SIRI
episode 28
Mtunzi.Patrick CK
ENDELEA………………………….
DAR ES SALAAM
MathewMulumbi aliwasili
katika uwanja wa kimataifa wa
Julius Nyerere Dar es salaam
akitokea jijini Arusha.Alitoka
ndani ya uwanja na kupokewa
na dereva wake safari ya
kuelekea nyumbani ikaanza “Tukio gani limetokea hapa
jijini leo?Mathewakamuuliza
dereva wake kana kwamba
hajui chochote kilichotokea
“Kumetokea tukio la utekaji
leo.Yule rafiki yako Dr Olivia
ametekwa nyara na watu
wasiojulikana.Hujapata taarifa
hizo mpaka muda huu?akauliza
Athuman dereva wa Mathew
“Tayari ninazo taarifa hizo
nilitaka nipate uhakika kama
taarifa hizo ni za kweli.Kuna
taarifa zozote mpaka sasa kama
amepatikana? “Mpaka sasa hakuna taarifa
zozote zilizotolewa kama
amepatikana lakini naamini
bado hajapatikana kwani kama
angekuwa amepatikana
ingekwisha tangazwa” akasema
Athumani.Ukapita ukimya
Mathewakauliza
“Athumani wewe
unazunguka sehemu mbali
mbali na unasikia mengi,kwa
tetesi ulizozisikia huko mtaani
nini yaweza kuwa sababu ya
kutekwa kwake?akauliza
Mathew “Mkuu kwa kweli mpaka
sasa hakuna anayejua nini
sababu ya Olivia kutekwa.Kila
mtu anaongea la kwake.Wengi
wanaamini kwamba watekaji
wamefanya hivyo kwa ajili ya
kutaka fedha kwani Dr Olivia ni
mtoto wa bilionea na hata yeye
mwenyewe ana mafanikio
makubwa.Kikubwa kilichopo
mtaani ni hicho kwamba
watekaji lengo lao ni kujipatia
fedha.Michezo kama hii ya
kuteka watu na kudai fedha
haikuwepo nchini kwetu
imeibuka ghafla na kushika kasi.Wafanya biashara
wakubwa na matajiri wako
kwenye hatari kubwaya
kutekwa na kulazimishwa kutoa
fedha nyingi ili kuachiwa
huru.Serikali inatakiwa
kudhibiti mchezo huu
usiendelee kwani unaleta hofu
kubwa hasa kwa wafanya
biashara wakubwa.Leo katekwa
Dr Olivia kesho atakuwa nani?
Hofu kubwa imetanda” akasema
Athumani
“Uko sahihi Athumani
kwamba michezo kama hii ya
utekaji haijazoeleka hapa nchini kwetu.Ni wajibu wa wananchi
kushirikiana na serikali
kudhibiti matukio kama haya
yanayoanza kushika kasi hapa
nchini.Wananchi wanatakiwa
kutoa ushirikiano mkubwa kwa
jeshi la polisi kila pale
wanapokuwa na
taarifa.Michezo kama hii ya
utekaji hufanywa na watu
kutoka nje wakisaidiwa na watu
wachache wa ndani” akasema
Mathewa safari ikaendelea
kimya kimya
“Wamekosea sana hawa
jamaa kumteka Olivia.Hawakujua kama Olivia
ni mtu wangu wa
karibu?Nitahakikisha ninaingia
katika mapambano na kumuooa
Olivia kwa gharama zozote”
akawaza Mathew
“Lakini nini hasa sababu ya
kumteka Olivia? Wanahitaji
fedha? Nahisi lengo lao ni hilo la
kujipatia fedha lakini papo hapo
kuna kitu ndani mwangu
kinakataa kwamba lengo la
watekaji ni kujipatia
fedha.Nahisi kuna kitu zaidi ya
fedha.Toka nilipokutana na
Olivia nimehisi ana tatizo
linamsumbua na nilipomdadisi
alikiri kweli ana tatizo na watu
Fulani ambao hakutaka
kuwataja.Je ni watu hao ndio
walimteka nyara? Kama ni wao
nini hasa tatizo lao? Je
wamehitilafiana katika
biashara? Kama ndiyo ni
biashara gani anaifanya Olivia?
