Riwaya ya Kijasusi: "Msako wa Mwehu"

Riwaya ya Kijasusi: "Msako wa Mwehu"

- 14 -

Riwaya: MSAKO

Mtunzi: Japhet Nyangoro.

“Kwa herini, acha Poka awaonyeshe kazi!’’ Jacob alisema wakati akipotelea vichakani. Aliweza kuona magari kadhaa yakiwa na taa zinazomweta mweta juu, akabaini kuwa wale walikuwa ni askari. Bado Jacob Matata alikuwa na mshangao. Kuvamiwa kwenye eneo kama hilo aliona ni sawa na kuingiliwa na nyoka chumbani, kitandani kwako. Akatokomea maana hakutaka shari na askari ambao sasa walikuwa wakirusha risasi ovyo baada ya kuona maiti eneo lile.


*********************

"MAKAMANDA, nitasoma hii taarifa kama ilivyoletwa hapa na jopo la wataalam. Kama tulivyoomba, tumeletewa upembuzi juu ya ile nyumba iliyovamiwa kule porini” Alianza afisa huyu mwenye wasifa mkubwa jeshini.
“Kamanda, labda kabla hujaendelea sana, ni vema kikao hiki kikaambia ile nyumba ina kazi gani? Afisa mwingine aliuliza.
“Naomba kuwasilisha taarifa hii juu ya nyumba hiyo halafu juu ya huyu mtu aitwaye Jacob Matata. Baada ya kumaliza kusoma bila shaka tutaijadili na kuulizana maswali." Alisema afisa huyo.
"Taarifa inasema; Safe House au nyumba ya Hazina kama wengi tunavyoiita, ni nyumba inayoaminiwa kuwa na mafaili ya kihistoria na siri kubwa na nyingine zenye utata mkubwa. Uwepo wa nyumba hiyo na mahali ilipo imekuwa fumbo kwa muda mrefu sana. Ila sasa imebainika kuwa iko katika msitu mdogo wa Mabwepande ulioko katika Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam. Hadi jana, kaba ya tukio lilochukua maisha ya askari wetu watano, ni watu watano tu katika nchi hii ndiyo waliokuwa wakijua kuwa nyumba hiyo ndiyo Safe House. Wengi tumekuwa tukijua kuwa katika nchi hii kuna safe house lakini hakukuwa na hakika kuwa nyumba hiyo ilikuwa wapi. Kama ilivyo kawaida kuwa serikali huagiza Jeshi la Polisi au Jeshi la Ulinzi kutoa ulinzi sehemu nyingi ambazo hudhaniwa kuwa zinahitaji ulinzi. Mara nyingine jeshi huwa haliambiwi ni kwa nini sehemu fulani imeombewa ulinzi na sababu kubwa ambayo ukipewa huwezi kuuliza zaidi ni lile jibu lisemalo ni kwa usalama wa nchi. Afisa ukishaambiwa ni kwa usalama wa nchi basi, ulinzi hutolewa kwa sehemu au mtu husika. Kwa jinsi jengo hilo lilivyojengwa si rahisi mtu kuweza kuingia bila msaada wa hao watu watano wanaojua kuwa nyumba hiyo ni safe house. Watu hao ndiyo pekee ambao vidole gumba vyao ndiyo funguo za kila mlango katika nyumba hiyo”

“Imebainika kuwa, Jacob Matata aliingizwa humo juzi asubuhi kwa sababu alikuwa amepewa kazi maalum ndani ya nyumba hiyo. Kazi hiyo inahusiana moja kwa moja na jitihada za kutafuta ukweli juu ya kutoweka kwa Judith Muga yule mtaalam wa mambo ya gesi, kuanguka kwa ndege iliyokuwa imebeba wataalamu wa mambo ya gesi ambao walikuwa wamemaliza kazi ya kuchunguza na kupima kiwango cha gesi. Lakini pia kuuawa kwa waziri Sabodo Msumari kulisababisha Jacob Matata apewe kazi . Hivyo inasemekana na kuna mambo Jacob Matata alitakiwa kuyasoma na kisha kuyafanyia kazi katika jitihada za kujua chanzo cha mauaji haya na mtu aliyeko nyuma ya mauaji haya!!

“Leo asubuhi, iligundulika kuwa mlango wa kuingilia ndani ya nyumba hiyo ulikuwa wazi huku miili ya walinzi wawili ikiwa nje, wakiwa wamekufa. Baada ya kuingia ndani, imegundulika kuwa hakuna faili hata moja lililoibiwa, hakuna uharibifu mwingine uliofanyika. Sakafuni kwenye chumba ambacho Jacob Matata alitakiwa kufanyia kazi, kulikuwa na maiti nyingine mbili, ambazo inaonyesha muuaji hakutumia siraha ya aina yeyote kutekeleza mauaji. Haijulikani walinzi hao waliingiaje ndani ya nyumba hiyo na kwenda kwenye chumba alichokuwa Jacob Matata”

“Lakini pamoja na maiti hiyo kulikuwa na vipande vya kitu kilichovunjwa vunjwa, baada ya kukichunguza kitu hicho, wataalamu wetu wamejiridhisha kuwa kitu hicho ni ‘Vig - Spy AV Camera’ ambayo ilirekebishwa na kupewa uwezo wa kutuma taarifa mara mtumiaji anapofanikiwa kupiga picha au kurekodi tukio.Wanasema kamera hiyo huwa na ukubwa wa kiberiti. Hivyo kwenye kamera hiyo hakukuwa na kitu chochote cha maana. Haijulikani kama kamera hiyo ilikuwa ikitumiwa na Jacob Matata au yule mlinzi. Lakini vyovyote iwavyo katika mazingira waliyokuwepo hakuna hata mmoja aliyetakiwa kuwa na kamera kama ile, muda na mahali kama pale. Kingine kilichokutwa sakafuni ni kitabu cha riwaya kiitwacho Patashika kilichoandikwa na Mwandishi Japhet Nyang'oro”

“Janga jingine lililoongezeka jana ni kuibiwa kwa kisanduku cheusi kilichokuwa kwenye ndege iliyoanguka wiki na siku kadhaa zilizopita sasa. Hii inaamanisha idara nzima ya usalama iko gizani na haina usukani wa kile kinachoendelea sasa katika vita hii ambayo wengi wanaihusisha na hujuma dhidi ya kupatikana kwa gesi hapa nchini. Ambapo nchi kadhaa za kiarabu zinataka kushika soko ndani ya wiki au miezi michache ijayo hivyo wameona kuchelewesha Tanzania kuingia sokoni na pia kuyafanya makampuni ya Magharibi kuogopa kuja Tanzania kuwekeza kwa sababu za kiusalama”

“Jacob Matata ni kijana mwenye umri kati ya miaka 35 hadi 40. Ni mmoja kati ya wapelelezi bora kwa sasa waliopo Afrika. Mtu mwenye sifa zote za kuitwa Komandoo. Amehitimu kwa kiwango cha juu katika fani za karate, kung - fu, judo na mengineyo. Anadhaniwa ni kati ya watu wachache sana wenye uwezo wa hali ya juu katika kutumia silaha ya aina yoyote ile. Ni mtu hatari sana”.

“Tanzania imekuwa ikimtumia katika misheni mbalimbali za kipelelezi ambazo zilidhaniwa kuwa zilihitaji mtu mwenye mbinu za hali ya juu katika kukabiliana na ujasusi. Mara nyingi kitengo cha Usalama cha Umoja wa Mataifa (UUM), kimekuwa kikileta maombi ya kutaka kumtumia Jacob Matata katika pelelezi ambazo zilihitaji umakini na ufanisi wa hali ya juu. Hata hivyo kwa hapa nchini haijulikani anafanya kazi chini ya idara gani na hata ofisi yake haijulikani iliko. Jacob Matata anaishi Sinza. Mwisho wa taarifa.’’

"Makamanda, hiyo ndiyo taarifa iliyoandaliwa na wataalam wetu kutokana na vyanzo mbalimbali vya taarifa. Sasa labda tupate fursa ya kuijadili." Alisema afisa huyu huku akionyesha kuwa alikuwa amewapa fursa ya kuongea wenzie. Maafisa hawa wa ngazi za juu jeshini wote walikuwa wamevalia kiraia kabisa, ni tofauti na utaratibu, lakini walifanya hivyo makusudi kwa vile kikao hiki kilikuwa cha siri na hawakutaka kuvuta macho ya watu wengi. Hata kukutana kwao ilikuwa ni sehemu ambayo huwezi dhani kuwa maafisa wa usalama wa ngazi za juu kama hawa wangekutana.

