SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 9 : EPISODE 9
Mathew aliwasili
nyumbani kwake
“Mungu naomba
unisaidie” akawaza na kushuka
garini akaelekea ndani
akakutana na Lucy mlangoni
“Karibu kaka”
“Ahsante Lucy.Yuko wapi
Peniela?
“Yuko katika chumba cha
mapumziko anakusubiri huko”
akasema Lucy
“Nashukuru sana Lucy”
akasema Mathew na kupanda
ngazi kuelekea katika chumba
cha mapumziko kilichopo
ghorofani.Kupitia mlango
mkubwa wa kioo akamuona
Peniela akiwa amesimama
dirishani akitazama
nje.Akaufungua mlango
taratibu na kuingia
ndani.Peniela aliposikia
mlango ukifunguliwa akageuka
wakagonganisha macho.Kila
mmoja alisimama mahala pale
akimtazama mwenzake kwa
dakika mbili na taratibu
michirizi ya machozi
ikaonekana mashavuni mwa
Peniela
“Hallo Penny” akasema
Mathew
“Hallow Mathew” akasema
na kuchukua kitambaa akafuta
machozi
“Karibu sana.Pole na
safari” akasema Mathew na
kumtaka Peniela aketi.
“Ahsante sana kwa kuja
Peniela.Nimefurahi kukuona
tena” akasema Mathew
“Mathew I’m sorry
nimeshindwa nifanye nini
baada ya kuiona sura
yako.Nimeshindwa
nikukumbatie niangue kilio au
nifanye nini” akasema Peniela
“Nafahamu Peniela uko
katika mstuko bado na
itachukua muda kuamini kama
kweli ni mimi lakini naomba
nikuthibitishie kwamba ni
mimi Yule Yule
unayenifahamu” akasema
Mathew
“Kwa nini Mathew
umetutesa kiasi hiki?Unajua ni
mateso gani mimi na watoto
tumeyapitia ? akauliza Peniela
“Ninafahamu Peniela na
sipati neno zuri la kuwaomba
samahani kwa wakati mgumu
mliopitia lakini hata wewe
mwenyewe unafahamu
nising…..”
“Hapana hufahamu kitu
chochote Mathew ! akasema
Peniela kwa ukali na
kumkatisha Mathew
“Hufahamu chochote
kuhusu mateso ambayo mimi
na watoto
tumeyapitia.Ungejua kama
tutateseka usingetengeneza
kifo chako!
“Penny sikufanya hivyo na
siwezi kufanya hivyo hata siku
moja.Unajua ni namna gani
ninakupenda wewe na watoto
hivyo nisingeweza kufanya kitu
ambacho kingewaumiza”
“Mathew ninajuta
kukupenda mtu kama
wewe.Ningejua kama nitaishi
maisha kama haya nikiwa
nawe katu nisingekubali
kuolewa nawe!
“Usiseme hivyo Peniela”
“Ni lazima niseme ili
ufahamu.Ninajuta kuishi na
mtu kama wewe.Unadiriki
hata kutunga kifo chako na
hufikirii familia yako itateseka
kiasi gani.Kitu gani umekikosa
Mathew.Nimekupa utajiri
mkubwa maisha ya kifahari
lakini bado unarudia kazi zako
hizi zisizo na maana
yoyote.Unapata nini kutoka
katika kazi hizi zinazokufanya
uipe familia yako mateso
makubwa?Maneno yale ya
Peniela yakaonekana
kumchoma sana Mathew
“Peniela una haki ya
kunitukana mimi matusi ya
kila namna unayoyafahamu
lakini katu usithubutu
kuitukana na kuidharau kazi
yangu.Ni kazi hii hii ambayo
leo unaidharau ndiyo kazi
ambayo imekufanya leo hii
ukajulikana dunia
nzima.Isingekuwa kwa kazi hii
usingekuwa Peniela huyu wa
leo hivyo nakuonya usithubutu
kudharau kazi yangu !
“Lazima niseme ! Kazi hiyo
imekuingizia nini hadi sasa?
Toka umeanza kuifanya kazi
hii hakuna manufaa yoyote
uliyowahi kuyapata zaidi ya
hasara.Umeipoteza hadi
familia yako ya kwanza kwa
sababu ya kazi hii lakini bado
hujajifunza na sas…………..”
“Peniela stop !! akasema
Mathew kwa hasira
“You want to hit me?Go
ahead hit me I’m not scared of
you ! akatamba Peniela
“Sifahamu nani kakuloga
Mathew hadi unaacha hivi
vyote nilivyokupa na kurejea
katika kazi kama hizo zisizo na
mshahara wowote.I didn’t
know you are such a stupid…..”
