Roland T. Owen: Mwanaume aliyepatwa na masahibu ya kushangaza kwenye chumba No. 1046 ndani ya President Hotel, lakini kilichomkuta kimebaki kuwa fumbo

4G LTE

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2015
Messages
6,130
Points
2,000

4G LTE

JF-Expert Member
Joined Aug 4, 2015
6,130 2,000
Wadau wangu wa nguvu kwenye story za visa na mikasa mbali mbali iliyowahi kutokea na kukuna vichwa vya wapelelezi duniani, naomba leo tutembee pamoja kwenye kisa hiki maridhawa kabisa kilichotokea mwanzoni wa mwaka 1935 huko Missouri, Kansasi Marekani…….

IMG_20190813_201736.jpg

Katika jiji la Kansas, Missouri mchana wa January 2, 1935 mwanaume mmoja allingia ndani ya President Hotel akihitaji chumba kwenye ghorofa kadhaa za juu, hakuwa amebeba mzigo wowote ule zaidi ya brush ya nywele, chanuo na dawa ya meno ndani ya mfuko wa koti lake na akajisajili kwa jina Roland T. Owen wa Los Angeles na akalipia makazi kwa siku moja. Mwanaume huyu alielezewa kuwa mrefu na sauti ndogo ya kukwaruza na nywele nyeusi na kovu kubwa upande wa kushoto wa kichwa chake na akapewa chumba no. 1046.

IMG_20190813_202012.jpg

IMG_20190813_201840.jpg

Wakati akielekea kwenye chumba chake alichopewa Owen akamwambia mhudumu aliejulikana kama Randolph Propst kuwa mwanzoni alikuwa anataka kwenda Muehlebach hotel ila gharama zake zilikuwa juu sana. Walipofika chumbani, Owen alitoa vitu kadhaa kutoka kwenye mfuko wake wa koti ambavyo ni chanuo, dawa ya meno na brush ya nywele na akaviweka vyote bafuni na wote wakatoka chumbani huko kwani Owen alivyochukua tu ufunguo kwa mhudumu huyo aliondoka zake hotelini hapo na mhudumu akaendelea na kazi zake za kawaida.

Baadaye ndani ya siku hiyo hiyo mhudumu wa kike aliyekuwa amevalia nadhifu alianza kutimiza majukumu yake, na akaelekea chumba no. 1046 na Owen alikuwa ndani ya chumba akamruhusu mhudumu aingie ndani ya chumba akimwambia aache mlango wazi bila kuufunga kwani alikuwa anategemea ugeni wa rafiki yake muda si mrefu. Ndani ya chumba hicho pazia zilikuwa zimeshushwa na madirisha yamefungwa vyema huku chumbani kukiwa na taa ndogo ikiking’arisha chumba hicho, kiufupi mwanga haukuwa wa kutosha.

IMG_20190813_193716.jpg

Mhudumu baadaye alikuja kuwaambia polisi kuwa Owen alionekana mwenye wasiwasi muda mrefu ama asiye na amani, macho yake yalikuwa hayana furaha huku uso wake umezubazwa kwa uoga, wakati muhudumu akisafisha chumba oweni akavaa koti lake na kuondoka huku akiendelea kumsisitizia kutoufunga mlango. Ilipotimu saa nne usiku, mhudumu huyu akarudi kwenye chumba cha Owen huku amebebelea mataulo masafi mlango ulikuwa bado hujafungwa na chumba kikiwa bado gizani, Owen alikuwa amejilaza kitandani huku amevalia mavazi yake rasmi, mhudumu akaona kikaratasi kidogo juu ya meza kimeandikwa na kusomeka “Don nitarejea ndani ya dakika 15. Ningojee” nini maana ya ujumbe huo? Huo ujumbe haukuonesha tu alikuwa anatarijia ugeni lakini pia ni ugeni wa aina gani? Jina la Don ambapo ndio ujumbe umelengewa ni jina linatumika huko Uhispania, Ureno, Italia mpaka Ufilipino kama kianzio cha jina la mtu mwenye mamlaka au cheo, huko Amerika ya Kaskazini jina la Don lilifanywa maarufu sana kwa njia ya filamu za kimafia kama vile The Godfather ambapo ndani yake kiongozi wa uhalifu hudai ishara za heshima ambazo kiuhalisia zilikuwa zikitolewa kwa viongozi wa hadhi wa huko Italia.

Hivyo Owen alikuwa akingojea Don ujio mkubwa kabisa huu kwake, kwa kawaida madon hawakutani na watu/wafanyakazi wake kwa jambo dogo bali kwa ajili ya mambo nyeti na muhimu sana na huwa hawana masikhara kabisa wala muda wa kupoteza pia kwao suala la kuua ni kawaida sana, si bure Owen alikuwa anahofia wala hakuwa na furaha wala amani kwani alishindwa kukimbia ili kuiokoa nafsi yake si rahisi kama unavyowaza kwani Don akikuhitaji hakuna pa kuponea. Bila shaka rejea za Dons kama kama kina Richards Leornad Kuklinski “The Iceman”- huyu alitokea familia ya American Mafia iliyojulikana kama DeCavalcante crime family of Newark, Giovanni Brusaca “The Pig”- huyu alitokea Sicilian Mafia ya Italia, Roy Albert DeMeo- huyu alitokea The Gambino crime family huko New York na Joseph “The Animal” Barbosa- huyu alikuwa mixer ya Kireno na Kimarekani wa Patriarca crime family zinaweza kuonesha hawa viumbe ni watu wa aina gani hasa unapokatiza kwenye 19 zao. Utani kidogo mkuu Don Clericuzio una la kuzungumzia hapa kuhusu hawa madon wenzako .

