Riwaya: Siri

Riwaya: Siri

SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 5: EPISODE 4
Saa kumi na mbili za
asubuhi Melanie alipigiwa
simu na Edwin Mbeko
akamjulisha kwamba
amemtumia taarifa za balozi
wa jamhuri ya kidemokrasia
ya Congo hapa nchini katika
barua pepe yake.Melanie
akaamka na kuelekea katika
chumba cha mazoezi ambako
alimkuta Joyce naye
amekwisha amka akifanya
mazoezi.Waliungana pamoja
katika mazoezi kisha kila
mmoja akaelekea chumbani
kwake kujiandaa kwa ajili ya
kuianza siku.Hawakuwa na
mtumishi bado hivyo Joyce
akaandaa kifungua
kinywa.Wakati Joyce
akiandaa kifungua kinywa
Melanie alikuwa chumbani
kwake akijiandaa,siku hii
alivaa suti ya rangi nyeupe
ambayo sketi yake iliishia
juu kidogo ya magoti na
kuwa na mpasuo mdogo kwa
nyuma.Alijiangalia kwenye
kioo akatabasamu
“Walionitengeneza
namna hii wanastahili
pongezi kubwa.Kwa
muonekano huu hakuna
mwanaume anayeweza
kuponyoka kama
nikimuhitaji” akawaza na
kuchukua moja ya simu kati
ya simu tatu zilizokuwa
mezani ambazo alipewa na
Edwin kwa ajili ya
mawasiliano.Akaziandika
namba za simu alizopewa na
Gosu Gosu akampigia
“Hallow” akasema Gosu
Gosu baada ya kupokea simu
akiwa hafahamu namba zile
ni za nani
“Halo mpenzi
wangu.Habari za
asubuhi?akauliza Melanie
“Melanie.Habari yao
malaika wangu.Umeamka
salama?
“Nimeamka salama
mpenzi sijui wewe”
“Hata mimi nimeamka
salama kabisa.Mawazo yote
juu yako” akasema Gosu
Gosu na Melanie
akatabasamu
“Darling hiyo ndiyo
namba yangu nitakayoitumia
hapa Tanzania muda wowote
ukitaka kunitafuta
utanitafuta katika namba
hiyo.Kwa shughuli zote za
kiofisi itatumika namba
hiyo” akasema Melanie
“Ahsante sana
Melanie.Vipi kuhusu ratiba
yako ya siku ya leo?
“Nitakuwa na mizunguko
kadhaa leo lakini kabla ya
mizunguko yangu nataka
kwanza nijitambulishe kwa
wafanyakazi ili wanifahamu
na mimi niwafahamu na kazi
hiyo ya kunitambulisha
utaifanya wewe.Nataka
niifahamu ofisi yako halafu
ndipo nitaendelea na
shughuli nyingine.Nielekeze
tukutane wapi?akauliza
Melanie
“Nielekeze mahala ulipo
nije nikuchukue” akasema
Gosu Gosu
“Usijali Gosu Gosu
ninaye dereva ambaye
anaweza akanileta mahala
ulipo”
“Ouh safi sana.Basi
mwambie akulete ofisi kuu
za MAPEN GROUP CO
LTD.Mimi nitakuwepo pale
nikikusubiri” akasema Gosu
Gosu
“Ahsante sana Gosu Gosu
tutaonana muda si
mrefu.Nakupenda sana”
akasema Melanie
“Nakupenda pia Melanie”
akasema Gosu Gosu na
Melanie akakata simu
Melanie akatoka
chumbani kwake na
kuelekea chini ambako
alimkuta Joyce akiwa tayari
amejiandaa lakini hakuwa
peke yake alikuwa na
mwanamke mmoja mfupi
mwenye weusi wa kung’aa.
“Hello ladies” akasema
Melanie na Yule mwanamke
aliyekuwa anazungumza na
Joyce akastuka baada
kumuona Melanie
“Madam Melanie huyu
anaitwa Frimina Mbozi ndiye
atakayekuwa katibu wako
muhtasi” akasema Joyce
“Hallow Frimina”
akasema Melanie na kumpa
mkono Frimina
“Hallow madam
Melanie.Naamini tayari
taarifa zangu unazo”
“Hutajali nikikuita Mina
badala ya Frimina? Akauliza
Melanie
“Hakuna tatizo Madam
Melanie”
“Good.Mina taarifa zako
tayari ninazo karibu sana”
akasema Melanie na wote
wakaenda kupata kifungua
kinywa na baada ya
kumaliza safari
ikaanza.Kituo cha kwanza
ilikuwa ni katika ofisi kuu za
MAPEN Group .Gosu Gosu
ambaye alikwisha wasili toka
mapema ndiye aliyempokea
Melanie.Siku hii alikuwa
amevalia suti nzuri nyeusi
na kila mmoja alimsifia kwa
muonekano ule.Wengi
hawakuzoea kumuona aiwa
amependeza namna
ile.Baada ya kupokelewa
Melanie akatembezwa katika
ofisi mbali mbali za jengo lile
la ghorofa tatu halafu
akaingizwa katika ofisi yake
kubwa ambayo ilikuwa ni
ofisi ya Mathew Mulumbi
kisha ikatumiwa na Gosu
Gosu na sasa ni Melanie
Davis.
