Naumbu, Mbawala, Mayanga, Nanguruwe, Ziwani na Msangamkuu. Utekelezaji wa kazi hii uko katika hatua

ya kukusanya na kuchambua takwimu na taarifa mbalimbali za kisekta. Mpango huu unaandaliwa na Mtaalam Mwelekezi na utakamilika katika mwaka wa fedha 2015/16. Aidha, maandalizi ya Mpango Kabambe wa Mji wa Lindi yapo katika hatua ya awali ya uhamasishaji na uelimishaji wadau.

69. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri za Jiji la Mwanza na Arusha pamoja na Halmashauri za Manispaa ya Ilemela na Halmashauri za Arusha na Meru imeanza kuandaa Mipango Kabambe ya Halmashauri hizo kwa kutumia Mtaalam Mwelekezi. Kazi hii imeanza Februari 2015 na itakamilika Septemba, 2016.

70. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2015/16, Wizara itaendelea kuzijengea uwezo Halmashauri za Manispaa za Iringa, Songea, Lindi, Shinyanga na Halmashauri ya Mji wa Geita ili kukamilisha Mipango ya Uendelezaji Miji. Kadhalika, Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo na Chuo Kikuu Ardhi zitaandaa Mipango Kabambe ya Miji midogo ya Chalinze na Msata. Taarifa kuhusu hali halisi ya mipango kabambe inayoendelea kuandaliwa nchini imeainishwa katika Kiambatisho Na.2. Natoa wito kwa Halmashauri zote nchini ambazo hazina Mipango Kabambe kutenga fedha za kuandaa Mipango hiyo.

Uandaaji na Utekelezaji Mipangokina ya Uendelezaji Miji

71. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeendelea kutekeleza Mpango wa kuboresha makazi katika eneo la Makongo Juu kwa kufanya vikao vya maridhiano na wananchi/ wadau ili kupata uelewa wa pamoja wa kutekeleza mpango huo. Dhana mpya inayopendekezwa kutumika ni shirikishi ambapo wananchi kwa kushirikiana na wadau wengine watahusika katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa mpango. Aidha, 58 Mpango wa Uendelezaji upya wa eneo la kati la Mji wa Njombe umekamilika na unasubiri ridhaa ya wadau. Hadi Aprili, 2015 jumla ya michoro 834 ilipokelewa, kukaguliwa na kuidhinishwa. Wizara inaendelea na kazi ya kuandaa miongozo ya namna ya kupanga matumizi ya ardhi katika miji midogo nchini.

Uendelezaji wa Mji Mpya wa Kigamboni

72. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Wizara iliahidi kuendelea na uendelezaji wa Mji Mpya wa Kigamboni chini ya usimamizi wa Wakala wa Uendelezaji wa Mji Mpya wa Kigamboni (Kigamboni Development Agency-KDA). Hadi Aprili, 2015 Serikali, imefanya mapitio na kurekebisha Matangazo ya Serikali kuhusiana na Mji Mpya wa Kigamboni ambapo eneo la Mpango limepunguzwa kwa kuondoa kata tatu ambazo ni Pembamnazi, Kisarawe II na Kimbiji zenye ukubwa wa hekta 44,440 ambazo hazikuwemo katika mpango wa awali na hivyo kubaki na kata sita zenye eneo la ukubwa wa hekta 6,494. Aidha, Wizara imefanya mikutano ya mashauriano na wadau mbalimbali wa Mji Mpya wa Kigamboni ili kuwa na uelewa wa pamoja juu ya dhana mpya ya uendelezaji wa Mji wa Kigamboni. Kwa mujibu wa dhana hii, wananchi wa Kigamboni wana fursa ya kushiriki katika uendelezaji kwa kutumia mojawapo ya njia zifuatazo: kwanza; mwananchi mwenyewe kuwa mwendelezaji katika eneo lake kwa kuzingatia Mpango; pili; mwananchi kulipwa fidia au kuuza eneo lake kwa mwekezaji kwa hiari yake kwa kuzingatia bei ya soko; na mwisho kuingia ubia na mwekezaji kwa kutumia ardhi yake kama mtaji. Katika mwaka wa fedha 2015/16 Wizara kupitia KDA itaendelea na kazi zifuatazo: kuandaa Mipango ya Kina (Detailed Plans) ya maeneo yaliyopo ndani ya eneo la Mpango kwa kuainisha maeneo ya matumizi mbalimbali; kuthamini, kulipa fidia na kupima maeneo ya miundombinu na huduma za jamii.

MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI

Mpango wa Taifa wa Matumizi ya Ardhi

73. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara iliahidi kukamilisha na kuchapisha Mpango wa Taifa wa Matumizi ya Ardhi. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa kazi hii imekamilika na kusambazwa kwa wadau mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Wabunge ambao wamegawiwa kama sehemu ya hotuba yangu. Katika mwaka wa fedha 2015/16 Wizara itaendelea kutekeleza Mpango kwa kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya wilaya na vijiji hususan katika ukanda wa SAGCOT katika wilaya za Kilombero na Ulanga. Wilaya hizi mbili zitatumika kama wilaya za mfano katika kupanga, kupima na kumilikisha vipande vyote vya ardhi kupitia mradi wa ‘Land Tenure Support Programme.' Aidha, mpango wa Matumizi ya Ardhi katika ukanda wa Reli ya Uhuru umefanyiwa mapitio na kuhuishwa katika mikoa tisa (Pwani, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Ruvuma, Rukwa, Katavi na Dodoma) ya ukanda wa SAGCOT. Katika mwaka wa fedha 2015/16 Wizara itachapisha na kusambaza mpango huu, kutoa elimu kwa wadau na kuanza utekelezaji wake.

74. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara iliahidi kukamilisha kuandaa Kanuni za Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya mwaka 2007 pamoja na kutafsiri Mwongozo wa Upangaji na Usimamizi Shirikishi wa Matumizi ya Ardhi Vijijini katika lugha ya Kiswahili. Pia Wizara iliahidi kuchapisha na kusambaza kwa wadau kitabu cha Kiongozi cha Mwanakijiji katika Upangaji na Usimamizi Shirikishi wa Matumizi ya Ardhi Vijijini. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba vitabu vya Kiongozi cha Mwanakijiji vimechapishwa na kusambazwa kwa wadau wakiwemo Waheshimiwa Wabunge ambao wamegawiwa kama sehemu ya hotuba yangu. Kanuni za Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya mwaka 2007 zimeandaliwa na tafsiri ya Mwongozo wa Upangaji na Usimamizi Shirikishi wa Matumizi ya Ardhi Vijijini imekamilika. Kanuni na mwongozo huo vitachapishwa na kusambazwa kwa wadau katika mwaka 2015/16.

Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Wilaya na Vijiji

75. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara iliahidi kukamilisha kazi ya kuandaa Mipango ya Matumizi ya Ardhi katika Halmashauri za Wilaya za Tarime, Rorya, Newala na Geita pamoja na kutoa mafunzo kwa viongozi na watendaji wa Wilaya nne kuhusu Sheria za Ardhi na mbinu shirikishi za uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi na kuwezesha uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ya Wilaya kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya husika. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba Rasimu za mwisho za taarifa za mipango ya matumizi ya ardhi za Wilaya za Newala, Rorya, Muleba na Tarime zimekamilika na zitawasilishwa kwa wadau kwa maoni. Aidha, ukusanyaji wa takwimu kwa ajili ya kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi katika Halmashauri za Wilaya za Geita, Mvomero, Ulanga na Kilombero umekamilika na kwa sasa zinaandaliwa rasimu za mipango hii; ambayo itawasilishwa kwa wadau ili kutoa maoni na kukamilika katika mwaka wa fedha 2015/16.

76. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara iliahidi kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuandaa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji 200 pamoja na kuendelea na uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji na Wilaya katika ukanda wa SAGCOT kwa kutenga maeneo ya matumizi mbalimbali ikiwemo uwekezaji. Hadi Aprili, 2015, jumla ya vijiji 91 vimeandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi katika wilaya mbalimbali (Jedwali Na. 8). Aidha, mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji na uhakiki wa maeneo ya uwekezaji umefanyika katika vijiji 38 katika Halmashauri za Wilaya za Ulanga (6),
Kilombero (4), Iringa (4), Njombe (2), Makete
(2), Ludewa (2), Kibaha (2), Busokelo (4),
Bagamoyo (4) na Rufiji (8).

77. Mheshimiwa Spika, katika juhudi za utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi, hususan baina ya wakulima, wafugaji na hifadhi; Wizara kwa kushirikiana na wadau imewezesha upangaji, upimaji na umilikishaji wa ardhi katika vijiji 60 vya Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero na vijiji 10 vya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto. Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kipaumbele kimekuwa kuanza na vijiji kumi (10) vya Loltepes, Emart, Enguserosidan, Kimana, Namelok, Kinua, Taigo, Krash, Ndirigish na Knati vinavyopakana na pori la hifadhi ya Emboley Murtangos; ambavyo vilikuwa kitovu cha migogoro katika eneo hili.

78. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2015/16 Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itajenga uwezo na kuwezesha Halmashauri za Wilaya katika maeneo mbalimbali nchini kuandaa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji 200. Natoa rai kwa Halmashauri za Wilaya kutenga fedha kwa ajili ya utayarishaji na utekelezaji wa mipango hii kwa kufuata miongozo inayotolewa na Wizara yangu.