Mjadala uliendelea kabla ya Luteni Frank Misanya kuongea. “Sijui kama ina uhusiano na hali, hii mnamkumbuka yule jamaa hatari sanaliyetingisha nchi wakati ule wa kashfa ya Loliondo (KL) aitwaye Poka Kingu, ambaye alikuwa amewekwa kwenye jela maalum, ametoweka siku kadhaa zilizopita huku walinzi kadhaa wa gereza hilo wakiwa wameuawa. Hivi jitihada za kumtafuta zimepamba moto. Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa kuna watu walikuja kumchukua toka gerezani. Kwani nini na ni wakina nani? Hilo halijulikani.” Frank Misanya alisema na kuketi

“Hii ni ajabu sana, amewezaje kutoroka kwenye mazingira kama yale, lazima kuna mkono wa mtu hapa. Haiwezekani mtu hatari kama yule akawa ameingia mtaani. Nimjuavyo Poka Kingu ni wazi mji huu unaingia katika hekaheka kubwa sana. Yule si mtu wa kuwa huru, hafai kuitwa raia yule!’’ Kamanda mmoja alisema kwa jazba kuonyesha kuwa hiyo ilikuwa taarifa mbaya sana.

“Kwangu hii ni taarifa mbaya sana kuliko hata kutoweka kwa Jacob Matata. Poka Kingu ni mtu ambaye hata kikosi maalum kilimshindwa, mtu pekee ambaye alifanikiwa kumtia nguvuni kichaa yule ni Jacob Matata ambaye sasa hatujui yuko wapi na kama bado yu upande wa serikali. Hapa inabidi kuandaa kikosi cha makomandoo tayari kwa kukabiliana na Poka. Mshenzi sana yule, ile staili yake ya kupiga na kuua, natamani tungekuwa na watu kama yeye kwenye jeshi letu.” Alisema huyu afisa huku akitoa leso na kufuta kipaji chake cha uso.

“Mimi napendekeza atafutwe yeye na yeyote aliye nyuma ya kutoroka kwake.” Alisema mwenyekiti wa kikao, kisha akaongeza, “Je, kuna maendeleo yoyote kwenye uchunguzi wa kifo cha Mh. Sabodo?’’ Swali lake lilisababisha afisa mwingine atengeneze koo lake na kuanza kutoa maelezo.

“Uchunguzi ulikwenda vema sana lakini ulikatikia kwa msichana aitwaye Jo Mwa. Baada ya kupima na kujiridisha kuwa mabaki ya mifupa tuliyokuta kwenye gari lililoungua moto kule Masaki ilikuwa ya mheshimiwa Sabodo Sumari, upelelezi ukaanzia kwenye hilo gari ambalo mabaki ya mwili wake yalikutwa. Kwa kusoma namba za injini ya gari na kuwasiliana na TRA, tulikuja gundua kuwa gari lile lilikuwa likimilikiwa na msichana aitwaye Nanalungu. Upelelezi wa zaidi ukatuonyesha kuwa msichana huyo alinunuliwa gari hilo na Sabodo Sumari. Hivyo harakati za kumtafuta Nanalungu zikaanza, akapatikana akiwa maeneo ya Mbagala. Baada ya mahojiano naye ilikuja thibitika kuwa msichana huyo hakuwa anajua chochote kuhusu Sabodo Sumari, japo katika kupekua nyumba yake tulijikuta tumefanikiwa kupata kadi ya ya usajili wa gari lililoungua. Lakini ukimwangalia yule msichana kuna ishara zote kuwa hakuwa anajua chochote kuhusiana na Sabodo Sumari wala kifo chake. Kuna uwezekano kuwa zile nyaraka za gari zilipandikizwa kwenye nyumba yake bila yeye kujua. Tukaamua kuchukua alama za vidole zilizokuwa kwenye zile nyaraka. Hapo tukajiridhisha kuwa msichana yule hakuwahi kushika zile nyaraka”

“Tukajua yeyote aliyefanya vile alifanya kusudi kupoteza ushahidi. Sasa kazi ni kumtafuta msichana aliyehusika, maana alama za vidole zinaonyesha mtu wa mwisho kushika bahasha ile alikuwa ni msichana.” Afisa huyo alimalizia maelezo yake.

“Kazi nzuri, nadhani tukubaliane kimsingi kuwa kazi iwe kuwatafuta watu watatu; Jacob Matata, Poka Kingu na huyu msichana Nanalungu. Lakini labda pia, ni vema nikawaambia kuwa kuna msichana mwingine aitwaye Jo Mwa ambaye kwa mujibu wa Polisi ndiye aliyehusika kusuka mpango wa kumtorosha Poka Kingu toka gereza maalum. Katika ripoti hii nimeambatisha ripoti niliyokuwa nimeipata toka kwa marehemu Inspekta Lucas Mwenda. Hivyo ni vema huyu naye tukamwingiza kwenye mchakato wa kumtafuta. Kazi hii nampatia Luteni Frank Misanya.” Alimaliza maelezo yake. Minong’ono ilisikika huku kila mmoja akijaribu kuuliza na kuongea jambo na jirani yake.

“Tutakutana hapa baada ya siku mbili kwa kikao kingine muda kama huu wa leo.” Mwenyekiti wa kikao alisema na kikao kikawa kimefungwa.

Itaendelea
 
Ina maana misanya anakula huku na kule
 
- 15 -

Riwaya: Msako
Mtunzi: Japhet Nyang’oro

“Tukajua yeyote aliyefanya vile alifanya kusudi kupoteza ushahidi. Sasa kazi ni kumtafuta msichana aliyehusika, maana alama za vidole zinaonyesha mtu wa mwisho kushika bahasha ile alikuwa ni msichana.” Afisa huyo alimalizia maelezo yake.

“Kazi nzuri, nadhani tukubaliane kimsingi kuwa kazi iwe kuwatafuta watu watatu; Jacob Matata, Poka Kingu na huyu msichana Nanalungu. Lakini labda pia, ni vema nikawaambia kuwa kuna msichana mwingine aitwaye Jo Mwa ambaye kwa mujibu wa Polisi ndiye aliyehusika kusuka mpango wa kumtorosha Poka Kingu toka gereza maalum. Katika ripoti hii nimeambatisha ripoti niliyokuwa nimeipata toka kwa marehemu Inspekta Lucas Mwenda. Hivyo ni vema huyu naye tukamwingiza kwenye mchakato wa kumtafuta. Kazi hii nampatia Luteni Frank Misanya.” Alimaliza maelezo yake. Minong’ono ilisikika huku kila mmoja akijaribu kuuliza na kuongea jambo na jirani yake.

“Tutakutana hapa baada ya siku mbili kwa kikao kingine muda kama huu wa leo.” Mwenyekiti wa kikao alisema na kikao kikawa kimefungwa.