Peniela hakumaliza kile
alichotaka kuisema akajikuta
ameanguka sakafuni baada ya
kulambwa kofi zito.Akagala
gala pale chini na kuinuka
akavua kiatu chake akaipiga
meza ya kioo ikavunjika
akachukua kipande cha kioo
akakirusha lakini Mathew
akawa hodari akakikwepa
halafu akamfuata tena na
kumnasa kofi lingine zito
Peniela akajikuta amekaa
sofani.Damu zilianza kumtoka
mdomoni.
“Nimekuonya dhidi ya
dharau na kejeli zako kwa kazi
yangu.Nitukane utakavyo
lakini si kutukana na kudharau
hiki ninachokifaya.Do you
know what I’m going through
right now?Nina majukumu
mazito ya kuisadia nchi hivyo
sintavumilia kejeli za mtu
kama wewe.Sintajali wewe ni
mke wangu au nani lakini
utakaponikosea heshima
katika kazi yangu lazima
nikufunze adabu ! Hii ni mara
ya kwanza ninakupiga toka
nimekuoa na nimekupiga
kutokana na dharau
ulizozionyesha.Ulipaswa
kunionea huruma badala ya
kuanza kunikejeli.Unadai
umenipa utajiri ?Mimi ndiye
niliyekupa huo utajiri ambao
leo hii unakupa kiburi!
Akafoka Mathew
“Everything came from
blood.You have nothing you
stupid ! akafoka Peniela huku
akilia
“Fine.Kwangu mimi utajiri
wa mali si kitu na sihangaiki
nao.Ninahangaika kwa ajili ya
nchi yangu na watu wake
wakae kwa amani na wala
sihitaji mtu anilipe kwa kazi
hiyo bali ni Mungu mwenyewe
ndiye atakayenilipa kwa njia
anazojua yeye mwenyewe
hivyo tafadhali usinitusi
kuhusu mali hizi ambazo
ninaweza kuzitafuta na kupata
kushinda hata hizo
ulizonazo.Nimekuta umeuza
mali zote na sijakulaumu kwa
sababu sihangaiki na mali”
“Kama uhangaiki na mali
kwa nini ukanipigia simu?
“Nilitaka kupata uhakika
kama ni wewe uliyeuza”
“Ni mimi nimeuza jasho
langu.Siwezi kuacha mali
zangu kwa mtu asiye na
shukrani hata chembe!
“Ni wewe ambaye
umekosa shukrani kwangu
kwani kama nisingesimama
imara mimi haya yote
usingekuwa nayo”
“Huna uimara wowote
Mathew.Ungekuwa imara
usingetengeneza kifo chako na
kuiacha familia yako katika
mateso makubwa”
“I didn’t fake my death but
…..” akasema Mathew na
kunyamaza kidogo
“Hukuonekana kuumizwa
na kifo changu hata kidogo
ndiyo maana hukusumbuka
kutafuta ukweli hukusumbuka
hata kutafuta kaburi langu
liliko”
“Ninajutia hata machozi
niliyoyamwaga kwa ajili
yako.Hustahili machozi
yanguMathew ! Wewe ni mtu
mnyama sana !
“Ninalifahamu
hilo.Sikustahili machozi yako
kwa sababu tayari ulikwisha
nitoa ndani ya moyo
wako.Nafahamu mapenzi kati
yetu yalikwisha zamani ni
mimi ambaye niliendelea
kubembeleza na ulipopata
taarifa za kifo changu
ulishukuru” akasema Mathew
na kuvuta pumzi ndefu
“Ninafahamu kuhusu
mapenzi yako na Nahum
kijana wa kutoka Israel.I saw
you and I was hurt”akasema
Mathew na Peniela akabaki
kimya akimtazama Mathew
“Ulifanya haraka sana
kuamua kuwa na mwanaume
mwingine wakati hujaupata
ukweli halisi kuhusu kifo
changu”
“Ouh kumbe ulikuwa
unanifuatilia ! Stupid. !
akasema Peniela na kufuta
damu kwa kitambaa
“Imekuwa vizuri kama
ulikuwa unanifuatilia na
umegundua kwamba nilikuwa
na mwanaume mwingine
anayejitambua kuliko wewe !
“Nahum alikuwa
anakuchezea tu
Peniela.Alikuwa ni jasusi wa
Israel na alikuwa kazini!