MAENDELEO YA SEKTA YA NYUMBA

79. Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kusimamia sera na mikakati itakayowezesha kuwepo kwa ongezeko la nyumba bora zenye gharama nafuu, ushindani halali wa kibiashara, haki na uwazi kwenye sekta ya nyumba. Ukuaji wa sekta ya nyumba ni chachu ya kukuza ajira kwa vijana na kupunguza umaskini. Pia, sekta ya nyumba imekuwa ni miongoni mwa vichocheo vya ukuaji haraka wa sekta nyingine nchini.

80. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Wizara iliahidi kutoa elimu kwa umma kuhusu utaratibu wa utoaji wa mikopo ya nyumba, ikiwa ni pamoja na haki na wajibu wa mkopaji na mkopeshaji kwa mujibu wa Sheria. Vilevile, Wizara iliahidi kuweka utaratibu utakaowezesha kupatikana kwa mikopo ya nyumba kwa masharti nafuu. Pia, Wizara iliahidi kuweka mazingira ya kuvutia uwekezaji katika sekta ya nyumba ikiwemo sekta binafsi ili kujenga nyumba za kuuza na kupangisha.

81. Mheshimiwa Spika, ninapenda kuliarifu Bunge lako Tukufu, kuwa mazingira mazuri ya kibiashara, kisheria na kimuundo yamewekwa kwa ushirikiano kati ya Wizara, Benki Kuu ya Tanzania na Tanzania Mortgage Refinancing Company (TMRC) yamewezesha jumla ya benki 20 kuanza kutoa mikopo ya nyumba. Hadi Disemba, 2014 benki hizo zimetoa mikopo 3,598 yenye thamani ya shilingi bilioni 248.35.

82. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 utoaji wa mikopo ya nyumba uliongezeka kwa asilimia 59 ikilinganishwa na asilimia 23 kwa mwaka wa fedha 2013/14. Aidha, mikopo inatarajiwa kuongezeka katika mwaka wa fedha 2015/16 kutokana na Serikali kuiwezesha Kampuni ya TMRC kupata mtaji wa nyongeza wa Dola za Marekani milioni 40. Nachukua fursa hii kuzihimiza benki za biashara ambazo hazijaanza kutoa mikopo ya nyumba zianze kufanya hivyo sasa kwa kupata mtaji kutoka Kampuni ya TMRC.

83. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Serikali iliongeza mtaji wa Mfuko wa Mikopo Midogo ya Nyumba (Housing Microfinance Fund-HMFF) kutoka Dola za Marekani milioni 3 mwaka wa fedha 2013/14 hadi milioni 18 mwaka wa fedha 2014/15. Mfuko huu utakuwa ukizikopesha mtaji taasisi za fedha ambazo zinatoa mikopo midogo midogo ya nyumba kwa wananchi kwa masharti nafuu. Utekelezaji wake utaanza mwaka wa fedha 2015/16 baada ya Mwongozo kuhusu sifa za taasisi za fedha zinazostahili kupata mikopo hiyo kukamilika. 84. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha, 2014/15 Wizara iliratibu upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma kupitia Watumishi Housing Company. Kampuni hiyo imepata ekari 741.3 katika mikoa 12 ambayo ni; Dar es Salaam (36.3), Arusha (111), Pwani (262), Tanga (30), Morogoro (10), Dodoma (8), Mwanza (22), Shinyanga
(10), Lindi (25), Mbeya (157), Mtwara (20) na Kilimanjaro (50) kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ambazo zitauzwa kwa watumishi wa umma kwa bei nafuu.

Uwezeshaji Wananchi Kumiliki Nyumba

85. Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuwawezesha wananchi hususan wenye kipato kidogo kumiliki nyumba kwa kupata mikopo yenye gharama nafuu. Hata hivyo, tathmini iliyopo inaonesha kuwa wananchi walio wengi hawana uwezo wa kujenga nyumba kutokana na masharti magumu ya upatikanaji wa mikopo kutoka taasisi za fedha na mashirika yanayojenga na kuuza nyumba nchini. Aidha, wanaohitaji kumiliki nyumba binafsi wangependelea nyumba inayojitegemea (detached) yenye angalau vyumba vitatu vya kulala. Kwa bei za sasa, ujenzi wa nyumba ya aina hiyo isiyozidi eneo la meta za mraba 70 inagharimu shilingi milioni 44. Bei ya kununua nyumba kama hiyo ni Shilingi milioni 59.71 ambazo ni pamoja na faida ya asilimia 15 (shilingi milioni 6.6) na Kodi ya Ongezeko la Thamani-VAT asilimia 18 (Shilingi 9.11 millioni). Kwa kuzingatia wastani wa pato la Mtanzania ambalo ni kiasi cha Dola za Marekani 1,700 (shilingi milioni 3.4) kwa mwaka, familia yenye wastani wa watu watano itapata mkopo wa nyumba usiozidi shilingi milioni 37 iwapo itakopa kwa muda wa miaka 25 na kutozwa riba ya asilimia 15 kwa mwaka. Ili kuwapa wananchi wengi fursa ya kumiliki nyumba binafsi zenye ubora unaokubalika kijamii, Wizara ililiagiza Shirika la Nyumba la Taifa na Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba na Vifaa vya Ujenzi kubuni mikakati na kufanya utafiti kuwezesha upatikanaji wa nyumba zenye vyumba vitatu au zaidi kwa gharama isiyozidi shilingi milioni 35 bila VAT.

86. Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lako tukufu kuwa Shirika la Nyumba la Taifa limejiwekea lengo la kujenga nyumba zenye gharama isiyozidi shilingi milioni 25 bila tozo la VAT. Aidha, Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba na Vifaa vya Ujenzi unaendelea na utafiti wa vifaa mbadala vya ujenzi wa kuta na paa ili kuwezesha kujenga nyumba yenye sifa zilizotajwa hapo juu itakayogharimu siyo zaidi ya shilingi milioni 25.

87. Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutathmini njia mbalimbali zitakazowezesha kushuka kwa gharama za ujenzi na bei ya nyumba bila kuingilia mfumo wa soko huru ili wananchi walio wengi waweze kununua nyumba zinazojengwa na taasisi za umma kama vile, Shirika la Nyumba la Taifa, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na Watumishi Housing Company. Maeneo ambayo Serikali inayafanyia tathmini ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kupunguza au kuondoa VAT kwa nyumba ambazo zitauzwa kwa bei isiyozidi shilingi milioni 35, kuzishirikisha taasisi zinazotoa huduma za miundombinu kuwekeza kwenye maeneo yanayoendelezwa ili kupunguza gharama za ujenzi na hatimaye kupungua kwa bei za nyumba. Aidha, Serikali pale inapowezekana itaendelea kuzipatia taasisi hizo ardhi kwa gharama nafuu pamoja na kuwapa masharti maalum ya uendelezaji wa ardhi kwenye maeneo wanayoyaendeleza.

88. Mheshimiwa Spika, katika miaka ya hivi karibuni sekta ya nyumba imekua kwa kasi na inachangia kukuza Pato la Taifa, kuongeza fursa za ajira na hivyo kupunguza umaskini. Aidha, takwimu za awali zinaonesha kuna waendelezaji wa nyumba (Real Estate Developers) zaidi ya 60 nchini ambao wanafanya kazi hizo bila kuwa na chombo cha kuwaratibu. Ili kuwawezesha waendelezaji wa nyumba kuongeza kasi ya ujenzi wa nyumba, Serikali imemteua mtaalam mwelekezi atakayeshauri uanzishwaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Waendelezaji Milki (Real Estate Regulatory Authority-RERA) ambayo itakuwa na jukumu la kuratibu uwekezaji katika milki, kusimamia haki za wapangaji, mapato ya serikali na ubora wa majengo pamoja na huduma zake. Katika kipindi cha mpito Wizara imeanzisha dawati la 'Housing and Real Estate Information Center'. Azma hii inalenga kuongeza uwazi na upatikanaji wa takwimu sahihi za uwekezaji katika majengo na nyumba. Aidha, itasaidia kubainisha mchango wa sekta hii katika Pato la Taifa na ajira. Majukumu ya dawati hilo yatakuwa ni pamoja na kukusanya na kutunza taarifa za wadau wa sekta ya nyumba wakiwemo wajenzi, vyombo vya fedha vinavyotoa mikopo ya nyumba, kampuni zinazotoa huduma na ushauri mbalimbali kama vile madalali wa nyumba, viwanja na mashamba pamoja na taarifa za kodi za majengo na upangishaji. Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba na
Vifaa vya Ujenzi

89. Mheshimiwa Spika, Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) una majukumu ya kutafiti, kukuza, kuhamasisha na kusambaza matokeo ya utafiti na utaalamu wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu nchini. Kazi hizo zikifanyika kikamilifu zitainua na kuboresha viwango vya nyumba zinazojengwa kwa kutumia vifaa vinavyopatikana hapa nchini na kuinua maisha ya wananchi wenye kipato cha chini. Aidha, Wakala umeeneza teknolojia ya ujenzi wa nyumba kwa kutumia malighafi zipatikanazo katika maeneo mbalimbali mijini na vijijini. Teknolojia hiyo hutumia nguvu kazi za vijana katika kuzalisha vifaa vya ujenzi na ujenzi wenyewe. Kupitia vikundi vya uzalishaji, vijana wanawezeshwa kupata ajira na hivyo kubadili hali yao ya maisha kwa kujiongezea kipato na kuchangia Pato la Taifa.
90. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Wizara iliahidi kuhamasisha na kueneza teknolojia ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika wilaya za Nkasi, Kishapu, Chunya na Tandahimba. Aidha, iliahidi kujitangaza kupitia vyombo vya habari na kushiriki maonesho mbalimbali ya kitaifa. Hadi Aprili, 2015 semina za uhamasishaji wa ujenzi wa nyumba bora za gharama nafuu zilifanyika katika Kata za Chaume, Lukokoda na Lyenje katika Wilaya ya Tandahimba.

91. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wakala pia ulitoa mafunzo kwa vitendo katika Mikoa ya Shinyanga- Wilaya ya Kahama na Mbeya kwa kutumia vikundi vya SACCOS ya Muungano wa Vikoba (Mvita) na kikosi cha ujenzi "Salen Group" huko Mtwara. Vilevile, uhamasishaji wa ujenzi wa nyumba bora umefanyika kwa vikundi mbalimbali vya kijamii ambavyo ni "Youth Technology Hub" (Dar es Salaam) na Safina (Bagamoyo). Aidha, hadi Aprili, 2015, Wakala ulitengeneza mashine 210 za kufyatulia matofali ya kufungamana na kuziuza kwa vikundi mbalimbali. Kadhalika, Wakala ulishiriki katika maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Mkoani Lindi, Kongamano la Wahandisi lilifanyika Mlimani City, Dar es Salaam na Maadhimisho ya Siku ya Makazi Duniani yalifanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam.

92. Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa Wakala kwa kushirikiana na Shirika la Nyumba la Taifa pia uliendesha mafunzo katika Halmashauri za Wilaya zote 168 za Tanzania Bara. Jumla ya vijana 6,720 walishiriki mafunzo ambapo kulikuwa na washiriki 40 toka kila Halmashauri. Mafunzo haya yaliwezesha kuwa na ajira ya kudumu kwa washiriki. Pia kila Halmashauri ya Wilaya ilipewa mashine nne za kufyatulia matofali yanayofungamana ambapo jumla ya mashine 672 zilitolewa. 93. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2015/16, Wakala utaendelea kuhamasisha na kueneza teknolojia ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika Wilaya za Wanging'ombe, Bukombe, Nkasi na Nanyumbu. Aidha, Wakala utaendelea kufanya tafiti mbalimbali za kuendeleza teknolojia rahisi za uzalishaji wa vifaa vya ujenzi na utaandaa mwongozo wa usanifu na ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. Vilevile, Wakala utaendelea kufanya utafiti kuhusu matumizi ya nishati katika kutengeneza vifaa vya ujenzi na kulinda mazingira "Energy for Low Income Housing Technology (ELITH)". Kadhalika, Wakala utaendelea kujitangaza kwa kushiriki katika maonesho na makongamano ya wataalamu. Pia elimu kwa umma kuhusu huduma zinazotolewa na Wakala itaendelea kutolewa kupitia semina za vikundi pamoja na kujenga nyumba za mfano kwa kutumia teknolojia ya vifaa vya gharama nafuu. Vilevile katika mwaka wa fedha 2015/16 semina za uhamasishaji wa ujenzi wa nyumba bora za gharama nafuu zitafanyika katika Wilaya za Nkasi, Kishapu

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA

Ujenzi wa Nyumba za Makazi

94. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Shirika lilipanga kukamilisha miradi 16 inayoendelea na kuanza miradi mingine mipya 26 ya nyumba za gharama nafuu, kati na juu. Miradi hii, inatekelezwa katika mikoa yote ya Tanzania Bara ambapo lengo ni kujenga nyumba 50 kwa kila mkoa. Hadi Aprili, 2015 Shirika limetekeleza miradi 51 yenye jumla ya nyumba 4,856 (Jedwali Na. 9A). Miradi hiyo, imeliwezesha Shirika kuifikia mikoa yote ya Tanzania Bara isipokuwa Kilimanjaro ambako bado ardhi haijapatikana. Katika mwaka wa fedha 2015/16, Shirika litakamilisha baadhi ya miradi inayoendelea na kuanza ujenzi wa miradi mingine mipya. Jumla ya miradi itakayotekelezwa ni 73 yenye nyumba 7,628 yaani miradi 51 ya nyumba za gharama nafuu 2,175 na miradi 22 ya nyumba za gharama ya juu na kati 5,453.

Upatikanaji wa Ardhi kwa ajili ya Ujenzi wa Nyumba

95. Mheshimiwa Spika, ujenzi wa nyumba katika mikoa unategemea upatikanaji wa ardhi ya gharama nafuu. Hadi Aprili, 2015, Shirika lilinunua ardhi yenye ukubwa wa ekari 4,642.85 (Jedwali Na 9B) katika Halmashauri mbalimbali nchini. Pia, Halmashauri 63 zilitenga jumla ya ekari 3,018.1 kwa ajili ya kuliwezesha Shirika kujenga nyumba. Katika mwaka wa fedha 2015/16, Shirika litaendelea kushirikiana na Halmashauri ili kununua ardhi yenye gharama nafuu kwa ajili ya kuliwezesha kujenga nyumba.

Mauzo ya Nyumba za Makazi

96. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Mpango Mkakati wa kipindi cha 2010/11 – 2014/15, Shirika linatakiwa kuuza asilimia
70 na kupangisha asilimia 30 ya nyumba za makazi zinazojengwa. Hadi Aprili, 2015, Shirika limeuza jumla ya nyumba 959 kati ya 1,327 na kupata Shilingi bilioni 80.23 kati ya Shilingi bilioni 141.31 zilizotarajiwa sawa na asilimia 56.8. Katika mwaka wa fedha 2015/16, Shirika litaendelea kujenga na kuuza nyumba na matarajio ni kukusanya Shilingi bilioni 160.2 zikijumuisha fedha ambazo hazijakusanywa kutoka kwa wanunuzi wa awali.

Ujenzi wa Majengo ya Biashara

97. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Shirika lilipanga kutekeleza miradi 30 ya majengo ya biashara. Hata hivyo, Shirika liliweza kutekeleza miradi
11. Kati ya miradi hiyo miradi sita ni mipya na mitano ilikuwa inaendelea kutekelezwa.

Hadi Aprili, 2015 Shirika lilikamilisha miradi mitatu kati ya ile iliyokuwa inaendelea kutekelezwa. Miradi hii, ipo katika barabara ya Ufukweni, Dar es Salaam; Mtaa wa Mkendo, Musoma; na Mtaa wa Kitope, Morogoro. Katika miradi mipya, Shirika lipo hatua za mwisho kukamilisha miradi miwili katika Mtaa wa Lupa Way, Mbeya na Barabara ya Old Dar es Salaam Manispaa ya Morogoro. Aidha, Shirika linaendelea na ujenzi wa miradi mitano iliyoko Mtaa wa Mkendo, Musoma (Awamu ya II); eneo la Paradise, Mpanda; Mtukula, Kagera; pamoja na Mitaa ya Boma na Lumumba katika Manispaa ya Singida. Katika mwaka wa fedha 2015/16, Shirika litaendelea kukamilisha baadhi ya miradi inayoendelea kwa sasa na kuanza miradi mingine mipya 12 yenye jumla ya nyumba 674.
Uendelezaji wa Vitovu vya Miji (Satellite Towns)

98. Mheshimiwa Spika, ili kuliwezesha Shirika kufanya kazi kwa ufanisi na tija, Serikali imelipa Shirika la Nyumba la Taifa mamlaka ya kuwa mwendelezaji ardhi mkubwa (Master Estate Developer) katika maeneo yaliyoainishwa kwa ajili ya kujenga vitovu vya miji (Satellite Towns) ikijumuisha kujenga nyumba nyingi kwa ajili ya kuuza au kupangisha kwa wananchi.

99. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Shirika lilipanga kukamilisha mipangokina (detailed plans) ya vitovu vya miji kwenye maeneo ya Luguruni (ekari 156.53), Kawe (ekari 267.71), Uvumba, Kigamboni (ekari 202), Usa River (ekari 296) na Burka/Matevesi (ekari 579.2). Hadi Aprili, 2015, Shirika lilikamilisha matayarisho ya mipangokina ya maeneo ya Burka/Matevesi, Usa River na Kawe. Ujenzi wa majengo mawili (2) yenye jumla ya nyumba za makazi na biashara 700 katika eneo la Kawe ulianza Desemba, 2014 na ujenzi wa nyumba za gharama nafuu 300 katika eneo la Burka/Matevesi utaanza mwezi Julai, 2015.