Hajawahi kunieleza kama ana
biashara nyingine tofauti na
kumiliki kituo kile cha utafiti wa
magonjwa lakini naamini
hawezi kukosa biashara.Maisha
ya Olivia yametawaliwa na usiri
mwingi hapendi kuweka wazi maisha yake ndiyo maana
linapotokea tatizo kama hili
tunashindwa wapi tuanzie
kumtafuta.Hata hivyo nitafanya
uchunguzi na ukweli
utabainika” akawaza Mathew
Tayari kiza kilikwisha ingia
alipofika nyumbani
kwake.Akaenda chumbani
kwake na kukaa kitandani
akatafakari namna
atakavyoufanya uchunguzi ule.
“Tayari ninafahamu mahala
alipo Olivia lakini siwezi
kwenda huko kwa
kukurupuka.Natakiwa kujipanga vyema kwani
watekaji ni watu
waliojiandaa.Kabla ya kufanya
lolote natakiwa kwanza
nikaonane na wazazi wa Olivia
kujua kinachoendelea hadi
sasa.Yawezekana Olivia
amepatikana au yawezekana
tayari watekaji wamewasiliana
nao na kudai kiasi cha
fedha.Vile vile natakiwa
kuwaeleza azma yangu ya
kumtafuta Olivia na wao
waridhie na kunipa ruhusa ya
kulichunguza jambo hili.Siwezi
kukurupuka na kuanza kuchunguza bila kupata ridhaa
yao” akawaza Mathewna
kufungua kasiki lililkuwa
chumbani kwake akatoa
bastora akaiweka katika koti na
kuondoka.Hakuhitaji dereva
usiku huu aliondoka peke yake.
“Nimewaza sana kuhusu
sababu ya kutekwa Olivia lakini
bado sijapata jibu.Sababu
kwamba watekaji wanataka
fedha hainingii kabisa
akilini.Mgogoro aliowahi
kunidokeza waweza ukawa ni
sababu pia lakini kuna kitu
wengi wanakisahau kuna sababu ya kimapenzi pia.Hii
inawezekana ni mojawapo ya
sababu pia.Yawezekana kuna
kigogo mmoja anayemtaka
lakini Olivia amekataa kumpa
nafasi hivyo akaamua kutumia
nguvu.Nikikutana na wazazi
wake ninaweza kupata mwanga
zaidi kwani wao wanamfahamu
vyema kuliko mimi” Akawaza
akiwa garini akielekea
nyumbani wazazi wa Olivia
Alifika eneo la Mikindani
akautafuta mtaa wa
Themba.Kutokana na umaarufu
wake na namna alivyojitolea kusaidia jamii inayomzunguka
wakazi wa eneo la Mikindani
waliamua kumzawadia Agrey
Themba mtaa ambao waliuita
mtaa wa
Themba.Mathewaliuliza ilipo
nyumba ya bilionea Themba
akaelekezwa akapunguza
mwendo baada ya kulikaribia
geti.Ulinzi ulikuwa mkali eneo
lile.Gari la
Mathewlikasimamishwa na
walinzi waliokuwa wanalinda
geti la kuingilia ndani kwa
mlinzi mmoja
akamfuata.Mathewakashusha kioo akasalimia naye na mlinzi
yule akamtaka ajitambulishe
yeye ni nani
“Naitwa Mathewni rafiki wa
Olivia nimekuja kuonana na
wazazi wake”akasema Mathew
“watu hawaruhusiwi
kuingia ndani labda kwa miadi
maalum hata kama ni ndugu”
akasema yule mlinzi
“Sina miadi ya kuonana na
wazazi wa Olivia lakini mimi ni
mwanafamilia ni mchumba wa
Olivia”akasema Mathewyule
mlinzi akamtazama kwa makini “Kaka usiwe na hofu mimi