**************


"Kuna jambo haliko sawa hapa mheshimiwa." Bi Anita alisema huku akimwangalia Rais wa Nchi (RN) Mhe. Jovin Sekendu kwa macho ya maswali.
"Sijakuita kwenye hii ofisi ili uniambie kuwa kitu kiko sawa au hakiko sawa Mkurugenzi." Mhe. Jovin Sekendu alifoka huku akionyesha kuwa mwenye hamaki sana. "Ninachosema kama hujashirikiana na Jacob kufanya yale yaliyofanyika safe house usiku wa kuamkia leo basi inabidi uanze kuelewa kuwa Jacob Matata amekuwa msaliti wa nchi. Na ndani ya saa chache, kama nisipopata maelezo ya kutosha toka kwako, nitatoa amri ya Jacob Matata kusakwa kama haini." Rais wa Nchi (RN) Mhe. Jovin Sekendu alisema huku akijimiminia kinywaji kikali kwenye glasi. Macho yake yalikuwa mekundu huku akionekana kuwa mwenye kuchoka sana.
Bi. Anita hakusema lolote, alikuwa akimsikiliza Rais wa Nchi (RN) Mhe. Jovin Sekendu na kubaki na maswali mengi kichwani jinsi mambo yalivyokuwa yakienda kwa mwendo wa kuruka.
“Lakini iko wazi kuwa kidole cha Waziri Mkuu (WM) ndicho kimetumika kufungulia. Maana taarifa ya uchunguzi inasema kwenye kioo ambapo ndipo mfunguaji anatakiwa kuweka kidole, zimekutwa alama za kidole cha Waziri Mkuu.” Bi. Anita alisema
“Waziri Mkuu (WM) alikatwa kidole cha kushoto na pale wameona cha kushoto, ila kidole chenye uwezo wa kufungua mlango ni cha kulia.” Mhe. Jovin Sekendu alisema huku akiichukua ripoti ile ya tukio la kuvamiwa safe house na kuipekua tena.
“Ina maana wanataka kumhusisha tu Waziri Mkuu (WM) na tukio halafu ili iweje?’’ Bi. Anita alihoji.
“Wewe mkuu wa shirika la kijasusi ndo unaniuliza miye badala ya miye kukuuliza wewe!’’ Rais alisema.
“Lakini ukweli unabaki kuwa wazi kuwa, mlango lazima ufunguliwe na mmoja wetu sisi watu watano. Hivyo kama si Waziri Mkuu basi mmoja wetu ametumika kwa kujua au kutojua.” Bi. Anita alisema kwa sauti ya chini kisha akaongeza, “Waziri Sabodo Sumari mwili wake umekutwa ukiwa na vidole vyote japo ilikuwa mabaki ya mifupa iliyoungua moto. Mwili huo wa Sabpdp ulipatikana hata kabla ya tukio la safe house. Hii ina maana hakuna namna yeye amehusika. Mheshimiwa, naomba unipe muda wa kufikiri na kujua nini cha kufanya...."
"Muda nimeshakupa, ukasema unamwamini Jacob Matata anaweza kutupatia ufumbuzi wa jambo hili. Lakini matokeo yake, yeye ndiye kawaua walinzi wote safe house na kutoweka kiasi kuwa hata wewe mkuu wake wa kazi unaniambia hujui alipo....." Mhe. Jovin Sekendu alisema huku safari hii akiwa anamwangalia Bi. Anita kwa macho makali mekundu yaliyokuwa yamelemewa na uchovu, pombe kali, fadhaa, hasira na woga.
"Bado nahitaji Muda, hata kama si muda mwingi lakini bado nahitaji muda. Halafu nahitaji unisaidie jambo moja. Nahitaji kumtumia tena Jacob Matata. Bado namwamini!’’ Bi. Anita alisema kwa msisitizo.
"Tukubaliane mambo mawili; moja nataka kujua Jacob Matata yuko wapi na kwa nini amewaua walinzi wote wale. Pili, nataka kujua nani yuko nyuma ya haya mambo. Usipoweza kufanya haya mambo mawili ndani ya siku nne basi kama nilivyosema, nitamtangaza Jacob Matata kama haini alafu wewe utawekwa chini ya uchunguzi mkali. Nadhani unajua maana ya kuwekwa chini ya uchunguzi." Mhe. Jovin Sekendu alisema huku akikuna kichwa chake. Bi. Anita, mkuu wa kitengo Ofisi Fukuzi aliminya midomo yake kwa vidole bila kujibu neno. alijua kauli hiyo ya Mhe. Jovin Sekendu ilikuwa na ukubwa na ukali gani. Katika historia ya kazi yake amewahi kukutana na mikasa mingi sana mikubwa kwa midogo, lakini safari hii aliona kuwa hii ilikuwa na ugumu wake. Hawakuwa akipambana na gaidi au kundi la majambazi bali msaliti toka ndani ya mfumo wa usalama wa nchi. Yeye kama mkurugenzi wa Ofisi Fukuzi, alijiona kama mtu mwenye dhamana kubwa. Kwani sura iliyopo sasa ilikuwa wazi kuwa ujasusi au majasusi walikuwa kazini ili kuchanganya hali ya mambo.

Muda wote ambao Mhe. Jovin Sekendu alikuwa akiongea na Bi. Anita, Waziri Mkuu, Mhe. Silas Kiondo alikuwa kimya kabisa ndani ya chumba hicho, ambacho walikuwepo watu watatu tu. Ilikuwa inagonga saa nne kasoro dakika kumi na tisa asubuhi.

* * *

"Afuatiliwe, nataka kujua mienendo yote na mawasiliano ya Bi. Anita tangu sasa" Mhe. Jovin Sekendu alisema mara baada ya Bi. Anita kuondoka. Mhe. Silas Kiondo ambaye ndiye Waziri Mkuu (WM) alitingisha kichwa kuitikia. Halafu aliminya namba kadhaa kwenye simu yake kisha akaiweka simu sikioni.
"Nyoso, hakikisha unajua kila kitu kinachofanywa na huyo mama anayetoka hapo getini. Namba yake ya simu naituma sasa hivi kwenye simu yako. Sitaki ujue ni nani na hutoweza kujua ila nataka ujue anaongea na nani na ameenda wapi. Utanipa taarifa kila baada ya saa tatu. Usimguse wala kumfanya chochote." Mhe. Silas Kiondo alitoa maelezo kisha akakata simu.
"Utaratibu wetu uwe ni uleule, zaidi yako wewe na Nyoso sitaki mipango na mawasiliano yetu yaende kwa mtu mwingine zaidi. Waache wakuu wengine waendelee na taratibu zao kama taratibu za mamlaka na mipaka zinavyotaka!’’ Mhe. Jovin Sekendu alisema huku akijiweka vema kitini.

Itaendelea
 
- 15 -

Riwaya: Msako
Mtunzi: Japhet Nyang’oro

“Tukajua yeyote aliyefanya vile alifanya kusudi kupoteza ushahidi. Sasa kazi ni kumtafuta msichana aliyehusika, maana alama za vidole zinaonyesha mtu wa mwisho kushika bahasha ile alikuwa ni msichana.” Afisa huyo alimalizia maelezo yake.

“Kazi nzuri, nadhani tukubaliane kimsingi kuwa kazi iwe kuwatafuta watu watatu; Jacob Matata, Poka Kingu na huyu msichana Nanalungu. Lakini labda pia, ni vema nikawaambia kuwa kuna msichana mwingine aitwaye Jo Mwa ambaye kwa mujibu wa Polisi ndiye aliyehusika kusuka mpango wa kumtorosha Poka Kingu toka gereza maalum. Katika ripoti hii nimeambatisha ripoti niliyokuwa nimeipata toka kwa marehemu Inspekta Lucas Mwenda. Hivyo ni vema huyu naye tukamwingiza kwenye mchakato wa kumtafuta. Kazi hii nampatia Luteni Frank Misanya.” Alimaliza maelezo yake. Minong’ono ilisikika huku kila mmoja akijaribu kuuliza na kuongea jambo na jirani yake.

“Tutakutana hapa baada ya siku mbili kwa kikao kingine muda kama huu wa leo.” Mwenyekiti wa kikao alisema na kikao kikawa kimefungwa.