100. Mheshimiwa Spika, Shirika linaendelea kukamilisha matayarisho ya mipangokina ya maeneo ya Luguruni (Kwembe) na Uvumba (Kigamboni). Katika mwaka wa fedha 2015/16, Shirika kwa kushirikiana na waendelezaji mbalimbali litaendelea kuratibu na kujenga katika maeneo ya Kawe, Burka/Matevesi na Usa River na kuanza ujenzi katika maeneo ya miradi ya Luguruni (Kwembe) na Uvumba (Kigamboni) ambapo kupitia miradi hii jumla ya nyumba 15,000 za makazi na biashara zitajengwa.
Utafutaji wa Mitaji kwa ajili ya Miradi

101. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Shirika lilipanga kukopa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi na majengo ya biashara pamoja na kuwahamasisha wananchi kuchukua mikopo kwa ajili ya ununuzi wa nyumba zinazojengwa na Shirika. Hadi Aprili, 2015, Shirika limekopa jumla ya Shilingi bilioni 242.4 toka benki tisa, ambapo mpaka sasa limetumia Shilingi bilioni 192.1 kutekeleza miradi yake.

Mapato ya Shirika

102. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Shirika lilitarajia kupata Shilingi bilioni 70.1 kutokana na kodi za pango la nyumba. Hadi Aprili, 2015, Shirika lilipata Shilingi bilioni 71.15 ambayo ni asilimia 118 ya lengo la kipindi husika [Jedwali Na 9C). Katika mwaka wa fedha 2015/16 Shirika linatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi bilioni 82.2 kutokana na kodi za pango la nyumba.
84 Mchango wa Shirika kwa Serikali

103. Mheshimiwa Spika, hadi Aprili, 2015 Shirika limechangia mapato ya Serikali jumla ya shilingi bilioni 18.66 kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani kama vile kodi ya pango la ardhi, kodi ya ongezeko la thamani, kodi ya majengo, kodi ya mapato, ushuru wa huduma za Halmashauri za Miji na Manispaa, kodi za mapato ya wafanyakazi, ushuru wa maendeleo ya taaluma na mchango wa pato ghafi kwa Serikali (Jedwali Na.9D).

Matengenezo ya Nyumba na Majengo

104. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Shirika lilipanga kutumia Shilingi bilioni 6.1 kwa ajili ya matengenezo na ukarabati wa nyumba zake. Hadi Aprili, 2015, Shirika lilizifanyia matengenezo makubwa na ya kawaida nyumba 2,792 kwa gharama ya Shilingi bilioni 4.67. Matengenezo hayo yameliwezesha Shirika kupunguza malalamiko kutoka kwa wapangaji. Katika mwaka wa fedha 2015/16, Shirika litatenga kiasi cha shilingi bilioni 7.5 kwa ajili ya matengenezo ya nyumba zake.

HUDUMA ZA KISHERIA

105. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara yangu iliahidi kukamilisha kazi ya uhuishaji wa sheria mbalimbali za ardhi zikiwemo Sheria ya Ardhi Sura 113, Sheria ya Ardhi ya Vijiji Sura 114, Sheria ya Mahakama za Ardhi Sura 216 na Sheria ya Upimaji Sura 324. Wizara imepokea maoni ya wadau na inayafanyia kazi kwa ajili ya kuyawasilisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Wizara imewasilisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali marekebisho ya Sheria za Usajili wa Ardhi Sura 334, Sheria ya Usajili wa Nyaraka Sura 117, Sheria ya Usajili wa Rehani ya Mali zinazohamishika Sura 210, Sheria ya Mipangomiji Sura 355 pamoja na Sheria ya Usajili wa Maafisa Mipangomiji Na.7 ya mwaka 2007 kwa ajili ya kuwasilishwa Bungeni.

106. Mheshimiwa Spika, Wizara katika mwaka wa fedha 2015/16 inapendekeza kutungwa kwa Sheria mpya ya Usimamizi wa Mawakala wa Ardhi (The Real Estate Agents Act), Sheria ya Utwaaji wa Ardhi, Sheria itakayosimamia Uanzishwaji wa Chuo cha Ardhi – Tabora pamoja na Sheria ya Uthamini na Usajili wa Wathamini.

MAWASILIANO SERIKALINI

107. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 niliahidi kukamilisha kuhuisha mkakati wa mawasiliano wa Wizara, kuratibu mawasiliano kati ya Wizara na wadau wake; kuandaa na kurusha vipindi vya televisheni na redio na kuboresha mawasiliano. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa Wizara imekamilisha kuhuisha mkakati wa mawasiliano ambao unawezesha namna bora ya kuwasiliana na wadau wa Sekta ya ardhi.

108. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara iliratibu uandaaji wa jumla ya vipindi 12 vya luninga ambavyo vilirushwa hewani na Televisheni ya Taifa. Vipindi hivi vilielezea huduma mbalimbali zinazotolewa na Wizara. Aidha, taarifa mbalimbali kwa umma kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara zilitolewa kwenye vyombo vya habari kwa njia mbalimbali ikiwemo mikutano kati ya Wizara na wanahabari (Press Conferences) na kuchapisha nakala 5,000 za Jarida la Wizara la 'Ardhi ni Mtaji' linalosaidia kuelimisha jamii kuhusu Sekta ya ardhi. Katika mwaka wa fedha 2015/16 Wizara itaendelea kuelimisha umma kuhusu Sera, Sheria, Kanuni na taratibu zinazosimamia sekta ya ardhi kwa kuratibu mawasiliano.

HUDUMA ZA UTAWALA NA RASILIMALI WATU

109. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara iliendelea kutoa huduma za utawala na usimamizi wa rasilimali watu kwa madhumuni ya kuboresha utendaji kazi unaolenga kuongeza tija na ufanisi hadi katika ngazi ya Halmashauri. Hatua hii itawezesha kazi za upimaji na upangaji kufanywa na wataalam waliopo katika ngazi ya kanda na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Wizara itaendelea kupeleka watumishi wa sekta ya ardhi katika ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

110. Mheshimiwa Spika, Taifa limeshuhudia ongezeko la migogoro ya ardhi ambayo baadhi yake inasababishwa na watumishi wasio waadilifu. Katika maeneo ya mijini, malalamiko mengi ni yale yanayohusu kiwanja kimoja kutolewa kwa zaidi ya mmiliki mmoja, maeneo ya wazi kujengwa na wamiliki wengine kutozingatia matumizi ya ardhi yaliyoidhinishwa. Wizara imewachukulia hatua za kinidhamu watumishi waliobainika kujihusisha na migogoro hiyo. Hadi Aprili, 2015 watumishi sita wamefukuzwa kazi, tisa wamepewa onyo na wanne wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi. Nawaagiza watumishi wote wa sekta ya ardhi kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu wa hali ya juu na kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ili kuwaondolea wananchi kero zisizo za lazima.

Kituo cha Huduma kwa Mteja (Customer Service Centre)

111. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara ilianza kutoa huduma kupitia Kituo cha Huduma kwa Mteja (Customer Service Centre) katika Makao Makuu ya Wizara. Lengo la Kituo hiki ni kuboresha utoaji wa huduma kwa mpangilio na kwa uwazi unaosaidia kuleta ufanisi katika utendaji wa pamoja ambao unasaidia kupunguza mianya ya rushwa. Hadi kufikia Aprili 2015, Kituo kilipokea wateja takriban 80,000 na kushughulikia masuala mbalimbali yanayohusiana na umiliki wa ardhi. Katika mwaka wa fedha 2015/16 Wizara itaendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa kuweka mifumo inayorahisisha utendaji kazi.

Huduma kwa Mteja kwa Njia ya Simu (Customer Service Call Centre)

112. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2015/16, Wizara yangu itaanzisha Kituo cha Huduma kwa Mteja kwa Njia ya Simu. Kupitia Kituo hiki wananchi wataweza kuuliza na kupata majibu ya masuala mbalimbali yanayohusu ardhi kwa kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi. Ili kutekeleza azma hii, Wizara itatoa namba maalum za simu kabla ya Septemba 2015 na hivyo, kuwawezesha wananchi kuuliza na kutoa taarifa zinazohusu masuala ya ardhi kwa kutumia simu za mkononi ambayo ni njia yenye gharama nafuu ambazo zitagharamiwa na Wizara.

113. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeendelea kuwawezesha watumishi kuhudhuria mafunzo ya aina mbalimbali nje na ndani ya nchi kwa ajili ya kuwajengea uwezo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Katika mwaka wa fedha 2014/15 jumla ya Watumishi 58 walihudhuria mafunzo ya muda mrefu na mfupi ndani na nje ya nchi. Watumishi 22 wa taaluma mbalimbali waliajiriwa, watumishi watatu walibadilishwa kazi baada ya kupata sifa na watumishi sita walithibitishwa katika vyeo vyao. Katika mwaka wa fedha 2015/16 Wizara inatarajia kuwapatia mafunzo watumishi 250 wa kada mbalimbali katika sekta ya ardhi. Kwa kutambua umuhimu wa michezo kwa ajili ya kuimarisha afya za watumishi, Wizara yangu ilishiriki katika mashindano ya SHIMIWI.

Vyuo vya Ardhi

114. Mheshimiwa Spika, Wizara ina vyuo viwili vya Ardhi vilivyopo Tabora na Morogoro. Vyuo hivi vinatoa mafunzo ya Stashahada katika fani za Urasimu Ramani na Upimaji Ardhi, Cheti katika fani za Upimaji Ardhi, Umiliki Ardhi, Uthamini, Usajili na Uchapaji Ramani. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa katika mwaka wa fedha 2014/15 Chuo cha Ardhi Tabora kimeanzisha Stashahada katika fani ya Umiliki, Uthamini na Usajili wa Ardhi ambayo itawapa wanachuo sifa ya kujiunga na Vyuo Vikuu. Aidha, Chuo cha Ardhi Tabora kimeboresha mitaala ili kutoa mafunzo yanayokidhi mahitaji ya soko la wataalam wa sekta ya ardhí nchini.

115. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 idadi ya wahitimu katika vyuo vya ardhi vya Morogoro na Tabora ilikuwa ni 375; kati yao wahitimu 204 ni wa Chuo cha Ardhi Morogoro na wahitimu 171 ni wa Chuo cha Ardhi Tabora
Na. 10). Katika mwaka wa fedha 2015/16 Wizara itaendelea kuviimarisha vyuo hivi ili viweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Udhibiti wa UKIMWI

116. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeendelea kuelimisha watumishi namna ya kujihadhari na janga la UKIMWI na kuwahamasisha watumishi kupima afya zao. Watumishi waliojitambulisha kuwa wanaishi na virusi vya UKIMWI wameendelea kupatiwa huduma na msaada wa fedha kwa ajili ya dawa na lishe. Katika mwaka wa fedha 2015/16 Wizara itaendelea kuhamasisha upimaji wa afya na kuendelea kutoa huduma stahiki.

C. CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKTA YA ARDHI

117. Mheshimiwa Spika, pamoja na juhudi zinazoendelea kufanyika kusimamia sekta ya ardhi nchini, Wizara inakabiliwa na changamoto zifuatazo:-
i) Kutopatikana kwa taarifa sahihi za
ardhi;

ii) Migogoro ya matumizi ya ardhi nchini
baina ya watumiaji wa ardhi;

iii) Upungufu wa ardhi iliyopangwa na kupimwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo uwekezaji;

iv) Makundi mbalimbali yanayochukua ardhi ya wananchi kwa ajili ya matumizi mbalimbali kutokulipa fidia kwa mujibu wa Sheria;

v) Uelewa mdogo wa wananchi kuhusu sekta ya ardhi pamoja na sheria zake, taratibu na miongozo iliyopo, haki zao na wajibu wao;

vi) Uhaba wa wataalamu na vitendea kazi vinavyohitajika ili kukidhi mahitaji ya sekta ya ardhi; na

vii) Kuwepo kwa watumishi wa sekta ya ardhí wanaosababisha kero kwa wananchi hususan kwenye baadhi ya Halmashauri.

118. Mheshimiwa Spika, katika hotuba yangu nimeainisha mikakati mbalimbali itakayotekelezwa katika mwaka wa fedha 2015/16 na hivyo, kukabiliana na changamoto hizo. Kuhusu changamoto ya migogoro ya matumizi ya ardhi nchini baina ya watumiaji, Serikali imeendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ikiwemo kusogeza huduma za usimamizi wa ardhi karibu na wananchi kwa kuanzisha Ofisi 8 za Kanda. Lengo la hatua hii ni kuongeza ufanisi na kasi ya upangaji, upimaji na utoaji wa hati miliki za ardhi kwa wananchi kama ufumbuzi wa kudumu wa kutatua migogoro ya ardhi nchini.

119. Mheshimiwa Spika kuhusu utatuzi wa migogoro inayosababishwa na ukiukwaji wa taratibu za upangaji na umilikishwaji wa ardhi, nilishatoa maagizo kwa Halmashauri zote nchini kuanzisha dawati la kushughulikia migogoro ya ardhi. Kwa wale waliobainika kukiuka masharti ya ajira zao na kusababisha migogoro, hatua za kinidhamu zimeshaanza kuchukuliwa dhidi yao. Ili kudhibiti wavamizi wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya matumizi ya umma, Serikali itaendelea kusimamia mipango ya matumizi ya ardhi iliyoidhinishwa na kuchukua hatua stahiki kwa wakiukaji. Kuhusu kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa taarifa sahihi za ardhi, nimeeleza katika hotuba yangu kuwa Serikali imeanza kujenga Mfumo Unganishi wa Kuhifadhi Kumbukumbu za Ardhi (ILMIS) ambao utatumika kutunza kumbukumbu zote za ardhi.

120. Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na changamoto inayohusu ulipaji wa fidia, natoa rai kwa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Taasisi na Wakala kutenga fedha kwa ajili ya kulipa fidia kwa mujibu wa Sheria, kabla ya kutwaa ardhí kwa matumizi mbalimbali.

SHUKRANI

121. Mheshimiwa Spika, mafanikio ya Wizara yangu yametokana na kuwepo kwa ushirikiano kati ya Serikali, Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji na Wadau wa Maendeleo zikiwemo taasisi za fedha za kimataifa, nchi wahisani, taasisi zisizokuwa za kiserikali na mashirika ya kidini. Wadau hao ni pamoja na Benki ya Dunia, Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN-HABITAT), Shirika la Maendeleo la Ujerumani; na Serikali za Denmark, Sweden, Uholanzi na Uingereza, Marekani, China na Norway.

122. Mheshimiwa Spika, kwa mara nyingine napenda kumshukuru Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Angellah Jasmine Kairuki (Mb), kwa kunisaidia katika kutekeleza majukumu yangu. Pia napenda kumshukuru Katibu Mkuu Bw. Alphayo Japani Kidata, na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Selassie David Mayunga kwa ushirikiano mkubwa wanaonipa. Namshukuru Kamishna wa Ardhi, Wakuu wa Idara na Vitengo, Makamishna Wasaidizi na Wasajili Wasaidizi wa Kanda, Wakurugenzi Wasaidizi na viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara, watumishi na wataalamu wote wa sekta ya ardhi kwa kunisaidia katika kutimiza majukumu yangu kwa ufanisi. Naomba kila mmoja wetu aendelee kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

123. Mheshimiwa Spika, mwaka huu ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani. Ni wazi kwamba miongoni mwetu wapo waliotangaza kutogombea tena nafasi ya Ubunge. Kwa wale ambao wanatarajia kurudi kwa wananchi kuomba ridhaa yao ya kurudi tena Bungeni nawatakia kila la heri. Kipekee niwatakie kila la heri wale wote waliotangaza na wale watakaotangaza nia ya kupeperusha bendera za Vyama vyao katika nafasi ya Urais. Tukumbuke maneno ya Baba wa Taifa kwamba: Rais anaweza kutoka chama chochote, lakini Rais bora atatoka CCM.

C. HITIMISHO

124. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2015/16 Wizara imeazimia kuendelea na utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Sheria za Ardhi uliohuishwa mwaka 2013 (Strategic Plan for Implimentation of Land Laws - SPILL 2013); na Mpango Mkakati wa Wizara wa miaka mitano (2012/13 - 2016/17) ili kufikia malengo yaliyoainishwa kwenye Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015/16) na MKUKUTA II ambayo kwa pamoja yanalenga kufikia malengo makuu ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025.

125.Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2015/16 Wizara imejipanga kutayarisha mipango ya kuendeleza miji na vijiji na kusimamia, kupanga matumizi ya ardhi, kupima ardhi, kuhakiki milki, kusajili na kutoa hati ili kuwezesha kuwepo kwa usalama wa milki. Natoa rai kwa mamlaka na asasi mbalimbali kutoa ushirikiano unaotakiwa kuhakikisha kuwa ardhi inaziwezesha sekta zote ili kufikia malengo ya maisha bora kwa kila Mtanzania. 100
D. MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2015/16

126. Mheshimiwa Spika, ili Wizara yangu iweze kutekeleza majukumu niliyoyaeleza katika hotuba hii kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/16, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu lijadili na kuidhinisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara kama ifuatavyo:-

AMAPATO YA SERIKALI14,262,718,000Shilingi
BMATUMIZI YA KAWAIDA
Matumizi ya Mishahara55,321,629,000 Shilingi
Matumizi Mengineyo (OC)69,584,347,000 Shilingi
Jumla Matumizi ya Kawaida10,000,000,000 Shilingi
CMATUMIZI YA MAENDELEO
Fedha za Ndani3,458,996,000 Shilingi
Fedha Nje13,458,996,000 Shilingi
Jumla Matumizi ya Maendeleo83,043,343,000Shilingi
JUMLA MATUMIZI YA KAWAIDA NA MAENDELEO (B+C)70,000,005,000

Jumla ya Matumizi ya Mishahara, Matumizi Mengineyo na Matumizi ya Miradi ya Maendeleo ni Shilingi 83,043,343,000/=.

127. Mheshimiwa Spika, pamoja na hotuba hii nimejumuisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara pamoja na viambatisho mbalimbali. Naomba taarifa hiyo na viambatisho vichukuliwe kuwa ni vielelezo vya hoja hii. Aidha, hotuba hii inapatikana pia kwenye tovuti ya Wizara kwa anuani ya www.ardhi.go.tz na kwenye app store inayoitwa ardhí tza inayopatikana kwenye programu za simu.