akasema Mathew na Peniela
akawa kimya.Baada ya muda
akasema
“Sijali kama alikuwa
ananichezea ama vipi lakini
alikuwa anajielewa kuliko
wewe.Sitaki mjadala mrefu na
wewe.Nimesafiri usiku kucha
kuja hapa Tanzania kwa ajili ya
kitu kimoja tu” akasema
Peniela na kunyamaza
akamtazama Mathew
“Nimekuja kulimaliza hili”
akasema tena na kufuta
machozi
“Mathew nilitegemea kuwa
mwanamke mwenye furaha
kubwa katika maisha yangu
lakini imekuwa kinyume chake
nimekuwa ni mwanamke
mwenye mateso makubwa
kuliko furaha.Nyakati
nilizowahi kuwa na furaha
toka nimekuwa nawe ni chache
sana.Nimejitahidi kuvumilia
nikitegemea labda siku moja
mambo yatabadilika lakini
hakuna dalili zozote za
mabadiliko na ninaendelea
kuumia na wewe mwenzangu
huonekani kujali furaha yangu
na wanangu.Umesema
nisidharau kazi yako na siwezi
kufanya hivyo lakini kwa kauli
hiyo umedhihirisha wazi
kwamba umechagua kazi
kuliko mimi na watoto.Hauoni
tena thamani yetu ndiyo
maana umekuwa ukiendelea
na maisha yako huku sisi
tukimwaga machozi kila siku
kukulilia na kukuombea.Sitaki
kuendelea na maisha haya
Mathew na Mungu
atanisamehe kwa maamuzi
haya niliyoyachukua” akasema
Peniela na kuinuka akaenda
kuchukua mkoba wake
akaufungua na kutopa bahasha
ya khaki akampatia Mathew
akaifungua na kukuta ni
nyaraka za mahakama za
kutengua ndoa.Mathew
akaziweka karatasi zile na
kumtazama Peniela kwa hasira
“Utanisamehe Mathew
hayo ndiyo maamuzi
niliyoyachukua na sintabadili
tena maamuzi yangu.Nataka
niwe na furaha katika maisha
yangu na furaha hiyo siwezi
kuipata nikiwa nawe hivyo
nimeamua kuachana nawe ili
kila mmoja aendelee na
maisha yake kwa amani.Wewe
utaendelea na kazi yako
ambayo ni ya muhimu kuliko
sisi na mimi nitaendelea na
maisha yangu na kama Mungu
akinijalia basi nitampata Yule
ambaye atanipa furaha ya
maisha ninayoihitaji” akasema
Peniela na Mathew
akazichukua tena zile karatasi
akazisoma kisha akamtazama
Peniela
“Are you sure you want to
do this?akauliza Mathew
“I’m sure 100%” akajibu
Peniela
“Please sign the papers
Mathew.Hakuna namna
unayoweza ukanishawishi
nikabadili maamuzi yangu.It’s
over please accept it.Kuhusu
mali usiwe na wasiwasi
nitakugawia robo ya mali
zangu zote” akasema
Peniela.Mathew akatafakari
akavuta pumzi ndefu na
kusema
“Arlight let’s end
this.Lakini…” akasema
Mathew na kumtazama
Peniela
“Naomba ufahamu
kwamba ninapo weka saini
makaratasi haya ninaufunga
mlango ambao hautafunguliwa
tena.Lifahamu hilo na
ninaomba uwe na uhakika na
hiki unachotaka kukifanya”
“Saini karatasi Mathew.I
don’t care if there is a door or
window between
us.Ninachokihitaji ni kuachana
nawe rasmi.Siwezi kuishi na
mtu ambaye anakufa na
kufufuka.Hujui lini atakufa
kifo cha kweli.Siwezi
kuendelea kuteseka kiasi
hiki.Labda Mungu atakujalia
utampata Yule ambaye
atakuelewa na atakuwa tayari
kuishi nawe lakini mimi
nimeshindwa kukuelewa na
siko tayari kuendelea kuishi
nawe” akasema
Peniela.Mathew akazitazama
tena zile karatasi kwa makini
“Kama alivyotamka yeye
mwenyewe kwamba it’s
over.Hakuna namna
ninavyoweza kumshawishi
akabadili maamuzi yake na
mimi siwezi nikaacha kazi hii
muhimu kwa nchi nikamfuata
mwanamke.Kwangu nchi
kwanza na mengine baadae
kwa hiyo niko tayari kuitoa
sadaka ndoa yangu.Ngoja
nimuache aende kwani
sintaweza kumpa furaha
anayoihitaji katika maisha
yake.Nitakuwa mchoyo kama
nitaendelea kung’ang’ania
kuwa naye” akawaza Mathew
“Peniela naomba
unisikilize” akasema Mathew
“Nimekuelewa kile
unachokitaka na
nitakutimizia.Sitaki kuwa
mchoyo nataka ukaitafute
furaha ya maisha unayoihitaji
lakini kabla ya kuweka saini
karatasi hizi kuna mambo
ambayo nataka tukubaliane”
akasema Mathew na
kunyamaza kidogo halafu
akasema
“Kwanza kabisa ni kuhusu
watoto.Ninaomba sana jambo
hili liwe ni letu peke yetu na
watoto wasifahamu
chochote.Wataendelea
kufahamu kuwa nimefariki
dunia hadi hapo baadae
mambo yangu yatakapotulia
nitawatafuta na kuwaeleza
ukweli.Jambo la pili ni kuhusu
mali” akanyamaza tena kidogo
“Sihitaji chochote kutoka
katika mali zako Peniela.Kama
uliamua kunitengea fungu
langu ligawanye mafungu
manne na kila mtoto wangu
apate fungu lake.Jambo la tatu
kuna msaada ninauhitaji
kutoka kwako”
“Kama umekataa mali
nilizokupa unataka nikusaidie
nini tena? akauliza Peniela.
