ukute kupondea kote huku kazi za wenzako hata Essay ya page mbili huwezi kuandikaHii sio story ya movie ina makosa mengi sana ya kiufundi,hii kwaajili ya kufurahisha ubongo,na ata kitabu hawezi chapisha kwa hii story, amemfanyia overestimated character wake mkuu mpka amewakalisha chini Marais na ata wakuu wa mashirika kama mossad,# doest work that way
Ndugu yangu we,kila mtu kwenye mtandao siku hizi mjuaji...ukute kupondea kote huku kazi za wenzako hata Essay ya page mbili huwezi kuandika
Weka yako isiyo na makosa,hii ni riwaya tu,hata movie ni uongo mtupu,ukitaka movie ya ukweli angalia za porn (x),halafu sidhani kama umelazimishwa kuifuatilia,kama unaona siyo pita kushoto,achana nayo, tuwekee mambo tuburudike kiongozi!Hii sio story ya movie ina makosa mengi sana ya kiufundi,hii kwaajili ya kufurahisha ubongo,na ata kitabu hawezi chapisha kwa hii story, amemfanyia overestimated character wake mkuu mpka amewakalisha chini Marais na ata wakuu wa mashirika kama mossad,# doest work that way
Kuna watu wanajidai wajuaji kumbe ni empty tu.ukute kupondea kote huku kazi za wenzako hata Essay ya page mbili huwezi kuandika
Ndugu yangu we,kila mtu kwenye mtandao siku hizi mjuaji...
Booonge la storySIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 6: EPISODE 5
Melanie Davis akiwa katika
chumba chake akifuatilia habari
za kuhusiana na tukio lile huku
mezani akiwa na chupa ya
shampeni simu yake ikaita
alikuwa ni Edwin Mbeko
“Hello Edwin” akasema
Melanie
“Madam wale watu tayari
wamekwisha ondoka na ndege
inayoelekea Nairobi Kenya”
“Ahsante sana Edwin.Kazi
nzuri.Endelea kufuatilia kwa
karibu sana taarifa zote za
usalama na unijulishe kama
kutakuwa na tatizo lolote kwa
upande wetu” akasema Melanie
na kukata simu
“Damu ya wazazi wangu
haitamwagika bure.Lazima
itaondoka na watu wengi na
kama nilivyoahidi huu ni
mwanzo tu” akawaza na
kuchukua glasi ya shampeni
akanywa
“Sikutegemea kama siku
moja ninaweza nikawa mkatili
namna hii lakini ni wao
wenyewe ndio walionifanya
mimi niwe mkatili kiasi hiki
kwa kuwaondoa wazazi wangu
kikatili.Walifanya makosa
makubwa sana kushindwa
kuniua na sasa nitawawinda
usiku na mchana na wote
walioshiriki suala hili watalipa
uovu wao” akawaza Melanie na
simu yake ikaita alikuwa ni
Devotha.
“Hallo Devotha” akasema
Melanie
“Melanie nini
umekifanya?akauliza Devotha
kwa ukali
“Devotha kwa nini badala
ya kunipongeza unaanza
kunifokea?Melanie akahamaki
“Ninakufokea kwa kitendo
ulichokifanya ! akaendelea
kufoka Devotha
“Kwa kitendo
nilichokifanya ! Melanie
akashagaa
“Nilichokifanya si ndicho
nilitumwa kukifanya? Sasa
nimekosea wapi?akauliza
Melanie
“Umekosea sana
Melanie.Kwa nini
umewashirikisha IS? Kwa nini
umeshirikiana na magaidi?
Akauliza Devotha kwa ukali
“Devotha mlinituma Afrika
Mashariki kwa ajili ya misheni
maalum hivyo basi ni jukumu
langu kuhakikisha misheni
inafanikiwa bila kujali
ninashirikiana na
nani.Ninaomba msianze
kunivuruga niacheni nitekeleze
kazi mliyonituma niitekeleze”
akasema Melanie kwa ukali
“Melanie hujui kwamba
kwa kushirikiana na magaidi wa
IS unalifanya suala hili kuwa
kubwa zaidi tofauti na
tulivyokuwa tumelipanga?
“Nimekwisha kueleza
Devotha na ninarudia tena
kukueleza kwamba hii ni
misheni yangu na ninaitekeleza
vile nitakavyo.Naomba kama
huna lingine la kunieleza
tafadhali kata simu ! akasema
Melanie kwa ukali
“Nisikilize Melanie.Kuanzia
sasa hakuna tena mashirikiano
baina yako na hao magaidi wala
kikundi kingine
chochote.Unafanya kitu cha
hatari sana Melanie.Mpango
huu ni wa siri kubwa lakini kwa
hiki ulichokifanya cha
kuwashirikisha waasi na
magaidi kitaufanya mpango
wetu huu
kufahamika.Ninakuelekeza
kuanzia sasa vunja kabisa
mahusiano yoyote uliyo nayo na
hao watu.Umenielewa
Melanie?! Akauliza Devotha
“Devotha kwa mara ya
mwisho ninarudia kukusisitiza
kwamba mmenituma kufanya
kazi na nitaifanya kwa jinsi
nitakavyo mimi.Naomba iwe ni
mara ya mwisho kunifokea bila
kujua ni magumu gani nimepitia
hadi kufanikisha tukio lile
kubwa ! akasema Melanie na
kukata simu
“Huyu Devotha kwa nini
ananilazimisha nimuondoe
kabla ya wakati wake?Yeye pia
yumo katika orodha ya watu
ambao lazima damu yao
imwagike kwani ni yeye
aliyemfuata mama yangu na
kumshawishi ajiunge katika
siasa.Kwa kuwa anaonekana
kutaka kunipanda kichwani
dawa yake ni ndogo tu.Lazima
nimuondoe na kazi hii ataifanya
Gosu Gosu.Nitamtuma kwenda
Ufaransa kumuua Devotha”
akawaza Melanie na kuinua
glasi yake ya shampeni
akanywa.
NDUGU MSOMAJI TUKUTANE
SEHEMU IJAYO……………..