Baada ya hapo Owen alikuja kuonekana kesho yake 4:30 asubuhi mhudumu alipokuja kusafisha chumba chake. Alipofungua mlango kwa kutumia pass key ambapo mhudumu atafanya endapo tu mlango umefungwa kwa ndani, alipoingia kashangaa kumkuta Owen ameketi kimya kwenye kiti akitazama nje na hakuonekana kama mtu anaejali, hali hii ya tahamaki ilivunjwa na mlio wa simu ya Owen akapokea simu baada ya muda akasema “hapana Don sihitaji kula, sina njaa nimepata tu kifungua kinywa” kisha akakata simu kwa sababu flani ambazo hazikuweza kufahamika akaanza kumpeleleza mhudumu kuhusu ile hoteli na majukumu yake ndaniya hoteli na karudia tena malalamiko yake kuhusu ile hoteli juu ya ughali wake uliomfanya aachane nayo na kuja hapo kwenye hoteli hiyo. Mhudumu alipomaliza kufanya usafi akachuku mataulo yaliyotumika kisha akaondoka pasipo mashaka akiwa na furaha kwa kumuacha mgeni huyo wa ajabu.

Sasa tuangalie mkasa hotelini hapo kwenye chumba hicho ulipoanza kujitengeneza.

Mchana wa siku hiyo kwa mara nyingine tena yule mhudumu akampelekea taulo za kubadilisha, nje ya mlango akasikia wanaume wawili wanaongea kwa ndani ikabidi abishe hodi na kujitambulisha na dhamira yake ila sauti nzito ikamjibu mhudumu huyo kuwa hawahitaji mataulo yoyote yale basi akajiondokea zake. Ina maana huyo ndiyo alikuwa Don mgeni aliyekuwa anasubiriwa na Owen? Mhudumu alikuwa anajiuliza kuhusu sauti hiyo aliyoisikia kuwa ni ya nani? Ila akaona asijisumbue na akaendelea na yanayomuhusu, baadaye ndani ya siku hiyo kuna mteja alikuja ndani ya hoteli akihitaji chumba kwa ajili ya mapumziko alikuwa ni mwanamke akijisajili kwa jina Jean Owen, huyu hakuwa mahusino na Owen wa chumba no. 1046 basi akapewa chumba no. 1048 karibu kabisa na chumba cha Owen mwanamke huyu hakupata usiku wa amani kabisa, alisumbuliwa pasipo kikomo na sauti ya juu kama mwanaume namwanamke wakizozana vikali juu ya jambo flani basi baadaye akasikia sauti kama mtu anahahahaha (scuffle and gasping noises) kutafuta hewa ila akadhani pengine labda ni kukoroma, alijiuliza kama kuna haja ya kutoa taarifa ila akaamua kupuuzia.

Charles Blocher mwendesha lift wa hoteli hiyo aligundua kuna kitu hakipo sawa kwenye chumba hicho usiku huo kwani kulikuwa na mambo ambayo alidhania ni tafrija ya makelele ndani ya chumba no. 1055 muda flani baada ya usiku wa manane alimpeleka mteja falani mwanamke kwenye floor ya 10 ya hoteli, mwanamke huyu alikuwa anaulizia chumba no. 1026. Blocher alishawahi kumuona mwanamke huyo maeneo ya hoteli hapo mara kadhaa akiwa na wanaume kadhaa kwenda kwenye vyumba kadhaa, baada ya dakika chache alipewa taarifa ya kurejea kwenye floor ya 10 mwanamke huyo alikuwa amechomeshwa mahindi maana mwanaume aliyekuwa na miadi naye hakuonekana hivyo Blocher hakuwa na cha kumsaidia hivyo akajishukia zake chini lakini nusu saa baadaye mwanamke huyo akamwiita tena amshushe chini kwenye korido kubwa ya kuchagulia vyumba punde mwanamke huyo akashuka kwenye lift akiwa ameongozana na mwanaume Bolcher akawapeleka kwenye sakafu ya tisa na akajiondokea zake mida ya saa kumi alfajiri akifuatiwa na mwanaume nyuma.

Hii couple haikuja kutambulika na haikuthibitika kama ilihusika kwa namna yoyote na Owen na chumba no. 1046 ila mazingira yao kwa namna moja ama nyingine ilitengeneza haja ya kutiliwa mashaka na hawakuwa wa kupuuza kwenye upelelezi.

Tuangalie kisa cha mfanyakazi wa jiji ndani ya stori hii, ndani ya usiku huo huo tukirudi nyuma kwenye majira ya saa tano usiku mfanyakazi wa jiji aitwaye Robert Lane alikuwa anendesha kuelekea katikati ya jiji alimuona mwanaume mmoja akiwa anamkimbilia akidhani ni dereva taxi ila akumuelezea yeye kuwa ni mfanyakazi tu wa jiji, mwanaume huyu alikuwa amevalia nguo ya ndani tu. Alistaajabu kuona hilo jambo kwenye majira ya baridi, mwanaume huyo alimuomba Robert ampeleke sehemu anapoweza kupata taxi na akakubali kumsaidia na alikuja kugundua kuwa mtu huyo alikuwa na jereha mkononi. Robert akamuuliza vipi umekutana na msala? Mtu huyo akatikisa kichwa kisha akaunguruma “mmnnh nitamuua yule kesho” walifika pahala panapopatikana taxi yule mtu akashuka akachukua taxi na kutokomea Robert hakujua kama anahusika kwa namna moja ama nyingine kwenye jambo kubwa na la kutisha kama hilo.

