Riwaya: Siri

mbududa

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2017
Messages
596
Points
1,000

mbududa

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2017
596 1,000
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 10 : EPISODE 10
Edwin Mbeko aliwasili
ikulu alikoitwa na Rais.
“Edwin karibu
sana.Nashukuru umefika kwa
wakati” akaanzisha maongezi
Dr Fabian
“Nashukuru sana
mheshimiwa Rais”
“Nimetaka uje asubuhi hii
tuzungumze kwa sababu nina
ratiba ndefu siku ya leo.Nina
ugeni wa marais wa Uganda na
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo.Tutakuwa na kikao
muhimu sana hivyo
mazungumzo yetu yatakuwa
mafupi sana” akasema Dr
Fabian
“Edwin nimekuta hapa
kuja kukujulisha rasmi
kwamba kuanzia sasa wewe
utakuwa ndiye mkurugenzi
mkuu wa SNSA.Umekaimu
nafasi hii kwa miaka mitatu na
umefanya kazi nzuri sana
hivyo kwa mamlaka yangu
nimekuteua kuwa mkurugenzi
mkuu na msaidizi wako
nitamteua hapo baadae”
akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais
umenistua sana.Sikutegemea
kabisa ama ungeweza kuniteua
kushika nafasi hiyo” akasema
Edwin
“Unastahili nafasi hiyo”
akasema Dr Fabian
“Nashukuru mno
mheshimiwa Rais kwa kuniona
ninafaa”
“Unafaa Edwin.Umekuwa
katika nafasi ya ukaimu kwa
miaka mitatu na hakujawahi
kutokea tatizo lolote.Nilifanya
makosa makubwa kuamua
kumleta mtu ambaye haijui
vyema idara ile na tazama
mambo yaliyotokea.Ndani ya
siku mbili tu ambazo Annabel
amekuwa katika nafasi ya
ukurugenzi yametokea mambo
ya ajabu sana.Ameingiza watu
wasio watumishi wa
idara.Vimetokea vifo vya
wafanyakazi wawili n.k.Kama
angeendelea kwa mwezi
mzima sifahamu nini
kingetokea hivyo sitaki tena
kumuona katika idara
ile.Ulifanya vizuri sana
kutumia kanuni kumuondoa
katika nafasi yake.”
“Mheshimiwa Rais
ninashukuru sana kwa uteuzi
huu na ninakuahidi kufanya
kazi iliyotukuka
kabisa”akasema Edwin
“Edwin nataka ukafanye
kazi .Nataka nchi iwe salama”
akasema Dr Fabian
“Usiwe na hofu
mheshmiwa Rais.Idara yetu
hailali watu wanafanya kazi
saa ishirini na nne kuhakikisha
nchi inakuwa salama”
“Good.Kubwa nililokuitia
hapa ni hilo la kukupa hiyo
taarifa nzuri” akasema Dr
Fabian
“Mheshimiwa rais kwa
mara nyingine ninashukuru
sana na ninakuahidi kazi
nzuri.Hata hivyo nina swali
dogo kama utaniruhusu
kuuliza”akasema Edwin na Dr
Fabian akaitazama saa yake
kisha akasema
“Uliza”
“Ni kuhusiana na tukio la
jana usiku.Uliniambia mtu
ambaye alivamia ofisi zetu
anaitwa Mathew Mulumbi.Ni
nani huyo mtu?
“Mathew Mulumbi hata
mimi simfahamu vyema lakini
wanaomfahamu wanadai
aliwahi kufanya kazi katika
idara ya ujasusi kabla ya
kuanza kujishughulisha na
biashara zake binafsi.Licha ya
kuacha kazi katika idara ya
ujasusi lakini inadaiwa
Mathew ameendelea kufanya
kazi za ujasusi kwa
kujitegemea na inasemekana
miaka mitatu iliyopita
alishiriki katika misheni ya
kuwakomboa mateka
waliotekwa na kundi la IS na
mmoja wa mateka hao akiwa
ni mtoto wa Rais aliyemaliza
muda wake kwa bahati mbaya
katika misheni hiyo inadaiwa
alifariki dunia lakini kwa
mshangao mkubwa Mathew
ameibuka wiki hii kutoka
kusikojulikana.Mambo
anayoyaongea na kuyafanya
yanatia shaka sana kama kweli
ni binadamu wa kawaida au ni
mzimu unatuchezea.Kwa
mfano jana aliwezaje kutoka
ndani ya jengo lile bila
kuonekana? Akauliza Dr
Fabian
“Mheshimiwa Rais hata
sisi tumejiuliza alitokaje ndani
ya jengo lile bila
kuonekana?Lakini
mheshimiwa Rais bado kuna
kitu kimoja nataka
kukifahamu kama
itakupendeza “
“Sema Edwin usiogope”
“Nataka kufahamu chanzo
cha taarifa ile ya Mathew
kuingia ndani ya jengo letu”
akasema Edwin
“Ni Annabel”
“Annabel?Edwin
akashangaa
“Ndiyo.Yeye ndiye
aliyeniambia kwamba
anamsaidia Mathew kuingia
ndani ya ofisi zenu na ndipo
nikakupigia.Hiyo ni moja ya
sababu kubwa iliyonifanya
nikamuondoa katika nafasi ile
ya ukurugenzi”
“Mheshimiwa Rais
Annabel alikueleza Mathew
alikuja kutafuta nini katika
ofisi zetu?akauliza Edwin
“Hakunieleza sababu za
kumsaidia Mathew kuingia
SNSA”
“Mheshimiwa rais
utaniwia radhi lakini kwa hiki
alichokifanya Annabel na
Mathew wamekwisha ingia
kwenye orodha ya watu hatari
kwa usalama wa nchi.Annabel
japo amekuwa mkurugenzi wa
SNSA kwa siku mbili lakini
ameyafahamu mambo mengi
ya idara,tayari amezifahamu
siri nyingi za usalama wa nchi
na kama amemsaidia Mathew
kuingia ndani ya ofisi zetu ni
wazi kuna siri wanazitafuta na
watajaribu kila njia hadi
wafanikiwe lengo lao” akasema
Edwin
“Unalolisema Edwin ni la
kweli kabisa.Tayari Annabel
amekwisha onekana kuwa
hatari hivyo tunatakiwa
kuanza kummulika na kujua
mwenendo wake.Nitakuita
tena kesho tutalizungumza hili
kwa kirefu zaidi” akasema Dr
Fabian huku akinyanyuka
kitini
“Kwa heri mheshimiwa
rais,jivinjari ikulu mara ya
mwisho kwani kabla ya
machweo leo tayari utakuwa
umerejea kwa muumba wako”
akawaza Edwin wakati
akiagana na Rais
 

mbududa

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2017
Messages
596
Points
1,000

mbududa

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2017
596 1,000
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 10 : EPISODE 11
Mathew na Ruby
waliegesha gari lao mita
chache kutoka geti la kuingilia
jumba la Melanie Davis.Ni
mtaa wanaoishi matajiri
wakubwa hivyo kulikuwa na
ukimya mkubwa.Kulikuwa na
magari mawili yameegeshwa
kandoni mwa barabara hivyo
gari la akina Mathew likawa la
tatu.
“Kwa mujibu wa ramani
yetu,Melanie Davis
alizungumza na Peniela akiwa
katika nyumba ile pale”
akasema Ruby huku
akiitazama ramani yake
“Tunarusha kwanza
kamera ya ndege ichunguze
ndani ya nyumba ile kuna nini
halafu tutarusha ile kamera
ndogo ya nyuki” Akasema
Mathew na kufungua boksi
lililokuwa na ndege wa bandia
aliyefungwa kamera.Kwa
kumtazama kwa haraka haraka
isingekuwa rahisi kujua kama
ndege ile ni bandia kwani
alionekana kama ndege halisi
mwenye rangi za
kuvutia.Mathew akatazama
pande zote kama kuna watu
wanaowatilia shaka halafu
akaiwasha kamera ile
akafungua dirisha na
kumrusha Yule ndege huku
Ruby akiwa na kifaa cha
kumuongozea.Ndege Yule
alipaa na kutua juu ya paa la
nyumba ya Melanie na eneo
lote la nyumba ile likaanza
kuonekana.Hakukuwa na mtu
yeyote nje.Kulikuwa na
bustani nzuri ilyopandwa
maua mazuri na eneo kubwa la
nje lilipandwa majani mazuri
ya kijani.Ruby akaizungusha
kamera ile upande wa nyuma
ya nyumba na mwanamke
mmoja akaonekana akifanya
usafi.Ruby akachukua picha ya
mwanamke Yule akaiingiza
katika programu na kumtafuta
lakini hakuweza kupatikana
“Mwanamke Yule hayupo
katika mfumo wowote wa
serikali” akasema Ruby
“Tumekuja sehemu
husika.Hii ni kazi ya mtandao
wa akina Melanie.Watu wao
wengi hawajulikani katika
mifumo ya serikali” akasema
Mathew.Ruby akampeleka
ndege Yule juu ya ukuta
akaielekeza kamera katika
mlango mkuu wa kuingilia
ndani ili waweze kushuhudia
kila anayeingia na kutoka
kupitia mlango ule mkubwa
“Time to send in our
second camera” akasema
Mathew na kufungua sanduku
lingine dogo akatoa kiboksi
kidogo ambacho ndani yake
kulikuwa na kamera ndogo
yenye muundo sawa na nyuki.
“Teknolojia imekua sana
zama hizi hadi vitu kama hivi
vinatengenezwa.This is
wonderfull” akasema Ruby
“Hizi ni kamera za hali ya
juu za kijasusi ambazo
zinatumiwa na mataifa
makubwa” akasema Mathew
na kuiwasha ile kamera ndogo
“Sweet bee go inside and
do a nice job” akasema
Mathew akamrusha Yule nyuki
nje Ruby akaanza kumuongoza
kuelekea ndani huku wakipata
picha nzuri
“This is
amazing.Sikutegemea kama
nyuki Yule anaweza akarusha
picha nzuri namna hii”
akasema Ruby na kumuongoza
nyuki Yule hadi katika mlango
mkubwa wa mbele akitafuta
nafasi ya kumuingiza ndani
lakini hakukuwa na upenyo
wowote.Akamzungusha nyuma
ya nyumba ambako nako
tayari mlango ulikuwa
umefungwa.
“Betri ya huyu nyuki
inaweza kudumu kwa muda
gani? Ruby akauliza
“Saa tatu hadi
nne.Tutaendelea kusubiri hadi
pale mlango
utakapofunguliwa” akasema
Mathew
 

mbududa

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2017
Messages
596
Points
1,000