“Ofisi nzuri sana hii
nimeipenda” akasema
Melanie halafu akaenda
kukutana na wafanyakazi
ambao walitaarifiwa kuacha
kila kitu na kukusanyika
katika ukumbi mkubwa wa
mikutano.Walifahamu kuna
ugeni lakini hawakujua
mgeni Yule ni
nani.Aliyefahamu ni Gosu
Gosu pekee
Gosu Gosu akiwa
ameongozana na Melanie na
katiku wake Frimina
waliingia katika ukumbi wa
mikutano.Gosu Gosu
akawasalimu wafanyakazi
wale halafu akatumia nafasi
ile kuwatangazia rasmi
kwamba kuanzia wakati ule
Melanie Davis ndiye mmiliki
mpya wa kampuni ya
MAPEN.Wafanyakazi wote
walipatwa na mshangao
mkubwa Gosu Gosu
akawaeleza sababu za
mmiliki wa kampuni ile
kuamua kuuza biashara zake
kwa mtu mwingine.Melanie
akakaribishwa kuzungumza
na wafanyakazi
akazungumza nao kwa muda
mfupi na kuwahakikishia
hakutakuwa na mabadiliko
yoyote,kila kitu kitaendelea
kuwa kama kilivyokuwa
awali na kuwaomba
wafanyakazi ushirikiano
mkubwa.Baada ya mkutano
ule na wafanyakazi Melanie
akarejea ofisini kwake na
rasmi Gosu Gosu
akamkabidhi ofisi
“Gosu Gosu huna haja ya
kunikabidhi ofisi.Hii
itaendelea kuwa ni ofisi
yako.Mimi nitatafuta ofisi
nyingine.Wewe bado ni
meneja mkuu wa
makampuni haya yote.Kama
alivyokuamini Peniela na
mimi pia ninakuamini vile
vile.Kila kitu kitakuwa chini
yako”akasema Melanie na
kumfuata Gosu Gosu
akambusu
“Japo bado nasubiri jibu
lako kuhusu kufunga ndoa
lakini wewe tayari ni mume
wangu Gosu Gosu.Wewe ni
mfalme wangu na kila kilicho
changu ni cha
kwako”akasema Melanie na
kumbusu
“Ahsante sana Melanie
kwa
kuniamini.Nitahakikisha
hujutii kuniamini” akasema
Gosu Gosu huku Melanie
akichezea tai yake
“Gosu Gosu kulala usiku
mmoja bila uwepo wako
pembeni yangu naona kama
ni miezi mitatu.Jioni ya leo
nitakuja nyumbani kwako
japo sintalala”akasema
Melanie na kumbusu tena
halafu akamuaga kwamba
anakwenda katika
mizunguko yake mingine
wataonana jioni kisha
Melanie akaondoka katika
ofisi kuu za MAPEN GROUP
huku akiacha gumzo watu
wakijadili uzuri wake.
Kutoka ofisi za MAPEN
group Melanie alielekea
katika ubalozi wa jamhuri ya
kidemokrasia ya
Congo.Alipokewa vizuri
akajitambulisha kama yeye
ana asili ya Congo lakini
ametokea Ufaransa na
anahitaji kuonana na balozi
wa DRC nchini
Tanzania.Balozi hakuwa na
mtu yoyote ofisini hivyo
Melanie akakaribishwa
ndani.
“Mheshimiwa balozi”
akasema Melanie akitumia
lugha ya kifaransa huku
akitabasamu na kumpa
mkono balozi
“Hallow habari
yako.Karibu sana”akasema
balozi na kumuelekeza
Melanie katika sofa nzuri
zilizokuwamo mle ofisini.
“Naitwa Melanie Davis
nina asili ya Congo lakni
ninaishi Ufaransa” akasema
Melanie
“Nafurahi kukufahamu
Melanie.Mimi naitwa
Germinus Mapupu balozi wa
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo hapa Tanzania.Karibu
sana katika ubalozi wetu
hapa Dar es salaam”
“Nashukuru sana
mheshimiwa balozi” akasema
Melanie na kukaa vizuri
kwani sketi yake fupi
aliyovaa ilikuwa imepanda
sana juu na kuyaacha
sehemu kubwa ya mapaja
yake wazi
“Niite Mr Mapupu
inatosha” akasema balozi
huku akitabasamu
“Kaona paja tu tayari
amekwisha anza
kujichekesha
chekesha”akawaza Melanie
“Mhehimiwa balozi Mr
Mapupu,kama
nilivyokujulisha mimi nina
asili ya Congo,wazazi wangu
wote wawili ni wazaliwa wa
Congo lakini walihamia
Ufaransa kibiashara.Kwa
sasa wote wawili
wametangulia mbele za haki
na mimi ndiye niliyebaki
nikisimamia mali
walizoziacha.Ninataka
kupanua biashara
walizoacha wazazi wangu
nataka kuogeza uwekezaji
zaidi hasa katika ukanda
huu wa Afrika
Mashariki.Tayari nimenunua
makampuni kadhaa hapa
Tanzania na sasa nataka
nikawekeze pia nyumbani
Congo”akasema Melanie
“Hongera sana Melanie
kwa uamuzi huo mkubwa wa
kuamua kuja kuwekeza
nyumbani.Wapo watu wengi
wa kutoka bara la Afrika
wamepata fedha nyingi huko
ughaibuni na hawakumbuki
tena kurejea kuwekeza
nyumbani na kuwapatia
ajira ndugu zao.Wewe
umefanya maamuzi mazuri
sana.Tunahitaji sana
uwekezaji kutoka nje na kwa
hivi sasa nchi ya Congo
imeweka sera nzuri sana za
kuvuta wawekezaji na wewe
ukiwa kama ni mkongo basi
utapewa kipaumbele
kikubwa.Ni sekta zipi
unataka kuwekeza?akauliza
balozi Mapupu
“Bado sijajua ni sekta ipi
ninaweza kuwekeza na
kupata faida ndiyo maana
nimekuja hapa kwako
nikitaka kupata kibali cha
dharura niweze kuingia
nchini Congo nikaonane na
idara inayohusika na
uwekezaji nizungumze nao
na nikitoka huko ntakuwa
nimepata picha kamili ni
sehemu gani ninaweza
kuwekeza” akasema Melanie.
Balozi Mapupu alielekeza
Melanie aandaliwe nyaraka
za kumuwezesha kuingia
nchini jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo na
ndani ya ya dakika kumi na
tano kila kitu kilikuwa tayari
“Hapa Dar es salaam
unapatikana sehemu gani?