Sasa turudi kule chumba no. 1046, kwenye mishale ya saa moja asubuhi kesho yake baada ya mhudumu kuambiwa mataulo hayahitajiki, mfanyakazi wa hoteli anayehusika na masuala ya mawasiliano aligundua simu ya chumba hicho iliachwa wazi baada ya kutumia yaani haikukobekwa kitakoni pake baada ya saa tatu kupita bila kukobekwa ikabidi amtume mhudumu Propst akamwambie yeyote aliyechumbani akakate simu. Mhudumu akakuta mlango umefungwa huku pamening’inizwa lebo ya “Do Not Disturb” ikabidi agonge mlango na akasikia sauti ikimruhusu aingie ndani, ila alipofungua mlango alikuta umefungwa akagonga kwa mara nyingine tena mara hii akasikia sauti ikimwagiza taa ziwashwe baada ya kugonga mara kadhaa pasipo matunda akaamua kufoka “wewe weka simu kwenye kitako chake” kisha akijiondokea zake.

Saa moja na nusu baadaye mtu wa mawasiliano akagundua kuwa simu haijakobekwa kitakoni pake basi akamtuma mhudumu mwingine huyu ni Harold Pike kwenda kushughulikia hilo tatizo. Harold akakuta bado mlango umefungwa na kile kinote bado kipo, ikabidi atumie pass key kufungulia mlango ndani ya kiza akaona kuwa Owen alikuwa amelala uchi na simu ilikuwa haijakobekwa kitakoni pake basi akainyanyua na kuirudisha basi akajiondokea zake akijua Owen amejiliwea zake wali hakutaka kutazama hali ya Owen kwa ukaribu zaidi. Mida ya saa tano asubuhi yule mtu wa mawasiliano akagundua tena simu imeondolewa kwenye kitako chake tena akamtuma mhudumu kushughulika na hilo tatizo, alipofika akakuta bado kile kinote kipo mlangoni basi akatumia pass key kuingia ndani lakini mara hii aligundua kitu kisicho cha kawaida.

Alimkuta Owen amepiga magoti huku ameshikilia kichwa chake kilochokuwa kimetapakaa damu, kwa mshtuko mkubwa ikabidi awashe taa ndipo alipokuta damu zimetapakaa ukutani na bafuni, mbio akaenda kutoa taarifa.

Owen alifanywa nini?

Maafisa wa polisi walijagundua kuwa saa sita au saba nyuma kuna mtu alimfanyia kitu kibaya mno Owen, alikuwa amefungwa na kuchomwa kisu mara kadhaa huku fuvu lake lilikuwa na ufa kwa kupigwa mno, shingo yake ilikuwa na mikwaruzo iliyothibitisha kunyongwa. Owen alipoulizwa nini kimetokea akiwa mdhaifu wa fahamu akajibu nilidondokea kwenye sinki la kuogea. Walipofanya ukaguzi ndani ya chumba iligundulika hakukuwa na nguo zozote ndani ya hicho chumba, sabuni, shampoo ma mataulo hayakuwepo pia. Kilichopatikana kilikuwa ni tai, sigara iliyokuwa haijavutwa, alama za damu kwenye taa na kibanio cha kike cha nywele.

Mfanyakazi mmoja wa hoteli alisema saa kadhaa nyuma wakati anamhudumia Owen aliona mwanamke na mwanaume mmoja wanaongozana wakitoka hotelini hapo haraka, hakuwa na shaka kuwa kulikuwa na watu wengine waliojichanganya na hili. Wakati Owen akikimbizwa hospitalini alipoteza fahamu kabisa (coma) na alijafriki usiku wake. Kwanini sasa owen adanganye alianguka kwenye sinki? Ina maana alikuwa anafurahia kifo chake? Au hakuta wauaji wake wajulikane na kukamatwa?

Polisi vichwa vikaanza kuwawaka moto kwani hawaelewi huyo Owen ni mtu wa aina gani. Wapelelezi walikuja kugundua kuwa hayo mauaji ya Owen hayakuwa ya kawaida na polisi wa Los Angeles hawakupata rekodi yoyote kuhusu jina lake jambo ambalo lilipelekea waamini kuwa mtu huyo alighushi jina. Mwili wa Owen ulitangazwa kwa matumaini kuwa kuna mtu anaweza kuutambua, wa kwanza kuja kuuona huo mwili alikuwa Robert Lane ambaye alimfananisha kabisa owen na mtu aliyemuona usiku wa Januari 3, wahudumu kadhaa wa baa nao wakakiri kumuona mwanaume aliyefanana na Owen akiwa ameongozana na wanawake waili. Polisi waligundua pia usiku kabla ya owen kwenda hotelini hapo, mwanaume anaefanana naye alikaa hoteli ya Muehlebach, Kansas City na St. Regis aliyejiandikisha kwa jina Eugene Scott, jina hili pia halikupatikana rekodi zake. Wafanyakazi wa hoteli ya Regis walisema kuna mtu ambaye hakufahamika mara moja alikuwa amemsindikiza Owen hoteli hapo.

Polisi walijitahidi sana kumpata Don ili waligonga mwamba wakabaki tu wanahisi, huenda Don alikuwa mtu aliyemtembelea Owen ambaye alisisitiza kwa mhudumu wa hoteli ile kuwa mataulo safi hayahitajiki, au mgeni yule aliyekuwa ameambata na mwanamke majira ya saa kumi alfajiri au ni yule mtu aliyemsindikiza Regis hotel au yule aliyemuambia Rorbert Lane kuwa atamuua kesho yake? Maswali yote haya hayakuweza kujibiwa.