ni mwanafamilia,nimetoka
safari Arusha jioni hii nikapata
taarifa za tukio lililotokea
nikaona nije moja kwa moja
nyumbani” akasema
Mathewambaye alikuwa ndani
ya gari la kifahari sana hivyo
mlinzi yule akaruhusu geti
lifunguliwe na Mathewakaingia
ndani.Ilikuwa ni mara yake ya
kwanza kuingia katika jumba
lile kubwa.Magari kadhaa ya
kifahari yaliyopata matano
yalikuwa yameegeshwa.Kijana
mmoja ambaye alionekana ndiye mpokeaji wa wageni
akamuelekeza sehemu ya
kuegesha
magari,Mathewakashuka
akapokewa na yule kijana
akamkaribisha na kumuongoza
kuelekea sebuleni ambako
kulikuwa na watu
kadhaa.Mathewakawasalimu
wote aliowakuta mle
ndani.Alimfahamu Agrey
Themba ingawa hawakuwa
marafiki.Pembeni yake alikaa
mwanamama ambaye kwa
haraka Mathewakamtambua
kuwa alikuwa mama yake Olivia kwa namna
walivyofanana.Muhudumu
akafika haraka na
kumuhudumia
Mathewkinywaji.
Dakika tano baada ya
Mathewkuingia mle sebuleni
wale wageni waliokuwamo
wakaaga na kuondoka,Agrey
akawasindikiza na pale sebuleni
akabaki mama yake Olivia
“Karibu sana baba”akasema
bi Lucy Themba mama yake
Olivia “Nashukuru mama.Pole
sana kwa tatizo lililotokea”
akasema Mathew
“Tunashukuru baba.Dunia
hii imekuwa na watu makatili
sana.Siku hizi ubinadamu
umetoweka.Watu wanatenda
matendo ya kinyama mchana
wa jua bila kuogopa.Mambo
haya sijui yanatokea
wapi.Yanataka kupoteza amani
tuliyo nayo Tanzania” akasema
bi Lucy
“Ni kweli mama mambo
haya ni mageni kabisa katika
nchi yetu.Watanzania tumezoea amani na hatujazoea kusikia
matukio kama haya ya kuteka
watu tena mchana wa
jua.Mambo kama haya
yanatokea sana katika nchi za
wenzetu lakini taratibu
yameanza kutokea na hapa
kwetu pia.Serikali kupitia
vyombo vyake wanapaswa
kudhibiti hali hii isiendelee
kwani kama matukio ya namna
hi yakiendelea yanaweza kuzua
hofu kubwa hasa kwa wafanya
biashara ambao ndio walengwa
wakubwa” akasema Mathew na Agrey Themba akarejea mle
sebuleni
“Kijana karibu
sana.Samahani hatukusalimiana
vyema wakati ulipoingia”
akasema Agrey na kumpa
mkono Mathew
“Karibu sana” akasema
Agrey
“Nimekaribia mzee.Poleni
sana na tukio la leo”akasema
Mathew
“Tumekwisha poa kijana
wangu.Ni jambo ambalo
limetuacha katika simanzi
kubwa”akasema Agrey huku akimtazama Mathewkwa
makini sana
“U mgeni kabisa machoni
kwangu.Tumewahi kuonana
sehemu fulani? Naomba
unikumbushe tafadhali kwani
uzee umekwisha piga hodi na
kuna nyakati ninasahau”
akasema Agrey
“Mzee mimi nakufahamu ila
wewe sidhani kama
unanifahamu.Ninaitwa
MathewMulumbi ni
mfanyabia………….” Kabla
Mathewhajaendelea Agrey
akamkatisha“MathewMulumbi hili si
jina geni kwangu.Wewe ndiye
mwenye kiwanda cha
kutengeneza maziwa cha Masai
Milk?