128. Mheshimiwa Spika, natoa shukrani zangu za dhati kwako binafsi na kwa Waheshimiwa Wabunge kwa kunisikiliza.

129. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

Kiambatisho Na. 1

MUHTASARI KUHUSU MIGOGORO YA MATUMIZI YA ARDHI NCHINI NA HATUA ZILIZOCHUKULIWA/ZINAZOCHUKULIWA
ILI KUITATUA
NA.MIGOGORO YA ARDHI
1.Chimbuko/ Misingi ya Migogoro ya Ardhi Nchini:

a) Ukosefu wa mipango ya matumizi ya ardhi katika baadhi ya maeneo na kutozingatiwa kwa mipango ya matumizi ya ardhi iliyoandaliwa;
b) Utunzaji hafifu wa kumbukumbu za ardhi katika ngazi mbalimbali zinazotoa huduma za ardhi;
c) Mamlaka mbalimbali zinazosimamia sekta ya ardhi kutozingatia mipaka ya mamlaka zao (OWM-TAMISEMI, Maliasili na Utalii, Nishati na Madini na Wizara ya Ardhi n.k) katika kutekeleza majukumu yao;
d) Uelewa mdogo wa Sheria, Kanuni na taratibu zinazotawala ardhi;
e) Uhaba wa rasilimali ardhi katika baadhi ya maeneo kwa ajili ya kilimo na ufugaji kutokana na ongezeko la idadi ya watu na mifugo;


104f) Kukosekana kwa miundombinu ya ufugaji (maji na malisho) katika maeneo ya
ufugaji hivyo kusababisha wafugaji kuhamahama;
g) Mashamba/maeneo yaliyotelekezwa kwa muda mrefu ambayo yamekuwa kivutio kwa wavamizi; yakiwemo, maeneo ya Taasisi za Umma;
h) Upungufu wa rasilimali watu, fedha na vitendea kazi katika Sekta ya Ardhi hivyo kusababisha maeneo mengi kutopangwa na kupimwa;
i) Baadhi ya watendaji kutokuzingatia taaluma na maadili ya kazi zao wakati wa
kushughulikia masuala ya ardhi;
j) Baadhi ya mamlaka (Wizara, Taasisi, Halmashauri) kutokulipa/ kuchelewesha kulipa
fidia stahiki kwa wananchi wakati wa kutwaa ardhi;
k) Kauli za kisiasa zinazotolewa na baadhi ya viongozi katika ziara mbalimbali; na
l) Mila na desturi za wakulima na wafugaji kuhamahama na kukosekana kwa teknolojia ya kisasa inayowezesha wafugaji na wakulima kuwa na ufugaji wa kisasa.



2.Sura za Migogoro ya Matu- mizi ya Ardhi nchiniMigogoro ya matumizi ya ardhi nchini iko katika sura zifuatazo:-
a) Migogoro kati ya watumiaji mbalimbali wa ardhi kwa mfano wakulima na wafugaji, wanavijiji na wawekezaji;
b) Migogoro ya mipaka kati wilaya na wilaya na kijiji na
kijiji/ mamlaka nyingine; na
c) Migogoro ya fidia kati ya mamlaka mbalimbali na
wananchi.

106Maeneo yenye migogoro mikubwa ya ardhi ni pamoja na Wilaya za Kiteto, (Eneo la hifadhi ya Emborley Mortagos), Kilosa (Mabwegere, Rachi ya Mkata, Mabwengwa, Mfuru na Mbigili, Twatwatwa na Ludewa Mbuyuni) Mvomero ( Bonde la Mgongola, TANAPA na Kijiji cha Wami Sokoine, Kimambila na Mziha), Babati (Bonde la Kiru), Ngorongoro (Tanzania Conservation Co. Safari), Simanjiro (Lolksale Farm), Kinondoni (Chasimba, Kwembe na Mloganzila), Kondoa, Hanang (kijiji cha Gidika, Waranga na Matangalimo, Shamba la Basutu na Mbuga ya Sinyareda), Mbarali (Shamba la Kapunga), Kilombero (Chita JKT, kijiji cha Zijinali, Mkangawalo), Arusha (W) (Tanganyika Parkers, Themi Hill), Monduli (Shamba Na. 6), Manyoni (vijiji vya Kintiku na Simbanguru), Bahi (vijiji vya Nagulo na Chifutuka, Mbabala A, Nhol, Chibelela, Babayu, Mkonday, Mzogole) Shinyanga (Kijiji cha Sakamaliwa) na Chamwino (Kijiji cha Mpwayungu).
CHANZO CHA MIGOGORO YA ARDHI NCHINIHATUA ZA UTEKELEZAJI

3.Utwaaji wa Ardhi Bila Fidia Stahikia) Sheria ya Utwaaji Ardhi Na. 47 ya mwaka 1967 na Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 zinatamka kwamba, kabla ya kuwahamisha wananchi kwenye maeneo yao kupisha shughuli za maendeleo ya umma ni sharti fidia stahiki na kwa wakati (full, fair and prompt compensation) ilipwe. Aidha, Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya mwaka 1999 inatamka fidia inatakiwa kuwa ya haki, kamili na inayolipwa kwa wakati. Msingi mkuu wa fidia kamilifu ni thamani ya ardhi na viwango vya soko katika maeneo husika. b) Wizara
imetoa mwongozo kwa Halmashauri zote nchini kuzingatia Sera, Sheria za Ardhi na Utwaaji Ardhi kwa kulipa fidia stahiki kulingana na Sheria hizo pale zinapotekeleza miradi ya maendeleo inayohitaji kuhamisha wananchi kwenye maeneo yao.
c)Pamoja na Taasisi zote kutakiwa kuzingatia Sera, Sheria na Kanuni za Ardhi, zinatakiwa kabla ya kutwaa ardhi ziwe na fedha kwa ajili ya fidia. d)
Serikali imeendelea kuimarisha Mfuko wa Fidia ya Ardhi (Land Compensation Fund) utakaotumika kulipa fidia kwenye maeneo yatakayotwaliwa kwa matumizi ya umma na uwekezaji.








1084.Kuwepo kwa Mashamba Pori/Wananchi na Taa- sisi Kuhodhi Ardhi Bila ya Kuiendeleza.a) Serikali inaendelea kuchukua hatua ya kubatilisha milki za mashamba yasiyoendelezwa katika maeneo mbalimbali nchini ili baada ya milki za mashamba hayo kubatilishwa yagawiwe kwa wananchi wenye mahitaji ya ardhi. Mashamba pori yaliyopo katika Wilaya za Muheza, Lindi, Kibaha na Mvomero yapo katika hatua mbalimbali za kubatilishwa baada ya Halmashauri za Wilaya husika kuwasilisha mapendekezo.

b) Serikali imeanza uhakiki wa maeneo yanayozidi ukubwa wa ekari 50 yaliyomilikishwa na viongozi wa vijiji kwa wawekezaji kinyume na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya Mwaka 1999. Pia, hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi ya viongozi wa vijiji waliochukua maeneo hayo kinyume cha sheria na mashamba yaliyochuliwa yatarudishwa kwenye vijiji husika na kugawiwa kwa wananchi.

Halmashauri zote nchini zinashauriwa ziendelee kuainisha mashamba pori na kuyawasilisha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili utaratibu wa kubatilisha milki za mashamba hayo ufanyike.


clip_image033.gif
clip_image036.gif







5.Taasisi za Umma kuwa na Maeneo ya Ardhi Bila Hatimilikia) Taasisi zote za Serikali zilizoanzishwa kwa sheria maalum ya uanzishwaji (Establishment Act) zinaendelea kukamilishwa na kupewa nyaraka za umiliki. Aidha, majengo ya Serikali Kuu (Wizara) ambazo hazina ‘establishment', hazijaandaliwa hati. Wizara ya Ardhi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ziko katika majadiliano ya kutafuta utaratibu utakaotumika kumilikisha majengo hayo kisheria.

b) Serikali imeendelea kuhakiki, kupima na kuweka alama za kudumu zinazoonekana ili kuepusha migogoro baina ya taasisi za umma (Jeshi) na Wananchi. Lengo ni kumaliza zoezi hili katika muda mfupi ili kuleta amani kati ya taasisi na wananchi.

c) Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inazishauri Taasisi za Serikali zenye kumiliki ardhi ziwe na utaratibu wa kulinda ardhi zao kwa kujengea uzio ili kuepuka kuvamiwa.

110UTATUZI WA MIGOGORO NCHINIUTEKELEZAJI
6.Migogoro ya Ardhi Kati ya Wakulima na Wafu- gaji (Wilayani Mvomero na Kiteto).a) Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaendelea na kazi ya kupima ardhi katika mipaka ya vijiji ili kutoa Vyeti vya Vijiji na Hati za Hakimiliki za Kimila. Kipaumbele ni katika vijiji vyenye migogoro
ya ardhi nchini. Aidha, katika maeneo yote ambayo Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji inaandaliwa, zoezi na mipaka kuhakikiwa. Hata hivyo, kasi ndogo iliyopo katika kazi hii inatokana na uhaba wa fedha.
b) Mashamba ambayo hayaendelezwi orodha yake imeandaliwa na utaratibu wa kubatilisha milki zake unaendelea.

c) Mashamba yaliyotolewa kwa wawekezaji kinyume na utaratibu yanaendelea kurejeshwa.
d) Kuendelea kuimarisha na kuanzisha Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya ili kuongeza uwezo wa kutatua migogoro ya ardhi nchini.


e) Kuendelea kuzijengea uwezo halmashauri na kuratibu uandaaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi katika wilaya na vijiji.
f) Kuendelea kuhimiza Halmashauri za Wilaya kutenga bajeti za kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi katika vijiji nchini. Aidha, Serikali kupitia Wizara ya Ardhi inarudisha asilimia 30 ya makusanyo katika Halmashauri ili yatumike kuimarisha Sekta ya Ardhi. Kipaumbele ikiwa ni Mipango ya Matumizi ya Ardhi Vijijini.

g) Serikali kwa kushirikiana na wadau imewezesha vijiji 1,560 kutayarishiwa Mipango ya Matumizi ya Ardhi nchini, na Serikali itaendelea kutenga fedha kwa kazi hiyo.
h) Kuendelea kuhakiki na kupima mipaka ya ardhi ya vijiji vyenye migogoro na vijiji ambavyo vinazalishwa kutokana na kugawa vijiji vilivyokwishapimwa. Hadi sasa jumla ya vijiji 10,700 vimeshapimwa nchini kote.