Siku tisa baada ya Owen kufariki promota wa michezo ya mieleka aitwaye Tony Bernardi alimtambua Owen kama mtu ambaye alimtembelea siku kadhaa nyuma na kujiandikisha kwa ajili ya michezo ya mieleka. Berardi alisema mwanaume huyo alijitambulisha kama Cecil Warner, maelezo hayo hayakusaidia kupata chochote cha kusaidia kuhusu mtu huyo achilia muuaji, kile kibanio cha kike cha nywele kinaamsha hoja, je, mauaji haya yalikuwa mchezo wa mapenzi? Unakumbuka yale maneno ya mwanamke Jean Owen wa chumba no. 1048 kuhusu kusikia sauti ya mwanaume na mwanamke wakizozana na kufokeana? Mwanamke huyo alikuwa ni nani? Na alikuwa anazozana na nani? Nadharia hii imebaki hewani pasi majibu yoyote.

Siku zikiwa zimeenda hadi mwezi wa tatu mwanzoni wapelelezi wakaona hii kesi wameishindwa ikabidi waanze mipango ya mazishi. Muda mfupi kabla ya maziko, wakapata simu siyofahamika kutoka kwa mwanaume mmoja ambaye hakufahamika mara moja akiwasisitiza waahirishe maziko hayo mpaka hela ya huduma hiyo itakapotumwa. Mtu huyo alidai ni shemeji yake Owen yaani alikuwa na mahusiano na dada yake na hilo ni jina lake halisi. Mpigaji simu huyo aliendelea kuwa Owen alikumbana na masahibu magumu na upelelezi huo haupo njia sahihi kiufupi wameingia chaka “on the wrong track”. Siku chache baadaye, hela hiyo ilitumwa kweli huku haina anwani ya kurudisha. Mazishi yalifanyika kwenye makaburi ya Memorial Park na waliohudhuria walikuwa waplelezi hao tu.

Pesa zaidi ikatumwa kwa muuza maua kwa ajili ya maua mengi ya kuweka juu ya kaburi la Owen, huku maua hayo yakiwa na kadi iliyosomeka “Love Forever- Louise”. Wapelelezi walikasirishwa na dharau zinazoendelea na kuona kama maagizo, wakaanza kufuatilia mfumo huo wa pesa ili kubaini ila mtumaji wa pesa hakuwa mjinga na alijua wazi atafuatiliwa hivyo akatumia njia ambayo ni ngumu kung’amua.

Kesi hii ilitupiwa mbali mnamo mwa 1936, ambapo mwanamke mmoja kwa majina Eleanor Ogletree alipoona taarifa za mauaji ya Owen kwenye jarida la American Weekly aligundua taarifa za Owen zinafanana kabisa na za kaka yake aliyepotea anaeitwa Artemus. Familia yao haijapata kumuona tokea mwezi wa nne 1934 alipoondoka nyumbani kwao Birmingham, Alabama kwenda kwenye matembezi.

IMG_20190813_201927.jpg

Mara ya mwisho mama yake Eleanor kwa jina Ruby alipata kusikia jambo kutoka kwake kupitia barua tatu fupi, ambapo kwa mujibu wa tarehe barua ya kwanza aliipokea mwaka 1935 wakati Owen teyari ameshafariki, mama alisema alishangazwa sana na hizo barua kwani alijua fika kuwa mwanae hawezi kutype. Miezi kadhaa mbele akapokea simu kutoka kwa mwanaume aliejitambulisha kwa jina Jordan akimwambia kuwa mwanae amemuokoa maisha yake huko Misri na kwamba mwanaye ameoana na mwanamke tajiri sana huko Cairo. Je, ndiye yule aliyetuma yale maua na pesa za mazishi akidai Owen alikuwa na mahusiano na dada yake? Kuhusu kukawia kwa barua hizo tunaweza kusema ni ufinyu wa teknolojia kipindi hicho lakini alikuwa anaziandika nani ilihali Owen alikuwa kutype!

Kwasasa tushamjua Owen kuwa ni Artemus Ogletree kwa jinsi mama yake alivyothibitisha hilo kwa kuitambua picha ya marehemu, lakini haki ya kifo chake hicho cha kinyama imeyeyuka na kueleaelea kwa kukosa nyama. Kwanini sasa Artemus alikuwa anatumia majina mengi ya kughushi? Nini alikuwa anaficha kuhusu aliyemua na kwanini? Je, Louis ni nani ambaye jina lake lilikuwa kwenye kadi za maua? Jordan ni nani, na nani alituma pesa zake za mazishi na nani alimuandikia mama yake barua hizo na nini kilitokea chumba no.1046. Wapelelezi waligonga mwamba hapa na kichwa kuwauma kila wanapofungua faili la kesi hii, na kuamua kukubaliana tu kuwa muuaji ni Don pasipo ubishi ila Don huyo hafahamika mpaka hii leo, amekuwa ni kivuli kinachoonekana uwepo wake ila hakamatiki nyayo alizoziacha kwenye mawasiliano ya mauaji hayo zimeshindikana kufuatiliwa na kumgundua.

Mpaka leo hii watu wanaosomea upelelezi nchini Marekani wanapenda kuitumia kesi hii kwenye mafunzo yao kutokana na ufundi wa hali ya juu uliyopangwa katika mauji ya Owen.