mbududa

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2017
596 1,000
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 10 : EPISODE 12
Baada ya kutoka ikulu
Edwin Mbeko alimuelekeza
Jakson ampeleke katika
nyumba za maafisa wa polisi
Mikunguni.
“Jackson ahsante kwa kazi
nzuri mliyofanya jana usiku”
akasema Edwin
“Usijali mkuu.Muda
wowote utakaponituma kazi
yoyote nitahakikisha
inafanyika kikamilifu”
“Nafurahi kusikia
hivyo.Ninakuahidi kukuweka
sehemu nzuri sana kwani kwa
sasa mimi ndiye
mkurugenzi.Rais ameniteua
leo niwe mkurugenzi wa
SNSA” akasema Edwin
“Hongera sana
mkuu.Unafaa kuongoza idara
ile.Rais hajakosea kukupa
nafasi hiyo”
“Ahsante sana Jack”
akasema Edwin
“Vipi kuhusu Yule mama
tuliyetambulishwa kuwa ndiye
mkurugenzi?Atarudi tena
SNSA?akauliza Jackson
“Yule habari yake
imekwisha.Hatarejea tena
SNSA.Ni mwanamke hatari
sana yule na ndiye
aliyesaidiana na Yule jaama
aliyeingia katika ofisi zetu jana
usiku.Ni hatari kabisa kwa
usalama wa nchi” akasema
Edwin
“Nini walikuwa
wanakitafuta katika ofisi zetu
jana? Akauliza Jackson
“Wanatafuta siri za
usalama wa nchi.Kuna mtu
anaitwa Mathew Mulumbi
nimeambiwa ndiye ambaye
alivamia ofisi zetu.Tukimpata
huyo atatueleza alichokuwa
anakitafuta katika ofisi zetu”
akasema Edwin
“Mathew Mulumbi ni
nani? Akauliza Jackson
“Hata mimi simfahamu
lakini nimeambiwa aliwahi
kufanya kazi katika idara ya
ujasusi na baadae akapotea
sasa amerudi tena na
haijulikani ametoka wapi.Ni
mtu hatari sana kwa usalama
wa nchi” akasema Edwin na
simu yake ikaita akaipokea
“Hallo Melanie” akasema
Edwin
“Edwin bado uko ikulu?
Huku kila kitu tayari na ni
wewe tunayekusubiri hivi sasa”
akasema Melanie
“Tayari nimekwisha toka
ikulu hivi sasa ninakwenda
kuchukua zile sare halafu
nitakuja hapo muda si mrefu”
akasema Edwin na kukata
simu halafu akamtaka Jackson
kuongeza mwendo zaidi ili
wawahi kufika mahala
wanakoelekea
Walifika katika nyumba za
maofisa wa polisi Mikunguni
Edwin akamuelekeza Jackson
kuegesha gari nje ya nyumba
Fulani ya mmoja wa maofisa
wa polisi halafu akashuka na
kugonga kengele ya geti na
ndani ya muda mfupi mlango
mdogo wa geti ukafunguliwa
akaingia ndani.
Mara tu Edwin alipoingia
ndani ya ile nyumba Jackson
akatoka nje ya gari akampigia
simu Mathew
“Jackson nini kinaendelea
kwa upande wako?Mathew
akauliza baada ya kupokea
simu
“Kaka nimekupigia simu
kukujulisha kuwa tayari
tumetoka ikulu na Edwin
amenielekeza nimlete hapa
Mikunguni katika nyumba za
maafisa wa polisi hivi sasa
ameingia katika mojawapo ya
nyumba hizi.Kuna mambo
mawili yametokea kwanza Rais
amemteua kuwa mkurugenzi
mkuu wa SNSA pili tukiwa
garini alipigiwa simu na mtu
anaitwa Melanie.Nadhani
atakuwa ni Yule Melanie
uliyenionyesha picha yake jana
unayemtafuta.Sikusikia
upande wa Melanie
alichokizungumza lakini kwa
upande wa Edwin nilimsikia
akisema kwamba tayari
ametoka ikulu na sasa
anakwenda kuchukua zile sare
kisha atamfuata.Kwa sasa
ameingia ndani ya nyumba
yenye kibao Block D 39”
“Ahsante sana Jackson
kwa kazi nzuri endelea
kumfuatilia na kutujulisha kila
kinachoendelea” akasema
Mathew na kukata simu
“Edwin amepewa
ukurugenzi wa SNSA na Rais”
Mathew akamwambia Ruby
“Hakuna
tatizo.Anamuamni ndiyo
maana amempa nafasi hiyo
lakini bado hajui kama Edwin
ni nyoka wa vichwa viwili.Siku
akilijua hilo tayari atakuwa
amechelewa sana” akasema
Ruby
“Ukiacha hilo Jackson
anasema wakiwa garini Edwin
alipigiwa simu na Melanie na
katika mazungumzo yao Edwin
akamwammbia Melanie
kwamba anafuatilia sare”
“Sare?Ruby akauliza
“Ndiyo amesema
anafuatilia sare na sasa yuko
Mikunguni ambako wanakaa
maafisa wa polisi.Kuna kitu
hapa kinajitokeza.Je huko
mikunguni ndiko amefuatilia
hizo sare?Je ni sare zipi hizo?
Akauliza Mathew na mara
katika kioo cha mashine ya
kuongozea ile kamera ya ndege
ukaonekana mlango mkubwa
wa mbele ya nyumba
ukifunguliwa.Mtu mmoja
aliyevaa fulana ya kukatwa
mikono akiwa na sigara
mkononi akatoka.
“James Kasai ! akasema
Mathew
Haraka haraka Ruby
akacheza na kompyuta yake
akaichukua picha ya yule mtu
aliyetoka ndani ya ile nyumba
akaiingiza katika programu ya
utambuzi na majibu yakaja
kwamba kwa asilimia mia
moja Yule ni James Kasai
“Oh my God it’s him !
akasema Ruby
James Kasai akiwa na
sigara yake alikwenda kuketi
katika bustani mahala
kulikokuwa na viti vzuri vya
kupumzika.Baada ya muda
mlango ukafunguliwa akatoka
Yule mwanamke ambaye
walishindwa kumtambua awali
akiwa amebeba sinia lenye
chupa kubwa ya mvinyo na
glasi akamuwekea James
mezani na kummiminia kidogo
katika glasi.James akavuta
sigara akapuliza moshi mwingi
halafu akainua glasi ya mvinyo
akanywa akaendelea kuvuta
sigara yake.
“Enjoy life for the last time
bastard ! akasema Mathew
akimtazama James kwa
hasira.Mlango ukafunguliwa
akatoka mwanamke ambaye
hakukuwa na haja ya kutumia
programu ya utambuzi
kumtambua.Wote
walimtambua haraka haraka
alikuwa ni Melanie Davis
“That’s Melanie Davis.Yule
ndiye shetani wa kike
anayetusumbua ambaye
tumekuwa tukimsaka bila
mafanikio” akasema Ruby
“Kwa nini mwanamke
mzuri namna hii akavaa roho
ya kishetani anaua watu bila ya
huruma?akauliza Mathew
“Nani alikwambia shetani
ana sura mbaya?Kumbuka
shetani aliwahi kuwa malaika
kabla ya kufukuzwa kwa hiyo
usishangae ukiona mwanamke
mzuri kama huyu ana roho ya
kishetani” akasema Ruby
“Your days are over
Melanie.Leo ni wewe au sisi !
akasema Mathew akiendelea
kumtazama Melanie
akitembea kwa kuringa
kuelekea mahala alipokuwa
James Kasai ambaye aliinuka
akavuta kiti Melanie akaketi
halafu akammiminia kinywaji
katika glasi
“What a gentleman !
akasema Ruby huku
akitabasamu.Mathew
akageuka akamtazama na wote
wakajikuta wakitabasamu
Melanie na James
waliendelea na mazungumzo.
“Natamani nisikie kile
wanachokizungumza.Tunawez
a kumsogeza Yule nyuki karibu
kusikia maongezi yao”
akasema Mathew na Ruby
akairusha kamera ile hadi
karibu na mahala walipokuwa
akina Melanie akaishusha
katika majani halafu nyuki
Yule akaanza taratibu
kutembea katika majani hadi
chini ya meza na sauti za
maongezi ya Melanie na James
Kasai zikaanza kusikika
“Nimependa sana Dar es
salaam ! akasema James Kasai
“Usijali utakuja na
kuondoka Dar es salaam kila
pale utakapohitaji.Unaweza
ukaja kila mwisho wa wiki
ukastarehe kisha ukaondoka
kurejea Uganda.Uwezo huo
upo kwani tunaweza kufaya
chochote ndani ya nchi
hii”akasema Melanie
“Ningefurahi sana kama
ingekuwa hivyo.Naipenda
Tanzania na ninaishambulia
kwa kuwa imebidi iwe hivyo
lakini sikuwahi kuwa na
mpango wa kushambulia”
akasema James
“Hata mimi ninaipenda
Tanzania.Nimeishi na kusoma
hapa,watu wake ni
wakarimu,watanzania hawana
ugomvi na mtu yeyote.Kwa
ujumla Tanzania ni nchi nzuri
wabaya ni viongozi wake !
Lakini baada ya leo mambo
yatatulia” akasema Melanie na
mmoja watumishi wake
akamfuata akamjulisha
kwamba anahitajika ndani.
“Melanie anadai ameishi
na kusoma hapa.Ni nani huyu
mwanamke?Mbona
inaonyesha ametokea
Ufaransa? Akauliza Ruby
“Kuna jambo kubwa liko
nyuma ya huyu mwanamke na
leo lazima tulifahamu.Melanie
Davis ni zaidi ya
tunavyomdhania.Halafu katika
maongezi yao kuna kitu
amekiongea Melanie amesema
baada ya leo mambo
yatatulia.Kauli hii inaashiria
kuna kitu kinakwenda kutokea
leo.What are they planning
today?akauliza Mathew na
simu yake ikaita alikuwa ni
Jackson
“Jackson nipe habari”
akasema Mathew
“Edwin ametoka katika ile
nyumba alimoingia akiwa na
sanduku dogo.Hakutaka
niongozane naye tena amenipa
shilingi laki moja nitafute
usafiri nirejee ofisini”akasema
Jackson
“Ahsante sana Jack kwa
taarifa.Usiondoke maeneo
hayo.Fanya utafiti kujua
nyumba hiyo ni afisa gani wa
polisi anaishi na mwenye cheo
gani halafu nijulishe mara
moja” akasema Mathew
“Sawa kaka” akasema
Jackson na kukata simu
“Edwin amekwisha ondoka
katika ile nyumba
alimoingia.Hajataka
kuongozana na Jack bali
amempa shilingi laki moja
atafute usafiri
mwingine.Ametoka akiwa na
sanduku dogo mfuatilie tujue
anaelekea wapi” akasema
Mathew na Ruby akaigeukia
kompyuta yake akaanza
kukifuatilia kile kifaa
kilichowekwa katika gari la
Edwin.
“Kama utakumbuka Jack
alisema wakati wanaelekea
Mikunguni Edwin
alizungumza na Melanie
simuni na akamjulisha
kwamba anafuatilia sare.Kwa
taarifa ya sasa hivi Jack anadai
kwamba Edwin alitoka ndani
ya hiyo nyumba alimoingia
akiwa na sanduku dogo.Je
humo alimoingia ambamo ni
kwa afisa wa polisi ndimo
alimokwenda kuchukua hizo
sare? Je ni sare zipi hizo?
Akauliza Mathew
“Mathew ukiunganisha
hilo la sare na yale maneno ya
Melanie kwamba “baada ya
leo” unapata picha kwamba
kuna kitu kinaandaliwa leo na
hawa watu”akasema Ruby
“Bado kuna mtu mmoja
hatujathibtisha kama yuko
ndani ya nyumba hii Khalid
Sultan Khalid.Je yumo humu
ndani au yuko sehemu
nyingine? Lakini taarifa
zilionyesha kwamba anakuja
Tanzania kuonana na James
Kasai hivyo basi kama James
yuko humu ndani kuna
uwezekano mkubwa Khalid
akawa mle ndani.Tuendelee
kuvuta subira tutajua kila kitu”
akasema Mathew
 

mbududa

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2017
Messages
596
Points
1,000

mbududa

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2017
596 1,000
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 10 : EPISODE 13
Edwin Mbeko alipotoka
Mikunguni akaelekea moja
kwa moja nyumbani kwa
Melanie Davis.Mathew na
Ruby waliendelea kumfuatilia
bila yeye kufahamu na
kugundua alikuwa anaelekea
maeneo yale.Alipofika katika
geti la nyumba ya Melanie gari
lake likasimama kwa sekunde
kadhaa halafu geti
likafunguliwa akaingia
ndani.Kamera mbili za akina
Mathew zilizokuwa mle ndani
zote zikaelekezwa katika
mlango mkubwa wa kuingilia
sebuleni.Gari likasimama
mlango ukafunguliwa
akashuka Edwin Mbeko
akafungua mlango wa nyuma
akachukua sanduku dogo
kisha akaingia ndani haraka
haraka
“Sanduku lile dogo ndilo
alilotoka nalo kule Mikunguni
kwa mujibu wa
Jackson.Natamani nikaingie
mle ndani nishuhudie kile
kinachoendelea lakini
tutaharibu mambo” akasema
Mathew
“Tuwe wavumilivu na
tutajua tu kila kinachoendelea
mle ndani” akasema Ruby
Edwin alipoingia mle
ndani akasalimiana na James
Kasai na Melanie
“Kwema huko
utokako?akauliza Melanie
“Kwema kabisa.Kuna
habari nzuri.Rais ameniteua
kuwa mkurugenzi wa idara ya
SNSA”
“Wow ! hongera sana”
“Ahsante.Kwa sasa tuna
nguvu kubwa na tunaweza
kufanya kila tutakalo”
“Imekuwa vyema
amekukabidhi cheo kwa mara
ya mwisho”
“Marais wa Uganda na
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo tayari wamewasili na
hivi sasa kikao kinaendelea
ikulu Dar es salaam” akasema
Edwin
“Jenerali Akiki alinipigia
simu wakati anaondoka
Kampala kuja Dar es salaam”
akasema Melanie
“Melanie hii ni siku yetu
kubwa sana na kizuri ni
kwamba mipango yetu yote
inakwenda vizuri.Inapendeza
sana kama kila
mnachokipanga kinakwenda
vyema” akasema Edwin na
kufungua sanduku alilokuja
nalo na kutoa sare za jeshi la
polisi kikosi cha kutuliza
ghasia.Wakazikagua halafu
wakaelekea katika chumba
alimokuwamo Khalid
Sultan.Akasalimiana na Edwin
halafu akamuonyesha bomu
alilolitengeneza ambalo
lilifanana na fulana za kuzuia
risasi wavaazo jeshi la polisi.
“Bomu ambalo niliitwa
kulitengeneza ni hili hapa
limekamilika na kazi imebaki
upande wenu kulilipua.Hili ni
bomu kubwa na madhara yake
ni makubwa pia.Nina hakika
wale wote waliolengwa kuuawa
na bomu hili
hawatasalimika.Nimetengenez
a pia bomu lingine la akiba
kwa ajili ya siku nyingine”
akasema Khalid halafu
akaenda kumchukua Abdi
kijana wa miaka ishirini na
nane kutoka katika kundi la
Alshabaab .
“eabdi kl shay’ jahiz wahan
alwaqt alan lildhahb” (Abdi
kila kitu kimekamilika na
muda wa kuingia kazini
umewadia) Khalid
akamwambia Abdi akitumia
lugha ya kiarabu.
“ana mustaeidum” (niko
tayari” akajibu Abdi
“eabdi eayilatuk satatrik
hayatan fakhiratan libaqiat
hayatihim bsbb ma tafealuh
alyawm (Abdi familia yako
itaishi maisha ya kifahari kwa
maisha yao yote kwa sababu ya
hiki unachokwenda kukifanya
leo” akasema Khalid
“amiyn ! akasema Abdi
halafu akavua mavazi
aliyokuwa amevaa akaanza
kuvaa mavazi yale ya askari
yaliyoletwa na
Edwin.Alionekana kama askari
halisi wa kikosi cha kutuliza
ghasia kwa mavazi
yale.Taratibu Khalid
akaichukua fulana ile ambayo
ni bomu akamvisha akaifunga
vizuri.
Khalid akazungumza na
Abdi kwa lugha ya kiarabu
halafu akawageukia akina
Melanie
“Kila kitu tayari Abdi
amekwisha pewa maelekezo
nini cha kufanya hivyo msiwe
na wasi wasi wowote.Kila kitu
kitakwenda kama
kilivyopangwa” akasema
Khalid
Hakukuwa na kupoteza
muda Edwin akaagana na
akina Melanie kisha
akamchukua Abdi wakaelekea
nje
Mlango mkubwa wa
kuingilia sebuleni
ukafunguliwa na Ruby
akamstua Mathew
“Mlango umefunguliwa”
akasema na mara akaonekana
Edwin Mbeko na nyumayake
akaonekana askari wa kikosi
cha kutuliza ghasia.
“What’s going on in
there?akauliza Mathew
“Sijaweza kuipata sura ya
Yule askari kwani ametoka
haraka haraka sana na kuingia
garini”akasema Ruby
“Edwin alipozungumza na
Melanie alimwambia
anakwenda kufuatilia sare na
alipotoka katika nyumba ya
mmoja wa afisa wa polisi
alikuwa na sanduku ambalo
alikuja nalo hapa akaingia nalo
ndani.Naamini sare alizokuwa
anafuatilia ni sare za jeshi la
polisi ambazo amevaa Yule
jamaa na hii inatoa picha
kwamba Yule jamaa
yawezekana si
askari.Yawezekana
wamemvisha sare zile ili
aonekane kama askari na
wamtumie katika mipango
yao.Ningeweza kumfuatilia
kujua wanakoelekea lakini kwa
kuwa kuna kifaa katika gari la
Edwin tutafahamu anaelekea
wapi.Ndani ya nyumba hii
kuna watu muhimu sana
ambao hatupaswi kuwapoteza”
akasema Mathew
Wakati Mathew na Ruby
wakiendelea kufuatilia kile
kinachoendelea ndani ya
nyumba ya Melanie Jackson
akapiga simu.
“Kuna taarifa gani
Jackson?Mathew akauliza
“Uliniambia nifuatilie ni
afisa gani anakaa katika ile
nyumba alimoingia Edwin”
“Ndiyo.Umekwisha
fahamu ni afisa gani?
“Anaitwa Inspekta Fanuel
Mwabukusi au kwa jina lingine
anaitwa afande mwarabu”
“Ahsante sana Jackson
usiondoke maeneo hayo hadi
nitakapokwambia” akasema
Mathew
Katika nyumba ya Melanie
bado milango iliendelea
kufungwa.
“Ruby hatuwezi kuendelea
kusubiri namna hii wakati
tayari tumekwisha pata
uhakika kwamba ndani ya
nyumba ile yupo James Kasai
na Melanie Davis.We have to
do something ! akasema
Mathew
“Unataka kufanya nini
Mathew?
“I want to get in there
and……….”
“Hapana Mathew
sikushauri ufanye hivyo.Kuna
mambo mengi tutashindwa
kuyafahamu kama
tukiwavamia sasa hivi.Tujipe
muda kidogo”akasema Ruby
“Ruby hujui ni namna gani
ninaumia kuwaona wale watu
walivyo huru wakiendelea na
mipango yao mle ndani”
“Muda utafika
Mathew.Vuta subira kidogo”
akasema Ruby
“Kuna mtu mmoja tu
ambaye bado hatuna uhakika
naye mahala alipo Khalid
Sultan.Kama ningekuwa na
uhakika yuko mle ndani
nisingekuwa na muda wa
kusubiri” akasema Mathew
“Subira yavuta
heri.Tuendelee kusubiri
tunaweza kugundua mambo
mengine mengi zaidi” akasema
Ruby na ile kamera ndogo ya
nyuki ikaonyesha kuanza
kuisha chaji ikalazimu Ruby
kuirudisha
“Kamrea hii imetusaidia
sana Mathew” akasema Ruby
“Teknolojia imerahisisha
sana kazi za ujasusi siku
hizi.Kama isingekuwa
teknolojia ingetuchukua muda
kufahamu kama James Kasai
na Melanie wako mle ndani”
akasema Mathew
 