**************


"Kuna jambo haliko sawa hapa mheshimiwa." Bi Anita alisema huku akimwangalia Rais wa Nchi (RN) Mhe. Jovin Sekendu kwa macho ya maswali.
"Sijakuita kwenye hii ofisi ili uniambie kuwa kitu kiko sawa au hakiko sawa Mkurugenzi." Mhe. Jovin Sekendu alifoka huku akionyesha kuwa mwenye hamaki sana. "Ninachosema kama hujashirikiana na Jacob kufanya yale yaliyofanyika safe house usiku wa kuamkia leo basi inabidi uanze kuelewa kuwa Jacob Matata amekuwa msaliti wa nchi. Na ndani ya saa chache, kama nisipopata maelezo ya kutosha toka kwako, nitatoa amri ya Jacob Matata kusakwa kama haini." Rais wa Nchi (RN) Mhe. Jovin Sekendu alisema huku akijimiminia kinywaji kikali kwenye glasi. Macho yake yalikuwa mekundu huku akionekana kuwa mwenye kuchoka sana.
Bi. Anita hakusema lolote, alikuwa akimsikiliza Rais wa Nchi (RN) Mhe. Jovin Sekendu na kubaki na maswali mengi kichwani jinsi mambo yalivyokuwa yakienda kwa mwendo wa kuruka.
“Lakini iko wazi kuwa kidole cha Waziri Mkuu (WM) ndicho kimetumika kufungulia. Maana taarifa ya uchunguzi inasema kwenye kioo ambapo ndipo mfunguaji anatakiwa kuweka kidole, zimekutwa alama za kidole cha Waziri Mkuu.” Bi. Anita alisema
“Waziri Mkuu (WM) alikatwa kidole cha kushoto na pale wameona cha kushoto, ila kidole chenye uwezo wa kufungua mlango ni cha kulia.” Mhe. Jovin Sekendu alisema huku akiichukua ripoti ile ya tukio la kuvamiwa safe house na kuipekua tena.
“Ina maana wanataka kumhusisha tu Waziri Mkuu (WM) na tukio halafu ili iweje?’’ Bi. Anita alihoji.
“Wewe mkuu wa shirika la kijasusi ndo unaniuliza miye badala ya miye kukuuliza wewe!’’ Rais alisema.
“Lakini ukweli unabaki kuwa wazi kuwa, mlango lazima ufunguliwe na mmoja wetu sisi watu watano. Hivyo kama si Waziri Mkuu basi mmoja wetu ametumika kwa kujua au kutojua.” Bi. Anita alisema kwa sauti ya chini kisha akaongeza, “Waziri Sabodo Sumari mwili wake umekutwa ukiwa na vidole vyote japo ilikuwa mabaki ya mifupa iliyoungua moto. Mwili huo wa Sabpdp ulipatikana hata kabla ya tukio la safe house. Hii ina maana hakuna namna yeye amehusika. Mheshimiwa, naomba unipe muda wa kufikiri na kujua nini cha kufanya...."
"Muda nimeshakupa, ukasema unamwamini Jacob Matata anaweza kutupatia ufumbuzi wa jambo hili. Lakini matokeo yake, yeye ndiye kawaua walinzi wote safe house na kutoweka kiasi kuwa hata wewe mkuu wake wa kazi unaniambia hujui alipo....." Mhe. Jovin Sekendu alisema huku safari hii akiwa anamwangalia Bi. Anita kwa macho makali mekundu yaliyokuwa yamelemewa na uchovu, pombe kali, fadhaa, hasira na woga.
"Bado nahitaji Muda, hata kama si muda mwingi lakini bado nahitaji muda. Halafu nahitaji unisaidie jambo moja. Nahitaji kumtumia tena Jacob Matata. Bado namwamini!’’ Bi. Anita alisema kwa msisitizo.
"Tukubaliane mambo mawili; moja nataka kujua Jacob Matata yuko wapi na kwa nini amewaua walinzi wote wale. Pili, nataka kujua nani yuko nyuma ya haya mambo. Usipoweza kufanya haya mambo mawili ndani ya siku nne basi kama nilivyosema, nitamtangaza Jacob Matata kama haini alafu wewe utawekwa chini ya uchunguzi mkali. Nadhani unajua maana ya kuwekwa chini ya uchunguzi." Mhe. Jovin Sekendu alisema huku akikuna kichwa chake. Bi. Anita, mkuu wa kitengo Ofisi Fukuzi aliminya midomo yake kwa vidole bila kujibu neno. alijua kauli hiyo ya Mhe. Jovin Sekendu ilikuwa na ukubwa na ukali gani. Katika historia ya kazi yake amewahi kukutana na mikasa mingi sana mikubwa kwa midogo, lakini safari hii aliona kuwa hii ilikuwa na ugumu wake. Hawakuwa akipambana na gaidi au kundi la majambazi bali msaliti toka ndani ya mfumo wa usalama wa nchi. Yeye kama mkurugenzi wa Ofisi Fukuzi, alijiona kama mtu mwenye dhamana kubwa. Kwani sura iliyopo sasa ilikuwa wazi kuwa ujasusi au majasusi walikuwa kazini ili kuchanganya hali ya mambo.

Muda wote ambao Mhe. Jovin Sekendu alikuwa akiongea na Bi. Anita, Waziri Mkuu, Mhe. Silas Kiondo alikuwa kimya kabisa ndani ya chumba hicho, ambacho walikuwepo watu watatu tu. Ilikuwa inagonga saa nne kasoro dakika kumi na tisa asubuhi.

* * *

"Afuatiliwe, nataka kujua mienendo yote na mawasiliano ya Bi. Anita tangu sasa" Mhe. Jovin Sekendu alisema mara baada ya Bi. Anita kuondoka. Mhe. Silas Kiondo ambaye ndiye Waziri Mkuu (WM) alitingisha kichwa kuitikia. Halafu aliminya namba kadhaa kwenye simu yake kisha akaiweka simu sikioni.
"Nyoso, hakikisha unajua kila kitu kinachofanywa na huyo mama anayetoka hapo getini. Namba yake ya simu naituma sasa hivi kwenye simu yako. Sitaki ujue ni nani na hutoweza kujua ila nataka ujue anaongea na nani na ameenda wapi. Utanipa taarifa kila baada ya saa tatu. Usimguse wala kumfanya chochote." Mhe. Silas Kiondo alitoa maelezo kisha akakata simu.
"Utaratibu wetu uwe ni uleule, zaidi yako wewe na Nyoso sitaki mipango na mawasiliano yetu yaende kwa mtu mwingine zaidi. Waache wakuu wengine waendelee na taratibu zao kama taratibu za mamlaka na mipaka zinavyotaka!’’ Mhe. Jovin Sekendu alisema huku akijiweka vema kitini.

Itaendelea
shukrani mkuu
 
RIWAYA: MSAKO WA MWEHU
MTUNZI: Badi .M. Bao
MWASILIANO. 0625920847, ( whatsap )
E- mail: badi.bao11@gmail.com
Dar es Salaam

SEHEMU YA KWANZA


SURA YA KWANZA


Idara ya magonjwa ya akili, Hospitali ya Taifa Muhimbili
Gangaganga ya mganga humwacha mgonjwa na matumaini, jitihada ya kutatua tatizo humpa mwenye tatizo tumaini. Bi Mwantumu Haji alikuwa amepatwa na maswahibu ya ulimwengu. Tatizo lililompata alijiona kama kaibeba dunia nzima mgongoni mwake. Ilikuwa ni majira ya saa tatu za asubuhi tulivu, iliyopambwa na mwangaza usioumiza wa jua ambalo lilikuwa tayari limeshachomoza upande wake wa mashariki, Bibi huyo alikuwa amekaa kwenye kiti na baadhi ya watu wengine akisubiria kuingia kwenye chumba cha daktari kilichopo kwenye bloku la hospitali ya Muhimbili, idara ya magonjwa ya akili.

Uso wake tu ukimuangalia ulionyesha ana jambo limemsibu, kwani daima dumu barua ya moyo husomwa juu ya panda la uso la mtu. Mtu akiwa na hali ya furaha au huzuni yote husomeka kwenye uso wake. Alikuwa amewasili katika hospitali ya taifa ya Muhimbili tokea muda wa jogoo la kwanza kuwika akimleta mtoto wake wa kiume anayeitwa "Masoud Masoud" maarufu kwa jina la Maso Maso” aliyerukwa na akili usiku huo wa manane uliopita.

Naam "Maso Maso" sasa kawa kichaa, mwehu, mwendawazimu, majinuni, akili zake zimetadathali, vyovyote utakavyopenda kutamka, lakini "Maso Maso" sasa akili zake ni maji kupwa na maji kujaa. Mgonjwa huyo alilazwa katika wodi ya wagonjwa wa afya ya akili katika Hospitali Taifa ya Muhimbili.

Mara ikasikika sauti toka kwenye kipaza sauti cha mhudumu wa zamu, mgonjwa mwenye kadi namba 10 aelekee kwa daktari chumba namba 02. Lilikuwa ni tangazo lililoleta faraja kwenye moyo wa Bi Mwantumu hasa ukichukulia yupo hapo hospitalini kwa zaidi ya saa sita tokea saa tisa za usiku na sasa saa tatu na dakika saba za asubuhi ndio anapata nafasi ya dhahabu aliyokuwa anaisubiria kwa hamu ya kuonana na daktari.

Bila simile, Bi. Mwantumu na uzee wake wa miaka 65 akajinyanyua kwa tabu pale kitini pake alipokuwa amejipweteka na kuingia kwenye chumba cha daktari bingwa wa Afya na Magonjwa ya Akili wa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Alipokelewa kwa uso wa bashasha na tabasamu toka kwa Dokta "Alshad Mpenumbe". Alikuwa ni daktari wa hospitali hiyo mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 20 sasa, na umri wake alikuwa ndio anaingia kwenye rika la uzee wa makamo, wa miaka 55.

Karibu sana mama yangu, na pole na matatizo yalikuwa ni makaribisho ya Dokta Mpenumbe kwa Bi Mwantumu. Ahsante mwanangu nimeshapoa, matatizo tumeumbiwa wanadamu hatuna budi kuyapokea na kuyakabili kwa subira na stahamala kubwa alijibu kwa unyenyekevu Bi Mwantumu huku akijiweka vizuri kitini. Samahani naomba hiyo kadi yako alisema Dokta Mpenumbe. Bi Mwantumu akajibu kwa vitendo kwa kunyoosha mkono wake wa kulia kuikabidhi kadi kwa daktari apate kuisoma.

Ukapita muda kama wa rakaateni, muda ambao Dokta Mpenumbe alikuwa ametingwa na kuandika andika kwenye kompyuta yake ya mezani kisha, akamaliza akavua miwani yake akaiweka pembezoni mwa kompyuta yake, akaitoa hanchifu yake nyeupe kutoka kwenye koti lake jeupe alilovaa, akajifuta kwenye macho akajikohoza kidogo kulisafisha koo lake na kuanza mazungumzo na Bi Mwantumu.