NIWATAKIE JUMAPILI NJEMA NA YENYE BARAKA TELE
 
google helper

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Messages
6,059
Points
2,000

google helper

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2013
6,059 2,000
Wadau wangu wa nguvu kwenye story za visa na mikasa mbali mbali iliyowahi kutokea na kukuna vichwa vya wapelelezi duniani, naomba leo tutembee pamoja kwenye kisa hiki maridhawa kabisa kilichotokea mwanzoni wa mwaka 1935 huko Missouri, Kansasi Marekani…….

View attachment 1184424

Katika jiji la Kansas, Missouri mchana wa January 2, 1935 mwanaume mmoja allingia ndani ya President Hotel akihitaji chumba kwenye ghorofa kadhaa za juu, hakuwa amebeba mzigo wowote ule zaidi ya brush ya nywele, chanuo na dawa ya meno ndani ya mfuko wa koti lake na akajisajili kwa jina Roland T. Owen wa Los Angeles na akalipia makazi kwa siku moja. Mwanaume huyu alielezewa kuwa mrefu na sauti ndogo ya kukwaruza na nywele nyeusi na kovu kubwa upande wa kushoto wa kichwa chake na akapewa chumba no. 1046.

View attachment 1184425

View attachment 1184426

Wakati akielekea kwenye chumba chake alichopewa Owen akamwambia mhudumu aliejulikana kama Randolph Propst kuwa mwanzoni alikuwa anataka kwenda Muehlebach hotel ila gharama zake zilikuwa juu sana. Walipofika chumbani, Owen alitoa vitu kadhaa kutoka kwenye mfuko wake wa koti ambavyo ni chanuo, dawa ya meno na brush ya nywele na akaviweka vyote bafuni na wote wakatoka chumbani huko kwani Owen alivyochukua tu ufunguo kwa mhudumu huyo aliondoka zake hotelini hapo nna mhudumu akaendelea na kazi zake za kawaida.

Baadaye ndani ya siku hiyo hiyo mhudumu wa kike aliyekuwa amevalia nadhifu alianza kutimiza majukumu yake, na akaelekea chumba no. 1046 na Owen alikuwa ndani ya chumba akamruhusu mhudumu aingie ndani ya chumba akimwambia aache mlango wazi bila kuufunga kwani alikuwa anategemea ugeni wa rafiki yake muda si mrefu. Ndani ya chumba hicho pazia zilikuwa zimeshushwa na madirisha yamefungwa vyema huku chumbani kukiwa na taa nddogo ikiking’arisha chumba hicho, kiufupi mwanga haukuwa wa kutosha.

View attachment 1184427

Mhudumu baadaye alikuja kuwaambia polisi kuwa Owen alionekana mwenye wasiwasi muda mrefu ama asiye na amani, macho yake yalikuwa hayana furaha huku uso wake umezubazwa kwa uoga, wakati muhudumu akisafisha chumba oweni akavaa koti lake na kuondoka huku akiendelea kumsisitizia kutofunga mlango. Ilipotimu saa nne usiku, mhudumu huyu akarudi kwenye chumba cha Owen huku amebebelea mataulo masafi mlango ulikuwa bado hujafungwa na chumba kikiwa bado gizani, Owen alikuwa amejilaza kitandani huku amevalia mavazi yake rasmi, mhudumu akaona kikaratasi kidogo juu ya meza kimeandikwa na kusomeka “Don nitarejea ndani ya dakika 15. Ningojee” nini maana ya ujumbe huo? Huo ujumbe haukuonesha tu alikuwa anatarijia ugeni lakini pia ni ugeni wa aina gani? Jina la Don ambapo ndio ujumbe umelengewa ni jina linatumika huko Uhispania, Ureno, Italia mpaka Ufilipino kama kianzio cha jina la mtu mwenye mamlaka au cheo, huko Amerika ya Kaskazini jina la Don lilifanywa maarufu sana kwa njia ya filamu za kimafia kama vile The Godfather ambpo ndani yake kiongozi wa uhalifu hudai ishara za heshima ambazo kiuhalisia zilikuwa zikitolewa kwa viongozi wa hadhi wa huko Italia.

Hivyo Owen alikuwa akingojea Don ujio mkubwa kabisa huu kwake, kwa kawaida madon hawakutani na watu/wafanyakazi wake kwa jambo dogo bali kwa ajili ya mambo nyeti na muhimu sana na huwa hawana masikhara kabisa wala muda wa kupoteza pia kwao suala la kuua ni kawaida sana, si bure Owen alikuwa anahofia wala hakuwa na furaha wala amani kwani alishindwa kukimbia ili kuiokoa nafsi yake si rahisi kama unavyowaza kwani Don akikuhitaji hakuna pa kuponea. Bila shaka rejea za Dons kama kama kina Richards Leornad Kuklinski “The Iceman”- huyu alitokea familia ya American Mafia iliyojulikana kama DeCavalcante crime family of Newark, Giovanni Brusaca “The Pig”- huyu alitokea Sicilian Mafia ya Italia, Roy Albert DeMeo- huyu alitokea The Gambino crime family huko New York na Joseph “The Animal” Barbosa- huyu alikuwa mixer ya Kireno na Kimarekani wa Patriarca crime family zinaweza kuonesha hawa viumbe ni watu wa aina gani hasa unapokatiza kwenye 19 zao. Utani kidogo mkuu Don Clericuzio una la kuzungumzia hapa kuhusu hawa madon wenzako .