mbududa

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2017
Messages
596
Points
1,000

mbududa

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2017
596 1,000
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 10 : EPISODE 14
Edwin Mbeko alipoondoka
kwa Melanie alielekea moja
kwa moja Mikunguni.Jackson
akiwa katika kibanda cha
kuuza juisi kilichotazamana na
nyumba ya afande mwarabu
aliiona gari ya Edwin ikikata
kona kuelekea katika geti la
nyumba ile.Akapiga honi na
geti likafunguliwa gari
likaingia ndani geti
likafungwa.Jackson akasogea
hadi katika geti akatafuta
upenyo na kuchungulia ndani
akamuona Edwin akiwa
amesimama na askari mmoja
wa kikosi cha kutuliza ghasia
pamoja na askari mwingine
aliyevaa mavazi ya kiofisa
akiwa na fimbo
mkononi.Walizungumza kwa
dakika kama tano halafu
Edwin akaingia peke yake
ndani ya gari yule askari
akabaki.Geti likafunguliwa gari
la Edwin likatoka na
kuondoka.Simu ya Jackson
ikaita alikuwa ni Edwin Mbeko
“Hallo mkuu” akasema
Jackson
“Jackson umekwisha fika
ofisini?akauliza Edwin
“Ninakaribia kufika mkuu”
“Fanya hivi.Nataka hapo
hapo ulipofika ugeuze.Nataka
nikukute katika bohari ili
nikuachie gari langu nitakuwa
na safari”
“Sawa mkuu ninaelekea
huko sasa hivi” akasema
Jackson halafu akampigia
simu Mathew
“Jackson tumeona hapa
Edwin amerejea tena
mikunguni” akasema Mathew
“Ndiyo mkuu amerejea
katika nyumba ile ile ya afande
mwarabu”
“Alipoondoka hapa kwa
Melanie alikuwa na mtu
aliyevaa sare za jeshi la polisi”
“Nimemuona huyo mtu
alikuwa amesimama naye
wakizungumza na afande
mwenye mavazi ya kiofisa
ambaye naamini ni afande
Mwarabu.Kwa sasa Edwin
ameondoka lakini yuko peke
yake garini Yule askari
amemuacha hapa kwa
Mwarabu.Amenipigia simu na
kunitaka niende katika bohari
ili anikute kule aniachie gari
anadai anataka kusafiri”
akasema Jackson
“Anataka kusafiri?!
“Ndiyo.Ameniambia
hivyo” akajibu Jackson
“Jackson naomba
unisubiri hapo mahala
ulipo.Ninakuja sasa hivi
nataka twende wote huko
katika bohari” akasema
Mathew
“Sawa mkuu nakusubiri”
akajibu Jackson na Mathew
akakata simu
“Mathew unataka kufanya
nini?akauliza Ruby
“Sikiliza Ruby.Edwin
anataka kusafiri.Ninahisi
safari hii ni nje ya mkoa hivyo
lazima kuna kitu.I have to stop
him.Ninakwenda huko katika
bohari pamoja na Jackson na
kumdhibiti Edwin asiweze
kuondoka.Wewe utaendelea
kukaa hapa hapa ukiendelea
kufuatilia kwa karibu kila
kinachoendelea na
utanijulisha.Usiogope you’ll be
safe.Kama kutatokea hatari
yoyote kuna silaha iko humu
utatumia.Nikimaliza huko
nitarejea hapa mara
moja”akasema Mathew
“Sawa Mathew mimi
nitaendelea kufuatilia kila
kinachoendelea hapa na
kukujulisha” akasema
Ruby.Mathew akashuka ndani
ya gari na kuanza kutembea
haraka haraka kuelekea
barabara kuu kwa ajili ya
kuchukua piki piki
akamuelekeza Jackson sehemu
ya kukutana.
 

mbududa

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2017
Messages
596
Points
1,000

mbududa

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2017
596 1,000
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 10 : EPISODE 15
Mathew alimchukua
Jackson mahala
alipomuelekeza wakutane
kisha wakaelekea nyumbani
kwake.
“Jackson karibu sana hapa
ni nyumbani kwangu”
“Hapa ni kwako?akauliza
Jackson
“Ndiyo.Mbona
umeshangaa?
“Una nyumba nzuri
mno.Unaonekana una maisha
mazuri kwa nini unafanya kazi
hizi za hatari?akauliza Jackson
“Tutazungumza hayo
baadae lakini kwa sasa nataka
kufahamu ulinzi ulivyo katika
bohari”
“Kuna walinzi wanne
getini.Wawili wana silaha
mmoja ana mbwa na mmoja
kwa ajili ya mawasiliano.Kuna
walinzi wengine sita wenye
silaha kuzunguka ukuta wa
bohari.Ndani huwa kuna
wafanyakazi kumi na
mbili.Kwa kawaida ni
wafanyakzi wa bohari pekee
ambao huruhusiwa
kuingia.Wewe si mfanyakazi
wa bohari hivyo hautaweza
kuingia”akasema Jackson
“Nitaingia katika buti ya
gari”
“Ikiwa hivyo utaweza
kuingia mle ndani” akasema
Jackson.
“Jackson kabla ya
kuondoka hapa naomba
nikuonye kwamba hiki
tunachokwenda kukifanya
huko ni kitu cha hatari sana
hivyo endapo hauko tayari
kwenda unaweza ukaniambia
na mimi nitakuelewa” akasema
Mathew
“Kaka mimi nimejitolea
kwa ajili ya nchi yangu hivyo
siogopi hata kama nikifa
nitakuwa nimekufa nikilinda
usalama wa taifa langu”
akasema Jackson
“Good ! akasema Mathew
kisha akaenda chumbani
kwake akaongeza silaha katika
begi lake dogo akachagua gari
ambalo lingeweza kuwafaa
kwa shughuli ile akaingia
katika buti na safari ikaanza
 

mbududa

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2017
Messages
596
Points
1,000

mbududa

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2017
596 1,000
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 10 : EPISODE 16
Edwin Mbeko alirejea kwa
Melanie Davis baada ya kutoka
Mikunguni
“Kila kitu kimekamilika na
hivi tuongeavyo tayari Abdi
anapelekwa uwanja wa ndege
kutimiza jukumu lake”
“Huyo mtu anayempeleka
Abdi uwanja wa ndege
unamuamini?akauliza Melanie
“Ninamuamini .Ni mtu
wangu wa karibu na licha ya
hayo amechukua tayari
milioni mia moja hivyo kila
kitu kitakwenda vizuri.Msiwe
na wasi wasi wowote kila kitu
kimekaa vizuri” akasema
Edwin
“Edwin umenifurahisha
sana kwa namna unavyofanya
kazi zako.Ahsante sana kwa
kuukamilisha mpango huu”
akasema James Kasai
“James Kasai hata mimi
ninafurahi kukutana na
kufanya nawe kazi” akasema
Edwin
“Nilimwambia Melanie
kwamba nitapenda kuja tena
Dar es salaam kwa mapumziko
ya hata wiki moja na
amenihakikishia
nisihofu.Ninakubaliana na
Melanie kwamba nisihofu
kuhusu kuja Tanzania kwani
nina hakika wa kuja na
kuondoka salama kwa sababu
yako.Hongera sana Edwin”
akasema James Kasai na
kumpa mkono Edwin
kumpongeza
“Nashukuru sana James
na ninakuahidi kwamba kwa
muda wowote ambao utahitaji
kuja nchini Tanzania
unakaribishwa na
ninakuhakikishia utakuwa
salama” akasema Edwin
“Ndugu zangu
ninawashukuru sana kwa
ushirikiano wenu
mkubwa.Tutaendelea
kuwasiliana”akasema James
Kasai huku akiwapa mikono
Melanie na Khalid halafu
akaagana na watumishi wawili
wa Melanie kisha wakatoka nje
kuelekea garini.
Melanie na James
wakakumbatiana
wakaagana.James
akafunguliwa mlango akaingia
garini Edwin akaliondoa
taratibu huku Melanie
akipunga mkono kisha
akarejea ndani.
 

mbududa

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2017
Messages
596
Points
1,000