Daktari: “Eheemwanao Masoud hili tatizo lake la akili limemuanza lini"?. Lilikuwa ni swali lililovunja ukimya uliopita baina yao kwa dakika kadhaa.

Bi Mwantumu: "Jana kuanzia saa mbili usiku alikuwa anazungumza mambo mchafukoge mara anasema kuna watu wapo nje ya nyumba wamekuja kumchukua. Wakati mwingine anasema amepigiwa simu na Rais kuwa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa. Ila ilipofika saa sita usiku, ndio akaanza kufanya fujo na kuvunja vitu vya ndani anataka tumruhusu atoke nje ya nyumba."

Daktari: "Kwenye ukoo wenu au familia yenu ameshawahi kutokea mgonjwa wa afya ya akili"? Bi Mwantumu: "Billahi wa Rasuli hakuna mtu huyo kwenye ukoo wetu, sio upande wangu wala upande wa marehemu mume wangu." alitoa kiapo kwa kutumia kidole chake cha shahada kukwangua juu ya koo lake kuweka msisitizo wa maneno yake.

Daktari: "Mwanao, ni Mwanachuo au Muajiriwa?"
Bi Mwantumu: "Mwanangu amemaliza Chuo mwaka juzi, Shahada ya Uhandisi huko nchini Uingereza, na mwaka huo huo akapata kismati cha kazi nchini Saudi-Arabia, lakini akaacha ghafla kazi, sasa ana miezi kama 6 yupo tu nyumbani, na wala hajatuambia kilichomsibu huko alipokuwa mpaka akaacha kazi."

Daktari: "Je mwanao, ni mtu wa kujichanganya na marafiki na je ameoa au kuwa na rafiki wa kike?"
Bi Mwantumu: "Zamani kabla hajasafiri kwenda masomoni Uingereza alikuwa mtu wa watu, mpenda marafiki. Nyumbani kwangu walikuwa hawakauki marafiki zake kama maji ya kisima, lakini tokea arejee masomoni akawa ni mtu wa kujitenga tu, hana marafiki na hata sijawahi kusikia wala kumuona yupo na rafiki wa kike tokea amebaleghe. Na nimemzaa akiwa ni mzima wa afya jogoo linapanda mtungi"

Daktari: (Akatabasamu kwa jibu la Bi Mwantumu akifurahishwa na msisitizo aliouonyesha kuthibitisha mtoto wake sio hanithi). "Sasa mama yangu, vipimo vya maabara vimerudi, mtoto wako hana malaria wala ugonjwa wowote ule. Maana mwanzoni nilihisi huenda malaria yamepanda kichwani, lakini hana malaria. Kutokana na maelezo yako, mtoto wako ana ugonjwa wa akili kitaalamu tunauita Schizophrenia. Huu ni miongoni mwa magonjwa makubwa ya akili. Jina hilo limetoholewa kutoka katika lugha ya Kilatini ambayo ni maneno mawili "Schizo" na "Phrenia". Mgonjwa anayeugua ugonjwa huo anakosa muunganiko kati yake na akili yake", akaweka kituo kidogo cha maelezo yake Dokta Mpenumbe kwa kumeza mate kisha akaendelea kuelezea.

"Kwa kawaida binadamu huwa na hisia tano muhimu, ambazo ni za kuona, kugusa, kuonja, kusikia na kunusa. Mtu aliyechanganyikiwa kutokana na ugonjwa huu anaweza kuona, kuhisi, kunusa, kugusa au kusikia vitu ambavyo wengine hawaoni, kuhisi wala kusikia. Mgonjwa anaweza kusema anaona simba anapita eneo ambalo mmekaa naye, lakini nyie msimuone au anasikia sauti na watu wanazungumza habari zake, wanamshurutisha au wanamtisha lakini nyie hamuoni wala hamsikii chochote". Machozi yalikuwa yanamchuruzika churururu bila kikomo Bi Mwantumu pindi alipokuwa anasikiliza maelezo ya daktari kwa umakini mkubwa.

Bi Mwantumu: "Sasa kitinda mimba wangu kweli atapona daktari"? Nieleze ukweli usinifiche kitu kabisa" alikatisha mazungumzo ya daktari kwa kuuliza swali kisha akaanza kutoa kilio cha sauti ya uchungu.
Daktari: "Mama, huwa tunatumia njia tatu kuwatibu wagonjwa wa akili ambazo ni za kibaiolojia, kisaikolojia na kijamii. Hivyo shaka ondoa mama yangu"

Bi Mwantumu: "Nashukuru sana Daktari, Mwenyezi Mungu akubariki na kukupa afya uendelee kutupa huduma wahitaji".
Daktari: "Sawa, mama yangu, tutajuzana kinachoendelea. Tutamlaza kwa siku kadhaa ili tuzidi kuangalia maendeleo yake".

Bi Mwatumu akanyanyuka na kutoka nje ya ofisi ya Daktari. Akaelekea kwa keshia kwenda kufuatilia bili yake ya matibabu ya mwana wake ili apate kufanya malipo.
[emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji737]

"Mimi ndio "Maso Maso" msela toka Sinza kwa wajanja. Nyie Watanzania maboya tu, unakuta Mbunge anakuhonga buku tano umpigie kura, halafu unamchagua kwa miaka mitano, maana yake kila mwaka mmoja amekununua kwa buku". Ha..... Ha.....Ha.....Ha.......mazwazwa sana nyie watu tembeeni duniani mfunguke akili. Kutwa mnashindia "chips-dume" na maji, maziwa kwa watoto wenu hawanywi mpaka wanywe sumu, tokea wakiwa shule ya vidudu akili za kugundua ndege na magari kama wazungu mtapata wapi sasa, wakati watoto wa wenzenu Ulaya wanashiba baga kwa maziwa. Viongozi wenu nao ni janga la kitaifa, watoto wao wanawasomesha shule za kuzungumza "Yes... Yes.. Mzungu kala mafenesi" mpaka anamaliza chuo kikuu huko Ulaya mtoto kagharimu milioni mia tatu.

Afu anarudi 'Bongoland' kugombania ajira na watoto wa akina yahe waliosoma shule za kata. Ambao gharama zao mpaka chuo kikuu haifiki hata milioni moja. Hizo akili au matope!. Ukiwekeza kwa mtoto wako milioni mia tatu, basi muandalie mazingira ya kuja kuendeleza kampuni zako za mabilioni na sio kuja kuajiriwa kwa kamshahara cha laki nne na watoto wa walalahoi". Ha.... ha.... ha... ha.... sogeeni hapa mpate elimu kitaa bure, mupate rai tumbitumbi zenye mafundisho.

Wakulima wenu nao majanga tupu, shamba lake, mbegu za kwake, kupanda, palizi zote kwa gharama zake lakini akivuna mazao yake, serikali inaanza kumpangia sijui Ooh...usiuze nje ya nchi, huo ni unyonyaji mbona Wafanyabiashara hamuwazuii kuuza bidhaa zao nje ya nchi, mbona watumishi wa umma hamuwapangii matumizi ya ndururu zao za mwezi!.

Ningekuwa Rais wa nchi wagonjwa nyie mngekula bata tu, sio viporo mnavyoletewa na ndugu zenu. Dripu zingekuwa za juisi na sio za maji kwani nyie mmekuwa samaki... Ha...Ha..Ha....Ha....! "

Wakati Masoud anaendelea kubwabwaja mbovu, akasikika nesi mmoja anamuongelesha mwenzake, "Huyo ndio Masoud bana akianza kumwaga sera hapo ni usiku kucha mtakesha nae na kuna wakati anaongea vitu vya msingi hata sisi wenye akili timamu hatuwezi kuviwaza".

"Afu nasikia kasomea Uingereza ana Shahada ya Uhandisi, labda karogwa maana familia zetu za kiswahili nazo ni shida, wana roho ya tukose wote. Wanapenda wote tufanane hali zetu za maisha, wote tuwe wali deni mchuzi karadha. Babu dobi, Baba muuza kahawa, Mjomba fundi seremala, Shangazi kazi yake mchambaji kwenye "kitchen party", Mama mchoma vitumbua, hivyo ndivyo wanavyotaka. Akitokea mmoja tu anataka kujifanya msomi msomi wataanza kumpiga tunguri mpaka atakoma", nesi mwenzake nae alichangia kusherehesha mazungumzo yao.