“Ninahitaji taarifa”
“Taarifa zipi
unahitaji?akauliza Peniela
“Nataka kumfahamu Yule
mtu uliyemuuzia mali za hapa
Dar es salaam Melanie Davis”
akasema Mathew na uso wa
Peniela ukaonyesha mshangao
“Melanie Davis?! Kwa nini
unataka kumfahamu?
“Ninahitaji kupata taarifa
zake.Wewe ndiye
unayemfahamu vyema hivyo
basi nakuomba unipe taarifa
zake” akasema Mathew
“Unataka kumfanya nini
Melanie? Tafadhali naomba
usimguse mimi ndiye
niliyemuuzia mali zangu na
zilizobaki nikampa Gosu
Gosu.Sikujua kama utafufuka
tena” akasema Peniela
“Peniela narudia tena
kukukumbusha kwamba
sihitaji mali.Ninao uwezo wa
kuishi maisha ya aina yoyote
ile hivyo mali si kipaumbele
kwangu.Huyu Melanie sihitaji
kumsumbua kwa chochote
kuhusu mali alizonunua kwani
amenunua kihalali kabisa”
“Kwa nini sasa unataka
taarifa zake?
“Utanipa taarifa zake au
haunipi?Mathew akauliza
“Utanifanya nini kama
nisipokupa taarifa zake?
“Sintasaini karatasi hizi na
wewe utaendelea kuwa mke
wangu hadi kifo
kitutenganishe” akasema
Mathew na kuweka kalamu
chini.
“Simfahamu Melanie
Davis vizuri.Niliwatangazia
watu wangu wa karibu hasa
wafanya bishara kuhusu
mpango wangu wa kuuza mali
zilizoko Tanzania na kuwataka
wanisaide kutafuta
mnunuzi.Walikuja wanunuzi
wengi lakini akajitokeza
Melanie ambaye alikuja na bei
nzuri na kuwazidi wale wote
waliokuja mwanzo hivyo basi
nikamuuzia kila kitu”
“Melanie anatajwa kuwa
mmoja wa mabilionea
wakubwa nchini Ufaransa
utajiri ambao alirithi kutoka
kwa wazazi wake.Wewe
umekuwa miongoni mwa
mabilionea wa Ufaransa je
umewahi kumsikia Melanie
Davis hapo kabla?akauliza
Mathew.Melanie akafikiri na
kusema
“Hapana sikufahamu
Melanie kabla”
“Umewahi kuwasikia
wazazi wake?akauliza Mathew
“Hata wazazi wake sina
kumbu kumbu kama nimewahi
kuwasikia.Taarifa hizi zote
umezipata wapi?akauliza
Peniela
“Ukiacha haya makampuni
uliyomuuzia hapa Tanzania
unazifahamu biashara zake
nyingine? Akauliza Mathew
“Hapana sizifahamu”
“Ikawaje ukamuuzia
kampuni zako mtu ambaye
humfahamu vyema?akauliza
Mathew
“Nilihitaji mnunuzi na
alipojitokeza sikutaka
kumchunguza mara mbili
nikamuuzia” akajibu Peniela
“Unafahamu yalipo makazi
yake jijini Paris? Mathew
akauliza
“Mathew sihitaji maswali
yako tena.Kama unahitaji
kumfahamu mtafute wewe
mwenyewe ukamuhoji !
akasema Peniela kwa ukali
“Peniela I real need your
help.Muda mfupi ujao
nitakapoweka saini yangu
katika hizi karatasi utakuwa ni
mwisho wetu na mlango
utafungwa.Only God knows
when we’ll meet again hivyo
basi huu ni msaada wangu wa
mwisho ninakuomba
unisaidie.Ni muhimu sana
kwangu na ….” Akasema
Mathew na Peniela
akamkatisha
“Melanie ana umuhimu
gani kwako? Kwa nini
unatafuta taarifa zake
unamchunguza? Akauliza
Peniela
“Peniela nisingependa
kukueleza chochote kwa sa…”
“Kama hutanieleza sababu
za kutafuta taarifa za Melanie
sintakueleza chochote
ninachokifahamu” akasema
Peniela.
“Arlight unataka
kufahamu? Ni kwamba mtu
uliyemuuzia makampuni yako
hapa Tanzania Melanie Davis
ana mahusiano na kikundi cha
kigaidi cha IS na vile vile ana
mashirikiano na James Kasai
kiongozi wa kundi la waasi
ambaye hivi karibuni alifanya
shambulio hapa nchini ambalo
liliua wake za marais wa
Tanzania,Congo na Rwanda.IS
wamekuwa wakimtumia
Melanie kupitishia fedha
kwenda kwa James
Kasai.Umemuuzia mali mtu
hatari kabisa kwa usalama wa
nchi yetu” akasema Mathew na
Peniela akabaki mdomo wazi
na mara simu ya Mathew
ikaita alikuwa ni Dr Masawe.
“Samahani nataka
kuipokea hii simu” akasema
Mathew na kuipokea ile simu
“Dr Masawe” akasema
Mathew
“Mathew nimekupigia
kukupa taarifa kwamba
tumepokea taarifa muda mfupi
uliopita kutoka polisi kwamba
mwili wa Dr Sebastian
umeokotwa ufukweni akiwa
amekufa.Polisi wanasema
alipigwa risasi ya kichwa”
“Sebastian ameuawa!
Mathew akashangaa
“Ndiyo Mathew ameuawa”
“Dr Masawe suala hili ni
kubwa.Nitafika hapo hospitali
tutazugumza kwa kirefu
zaidi.Nashukuru sana kwa
taarifa” akasema Mathew na
kukata simu akamtazama
Peniela.
“Unafahamu kama
Melanie na Gosu Gosu wana
mahusiano ya
kimapenzi?akauliza Mathew
“Ndiyo ninafahamu.Ni
mimi ndiye
niliyewaunganisha.Nilimuita
Gosu Gosu Ufaransa kwa ajili
ya kufanya mauziano na
Melanie na walipokutana
wakapendana wakawa
wapenzi” akasema Peniela
“Tunahisi kwamba Gosu
Gosu kuna kitu alikigundua
kuhusu Melanie ndiyo maana
wakataka kumuua.Alipigwa
risasi nyingi ili afariki lakini
siku yake haikuwa imefika
akanusurika na jana
likafanyika tena jaribio lingine
la kutaka kumuua.Daktari
mmoja alitumika kumchoma
sindano ya sumu Gosu Gosu
kwa bahati mbaya jaribio hilo
la kumuua halikufanikiwa
lakini imelazimu Gosu Gosu
kufanyiwa upasuaji wa
kupandikizwa ini jana usiku
kwani ini lake liliharibiwa
kabisa na sumu.Melanie ni
mwanamke hatari kabisa hata
wewe ujihadhari naye sana
kwani mtandao wake ni
mkubwa” akasema Mathew
“Kwa hiyo hivi sasa
unaendesha zoezi la kumsaka
Melanie Davis?akauliza
Peniela
“Ndiyo.Ninamsaka
Melanie Davis na ndiyo maana
ninahitaji sana msaada wako”
“Mathew unamtafuta
Melanie kwa sababu
anashirikiana na magaidi wa
IS au kwa sababu amenunua
mali zako? Peniela akauliza
“Kwa mara nyingine tena
Peniela nakukumbusha
kwamba mimi sihitaji
mali.Hizi zote ni mali zako na
mimi nilikuwa msimamizi
wake tu hivyo sina kinyongo
chochote na Melanie kununua
mali zangu.Nilikuwa
naendelea na operesheni
yangu ya kuwasaka magaidi na
ndipo Melanie Davis
alipojitokeza na nikaanza
kumfuatilia na kugundua
ndiye aliyenunua mali zangu.
Sikuwa na sehemu nyingine ya
kuweza kupata taarifa zake ila
kwako ndiyo maana
nikakupigia” akasema Mathew
“Nilichokueleza ndicho
kitu niachokifahamu kuhusu
Melanie labda nitakusaidia
kufanya uchunguzi na nikipata
taarifa zozote za kumuhusu
yeye nitakujulisha” akasema
Peniela
“Nitashukuru sana”
akasema Mathew
“Maswali yamekwisha can
you sign now?akauliza Peniela
Mathew akaishika kalamu
na kumtazama Peniela kisha
akaanza kusaini zile
karatasi.Alipomaliza
akazirudisha ndani ya bahasha
na kumkabidhi Peniela
“Ahsante Mathew na
samahani sana kwa maamuzi
haya ” akasema Peniela.