112i) Mgogoro wa Ardhi Wilayani Kiteto: Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wadau wengine iliundwa na kufanya kazi ya usuluhishi na utoaji elimu wilayani Kiteto tangu mwezi Novemba, 2014. Pamoja na shughuli nyingine timu ilifanya yafuatayo:-
• Marekebisho ya mipaka ya vijiji vyote 63 katika wilaya ya Kiteto yamefanyika;

• Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya vijiji10 vinavyopakana na Bonde la Emboley Murtangos imekamilika;

• Mipaka ya mashamba 2,110 katika vijiji 3 yamepimwa, ili wananchi wapate hatimiliki za kimila; na

• Eneo la Emboley Murtangos linaendelea kuwa eneo
la hifadhi kama ilivyoamuliwa na Mahakama.

j) Mgogoro wa matumizi ya Ardhi Wilaya ya Mvomero: Kikosi kazi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kiliundwa mwaka 2014 kuandaa na kutekeleza mkakati wa kutatua Migogoro ya Matumizi ya Ardhi Wilayani Mvomero. Kikosi kazi kilishirikiana na wataalam kutoka Halmashauri za Wilaya ya Mvomero; Morogoro; Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro na Chuo cha Ardhi Morogoro. Shughuli za mkakati zilifanyika katika Vijiji 60 na usuluhishi ulifanyika katika Vijiji 5 vinavyozunguka Bonde la Mgongola. Kazi zingine zilizofanyika ni:
• Kutoa elimu ya Sheria za Ardhi katika Vijiji 63;
• Kufanya mipango ya matumizi ya Ardhi ya Vijiji 32;
• Kufufua mipaka ya Vijiji 36;
• Kupima vipande 5,929 vya ardhi ya Kijiji;
• Kufanya mipango kina katika maeneo ya Makazi katika
Vijiji 7;
• Kuandaa Hati za Haki Miliki za Kimila 3,929;
• Kubaini mashamba pori 85;
• Kuimarisha Mabaraza ya Kata na Vijiji 63; na
• Kuimarisha Mabaraza matatu ya Ardhi na Nyumba (W).

114














7.















Mgogoro wa JWTZ na wananchi wa Ronsoti - Tarime.
Katika kutatua mgogoro wa matumizi Bonde la Mgongola, Kikosi Kazi kilishirikiana na wadau 47 wa Sekta ya Ardhi, kwa kutembelea Bonde la Mgongola na kufanya tathimini ya chanzo cha mgogoro, kufanya usuluhishi kati ya Wakulima na Wafugaji wanaotumia Bonde na kutoa maazimio ya utatuzi wa mgogoro huo tarehe 15-18/12/2014. Wadau waliohusika ni pamoja na Wizara za Kilimo, Chakula na Ushirika, Mifugo na Uvuvi, Maji na Umwagiliaji, Maliasili na Utalii, Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Mambo ya Ndani; Sekretarieti ya Mkoa, Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Umwagiliaji Kanda Morogoro na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya. Maazimio haya yameanza kutekelezwa uwandani tarehe 30 Mei, 2015.
Uthamini wa fidia kwa ajili ya kuwalipa wananchi wa Kata ya Nyamisangura waliopo katika eneo la JWTZ umekwishafanyika tangu mwaka 2012 na taratibu za kulipa fidia hiyo zinaendelea.


8.Mgogoro wa wananchi wa Nyamongo na mgodi wa North Mara.Serikali imeshughulikia mgogoro wa fidia katika Mgodi wa North Mara kwa kuelekeza wamiliki wa mgodi kulipa fidia wananchi waliopo katika vijiji vya Kiwaji na Nyamongo. Wananchi wa vijiji vya Kiwaji na Nyamongo waliopo katika eneo la Mgodi wa North walilipwa fidia katika awamu mbalimbali. Hata hivyo, mgogoro unasababishwa na baadhi ya wananchi waliokwishalipwa fidia kurejea na kujenga tena katika maeneo mengine ya Mgodi (tegesha) kwa nia ya kulipwa fidia jambo ambalo linautia mgodi hasara.
9.Mgogoro JKT na wananchi Tarime.Eneo hilo lilikuwa la vita kati ya makabila ya Wanchira na Wanchari. Serikali imechukuwa hatua ya kudhibiti mapigano baina ya makabila haya kwa kuweka kambi ya JKT katika eneo hili.
10.Wananchi kuvamia viwanja vya watu, maeneo ya wazi na barabaraSerikali imeendelea kukagua na kubomoa maendelezo yote yaliyofanyika kwenye viwanja na maeneo ambayo hayastahili kuendelezwa kwa mujibu wa sheria. Ubomoaji umefanyika maeneo ya wazi ya Kitalu ‘E' na ‘F' Tegeta katika Jiji la Dar es Salaam kwa waliojenga barabarani Kitalu ‘J' na ‘K' Mbezi na kwa wavamizi wa viwanja vya watu. Aidha, zoezi la ubomoaji linaendelea kwa wavamizi wengine nchini.
115



11611.Mgogoro wa Mashamba ya Karangai, Lucy na Iman wilayani Arumeru.Ubatilisho wa mashamba hayo ulikamilika na kutangazwa katika Gazeti la Serikali mwaka 2000. Kwa kuwa mashamba hayo yamekwishabatilishwa, taratibu za kuyamilikisha kwa wananchi zinaendelea.
12.Mgogoro kati ya
wakulima wakubwa
na wakulima wadogo
katika Bonde la Kiru.
a) Baadhi ya vijiji
kuanzishwa kwenye
mashambayamikatabana
b) Baadhi ya wananchi
kuvamia mashamba
yenye hati c) Uhaba
wa ardhi kwa baadhi ya
vijiji vya bonde la Kiru.
Vikao vilifanyika kuhusisha pande husika. Mgogoro huu unashughulikiwa na Kamati inayosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ikihusisha wataalam wa Wizara mbalimbali. Aidha, wawekezaji wamekubali kulipwa fidia ili waweze kuyaachia mashamba hayo.
13.Mgogoro kati ya wananchi wa vijiji vya Ayamango, Gedamar na Gijedabung na hifadhi ya Tarangire.Katika kutatua mgogoro huu, Shamba la Ufyomi/Gallapo limefutwa ili kuwezesha wananchi wa vijiji vya Ayamango, Gedamar na Gijedabung waliokuwa wamevamia kwenye Hifadhi ya Tarangire kuhamishiwa kwenye shamba hilo.

Uongozi wa Mkoa wa Manyara unaendelea na zoezi la uhakiki ili kubaini mahitaji ya wananchi na kuandaa mpango wa matumizi ya shamba hilo.

Chanzo: Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, 2015

Kiambatisho Na. 2 HALI HALISI YA MIPANGO KABAMBE INAYOENDELEA KUANDALIWA
NAMPANGOANAYEGHARAMIAANAYEANDAAHATUA ILIYOFIKIAGHARAMAMUDA WA KUKAMILIKAUHUSIKA WA WIZARA
1Mpango Kabambe wa Jiji Dar es Salaam (2012 – 2032)

(Haijatangazwa katika Gazeti la Serikali)
BEST Program kupitia mradi wa SPILLDodi Mosi kutoka Italia pamoja na Burro Hapold kutoka Uingereza na watalam wa ndani Afri- Arch na Q-ConsultRasimu ya mwisho ya MpangoUSD. 1,870,643Juni, 2015Kuratibu
2Mpango Kabambe wa Jiji la Arusha (2015 – 2035)

(Taratibu kutangaza katika Gazeti la Serikali zinaendelea)
Wizara ya ArdhiMtaalam mwelekezi Singapore Cooperation Enterprise (SCE) in association with Surbana International Consultants Ptc Ltd.Taarifa ya hali halisi ya eneo la mpango imekamilika na maandalizi ramani ya msingi yanaendeleaUSD 4,927,415Septemba, 2016Kuratibu
3Mpango Kabambe wa Jiji la Mwanza (2015 – 2035)

(Taratibu kutangaza katika Gazeti la Serikali zinaendelea)
Wizara ya ArdhiMtaalam mwelekezi Singapore Cooperation Enterprise (SCE) in association with Surbana International Consultants Ptc Ltd.Taarifa ya hali halisi ya eneo la mpango imekamilika na maandalizi ramani ya msingi yanaendeleaUSD 4,483,095Septemba, 2016Kuratibu
4Mpango Kabambe wa Jiji la Tanga (2012 – 2032)