Akauliza balozi
Mapupu.Melanie akatoa
simu na kumpatia balozi
namba zake naye balozi
akampatia za kwake
“Nitakaporejea kutoka
Congo nitakupigia
kukujulisha na kama
utakuwa na nafasi basi
tunaweza kukutana jioni
moja kwa chakula na
kinywaji tukabadilishana
mawazo” akasema Melanie
huku akitabasamu
“Nitafurahi sana
Melanie.Utakaporejea
tafadhali usiache kunipigia
simu” akasisitiza balozi
Mapupu na kumsindikiza
Melanie hadi katika gari lake
wakaagana akaondoka
“Balozi Mapupu tayari
amekwisha ingia katika
kitabu changu
chekundu.Mate yamemtoka
hasa alipoliona paja
linavyong’aa.Sikuwahi kujua
kama wanaume ni wadhaifu
kiasi hiki.Walionitengeneza
nikawa na umbo hili
nitaendelea kuwasifu siku
zote kwa akili kubwa
waliyotuma walijua kabisa
nikiwa na umbo la namna hii
hakuna mwanaume anaweza
akanikatalia jambo lolote.”
Akawaza Melanie na
kutabasamu
RIYADH – SAUDI ARABIA
Dr Abiha aliingia katika
chumba alimo Mathew
Mulumbi,kama kawaida
alikuwa ameongozana na
wale jamaa waliokuwa na
silaha akawataka wamsubiri
nje amuhudumie mgonjwa
“Habari yako Abu
Zalawi” akasema Dr Abiha
“Nzuri kabisa Dr Abiha”
“Vipi maendeleo yako?
“Ninaendelea vizuri
tofauti na jana”
“Nafurahi kusikia hivyo”
akasema Dr Abiha na
kumpima Mathew halafu
akasema
“Unaendelea vizuri Abu
Zalawi”
“Ahsante kwa huduma
nzuri Dr Abiha.Ulifanikiwa
kupata taarifa zozote
kuhusiana na Yule
mwenzangu Nawal? Akauliza
Mathew
“Hapana bado
sijafanikiwa kupata taarifa
zake zozote.Unaweza
ukanielezea zaidi kuhusu
huyo mwenzako?Ni mpenzi
wako?akauliza Dr Abiha
“Hapana si mpenzi
wangu.Ni mke wa kiongozi
wangu” akasema Mathew
“Wewe ni mwanachama
wa kikundi kipi?Abiha
akauliza
“Mimi ni mwanacahama
wa kikundi cha Ammar
Nazari brigades ambacho
kinapambana na Israel kudai
haki ya taifa la Palestina”
akasema Mathew
“Wewe ni Mpalestina?
“Hapana mimi si
mpalestina.Asili yangu ni
Misri baba yangu alijulikana
kama Khalid Al Zalawi na
aliuliwa na majeshi ya
Israel.Baada ya hapo ndipo
nilipoamua kuingia katika
mapambano na
Israel.Nilijiunga na kundi la
Ammar Nazari brigades na
huko tumekuwa tukiendeleza
mapambano dhidi ya Israel
na juzi kiongozi wetu ambaye
ni Ammar Nazari ameualiwa
na vikosi vya Israel.Yule
mwanamke niliyekuwa naye
Nawali alikuwa mke wa
Ammar Nazari na
alinikabidhi nimlinde
nihakikishe anakuwa
salama” akasema Mathew
“Kwa nini unamtafuta
Habiba Jawad?akauliza Dr
Abiha
“Kuna taarifa muhimu
nataka kumpatia”
“Kuhusu nini?akauliza
Dr Abiha
“Kuna mtu wake wa
muhimu ambaye ninafahamu
mahala alipo” akasema
Mathew
“Abu Zalawi utakataa
nikisema kwamba wewe ni
gaidi?akauliza
“Mimi si gaidi” akajibu
Mathew
“Kama si gaidi kwa nini
mnaua watu wasio na hatia?
“Haya ni mapambano Dr
Abiha na ni mapambano ya
kudai haki.Wapalestian
wana haki ya kupigana kwa
ajili ya ardhi yao ambayo
inakaliwa kimabavu na
Israel.Kwa nini Israel
wanapoua wapalestina dunia
inaona sawa lakini
wapalestina wanapoua
waisrael viongozi wa mataifa
wanasimama na kulaani?
Palestina wanapigana kwa
haki ya ardhi yao na Israel
hawana budi kurejesha ardhi
hiyo na kuacha ukandamizaji
inaowafanyia wapalestina”
akasema Mathew
“Abu wewe ni muislamu
na ninaamini unasoma
kitabu chetu
kitukufu.Unaweza
ukaniambia kitabu chetu
kinasemaje kuhusu kuua
watu wasiokuwa na
hatia?akauliza Dr Abiha
“Mwenyezi Mungu
Subhanahu wa ta’ala
ameagiza kwamba tusiue
nafsi ambayo
amekataza”akajibu Mathew
“Kwa nini saa mnaua
watu wasio na
hatia?akauliza Dr Abiha
“Katika Surah Al
Baqarah 2:190 – 192
tunaaambiwa “Na piganeni
katika njia ya Allaah na wale
wanaokupigeni, wala
msipundikie mipaka
(mkawapiga wasiokupigeni).
Kwani Allaah hawapendi
warukao mipaka. Na waueni
popote muwakutapo, na
muwatowe popote
walipokutoweni; kwani
kuwaharibu watu na dini yao
ni kubaya zaidi kuliko kuua.
Wala msipigane nao karibu
na Msikiti Mtakatifu (wa
Makka) mpaka wakupigeni
huko. Wakikupigeni (huko)
basi nanyi pia wapigeni.
Namna hivi ndivyo yalivyo
malipo ya makafiri. Lakini
kama wakikoma, Allaah ni
Mwingi wa kusamehe na
Mwingi wa kurehemu”
akasema Mathew na Dr
Abiha akabaki anamtazama.