“Usijali
Peniela.Ninakupongeza kwa
maamuzi haya magumu
ambayo umeyafanya.Unahitaji
furaha katika maisha yako na
mimi si mtu sahihi ninayeweza
kukupa hiyo furaha.Maisha
yangu hayataweza kubadilika
kamwe kwani nililetwa duniani
kwa ajili ya kazi hii na
nitandelea nayo hadi siku ya
kufa kwangu.Ninakushukuru
sana kwa kunivumilia kwa
muda mrefu na samahani vile
vile kwa kuwasababishia
maumivu makubwa lakini
halikuwa kusudi langu
kuwaumiza.Ninachokuomba
wakuze watoto katika maadili
mazuri wawe na bidii katika
masomo,wamjue Mungu
wafundishe kusaidia watu
wenye uhitaji kwa kuwa wao
wamezaliwa katika utajiri
mkubwa.Wasaidie kuhakikisha
wanatimiza ndoto zao lakini
kamwe,narudia tena kamwe
usiruhusu mtoto wangu yeyote
akafanya kazi kama
ninayoifanya mimi.Sitaki waje
kuishi maisha kama ninayoishi
mimi.Sitaki wayapitie yale
ninayoyapitia.Waweke mbali
kabisa na dunia hii ninayoishi
mimi.Nadhani umenielewa
Peniela” akasema Mathew na
Peniela akafuta machozi
“Nimekuelewa Mathew na
mimi pia ninakuomba
samahani sana kila pale
nilipokukosea.Najua sikuwa
mkamilifu nimekukwaza mara
nyingi,tuliwahi kutengana na
mimi nilikuwa
chanzo,nimewahi kuwa na
mahusiano na wanaume
kadhaa ulifahamu lakini
ulinivumilia.Nisamehe sana
kwa yote” akasema Peniela
“Hakuna mwanadamu
mkamilifu.Sote tuna
mapungufu yetu na mimi
niliyafahamu mapungufu yako
nikayakubali na
kuyabeba.Nategemea Yule
atakayekuja baada yangu naye
atakuwa mvumilivu kama
mimi.Ninakutakia kila la heri
Peniela”akasema Mathew na
kusimama
“Mathew kabla
hatujapeana kwa heri ya
kuonana kuna kitu nataka
kukifahamu.Ulizungumza
kuhusu
Nahum.Umemfahamuje?Ulifa
hamuje kama mimi na yeye
tulikuwa na
mahusiano?akauliza Peniela
na Mathew akaketi
“Haitakuwa na umuhimu
wowote tena kwako kwa sasa
lakini kwa umeuliza
nitakueleza ukweli wa kile
kilichotokea” akasema Mathew
na kumsimulia kuanzia Olivia
Themba alivyotekwa na
SNSA,sakata la Edger Kaka na
hadi operesheni ile ya
kuwakomboa mateka
waliotekwa na IS na hadi
alivyopigwa risasi na
kutekwa.Mashavu ya Peniela
yaliloa machozi
“Nilipofumbua macho
nilijikuta katika chumba
chenye kiza na baadae
nikagundua nilikuwa nchini
Israel. Nilianza kupatiwa
mateso makali na nimeteswa
kwa muda wa miaka mitatu”
akasema Mathew na kuvua
fulana akamuonyesha Peniela
makovu ya vidonda
vilivyotokana na mateso
aliyoyapata.Peniela akafumba
macho hakutaka
kutazama.Mwili wa Mathew
ulijaa makovu ya vidonda.
“Haya ndiyo niliyoyapitia
huko Israel kwa miaka
mitatu.Sikumbuki ni mara
ngapi nilipoteza fahamu
wakati nikiteswa lakini ni
mara nyingi.Pamoja na mateso
hayo makali lakini sikuwahi
kufungua mdomo wangu
kusema chochote na ndipo
walipoamua kuitumia familia
yangu kunilazimisha
niongee.Wakamtuma Nahum
Yatom aje Ufaransa aanzishe
mahusiano nawe na lengo lake
likafanikiwa.Nahum alikuwa
ni jasusi kutoka shirika la
ujasusi la Israel
Mossad.Hakuwa na malengo
yoyote nawe bali alikuwa
kazini.Zilifungwa kamera
chumbani kwako na Mossad
walikuwa wanafuatilia kila
mlichokuwa mnakifanya na
Nahum.Nilionyeshwa mkiwa
chumbani mkifanya mapenzi
na Nahum nikaumia sana na
Mossad walikuwa wakihitaji
niumie ili niweze kuzungumza
na kwa maumivu niliyokuwa
nayo nikajikuta nikianza
kuzungumza” akasema
Mathew
“It was true then ….”
Akasema Peniela akifuta
machozi
“Nini Peniela?
“Kabla ya kuuawa Nahum
aliniambia uko hai nikutafute
lakini nikapuuza maneno
yake”
“Alikwambia
hivyo?akauliza Mathew
“Ndiyo aliniambia hivyo”
akajibu Peniela
“Nani alimuua
Nahum?Mathew akauiza
“Hadi leo hii haijulikani
nani waliomuua”
“Lazima atakuwa
ameuawa na Mossad” akasema
Mathew
“Mathew I’m sorry
sikuyafahamu hayo yote
uliyoyapitia” akasema Peniela
“Usijali Penny yamekwisha
pita ila nakuomba usimueleze
mtu yeyote haya niliyokueleza”
“Sintamueleza mtu yeyote
Yule” akasema Peniela
“Naamini sasa utakuwa
huru Peniela jitahidi uwe na
furaha katika maisha
yako.Usiwaze chochote kuhusu
mimi.Maamuzi haya
uliyoyafanya ni maamuzi
sahihi kwa wakati sahihi”
akasema Mathew na Peniela
akaendelea kulia.