mbududa

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2017
596 1,000
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 10 : EPISODE 17
Mathew Mulumbi akiwa
ndani ya buti ya gari akielekea
bohari kuu la SNSA simu yake
ikaita alikuwa ni Ruby
“Hallo Ruby ! akasema
Mathew
“Mathew uko wapi mbona
unapatikana kwa mbali sana?
“Niko ndani ya buti ya gari
ninaelekea bohari kuu
SNSA.Vipi maendeleo
huko?Kuna chochote
umekipata?akauliza Mathew
“Edwin Mbeko ameondoka
hapa muda mfupi uliopita
akiwa na James
Kasai.Inaonekana James Kasai
anaondoka nchini”akasema
Ruby
“Kama vile
nilivyohisi.Thank you
Ruby.Watanikuta kule katika
bohari”
“Mathew kuwa makini
sana na hawa jamaa” akasema
Ruby
“Usihofu Ruby.Endelea
kufuatilia kila kinachoendelea
hapo katika hiyo nyumba”
akasema Mathew na kukata
simu.
Taratibu Jackson alianza
kupunguza mwendo wa gari
alipokaribia kufika geti kuu la
bohari ambako mmoja wa
walinzi aliwasha taa yenye
maandishi yanayomtaka
asimame.Taratibu akapunguza
mwendo wa gari na kusimama
walinzi wakaanza kulisogelea
gari.Akiwa ndani ya buti ya
gari Mathew alikuwa
amejiweka tayari endapo
kungetokea tatizo
lolote.Jackson akashusha kioo
cha gari na walinzi wakajikuta
wakiangua kicheko baada ya
kumuona.Hawakulikagua tena
gari bali yakaanza maongezi
mafupi
“Samahani mkuu
hatukujua kama ni
wewe.Unabadili magari sana
siku hizi” akasema mmoja wa
wale walinzi kisha geti
likafunguliwa Jackson
akaingia ndani ya bohari.Moja
kwa moja akaenda kuegesha
gari katika maegesho ya
magari.Kulikuwa na magari
manne ya wafanyakazi lake
likawa la tano.Akafungua
mlango akashuka na kuangaza
angaza kama kuna mlinzi
karibu na eneo lile lakini
hakuona mlinzi yeyote
akaenda nyuma ya gari na
kugonga buti mara
mbili.Mathew Mulumbi
taratibu akafungua buti na
kuchungulia nje
“Kuko shwari kaka hakuna
mlinzi yeyote mahala hapa”
akasema Edwin huku macho
yake yakigeuka kama kinyonga
kutazama kila upande.Haraka
haraka Mathew akatoka ndani
ya buti ya gari na kuingia
katika kiti cha nyuma.
“Eneo liko kimya sana hili”
akasema Mathew
“Ile pale ni karakana ya
kutengenezea magari mabovu
ya idara ingawa kwa sasa
haitumiki tena kwani magari
yote hupelekwa katika gereji
binafsi.Lile pale ndilo jengo la
bohari.Ndani mle kuna vitu
mbalimbali vya idara” Jackson
akamuelekeza Mathew
“Silaha pia mnahifadhi
mle?
“Hapana silaha
hazihifadhiwi hapa.Hifadhi ya
silaha iko kule wanakoishi
kikosi cha makomando wa
SNSA” akajibu Jackson na
mara ukasikika mlio wa
helkopta
“Hiyo ndiyo helkopta ya
idara ambayo ataondoka nayo
Edwin” akasema Jackson na
wote wakaishuhudia helkopta
ile ikitua katika sehemu yake
maalum.
“Sogeza gari karibu”
akasema Mathew na Jackson
akawasha gari akalisogeza
taratibu karibu na helkopta
kama alivyoelekezwa na
Mathew.Injini ya helkopta
ikazimwa
“Nataka ukamtoe Rubani
ndani ya helkopta umpeleke
ndani ya jengo.Can you do
that?akauliza Mathew na
Jackson akashuka garini
akafungua mlango mkubwa wa
helkopta.
“Desmond ! akasema
Jackson akisalimiana na Yule
rubani
“Jack mambo vipi.Naona
umewahi sana”
“Nimefika hapa dakika
chache zilizopita.Safari ya
wapi?
“Tunaelekea Kagera”
akajibu Yule rubani
“Safari ndefu sana.Twende
ndani tukapate vitafunwa
kabla bosi hajafika.Yuko mbali
hataweza kufika sasa hivi”
akasema Jackson
“Wazo zuri Jack.Ninahitaji
pia kujisaidia” akasema Yule
rubani na kushuka ndani ya
helkopta
“Gari zuri sana
hili”akasema Desmond baada
ya kuliona gari lile alilokuwa
anaendesha Jackson
“Usafiri wangu mpya
huu.Twende ndani utakuja
kulijaribu ukirejea kutoka
Kagera.Nitakuachia wiki
nzima ulitumie” akasema
Jackson na kumuondoa
Desmond aliyekuwa ameshika
kitasa cha mlango akitaka
kufungua kuangalia gari lile
kwa ndani.
Mara tu walipoondoka
Mathew Mulumbi akashuka
kutoka ndani ya gari
akaufungua mlango wa
helkopta akaingia ndani
akafungua begi lake akatoa
bomu na kulitega ndani ya
helkopta halafu akatoka na
kuingia ndani ya gari.Kilikuwa
ni kitendo cha haraka sana.
Kwa mbali aliwaona
Jackson na Desmond
wakirejea.Desmond akafungua
mlango wa mbele akaenda
kuketi katika kiti chake akiwa
ameshika mfuko uliokuwa na
vitafunwa mbalimbali
walivyovitoa ndani.Jackson
akaliondoa gari na kulirejesha
sehemu ya maegesho
Zilipita dakika thelathini
na nane gari la Edwin Mbeko
likawasili kwa kasi na kwenda
kusimama mbali kidogo na
helkopta.
“Edwin tayari
amewasili.Nini
kinaendelea?akauliza Jackson.
“Subiri kwanza washuke
garini” akasema Mathew.
Rubani wa helkopta
akashuka na kwenda katika
gari la Edwin akafungua
mlango Edwin
akashuka.Akazunguka upande
wa pili akafungua mlango
akashuka James Kasai
wakaanza kutembea kuelekea
ilipo helkopta.
“It’s show time” akasema
Mathew na kukibonyeza
kidude alichokuwa amekishika
mkononi na mara ukatokea
mlipuko mkubwa helkopta
ikalipuka.Edwin,James Kasai
na Desmond wote wakaanguka
chini.Kama mshale Mathew na
Jackson wakachomoka kutoka
katika lile gari kuwafuata
akina Edwin.James Kasai
ndiye aliyekuwa wa kwanza
kuinuka kutoka mahala pale
walipoangukia akamfuata
Edwin Mbeko aliyekuwa
ameanguka na kumsaidia
kuinuka.Mara Edwin
akachomoa bastora baada ya
kuiona sura ya Mathew
Mulumbi akikimbia kuelekea
mahala walipo
“Run ! Edwin
akamwambia James Kasai
kisha akaanza kuachia risasi
kuelekea upande wa Mathew
mara kiganja cha mkono wake
kikapigwa risasi bastora
ikaanguka.
“Aaaaggghhh ! Edwin
akatoa mguno na mara
akapigwa tena risasi nyingine
ya paja.James Kasai aliinuka
na kuanza kukimbia huku
akigeuka nyuma na kuachia
risasi lakini Mathew aliendelea
kumkimbiza.
“Leo ni mimi au wewe
shetani wewe ! akasema
Mathew na kuongeza mbio
kumfukuza James aliyekuwa
anaelekea yalipo magari
mabovu.James aligeuka
akaachia risasi Mathew
akajibanza katika mnazi James
alipogeuka ili aendelee
kukimbia Mathew akaachia
risasi mfululizo na James
akaanguka chini.Alipigwa
risasi kiunoni.Licha ya
kupigwa risasi bado James
aligeuka na kuanza kuachia
risasi hovyo na moja ya risasi
ikamchubua Mathew shingoni
akajibanza nyuma ya mti
uliokuwa karibu.
“Shetani Yule angeweza
kuniua ! akawaza Mathew
huku akiendelea kusikia
mivumo ya risasi kutoka kwa
James Kasai.
“Siwezi kumuacha huyu
muuaji akatoroka” akawaza
Mathew na kugeuka haraka
akaanza kuachia risasi
mfululizo.James Kasai
aliyekuwa anajivuta kuelekea
katika mojawapo ya gari
akapigwa risasi nyingine
katika mguu wa kushoto na
katika bega la kushoto akalala
sakafuni.Huku akigugumia
kwa maumivu James akageuka
akiwa ameishika bastora yake
akamuona Mathew akimfuata
akaizinga bastora ili kuachia
risasi lakini bastora yake
haikuwa na kitu.Risasi
zilikwisha malizika.
“Aaaaghh ! akasema
Mathew kwa hasira huku
akimimina risasi katika
bunduki yake na kifua cha
James hakikutazamika
tena.Bunduki ile ya Mathew
ilikwisha risasi akaitupa
akachukua bastora
akamtazama kwa hasira James
ambaye tayari alikwisha fariki.
“Edwin weka bastora yako
chini.It’s over ! sauti kali
ikamuamuru Edwin aliyekuwa
anagugumia kwa maumivu ya
kupigwa risasi.Edwin alipatwa
na mstuko mkubwa akabaki
anashangaa asiamini macho
yake alipomuona Jackson
akiwa na bastora inayofuka
moshi.
“Jack ?!! akasema Edwin
kwa mshangao
“It’s over Edwin ! akasema
Jackson ambaye alifanya kosa
kubwa kugeuka kutazama
walinzi waliokuwa wakikimbia
kuelekea eneo lile.Edwin
akaitumia nafasi ile akaiokota
bastora yake kwa mkono wa
kushoto akamlenga Jackson na
kuachia risasi zilizompata Jack
akaanguka chini.
Walinzi waliokuwa na
vizimia moto walifika na
kuanza kuuzima moto ule.
“Kuna jambazi
amekimbilia kule
karakana.Hakikisheni
mnampata ! akaelekeza Edwin
kisha Desmond akamtaka
mmoja wa walinzi amsaidie
wakamnyanyua Edwin
kumpeleka katika bohari.
Baadhi ya walinzi
waliokuwa na silaha wakaanza
kuelekea eneo lile la karakana
kulikokuwa na magari mabovu
kwa ajili ya kumsaka jambazi
waliyeelekezwa na Edwin.
“Hatimaye nimefanikisha
kile nilichokuja
kukifanya.Nilikuja Tanzania
kukuua na nimefanikiwa
kukuua ! akasema Mathew
huku akimtazama James Kasai
aliyekuwa amechafuliwa kwa
risasi.Mara akasikia sauti ya
mbwa akibweka.
“Wananitafuta ! akawaza
kisha akazama ndani ya
uvungu wa gari na kutokea
upande wa pili akajibanza
katika moja wapo ya
gari.Walinzi wale
walioongozwa na mbwa
mkubwa wakaukuta mwili wa
James Kasai.Mmoja wa walinzi
akachukua redio ya
mawasiliano na kuibonyeza
akawataarifu wenzake
“Jambazi mmoja ameuawa
huku katika karakana ya
magari” akasema Yule jamaa
akidhani James Kasai ndiye
jambazi waliyetumwa
wamtafute.Ghafla Mathew
Mulumbi akajitokeza akiwa na
bastora mbili na kuanza
kunyesha mvua ya risasi
walinzi wale wakaanguka chini
wote.Mbwa Yule mkubwa
akatoka mbio na kutaka
kumrukia lakini Mathew
alikwisha muona na kumpa
konde zito la mkono wa kuliwa
mbwa akaanguka chini
hakuinuka tena
“Zamu ya Edwin Mbeko”
akasema Mathew na kutoka
eneo lile la karakana akawaona
baadhi ya walinzi na
wafanyakazi wakiendelea na
zoezi la kuzima moto.
“Lazima nimpate Edwin”
akawaza Mathew kisha
akachukua bomu la kurusha
kwa mkono akang’oa kifuniko
na kulirusha mbali kidogo na
ule moto uliokuwa unawaka
likalipuka na kuzua taharuki
kubwa watu wakaacha kuzima
moto wakaanza kukimbia
kunusuru maisha yao.Mathew
akaitumia fursa ile akatoka
mbio kuelekea mahala moto
ulipokuwa unawaka akastuka
baada ya kumuona Jackson
akiwa amelala chini
“Oh no ! akasema Mathew
kwa mstuko na kumfuata
Jackson akamtingisha
“Jack ! Jack ! akaita
Mathew na Jack akafumbua
macho
“Edwin alinipiga risasi
akadhani ameniua nami
nikalazimika kujifanya
nimekufa.Ahsante kwa hii
fulana ya kuzuia risasi
imeokoa maisha yangu”
akasema Jackson
“Yuko wapi Edwin?
“Ameingia ndani ya jengo”
akasema Jackson Mathew
akamshika mkono
akamnyanyua
“James Kasai tayari
nimemuua.Tunamfuata
Edwin” akasema Mathew
wakaanza kukimbia kuelekea
katika jengo la bohari
alikoenda Edwin
Desmond alikwenda katika
stoo ya vifaa vya afya
akachukua bandeji na
kumfunga Edwin jeraha lake la
risasi katika kiganga cha
mkono ili kuzuia damu
kuendelea kuvuja.
“Desmond I need to get
out of here before that nataka
uende ukamtafute Yule jamaa
niliyekuwa naye garini.Chukua
walinzi muelekee katika
karakana ndiko
alikoelekea.Hakikisha
unampata” akasema Edwin na
kumpa Jackson bastora
“Mkuu kwa nini
nisichukue gari nikakuondoa
kwanza wewe haraka ili
ukapate matibabu?Eneo hili
limekwisha kuwa hatarishi na
yawezekana wale jamaa wakaja
na kukukuta humu
wakakumaliza” akasema
Desmond
“Desmond siwezi
kuondoka hapa bila Yule mtu
niliyekuja naye ! Go find him !
akasema Edwin.Desmond na
Yule mlinzi walitoka Edwin
akachukua simu yake
akampigia Melanie
“Edwin ! akasema Melanie
“Melanie tumevamiwa !
akasema Edwin
“Mmevamiwa?! Melanie
akastuka
“Ndiyo.Tumevamiwa na
watu siwafahamu.Helkopta
yetu imelipuliwa na bomu”
“Mungu wangu.Are you
okay?akauliza Melanie kwa
sauti iliyojaa wasi wasi
“Nimepigwa risasi lakini
James amekimbia nimetuma
watu wakamtafute”
“Edwin get out of there
now !
“Melanie siwezi kuondoka
nikamuacha James
Kasai.Lazima nimpate ndipo
tuondoke hapa.Melanie sikiliza
kama kuna kitu chochote
kitanitokea basi usihofu kila
kitu kitakwenda kama
kilivyopangwa.Tayari Yule
kijana wetu aliyebeba bomu
yuko uwanjani akiwasubiri
marais wafike” akasema Edwin
“Edwin tafadhali jitahidi
uweze kuondoka hapo mara
moja” akasema Melanie
“Nitaondoka
Melanie.Nimewatuma watu
wakamchukue James kisha
tutaondoka.Nitakujulisha
kinachoendelea” akasema
Edwin na kukata simu
“Taratibu wekeni silaha
zenu chini na kisha muinue
mikono” Sauti kali
ikawaamuru Desmond na Yule
jamaa aliyekuwa naye mara tu
walipojitokeza katika mlango
wa kuingilia katika
bohari.Taratibu wakaweka
silaha chini.
“Yuko wapi Edwin
Mbeko?akauliza Mathew
.Desmond akamtazama
Jackson kwa hasira
“Sikujua kama u msaliti
kiasi hiki Yuda wewe !
akasema kwa ukali
“Shut up ! akafoka Mathew
“Yuko wapi
Edwin?akauliza Mathew
“Hatufahamu alip……”
Kabla Desmonda hajamaliza
sentensi yake tayari Mathew
aliizinga bastora na kumchapa
risasi Desmond akabaki Yule
mlinzi
“Yuko wapi
Edwin?akauliza Mathew
“Yuko ndani ! akajibu Yule
mlinzi kwa woga na Mathew
akamtaka ampeleke mahala
alipo Edwin Mbeko.
“Desmond ! akaita Edwin
Mbeko aliposikia hatua za
watu wakielekea mahala alipo
“Desmond is that you?
Akauliza tena Edwin na
Mathew akampiga Yule mlinzi
pigo moja kichwani akaanguka
chini akaanza kunyata akifuata
sauti ile
ilikotokea.Akausukuma
mlango wa moja wapo ya
chumba na Edwin Mbeko
akakutwa akiwa amekaa
chini.Wakatazamana kwa
sekunde kadhaa.
“Ni wewe uliyeshirikiana
na Annabel kumuua Fidelis na
mmeshirikiana tena kuvamia
bohari yetu na kufanya
uharibifu mkubwa.Umekosea
sana kwa hiki
ulichokifanya”akasema Edwin
Mbeko
“Naamini umeniona lakini
hunifahamu .Naitwa Mathew
Mulumbi”
“Mathew Mulumbi?!
Edwin akashangaa
“Wewe ndiye uliyevamia
ofisi zetu !
“Ni mimi niliyevamia ofisi
zenu na nilikuja kukutafuta
wewe ! Sikukupata siku ile
lakini leo nimekupata.Edwin
nafahamu yote
unayoyafanya.Nafahamu
umekuwa unashirikiana na
Melanie Davis.Ninafahamu
kila kitu unachokifanya
kushirikiana na magaidi na
sitaki kuyasema hapa.Kwa
taarifa yako James Kasai
amekwisha fariki
dunia.Nimemuua kwa mkono
wangu.Fahamu vile vile
kwamba hivi tunavyoongea
kuna watu wako nje ya
nyumba ya Melanie Davis na
muda wowote atatiwa nguvuni
na mtandao wenu wote
utasambaratika.Naweza
kukusaidia Edwin na kukuacha
hai lakini ni pale utakapoamua
kunieleza ukweli”
“Unajidanganya wewe
marehemu.Hakuna chochote
utakachoweza kukipata.Wewe
na hao waliokutuma
mmejidanganya” akasema
Edwin.Simu ya Mathew ikaita
alikuwa ni Ruby
“Mathew nimemuona
Khalid.Yuko ndani ya nyumba
hii” akasema Ruby
“Ruby are you sure?
“Ndiyo
Mathew.Nimemuona.Ametoka
muda si mrefu nje.Yuko na
Melanie wamekaa katika
sehemu ya kupumzikia
bustanini wakijadiliana jambo”
“Ahsante Ruby.Nitafika
hapo muda si mrefu” akasema
Mathew na kukata simu
“Tayari tunafahamu
mahala alipo Khalid Sultan
Khalid na muda si mrefu
kutoka sasa naye
atauawa.Nitakuacha hai kama
utanieleza ni kitu gani
mmepanga kukifanya hapa
Dar es salaam leo?akauliza
Mathew
“Go to hell ! akasema
Edwin
“Mara ya mwisho Edwin
nakuuliza nini mmepanga
kukifanya leo hii?Nijibu na
ninakuahidi sintakuua”
“Unadhani ninaogopa
kufa? Najua nitakufa lakini
mmeshachelewa sana.Hakuna
chochote mtakachoweza
kukifanya kwa sasa.Hadi jioni
ya leo tayari mtakuwa
mmepata salamu” akasema
Edwin
“Mara ya mwisho Edwin
nakuuliza nini mmepanga
kukifanya leo?Wapi
mmepanga
kushambulia?akauliza Mathew
na Edwin akacheka
“Wewe na wapumbavu
wenzako nimewaambia tayari
mmechelewa sana.Subirini
mtapata majibu! Akasema
Edwin Mathew akapandwa
hasira akaanza kummiminia
Edwin risasi na kumuua
akaichukua simu yake haikuwa
na laini.Pembeni yake
kulionekana vipande vya laini
ya simu iliyoharibiwa
“Bazazi huyu ameharibu
laini yake ya simu ! akasema
Mathew.
“Jackson tuondoke haraka
eneo hili” akasema Mathew
wakatoka kwa
haraka.Hakukuwa tena na
watu eneo lilikuwa tupu watu
wote walikimbia kuokoa
maisha yao.Jackson aliingia
katika gari lao Mathew
akamuelekeza kulisogeza
katika karakana wakasaidiana
kuubeba mwili wa James Kasai
wakauweka katika buti ya gari
kisha wakaondoka.Katika geti
kuu la kuingilia bohari
waliwakuta baadhi ya walinzi
na wafanyakazi wakiwa
wamekusanyika Mathew
akatoa bomu la kutupa kwa
mkono akang’oa kifuniko na
kulirusha likalipuka na watu
wote wakalala chini halafu
wakainuka na kuanza
kukimbia.Mathew akashuka
akafungua geti wakaondoka.
“Kilichotokea pale ndani ni
kama filamu lakini ni kitu cha
kweli.Huyu jamaa ni mtu
hatari sana.Sikujua kama ana
uwezo mkubwa namna hii wa
kupambana.Sikutegemea
kama tungeweza kutoka
hai.Nashukuru alinipa fulana
ya kuzuia risasi kwani bila ile
hivi sasa ningekuwa
marehemu” akawaza Jackson
 

mbududa

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2017
Messages
596
Points
1,000