"Madame Neesi eeh....Madame Neeesi....!, Nataka kwenda chooni kujisaidia, au nijisaidie hapa hapa wodini, mie sioni noma fumbeni macho tu nimtoe nyoka pangoni hadharani" ilikuwa ni sauti ya Masoud, alikatiza mazungumzo yao waliyokuwa wanateta wale manesi mawili.

"Aaaah.... hapana rafiki yangu Masoud usifanye hivyo, nenda chooni bana, tena leo simuiti mlinzi akusindikize nenda mwenyewe na urudi haraka rafiki" alisema nesi yule akimrai Masoud asijisaidie ndani ya wodi hiyo ya wagonjwa akili. Masoud alikuwa tayari ameanza kufungua mkanda wa suruali yake akitishia kujisaidia tayari.

Masoud akaondoka zake wodini kuelekea chooni kwa mwendo wa chapuchapu. Muda ulikuwa ni saa nne za usiku. Hiyo ndio ikawa ni kwaheri ya kuonana, kama vile kawapa mkono wa buriani, hawakumuona tena. Kwa ufupi Masoud alikuwa ametorokea mtaani kusikojulikana, alichoka maisha ya kufungiwa wodini kama ndege tunduni.

[emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji737]

ITAENDELEA

MSAKO%20WA%20MWEHU%20BOOK%20MOCKUP.jpg
IMG-20200601-WA0044.jpg
 
RIWAYA: MSAKO WA MWEHU
MTUNZI: Badi .M. Bao
MWASILIANO. 0625920847, ( whatsap )
E- mail: badi.bao11@gmail.com
Dar es Salaam

SEHEMU YA PILI

️[emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji737]
Masoud Masoud au "Maso Maso Mwehu" kama alivyojipachika mwenyewe, aliacha mambo wodini hamkani si shwari kwa kutoroka kwake. Alipoingia chooni alijifungia mlango kwa ndani na kupapachua dirisha dogo la kioo lililopo chooni kisha akavunja nondo zake.
Nesi wa zamu alisubiria arudi, akawa anaona amechelewa. "Huyu amezidiwa ugonjwa huko chooni au amejiua?" ni swali alilokuwa anajiuliza nesi huyo aliyetoa ruksa kwa hofu.
Ndipo alipotoa taarifa kwa walinzi wakaja kuvunja mlango wa chooni ndipo walipokuta kidirisha kimechomolewa. Kila mtu alishangaa na kustaajabishwa na namna alivyopenya dirishani baada ya kufanikiwa kukata vyuma vya dirishani.
"Huyu atakuwa na nguvu za ajabu sana mithili ya Samson wa kwenye Biblia, haiwezekani kwa kutumia mikono na vidole uweze kupindisha vyuma vya dirisha na kufanikiwa kutoroka" aliropoka mlinzi mmoja wapo akiwa ameshikwa na butwaa haamini kama binadamu wa kawaida anaweza kupachua dirisha lile madhubuti kwa kutumia mikono tu bila kifaa chochote.
Daktari wake anayemtibu alivyopita kuzungukia wagonjwa wake asubuhi na mapema ndio akakuta kaachiwa manyoya tu kitandani kwa Masoud. "Utaratibu upo wazi kabisa kuwa lazima asindikizwe popote anapokwenda, sasa ulishindwa nini kumpa taarifa mlinzi amsindikize chooni?" Dokta Mpenumbe alikuwa anaongea kwa hamaki huku anafoka.
Yule nesi wa watu masikini ya Mungu akawa hana cha kujitetea wala pakushikilia, amejiinamia kama zoba ulikuwa ni uzembe wake kazini.
"Sasa naomba uniandikie barua ya maelezo ya utetezi kwanini nisikufikishe kwenye vikao vya nidhamu uchukuliwe hatua haraka sana, kukomesha tabia hii mbaya iliyomea ya uzembe kazini" Daktari alitoa maagizo kwa nesi yule wa zamu, ambaye alionekana amegwaya na anajuta kwa uzembe wake lakini majuto daima ni mjukuu na maji yakishamwagika hayazoleki tena. Nesi yule alitamani muda urudi nyuma aweze kurekebisha kosa lake alilolifanya lakini alikuwa ameshachelewa, "Maso Maso" mwehu kashatimka zake mtaani.
Bi Mwantumu alijihimu alfajiri na mapema jogoo la pili akiwa ameambatana bega kwa bega na shoga yake Bi Mwazani wakiwa na kapu lao kubwa ndani yake kuna chupa yao kubwa ya chai ya maziwa na mapochopocho, michapalo kedekede kwa ajili ya mgonjwa. Wakiwa hawajui yaliyompata mtoto wao hospitalini usiku wa kuamkia leo yao. Walipofika nao wakakutana na taarifa za kutoweka kwa mtoto wao Masoud.
Bi Mwantumu alikuwa hashikiki kwa kilio cha kwikwi, "mwanangu eeeeeh.......Masooo mwanangu unateseka babaaaa...upo wapi babaaa eeeeeeh...unakula nini huko ulipo.... umelala wapi sasa mwanangu,..... nguo za kuvaa utapata wapi woooohi woooooohi.... uchungu mama tumbo la uzazi uchungu mamaaaaaa... Wooooh" kilio mtindo mmoja kama vile yupo msibani.
"Shoga nilikuambia hukunisikiza ukayataka matibabu ya kizungu, huyu katupiwa jini tu, tungewahi kwa mtaalamu sasa angekuwa mzima wa afya. Jisaidie Mungu akusaidie, mambo yenu ya kudharau mila zilizotulea ndio matokeo yake haya. Kiatu cha mtoto hakimponyi mama mbigili. Njia unazotumia kumponya mtoto wako haziendani na uhalisia shoga yangu, ulikuwa ni ushauri wa Bi Mwazani kwa shoga yake, huku akiongea kwa hisia kali na uchungu mkubwa.
"Shoga nimekuelewa sasa ama zao au ama zangu, wabaya wangu wamenibipu sasa mimi nina wapigia simu wakae mkao wa mapambano", tusiombane poo tu" Bi Mwantumu alijibu, majibu ya kukubaliana na ushauri wa shoga yake wa kufa na kuzikana, tokea utotoni na unyago wamechezwa na kungwi mmoja, huko kijijini kwao Utete, Rufiji.
Bi Mwantumu na rafiki yake waliondoka zao kurejea nyumbani kwao, baada ya kupewa taarifa na daktari kuwa juhudi zote za kumsaka mwehu "Maso Maso" kila kona zimegonga mwamba. "Mama tunasikitika kukutaarifu kuwa tumeshindwa kumpata, unaweza kwenda polisi upate msaada wa kumsaka mwanao Masoud" yalikuwa ni maneno yake kuaga ya Dokta Mpenumbe kwa Bi. Mwantumu.
[emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji737]
Shekhe Abeid Mbonde alikuwa maarufu Rufiji nzima na vitongoji vyake kutokana na kazi ya upigaji ramli. Alikuwa anaishi kijiji cha Mkongo kilichopo kama makadirio ya umbali wa kilometa 4 kutoka mto Rufiji. Zamani kijiji hicho ndio ulikuwa Mji mkubwa wa Wilaya ya Rufiji. Kijiji hiki umaarufu wake unatokana na kuwa ndipo yalipo Makao Makuu ya Mamlaka ya Maendeleo ya Bonde la Mto Rufiji "Rufiji Basin Development Authority" (RUBADA).