Baada ya hapo Owen alikuja kuonekana kesho yake 4:30 asubuhi mhudumu alipokuja kusafisha chumba chake. Alipofungua mlango kwa kutumia pass key ambapo mhudumu atafanya endapo tu mlango umefungwa kwa ndani, alipoingia kashangaa kumkuta Owen ameketi kimya kwenye kiti akitazama nje na hakuonekana kama mtu anaejali, hali hii ya tahamaki ilivunjwa na mlio wa simuya Owen akapokea simu baada ya muda akasema “hapana Don sihitaji kula, sina njaa nimepata tu kifungua kinywa” kisha akakata simu kwa sababu flani ambazo hazikuweza kufahamika akaanza kumpeleleza mhudumu kuhusu ile hoteli na majukumu yake ndaniya hoteli na karudia tena malalamiko yake kuhusu ile hoteli juu ya ughali wake uliomfanya aachane nayo na kuja hapo kwenye hoteli hiyo. Mhudumu alipomaliza kufanya usafi akachuku mataulo yaliyotumika kisha akaondoka pasipo mashaka akiwa na furaha kwa kumuacha mgeni huyo wa ajabu.

Sasa tuangalie mkasa hotelini hapo kwenye chumba hicho ulipoanza kujitengeneza.

Mchana wa siku hiyo kwa mara nyingine tena yule mhudumu akampelekea taulo za kubadilisha, nje ya mlango akasikia wanaume wawili wanaongea kwa ndani ikabidi abishe hodi na kujitambulisha na dhamira yake ila sauti nzito ikamjibu mhudumu huyo kuwa hawahitaji mataulo yoyote yale basi akajiondokea zake. Ina maana huyo ndiyo alikuwa Don mgeni aliyekuwa anasubiriwa Owen? Mhudumu alikuwa anajiuliza kuhusu sauti hiyo aliyoisikia kuwa ni ya nani? Ila akaona asijisumbue na akaendelea na yanayomuhusu, baadaye ndani ya siku hiyo kuna mteja alikuja ndani ya hoteli akihitaji chumba kwa ajili ya mapumziko alikuwa ni mwanamke akijisajili kwa jina Jean Owen, huyu hakuwa mahusino na Owen wa chumba no. 1046 basi akapewa chumba no. 1048 karibu kabisa na chumba cha Owen mwanamke huyu hakupata usiku wa amani kabisa, alisumbuliwa pasipo kikomo na sauti ya juu kama mwanaume namwanamke wakizozana vikali juu ya jambo flani basi baadaye akasikia sauti kama mtu anahahahaha (scuffle and gasping noises) kutafuta hewa ila akadhani pengine labda ni kukoroma, alijiuliza kama kuna haja ya kutoa taarifa ila akaamua kupuuzia.

Charles Blocher mwendesha lift wa hoteli hiyo aligundua kuna kitu hakipo sawa kwenye chumba hicho usiku huo kwani kulikuwa na mambo ambayo alidhania ni tafrija ya makelele ndani ya chumba no. 1055 muda flani baada ya usiku wa manane alimpeleka mteja falani mwanamke kwenye floor ya 10 ya hoteli, mwanamke huyu alikuwa anaulizia chumba no. 1026. Blocher alishawahi kumuona mwanamke huyo maeneo ya hoteli hapo mara kadhaa akiwa na wanaume kadhaa kwenda kwenye vyumba kadhaa, baada ya dakika chache alipewa taarifa ya kurejea kwenye floor ya 10 mwanamke huyo alikuwa amechomeshwa mahindi maana mwanaume aliywkuwa na miadi naye hakuonekana hivyo Blocher hakuwa na cha kumsaidia hivyo akajishukia zake chini lakini nusu saa baadaye mwanamke huyo akamwiita tena amshushe chini kwenye korido kubwa ya kuchagulia vyumba punde mwanamke huyo akashuka kwenye lift akiwa ameongozana na mwanaume Bolcher akawapeleka kwenye sakafu ya tisa na akajiondokea zake mida ya saa kumi alfajiri akifuatiwa na mwanaume nyuma.

Hii couple haikuja kutambulika na haikuthibitika kama ilihusika kwa namna yoyote na Owen na chumba no. 1046 ila mazingira yao kwa namna moja ama nyingine ilitengeneza haja ya kutiliwa mashaka na hawakuwa wa kupuuza kwenye upelelezi.

Tuangalie kisa cha mfanyakazi wa jiji ndani ya stori hii, ndani ya usiku huo huo tukirudi nyuma kwenye majira ya saa tano usiku mfanyakazi wa jiji aitwaye Robert Lane alikuwa anendesha kuelekea katikati ya jiji alimuona mwanaume mmoja akiwa anamkimbilia akidhani ni dereva taxi ila akumuelezea yeye kuwa ni mfanyakazi tu wa jiji, mwanaume huyu alikuwa amevalia nguo ya ndani tu. Alistaajabu kuona hilo jambo kwenye majira ya baridi, mwanaume huyo alimuomba Robert ampeleke sehemu anapoweza kupata taxi na akakubali kumsaidia na alikuja kugundua kuwa mtu huyo alikuwa na jereha mkononi. Robert akamuuliza vipi umekutana na msala? Mtu huyo akatikisa kichwa kisha akaunguruma “mmnnh nitamuua yule kesho” walifika pahala panapopatikana taxi yule mtu akashuka akachukua taxi na kutokomea Robert hakujua kama anahusika kwa namna moja ama nyingine kwenye jambo kubwa na la kutisha kama hilo.