mbududa

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2017
596 1,000
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 10 : EPISODE 18
Melanie alichanganyikiwa
baada ya kupigiwa simu na
Edwin akamjulisha kwamba
wamevamiwa na watu
wasiojulikana.Mara tu Edwin
alipokata simu Melanie
akamfuata Khalid chumbani
kwake akamtaka watoke nje
wakazungumze wakaenda
kuketi nje bustanini
“Melanie kuna
nini?Mbona unaonekana una
wasiwasi mwingi?akauliza
Khalid
“Kuna jambo limetokea
Khalid”
“Jambo gani
Melanie?akauliza Khalid
“Nimepigiwa simu na
Edwin ameniambia
wamevamiwa na watu
wasiojulikana”
“Wamevamiwa?
“Ndiyo”
“Imekuaje wakavamiwa?
Ni tukio la ujambazi? akauliza
Khalid
“Hajanieleza vizuri kwa
undani”
“Wako salama yeye na
James Kasai?akauliza Khalid
“Helkopta yao
imelipuliwa,Edwin amepigwa
risasi na James
amekimbia.Nimechanganyikiw
a Khalid sina hakika kama
watatoka salama”
“Melanie tunatakiwa
kutafuta namna ya kuwasaidia
wenzetu kabla mambo
hayajawa mabaya.Kwanza
kama James Kasai amekimbia
ni mbaya zaidi kwani
anafahamika,picha zake ziko
kila mahali hawezi kufika
mbali atajulikana.Edwin naye
amepigwa risasi na Yule ndiye
pekee tuliyekuwa
tunamtegemea aweze
kumuondoa James Kasai hapa
nchini.Kama helkopta
imelipuliwa basi utakuwa ni
mlipuko mkubwa na lazima
litakuwa ni bomu hivyo basi
watu wa karibuna eneo hilo
watakuwa wameusikia
mlipuko huo na kutoa taarifa
kwa vyombo vya
usalama.Polisi wakifika hapo
wanaweza wakampata James
Kasai na kila kitu
kikaharibika.Tunatakiwa
kuwaondoa haraka sana eneo
la tukio Edwin na James Kasai
kabla polisi hawajafika”
akasema Khalid
“Hilo unalosema ni la
kweli Khalid lakini namna gani
tutaweza kuwaondoa James
Kasai na Edwin mahala
hapo?Mimi sina kikosi na mtu
pekee niliyekuwa namtegemea
ni Edwin ambaye naye
amepigwa risasi”akasema
Melanie
“Usihofu.Sisi tunao vijana
wetu hapa Dar es
salaam.Ninaomba simu yako
nataka kuwasiliana na mtu
Fulani ili anipatie vijana wa
kwenda kuwakomboa James
na Edwin” akasema Khalid na
Melanie akampa simu
yake.Khalid akaenda ndani na
baada ya muda akarejea akiwa
na kitabu kidogo akakifungua
akaipata namba ya simu ya
mtu aliyetaka kumpigia
akapiga.Akazungumza kiarabu
na mtu Yule kwa takribani
dakika tano halafu akampa
simu Melanie akamtaka
amuelekeze Yule mtu pale
mahala walipo Melanie
akamuelekeza Yule mtu kisha
akampatia simu Khalid
ambaye aliendelea
kuzungumza tena na Yule
jamaa halafu akakata simu
“Huyu niliyezungumza
naye ni mkuu wa kundi la IS
hapa nchini na ukanda wote
wa Afrka Mashariki anaitwa
Sayid Al Noor.Nilitakiwa
kuonana naye jioni ya leo
baada ya shambulio kutokea
lakini kwa hili lililojitokeza
nimelazimika kumuomba
msaada na vijana watakuja
hapa muda si mrefu ili kupata
maelekezo ya mahala walipo
Edwin na James Kasai.Kitu
cha msingi kabla vijana hao
hawajafika tunatakiwa
kufahamu mahala walipo
akina Edwin” akasema Khalid
“Sifahamu mahala
walipo.Alisema wanakwenda
katika bohari kuu na sifahamu
bohari hilo liko wapi.Ngoja
nimpigie simu nimuombe
anielekeze” akasema Melanie
na kupiga namba za simu za
Edwin lakini simu yake
haikupatikana.Akajaribu tena
lakini bado simu
haikupatikana.
“Simu yake haipatikani
tena.Nitawasiliana na nani
anisaidie?Simfahamu mtu
mwingine yeyote wa idara
yake” akawaza Melanie na
mara akapata wazo
“Devotha ! Ngoja
nimtafute” akawaza na
kuzitafuta namba za simu za
Devotha akampigia lakini simu
ya Devotha haikuwa
ikipatikana.
“Mungu wangu nini hiki
kinaendelea? Mbona kila
ninayempigia kumuomba
msaada hakuna
anayepatikana?Devotha naye
yuko wapi?Kwa nini
hapatikani kuanzia jana?Joyce
naye hayupo najuta kwa nini
nilimkubalia aondoke asubuhi
ya leo kwenda Kigoma.Ngoja
nimjaribu pengine anaweza
kuwa na msaada” akawaza
Melanie akampigia simu Joyce
dereva wake lakini naye simu
yake haikupatikana
“Aliyesema siku ya kufa
nyani miti huteleza
hakukosea.Timu ya kwenda
kuwaokoa akina Edwin inakuja
na sijui mahala Edwin
alipo.Nimepata wazo ngoja
nimjaribu Peniela yawezekana
akawa amepata taarifa za alipo
Devotha.Yule ndiye msuka
mipango yote kwa nini
ametoweka ghafla wakati
kama huu?Hakupaswa
kuondoka bila kutujulisha
kwani yeye ndiye
tunayemtegemea sana kwa kila
kitu” akawaza Melanie na
kumpigia Peniela simu ikaita
akashusha pumzi
“Afadhali huyu simu yake
inaita” akawaza Melanie na
mara simu ikapokelewa
“Hallo Melanie” akasema
Peniela
“Peniela samahani kwa
usumbufu”
“Bila samahani
Melanie.Nikusaidie nini?
“Nataka kujua kama
ulifanikiwa kumpata Devotha”
“Hapana sikufanikiwa
kumpata”
“Mungu wangu ! akasema
Melanie
“Kwani vipi Melanie?Una
shida naye sana?
“Ndiyo Peniela nina shida
naye kubwa sana” akasema
Melanie
“Sikiliza Melanie kama
Devotha hayupo hata mimi
ninaweza kukusaidia.Kama
kuna kitu kimekwama niambie
nina mtandao mkubwa tu
hapo Tanzania na mashariki
kwa ujumla” akasema Peniela
“Kuna rafiki yangu
amevamiwa na
majambazi.Amenipigia simu
muda si mrefu akaniambia
kwamba amevamiwa na
amepigwa risasi.Ninataka
kufahamu mahala alipo ili
nitume watu
wakamsaidie.Devotha
anafahamiana na watu wa
mitandao ya simu ambao
wanaweza wakafahamu huyo
rafiki yangu alikuwa wapi
aliponipigia simu. Hilo ndilo
kubwa ninalolihitaji”
“Usiwe na wasiwasi
Melanie.Hata kama Devotha
hayupo nitakusaidia.Ninao
mtandao mkubwa tu hapo
Tanzania.Nielekeze mahala
ulipo kuna mtu ambaye ni
mtaalamu wa hayo mambo ya
mtandao.Nitamuelekeza afike
kwako haraka sana akusaidie”
akasema Peniela na Melanie
akamuelekeza mahala alipo
“Usihofu
Melanie.Ninamuelekeza huyo
mtu wangu anakuja hapo sasa
hivi atakusaidia kujua mahala
alipo mtu wako” akasema
Melanie
“Nashukuru sana Peniela”
“Usijali Melanie.Muda
wowote ukiwa na tatizo
nijulishe nitakusaidia”
akasema Peniela na kukata
simu
“Umejileta wewe
mwenyewe katika mdomo wa
Mamba na mimi kazi yangu ni
kukutafuna.Pole sana Melanie
kwani mbio zako zimefika
ukingoni” akasema Peniela na
kumpigia simu Mathew
“Peniela ! akasema
Mathew
“Mathew nimepigiwa simu
na Melanie muda mfupi
uliopita anamtafuta Devotha
nikamuomba anieleze shida
yake nimsaidie akaniambia
kwamba anamtafuta rafiki
yake ambaye ametekwa na
watu wasiojulikana na anataka
atume watu wakamsaidie
lakini hafahamu mahala huyo
rafiki yake alipo.Anachohitaji
ni mtu wa kumsaidia kujua
rafiki yake alipiga simu akiwa
wapi? Nimemwambia kwamba
ninamtumia mtu ambaye ana
uwezo huo wa kumsaidia na
kujua mahala alipo huyo rafiki
yake.Mathew hii nafasi
imepatikana ya kummaliza
Melanie.Utakwenda nyumbani
kwake na utajifanya wewe
ndiye huyo mtu ambaye
unataka kumsaidia kujua
mahala alipo rafiki
yake”akasema Peniela
“Peniela sijui
nikushukuruje kwa msaada
huu mkubwa
ulionisaidia.Sikutegemea
kab….”
“Mathew tusipoteze
muda.Melanie anakusubiri
sasa hivi.Ukifika mwambie
umetumwa na Peniela”
akasema Peniela
“Ahsante Peniela”
akasema Mathew na kukata
simu na kumpigia simu Ruby
“Ruby nimepigiwa simu na
Peniela muda si mrefu
ameniambia kwamba Melanie
amempigia simu akamuomba
amsaidie kupata mtu ambaye
atamsaidia kujua rafiki yake
aliyetekwa yuko wapi ili atume
watu wakamsaidie.Nadhani
Edwin Mbeko alimpigia simu
akamjulisha kilichotokea.
Peniela amemwambia kwamba
anamtuma mtu nyumbani
kwake muda si mrefu ili aweze
kumsaidia”
“Mathew this is our chance
to finish Khalid Sultan”
akasema Ruby
“Ondoka hapo ili tukutane
tuweze kujipanga namna ya
kuingia mle ndani” akasema
Mathew na kumueleza Ruby
sehemu ya kukutana.”
akasema Mathew na kukata
simu akamuelekeza Jackson
aongeze mwendo wa gari.
 

mbududa

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2017
Messages
596
Points
1,000

mbududa

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2017
596 1,000
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 10 : EPISODE 19
Mazungumzo kati ya
marais watatu yalimalizika
ikulu Dar es salaam na marais
wale ambao kwa siku chache
zilizopita hawakuwa
wakitazamana usoni kufuatia
shambulio lililofanywa na
James Kasai nchini Tanzani
ambaye anatajwa kufadhiliwa
na serikali ya Uganda.Katika
kikao hicho ambacho
mazungumzo yake yalikuwa ya
kirafiki sana Jenerali Akiki
Rwamirama Rais wa Uganda
aliahidi kutoa ushirikiano
katika zoezi la kumsaka James
Kasai.
Kikao kilimalizika kwa
mafanikio makubwa sana na
marais wote wakashikana
mikono kupongezana kwa
mafanikio yale makubwa
“Tulichokifanya leo ni kitu
cha kihistoria na kitaingia
katika vitabu vya
historia.Tumeonyesha mfano
kwa mataifa mengine kwamba
tunaweza kuzungumza na
kumaliza tofauti zetu sisi
wenyewe.Tumewaabisha wale
waliodhani labda Afrika
Mashariki itasambaratika
.Ahsante sana Jenerali Akiki
kwa kujisusha kwa ajili ya
maslahi ya Afrika Mashariki”
akasema Dr Fabian
Jenerali Akiki ndiye
aliyekuwa wa kwanza
kuondoka kurejea Uganda na
kuwaacha Rais Patrice Eyenga
na Dr Fabian ambao walikuwa
na mazungumzo mengine ya
faragha.Waziri wa mambo ya
nje wa nchi ndiye
aliyemsindikiza Rais Akiki
uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere.
 

mbududa

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2017
Messages
596
Points
1,000