Shekhe Mbonde kazi yake ya kupiga ramli au kusaga mkungu hiyo ndio kazi ambayo ilimpatia umaarufu mkubwa mpaka watu walifunga safari toka pande mbalimbali za dunia kuja kupata huduma yake. Umri wake sasa alikuwa ni shaibu wa miaka 80 na ushee. Alikuwa anaogopwa haswa ikisemekana anafuga Majini anaowatumia kwenye kazi zake za uganga.
Bi Mwantumu na shoga yake Bi Mwazani asubuhi ya saa nne iliwakuta wamekaa kwenye jamvi wakisubiria huduma ya Shekhe Mbonde. Walirauka alfajiri na mapema na basi linaloelekea Rufiji wakipandia Mbagala kuu. Bi Mwazani alijifunga kibwebwe kuhakikisha mtoto wa rafiki yake anayesakwa kwa hali na mali anarudi katika uzima wa afya yake ya akili.
Hawakupata tabu sana kufika nyumbani kwa Shekhe kwa sababu nao pia kwa asili ni Wandengereko walikuwa wanasikia sifa za Shekhe Mbonde tokea wakiwa wanawali wabichi kabisa. Walipofika walikuta kadamnasi ya watu wamejazana kwenye msambweni wa nyumba ya mtaalamu huyo.
"Shosti hapa kwa Shekhe Mbonde ndio Kigoma mwisho wa reli, kuwa na matumaini mwanetu Masoud amepatikana na amepona tayari ondoa mashaka atafanyiwa ruzuna atakuwa mzima wa afya" Bi Mwazani alivunja ukimya kwa kuanzisha mazungumzo kwa shoga yake. "Nashukuru sana shoga ama kweli akufaaye kwa dhiki ndio rafiki wa kweli, wengi wa marafiki ni mafarisayo ila wanajifanya wema machoni pa watu" alitoa shukrani za dhati Bi Mwantumu kwa shoga yake huku akiwapiga kijembe marafiki zake wengine
"Kikulacho kinguoni mwako, wapo majirani zetu hata kukujulia hali kwa matatizo haya uliyopata hawajaja, pengine ni wahusika wanaona haya kukuangalia usoni" Bi Mwazani alizidi kuchochea kuni za fitina kwa majirani wenzake ili yeye aonekane peke yake ndio mwema.
"Leo ndio fainali, hapa mganga akipiga bao akanionyesha fulani ndio mbaya wangu, sitosikia la mwadhini wala la mteka maji msikitini, tutagawana majengo ya serikali nakwambia mimi naenda Segerea yeye anaenda mochwari Muhimbili." alipandisha mzuka wa hasira Bi Mwantumu.
"Haya haya aliyebakia bado kutanguliza kishauzu cha Shekhe afanye haraka kabla hajafungua kazi" ilisikika sauti ya msaidizi wa mganga. Msaidizi huyo alikuwa anapigia debe advansi anayolipwa mganga kama sadaka, unatoa yoyote ile unayoguswa nayo.
Bi Mwantumu akatumbukiza elfu hamsini taslimu kwenye kapu la mganga lilipopitishwa usoni pake. Akabaki anasubiria kwa hamu zamu yake ifike aingie kwenye kilinge cha mganga akatapike yanayomsibu.
[emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji737]
"Woooooh...wooooooh........woooooh....paachiiithhhh... chi...chi.... chi..... paraka parakata paaaah... pepo mchafu mama mwanao ametupiwa, amepatwa na shonga, amekuwa kichaa kweli si kweli? " aliulizwa Bi Mwantumu akiwa amekaa juu ya kinu cha Shekhe Mbonde aliyekuwa amekaa kwenye jamvi akizungumza maneno ya kurogonya baada ya kupandisha ruhani wake kichwani.
"Tawile mganga tawile" alijibu Bi Mwantumu huku anahema juu juu kwa huku fundo la hasira limejikusanya kooni kwake kwa wabaya wake. "Kapotelea mtaani hajulikani alipo sawa sawa mama?" aliendelea kuuliza ramli yake Shekhe Mbonde. "Tawile Shekhe tawile nimewakosea nini hawa walimwengu mimi jamani, unalala nao, unakula nao lakini kumbe ni wabaya wako" akawa analalamika Bi Mwantumu kwa sauti ya juu huku anamwaga mchozi wa nguvu.
"Usilie mama, hapa ndio mwisho wa matatizo umefika, wabaya wako mwisho wao umefika, ukisikia mwana wa Mbonde fimbo ya chuma kwa wachawi ndio mimi, viongozi wengi wa serikali mimi ndio kamati yao ya ufundi, ndio nawapangia nini cha kuvaa na siku gani, ndio nawapangia hotuba za kuzungumza mbele ya kadamnasi ya watu ha.... ha... ha... ha...." aliongea kwa sauti ya kujigamba huku anachezea tasbihi mkononi mwake. Shekhe Abeid Mbonde alikuwa tayari ameshamuingiza kwenye kumi na nane zake Bi Mwantumu hachomoki tena.
"Sasa chukua kipande cha kanga hiki, na hii sarafu ya Mjerumani uishike mkononi. Uende msalani kuoga, ukishaoga tu usijifute maji uivae mara moja hiyo kanga kisha uikumbate hiyo sarafu uanze kunuiza unayotaka kwa wabaya wako na kwa mema unayotaka kwa mtoto wako". Bi Mwantumu akawa ananyanyuka kwenye kinu na kuelekea bafuni, huku Shekhe Mbonde jicho limemsimama dede kukodolea mirindimo ya makalio ya Bi Mwantumu yanavyotikisika alikuwa amevalia vazi teketeke la dela.
Waswahili wanasema huba mwanzowe jicho, Shekhe moyo ulikuwa unamwenda mbio kama ametumia Mkuyati wa kuongeza nguvu za kiume au amekunywa kikombe cha Alkasusu.
"Afanalek! Mwenyezi Mungu ni fundi wa kuumba mashallah.....fatabaaraka llahu ahsanul-khaaliqiina" alijikuta Shekhe Mbonde anaropoka bila kujijua kusifia uumbaji kwa kutumia maneno ya kiarabu. Tayari alishachanganywa na umbo sotojo sotojo, laini laini la Bi Mwantumu ambaye licha ya umri wake kumtupa mkono wa miaka 65 lakini bado alikuwa ana mvuto.
Kwanini asiwe na mvuto wakati hajawahi kufanya kazi ngumu maishani mwake zaidi ya kuwa ndani kukatakata vitunguu na nyanya za kumpikia biriani na pilau marehemu mumewe ambaye alikuwa ni Mfanyabiashara mwenye pesa sufufu Jijini Dar es Salaam. Baada ya dakika kama 10 kupita, Bi Mwantumu akawa anarejea kutoka msalani huku akiwa amejifunga upande wa kanga kuu kuu iliyo nyepesi.
Ilikuwa imemgandia mwilini kanga hiyo vilivyo ikilichora umbo lake nene, akitembea huku nyonga zake zikijionyesha namna zilivyoumuka kama mikate iliyosusiwa hamira na mpishi.
Mganga Shekhe Mbonde udhaifu wake mkubwa ulikuwa wanawake vibonge, tipwatipwa, wenye miili laini. Wakeze wote kwenye ndoa yake ya mitara aliowafanyia nikaha ukiwaangalia nyuma wamejazia msondo wa nguvu. Hajawahi kuoa tokea ujanani mwake mpaka uzeeni, mwanamke kimbaumbau mwiko wa pilau.
Na wote aliwapata kupitia kazi yake ya uaguzi, "kuku hula sawa na mdomo wake", hivyo wateja wake wanawake ndio walikuwa mboga yake rahisi kuwinda. Tayari Bi Mwantumu alishajiingiza kwenye rada za Shekhe Mbonde ilikuwa ngumu kwake kuchomoka.
ITAENDELEA
 