“Ndiyo mimi mzee” akajibu
Mathew
“Nimefurahi kukutana
nawe Mathewkaribu
sana.Ninamiliki shule kadhaa
hapa jijini dare s salaam
ambazo hupata huduma ya
maziwa kutoka kiwandani
kwako.Niliambiwa kiwanda kile
kinamilikiwa na kijana mmoja
anaitwa Mathewlakini sikuwahi kukutia machoni.Niliambiwa
ukiacha kiwanda kile unazo pia
biashara nyingine kubwa
kubwa.” akasema Agrey
“Ndiyo mzee.Nina biashara
nyingine mbali mbali,viwanda
mashamba nk”
“Hongera sana
Mathew.Nimefurahi
nimekutana nawe leo ingawa
tumekutana katika wakati kama
huu wa matatizo.Naamini pale
tatizo hili litakapokuwa
limemalizika tutapata wasaa
mzuri wa kukutana na
kuzungumza mambo mengi hususan masuala yetu ya
kibiashara”akasema Agrey
“Ahsante sana
mzee,nitafurahi sana kupata
wasaa wa kuzungumza nawe
mambo mengi na kupata
mawazo mengi zaidi ya
biashara” akasema
Mathewukimya mfupi ukaputa
Mathewakasema
“Mzee na mama
mtanisamehe kwa kuja bila
taarifa lakini nimekuja
kuwapeni pole kwa tukio
lililotokea leo.Nilikuwa katika
mkutano Arusha ndipo nilipopata taarifa za kutekwa
Olivia hivyo ikanilazimu
kukatisha mkutano na kurejea
Dar es salaam.Dr Olivia ni rafiki
yangu.Nimefahamiana naye
miezi kadhaa iliyopita na
amekuwa rafiki yangu mkubwa
ndiyo maana nilipopata taarifa
za kutekwa kwake
nimelazimika kuja mara moja
kuungana na familia yake katika
wakati huu mgumu vile vile
kusaidia katika
kumtafuta”akasema Mathew
“Mathewninakushukuru
sana kwa kuguswa na suala hili.Wewe ni rafiki wa kweli na
kwa hili ulilolionyesha la
kuacha shughuli zako zote na
kuja kuungana nasi kutufariji
katika wakati huu mgumu
limetugusa sana.Kwa nini Olivia
hajawahi kututambulisha
kwetu? Wewe unapaswa kuwa
sehemu ya familia yetu.Olivia
anao marafiki wengi lakini
hakuna aliyeonyesha kuguswa
kama wewe” akasema Agrey
“Mzee mpaka sasa kuna
taarifa zozote zimepatikana
kujua mahala alipo
Olivia?akauliza Mathew “Nimekuwa na mawasiliano
ya karibu sana na rais,mkuu wa
jeshi la polisi nchini na hao
wote tunawasiliana kila mara
na hadi nilipowasiliana nao
kama dakika ishirini zilizopita
bado Olivia hakuwa
amepatikana.Jeshi la polisi
linaendelea na juhudi zake na
hakuna kulala hadi wahakikishe
Olivia anapatikana.Rais
amekwisha toa maelekezo kwa
jeshi la polisi wahakikishe
wanatumia kila uwezo walio
nao kumtafuta Olivia na
kumpata.Ninaamini mpaka kesho asubuhi tunaweza
tukawa na taarifa nyingine
nzuri lakini taarifa tuliyonayo
hadi muda huu bado Olivia
hajapatikana” akasema
Agrey.Ukapita ukimya wa
sekunde kadhaa halafu
Mathewakasema
“Mzee samahani tunaweza
kuzungumza faragha kidogo?