“Sina haja ya kueleza
zaidi kwani maelezo hayo
yanajitosheleza”akasema
Mathew
“Kweli
yanajitosheleza”akasema Dr
Abiha
“Lini utanisaidia niweze
kutoka humu ndani? Vipi
kuhusu Habiba Jawad
umepata taarifa zake
zozote?akauliza Mathew
“Ninaendelea
kutengeneza mpango wa
kukutorosha pale
nitakapokuwa tayari
nitakujulisha” akasema Dr
Abiha
“Dr Abiha tafadhali
naomba unisaidie kupata
taarifa za Habiba
Jawad.Ninahitaji sana
kumuona”akasema Mathew
“Sawa nitakusaidia Abu
Zalawi “ akasema Dr Abiha
na kutoka mle ndani
akamauacha Mathew
“Niliwahi kukaa Libya
miaka miwili nikiwa kule
nilipata mafunzo ya lugha ya
kiarabu na kupata mafunzo
kuhusu Uislam.Kama
nisingepata mafunzo yale
swali aliloniuliza Dr Abiha
lingeniumbua.Anaonekana
ana nia ya dhati ya
kunisaidia.Namuomba
afanye haraka anisaidie
kwani wale jamaa wakijua
nimepata nafuu
watanirejesha tena
kuendelea kunitesa.Akinitoa
hapa lazima nifanye juu
chini nimpate Habiba
Jawad.Naamini yuko hapa
Saudi Arabia na siwezi
kuondoka bila kuonana naye”
akawaza Mathew
KINSHASA – JAMHURI YA
KIDEMOKRASIA YA
CONGO
Ndege ndogo iliyokodiwa
kutoka Dar es salaam
Tanzania iliwasili katika
uwanja wa ndege wa
kimataifa jijini
Kinshasa.Ndani ya ndege
hiyo alikuwa amepanda
Melanie Davis na dereva
wake Joyce.Ndege ilipotua
wakashuka na kufuata
taratibu za pale uwanjani
kisha wakaruhusiwa kuingia
jijini Kinshasa.Nje ya uwanja
tayari gari kutoka kampuni
ya kukodisha magari
lilikuwa linawasubiri.Kabla
ya kufika Kinshasa
maandalizi yote yalikwisha
fanyika.Melanie na Joyce
wakaingia katika gari lile la
kukodi wakaelekea mahala
ambako Melanie alielekeza
nje kidogo ya jiji la Kinshasa.
Siku hii Melanie alikuwa
amevaa mavazi meusi na
macho yake aliyafunika kwa
miwani mikubwa myeusi
kwani yalikuwa mekundu
kutokana na kulia sana
usiku kila alipowakumbuka
wazazi wake.Safari ilikuwa
ya kimya kimya hadi
walipofika katika shamba
walilokuwa wanalimiliki
wazazi wake ambako ndiko
walikozikwa.Kulikuwa na
geti lenye walinzi na Melanie
akajitambulisha kwamba
amekuja kutoa heshima za
mwisho kwa Lucy na
Laurent
Muganza.Walimuhoji yeye ni
nani na akawadanganya
kwamba anatokea Ufaransa
na marehemu Lucy Muganza
aliwahi kumsomesha ndiyo
maana amefunga safari
kutoka Paris kuja kutoa
heshima za mwisho.Walinzi
wale wakamjulisha mtu
mmoja ambaye ni mdogo
wake Laurent Muganza naye
akaelekeza watu wale
waruhusiwe kuingia
ndani.Lilikuwa shamba
kubwa na kutoka getini hadi
kufika mahala iliko nyumba
kubwa ni umbali wa kilometa
moja.Shamba lilisheheni
mazao mbali mbali
Walifika katika jumba
lile kubwa na kupokewa na
mdogo wake Laurent
Muganza.Melanie
alipomuona alishindwa
kuyazuia machozi kumtoka
kwani alikuwa amefanana
mno na baba
yake.Walikaribishwa ndani.
“Hii ni nyumba yetu
nilizoea kuja kukaa hapa
mara nyingi nirudipo kutoka
likizo kutokana na utulivu
unaopatikana mahala hapa
lakini leo hii ninakaribishwa
kama mgeni.Hakuna
anayenifahamu tena.Hata
nikiwaeleza mimi ni Theresia
Muganza hakuna
atakayeniamini” akawaza
Melanie
“Karibuni sana jamani”
baba yake mdogo Melanie
akasema
“Tunashukuru
sana.Mimi naitwa Melanie
Davis na huyu mwenzangu
anaitwa Joyce.Ninatokea
Paris Ufaransa na nimekuja
hapa kwa ajili ya kutoa
heshima kwa marehemu
Lucy na Laurent Muganza”
akasema Melanie
“Karibu sana”
“Ahsante baba.Lucy na
mumewe walikuwa watu
wakarimu sana na waliwahi
kunilipia ada ya chuo kikuu
pale nilipofiwa na wazazi
hivyo ni watu wangu wa
muhimu sana.Nilipata
taarifa za kuuawa kwao
nikiwa nchini Urusi hivyo
nikashindwa kuhudhuria
mazishi.Baada ya kupata
nafasi nimeona nije nami
nitoe heshima zangu kwa
watu hawa wema ambao
wamenifikisha hapa
nilipofika” akasema Melanie
na kufuta machozi
“Pole sana Melanie.Kifo
cha Laurent na mke wake
kinaumiza sana.Walikuwa ni
watu wema hawakuwa na
maadui na walipendwa na
kila mtu.Hata sisi
imetuumiza mno.Mimi ni
mdogo wake na Laurent”
akasema Yule jamaa
“Mmefanana
sana”akasema Melanie
halafu ukimya mfupi ukapita
“Vipi kuhusu waliofanya
mauaji haya wamekwisha
kamatwa hadi sasa?Melanie
akauliza
“Kuna utata
mwingi.Serikali ya Tanzania
inadai kwamba waliofanya
mauaji yale ni majambazi
lakini hadi leo hii hawajatoa
tena taarifa nyingine na
hawataki kuruhusu
wachunguzi wa kimataifa
wakalichunguze hili
suala.Kwa upande wa
serikali ya Congo imekuwa
kimya kabisa na hawajahi