mbududa

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2017
596 1,000
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 10 : EPISODE 20
Mathew akiwa na Ruby
ndani ya gari waliwasili
nyumbani kwa
Melanie.Mathew aliyekuwa
katika usukani akapiga honi
mara tatu halafu geti
likafunguka
“Are you ready
Ruby?akauliza Mathew
“I’m ready” akajibu Ruby
kisha gari likaingia ndani
taratibu geti
likajifunga.Mathew akapeleka
gari hadi katika
baraza.Mwanamke mmoja
akaenda katika kioo cha
dirisha akagonga.Ruby
akafungua mlango akashuka
.Yule mwanamke akampekua
kama ana silaha
“Huyu nani ndani ya
gari?akauliza Yule mwanamke
“Huyu ni dereva wangu”
akasema Ruby na Yule
mwanamke akamtaka Mathew
atoe gari pale karibu na
mlango mkuu wa kuingilia
sebuleni.
“Hakuna haja.Ninachukua
muda mfupi sana hapa kisha
naondoka” akasema Ruby
akionekana kuwa na
haraka.Yule mwanadada
akamuongoza Ruby kuingia
sebuleni akakutana na Melanie
“Karibu sana dada”
akasema Melanie
“Melanie Davis?akauliza
Ruby
“Ndiyo.Umetumwa na
Peniela?
“Ndiyo nimetumwa na
Peniela”akasema Ruby
“Karibu sana”
“Ahsante.Wapi tunafanyia
kazi yetu?akauliza Ruby
“Hapa hapa sebuleni
hakuna tatizo” akajibu Melanie
na Ruby akaitoa kompyuta
katika mkoba akaanza kazi
yake.Ruby alicheza na
kompyuta haraka haraka kama
vile ana vidole sita kila mkono
na hakuna aliyejua kitu
alichokuwa anakifanya.Kitu
cha kwanza alichokifanya ni
kuunganisha kamera ya siri
katika kompyuta yake na
kompyuta ndogo iliyokuwamo
ndani ya gari ili kumuwezesha
Mathew kuona kile
kinachoendelea mle
ndani.Alipokamilisha hilo
akaomba namba za simu za
mtu ambaye anamtafuta kisha
akaziingiza katika program
yake na kuanza kutafuta
mahala alipo Yule mtu.
Kupitia ile kompyuta
ndogo aliyounganishwa na
Ruby,Mathew aliweza kuona
namna watu walivyokaa mle
ndani.Ruby alikuwa mezani
halafu kukawa na wanawake
wawili wakiwa nyuma ya
Melanie.Mathew akaziweka
sawa bastora zake halafu
akafungua mlango taratibu na
kwa tahadhari akashuka
akatembea kuelekea katika
mlango mkubwa wa
sebuleni.Akakishika kitasa cha
mlango akakinyonga na
kufungua mlango kisha kama
kima akajitoma ndani.
Kabla hajafanya chochote
mmoja wa wale wanawake
akamsukuma Melanie
akaanguka chini kisha
mwingine akachomoa bastora
na kuanza kumimina risasi
kuelekea kule alikokuwa
Mathew ambaye aliruka na
kujificha nyuma ya kabati
kubwa la vitabu.Yule
mwanamke mwingine
aliyemuangusha chini Melanie
akamuinua na kumuongoza
kukimbia pale sebuleni huku
Yule mwanamke mwingine
akiendelea kuachia risasi
kumzuia Mathew asiweze
kujitokeza.Risasi zilimalizika
katika bastora ya kwanza na
kwa haraka akachukua bastora
ya pili na Mathew akautumia
mwanya huo akajitokeza na
kuanza kuachia risasi.Yule
mwanamke akainua stuli
akairusha Mathew akayumba
kuikwepa na Yule mwanamke
akapata upenyo akainuka na
kuanza kukimbia kufuata
varanda ambalo Melanie na
Yule mwanamke mwingine
walipita.Macho ya Mathew
yalikwisha mng’aza akarukia
katika sofa kisha akarukia juu
ya meza na kuanza
kuvurumisha risasi Yule
mwanadada akaingia katika
mojawapo ya chumba Mathew
akanyata taratibu hadi katika
mlango wa chumba kile
akaupiga teke ukafunguka
akaingia ndani na kwa kasi ya
ajabu mkono wake uliokuwa
na bastora ukapigwa teke
bastora ikaanguka chini
akapigwa teke lingine la
mbavu akaanguka chini na
Yule mwanadada
akamuelekezea bastora.Mara
ghafla akatoa mguno na
kuanguka.Ruby alisimama
mlangoni akiwa na bastora
aliyokuwa ameificha katika
sanduku dogo aliloingia nalo
mle ndani
“Thank you Ruby uko
salama?akauliza Mathew
“Niko salama Mathew.”
akaelekeza Ruby
“Ruby unatakiwa uende
nje niachie mimi nipambane
na hawa watu humu
ndani.Mpigie simuJackson aje
ndani” akasema Mathew
“Mathew siwezi kukuacha
peke yako humu ndani”
akasema Ruby
“Ruby nisikilize.Hii
sehemu ya hatari nenda nje !
akafoka Mathew na Ruby
hakutaka kubishana na
Mathew akachukua kompyuta
yake akatoka kwa tahadhari
hadi katika gari akaliwasha na
kutoka hadi getini akashuka
akajaribu kulifungua geti
halikufunguka akatoa bastora
na kumimina risasi sehemu
ambayo inapokea taarifa
kutoka kompyuta iliyo ndani
akakisambaratisha kiboksi kile
halafu akafungua geti na
kutoka nje.
Baada ya Ruby kutoka
Mathew akaanza kufuata lile
varanda kwa tahadhari
akiingia katika chumba kimoja
kimoja na mara akapigiwa
simu na Ruby
“Kuna gari mbili zimefika
katika geti.Geti halitaweza
kufunguka kwa kompyuta
kwani nimeliharibu” akasema
Ruby
Gari zile mbili zikaanza
kupiga honi ili geti
lifunguliwe.Mathew akasikia
mlio wa simu sebuleni
akaufuata mlio ule na kuiokota
simu iliyokuwa ikiita na mara
ujumbe ukaingia akausoma.
“Vijana tayari wamefika
mahala
mlipoelekeza.Wapokeeni na
muwaelekeze mahala alipo
huyo mtu wakamfuatilie
haraka” ukasomeka ule
ujumbe. Mathew akatoka mle
ndani na kutembea kwa
tahadhari kubwa kuelekea
getini alipolikaribia akatoa
mabomu mawili ya kutupa
kwa mkono akang’oa vifuniko
na kuyarusha nje ya geti yaliko
magari ya wale jamaa na
milipuko kutokea.
Baada ya kuokolewa
sebuleni Melanie Davis na Yule
msaidizi wake walikimbilia
ghorofa ya pili kilipo chumba
cha Melanie
“Mfuate Khalid haraka
chumbani kwake mwambie
tumevamiwa ! akaelekeza
Melanie na kuingia chumbani
kwake.Akajipekua kutafuta
simu yake lakini hakuwa nayo
“Mungu wangu
nimeangusha simu ! akasema
Melanie kwa mstuko.
“Kitu gani Peniela
amenifanyia? Hawa watu
aliowatuma ni akina
nani?akajiuliza Melanie na
kuhisi
kuchanganyikiwa.Akafungua
dirisha akachungulia nje kama
anaweza akaruka akaogopa na
kulifunga.Akatazama saa yake
na kuvuta pumzi ndefu
“It’s over ! hawa watu
wanaonekana tayari
wamekwisha
tufahamu.Naamini ndio hawa
hawa waliomvamia Edwin na
sasa wamekuja kwangu.It’s
over” akawaza kisha haraka
haraka akaenda mezani
akaikunjua kompyuta yake
akaanza kujirekodi.
Kupitia kamera zilizo nje
ya chumba chake Melanie
alimuona Khalid akielekea
katika mlango wa chumba
chake akiwa ameongozana na
Yule mwanamke aliyetumwa
kwenda kumjulisha kwamba
wamevamiwa.Haraka haraka
Melanie akabonyeza sehemu
Fulani na mlango wake
ukajifunga.Khalid alianza
kugonga mlango kisha kwa
hasira akampiga risasi Yule
mwanamke akaanguka
chini.Akaendelea kugonga
mlango kwa nguvu akimtaka
Melanie afungue na alipoona
hafungui akaanza kumimina
risasi katika mlango lakini
mlango ule haukuwa ukipenya
risasi
Baada ya kurusha yale
mabomu nje ya geti,Mathew
akakimbia kuelekea ndani na
alipofika mlangoni akasikia
mlio wa risasi ukitokea ndani
ya ile nyumba.Akaanza
kutembea kwa tahadhari
akifuata ngazi kuelekea
ghorofa ya kwanza akasikia
tena milio ya risasi mfululizo
katika ghorofa ya juu
yake.Akapanda kwa tahadhari
kubwa.Mara tu Mathew
alipojitokeza katika ghorofa ya
pili akakoswa na risasi
ikamlazimu kushuka chini
kidogo.Akachukua kioo kidogo
akakiinua juu na kumuona
mtu mmoja akiwa na bastora
amesimama katika mlango
huku mtu mwingine akiwa
ameanguka chini amepigwa
risasi.Mathew alipoinua
kichwa tu ikasikika milio ya
risasi akajificha tena halafu
akaambaa na mbao ya ngazi
taratibu kisha akaruka na
kutokeza katika varanda
akaachia risasi na kumpiga
Yule jamaa risasi katika bega
la kushoto akaanguka chini
akaanza kumsogelea
“Khalid ! akasema Mathew
baada ya kumgundua mtu Yule
alikuwa ni Khalid Sultan
Khalid.
“Usinisogelee nina bomu !
akasema Khalid na
kumuonyesha Mathew kilipuzi
alichokuwa nacho
mkononi.Khalid alikuwa
amevaa fulana ya
mabomu.Jicho la Mathew
liliona kama la
kinyonga.Aliweza kukiona
kidole gumba kikibonyeza kile
kilipuzi akageuka na kuruka
hatua tatu kubwa na mara
ukasikika mlipuko.Khalid
akajilipua.Mathew akajikuta
amerushwa na kujigonga
ukutani.Baada ya sekunde
kadhaa akajiinua mahala
alipoangukia.Alikuwa
amepasuka juu ya
jicho.Varanda lilijaa
moshi.Akatoa kopo Fulani
katika begi lake alilovaa
mgongoni akapuliza hewa
iliyokuwamo ili kuondoa ule
moshi.
Bomu lile alilolipua Khalid
liliusambaratisha mlango wa
chumba cha Melanie na
sehemu ya chuma ya mlango
ule uliosambaratika ilimpiga
Melanie kichwani akaanguka
chini na kupoteza fahamu.
Moshi ulipungua kufuatia
hewa ile aliyoipuliza Mathew
na akaweza kumuona Khalid
akiwa amesambaratishwa na
bomu.Mlango wa chumba cha
Melanie uling’oka,Mathew
akapuliza ile hewa toka ndani
ya kopo na moshi ukatoka mle
chumbani akauona mwili wa
mwanamke ukiwa umelala
sakafuni akamuendea haraka
haraka akamgeuza alikuwa ni
Melanie Davis ambaye hakuwa
na fahamu.
“I need you Melanie !
akasema Mathew na
kumchunguza kama amekufa
akagundua hakuwa amekufa
bali alipoteza fahamu kwani
bado mapigo ya moyo
yalikuwepo.Haraka haraka
akatoa simu na kumpigia simu
Ruby
“Mathew are you okay?
Tumesikia mlipuko mkubwa
na moshi ukatoka humo
ndani.Nimeogopa”akasema
Ruby
“I’m okay Ruby.Nini
kinaendelea huko nje?
Akauliza Mathew
“Huku nje kuna taharuki
kubwa kufuatia milipuko ile ya
mabomu”
“Jackson yuko karibu?
“Niko hapa kaka” Jackson
akajibu akitokea nje ya kile
chumba kile alimo Mathew
“Niliamua kuingia ndani
kuhakikisha kama uko salama
baada ya mlipuko kutokea”
akasema Jackson
“Niko salama Jackson”
akasema Mathew
“Ruby tayari nimemuona
Jackson”
“Mathew nasikia ving’ora
vya polisi wanaelekea eneo
hili”akasema Ruby
“Tayari wamekwisha pata
taarifa za milipuko ile ya
mabomu” akasema Mathew na
kuiokota kompyuta
iliyoanguka chini.Programu ya
kurekodi ilikuwa
inaendelea.Mathew
akaisimamisha na kuanza
kupitia kile ambacho Melanie
alikuwa
anakirekodi.Akasikiliza kile
alichokisema Melanie
“Mungu wangu ! akasema
Mathew kwa mstuko baada ya
kumaliza kusikiliza maelezo
yale ya Melanie
“President ! akasema na
kumtaka Jackson ambebe
Melanie wakatoka na kuanza
kushuka chini
Magari mawili ya polisi
yaliyojaa askari yakawasili
katika jumba la Melanie na