“Mathew please I need a
hug” akasema Peniela na
Mathew akainuka akaenda
kumkumbatia.
“Mathew I’m very sorry !
akasema Peniela akilia na
kumwaga machozi katika bega
la Mathew
“Peniela unahitaji kuwa
jasiri wala usisikitike kwa
maamuzi haya uliyoyachukua”
akasema Mathew na
kumuachia Peniela.
“Unarejea leo
Paris?Mathew akauliza
“Nimekuja na ndege yangu
ninaondoka leo hii kurejea
Paris.Kabla sijaondoka
naomba unipeleke nikamuone
Gosu Gosu” akasema Peniela
na Mathew akamuogoza hadi
katika gari lake wakaondoka
kuelekea hospitali kumtazama
Gosu Gosu.
“Watoto
wanaendeleaje?akauliza
Mathew
“Kwa sasa wametulia
wanaendelea vizuri na
masomo na maisha yao kwa
ujumla lakini kwa miaka
miwili hapo nyuma walikuwa
wameathiriwa sana na kifo
chako”
“Ndiyo maana sitaki
wafahamu chochote kuhusu
mimi kuwa hai kwa sasa hadi
hapo baadae.Nakuomba tena
usiwaeleze chochote kuhusu
mimi” akasema Mathew
“Sintawaeleza chochote
kwani watachanganyikiwa
zaidi”
“Peniela …” akaita Mathew
“Unasemaje Mathew?
“Naomba ufahamu
hayakuwa mategemeo yangu
maisha yetu yawe namna
hii.Sikutegemea kama siku
moja tungemaliza mahusiano
yetu namna h……” akasema
Mathew na Peniela
akamkatisha
“Mathew tumekwisha
yamaliza hayo kitu cha msingi
ni kutazama yale ya mbele
yetu.Muda wowote ukihitaji
kitu chochote tafadhali usisite
kuniambia.Namba yangu ya
simu ni ile ile”akasema Peniela
“Am I doing the right
thing?akajiuliza Peniela na
kumtazama Mathew kwa jicho
la wizi
“Namuonea huruma sana
Mathew kwa mambo
anayoyapitia.Mwili wake
umeumizwa vibaya sana hadi
nilisisimkwa mwili nilipoyaona
makovu yale katika mwili
wake.Sikuufahamu ukweli na
nikadhani alitengeneza kifo
chake kumbe alikuwa katika
mateso.Nimechanganyikiwa.N
ifanyaje wakati tayari
amekwisha saini hizi
karatasi?Nilimtamkia maneno
mabaya sana yaliyomuudhi
hadi akaamua kunipiga kitu
ambacho hajawahi kukifanya
toka tumekuwa wapenzi.I was
so stupid.Nilikurupuka sana
kufanya maamuzi kama haya
kwa mtu kama huyu ambaye
amekwisha fanya mambo
mengi sana kwa ajili
yangu.Amesimama nami
katika nyakati ngumu ambazo
hakuna
aliyewezaa,amenivumilia kwa
mengi,huyu ni mwanaume wa
kipekee kabisa na ninaumia
kwa hiki nilichokifanya lakini
maamuzi haya ni kwa faida
yetu sote.Mathew amechagua
kuendelea na kazi yake ya
ujasusi” akaendelea kuwaza
Peniela.
Walifika katika hospitali
kuu ya Mtodora alikolazwa
Gosu Gosu.Mathew akafanya
mpango na Peniela
akaruhusiwa kuingia kwenda
kumuona Gosu Gosu
akamwaga machozi
alipomuona akiwa amelala
kitandani hana fahamu.Baada
ya kutoka kumuona Gous Gosu
Mathew akampeleka katika
chumba alimolazwa Austin
akamtambulisha kwa Peniela.
“Huyu ndiye aliyejitolea
sehemu ya ini alilopandikizwa
GosuGosu” akasema Austin na
Peniela akamshukuru kwa kile
alichokifanya.Baada ya zoezi
hilo kukamilika Peniela
hakuwa na kitu cha ziada
ulikuwa ni wakati wake wa
kuondoka kurejea
Paris.Mathew akamsindikiza
uwanja wa ndege
“Nimeumizwa sana na hali
ya Gosu Gosu.Nakuahidi
nitakwenda kutafuta taarifa za
kuhusu Melanie Davis na
nitakujulisha” akasema
Peniela wakiwa garini
“Ahsante sana” akasema
Mathew
Hakukuwa na
mazungumzo mengi garini
hadi walipofika uwanja wa
ndege wa Julius
Nyerere.Mathew akashuka na
kumfungulia Peniela mlango
“Penny this is it.” Akasema
Mathew
“Mathew thank you for
everything” akasema Peniela
wakakumbatiana na kwa mara
ya mwisho Mathew akambusu
Peniela
“Please go and don’t look
back” akasema Mathew na
Peniela akaelekea ndani ya
jengo la uwanja wa ndege wa
Julius Nyerere huku machozi
yakimdondoka.