RIWAYA: MSAKO WA MWEHU
MTUNZI: Badi .M. Bao
MWASILIANO. 0625920847, ( whatsap )
E- mail: badi.bao11@gmail.com
Dar es Salaam

SEHEMU YA NNE

"Wewe mimi sio wa nchi hii, hata Trump Rais wa Marekani atanipigia saluti, hata nyinyi bendera hufuata upepo mtaniimba sana tu tena huku mnalia, nitakuwa maarufu kwenye kila kinywa cha Mtanzania, jiandae tu kunipigia kura kwa hiari au kwa lazima" alijibu "Maso Maso" huku anashushia tumboni mwake mtindi uliochanganywa na soda.
" Unaambiwa yule Inspekta wa polisi anamheshimu sana "Maso Maso", ile gari aliyopanda "v8" wakati imefika ndio ina wiki tu ilipata hitilafu, mafundi wa jeshi la polisi wote walichemka. Ndio mwishoni wakamkumbuka "Maso" kuwa anajua ufundi magari. Walimfata hapa, aliwaletea madahiro kweli kweli maana baadhi ya polisi walikuwa na tabia ya kumpiga piga wakimuona hapa getini. Huyu Bosi wao aliyempa elfu kumi alimbembeleza mpaka akakubali ndani ya dakika 5 tu gari ikawaka na kupona kabisa. Tokea hapo wanamuacha afanye anavyotaka, siku akiamka vizuri anaweza kuingia mpaka kule karakana yao akawasaidia kutengeneza magari. Na siku kichaa chake kikimpanda atamwaga matusi, hamna anayeweza kumsogelea," alieleza fundi Peter tukio la ukaribu wa "Maso Maso" na kigogo wa polisi.
Soga za hapa na pale zikaendelea ili mradi siku imalizike kwa usalama. Mpaka jua likazama, hayo ndio yalikuwa maisha mapya ya Masoud Masoud, maisha ya kuwa punguwani wa akili asiyejua kesho yake itakuchaje, asiye na uhakika wa kula yake wala afya yake. Analala vibarazani, mbu wake, baridi yake. Wapo waliomsikitikia kwa tatizo lililompata na wapo waliompuuza na kumbeza kuwa kayataka mwenyewe kutembea na mke wa mtu, wakatoa hukumu bila kufahamu chanzo chake ni nini!.
[emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji737]
Kikao kizito ofisini kwa Inspekta Haroub
Ofisini kwa Inspekta Haroub Farouq, mmoja wa vigogo wa Jeshi la Polisi kulikuwa na kikao kizito kinachoendelea baina ya maafisa wa ngazi za juu wa Polisi Makao Makuu na wale wa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani na Ustawi wa Nchi. Ni kama kikao cha baba na mtoto kwa sababu hawa wote walikuwa ofisi zao zipo pua na mdomo na wanatumia geti moja na majukumu yao ya kikazi yanashabihiana. "Nimewaiteni kikao hiki kifupi cha kabla ya kuanza kazi, ili kukumbushana majukumu yetu mazito yalioyopo mbele yetu. Kama mnavyofahamu tunatarajia kupata ugeni mzito wa Mabalozi wawili toka Marekani na Canada." Akapumzika kidogo mazungumzo yake na kumeza mate kisha akaendelea. "Wanakuja kutukabidhi msaada wao wa vifaa walivyotoa kwa Jeshi la Polisi. Vifaa hivyo ni magari ya doria idadi yake 50, pamoja na kompyuta zaidi ya 1000. Ni msaada ambao umetufikia katika wakati muafaka hasa ukichukulia bado vituo vyetu vya Polisi Tanzania nzima tunaandaa mashauri ya watuhumiwa kwa kutumia mtindo wa karne za ujima wa peni na daftari.
Pia tuna uhaba mkubwa wa magari ya kufanya doria hasa nyakati za usiku. Huko nje ya Miji, majambazi yanajitawanya kwa mapana na marefu. Sio jambo zuri kwa Jeshi la Polisi, ni dalili ya kuwa tumeshindwa kwa kila njia na jiha kudhibiti uhalifu nchini Tanzania. Sasa anapotokea mhisani wa kutupa magari 50 ni jambo la kupongezwa sana.
Sasa maandalizi ya mkutano huo wa makabidhiano yapambe moto, kila mwenye jukumu lake alitekeleze kwa ufanisi mkubwa. Habari nilizopata ni kuwa mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Ustawi wa Nchi Mheshimiwa "Ngaiza Jacob Ngaiza", na pia baadhi ya vigogo wa serikali watahudhuria hafla hiyo wakiwemo Wabunge wetu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tengenezeni naizesheni yenu vizuri kabisa kila kitu kiende kama tulivyopanga. Uzembe wowote utakaosababisha aibu na izara mbele ya wageni wetu, tutahesabu ni uzembe kazini na unaweza kukupelekea kufukuzwa kazi, hivyo tekelezeni wajibu wenu, kumbukeni cheo ni dhamana, ahsanteni sana" akawa Inspekta Haroub ameshafunga kikao kifupi cha kulishana yamini ya utendaji kazi uliotukuka.
Kila Afisa akawa anatawanyikia ofisini kwako kichwa chini kwenda kujipanga vyema kutimiza majukumu yake. "Koplo Michael njoo hapa" ulikuwa ni wito wa Inspekta Haroub kwa fundi mkuu wa karakana ya Jeshi la Polisi. "Naam afande" aliitikia wito huku akigeuka na kupiga saluti maana tayari alishakishika na kunyonga kitasa cha mlango wakutokea. Ikabidi akiache kitasa na kupiga hatua mbili tatu za kurejea karibu na Bosi wake.
"Uzembe kama wa kipindi kile cha kushindwa kutengeneza v8 sitaki ujirudie tena mpaka anakuja kukusaidieni kichaa nyie wenye akili timamu mnaolipwa mishahara na posho mpo mpo tu mnapigwa ubwete! "alizungumza kwa kufoka Inspekta. "Samahani Afande kosa halitojirudia tena" alijibu Koplo Michael kwa unyenyekevu akiwa amekakamaa hatikisiki. "Kama mtamhitaji yule mwehu "Maso Maso" tena mie namuweza sana yule atakusaidieni hasa ukichukulia baadhi ya magari yamekaa bandarini muda mrefu na yatajaribiwa pale kama yanafanya kazi, sasa inaweza kuja aibu ya mwaka, au unasemaje"? aliuliza swali la mtego Inspekta Haroub.
"Itakuwa vizuri sana, unajua sasa pale karakana wenzetu wawili wapo likizo na mmoja amefiwa na mzazi wake sasa, ukaguzi wa magari yote ni shughuli pevu bora "Maso Maso" aje tu kama utamdhibiti asilete Ukichaa wake" akajibu Koplo Michael ili kumridhisha Bosi wake asije kukataa msaada likazuka la kuzuka akatimuliwa kazi.
"Haya niachie mimi hilo jukumu kesho tu utamuona karakana" akajibu Inspekta Haroub, wakaagana akaendelea na majukumu yake mengine.
[emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji737]
SURA YA TATU
Hafla ya makabidhiano ya vifaa kwa Jeshi la Polisi
Ilikuwa ni siku ya Ijumaa majira ya kuanzia saa nane mchana jua lilikuwa bado linatoa miale yake yenye kuchoma mwili, kadamnasi ya watu ilikuwa imekusanyika mbele ya jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani. Kulikuwa na hafla kubwa ya makabidhiano ya vifaa vya kazi vikiwemo magari na kompyuta kwa Jeshi la Polisi. Vifaa hivyo vilikuwa ni msaada kutoka nchi ya Marekani na Canada kwa ajili ya kuboresha utendaji wa jeshi hilo.
Bendi ya Jeshi la Polisi ilikuwa inatumbuiza nyimbo yao mpya ya kusifia ushirikiano mwema wa kidugu baina ya Tanzania na Marekani. Bendi hii ya "Polisi Jazz Band" ni moja ya bendi kongwe nchini iliyozoeleka miaka ya 70's-80's kwa mtindo wao wa "vangavanga". Pia wakaanza kuimba nyimbo zao zilipendwa kama "Naamua kurudi kijijini","Halima" na "Baba yupo wapi" nyimbo ambazo zilisuuza roho za watu wazima waliohudhuria ambao walikuwa wanakumbushwa enzi wapo vijana. Ilimradi hafla nzima ilikuwa imefana sana kila mtu alikuwa ana furaha sheshe.
Ilipofika saa kumi alasiri, shangwe, hoihoi, nderemo na vigeregere vikaibuka kisha watu wakatulia vitini raha mustarehe kama Sultan bin Jerehe. Nderemo hizo zilikuwa ni kuashiria kuwasili kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mheshimiwa Ngaiza Jacob Ngaiza akiwa ameambatana sambamba na wageni wake watukufu Mabalozi wa Marekani na Canada. Wakakaribishwa meza kuu huku viongozi wengine wa chama na serikali wakiwa wameshachukua viti vyao. Zikaanza hotuba mbalimbali za wageni hao wakiwa wameambatana na Maofisa wao wa kutoka Ubalozini. Kisha ukafika wakati adhimu wa kukabidhiana vifaa hivyo. Wakaitwa mbele ya kadamnasi wageni wa heshima wote wakasogelea yale magari na kompyuta. Wakaanza kuzungukwa na wanahabari kwa ajili ya kuchukuliwa picha na video za kutosha kwa ajili ya vyombo vyao vya habari.
Balozi wa Marekani na Balozi wa Canada wakapanda kwenye magari pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani kwa ajili ya kuyajaribisha. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Ngaiza, alipopachika funguo kwenye swichi ili awashe gari alipowasha tu, gari linataka kuwaka kisha likagoma kwa kuzimika. Ghafla moshi mzito ukaanza kufuka mbele ya boneti la gari, kabla hawajafahamu kinachendelea ukalipuka mlipuko mkubwa wa bomu kwenye lile gari haujapata kusikika tokea Jiji la Dar es salaam ligeuzwe jina kutoka kuitwa Mizizima. Kishindo kikubwa hicho kikazusha taharuki na tafrani eneo zima la Posta Mpya kila mtu akawa anakimbilia upande wake kuokoa roho yake. Ajali nyingi zilitokea barabarani siku hiyo kwa magari kugongana yenyewe kwa yenyewe na watu kugongwa kwa sababu ya hofu iliyotokana mlipuko huo uliotokea jioni hiyo.
[emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji3586][emoji737]
ITAENDELEA
KUPATA KITABU KUANZIA JUMAMOSI IJAYO NICHEKI KWA NAMBA
0625920847
 
Poti poti poti naona inaanza na mwehu huyu maso maso nimepata shaka ndo stealing wa hii kitu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom