SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 7: EPISODE 3
Kikao cha faragha baina ya
marais wa Tanzania,Rwanda na
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo kilichochukua saa tatu
kilimalizika halafu marais wote
watatu wakajitokeza mbele ya
waandishi wa habari waliokuwa
wamekusanyika ikulu
wakisubiri kikao kile kimalizike
ili wapate walau neno kutoka
kwa marais wale.Toka
lilipotokea shambulio lile baya
Rais wa Tanzania Dr Fabian
hakuwa amezungumza
lolote.Vituo karibu vyote vya
matangazo vilikatisha
matangazo yao na kujiunga
moja kwa moja ikulu kusikiliza
hotuba ya Rais.
Ndani ya ukumbi watu
wote wakasimama baada ya
marais kuingia.Mkurugenzi wa
mawasiliano ya Rais
hakupoteza muda
akamkaribisha moja kwa moja
Rais Dr Fabian aweze kusema
neno kwa niaba ya marais
wenzake wa Rwanda na
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo.
“Poleni sana ndugu
waandishi wa habari kwa
kutusubiri muda
mrefu.Tulikuwa na kikao kizito
kidogo ndiyo maana
tumechelewa” akasema Dr
Fabian halafu akaitazama
karatasi yake na kuendelea
“Ndugu wanahabari awali
ya yote nipende kuwashukusu
sana kwa kufika kwenu kwa
wingi.Nimeelezwa kwamba
wengi wenu mmefika hapa toka
asubuhi lakini hamjakata tamaa
kusubiri ili kuwapelekea
watanzania taarifa” akasema Dr
Fabian na kunyamaza kidogo
halafu akaendelea
“Ndugu zangu siku ya jana
nchi yetu na jumuiya ya Afrika
Mashariki imepata pigo
kubwa.Watu wasio na hata
chembe ya huruma wamefanya
shambulio ambalo limepelekea
mauaji ya watu hamsini na saba
kupoteza maisha na miongoni
mwao ni wake za marais wa
Rwanda,jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo na mke
wangu mimi,pia mabalozi wa
Rwanda na jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo wao
wanaoziwakilisha nchi zao hapa
nchini pamoja na familia zao
wamepoteza maisha.Hili ni
moja ya tukio baya kabisa.
Tukio hilo lilitokea
nyumbani kwa balozi wa
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo ndugu Germinus Mapupu
ambapo walikuwa
wamehudhuria hafla ya chakula
cha jioni ambacho balozi
Germinus Mapupu alikuwa
amekiandaa kwa ajili ya bi
Rebeca Muyenga mke wa Rais
wa Congo na Agatha Ntezimana
mke wa Rais wa Rwanda.Lengo
kubwa la kuandaa chakula
hicho lilikuwa ni
kuwakutanisha pamoja wake
hao za marais ikiwa ni katika
jitihada za kuondoa tofauti
zao.Kama mnavyofahamu kwa
muda sasa nchi za Rwanda na
Congo hazina maelewano
mazuri na balozi Mapupu
alitaka kutumia fursa hii
ambayo wake hao za marais
wote wanakutana hapa Dar es
salaam kwa ajili ya kuanza
mchakato wa kutafuta
maelewano baina ya nchi zao
lakini lengo lake hilo jema
halikuweza kufanikiwa kwani
wote waliuawa.Ni ukatili
mkubwa sana ambao
haukubaliki.
Baada ya tukio lile la mauaji
hayo ya kinyama mtu anayejiita
James Kasai alijitokeza na
kusambaza video akidai
kuhusika katika shambulio hilo
akishirikiana na kikundi cha
kigaidi cha IS ambacho kwa
miaka ya karibuni kimekuwa
kikijiimarisha sana katika bara
la Afrika hususan ukanda huu
wa Afrika Mashariki.Si mara ya
kwanza kwa kikundi cha IS
kufanya shambulio katika nchi
yetu.Watanzania bado
hawajasahau kitendo
walichokifanya IS miaka
michache iliyopita pale
walipoteka wanafunzi na
kuwachinja kama kuku na sasa
wamerejea tena” Dr Fabian
akanyamaza kwa sekunde
chache halafu akasema
Huyu mtu anayeitwa James
Kasai ni nani? Akauliza Dr
Fabian na kunyamaza akameza
mate
“James Kasai anatokea
nchini Jamhuri ya kidemokrasia
ya Congo na anaongoza kikundi
cha waasi ambao kwa miaka
zaidi ya kumi wamekuwa
wakipigana na
serikali.Alipoingia madarakani
Rais Patrice Eyenga aliwaita
mezani viongozi wa makundi
yote ya serikali ambayo kwa
miaka mingi yalikuwa
yakipigana na serikali kwa
lengola kutafuta amani lakini ni
James Kasai pekee ambaye
alikataa kushiriki katika
majadiliano ya kuleta amani ya
Congo na aligoma kuweka
silaha chini hivyo akafurushwa
na jeshi la Congo na inaaminika
alikimbilia katika misitu ya
Kaskazini mwa Uganda na sasa
ameamua kushirikiana na
kikundi cha kigaidi cha IS na
kufanya shambulio baya katika
ardhi yetu.James Kasai
amekuwa ni tishio kubwa si
kwa Tanzania tu bali kwa
jumuiya nzima ya Afrika
Mashariki na hatuwezi
kumuacha akaendelea kuwa
tishio kwa nchi zetu lazima
uovu wake ufike mwisho
Mimi na wenzangu marais
wa Rwanda na jamhuri ya
kidemokrasi ya Congo
tumekuwa na kikao kizito cha
faragha na katika kikao hicho
tumeazimia kuunganisha nguvu
kuhAkikisha tunampata James
Kasai akiwa mzima au
amekufa.Kila nchi itatoa kikosi
cha wanajeshi na tutaunda
kikosi kimoja ambacho
kitakuwa na silaha na zana kali
za kivita ambacho kitakwenda
kumsaka James Kasai kokote
aliko.Kitapanda milima na
mabonde,kitavuka mito na
bahari,misitu na nyika na
kuhAkikisha James Kasai
anatikana akiwa mzima au
mfu.Narudia tena tutapanda
milima na mabonde,tutavupa
mito na bahari,misitu na nyika
tukimsaka James Kasai na
lazima tumpate akiwa mzima au
amekufa.
Tunaamini James Kasai
yuko katika misitu iliyo
Kaskazini mwa Uganda na
tunaamini serikali ya Uganda
wanalifahamu hilo lakini
wamekuwa wakimkingia kifua
hivyo basi tunaitaka serikali ya
Uganda ihAkikishe
inashirikiana na kikosi ambacho
kitaundwa kwa ajili ya
kumtafuta James Kasai.Mtu
huyu mkatili asiye na hata
chembe ya ubinadamu yuko
ndani ya jumuiya ya Afrika
Mashariki na kwa mujibu wa
taratibu za jumuiya ya Afrika
Mashariki kunapotokea kitisho
chochote katika mojawapo ya
nchi wanachama basi nchi
nyingine zote wanachama
hujitolea vikosi vya jeshi
ambavyo vitakwenda
kupambana kuhAkikisha
kwamba nchi hiyo inakuwa
salama.James Kasai ni hatari si
kwa jamhuri ya kidemokrasia
ya Congo pekee bali kwa
jumuiya nzima ya Afrika
Mashariki hivyo nchi
wanachama zinatakiwa
kuunganisha nguvu kupambana
na adui huyu na ninawaahidi
wana Afrika mashariki
tutamfutilia mbali James
Kasai.Siku zake zinahesabika”
Dr Fabia akanyamaza baada
ya mpambe wake kumsogelea
na kumpa kijikaratasi
kilichosomeka
“Miili iko tayari kuelekea
uwanja wa ndege”
Dr Fabian akakisoma
kijikaratasi kile halafu
akaendelea na hotuba yake
Narejea tena kuwapeni pole
wana jumuiya ya Afrika
Mashariki kwa msiba huu mzito
uliotupata.Mimi nikiwa
mwenyekiti wa jumuiya hii
ninawahAkikishia kwa
kushirikiana na wenzangu
tutahAkikisha jumuiya yetu
inakuwa salama.TutahAkikisha
hakuna tena kitisho chochote
cha namna hii na watu kama
hawa wanaondolewa haraka
sana katika jumuiya yetu pale tu
wanapoibuka.
Mungu ibariki Afrika
Mashariki
Ahsanteni kwa kunisikiliza
Dr Fabian akamaliza hotuba
yake fupi na hakukuwa na
nafasi yoyote ya kuuliza
maswali.Akawaongoza wale
maraisi wenzake kutoka ndani
ya ukumbi ule wakaelekea nje
ambako magari yalikuwa
yameandaliwa na kwa pamoja
wakaondoka kuelekea uwanja
wa ndege wa Julius Nyerere
ambako miili ya marehemu
ilikuwa inapelekwa tayari kwa
kusafirishwa kuelekea katika
nchi zao.
Msafara wa marais watatu
uliwasili katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere ambako kuliandaliwa
shughuli maalum kwa ajili ya
kuaga miili ya marehemu kabla
ya kusafirishwa.Marais
walichukua nafasi zao
wakindelea kusubiri miili
iwasili.Watu walikuwa wengi
wakiwa wamekaa kwa utulivu
mkubwa na simanzi katika
mahema huku kwaya ikiwa
jukwaani ikiimba kuwafariji
.Ulinzi ulikuwa mkali mno eneo
lote la uwanja wa ndege.
Dakika chache baada ya
marais kuwasili pale uwanja wa
ndege wa Julus Nyerere magari
yaliyobeba majeneza yenye
miili ya marehemu yakawasili
na kufuata utaratibu majeneza
yakashushwa na
kupangwa.Viongozi wa dini
waliokuwepo mahala pale
wakapewa nafasi ya mwanzo ya
kuwaombea
marehemu.Hakukuwa na
hotuba yoyote iliyopangwa
kutolewa pale uwanjani hivyo
baada ya viongozi wa dini
kuwaombea marehemu
likafuata zoezi dogo la kuaga
miili ya
marehemu.Waliopangwa kuaga
miili ile pale uwanjani ni
wafanyakazi wa balozi za
Rwanda na jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo vile vile
raia wa nchi hizo wanaoishi
hapa nchini.Kulikuwepo vile
vile na kundi la wake za marais
walikuwa wamefika nchini
kuhudhuria mkutano wa wake
za marais ulioandaliwa na mke
wa Rais wa Tanzania marehemu
Millen Kelelo.Majeneza
hayakufunguliwa bali watu
walipita mbele yake kutoa
heshima za mwisho kwa
marehemu.Wakati zoezi
likiendelea,taratibu ndege mbili
za jeshi zilianza kusogea na
kujipanga vizuri.Zoezi la kutoa
heshima za mwisho kwa miili
ile ya marehemu lilimalizika na
wanajeshi wakasogea
wakabeba jeneza lenye mwili
wa marehemu Agatha
Ntezimana mke wa Rais wa
Rwanda wakaupeleka katika
ndege ya jeshi,ukafuatia mwili
wa balozi wa Rwanda na mke
wake pamoja na watu wengine
wa kutoka Rwanda waliouawa
katika shambulio.Lango la
ndege likafungwa na ndege
ikaondoka.Kikosi kingine cha
askari wakabeba jeneza lenye
mwili wa marehemu Rebeca
Eyenga mke wa Rais Patrice
Eyenga wa jamhuri ya
kidemokrasia na kuupakia
katika ndege ikafuatia miili ya
balozi Germinus Mapupu na
mingine ya watu kutoka
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo waliouawa katika
shambulio.Lango la ndege
likafungwa na ndege ikapaa
kuelekea Kinshasa.Lilikuwa ni
tukio lililoleta simanzi
kubwa.Dakika tatu baada ya
ndege za jeshi kuondoka,ndege
ya Rais Patrice Eyenga ikasogea
akakumbatiana na Dr Fabian
Kelelo pamoja na Rais Benjamin
Ntezimana kisha akaelekea
katika ndege yake ambayo
haikuchukua muda ikapaa na
kuondoka.Baada ya muda mfupi
ndege ya Rais Benjamin nayo
ikasogea akaagana na Dr Fabian
akapanda ndegeni naye
akaondoka kuelekea Kigali.
Rais Dr Fabian Kelelo
akaenda kuwasalimu
wanakwaya waliofika pale
kuwafarijji
waombolezaji,akasalimiana pia
na viongozi wa dini,akaagana na
baadhi ya wake za marais
waliokuwa wamekuja
kuhudhuria mkutano wa wake
za marais kisha akaondoka pale
uwanjani kurejea ikulu
“James Kasai ! akawaza Dr
Fabian akiwa garini.Jina hili
lilipita kichwani kwake kila
mara na kumfanya akunje sura
kwa hasira
“Bazazi huyu nitamfundisha
adabu.Hiki alichokifanya atalipa
kwa gharama kubwa sana”
akawaza na kuchukua simu
akazitafuta namba za simu za
Rais wa Uganda akampigia na
kuelezwa kwamba yuko katika
kikao muhimu
“Huyu ndiye ambaye
amemuhifadhi James Kasai
nchini Uganda japokuwa
amekuwa akikanusha vikali
kufanya hivyo lakini ukweli
tunao kwamba James Kasai
yuko nchini Uganda na sintajali
kama mimi na yeye ni
marafiki,tunakwenda kuvamia
Uganda kumtafuta James
Kasai.Sijali kitakachotokea
kama ni vita niko tayari
kuingiza nchi vitani lakini
lazima James apatikane”
akawaza Dr Fabian ambaye
sura yake ilitawaliwa na
majonzi makubwa.
Alipokaribia kufika ikulu
simu yake ikaita alikuwa ni
Jenerali Akiki Rwamirama Rais
wa Uganda.Dr Fabiana
akaitazama simu ile kwa hasira
kisha akaipokea
“Hallow mheshimiwa Rais”
akasema Dr Fabian
“Dr Fabian nimeikosa simu
yako nilikuwa katika kikao
muhimu”
“Mheshimiwa naomba
nikupigie simu baada ya dakika
tano” akasema Dr Fabian na
kukata simu.Gari lilifika ikulu
akashuka na kuelekea
chumbani kwake akachukua
simu na kuvuta pumzi ndefu
kisha akampigia Jenerali Akiki
“Dr Fabian habari yako.Pole
sana kwa tukio lililotokea.Mara
tu nilipopata taarifa za tukio lile
nilikupigia simu kukupa pole
lakini simu yangu
haikupokelewa.Kwa niaba ya
wananchi wa Uganda ninakupa
pole sana kwa tukio
lililotokea.Tuko pamoja na
msiba huu ni wetu sote.Pole
sana mheshimiwa Rais”
akasema Jenerali Akiki na sura
ya Dr Fabina ikajikunja kwa
hasira
“Jenerali Akiki hauko
pamoja na sisi na
usinidanganye kwamba msiba
huu umekugusa!
“Kwa nini unasema hivyo
mheshimiwa Rais? Sisi ni
ndugu.Uganda na Tanzania tuna
mahusiano ya kindugu hivyo
msiba huu ni msiba wa
Tanzania ni msiba wa Uganda
na ni msiba wa Afrika
mashariki.Uganda tunalia kama
mnavyolia watanzania Congo na
Rwanda” akasema Jenerali
Akiki
“Kama kweli msiba huu
umekugusa nataka unieleze
mahala alipo James Kasai !
akasema Dr Fabian
“James Kasai?
“Ndiyo.Humfahamu?
“Ninamfahamu James Kasai
lakini hayupo Uganda !
“Usinidanganye Jenerali
Akiki.James Kasai yuko Uganda
na umempa hifadhi”
“Hilo si kweli Dr
Fabian.James Kasai hayupo
nchini Uganda.Taarifa
nilizonazo ni kwamba James
Kasai amejificha katika misitu
ya Congo.Tafadhali usiziamini
taarifa zinazotolewa na Congo
na Rwanda wakidai kwamba
James Kasai yuko Uganda”
“Jenerali Akiki,tunao
ushahidi wa kutosha kwamba
James yuko nchini Uganda na
kwa kuwa hutaki kuweka wazi
mahala alipo,sisi tunaandaa
kikosi ambacho kitaingia katika
misitu ya Uganda kuendesha
operesheni ya kumsaka.Itakuwa
ni operesheni kubwa kuwahi
kufanywa na vikosi vya afrika
mashariki.Tutapita msitu kwa
msitu hadi tuhAkikishe James
Kasai anapatikana akiwa mzima
au mfu ! akasema Dr Fabian
ambaye uso wake ulionyesha
hakuhitaji masihara.Zilipita
sekunde kadhaa Jenerali Akiki
akasema
“Usiku wa kuamkia
jana,ndege za jeshi la Rwanda
zilivamia anga letu na kufanya
mashambulizi katika vijiji
vilivyopo kandoni mwa misitu
iliyopo Kaskazini ambako
wanadai James Kasai
amejificha.Katika mashambulio
hayo watu tisa waliuawa na
vijiji kadhaa kharibiwa
vibaya.Vikosi vya jeshi letu la
anga vilifanikiwa kuangusha
ndege mbili za Rwanda
zilizoingia katika anga letu kwa
lengo la kufanya mashambulizi”
akanyamaza kidogo na
kuendelea
“Asubuhi ya leo
nimezugumza na vikosi vya
jeshi na nimeagiza vikosi vyote
vya jeshi vikae katka utayari wa
vita.Tayari nimepeleka vikosi
katika mpaka wetu na Rwanda
na muda wowote vikosi
vitaingia Rwanda kulipiza kisasi
kwa kile ambacho tunakiita ni
uchokozi mkubwa.Rwanda
wametuvamia na kuua watu
wetu bila hata kuwa na uhakika
kama kweli James Kasai yupo
nchini Uganda.Kitendo kile
hakivumiliki na hakiwezi
kuachwa hivi hivi lazima
tuchukue hatua kali ndiyo
maana nataka niifanye nchi ya
Rwanda kama mfano kwa wale
wengine wote ambao wanataka
kufanyia mchezo
Uganda.Naomba nikuweke wazi
Dr Fabian kwa kuwa wewe
ndiye mwenyekiti wa jumuiya
ya Afrika Mashariki kwamba
ninajiandaa kuingia katika vita
na Rwanda na nchi nyingine
yoyote ambayo itathubutu
kuvamia Uganda” akasema
Jenerali Akiki
“Jenereali Akiki tafadhal
usithubutu kufanya hicho
unachotaka
kukifanya.Ukithubutu kuivamia
kijeshi Rwanda basi nchi zote za
Afrika mashariki zitamuunga
mkono Rwanda”
“Hilo haliniogopeshi Dr
Fabian.Umekwisha nihAkikishia
kwamba mmekutana Dar es
salaam na marais wa Rwanda
na Congo na tayari mmepanga
kuivamia Uganda.Ninawaonya
msithubutu kufanya
hivyo.Msithubutu kamwe
kutuma wanajeshi wenu nchini
Uganda kwani hawatafika
kokote nitawafyekelea
mbali.Jeshi langu limekwisha
jiandaa na liko tayari kwa
vita.Siogopi kama
mtaunganisha nguvu lakini
nataka kukuhAkikishia jambo
moja kwamba jeshi langu linao
uwezo wa kupambana na
majeshi yenu yote.Nakuonya Dr
Fabian usiingize nchi yako
vitani utajutia uamuzi
wako.Jeshi la Uganda la sasa si
lile la Iddi Amin mliyemchakaza
wakati ule.Hili ni jeshi jipya
ambalo lina uwezo wa
kupambana na majeshi ya nchi
yoyote.Ninawakaribisha
wanajeshi wenu lakini chimbeni
makaburi ya kutosha kwani
hakuna atakayerejea nyumbani
salama.Hakuna ambaye
atavamia ardhi ya Uganda
akatoka akiwa salama.Hivi si
vitisho nazungumza ukweli na
kama hamuamini
ninachokisema basi subirini
muone kile kitakachotokea
nchini Rwanda ! akasema
Jenerali Akiki na kukata simu
“Aaagh !! akasema kwa
hasira Dr Fabian
“Hakuna nchi yoyote ndani
ya Afrika Mashariki inayoweza
kuitisha Tanzania kijeshi.Akiki
akitaka kupigana na Tanzania
utakuwa ndio mwisho
wake.Tutatuma kwanza kikosi
cha umoja kwenda kumtafuta
James Kasai na kama
ikionekana upo ulazima basi
nitalituma jeshi la wananchi
kwenda Uganda lakini
operesheni kama hii ni
ndogo.Kikosi kidogo tu
kitakwenda kikishirikiana na
vikosi vingine kutoka Rwanda
na Congo” akawaza Dr Fabian
na simu yake ikaita akajulishwa
kuwa anahitajika katika kamati
ya maandalizi
KAMPALA – UGANDA
Baada ya kumaliza
mazungumzo na Dr
Fabian,Jenerali Akiki akampigia
simu James Kasai
“Mheshimiwa Rais”
akasema James Kasai
“James nimekupigia
tena.Nimetoka kuzungumza na
Rais wa Tanzania muda mfupi
uliopita na mazungumzo yetu
hayakwenda vizuri.Kwa mara
ya kwanza tumefokeana na
kutoleana vitisho vya
kushambuliana kijeshi.Jambo
lingine ni kwamba marais wa
Congo na Rwanda wote
wamekutana nchini Tanzania
na kwa pamoja wamekubaliana
kuunda kikosi ambacho
kitafanya operesheni ya kijeshi
kukusaka.Hivi tuzungumzavyo
tayari maandalizi ya kikosi
hicho yameanza na pale
kitakapokuwa tayari kitatumwa
Uganda.Wanafahamu mahala
vilipo vikosi vyako hivyo kwa
usalama wao nakuomba
uviondoe ili kikosi hicho
kitakapofika wakute tayari
wamekwisha ondoka” akasema
Jenerali Akiki
“Nimekuelewa mheshimiwa
Rais na tayari maandalizi
yamekwisha anza ya
kuondoka.Nategemea usiku wa
leo vijana wataanza
safari.Nitakujulisha pale
watakapokuwa wameanza
kuondoka”
“Vizuri sana.Endapo kuna
msaada wowote utauhitaji
usisite kunijulisha mara moja
nitakusaidia” akasema Jenerali
Akiki
“Nashukuru sana
mheshimiwa Rais kwa kila
kitu.Pale nitakapokuwa na
uhitaji wa chochote basi
nitakujulisha” akasema James
Kasai na kuagana na Rais.
“Pamoja na umuhimu wake
kwetu lakini James Kasai
ameniingiza katika matatizo
makubwa sana.Amevuruga
mahusiano yetu mazuri na nchi
nyingine za Afrika Mashariki na
hadi tumefikia hatua ya
kutishiana kijeshi.Sikupenda
kabisa kulumbana na Rais wa
Tanzania ambao wamekuwa ni
ndugu zetu kwa miaka mingi
lakini imelazimu kufanya hivyo
kwa ajili ya kumlinda
James.Sitaki kuingia katika vita
na Tanzania kwani ina jeshi
bora mno…” akawaza Jenerali
Akiki na kukuna kichwa.
“Kwa sasa mambo
yamekwisha haribika
nimekwisha tunisha misuli
hivyo sitakiwi kulegea.Natakiwa
kuendelea kutunisha misuli ili
kuonyesha kweli nimedhamiria
kupigana na jeshi la nchi yoyote
ambayo itathubutu kuvuka
mpaka na kuingia Uganda.Kwa
nchi ya Rwanda lazima niipe
onyo ili siku nyingine wasirudie
kitendo walichokifanya cha
kuvuka mpaka na kushambulia
Uganda” akawaza Jenerali Akiki
na kumpigia simu waziri wa
mambo ya nje wa Uganda
akamtaka awarejeshe
nyumbani mabalozi wa Uganda
walioko katika nchi za Rwanda
na jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo na vile vile akamtaka
awaelekeze mabalozi
wanaoziwakilisha nchi hizo
nchini Uganda waondoke
haraka sana Uganda ndani ya
saa ishirini na nne.
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Ilikaribia saa moja za jioni
jijini Dar es salaam muda
ambao Melanie Davis alikuwa
akijiandaa kwenda nyumbani
kwa Gosu Gosu kwani
waliahidiana kukutana jioni ya
siku ile kwa ajili ya
mazungumzo.Akiwa chumbani
kwake akijiandaa simu yake
ikaita akatazama mpigaji
alikuwa ni katibu wake muhtasi
Frimina
“Mina unasemaje?akauliza
Melanie
“Madam kuna tatizo”
akasema Frimina na Melanie
akastuka kidogo
“Kuna tatizo gani? akauliza
“Nimepata taarifa muda si
mrefu kwamba Gosu Gosu
amepigwa risasi”
“Gosu Gosu ! Oh my God !
Melanie akastuka sana na
kuangusha kifaa alichokuwa
amekishika mkononi
“Madam Melanie ! akaita
Frimina
“Mina kuna kitu kimoja tu
ambacho nataka kukisikia
kutoka kwako.Is he okay?
“Nimeambiwa kwamba
amekimbizwa hospitali na hali
yake ni mbaya sana”
“Yuko hospitali
gani?akauliza Melanie
“Nimeambiwa amepelekwa
hospitali kuu ya Mtodora”
akasema Frimina na Melanie
akahisi miguu yake inaisha
nguvu akakaa kitandani.
“Gosu Gosu jamani !
akasema Melanie.Hakupoteza
muda akachukua mkoba wake
na kutoka mbio akamfuata
Joyce akamtaka ampeleke
katika hospitali ya Mtodora
“Gosu Gosu tafadhali
naomba usiniache.Bado
ninakuhitaji sana katika maisha
yangu.Una umuhimu mkubwa”
akawaza Melanie huku machozi
yakimporomoka
“Ni nani hawa waliompiga
risasi Gosu Gosu na kwa nini?
Akaendelea kujiuliza maswali.
“Endapo Gosu Gosu
akifariki dunia litakuwa ni pigo
lingine kubwa kwa upande
wangu.Ni mtu ninayemtegemea
kwa mambo mengi.Kama si
yeye nisingeweza kuonana na
James Kasai.Ni yeye ambaye
kila wakati anaifanya akili
yangu ikae sawa.Ni mtu
muhimu sana katika maisha
yangu” akaendelea kuwaza
huku gari likiwa katika mwendo
mkali kuelekea hospitali.Mara
kwa mara alivua miwani na
kufuta machozi
“Gosu Gosu kupigwa risasi
imetonesha kidonda
changu.Kitendo hiki
kimenikumbusha machungu ya
wazazi wangu.” akawaza na
kuendelea kufuta machozi
Walifika katika hospitali ya
Mtodora na Melanie akashuka
na kukimbia hadi katika jengo
la mapokezi akajitambulisha
kuwa ndugu yake amepigwa
risasi na ameletwa pale
hospitali.
“Kuna wagongwa kadhaa
wamepokelewa hapa hospitali
jioni hii wakiwa na majeraha ya
sirasi.Ndugu yako anaitwa
nani?akauliza muuguzi wa
mapoezi
“Gosu Gosu”akatamka
Melanie na Yule muuguzi
akatazama katika kompyuta
yake
“Papi Gosu Gosu” akasema
Yule muuguzi
“Ndiyo”
“Mgonjwa wako yuko hapa
hospitali lakini kwa sasa
ameingizwa katika chumba cha
upasuaji” akasema Yule
muuguzi na kumuelekeza
Melanie kilipo chumba cha
upasuaji kisha kwa haraka
akiwa na Joyce wakaelekea
huko.
Mlango wa chumba cha
upasuaji ulikuwa umefungwa
na hakuruhusiwa mtu
asiyehusika kuingia ndani ya
chumba kile hivyo kuwalazimu
akina Melanie kusubiri nje.
“Ee Mungu naomba
umponye Gosu Gosu” hii ndiyo
kauli ambayo Melanie alibaki
anaitamka kimoyo
moyo.Alishindwa kukaa
akanyanyuka na kuanza
kuzunguka zunguka
“Madam Melanie kaa
upumzike tafadhali.Hatujui
upasuaji huo utachukua muda
gan..” akasema Joyce na mara
mlango ukafunguliwa akatoka
muuguzi mmoja aliyevaa
mavazi ya kijani Melanie
akamkimbilia
“Dada samahani” akasema
Melanie na Yule muuguzi
akasimama
“Ndugu yangu ameingizwa
humu kufanyiwa upasuaji
amepigwa risasi vipi hal….”
“Bado yuko kwenye
upasuaji.Endeleeni kusubiri
hadi upasuaji ukimalizika
mtajulishwa kila kitu” akasema
Yule mwanadada na kuendelea
na safari
“Madam Melanie kaa utulie
utachoka sana ukiendelea
kusimama.Yawezekana
upasuaji ukachukua muda
mrefu” akasema Joyce
“Nashindwa kukaa
Joyce.Ninapata wakati mgumu
sana” akajibu Melanie na
kuchukua simu akampigia
Frimina
“Frimina tayari niko hapa
hospitali lakini Gosu Gosu
ameingizwa katika chumba cha
upasuaji niko hapa na Joyce
tunasubiri upasuaji
umalizike.Nataka uniambie
tukio hili limetokea wapi?
“Gosu Gosu leo hakuwepo
kazini kwa siku nzima lakini
jioni ya leo alikuja ofisini kwake
kuna vitu alikuja kuchukua
akaniaga kwamba atakuwa na
safari ya Paris kesho
kutwa.Muda mfupi baada ya
kuondoka nikapigiwa simu na
walinzi kwamba Gosu Gosu
amepigwa risasi wakati
akijiandaa kuingia barabara
kuu.Inadaiwa kwamba
walijitokeza watu wawili
waliokuwa na pikipiki kubwa
wote wakiwa wamevaa mavazi
meusi na kofia ngumu kichwani
hivyo sura zao hazikuweza
kuonekana.Mmoja aliyekuwa
nyuma alikuwa na bunduki
ndogo akaanza kulimiminia
risasi gari la Gosu Gosu huku
mwenzake akimimina risasi juu
kuzuia watu wasisogee eneo lile
na baada ya kuhAkikisha
kwamba wamemimina risasi za
kutosha wakaondoka na hakuna
mpaka sasa aliyewatambua
watu hao ni akina nani”
akasema Frimina
“Dah ! akasema Melanie na
kushika kiuno
“Ahsante
Frimina.Nitaendelea
kuwasiliana nawe kuhusiana na
kile kinachoendelea hapa”
akasema Melanie na kukata
simu
“Ni nani hawa
waliomshambulia Gosu
Gosu?Nini walikuwa
wanakihitaji kutoka
kwake?Nadhani hawa jamaa
lengo lao lilikuwa ni kumuua tu”
akaendelea kuwaza
Walikaa pale nje kwa muda
wa saa tano ndipo alipotoka
daktari na kuwapa taarifa
“Poleni sana kwa
kusubiri.Tumefanya upasuaji
wa kuondoa risasi mwilini mwa
mgonjwa wenu.Jumla alikuwa
amepigwa risasi kumi na mbili
katika sehemu mbali mbali za
mwili wake.Risasi mbili
alipigwa katika bega la
kulia,risasi moja katika kiganja
cha mkono wa kulia,saba katika
sehemu ya juu ya paja,na mbili
sehemu ya chini ya mguu wa
kulia.Inaonekana mshambuliaji
alikuwa upande wa kulia kwani
ndio hasa
ulioshambuliwa.Risasi nyingine
zaidi ya kumi hazikuweza
kuingia mwilini mwake kwa
kuwa alikuwa amevaa fulana
isiyopenya risasi na bila fulana
hiyo asingeweza kuwa hai hadi
sasa kwani inaonekana
washambuliaji hao walikuwa na
lengo la kuua kabisa.Kwa sasa
atapelekwa katika chumba cha
uangalizi maalum huku
tukiangalia hali yake kwa
ukaribu zaidi” akasema daktari
“Daktari nakushukuru sana
kwa kazi kubwa mliyoifanya
lakini naomba ufanye kila lililo
ndani ya uwezo wako
kuhAkikisha ndugu yangu
anapona na kama utaona kuna
ulazima wa kumpeleka nje ya
nchi basi usisite kunishauri
hivyo daktari nakuomba sana”
akasema Melanie huku michirizi
ya machozi ikionekana machoni
pake
“Usijali mama.Ni kazi yetu
kuhAkikisha tunaokoa maisha
ya kila mgonjwa anayeletwa
hapa hospitali.Nakuahidi
kufanya kila lililo ndani ya
uwezo wangu kuhAkikisha
mgonjwa wako
anapona”akasema Melanie na
kuelekeza macho mlangoni
ambako mlango mkubwa
ulifunguliwa na kitanda
kikatolewa kikisukumwa na
wauguzi.Juu ya kitanda kile
alikuwa amelala Gosu Gosu
akiwa hana fahamu.Melanie na
Joyce wakawafuata wauguzi
wale hadi katika chumba cha
uangalizi maalum ambako akina
Melanie hawakuruhusiwa
kuingia kwa usiku ule
“Madam hakuna
tunachoendelea kukifanya hapa
twende nyumbani ukapumzike
kisha tutakuja tena kesho
alfajiri kujua maendeleo ya
mgonjwa.Kama kutakuwa na
mabadiliko yoyote wauguzi
wapo watatujulisha” akasema
Joyce
“Ni kweli Joyce.Twende
tukapumzike” akasema
Melanie.Joyce akazungumza na
wauguzi na kuwataka
wawajulishe endapo kutakuwa
na mabadiliko yoyote kwa
mgonjwa.
Waliondoka pale hospitali
huku kichwa cha Melanie
kikiwa kizito kwa mawazo
akijiuliza ni nani waliofanya
tukio lile na kwa nini Gosu Gosu
amepigwa risasi?
“Joyce twende nyumbani
kwa Gosu Gosu.Nataka
nikazungumze na mtumishi
wake wa ndani” akasema
Melanie na Joyce akaendesha
gari hadi nyumbani kwa Gosu
Gosu.Walinzi wote walikuwa
wakimfahamu hivyo
wakamkaribisha ndani na
kumuamsha mtumishi wa ndani
wa Gosu Gosu kama Melanie
alivyokuwa ameelekeza.
“Karibu sana mama
Melanie” akasema Yule
mtumishi ambaye alionekana
kutofahamu chochote
kilichokuwa kimetokea
“Ahsante nashukuru”
akasema Melanie
“Mama chumbani kwa kaka
kuko wazi kama unataka
kwenda lakini yeye bado
hajarudi hadi mida hii” akasema
Yule mtumishi
“Lucy hilo ndilo hasa
lililonileta hapa”akasema
Melanie na kunyamaza kidogo
“Nimetokea hospitali.Gosu
Gosu amepatwa na matatizo”
“Matatizo gani?akauliza
Lucy kwa mstuko
“Amepigwa risasi na watu
wasiojulikana” akasema
Melanie na Lucy akaangua kilio
“Tafadhali usilie Lucy.Gosu
Gosu hajafa lakini hali yake si
nzuri yuko katika chumba cha
uangalizi maalum baada ya
kufanyiwa upasuaji wa kuondoa
risasi alizokuwa amepigwa”
akasema Melanie na kumlazimu
Joyce kumbembeleza Lucy
anyamaze
“Nimekuja hapa kukupa
taarifa hizo kwani niliamini
bado hujazipata hata hivyo
kuna jambo nataka unisaidie
kulifahamu”
“Jambo gani?
“Nataka kujua kama kuna
mtu yeyote wa karibu wa Gosu
Gosu unayemfahamu aidha
ndugu au rafiki” akasema
Melane na Lucy akamtazama
kwa wasi wasi mkubwa.
“Usihofu Lucy Gosu Gosu ni
mzima” akasema Melanie baada
ya kuutambua wasiwasi
mkubwa aliokuwa nao Lucy
“Rafiki yake mkubwa
ambaye ninamfahamu anaitwa
Austin”
“Austin?
“Ndiyo”
“Anaishi wapi huyo Austin?
“Sifahamu anaishi wapi
lakini ninazo namba zake za
simu kama ukitaka kuwasiliana
naye” akasema Lucy na kwenda
chumbani akachukua simu yake
na kumpa Melanie namba za
simu za Austin akaziandika
katika simu yake akampigia
“Hallow” ikasema sauti ya
upande wa pili baada ya
kupokea simu
“Hallow Austin” akasema
Melanie
“Nani mwenzangu?
Akauliza Austin kwa mshangao
kidogo
“Naitwa Melanie
Davis.Unamfahamu Papi Gosu
Gosu?
“Ndiyo ni rafiki yangu.Kuna
nini? Akauliza Austin
“Naomba nikujulishe
kwamba Gosu Gosu amepatwa
na matatizo”
“Matatizo gani?
“Amepigwa risasi na watu
wasiojulikana jioni ya leo”
“Tafadhali
usinitanie”akasema Austin
“Si utani ni kitu cha kweli
kabisa.Alikimbizwa hospitali
amefanyiwa upasuaji na kwa
sasa amewekwa katika chumba
cha uangalizi maalum.Nimetoka
huko sasa hivi”akasema Melanie
“Wewe uko wapi hivi sasa”
akauliza Austin’
“Kwa sasa niko hapa
nyumbani kwake na mfanyakazi
wake Lucy ndiye aliyenipa
namba zako”
“Ahsante sana kwa taarifa
hii.Ninaelekea hospitali sasa
hivi” akasema Austin na
Melanie akakata simu akaagana
na Lucy wakaondoka kurejea
nyumbani.
Alipofika nyumbani kwake
akapitiliza moja kwa moja
chumbani akautupa mkoba
sofani “Kichwa kinaniuma
sana” akawaza Melanie na
kwenda kuchukua chupa ya
mvinyo akaenda kuketi sofani
na kuanza kunywa.Mara
akasikia mlio fulani ukitoka
katika mojawapo ya simu
yake.Ulikuwa ni mlio wa
kumfahamisha kwamba
kwamba kuna mtu alimpigia
simu lakini akamkosa.Akainuka
akaenda kuzitazama simu zake
na mojawapo ya simu
iliyopigwa ni ya Devotha.
“Devotha anataka nini
?Amepiga simu mara sita !
akawaza na kuamua kumpigia
“Hallo Devotha” akasema
Melanie baada ya simu yake
kupokelewa
“Hallo Melanie.How’s Gosu
Gosu?akauliza Devotha kwa
sauti yenye kicheko kidogo
ndani yake
“Gosu Gosu?
“Ndiyo anaendeleaje?Is he
dead? Akauliza Devotha na
Melanie akawa kimya huku
akihema haraka haraka.Sura
yake ilibadilika
“Sikiliza Melanie” akasema
Devotha
“Usihangaike kuumiza
kichwa chako nani waliompiga
risasi Gosu Gosu?My people
did” akasema Devotha
“What?! You wanted to kill
him?Why Devotha ?! akauliza
Melanie kwa uchungu
“Nilitaka kumuua kabla
hajaniua” akasema
Devotha.Melanie akastuka sana
kwa kauli ile ya Devotha
“Kwa nini unasema hivyo?
Akauliza Melanie
“Melanie Davis bado u
mchanga sana katika mambo
haya hivyo siku zote usitake
kushindana na wakubwa
zako.Ulidhani sintajua kama
umemtuma Gosu Gosu aje Paris
kuniua? Akauliza Devotha na
Melanie akawa kimya
“Nafahamu mipango yako
yote ninafuatilia kila
unachokifanya
Melanie.Ninafahamu Gosu Gosu
alikuwa aondoke kesho kuja
Paris kuniua.Ulifikiria nini
kumtuma Gosu Gosu aje kuniua
Melanie?Do you think it’s easy
to kill someone like me?
Akauliza Devotha huku akitoa
kicheko
“Bahati yake Yule jamaa
ana maisha marefu kama paka
lakini ule ni ujumbe kwamba
hata wewe ninaweza
nikakumaliza muda wowote
ninaotaka hivyo nataka uende
katika mstari tunaotaka
sisi.Nikikuelekeza fanya jambo
Fulani tekeleza na ukitaka
kwenda kinyume chake
matokeo yake hayatakuwa
mazuri.Hili ni onyo la mwisho
kwako na ukithubutu tena
kutaka kufanya mambo
unavyotaka wewe nitakuondoa
haraka bila kusita na
kumuweka mtu
mwingine.Umenisikia
Melanie?akauliza
Devotha.Melanie alikuwa
anatetemeka kwa ndani.
“Melanie umenielewa?
“Nimekuelewa”
“Good.Prepare yourself for
the next mission” akasema
Devotha na kukata simu.
“Oh my God ! akasema
Melanie na kuvuta pumzi ndefu
akaitupa simu kitandani
“Is this real or I’m
dreaming?akajiuliza
“Devotha amefahamuje
kama nimepanga mipango na
Gosu Gosu ya kwenda
kumuua?Kwa vyovyote vile
lazima kuna namna ambayo
amesikia mazungumzo
yetu.Hakuna mwingine ambaye
nimemueleza jambo hili zaidi ya
Gosu Gosu pekee.Nadhani ipo
namna ambayo hawa watu
wamefanya ili kuwawezesha
kufuatilia kila ninachokifanya
na kusikia kila
ninachokizungumza.Naamini
hivyo kwa sababu sifahamu
Devotha alifahamu vipi kuhusu
mimi kumfuata James Kasai?
Niliporejea kutoka Uganda
alinipigia na kunieleza kwamba
anafahamu nimetoka kuonana
na James Kasai.Nilijiuliza sana
amefahamu vipi sikupata jibu
lakini sasa nimefahamu.Swali
ninalojiuliza ni je kitu gani
wameniwekea ambacho
kinawafanya waweze
kunifuatilia kila
ninachokifanya? Kipo kitu
wameniwekea ambacho lazima
nikifahamu kwani bila
kukifahamu hakuna mpango
wangu utakaofanikiwa”
akawaza Melanie
Zaidi ya saa moja Melanie
alikuwa amekaa sofani akiwaza
namna Devotha anavyoweza
kunasa mazungumzo yake
akashindwa kupata jibu
“Kuna teknolojia kubwa
imetumika hapa na kufahamu
walichokifanya itanilazimu
nifanye majaribio
kadhaa.Kwanza nitahama hiki
chumba na kuhamia katika
chumba kingine ambacho
nitaweka kila kitu
kipya.Nitanunua kila kitu kipya
kuanzia mavazi hadi urembo.Hii
mikufu,heleni zote nitaziacha
sintazivaa tena yawezekana
kuna kifaa wameniwekea
ambacho kukibain itanichukua
muda mrefu.Nitaweka mfumo
mpya wa ulinzi katika chumba
change nitakachohamia ili
asiweze kuingia mtu mwingine
wakati sipo”akawaza Melanie
na kulala
RIYADH – SAUDI ARABIA
“Abu Zalawi unaonekana
kuguswa sana na tukio
lililotokea Tanzania.Umekuwa
unalifuatilia kwa karibu sana”
akasema Najma wakiwa
sebuleni ndani ya jumba lao
kubwa wakitazama runinga
huku Mathew akibadilisha
chaneli mbalimbali kutafuta
taarifa za kina za tukio
lile.Ulipita muda kidogo
Mathew akasema
“Fedha zile ulizosaini Dubai
kumtumia James Kasai ndizo
zimesababisha mauaji haya”
“Ni kweli.Tulipokwenda
Dubai nilisaini mkataba wa
kumtumia fedha James Kasai
ambaye ameingia mashirikiano
na kikundi cha IS.Usiniambie
umeguswa na kilichotokea
wakati nawe umewahi kuwa
gaidi na hizi ndizo zilikuwa
shughuli zenu kuua watu”
akasema Najma
“Uko sahihi nimepitia huko
katika ugaidi lakini kwa sasa
ninaanza kuondoka huko
taratibu”
“Usijali Abu Zalawi sisi kazi
yetu ni kutoa fedha kwa IS na
wanachokwenda kukifanya sisi
hakituhusu” akasema Najma
“Lakini ni ufadhili huu wa
fedha kwa vikundi vya kigaidi
ndiyo sababu inayomfanya
Habiba Jawad atafutwe sana na
mashirika makubwa ya kijasusi
duniani.Anatafutwa na
Mossad,CIA n.k. Kwa nini
tusiachane na mambo haya ya
kufadhili ugaidi tukaendelea na
maisha yetu ya kawaida?