Mathew hakuondoka pale
uwanjani hadi alipoiona ndege
ya Peniela yenye maandishi
makubwa Penny air ubavuni,
ikipaa na kuondoka.
“Kwa heri
Peniela”akasema Mathew na
kuingia katika gari lake
akaondoka.
“Naona kama ndoto lakini
ni kweli nimeachana na
Peniela.Nimetoka naye
mbali,tumepitia mengi na
hatimaye safari yetu
imehitimishwa rasmi
leo.Inaniumiza kuacha na mtu
ambaye niliahidi kuishi naye
hadi kifo lakini ahadi hiyo
imeshindwa kutimia” akawaza
Mathew
Kutoka uwanja wa ndege
wa Julius Nyerere akarejea
nyumbani kwake akaenda
moja kwa moja chumbani
kwake na kuchukua albamu
lenye picha mbali mbali
alizowahi kupiga na Peniela na
familia yake.
“Tumewahi kuwa na
nyakati nyingi nzuri lakini kwa
sasa sina hakika kama
ninaweza tena kumfanya
Peniela awe na furaha.Siwezi
kumlaumu kwa maamuzi
aliyoyachukua.Natakiwa
kusonga mbele na maisha
yangu” akawaza Mathew na
kumpigia simu Ruby
akamjulisha kilichotokea kati
yake na Peniela na Ruby
akamuahidi kwamba
atamfuata nyumbani kwake.
Ndege ya Peniela ilipokaa
sawa angani akachukua simu
yake ya intaneti akampigia
mtu Fulani na simu
ikapokelewa
“Peterson ni mimi
Peniela.Ninapozungumza
nawe hivi sasa niko
Afrika.Niliondoka jana jioni
lakini kwa sasa niko angani
narejea Paris”akasema Peniela
“Peniela pole kwa safari
ndefu” akasema Yule jamaa
aliyekuwa akizungumza na
Peniela simuni
“Nashukuru
Peterson.Nimekupigia simu
kuna kazi muhimu nataka
unisaidie kuifanya.Kuna mtu
mmoja anaitwa Melanie
Davis.Huyu anatajwa kuwa
mmoja wa mabilionea wa jiji la
Paris.Nataka umfanyie
uchunguzi wa kina na kesho
asubuhi uniletee ripoti
nyumbani” akasema Peniela
“Peniela nini hasa
unachotaka tukichunguze kwa
huyo Melanie Davis? Akauliza
Peterson
“Kila kitu kuhusu maisha
yake.Ametokea wapi,wazazi
wake,anakoishi hapa
Paris,anafanya biashara gani
na ziko wapi,akaunti zake za
benki,marafiki zake ni akina
nani wanafanya nini
n.k.Nataka kujua kila kitu
mnachoweza kukipata kuhusu
Melanie”akasema Peniela
“Sawa mama Peniela.Hiyo
ni kazi ndogo sana
kwetu.Kesho saa kumi na mbili
za asubuhi nitakugongea
mlango kukupa ripoti”
akasema Peterson na kuagana
na Peniela
“Ngoja niwatumie hawa
wapelelezi wa kujitegemea
kumchunguza
Melanie.Mathew amenistua
sana kuniambia kwamba
anashirikiana na magaidi wa
IS.Lakini Melanie ni
mwanamke mwenye uzuri wa
kipekee kabisa kwa nini
anashirikiana na magaidi wa
IS?Kinachoniumiza zaidi ni
kwamba anajificha nyuma ya
biashara nilizomuuzia
kutekeleza mambo
yake.Mathew aliniambia
kwamba amekuwa akipokea
kiasi kikubwa cha fedha
kutoka IS.Yawezekana ni fedha
hizo hizo ndizo ambazo
alizitumia kununulia kampuni
nilizomuuzia.Imeniuma sana
na ninajiona mjinga.Niliona
aibu kubwa mbele ya Mathew
aliponiuliza sababu ya kuuza
mali zetu kwa mtu
anayeshirikiana na magaidi.”
akawaza Peniela na sura ya
Mathew ikamjia akaanza
kutiririkwa machozi
“Mathew amepitia mateso
makubwa sana kwani mwili
wake wote umejaa makovu ya
vidonda vilivyotokana na
mateso makali aliyokuwa
akiteswa.Kwa nini lakini
Mathew ameamua kuchagua
kuendelea kufanya kazi hii na
kuacha maisha mazuri
aliyokuwa akiishi?akajiuliza
Peniela
“Mathew amenifanya
niwachukie magaidi na watu
wanaowasaidia kama akina
Melanie kwani ndio
waliomfanya Mathew
ashindwe kutulia na kutumia
muda wake mwingi
akihangaika kupambana nao
hadi kufikia hatua hii ya
kutengana” akawaza Peniela