askari wakashuka haraka
haraka wakalizingira jumba
lile na kuzungusha utepe wa
njano kuzuia watu kukaribia
mahala pale halafu wengine
wakaelekezwa kujiandaa kwa
ajili ya kuingia ndani.Geti
likasukumwa na kikosi cha
askari kumi wakaingia ndani
na mara katika mlango
mkubwa wa kuingilia sebuleni
wakajitokeza Mathew na
Jackson aliyekuwa amembeba
Melanie wakaamriwa
kusimama mahala walipo.
“SNSA” akasema Mathew
huku askari wakiwasogelea
kwa tahadhari
“SNSA tafadhali ! akasema
tena Mathew askari wale
walipowakaribia zaidi
“Tunatoka idara ya SNSA !
akasema Mathew
“SNSA ni kitu gani ?
akauliza kiongozi wa kikosi
kile cha askari
“Secret national security
agency” akasema Mathew na
Yule kiongozi wa kikosi
akachukua kile kitambulisho
cha Jackson akakisoma na
kumrudishia
“Sijawahi kusikia kitu
kama hicho.Ninyi nyote mko
chini ya ulinzi kama mmetoka
idara ya nini mtajitambulisha
huko mbele ya safari” akasema
Yule kamanda
“Afande SNSA ni idara ya
siri ya usalama wa ndani wa
nchi.Sisi tunafanya kazi kama
mnayoifanya ninyi lakini sisi
tunafanya kwa
siri.Unapoendelea kutuweka
hapa afande unatufanya
tushindwe kutimiza wajibu
wetu” akasema Mathew
“Hata sisi tuko kazini
ndugu yangu tusifundishane
kazi” akasema Yule kamanda
“Afande kuna shambulio
limepangwa kufanyika katika
uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere walengwa ni marais
wa Tanzania na jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo.Kuna
bomu liko tayari uwanja wa
ndege na tukichelewa marais
hao watauawa ! akasema
Mathew
“Wapekueni haraka watu
hawa kisha muwafunge pingu
tunakwenda nao kituoni
watajieleza huko mbele ya
safari ! akasema kwa ukali
Yule kamanda.Mathew na
Jackson wakapekuliwa silaha
zao zikachukuliwa na Yule
kamanda akaomba kukiona
kitambulisho cha
Jackson.Akakisoma halafu
akamtazama Mathew
“Nini kimetokea hapa?
Akauliza
“Magaidi wa IS walikuwa
wanaitumia nyumba hii kwa
ajili ya kuandaa mpango wao
wa kuwaua marais wa
Tanzania na Congo”
“Nitaamini vipi kama
kweli idara hii ipo na…..”
“Afande naomba twende
ndani tukazungumze” akasema
Mathew na Yule kamanda
akaongozana na Mathew hadi
ghorofa ya pili
“Huyu ambaye mwili wake
umesambaratika anaitwa
Khalid Sultan Khalid anatoka
kikundi cha IS.Ni mtaalamu
wa milipuko na alikuja hapa
Tanzania kutengeneza bomu
ambalo litatumika kuwaua
marais wetu na kila kitu
kimefanyika ndani ya nyumba
hii.Idara yetu imekuwa
ikiwafuatailia hawa watu kwa
muda sasa na leo tumewatia
nguvuni.Afande tunavyozidi
kukaa hapa maisha ya rais
wetu yako mashakani kwani
tayari bomu limekwisha
ingizwa uwanja wa ndege.Ni
jukumu letu sisi tukisaidiana
na ninyi kuweza kulizuia hilo
lisitokee”
“Bomu hilo unalosema
limeingiaje ndani ya uwanja
wa ndege?akauliza Yule
kamanda
“Kuna askari mmoja
mwenye cheo cha mkaguzi wa
polisi ndiye amesaidia bomu
hilo kuingizwa ndani ya
uwanja wa ndege”akasema
Mathew na Yule kamanda
akaonyesha mshangao
“Ngoja nipige simu
kuwajulisha viongozi walioko
uwanja wa ndege kulitafuta
hilo bomu” akasema Mathew
“Hiyo si njia nzuri na
hawataweza kulipata kwani
aliyelibeba bomu hilo amevaa
sare za askari polisi na endapo
akifahamu kuwa
amegundulika anaweza
akakimbia tukashindwa
kumpata”
“Nini unashauri tufanye?
“Nahitaji kuzungumza na
Rais kumuomba asiende
uwanja wa ndege sasa hivi ili
tuweze kumsaka huyo mtu
aliye na bomu na kumtia
nguvuni” akasema Mathew
“Unataka kuwasiliana na
Rais?
“Ndiyo.Nina mawasiliano
naye” akasema Mathew na
kufunguliwa pingu akampigia
simu Ruby akamueleza
kuhusiana na mpango ule wa
kumuua Rais na kumtaka
ampige simu Rais amzuie
asiende uwanja wa ndege hadi
hapo Yule jamaa mwenye
bomu atakapokamatwa.Ruby
akampigia simu rais lakini
simu hakupatikana.
“Simu ya rais
haipatikani.Tunahitaji kuwahi
uwanja wa ndege kabla
hajafika.Kutoka hapa hadi
uwanja wa ndege si umbali
mrefu.Chukua vijana
wachache tutumie gari la polisi
kuwahi uwanja wa ndege.”
akasema Mathew wakatoka
kwa haraka kwa ajili ya
kuelekea uwanja wa ndege.
Mathew akawaelekeza
Jackson na Ruby kumkimbiza
Melanie hospitali kisha yeye
akaingia katika gari la polisi
ambalo liliondoka kwa kasi
kuelekea uwanja wa ndege wa
Julius Nyerere.
Gari lile la polisi
lilikwenda kwa mwendo mkali
sana huku likipiga king’ora
kuomba kuachiwa njia na
baada ya dakika kumi na saba
wakawasili katika uwanja wa
ndege wa Julius
Nyerere.Kamanda Yule
aliyejitambulisha kwa Mathew
anaitwa Afande Titus
akashuka garini na kupiga
simu halafu akamtaka Mathew
amfuate wakaelekea katika
ofisi Fulani ambako
waliwakuta makamanda
watatu.Afande Titus
akamtambulisha Mathew kwa
makamanda wale wakataka
kufahamu kuhusiana na taarifa
ile ya uwepo wa bomu pale
uwanjani lililolenga kuwaua
marais.Mathew akawaeleza
namna bomu lile lilivyoingizwa
uwanjani wote wakabaki
wanashangaa.Mathew
akawaelekeza namna
watakavyoweza kumpata Yule
askari mwenye bomu
wakakubaliana kisha
akaongozana na afande Titus
wakaingia ndani ya
uwanja.Titus alikuwa na
kitabu na kuanza kumfuata
askari mmoja mmoja
akimuuliza namba yake
akaiandika katika
kitabu.Karibu na jukwaa
ambalo husimama marais kwa
ajili ya nyimbo za taifa
walisimama askari
wawili.Mathew na afande Titus
wakamfuata askari wa kwanza
wakamuhoji namba zake na
walipomfuata askari wa pili
akababaika
“Askari taja namba zako
tafadhali ! akasema afande
Titus lakini Yule askari
hakuweza kutamka
chochote.Mathew taratibu
akaupeleka mkono akaishika
bastora yake
“Askari taja namba yako
tafadhali ! akafoka afande
Titus na katika redio ya
mawasiliano akasikika mtu
aliyeko uwanja wa ndege
akiwajulisha askari wachukue
nafasi kwani msafara wa
marais umekwisha wasili pale
uwanjani.
“Askari !! akafoka afande
Titus
“Husikii ninachokuuliza?
Taja haraka sana namba yako
tafadhali ! akafoka afande
Titus.
Jicho la Mathew liliuona
mkono wa Yule askari
ulikokuwa unapelekwa
akaruka na kumsukuma
afande Titus akaanguka chini
kisha akaupiga teke mkono wa
Yule jamaa akaaguka chini.
“Titus kimbiaaa !! akapiga
kelele Mathew na Titus
akainuka akaanza
kukimbia.Yule jamaa aligeuka
na kukishika kidude
chekundu.Kabla hajakishusha
kidole gumba katika kile
kilipuzi Mathew akawahi
kumrukia na kumtandika
kichwa kizito usoni na Yule
jamaa akaachia kile
kilipuzi.Mathew akakikamata
kidole gumba
akakivunja,akamtandika
ngumi mbili mfululizo
usoni.Yule jamaa akaukunja
mguu wa kulia akampiga
Mathew kichwani kwa
kutumia goti na kumsukuma
Mathew pembeni.Akainuka na
kukishika kilipuzi kwa mkono
wake wa kushoto Mathew
akamkata mtama akaanguka
ksha akaushika mkono wa
kushoto akauvunja.Yule jamaa
akalia kwa
maumivu.Akaukamata pia
mkono wa kulia akauvunja
Yule gaidi akaendelea kupiga
kelele za maumivu.
Taharuki kubwa ilitanda
pale uwanja wa ndege wa
Julius Nyerere baada ya taarifa
kusambaa kwamba kulikuwa
na bomu.Watu waliokuwa
ndani ya uwanja kwa ajili ya
kuwaaga marais waliondolewa
haraka.Marais waliondolewa
haraka sana pale uwanja wa
ndege na kurejeshwa ikulu.
Baada ya kumdhibiti Yule
gaidi Mathew akamvua ile
fulana yenye bomu akaiweka
pembeni akasimama na kutoa
ishara kwamba askari
wasogee.Wataalamu wa
mabomu kutoka jeshi la polisi
wakaondoka na lile bomu.
Baada ya kuikamilisha kazi
yake Mathew akawaachia
maafisha wa usalama
waendelee na kazi yao kwa
ahadi ya kwenda kituoni kutoa
maelezo ya kina kuhusiana na
suala lile.Mathew akampigia
simu Ruby na kutaka
kufahamu mahala walipo kisha
akaomba kupelekwa hospitali
ya Mtodora alikopelekwa
Melanie.Gari la polisi
lilimpeleka hadi hospitali ya
Mtodora ambako aliwakuta
Ruby na Jackson.Ruby
alimkumbatia Mathew kwa
nguvu huku akibubujikwa na
machozi
“We did it Mathew ! We
did it ! akasema Ruby huku
akimwaga machozi
“We saved our president !
akasema Mathew halafu
akamfuata Jackson
“Jackson Ahsante
sana.Tusingeweza kufika hapa
bila msaada wako.Umeingia
katika historia ya nchi hii kwa
kufanya kitu cha kizalendo”
akasema Mathew
akakumbatiana na Jackson
“Madaktari wanasemaje
kuhusu Melanie?
“Wanaendelea
kumuhudumia.Bado hajapata
fahamu mpaka sasa” akasema
Ruby
“Tutarejea hapa hospitali
lakini kwa sasa wasiliana tena
na Rais tukaonane
naye.Anapaswa kufahamu kila
kilichotokea” akasema Mathew
na Ruby akampigia simu rais
na simu yake ikapokelewa
“Unasemaje Ruby?
“Mheshimiwa Rais pole
sana kwa kilichotokea leo”
“Ahsante”
“Mheshimiwa Rais
tunahitaji kukuona”
“Haitakuwa rahisi
kuonana nanyi kwa sasa
kutokana na itifaki za
kiusalama hasa pale
kunapotokea kitisho cha
usalama kama kilichotokea
leo”
“Mheshimwia rais ni
muhimu sana tukaonana
nawe.Kuna mengi ambayo
unapaswa kuyafahamu.Kwa
ufupi tu sisi ndio tuliofanikisha
kila kitu kilichotokea leo.Ni
mambo mazito ambayo
unapaswa kutusikiliza”
akasema Ruby ukapita ukimya
kidogo na Dr Fabian akakubali
kuonana nao.
Wote watatu wakaingia
katika lile gari alilokuwa
anaendesha Jackson ambalo
lilikuwa na mwili wa James
Kasai katika buti ya gari
wakaondoka kuelekea
ikulu.Njiani bado Ruby
aliendelea kutiririkwa na
machozi.
“Ruby nini kinakuliza?
“Nimetazama rekodi ile ya
Melanie imenisikitisha
sana.Kumbe ni binti mdogo tu
lakini amegeuka akawa mkatili
kiasi hiki.Nimejikuta
nikimuonea huruma” akasema
Ruby
“Hakuna kumuonea
huruma mtu ambaye
anashirikiakana na
magaidi.Alichokipata
anastahili na ana bahati
ameingia katika mikono yangu
akiwa hana fahamu nilikuwa
na hasira naye sana ! akasema
Mathew akaichukua kompyuta
ile ya Melanie na kuanza tena
kusikiliza ile rekodi .
“Afrika Mashariki iko
salama.Njama za mabeberu
zimeshindwa
kufanikiwa.Mungu anaendelea
kusimama na Tanzania”
akasema Mathew
“Kwangu mimi naona ni
muujiza kumuua James Kasai
ambaye ameleta hofu kubwa
Afrika mashariki” akasema
Ruby kwa hisia kali na
kumwaga tena machozi
 