Hatutakuwa na maisha ya
furaha na amani kama
tutaendelea na mambo haya ya
kufadhili ugaidi” akasema
Mathew akionekana kuumizwa
na kile kilichotokea Tanzania
“Abu Zalawi usiwe na hofu
sisi tuko salama”akajibu Najma
“Hatuko salama
Najma.Hujui ni namna gani
Habiba Jawad anatafutwa na
mataifa makubwa ambayo
yanaongoza katika kupiga vita
ugaidi duniani hasa Marekani
na Israel.Sikuwa nimekueleza
jambo hili lakini haikuwa rahisi
kuufikisha mwili wa seif Jawad
hapa.Majasusi wa Mossad
waliuwekea kifaa maalum cha
kuufuatilia kufahamu mahala
ulipo wakiamini kwamba
unaweza ukawasaidia kufika
kwa Habiba Jawad.Kwa bahati
nzuri niliweza kukigundua kifaa
hicho na kukiondoa.Kama
nisingeweza kukigundua mama
angekuwa katika matatizo
makubwa na yeye akiingia
katika matatizo sisi sote
mnakuwa kwenye
matatizo.Ninadhani ni wakati
wa mama Habiba kuachana na
mambo haya ya kufadhili ugaidi
akajielekeza katika biashara
zake” akasema Mathew Najma
akabaki kimya
“Najma mimi nilikuwa gaidi
na katika harakati zangu
nimekwisha ua watu wengi.Si
siku nyingi sana nililipua bomu
katika kituo cha treni jijini
Jerusalem na katika shambulio
lile watu wengi walipoteza
maisha.Baada ya kunusurika
katika mashambulio ya Israel
nilijiuliza nini sababu ya
kuendelea kuua watu?
Nimekuwa nikisoma
mafundisho mbali mbali ya dini
yetu na nimegundua kwamba
nilikuwa ninafanya kosa kubwa
kutumia kigezo cha dini
kuendesha mambo ya
kigaidi.Dini yetu ni dini safi na
hairuhusu ugaidi.Uislamu si
ugaidi bali wapo magaidi ndani
ya Uislamu.Binafsi nimeama
kuachana na mambo yale ya
ugaidi na kumcha mwenyezi
Mungu Subhanahu wa
ta’ala.Naamini hata wewe
ndicho kitu unachokitaka kwani
nakumbuka siku ile tukiwa
Dubai ulistuka sana baada ya
kuuona mgongo wangu na
ukanihAkikishia kwamba
maisha yale yamekwisha”
akasema Mathew
“Abu Zalawi hayo yote
uliyoyasema ninayafahamu na
ninatamani sana kutoka katika
maisha haya niishi maisha ya
kawaida ya amani.Hata mimi
sifurahii kufadhili ugaidi na kila
ninaposikia kundi Fulani la
kigaidi ambalo tunalifadhili
fedha limefanya shambulio
moyo wangu huumia sana
kwani katika mauaji hayo wapo
watoto,wanawake,wapo
waislamu na wasio
waislamu.Lakini mikono yangu
imefungwa na siwezi kufanya
chochote.Ninafuata maelekezo
ya mama.Kwa sasa mimi ndiye
ambaye amekuwa akinituma
sehemu mbali mbali
kumuwakilisha katika shughuli
zake mbali mbali na mikataba
mingi ya fedha mimi ndiyo
husaini badala yake”
“Ahsante sana Najma kwa
maneno hayo ambayo nilihitaji
sana kuyasikia.Lakini umewahi
kukaa na mama yako ukajaribu
kuzungumza naye kuhusiana na
athari za kufadhili ugaidi?
“Hapana sijawahi
kuzungumza naye
chochote.Kuna mambo ambayo
siwezi kuzungumza naye na
mojawapo ni suala hilo.Ni
mama yangu lakini Habiba
Jawad anatisha na akikasirika
wanasema huwa ni mbaya sana
ingawa sijawahi kumuona
akiwa amekasirika.Nasikia kuna
mambo ambayo ameyapiga
marufuku kuyazungumzia na
hilo ni kubwa ambalo hataki
lizungumzwe na neno la Habiba
Jawad ni amri” akasema Najma
“Nitazungumza naye kesho
juu ya suala hili” akasema
Mathew na Najma akamtazama
kwa mshangao
“Unataka kwenda
kuzungumza naye jambo hili?
“Ndiyo nitazungumza naye”
“Utaanzaje Abu
Zalawi?akauliza Najma
“Usihofu nitazungumza
naye kesho.Nitamfuata
nyumbani kwake” akasema
Mathew na Najma akaonyesha
wasiwasi kidogo
“Mbona unaonyesha hofu
Najma?
“Usimfuate nyumbani
kwake.Hapendi kufuatwa
kwake na kama ana jambo la
kukueleza basi atakuita yeye
mwenyewe.Labda umsubiri
atakapotoka kwenda kupata
kifungua kinywa ndipo uombe
kuzungumza naye lakini
usimfuate katika nyumba yake
ya kulala” akasema Najma
“Hujawahi kuingia katika
nyumba yake?
“Nimeingia mara nyingi
lakini pale tu yeye mwenyewe
aliponiita kwenda kuzungumza
au kunipa maagizo mbali mbali”
“Kwa nini hapendi watu
waingie ndani ya nyumba
yake?Kuna siri yoyote
anaificha?
“Mama yangu ni mtu
mwenye siri nyingi nadhani
ndiyo maana anachunga sana
watu kuingia ndani mwake.Kwa
mfano ofisi yake ipo ndani ya
jumba lake lakini hakuna
anayefahamu iko sehemu gani
bali yeye peke yake.Nasikia
kuna handaki ambalo anaweza
akajificha na kukaa humo hata
miaka mitano bila kutoka nje
lakini hakuna anayefahamu
mahala lilipo wala mlango wa
kuingilia.Kuna mtu mmoja tu
anayefahamu mengi kuhusu
jumba lile la mama naye ni bi
Nasrat Jazer.Huyu ninaambiwa
amekuwa mtumishi wa ndani
wa mama toka akiwa msichana
na hadi sasa amekuwa
mzee.Huyu ndiye ambaye
mama anamuamini sana kati na
ndiye pekee ambaye anaweza
akaingia na kutoka muda
wowote ndani ya jumba la
Habiba Jawad” akasema Najma
“Naj nakushukuru sana kwa
maelezo haya uliyonipa lakini
kesho nitamtafuta Habiba
nizungumze naye.Najua
haitakuwa rahisi kunielewa
lakini nitajaribu” akasema
Mathew akazima runinga na
kuelekea chumbani kulala.
“Nimeumizwa sana na tukio
lile la kigaidi nchini
Tanzania.Nilishuhudia wakati
fedha zikisainiwa ambazo
zimekwenda kumfadhili James
Kasai ambaye ametekeleza
shambulio lile.Kuua wake
watatu wa marais kwa mara
moja pamoja na mabalozi nini
hasa kusudio lake?Huyu James
anatokea jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo na
inasemekana anaishi nchini
Uganda kwa nini akashambulia
Tanzania ambayo kwa miaka
mingi imekuwa ni mhifadhi
mkuu wa wakimbizi wengi
kutoka nchini Congo?