“Sawa hakuna tatizo”
akasema Agrey akamchukua
Mathewwakatoka nje ya
nyumba wakaelekea katika
bustani ambako kulikuwa na
sehemu za kukaa kupumzika “Nakusikiliza Mathew”
Akasema Agrey
“Mzee nitakuchukulia muda
wako kidogo lakini nataka
nipate picha ya namna tukio lile
lilivyotokea.Mimi sijabahatika
kufika eneo la tukio kama
nilivyokueleza kwamba
nilikuwa Arusha.Naamini
utakuwa umefika eneo la tukio
na utakuwa umeshuhudia
namna tukio
lilivyotokea.Nataka kufahamu
mazingira ya namna tukio lile
lilivyotokea kwani nimesoma tu
mtandaoni na sijapata picha halisi” akasema Mathew.Agrey
akamtazama Mathewkidogo na
kusema
“Niliwasiliana na Olivia
asubuhi ya leo akiwa jijini
Kinshasa na akanieleza kwamba
atarejea leo nyumbani.Alirejea
salama na tukio la kutekwa
limetokea wakati akijiandaa
kuingia ndani ya nyumba yake
akitokea uwanja wa ndege.Kwa
siku za karibuni Olivia aliamua
kuwa na walinzi kwa kuwa
wewe ni mtu wake wa karibu
nadhani umekwisha waona
akiwa nao sehemu mbali
mbali.Aliamua kuwa na walinzi
baada ya kuwa na wasi wasi na
usalama wake hivyo alipotoka
uwanja wa ndege alikuwa na
magari mawili moja alikuwamo
yeye na mlinzi wake mmoja
pamoja na dereva na lingine
walikuwemo walinzi wake
wengine.Kwa mujibu wa
mashuhuda ni kwamba magari
yalipokaribia katika geti la
nyumba ya Olivia ilitokea
helkopta na mtu mmoja
akajitokeza katika helkopta ile
akiwa na bunduki kubwa na
kuanza kumimina risasi katika magari yale na dereva wa gari la
Olivia akapigwa risasi akafa
pale pale na gari la Olivia
likaenda kugonga ukuta.Walinzi
wake nao waliuawa
wote.Taarifa kutoka kwa mlinzi
wa getini ambaye alijificha
wakati tukio lile linatokea
alisema kwamba zilitokea gari
mbili kwa kasi na kumchukua
Olivia wakaondoka naye.Jeshi la
polisi walijaribu kufuatilia picha
za kamera za ulinzi lakini
hawakuweza kuwatambua watu
wale kwani walikuwa
wamefunika nyuso zao na vile vile gari zote mbili zilikuwa na
namba zinazofanana.Helkopta
ile imepatikana imekutwa
imetelekezwa sehemu nje ya jiji
na dereva wake amekutwa
ameuawa yeye na familia yake
inaonekana helkopta ile iliibwa
na watekaji wakaitumia kisha
wakaitelekeza.Hapo ndipo
walipofikia jeshi la polisi na
uchunguzi unaendelea”
akasema Agrey
“Pole sana mzee wangu.Hili
linaonekana ni tukio
lililopangwa kitaalamu
sana.Kuna mtu yeyote ambaye anashikiliwa hadi sasa kufuatia
tukio hilo?akauliza Mathew
“Kwa taarifa nilizozipata ni
kwamba hadi sasa watu zaidi ya
ishirini wanashikiliwa na jeshi
la polisi vile vile watumishi
wote wa nyumbani kwa Olivia
nao pia wanashikiliwa na jeshi
la polisi kwa
mahojiano.Mtandao uliofanya
tukio hili unaonekana ni mrefu
ndiyo maana idadi hiyo kubwa
ya watu inashikiliwa ndani ya
kipindi kifupi” akasema Agrey
na gari Fulani likaingia
wakashuka watu wawili Agrey akamuomba Mathewamsubiri
akawapokee wageni wale
atarejea.Agrey akaenda
kuwapokea wageni wake na
kuwakaribisha ndani baada ya
muda mfupi akarejea
“Samahani kwa kukuacha
mwenyewe Mathew,mgeni yule
ni naibu waziri wa mambo ya
nje amekuja kutupa pole,ni
rafiki yangu sana.Tuendelee na
mazungumzo yetu” akasema
Agrey
“Mzee nimeomba
tuzungumze faragha kuna suala
la muhimu sana la kujadiliana mimi na wewe na sikupenda
mtu mwingine alifahamu’
akasema Mathew
“Ni suala gani
Mathew?akauliza Agrey.