(Imetangazwa katika Gazeti la serikali)
Halmashauri ya Jiji la Tanga na Tanzania Strategic Cities Program (TSCP)Halmashauri ya Jiji la TangaRasimu ya Mwisho ya MpangoTsh. 350,000,000Desemba, 2015Kusaidia utaalamu
5Mpango Kabambe wa Manispaa ya Shinyanga (2015 – 2035)

(Rasimu ya G.N. imesainiwa na Mh. WAR tarehe 16/4/2015)
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Benki ya DuniaHalmashauri ya Manispaa ya ShinyangaRasimu ya Kwanza ya MpangoTsh. 155,000,000Juni, 2015Kusaidia utaalamu
6Mpango Kabambe wa ManispaaBenki ya DuniaHalmashauri ya ManispaaRasimu ya KwanzaTsh.Juni, 2015Kusaidia

118ya Iringa (2015 – 2035)

(Rasimuya G.N. imesainiwa na Mh. WAR tarehe 9/5/2015)
ya Iringaya Mpango150,000,000utaalamu
7Mpango Kabambe wa mji wa Geita (2015 – 2035)

(Haijatangazwa katika Gazeti la Serikali)
Benki ya DuniaHalmashuri ya mji wa GeitaHatua za awali za uandaaji MpangoTsh. 250,000,000Septemba, 2015Kusaidia utaalamu
8Mpango Kabambe wa Manispaa ya Songea (2015 – 2035)

(Rasimu ya G.N. imesainiwa na Mh. WAR tarehe 16/4/2015)
Halmashuri ya Manispaa ya SongeaHalmashauri ya Manispaa ya SongeaHatua za awali za uandaaji MpangoTsh. 250,000,000Juni, 2015Kusaidia utaalamu
9Mpango Kabambe Manispaa ya Bariadi (2015 – 2035)

(Rasimu ya G.N. imesainiwa na Mh. WAR tarehe 16/4/2015)
Halmashauri ya Mji wa Bariadi na Benki ya DuniaHalmashauri ya Mji wa Bariadi kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na Chuo Kikuu ArdhiRasimu ya Kwanza ya MpangoTsh. 450,000,000Juni, 2015Kusaidia utaalamu
10Mpango Kabambe wa Manispaa ya Musoma (2015 – 2035)

(Rasimu ya G.N. imesainiwa na Mh. WAR tarehe 16/4/2015)
Benki ya DuniaCRM Land Consult Ltd. DSMRasimu ya Pili ya MpangoTsh. 298,000,000Juni, 2015Kusaidia utaalamu
11Mpango Kabambe wa Mji Mdogo wa Bagamoyo 2014 – 2034

(Haijatangazwa katika Gazeti la serikali)
Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo na Wizara ya ArdhiHalmashauri ya Mji Mdogo wa Bagamoyo kwa kushirikiana na Wizara ya ArdhiRasimu ya Mwisho ya MpangoTsh. 150,000,000Juni, 2015Kusaidia utaalamu
12Mpango Kabambe wa Manispaa ya Singida (2014 – 2034)

(Haijatangazwa katika Gazeti la serikali)
Halmashuri ya Manispaa ya Singida na Benki ya DuniaHalmashauri ya Manispaa ya SingidaMaandalizi ya Rasimu ya kwanza ya MpangoTsh. 598,000,000Desemba, 2015Kusaidia utaalamu
13Mpango Kabambe wa Mji wa Korogwe (2015 – 2035)Benki ya DuniaHalmashauri ya Mji wa Korogwe na Chuo KikuuHatua za awali za Maandalizi yaTsh. 250,000,000Juni, 2016Kusaidia utaalamu

(Rasimu ya G.N. imesainiwa na Mh. WAR tarehe 16/4/2015)ArdhiMpango
14Mpango Kabambe wa Mji wa Mtwara (2015 -2035)

(Umetangazwa katika G.N. No. 404 la tarehe 8/11/2013)
Benki ya Biashara ya Afrika KusiniAurecon South Africa (PTV) LimitedHatua za awali za Maandalizi ya MpangoUSD. 1,000,000Agosti, 2015Kusaidia utaalamu
15Mpango Kabambe wa Manispaa ya Sumbawanga
(2014 – 2034 )

(Rasimu ya G.N. imesainiwa na Mh. WAR tarehe 16/4/2015)
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na Wizara ya ArdhiHalmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa kushirikiana na Wizara ya ArdhiMaandalizi ya Rasimu ya MpangoTsh. 150,000,000Juni , 2015Kusaidia utaalamu
16Mpango wa Muda wa Kati wa Matumizi ya Ardhi ya Mji Mdogo wa Kilindoni Mafia

(Haijatangazwa katika Gazeti la serikali)
Halmashauri ya Wilaya ya Mafia na Wizara ya ArdhiHalmashauri ya Wilaya ya Mafia kwa kushirikiana na Wizara ya ArdhiRasimu ya Pili ya MpangoTsh. 75,000,000Juni, 2016Kusaidia utaalamu

Jedwali Na. 1 MCHANGANUO WA MATUMIZI YA KAWAIDA NA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA MWAKA 2014/15

MatumiziKiasi Kilichoi- dhinishwa 2014/15Asilimia ya Jumla ya TengeoKiasi Kilichopo- kelewa Hadi Aprili,2015Asilimia ya Fedha Zilizopokelewa Ikilinganishwa na Zilizoidhi-nishwaKiasi cha Fedha Kilichotumika Hadi Aprili, 2015Asilimia ya Fedha Zilizotumika Ikilinganishwa na Zilizopokelewa
Matumizi ya
Fedha za Kawaida
Mishahara (PE)11,536,899,0001310,375,662,7709010,375,662,770100
Matumizi Mengineyo OC)40,048,541,0004721,824,542,6025418,566,619,38785
Jumla ya Matumizi ya Kawaida51,585,440,0006032,200,205,3726228,942,282,15790
Matumizi ya Fedha za Miradi ya MaendeleoNdani (Local)20,850,000,000240000
Nje (Foreign)13,304,977,000160000
Fedha za Matumizi ya Miradi34,154,977,000400000
JUMLA KUU85,740,417,00010032,200,205,3723828,942,282,15790
Chanzo: Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, 2015

HATIMILIKI, VYETI VYA ARDHI YA KIJIJI NA HATIMILIKI ZA KIMILA ZILIZOTOLEWA KWA KIPINDI CHA JULAI, 2014 HADI APRILI, 2015

KANDAMKOAHALMASHAURIHATIVYETI
VYA ARD- HI YA KIJIJI
HATI ZA HATI- MILKI ZA KIMILAUHAMI- SHO WA MILKI ZA AR- DHIILANI ZA UBA- TILISHO ZILIZO- TUMWA
Kanda ya Dar Es Sa- laamDar es SalaamKinondoni14650066961
Ilala5240046327
Temeke19590058964
Hati za mradi- mlhsd5430000
JUMLA KANDA YA DAR ES SALAAM4491001721152

122KANDAMKOAHALMASHAURIHATIVYETI
VYA ARD- HI YA KIJIJI
HATI ZA HATI- MILKI ZA KIMILAUHAMI- SHO WA MILKI ZA AR- DHIILANI ZA UBA- TILISHO ZILIZO- TUMWA
Kanda ya MasharikiPwaniBagamoyo1184520001219
Kibaha mji6550085
Kibaha h/w558550236
Kisarawe990001
Mafia150001
Mkuranga71570004
Rufiji17890002
Jumla ndogo25992341022338
Moro- goroKilosa2912601228
Morogoro(u)626003646
Morogoro(r)675406033
Mvomero9723632734
Kilombero3319409016

KANDAMKOAHALMASHAURIHATIVYETI
VYA ARD- HI YA KIJIJI
HATI ZA HATI- MILKI ZA KIMILAUHAMI- SHO WA MILKI ZA AR- DHIILANI ZA UBA- TILISHO ZILIZO- TUMWA
Ulanga193460505
Jumla ndogo87193834841132
JUMLA KANDA YA MASHARIKI34701161245064170
Kanda ya KatiDodo- maDodoma370010
Chemba30000
Kondoa220410
Mpwapwa135037750
Kongwa701210
Chamwino1300100
Bahi10010
Jumla ndogo335039490
SingidaIramba00000
123Manyoni127090080
Singida(u)2140080

124KANDAMKOAHALMASHAURIHATIVYETI
VYA ARD- HI YA KIJIJI
HATI ZA HATI- MILKI ZA KIMILAUHAMI- SHO WA MILKI ZA AR- DHIILANI ZA UBA- TILISHO ZILIZO- TUMWA
Singida (w)00000
Ikungi40400
Mkalama00000
Jumla ndogo3450904160
JUMLA KANDA YA KATI68001298250
Kanda ya KusiniMtwaraMtwara6020017248
Mtwara(w)3041010
Masasi3220010950
Newala194380136
Masasi (w)0092600
Nanyumbu611012650
Tandahimba1042017433

Hii hotuba ina majedwali mengi, Kuisoma zaidi fungua hiki Kiambatanisho.
View attachment Hotuba ya Wizara ya ardhi JF PDF.pdf
 
Back
Top Bottom