Wanajeshi wa Tanzania
wamemwaga damu yao nchini
Congo wakiipigania amani ya
Congo kwa nini leo huyu mtu
mmoja aibuke na kufanya
mauaji yale makubwa?Au hii ni
mipango ya Habiba Jawad
kulipiza kisasi kwa kifo cha
mwanae Edger Kaka? Nadhani
ndilo hasa lilikuwa lengo lake
kumfadhili James Kasai fedha
nyingi ili aweze kufanya
shambulio lile.Nimeumizwa
sana na kitendo kile na ninaapa
lile litakuwa ni tukio la
mwisho.Sintakubali tena kundi
lolote la kigaidi kushambulia
Tanzania.Kesho nakwenda
kuzungumza na Habiba Jawad
anieleze ukweli kama
shambulio lile ni yeye ndiye
aliyelipanga na nini kusudio
lake?Nadhani uvumilivu
unaanza kunishinda siwezi tena
kuendelea kuvumilia kuona
ugaidi ukiendelea wakati ninao
uwezo wa kuzuia.Niko tayari
kupoteza maisha lakini niwe
nimemuua Habiba Jawad.Yule
mama bado hajanifahamu
vyema mimi ni kiumbe wa aina
gani” akawaza Mathew
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Saa kumi na mbili za
asubuhi juu ya alama ilimkuta
tayari Melanie amewasili
hospitali ya Mtodora kwenda
kumtazama Gosu
Gosu.Alichokikuta hospitali pale
kilimmaliza nguvu.Hali ya Gosu
Gosu ilibadilika usiku na
kulazimika kumuwekea
mashine ya kumsaidia
kupumua.Melanie
hakuruhusiwa kuingia ndani
bali alimuona Gosu Gosu kupitia
kioo kikubwa.
“Maskini Gosu Gosu mpenzi
wangu usiniache.Tafadhali
usiondoke na kuniacha peke
yangu ! Melanie akawaza huku
akimtazama Gosu Gosu kupitia
kioo.Mara akashikwa bega na
kugeuka
“Habari yako dada” jamaa
mmoja mwenye mwili
uliojengeka
akamsalimu.Melanie hakuwa
akimfahamu yule jamaa.Akafuta
machozi na kusema
“Nzuri habari yako”
“Naitwa Austin January ni
rafiki wa karibu wa Gosu
Gosu.Natumai wewe ndiye
uliyenipigia simu jana usiku
kunijulisha masahibu haya
yaliyompata mwenzetu”
akasema Austin
“Ndiyo ni mimi.Naitwa
Melanie Davis”
“Melanie pole sana.Ni mara
ya kwanza tunaonana je wewe
ni ndugu yake? Akauliza Austin
“Gosu Gosu ni mchumba
wangu” akasema Melanie na
Austin akastuka kidogo halafu
akatabasamu
“Nafurahi
kukufahamu.Mimi ni rafiki yake
mkubwa” akasema Austin
“Nilifika jana nyumbani
kwake baada ya kutoka hapa
hospitali nikamuuliza mtumishi
wake wa ndani kama
anamfahamu rafiki au ndugu wa
karibu wa Gosu Gosu akanipa
namba zako nikakupigia”
akasema Melanie
“Gosu Gosu ana asili ya
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo lakini kwa sasa ni Raia
wa Tanzania.Hana ndugu
ninaye mfahamu huku Tanzania
na toka nilipokutana naye mimi
ndiye nimekuwa ndugu
yake.Nilikutanishwa naye na
mtu mmoja ambaye sasa ni
marehemu anaitwa Mathew
Mulumbi na toka wakati huo
tumekuwa watu wa karibu
mno.Nashukuru kwa kunipa
taarifa.Nataka kufahamu tukio
hili limetokeaje?
“Kwa mujibu wa taarifa
nilizopewa ni kwamba Gosu
Gosu alikuwa anatoka ofisini
kwake jana jioni na wakati
akisubiri kuingia barabara kuu
wakatokea watu wakiwa katika
piki piki na mmoja aliyekaa
nyuma alikuwa na bunduki
akaanza kumimina risasi katika
gari la Gosu Gosu.Mimi nilipewa
taarifa hizo na katibu wangu
muhtasi ndipo nikaja moja kwa
moja hospitali kujua maendeleo
yake” akasema Melanie
“Nimejaribu kupiga simu
polisi kufuatilia kama kuna mtu
yeyote aliyepatikana lakini
mpaka sasa hawajampata mtu
yeyote uchunguzi unaendelea”
akasema Austin na ukimya
ukapita.
“Nimejiuliza sana sababu ya
Gosu Gosu kushambuliwa
nimekosa jibu.Ninawaza je ni
sababu za kibiashara au ni
kulipiza kisasi? Akauliza Austin
“Nadhani tutapata jibu pale
jeshi la polisi
watakapokamilisha uchunguzi
wao na kuwapata watu
waliofanya shambulio hili”
akasema Melanie
“Nakuahidi Melanie mtu
huyu lazima atapatikana.Iwe
mvua au jua lazima atapatikana.
Kwa sasa tuendelee
kumuombea Gosu Gosu aweze
kupona.Hali yake si nzuri na
kwa mujibu wa daktari
niliyezungumza naye amenipa
ukweli kwamba hali hii
aliyonayo sasa kupona ni
hamsini kwa hamsini hivyo
tujiandae kwa lolote
litakalotokea” akasema Austin
na Melanie akaangua kilio
“Gosu Gosu wangu jamani
!!!
Austin akamnyamazisha
“Tafadhali Melanie jizuie
kumwaga chozi.Kwa sasa
tunahitaji sana kuwa
majasiri.Gosu Gosu anatuhitaji
sana” akasema Austin na
Melanie akafuta machozi.Austin
akamshika bega na kusema
“Sikiliza
Melanie.Ninamfahamu Gosu
Gosu ni mpambanaji.He’ll fight
this.Believe me Gosu Gosu will
fight this !
“Austin najua unajaribu
kunipa moyo lakini hali haisi ya
Gosu Gosu
inaonekana.Uwezekano wa
kupona ni mdogo sana.Oh
jamani mimi !!
“Melanie eneo hili halihitaji
kelele ! Austin akawa mkali
“Jitahidi kujizuia kumwaga
machozi eneo hili.Ndugu za
Gosu Gosu ni sisi wawili pekee
hivyo basi ninahitaji
kushirikiana na mtu mwenye
ujasiri.Kama hautakuwa na
ujasiri tafadhali kaa nyumbani
usifike hapa ! akasema Austin
“Samahani nimekuelewa
Austin”
“Good.Sasa nenda
nyumbani kapumzike mimi
nitaendelea kukaa hapa na
kama kuna chochote kitatokea
nitakujulisha”akasema Austin
na kumshika mkono Melanie
akamsindikiza hadi katika gari
lake ambamo alikuwemo Joyce
dereva wake
“Melanie kuwa jasiri,Gosu
Gosu atapambana na
atapona.Ninamfahamu vyema
ni mpambanaji” akasema Austin
na kuagana na Melanie
akaondoka
“Dah ! Gosu Gosu amemtoa
wapi Yule mtoto?Halafu mbona
hajanieleza chochote kama
tayari ana mchumba?Siku hizi
ameanza kuniweka mbali katika
masuala yake ndiyo maana hata
suala hili hakutaka
kunishirikisha.Hata hivyo
anastahili kupongezwa kwa
kumpata mwanamke mzuri
kama yule” akawaza Austin na
kurejea ndani.