kutoa taarifa zozote”
“Unadhani mauaji haya
yanaweza kuwa ni sababu za
kisiasa?Melanie akauliza
“Tunahisi hivyo kwa
sababu siku walipouawa ni
siku ambayo Lucy alikuwa
atangazwe na chama kikuu
cha upinzani kama mgombea
wa urais na Dar es salaam
alipita ili kumchukua
mwanae Theresia ili waje
wote Kinshasa lakini
hawakufika tena Kinshasa”
akasema Yule baba mdogo
wa Melanie
“Vipi kuhusu mtoto wa
marehemu yeye yuko
wapi?akauliza Melanie
“Theresia alinusurika
katika shambulio lile na
alipelekwa nchini Ufaransa
kwa matibabu.Tumekuwa
tunafuatilia kwa ubalozi wa
Ufaransa ili kupata taarifa
za maendeleo ya Theresia
lakini jibu ambalo tumekuwa
tukipewa ni kwamba
hatuwezi kuzungumza naye
kwani amefichwa mahala pa
siri akiendelea kupatiwa
matibabu.Kuna tetesi
kwamba toka alipotolewa
Tanzania akapelekwa
Ufaransa hajawahi
kuzinduka.Amewekwa
katika mashine za kumsaidia
kuishi”
“Mungu amsaidie aweze
kupona”akasema Melanie
“Tunasali usiku na
mchana Theresa aweze
kupona na kurejea.Wazazi
wake wameacha mali nyingi
sana ambazo zinamsubiri
yeye aweze kuziendeleza.Hivi
sasa tunaendelea na
mchakato wa kuorodhesha
mali zote za marehemu
wazazi wake na kuziweka
tayari kumsubiri aje
azisimamie”akasema Yule
jamaa.Melanie akavua
miwani na kufuta machozi
“Ninaweza tafadhali
kupelekwa mahala
walikozikwa wazee
hawa?akasema Melanie na
Yule mzee akawaongoza
kuelekea mahala
walikozikwa Lucy na
Laurent Muganza.Kulikuwa
na nyumba nzuri sana
ambayo ndani yake
kulijengwa makaburi mawili
ya Lucy na Laurent
Muganza.Mlango
ukafunguliwa na Melanie
akaomba apewe
faragha.Alilia machozi mengi
sana juu ya makaburi ya
wazazi wake
“Ninawaahidi wazazi
wangu yeyote ambaye
alishiriki katika kuwakatili
roho zenu hatabaki
salama.Nitawatafuta kokote
waliko na mmoja mmoja
lazima walipe.Damu yenu
haiwezi kupotea
bure.Ninapotoka ndani ya
nyumba hii mlimolala
ninakwenda kuanza kazi ya
kuwasaka wale wote
waliowalaza humu kabla ya
wakati wenu”Melanie
akatamka maneno hayo na
kuzibusu picha za wazazi
wake zilizokuwa katika
makaburi akafuta machozi
kisha akatoka.Hakutaka
tena kukaa eneo lile
wakaagana na Yule baba
yake mdogo kisha
wakaondoka.Hakutaka tena
kupita sehemu yoyote
akarejea uwanja wa ndege
ambako ndege ilikuwa
inawasubiri wakapanda na
kuondoka kurejea Dar es
salaam
“Kidonda changu
kimetoneshwa leo kwa
kuyaona makaburi ya wazazi
wangu.Nimeumia sana”
akawaza Melanie.Hakukuwa
na mazungumzo mengi ndani
ya ndege muda mwingi
Melanie alikuwa
ameinamisha kichwa
akiwaza na kulia.
Hatimaye ndege
ikawasili salama jijini Dar es
salaam tayari ilikuwa ni saa
kumi na mbili za jioni.Mara
tu waliposhuka
ndegeni,Melanie akampigia
simu Gosu Gosu na
kumjulisha kwamba
anakwenda kwake kisha
wakachukua gari lao
walilolicha pale uwanjani
wakaondoka.Walifika
nyumbani kwa Gosu Gosu
ambaye aliwapokea na
kuwakaribisha
sebuleni.Melanie akamtaka
waende chumbani
wakazungumze
faragha.Mara tu walipoingia
chumbani Melanie
akamrukia Gosu Gosu na
kumuangusha kitandani
kisha akaanza kutoa
nguo.Mambo yalikwenda
kimya kimya na Gosu Gosu
alielewa kile anachotakiwa
kukifanya na akashika
usukani.Ulikuwa ni
mtanange mzito sana lakini
Gosu Gosu aliumiliki vilivyo.
“Ahsante sana Gosu
Gosu,ahsante sana mpenzi
wangu” akasema Melanie
huku akimbusu Gosu Gosu
mfululizo na kumkumbatia
kwa nguvu baada ya
kumaliza mtanange ule
“Melanie ulinipania sana
siku ya leo” akasema Gosu
Gosu
“Gosu Gosu ni kweli.Sijui
ningefanya nini kama
ningekukosa.Ahsante
tena”akasema Melanie
“Nimekutafuta siku
nzima ya leo simu yako
haikuwa ikipatikana na hata
ofisini sijakuona” akasema
Gosu Gosu
“Ni kweli.Kutwa nzima
ya leo simu yangu ilikuwa
imezimwa nilikuwa na
mizunguko mingi” akasema
Melanie
“Pole sana.Kila kitu
kimekwenda vyema?akauliza
Gosu Gosu
“Usihofu kila kitu
kimekwenda
vizuri.Nashukuru
nimeimaliza siku nikiwa
kifuani kwako” akasema
Melanie na kuendelea
kukilaza kichwa chake
kifuani kwa Gosu Gosu
“Gosu Gosu nakupenda
sana na niko tayari kufanya
jambo lolote kwa ajili yako.Je
wewe uko tayari kufanya
chochote kwa ajili
yangu?akauliza Melanie
“Melanie nadhani jibu
unalifahamu kwamba niko
tayari kufanya chochote kwa
ajili yako” akasema Gosu
Gosu
“Nashukuru kwa kauli
hiyo”
“Kuna nini
Melanie?Mbona kama leo
hauko hauko sawa?
“Kuna kitu nitakuomba
unisaidie”
“Sema Melanie
nikusaidie nini?
“Kwanza kabla
sijakueleza ninachokitaka
kwako naomba nikueleze siri
yangu.Naomba tafadhali
uitunze siri hii kwani
sijawahi kumueleza mtu
mwingine yeyote”
“Usihofu Melanie.Siri
yako iko salama kwangu”
akasema Gosu Gosu
“Baba yangu na Rais
Patrice Eyenga wa DRC
walikuwa marafiki na kabla
Patrice hajawa Rais
walikuwa wanafanya
biashara pamoja.Walimiliki
kampuni kadhaa kwa
pamoja.Patrice alipotaka
kuwania urais wa Congo
kiasi kikubwa cha fedha za
kuendesha kampeni yake
alitegemea kutoka katika
biashara walizokuwa
wamechanga na
baba.Alitumia fedha nyingi
katika kampeni kwa ahadi
ya kuzirejesha pale
atakapokuwa ameshinda
urais.Baada ya kufanikiwa
kushinda urais baba
alimtaka aanze kurejesha
zile fedha ambazo ni nyingi
ili kunusuru biashara zao
lakini Rais Patrice Eyenga
alitengeneza mpango na
wazazi wangu wakauawa”
akasema Melanie na Gosu
Gosu akastuka na kuinuka
akakaa.Alihisi mwili wote
ukimsisimka kumbu kumbu
ya mauaji ya Lucy na
Laurent ikamjia
“Wazazi wako waliuawa
namna gani? Akauliza kwa
wasi wasi kidogo
“Walifariki katika ajali
ya gari ambayo tunaamini
ilitengenezwa.Gari lao dogo
liligongana na gari kubwa la
mizigo na wote wawili
wakafariki hapo hapo.Ripoti
ya wachunguzi wa
kujitegemea inaonyesha
kwamba ajali ile ilikuwa ya
kutengenezwa.Hakuna
ushahidi wa moja kwa moja
unaomuhusisha Rais Patrice
Eyenga na ajali ile lakini
tunaamini anahusika kwa
sababu kifo cha baba
kilitokea mara tu ulipoanza
mzozo kati yake na Patrice
kuhusu fedha”
“Pole sana Melanie”
akasema Gosu Gosu
“Ahsante
sana.Nimekwisha lia sana
kwa miaka mingi na machozi
yamekauka.Hivi sasa sina
tena machozi.Gosu Gosu
kilichopo katika akili yangu
kwa sasa ni jambo moja
tu.Ninataka kulipa kisasi
kwa Rais Patrice Eyenga
kwa kile alichonifanyia”
akasema Melanie na Gosu
Gosu akabaki
kimya.Alishindwa aseme nini
“Unanisikia Gosu
Gosu?akauliza Melanie
baada ya kumuona Gosu
Gosu amebaki kimya
“Nimekusikia Melanie”
“Naamini utaniunga
mkono katika harakati
zangu.Nataka Patrice
Eyenga naye apate maumivu
makali kwa kumpoteza mtu
wake wa karibu sana kama
mimi nilivyopata maumivu
makali kwa kuwapoteza
wazazi wangu” akasema
Melanie na Gosu Gosu
akahisi kama kuna kitu
kimekwama katika koo lake
akakohoa kidogo
“Gosu Gosu umekuwa
kimya ghafla baada ya
kukueleza jambo langu kuna
tatizo lolote?akauliza
Melanie
“Hapana niko sawa
Melanie”
“Unasemaje kuhusiana
nahiki
nilichokueleza?akauliza
Melanie
“Niko nawe Melanie
katika jambo lolote.Siwezi
kukuacha nyuma.Katika
jambo lolote lile nitatangulia
mbele na wewe utakuwa
nyuma yangu nitakulinda
dhidi ya hatari zozote
zinazoweza kujitokeza.Pole
sana kwa mara nyigine kwa
kifo cha wazazi wako na
Patrice Eyenga anapaswa
kulipa uovu wake
aliokufanyia.Nini unafikiria
kukifanya katika mpango
wako wa kulipiza
kisasi?akauliza Gosu Gosu
“Ahsante kwa kuniunga
mkono.Nitahitaji msaada
wako Gosu Gosu”
“Unahitaji nifanye nini
Melanie?Niambie chochote
nitakifanya” akasema Gosu
Gosu
Melanie akavuta pumzi
ndefu na kusema
“Nahitaji kuonana na
James Kasai”akasema
Melanie na Gosu Gosu
akahisi kama tumbo lake
limekuwa tupu ghafla
“James Kasai
yupi?akauliza Gosu Gosu
“Kwa miaka mingi
umekuwa katika mapigano
msituni.Humfahamu James
Kasai?akauliza Melanie
“James Kasai
ninamfahamu kama kiongozi
wa kundi la waasi walio
furushwa kutoka jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo na na
kukimbilia katika misitu ya
Uganda.Wakati James na
kundi lake wanafurushwa
jeshi la Congo lilivuka mpaka
na kuingia Uganda katika
kuwatafuta waasi hao ambao
walikataa kuweka silaha zao
chini.Uganda iliita kitendo
hicho cha wanajeshi wa
Congo kuvuka mpaka kama
kitendo cha uvamizi na
kuongeza majeshi yake
mpakani.Jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo
inailaumu Uganda kuwa
inawahifadhi waasi hao na
Uganda inailaumu Congo
kwa jeshi lake kuvuka
mpaka na kuua raia wake”
“Safi sana kumbe bado
unafuatilia masuala hayo
kwa karibu.Huyo James
Kasai ambaye alikimbilia
Uganda baada ya
kufurushwa Congo ndiye
ambaye ninataka kuonana
naye.Nitakuachia wewe kazi
hiyo ya kutafuta namna ya
mimi kuweza kuonana
naye.Sifahamu utafanyaje
lakini ninachohitaji mimi ni
kupata nafasi ya kuonana na
James Kasai” akasema
Melanie
“Sawa Melanie
nitajitahidi kutafuta namna
ili uweze kuonana na huyo
mtu unayemuhitaji” akasema
Gosu Gosu
“Ndiyo maana
nakupenda sana Gosu Gosu”
akasema Melanie na kuanza
kumwagia mabusu mazito
kisha wakaingia katika
raundi nyingine ya
mtanange.