Sasa turudi kule chumba no. 1046, kwenye mishale ya saa moja asubuhi kesho yake baada ya mhudumu kuambiwa mataulo hayahitajiki, mfanyakazi wa hoteli anayehusika na masuala ya mawasiliano aligundua simu ya chumba hicho iliachwa wazi baada ya kutumia yaani haikukobekwa kitakoni pake baada ya saa tatu kupita bila kukobekwa ikabidi amtume mhudumu Propst akamwambie yeyote aliyechumbani akakate simu. Mhudumu akakuta mlango umefungwa huku pamening’inizwa lebo ya “Do Not Disturb” ikabidi agonge mlango na akasikia sauti ikimruhusu aingie ndani, ila alipofungua mlango alikuta umefungwa akagonga kwa mara nyingine tena mara hii akasikia sauti ikimwagiza taa ziwashwe baada ya kugonga mara kadhaa pasipo matunda akaamua kufoka “wewe weka simu kwenye kitako chake” kisha akijiondokea zake.

Saa moja na nusu baadaye mtu wa mawasiliano akagundua kuwa simu haijakobekwa kitakoni pake basi akamtuma mhudumu mwingine huyu ni Harold Pike kwenda kushughulikia hilo tatizo. Harold akakuta bado mlango umefungwa na kile kinote bado kipo, ikabidi atumie pass key kufungulia mlango ndani ya kiza akaona kuwa Owen alikuwa amelala uchi na simu ilikuwa haijakobekwa kitakoni pake basi akainyanyua na kuirudisha basi akajiondokea zake akijua Owen amejiliwea zake wali hakutaka kutazama hali ya Owen kwa ukaribu zaidi. Mida ya saa tano asubuhi yule mtu wa mawasiliano akagundua tena simu imeondolewa kwenye kitako chake tena akamtuma mhudumu kushughulika na hilo tatizo, alipofika akakuta bado kile kinote kipo mlangoni basi akatumia pass key kuingia ndani lakini mara hii aligundua kitu kisicho cha kawaida.

Alimkuta Owen amepiga magoti huku ameshikilia kichwa chake kilochokuwa kimetapakaa damu, kwa mshtuko mkubwa ikabidi awashe taa ndipo alipokuta damu zimetapakaa ukutani na bafuni, mbio akaenda kutoa taarifa. Owen alifanywa nini?

Maafisa wa polisi walijagundua kuwa saa sita au saba nyuma kuna mtu alimfanyia kitu kibaya mno Owen, alikuwa amefungwa na kuchomwa kisu mara kadhaa huku fuvu lake lilikuwa na ufa kwa kupigwa mno, shingo yake ilikuwa na mikwaruzo iliyothibitisha kunyongwa. Owen alipoulizwa nini kimetokea akiwa mdhaifu wa fahamu akajibu nilidondokea kwenye sinki la kuogea. Walipofanya ukaguzi ndani ya chumba iligundulika hakukuwa na nguo zozote ndani ya hicho chumba, sabuni, shmpoo ma mataulo hayakuwepo pia. Kilichopatikana kilikuwa ni tai, sigara iliyokuwa haijavutwa, alama za damu kwenye taa na kibanio cha kike cha nywele.

Mfanyakazi mmoja wa hoteli alisema saa kadhaa nyuma wakati anamhudumia Owen aliona mwanamke na mwanaume mmoja wanaongozana wakitoka hotelini hapo haraka, hakuwa na shaka kuwa kulikuwa na watu wengine waliojichanganya na hili. Wakati Owen akikimbizwa hospitalini alipoteza fahamu kabisa (coma) na alijafriki usiku wake. Kwanini sasa owen adanganye alianguka kwenye sinki? Ina maana alikuwa anafurahia kifo chake? Au hakuta wauaji wake wajulikane na kukamatwa?

Polisi vichwa vikaanza kuwawaka moto kwani hawaelewi huyo Owen ni mtu wa aina gani. Wapelelezi walikuja kugundua kuwa hayo mauaji ya Owen hayakuwa ya kawaida na polisi wa Los Angeles hawakupata rekodi yoyote kuhusu jina lake jambo ambalo lilipelekea waamini kuwa mtu huyo alighushi jina. Mwili wa Owen ulitangazwa kwa matumaini kuwa kuna mtu anaweza kuutambua, wa kwanza kuja kuuona huo mwili alikuwa Robert Lane ambaye alimfananisha kabisa owen na mtu aliyemuona usiku wa Januari 3, wahudumu kadhaa wa baa nao wakakiri kumuona mwanaume aliyefanana na Owen akiwa ameongozana na wanawake waili. Polisi waligundua pia usiku kabla ya owen kwenda hotelini hapo, mwanaume anaefanana naye alikaa hoteli ya Muehlebach, Kansas City na St. Regis aliyejiandikisha kwa jina Eugene Scott, jina hili pia halikupatikana rekodi zake. Wafanyakazi wa hoteli ya Regis walisema kuna mtu ambaye hakufahamika mara moja alikuwa amemsindikiza Owen hoteli hapo.

Polisi walijitahidi sana kumpata Don ili waligonga mwamba wakabaki tu wanahisi, huenda Don alikuwa mtu aliyemtembelea Owen ambaye alisisitiza kwa mhudumu wa hoteli ile kuwa mataulo safi hayahitajiki, au mgeni yule aliyekuwa ameambata na mwanamke majira ya saa kumi alfajiri au ni yule mtu aliyemsindikiza Regis hotel au yule aliyemuambia Rorbert Lane kuwa atamuua kesho yake? Maswali yote haya hayakuweza kujibiwa.