mbududa

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2017
Messages
596
Points
1,000

mbududa

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2017
596 1,000
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 10 : EPISODE 21
Akina Mathew waliwasili
ikulu ambako walinzi wake
uliongezeka
maradufu.Walipokewa na
kupelekwa moja kwa moja
katika chumba cha mikutano
midogo cha Rais
“Ni mara yangu ya kwanza
kufika ikulu” akasema Jackson
“Utaendelea kufika hapa
mara kwa mara.Huu ni
mwanzo tu” akasema Mathew
Dakika chache baadae
mlango ukafunguliwa
wakaingia walinzi wa Rais
halafu akaingia Rais Dr Fabian
Kelelo.Mathew na wenzake
wakasimama na Rais
akawataka
waketi.Akawatazama kwa
muda halafu akasema
“Nimechelewa kufika hapa
kuzungumza nanyi nilikuwa
katika simu na mkuu wa jeshi
la polisi nchini akinijulisha
kuhusiana na matukio
yaliyotokea leo jijini Dar es
alaam.Nimeambiwa kwamba
helkopta ya idara ya SNSA
imelipuliwa leo katika bohari
la idara hiyo na kumefanyika
mauaji ya watu
huko.Nikaambiwa tena kuna
milipuko ya mabomu imetokea
katika nyumba moja kwenye
kijiji cha mabilionea na huko
watu kadhaa wameuawa na
kwa taarifa ambayo mkuu wa
jeshi la polisi nchini ameipata
ni kwamba mlikutwa eneo hilo
na mkajieleza kuwa mnatoka
SNSA na mkaeleza kuwa kuna
mtu ana bomu katika uwanja
wa ndege wa Julius Nyerere na
amelenga kutuua mimi na Rais
Patrice Eyenga.Amenieleza
kile kilichotokea uwanja wa
ndege namna ulivyoweza
kumdhibiti Yule gaidi.Nataka
mnieleze kwa kina kila kitu
kilichotokea” akasema Dr
Fabian na Mathew akamueleza
kila kitu namna
walivyoendesha operesheni
yao hadi
walivyoikamilisha.Mashavu ya
Dr Fabian yalionekana na
michirizi ya machozi wakati
Mathew akiendelea
kumsimulia.Akatoa kitambaa
akafuta machozi akashinda
kujizuia kulia kwa kwikwi
“Let him cry ! Mathew
akawaambia wenzake.Dr
Fabian alilia kwa takribani
dakika tatu halafu akafuta
machozi akavaa miwani yake
“Mtanisamehe
nimeshindwa kujizuia
kumwaga machozi” akasema
Dr Fabian
“Mathew Mulumbi wewe
ni halisi au ni mzimu kama
wengi wanavyohisi?akauliza
Dr Fabian
“Mimi ni halisi
mheshimiwa Rais” akajibu
Mathew
“Nashindwa niseme
nini.Nilikudharau sana
Mathew Mulumbi.Sikujua
kama leo hii wewe
niliyekudharau ndiye ambaye
umeniokoa.Kama si wewe basi
hivi sasa mimi na mwenzangu
Patrice tungekwisha fariki
dunia”
“Ni Mungu anayepaswa
kushukuriwa kwanza kwani
hakutaka kukuchukua siku ya
leo kwani kama ingekuwa ni
kwa mipango yake hata mimi
nisingeweza kukuokoa lakini
vile vile kuna watu wengine
nyuma yangu ambao kwa
pamoja tumeshirikiana katika
operesheni hii kwa niaba yao
ninasema ninapokea ahsante
sana” akasema Mathew na Dr
Fabian akavua tena miwani
akafuta machozi
“Mtanisamehe vijana
wangu kwa hali hii nashindwa
kujizuia”
“Mheshimiwa rais nadhani
ungeitazama rekodi ile ya
Melanie” akasema Mathew na
kumsogezea Dr Fabian
kompyuta ya Melanie
akamchezea ile rekodi ya
Melanie
“Nafahamika kama
Melanie Davis au Melanie
Chuma lakini hilo si jina langu
halisi.Jina langu halisi ni
Theresia Muganza mtoto wa
Laurent na Lucy Muganza
kutoka jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo ambao
waliuawa nchini
Tanzania.Nilikuwa ninasoma
hapa Tanzania na niliipenda
sana nchi hii lakini mambo
yalibadilika pale walipouawa
wazazi wangu, mauaji ya
kikatili sana ambayo chanzo
chake ni sababu za
kisiasa.Mama yangu alikuwa
bilionea na hakuwahi kufikiri
hata mara moja kuingia katika
siasa hadi pale
aliposhawishiwa na serikali ya
Ufaransa agombee urais kwa
manufaa yao.Rais Patrice
Eyenga alipoingia madarakani
alikata mirija yote ya
mabeberu waliokuwa
wakinyonya rasilimali za
Congo na hilo
halikuwapendeza mabeberu
hivyo wakaanza kutafuta
namna watakavyoweza kurudi
tena kufaidika na rasilimali za
nchi ya Congo wakamshawishi
mama yangu awanie
urais.Waliamini atashinda
uchaguzi hivyo wakampa kazi
nyingine ya kuhakikisha
anaisambaratisha jumuiya ya
afrika mashariki .Kwa bahati
mbaya aligundulika mapema
akauawa na mimi
nikanusurika
Nilipelekwa Ufaransa kwa
matibabu na Mungu akanijalia
nikapona ndipo nilipoelezwa
ukweli wa kile kilichotokea
kuhusu mauaji ya mama
yangu.Nilipandikizwa hasira
ambazo zilizaa chuki kubwa
dhidi ya nchi za Tanzania
Congo na Afrika mashariki
kwa ujumla nikaulizwa kama
niko tayari kuvaa viatu vya
mama yangu nikakubali
nikafanyiwa upasuaji bandia
kubadili mwonekano wangu
halafu nikatumwa kuja
Tanzania kwa lengo la kulipiza
kisasi lakini kubwa likiwa ni
kuivuruga jumuiya ya afrika
Mashariki.Nilibadilishwa jina
nikapewa jina la Melanie
Davis.Hapa Tanzania
nilikutana na mtu anaiwa
Edwin Mbeko ambaye ni
mkurugenzi wa idara ya siri ya
usalama wa ndani wa nchi
SNSA ambaye huyu aliwekwa
maalum kwa ajili ya
kuhakikisha mipango yangu
yote inafanikiwa.Nilipewa jina
lingine la Melanie Chuma ili
wakati mwingne nijulikane
kama mtanzania.Nilinunua
makampuni hapa Tanzania na
fedha nilipewa na serikali ya
Ufaransa ambao ndio
wananifadhili.Niliingia hapa
nchini kama mwekezaji na
mpango wangu wa kwanza
ulikuwa ni kuwaua wake za
marais wa Tanzania na
Congo.Nilikutana na balozi wa
Congo hapa nchini
nikamshawishi aandae chakula
maalum na kuwakaribisha
wake za marais wa Congo na
Rwanda na lakini kukawa na
ugumu wa kumpata mke wa
Rais wa Rwanda na ndipo
alipomtumia mke wa Rais wa
Tanzania ili kumleta mezani
mke wa rais wa
Rwanda.Niliandaa mpango ule
nikishirikiana na James Kasai
ambaye nilikwenda kuonana
naye Uganda. Baada ya
shambulio lile lililowaua wake
za marais nikaelekezwa tena
kuandaa shambulio lingine
ambalo linalenga kumuua Rais
Patrice Eyenga.Nilimfuata
James Kasai nikaongea naye
suala hili naye akanipeleka
kwa Rais wa Uganda Jenerali
Akiki ambaye alikubali
kushirikiana nasi katika
mpango huo na alitaka baada
ya Patrice kuuawa James Kasai
achukue nchi.Akiki alinieleza
kwamba Majenerali wa jeshi la
Congo walikuwa wanandaa
mpango wa mapinduzi hivyo
akamuita mkuu wa majeshi wa
Congo akazungumza naye
lakini wakashindwa kuelewana
kuhusu James Kasai
kushirikishwa katika serikali
baada ya mapinduzi ndipo
tulipoamua kuendelea na
mpango wa kumuua James
Kasai bila kushirikiana na
wakuu wa jeshi la
Congo.Tulipanga Jenerali
Akiki aombe kukutana jijini
Dar es salaam na marais wa
Tanzania na Congo azungumze
nao kuhusu kutafuta muafaka
wa amani kufuatia
mashambulizi yale
yaliyofanywa na James Kasai
jijini Dar es salaam.James
aliwasiliana na IS wakamtuma
mtu anaitwa Khalid Khalid
ambaye ni mtaalamu wa
mabomu kuja kuandaa bomu
ambalo litaweza kuwaua
marais wa Tanzania na
Congo.Edwin Mbeko kwa
kutumia idara ya SNSA aliweza
kufanikiwa kuingia nchini kwa
James Kasai pamoja na Khalid
Khalid.Rais Akiki alimpigia
simu Rais wa Tanzania
akamtaka aandae mkutano
naye akakubali bila kujua ni
mtego.Kwa kumtumia Edwin
Mbeko pia tuliweza
kumuingiza nchini mtu
ambaye angejitoa mhanga na
kuwaua marais.
Leo hii kumefanyika kikao
hicho cha marais watatu na
ninaamini muda si mrefu
kutoka sasa AfrikaMashariki
itaingia katika msiba mkubwa
wa kuondokewa na marais
wawili kwa wakati
mmoja.Shambulio la bomu
litakalotokea muda mfupi ujao
na kuwaua marais wa
Tanzania na Congo
tumeliandaa sisi.
Nimeamua kueleza ukweli
huu kwani nyumba yangu kwa
sasa imezingirwa na watu
ambao naamini ni wapelelezi
hivyo sintatoka hai ndani ya
chumba hiki.Baada ya
kumaliza hii rekodi
nitajimaliza mwenyewe kwa
risasi,siko tayari
kukamatwa.Katika dakika hizi
ambazo nyumba yangu
imezingirwa na wapelelezi
ninakiona kifo changu na
ninaumia sana kwa mateso na
maumivu niliyowasababishia
watu ambao niliwaua ndugu
zao, nimejikuta nikijutia kile
nilichokifanya.Mimi ni
msichana mdogo bado lakini
nimeingia katika historia ya
watu makatili wakubwa si kwa
kupenda bali ni kwa sababu ya
maslahi ya
mabeberu.Ninajilaumu kwa
kukubali kutumika.Nilikubali
kuwa kibaraka wao na kuua
waafrika
wenzangu.Nimeyasema haya
ili waafrika wenzangu
wajifunze kwani si mimi peke
yangu ninayetumiwa na
mataifa makubwa ya nje.Wapo
watu wengi katika taasisi za
serikali na hasa viongozi wa
siasa.Hawa wamekuwa
wakitumiwa sana na serikali za
mabeberu katika kuleta
migongano ndani ya nchi
zao.Machafuko mengi
yanatokea katika nchi zetu za
afrika chanzo chake ni
wanasiasa ambao
ukiwachunguza wanatumiwa
na mabeberu kutuvuruga ili
mabeberu hao waweze kupata
mwanya wa kuingia katika
nchi zetu na kuchota
rasilimali.Wanafanya haya
kwa malipo ya fedha ambazo
zinawawezesha kuishi maisha
ya kifahari kama niliyoishi
mimi na kusahau kwamba nchi
zetu zinaendelea kuwa
masikini na kunyonywa kila
uchao.Niliingia katika mtego
wao nikanasa na katika dakika
zangu za mwisho nimegundua
kosa nililolifanya.Kama
nisingekubali kutumiwa na
mabeberu ningekuwa na
maisha marefu na ndoto zangu
nyingi zingetimia lakini
nimekatisha ndoto zangu
katika umri huu mdogo.Huu ni
mfano kwa wale wote wenye
kufanya mambo kama
niliyoyafanya mimi kuwa
mwisho wenu ni mbaya na
yawezekana mwisho wenu
ukawa mbaya kuliko wa
kwangu.Usaliti kwa nchi yako
ni dhambi
kubwa.Ninat………………”
Rekodi haikuendelea tena
kukasikika kishindo na
kukawa giza.Ni pale ambapo
Khalid alijilipua na kipande
cha mlango kikampiga Melanie
kichwani
“Nimekosa maneno ya
kusema ! akasema Dr Fabian
“Nani mwingine ambaye
ameiona rekodi hii? Akauliza
Dr Fabian
“Hakuna mwingine zaidi
yetu sisi” akajibu Mathew
“Good.Rekodi hii inapaswa
kufanyiwa kazi haraka sana na
vyombo husika……….”akasema
Dr Fabian na Mathew
akamkatisha
“Mheshimiwa rais sisi
tumekamilisha jukumu letu la
kuilinda nchi na hatua
zinazofuata tunaiachia
serikali.Kwa mfano kuna
mtandao wa IS hapa nchini
ambao unapaswa kufumuliwa
nk.Kama hutajali mheshimiwa
Rais ninaomba tukakukabidhi
mwili wa James Kasai ili
uthibitishe kwamba kweli
ameuawa”akasema Mathew
kisha Dr Fabian akaelekeza
Rais Patrice Eyenga aitwe ili
kwa pamoja wakashuhudie
mwili wa James Kasai.
Akina Mathew
wakiongozana na marais wale
wawili wakaelekea katika gari
la Mathew buti likafunguliwa
na mwili wa James Kasai
ukaonekana.Dr Fabian na
Patrice wakathibitisha kuwa ni
yeye,akaelekeza liitwe gari la
kubebea wagonjwa ili mwili
ule ukahifadhiwe
hospitali.Wakarejea ndani
katika chumba cha mikutano
midogo
“Vijana wangu sijui
nizungumze nini kwa hiki
mlichokifanya.Ni kitu kikubwa
sana ambacho vizazi na vizazi
vinapaswa kuusoma ujasiri
wenu.Hiki mlichokifanya
kinapaswa kuingia katika
historia ya nchi ili
mkumbukwe na watoto wa
watoto wenu kwamba
waliwahi kutokea vijana Fulani
ambao walionyesa uzalendo
wa ajabu kwa nchi hii.Mathew
umepambana na gaidi
aliyekuwa na bomu.Ni vipi
kama gaidi Yule angeweza
kulipua bomu lile wakati
ukimdhibiti?Hukulijali hilo
lakini ulichokuwa unahitaji ni
kuokoa maisha yangu.Sina
neno la kusema.Sijui ni tuzo
gani upewe itakayolingana na
hiki
ulichokifanya.Nitalihutubia
taifa usiku wa leo na
ningependa watanzania
wafahamu kitu kikubwa
mlichokifanya leo” akasema Dr
Fabiana na kuwatazama akina
Mathew
“Mheshimiwa Rais
tulichokifanya ndicho
tulichoapa kukifanya.Tuliapa
kuilinda nchi dhidi ya adui wa
ndani na wa nje na leo
tumetimiza wajibu wetu.Kwa
niaba ya wenzangu tunaomba
jambo hili libaki kama lilivyo
na tusitambulishwe kwamba
sisi ndio tuliomuua James
Kasai na kuzima shambulio la
kigaidi.Wewe ukitushukuru
basi tunaamini watanzania
wote wametushukuru hivyo
basi hatutapenda kutangazwa”
akasema Mathew
Kikao kiliendelea hadi
ilipotimu saa kumi na mbili za
jioni ndipo Rais Patrice
Eyenga akaondoka nchini
kurejea nchini kwake jamhuri
ya kidemokrasia ya
Congo.Mwili wa James Kasai
ukachukuliwa na kupelekwa
hospitali kuu ya Mtodora
kuhifadhiwa
Mathew na wenzake
wakaagana na Rais
wakaondoka wakaelekea
hospitali ya Mtodora kujua
maendeleo ya
Melanie.Walijulishwa na
madaktari kwamba ubongo wa
Melanie umekufa hivyo
hataweza kuamka tena.
Kutoka hospitali ya
Mtodora wakaelekea katika
nyumba walikolazwa Austin na
Gosu Gosu.Hali ya Gosu Gosu
iliendelea vizuri na aliweza
kufumbua macho lakini wakati
walipofika akina Mathew
alikuwa amelala na
hawakutaka
kumuamsha.Walimsimulia
Austin kilichotokea
“Nasikitika nimekosa
mengi” akasema Austin na
wote wakacheka
“Usijali Austin hata uwepo
wako hapa hospitalini ni
jambo kubwa sana kwani
umeokoa maisha ya
GosuGosu” akasema Mathew
kisha wakamuaga Austin na
kurejea nyumbani kwao.Ruby
akayaganga majeraha yote
aliyoyapata Mathew kisha
wakapata chakula halafu
wakaelekea sebuleni kutazama
hotuba ya Rais
“Ndugu watanzania
wenzangu,napenda kuanza
kwa kumshukuru Mwenyezi
Mungu mwingi wa rehema
kwa kutujalia uhai na
kuendelea kusimama na nchi
yetu
Ndugu watanzania
wenzangu siku,chache
zilizopita nilisimama hapa
nikiwapa taarifa za tukio baya
kabisa kutokea hapa nchini
ambapo watu wasio na
ubinadamu wenye roho za
kishetani walivamia nchi yetu
na kutekeleza shambulio baya
kabisa ambalo lilikatisha
kikatili maisha ya wapendwa
wetu. Niliposimama hapa
niliwaahidi kwamba mimi na
serikali yangu hatutakaa kimya
kwa yeyote aliyeshiriki katika
shambulio lile baya.Niliahidi
kwamba tutawasaka kokote
duniani wale wote waliomwaga
damu ya watanzania.
Shambulio lile baya kabisa
lilifanywa kwa ushirikiano wa
James Kasai kiongozi wa kundi
la waasi ambaye anashirikiana
na kundi la kigaidi la IS.James
Kasai alifurushwa nchini
Jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo baada ya kugoma
kushiriki katika mpango wa
amani na akakimbilia nchini
Uganda ambako amekuwa
akiishi na kukijenga kikundi
chake akifadhiliwa na serikali
ya Uganda. Wakati dunia
nzima ikiamini James Kasai
anaishi msituni nchini Uganda
lakini James Kasai amekuwa
akiishi katika jiji la Kampala
maisha ya kifahari sana na hili
hata wananchi wengi wa
Uganda hawalifahamu.
Kwa kushirikiana na nchi
za Rwanda na Congo tuliahidi
kumsaka James Kasai kokote
aliko duniani na kuhakikisha
tunamtia nguvuni.Wakati
mipango na mikakati yetu
ikiendelea , James Kasai kwa
kushirikiana na mtandao wake
aliweza kuingia hapa
nchini.Vijana wetu wazalendo
kwa nchi yao waliokula kiapo
cha kuifia nchi yao walizipata
taarifa hizo za James Kasai
kuja Tanzania wakamfuatilia.
Ndugu watanzania
wenzangu ninasimama hapa
kuwajulisha kwamba James
Kasai Yule muuaji aliyemwaga
damu ya watanzania bila hatia
ameuawa leo mchana na vijana
wetu wazalendo.Si yeye peke
yake bali pia washirika wake
wa karibu pia wameuawa na
wengine hivi sasa
wanatafutwa.
Ndugu watanzania vijana
hawa wazalendo ambao
wamefanikisha,kumuua katili
huyu na genge lake wameokoa
jumuiya ya Afrika mashariki
kusambaratika.Ndugu zangu
jambo hili ni pana zaidi ya
tunavyolifikiri.Ipo nguvu
kubwa kutoka mataifa
makubwa ambayo inataka
kutusambaratisha na kuvuruga
umoja wetu lakini Mungu
ameendelea kusimama na nchi
yetu pamoja na jumuiya ya
Afrika mashariki.Tumekwisha
zifahamu nchi
hizo,tumekwisha wafahamu
viongozi wa nchi hizo ambao
wanapanga mipango ya
kutuvuruga na tutaendelea
kuchukua hatua mbali mbali
lakini naomba mfahamu
kwamba tuko katika vita
mbaya ya kiuchumi na katika
vita hii tunapambana na
mataifa makubwa yenye nguvu
kutushinda sisi.Wanawatumia
watu wetu wenyewe kutugawa
na kutuvuruga .Wapo viongozi
ndani ya serikali,wapo
wanasiasa wapo viongozi wa
dini ambao wanatumiwa na
mataifa makubwa ya nje katika
vita hii.Ninawaomba ndugu
zangu watanzania tuipende
nchi yetu.Kuisaliti nchi yako
kwa fedha kidogo kutoka kwa
mabeberu ni dhambi kubwa na
mwisho wake ni mbaya.
“Mathew my love kuna
jambo nataka kuuliza”
akasema Ruby wakati
wakiendelea kutazama hotuba
ya Rais
“Uliza mpenzi” akasema
Mathew
“Hatimaye misheni
imekwisha,James Kasai
ameuawa,washirika wake pia
wameuawa na wengine wa
mtandao wa IS wanaendelea
kutafutwa na vyombo vya
usalama.Baada ya kazi hii
ngumu nini kinafuata?
Akauliza Ruby
“Kama nilivyokueleza
awali kwamba nitaondoka
baada ya kukamilisha misheni
hii lakini nitarejea tena kwa
ajili yako.Narudia tena
kukukumbusha kwamba
nitakapoondoka usijaribu
kunitafuta kuwa mvumilivu
nitarudi” akasema Mathew
BAADA YA SIKU 3
Afya ya Gosu Gosu
iliimarika sana na sasa aliweza
hata kuinuka na kukaa
mwenyewe kitandani.Ni siku
ya tatu toka alipouawa James
Kasai.
Saa nne za asubuhi gari la
wagonjwa liliwasili katika
hospitali kuu ya Mtodora
kitanda cha wagonjwa
kikashushwa garini na
kusukumwa kuelekea katika
wodi alikolazwa Melanie
Davis.Pembeni yake
walikuwepo Mathew na Ruby
Melanie aliwekewa
mashine ya kumsaidia
kupumua.Gosu Gosu
alipomuona sura yake
ikabadilika.Mathew
akawaomba watu wote watoke
mle ndani akabaki Gosu Gosu
akimtazama Melanie
“Sikujua kumbe u shetani
uliyevaa mwili wa binadamu
Melanie.Nilikupenda kwa
moyo wangu wote nikiamini
wewe ni mwanamke ambaye
umeumbwa kwa ajili
yangu.Nilikuwa tayari kufanya
kila ulichokitaka na kwa
sababu yako nilichungulia
kaburi.Ninashukuru
nimekuona ukiwa katika hali
hii kwani ungekuwa mzima
ningekuua kifo kibaya sana”
akasema Gosu Gosu kwa sauti
ya chini halafu Mathew
akaingia
“Gosu Gosu muda
umefika.Kamilisha zoezi
ukapumzike” akasema
Mathew na Gosu Gosu
akasogezwa kitufe ili azime
mashine ile ya kumsaidia
Melanie kupumua.
“Kwa heri Melanie”
akawaza Gosu Gosu na
kubonyeza kitufe kile akazima
mashine ya kupumua na
ukawa mwisho wa Melanie
Davis.
 

mbududa

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2017
Messages
596
Points
1,000

mbududa

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2017
596 1,000
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 10 : EPISODE 22
Ni Ruby pekee
aliyefahamu kuhusu kuondoka
kwa Mathew Mulumbi kwani
ndiye aliyemsindikiza uwanja
wa ndege akapanda ndege
kuelekea Cairo Misri.
“Nimemaliza misheni ya
kwanza.James Kasai ameuawa
na Afrika mashariki iko
salama.Njama za mabeberu
zimeshindwa.Ninamshukuru
sana Habiba Jawad ambaye
ameniwezesha kwa kiasi
kikubwa kufanikisha misheni
hii muhimu sana kwa nchi
yangu.Ninakwenda tena katika
misheni nyingine ambayo kwa
mujibu wa Habiba Jawad ni
kubwa kuliko hii
niliyoimaliza.Mungu
ataendelea kusimama nami”
akawaza Mathew akiwa
ndegeni
MWISHO WA SIMULIZI YA
MAISHA NA KIFO CHA
MELANIE CHUMA.USIKOSE
SEHEMU YA TATU NA YA
MWISHO YA SIMULIZI YA
SIRI IITWAYO
JASUSI/GAIDI.
 

Forum statistics

Threads 1,343,332
Members 515,022
Posts 32,780,950
Top