“Gosu Gosu jambo hili
nililokueleza ni siri kubwa
hivyo asifahamu mtu
yeyote”akasema Melanie
wakati akijiandaa kuondoka
“Mimi ni mwanajeshi
ninafahamu maana ya
kutunza siri hivyo usiwe na
wasiwasi mpenzi wangu”
akasema Gosu Gosu
“Nakupenda sana Gosu
Gosu” akasema Melanie na
kumbusu Gosu Gosu kisha
akaelekea katika gari lake
wakaondoka.Baada ya
Melanie kuondoka Gosu
Gosu akarejea ndani akiwa
ameinamisha kichwa alihisi
kitu kama nyundo inagonga
kichwa chake.Moja kwa moja
akaelekea katka baa yake
ndogo iliyoko mle ndani
akachukua chupa ya pombe
kali akaelekea chumbani
kwake akamimina katika
glasi akanywa yote akaweka
tena mara ya pili akanywa
yote kisha akashusha pumzi
“Melanie ametaka
kunipasua moyo wangu
leo.Mstuko nilioupata pale
aliponitamkia kwamba
Patrice Eyenga anahusika
katika vifo vya wazazi wake
ni mkubwa.Nashukuru
wazazi wake walifariki huko
Ufaransa” akawaza Gosu
Gosu na kunywa funda la
kinywaji kile kikali
akafumba macho
“Kwa nini Melanie
anataka kuonana na James
Kasai?Huyu ni mtu mbaya
na katili sana.Ni mtu
ambaye amekuwa
anatafutwa ili afikishwe
katika mahakama ya uhalifu
wa kivita kutokana na
ukatili mkubwa ambao kundi
lake liliufanya wakati
likipambana na majeshi ya
serikali ya Congo.Hadi leo
bado James ameshindwa
kukamatwa kwa sababu
anakingiwa kifua na nchi ya
Uganda ambao inadaiwa
wamempa hifadhi.Nahisi
kwamba Melanie anataka
kuandaa mipango ya kulipiza
kisasi kwa Rais Patrice
Eyenga na anataka
kumtumia James Kasai”
akawaza na kujiegemeza
sofani
“Sikutaka tena kujiingiza
katika masuala yoyote ya
mauaji,nilitaka niishi maisha
ya amani lakini siwezi
kumuacha Melanie peke
yake katika suala
hili.Lazima nisimame
naye.Ninampenda na huu ni
wakati mzuri wa
kumuonyesha ni namna gani
ninampenda na
kumthamini.Kama ni kuua
niko tayari kuua kwa ajili
yake.Nitatafuta namna ya
kumpata James Kasai”
akawaza Gosu Gosu na
kuchukua simu yake.
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 5: EPISODE 5
Melanie alifika nyumbani
kwake na kupokewa na
Edwin Mbeko ambaye
alikwisha fika pale
nyumbani kwake
akimsubiri.Hakuwa peke
yake alikuwa na wanawake
wawili wamewakaa sebuleni
wakitazama runinga.
“Melanie Davis karibu
sana” akasema Edwin Mbeko
“Ahsante sana
Edwin”akajibu Melanie
“Samahani kwa kuvamia
nyumbani kwako lakini
nimekutafuta sana simuni
kutwa nzima ya leo hakuna
simu yako hata moja
inapatikana ndiyo maana
nikaamua kuwaleta wageni
moja kwa moja hapa
nyumbani.Wamewasili jioni
ya leo”akasema Edwin
“Edwin tunaweza
kuzungumza kidogo
faragha?akasema Malanie na
kwenda katika chumba cha
mazungumzo ya faragha
wakiwaacha wale wasichana
wawili sebuleni.
“Ulikuwa wapi
Melanie?Nimetaarifiwa na
walinzi wako kwamba
ulikwenda uwanja wa ndege
ukapanda ndeg………………”
“Edwin ! akasema
Melanie na kumkatisha
Edwin.Sauti na sura ya
Melanie vilionyesha hakuwa
anataka masihara
“Edwin ninakuheshimu
sana lakini kitendo cha
kuingia ndani ya nyumba
yangu wakati sipo
kimeniudhi sana.Unafikiri
hapa ni bar au klabu ya
disko unakoweza kuingia
muda wowote na kutoka
utakavyo?akafoka
Melanie.Edwin hakuamini
kumsikia Melanie akifoka
“Ndiyo maana
nilitangulia kusema
samahani kwani baada ya
kukukosa simuni niliamua
kuwaleta wale wasichana
hapa moja kwa moja baada
ya kuwapokea uwanja wa
ndege” akasema Edwin
“Hukupaswa kuingia
humu ndani kama kwako.Hii
ni nyumba yangu na mimi
ndiye mwenye amri.Kuanzia
sasa sitaki uingie ndani ya
nyumba hii bila ya ruhusa
yangu na nitabadilisha
mfumo mzima wa kuingia
humu ndani.Lazima uwe na
heshima.Unanionaje
mimi?akauliza Melanie kwa
ukali
“Madam Melanie
samahani sana.Nimekosea
sintarudia tena” akasema
Edwin
“Na iwe
hivyo.Usithubutu tena
kurudia jambo kama hili!
Akasema Melanie kwa ukali
“Nimekuelewa madam”
“One more thing”
akasema Melanie
“Kuanzia sasa na
kuendelea sitaki uniulize
kuhusu safari zangu.This is
my operation and I’m doing it
my way.Kama unataka
kufanya kazi na mimi
utafuata masharti yangu.You
understand me? Akauliza
Melanie kwa ukali
“Nimekuelewa mama”
“Good.Tell your team…..”
Melanie akanyamaza kidogo
“Waambie watu wako
wanaonifuatilia kuacha mara
moja.I don’t need any back
up.Pale nitakapowahitaji
nitakujulisha but for now I
can manage on my own.You
understand me? Akauliza
Melanie
“Lakini madam Melanie
hayo yalikuwa ni maelekezo
ya kutoka kwa Devotha”
akasema Edwin
“Forget about Devotha !
akafoka Melanie
“She’s not here ! I repeat
this is my operation and I’m
I’m gong to do it my
way.You,Devotha and
everyone will listen to me
because I’m your boss.You
understand me?