Siku tisa baada ya Owen kufariki promota wa michezo ya mieleka aitwaye Tony Bernardi alimtambua Owen kama mtu ambaye alimtembelea siku kadhaa nyuma na kujiandikisha kwa ajili ya michezo ya mieleka. Berardi alisema mwanaume huyo alijitambulisha kama Cecil Warner, maelezo hayo hayakusaidia kupata chochote cha kusaidia kuhusu mtu huyo achilia muuaji, kile kibanio cha kike cha nywele kinaamsha hoja, je, mauaji haya yalikuwa mchezo wa mapenzi? Unakumbuka yale maneno ya mwanamke Jean Owen wa chumba no. 1048 kuhusu kusikia sauti ya mwanaume na mwanamke wakizozana na kufokeana? Mwanamke huyo alikuwa ni nani? Na alikuwa anazozana na nani? Nadharia hii imebaki hewani pasi majibu yoyote.

Siku zikiwa zimeenda hadi mwezi wa tatu mwanzoni wapelelezi wakaona hii kesi wameishindwa ikabidi waanze mipango ya mazishi. Muda mfupi kabla ya maziko, wakapata simu siyofahamika kutoka kwa mwanaume mmoja ambaye hakufahamika mara moja akiwasisitiza waahirishe maziko hayo mpaka hela ya huduma hiyo itakapotumwa. Mtu huyo alidai ni shemeji yake Owen yaani alikuwa na mahusiano na dada yake na hilo ni jina lake halisi. Mpigaji simu huyo aliendelea kuwa Owen alikumbana na masahibu magumu na upelelezi huo haupo njia sahihi kiufupi wameingia chaka “on the wrong track”. Siku chache baadaye, hela hiyo ilitumwa kweli huku haina anwani ya kurudisha. Mazishi yalifanyika kwenye makaburi ya Memorial Park na waliohudhuria walikuwa waplelezi hao tu.

Pesa zaidi ikatumwa kwa muuza maua kwa ajili ya maua mengi ya kuweka juu ya kaburi la Owen, huku maua hayo yakiwa na kadi iliyosomeka “Love Forever- Louise”. Wapelelezi walikasirishwa na dharau zinazoendelea na kuona kama maagizo, wakaanza kufuatilia mfumo huo wa pesa ili kubaini ila mtumaji wa pesa hakuwa mjinga na alijua wazi atafuatiliwa hivyo akatumia njia ambayo ni ngumu kung’amua.

Kesi hii ilitupiwa mbali mnamo mwa 1936, ambapo mwanamke mmoja kwa majina Eleanor Ogletree alipoona taarifa za mauaji ya Owen kwenye jarida la American Weekly aligundua taarifa za Owen zinafanana kabisa na za kaka yake aliyepotea anaeitwa Artemus. Familia yao haijapata kumuona tokea mwezi wa nne 1934 alipoondoka nyumbani kwao Birmingham, Alabama kwenda kwenye matembezi.

View attachment 1184429

Mara ya mwisho mama yake Eleanor kwa jina Ruby alipata kusikia jambo kutoka kwake kupitia barua tatu fupi, ambapo kwa mujibu wa tarehe barua ya kwanza aliipokea mwaka 1935 wakati Owen teyari ameshafariki, mama alisema alishangazwa sana na hizo barua kwani alijua fika kuwa mwanae hawezi kutype. Miezi kadhaa mbele akapokea simu kutoka kwa mwanaume aliejitambulisha kwa jina Jordan akimwambia kuwa mwanae amemuokoa maisha yake huko Misri na kwamba mwanaye ameoana na mwanamke tajiri sana huko Cairo. Je, ndiye yule aliyetuma yale maua na pesa za mazishi akidai Owen alikuwa na mahusiano na dada yake? Kuhusu kukawia kwa barua hizo tunaweza kusema ni ufinyu wa teknolojia kipindi hicho lakini alikuwa anaziandika nani ilihali Owen alikuwa kutype!

Kwasasa tushamjua Owen kuwa ni Artemus Ogletree kwa jinsi mama yake alivyothibitisha hilo kwa kuitambua picha ya marehemu, lakini haki ya kifo chake hicho cha kinyama imeyeyuka na kueleaelea kwa kukosa nyama. Kwanini sasa Artemus alikuwa anatumia majina mengi ya kughushi? Nini alikuwa anaficha kuhusu aliyemua na kwanini? Je, Louis ni nani ambaye jina lake lilikuwa kwenye kadi za maua? Jordan ni nani, na nani alituma pesa zake za mazishi na nani alimuandikia mama yake barua hizo na nini kilitokea chumba no.1046. Wapelelezi waligonga mwamba hapa na kichwa kuwauma kila wanapofungua faili la kesi hii, na kuamua kukubaliana tu kuwa muuaji ni Don pasipo ubishi ila Don huyo hafahamika mpaka hii leo, amekuwa ni kivuli kinachoonekana uwepo wake ila hakamatiki nyayo alizoziacha kwenye mawasiliano ya mauaji hayo zimeshindikana kufuatiliwa na kumgundua.

Mpaka leo hii watu wanaosomea upelelezi nchini Marekani wanapenda kuitumia kesi hii kwenye mafunzo yao kutokana na ufundi wa hali ya juu uliyopangwa katika mauji ya Owen.

NIWATAKIE JUMAPILI NJEMA NA YENYE BARAKA TELE
asante
 
Forum statistics

Threads 1,382,646
Members 526,426
Posts 33,832,678
Top