“Hakuna anayefahamu
sababu ya Olivia kutekwa lakini
wengi tunaamini yawezekana
watekaji wanataka fedha kwani
mchezo wa namna hii upo
katika nchi mbali mbali na mara
watekaji wanapomteka mtu
hupiga simu kwa familia yake
wakidai kiasi kikubwa cha
fedha.Hamjapigiwa simu na mtu yeyote msiyemfahamu?akauliza
Mathew
“Hata sisi tunaamini hivyo
kwamba watekaji hao
yawezekana lengo lao ni
kujipatia fedha lakini mpaka
sasa hawajapiga simu na
hatujapokea simu yoyote
ambayo hatuifahamu” akajibu
Edger
“Kama lengo lao ni fedha
basi watapiga simu na
watakapopiga watatoa vitisho
kwamba msiwasiliane na jeshi
la polisi” “Tumekwisha eleweshwa
tayari na jeshi la polisi
kuhusiana na suala hilo na
watakapopiga tutawasiliana na
polisi haraka sana” akasema
Agrey
“Hata hivyo umakini
mkubwa unatakiwa kwani watu
hawa ni hatari na wamejipanga
vyema hivyo kosa moja hata
dogo linaweza kuweka uhai wa
Olivia mashakani” akasema
Mathew
“Unaniogopesha
Mathew.Unashauri wakinipigia simu kutaka fedha nisiwasiliane
na polisi?akauliza Agrey
“Sina maana kwamba
usiwasiliane na jeshi la polisi
lakini umakini mkubwa sana
unatakiwa.Hata polisi
wasipokuwa makini mnaweza
mkapoteza fedha na Olivia
msimpate.Tuachane na hilo
kuna suala la pili ambalo nataka
tuzungumze” akasema
Mathewna kunyamaza kidogo
kisha akasema
“Nimefahamiana na Olivia
miezi kadhaa iliyopita na
tumekuwa marafiki wa karibu sana.Katika ukaribu wetu
nimekugundua kwamba Olivia
alikuwa na tatizo
linalomsumbua na siku moja
niliwahi kumuomba anieleze
tatizo lake lakini alinieleza kwa
kifupi kwamba ana matatizo na
watu Fulani.Nilimtaka anieleze
ni tatizo gani na watu hao ni
akina nani lakini hakutaka
kuliongelea suala hilo.Hali hiyo
imeendelea kwa muda mrefu na
baada ya tukio la leo nimeanza
kupata picha kwamba
yawezekana watu hao ambao
alinidokeza kwamba ana matatizo nao watakuwa na
mahusiano na kutekwa
kwake.Nimekuja kwako
kufahamu je hakuwahi
kukueleza chochote wewe au
mama kuhusiana na tatizo
lililokuwa linamsumbua?
Akauliza Mathew.Agrey
akafikiri kidogo na kusema
“Ni mara ya kwanza
ninasikia kutoka kwako
kwamba Olivia alikuwa na
tatizo linamsumbua.Kwa tabia
yake Olivia ni mtu msiri sana ni
nadra kuweka wazi tatizo
linalomsumbua.Akikueleza tatizo lake basi limemshinda
kulitatua na anahitaji
msaada.Anaamini sana katika
kutatua matatizo yake yeye
mwenyewe bila kuomba
msaada.Kutokana na wote kuwa
na shughuli nyingi,mimi naye
tumekuwa tukionana mara
chache na hata tunapoonana
hajawahi kunieleza kama ana
tatizo linamsumbua.Ni watu
gani hao aliokuwa katika
mgogoro nao? Inawezekana
kabisa wakawa wanahusika
katika tukio la leo kama
unavyosema” akasema Agrey.