“Nimekuelewa madam
Melanie”
“Good.Una taarifa zozote
mpya?
“Taarifa mpya leo ni ujio
wa hawa wanawake wawili
wasaidizi wako” akasema
Edwin kisha wakashuka
chini sebuleni ambako
Melanie akatambulishwa
kwa wale wanawake wawili
akawakabidhi kwa Joyce
yeye akaenda chumbani
kwake kupumzika
“Toka nilipoyaona
makaburi ya wazazi wangu
hali yangu
imebadilika.Najiona kama ni
Melanie mwingine
kabisa.Nimekuwa na hasira
kwa kila mtu nimeingiwa na
roho ya ukatili na siogopi
chochote.Ninachokihitaji ni
kitu imoja tu kulipa kisasi
kwa wale wote waliowaua
wazazi wangu kikatili na
kwa kuanzia ninaanza na
mke wa Patrice Eyenga
halafu nitakuja kwa Rais wa
Tanzania hadi wote wapate
maumivu kama haya
niliyonayo mimi” akawaza
Melanie
RIYADH – SAUDI ARABIA
Saa ya ukutani
ilionyesha ni saa saba za
usiku pale mlango wa
chumba alimolazwa Mathew
Mulumbi
ulipofunguliwa.Tayari
alikuwa usingizini lakini
alistuka baada ya kusikia
mlango
ukifunguliwa,akafumbua
macho na kustuka baada ya
kumuona aliyeingia mle
ndani ni mwanamke
alipomtazama vizuri alikuwa
ni Dr Abiha.Mathew
akainuka na kukaa
“Dr Abiha ! akasema
“shhhhh ! akasema Dr
Abiha akimtaka Mathew
akae kimya.Akatulia kwa
sekunde chache kusikia
kama kuna mtu yeyote
atajitokeza halafu akamtaka
Mathew ainuke.Akatoa
mfuko uliokuwa na nguo
suruali ya jeans na fulana ya
kijivu akavaa kisha
akamtaka amfuate.Dr Abiha
akafungua mlango taratibu
na kuchungulia katika korido
kama kuna mtu.Kulikuwa na
ukimya mkubwa.Wakatoka
na Dr Abiha akaufungua
mlango taratibu wakatokea
nje wakajibanza katika tanki
tupu la maji kwa sekunde
kadhaa halafu wakatembea
haraka haraka wakaelekea
katika geti la Dr
Abiha.Akafungua buti ya
gari na kumtaka Mathew
aingie kisha
wakaondoka.Akiwa ndani ya
buti Mathew aliingiwa na
hofu baada ya gari
kusimama na Abiha akaanza
kuzungumza na walinzi
kisha akasikia sauti
ikuamuru geti lifunguliwe na
gari la Dr Abiha
likatoka.Baada ya mwendo
wa kama nusu saa gari lie la
Dr Abiha likazima na
sekunde chache baadae buti
likafunguliwa Dr Abiha
akamtaka Mathew
ashuke.Akamuongoza
kuelekea ndani.Ilikuwa ni
nyumba nzuri
“Dr Abiha nakushukuru
sana kwa kunitoa katika
mikono ya wale jamaa”
“Usijali Abu Zalawi
ninawafahamu wale jamaa ni
watu makatili ndiyo maana
nikafanya kila niwezalo
kukusaidia”
“Ulifanikiwa kupata
taarifa zozote kuhusuana na
Nawal?
“Hapana sijapata taarifa
zake zozote.Abu Zalawi
umemapata nafasi ya
kuponyoka kutoka katika
mikono ya wale jamaa sahau
kuhusu Nawal” akasema Dr
Abiha
“Dr Abiha ninashukuru
sana kwa msaada wote
ulionisaidia hadi ukanitoa
katika mikono ya wale jamaa
lakini siwezi kuondoka
Riyadh bila ya
Nawal.Nitamsaka kila kona
hadi nimpate na kuhakikisha
yuko salama.Nilibeba
dhamana ya kuhakikisha
anakuwa salama” akasema
Mathew
“Abu Zalawi huyu Nawal
ana umuhimu gani kwako
hadi uwe tayari kuhatarisha
maisha yako kiasi hiki?
“Niliweka ahadi ya
kuhakikisha anakuwa
salama na lazima niitimize”
akasema Mathew
“Sawa nimekuelewa.Kwa
sasa ni usiku mwingi
utapumzika na kesho
asubuhi tutaanza harakati za
kumtafuta Nawal” akasema
Dr Abiha na kumpeleka
Mathew Mulumbi katika
chumba kimoja ndani ya
nyumba ile akamtaka alale
“Usihofu Abu hapa ni
sehemu salama sana.Wale
jamaa hawataweza kukufikia
wala kujua kama uko hapa”
“Vipi kuhusu
wewe?Hawatajua kama
ndiye uliyenitorosha pale
hospitali?akauliza Mathew
“Hawatafahamu kama ni
mimi ndiye
niliyekutorosha.Walinzi
wanaolinda geti
nilizungumza nao na
kuwalipa fedha”akasema Dr
Abiha na kumuaga Mathew
akatoka
“Ahsante Mungu kwa
kunisaidia nimeweza kutoka
katika mikono ya wale
mashetani.Wamenitesa
mno.Mikono yangu
wameitoboa kwa visu.Siwezi
kusahau mateso yale makali
waliyonipa” Mathew
akaomba kimya kimya
“Sasa baada ya kutoka
kwa wale jamaa
kinachofuata ni kumtafuta
Nawal nijue mahala
alipo.Naamini Abdel Fattah
atakuwa anafahamu mahala
alipo Nawal nitamuomba Dr
Abiha anisaidie nifike
anakoishi Abdel
Fattah.Nitavamia makazi
yake na nitafanya kitu
ambacho hataamini macho
yake na nitampata
Nawal.Nikisha mpata Nawal
nitaendelea na mchakato
wangu wa kumtafuta Habiba
Jawad.Nimefika katika ardhi
alipo Habiba na siwezi
kuondoka bila kuhakikisha
nimeonana naye” akawaza
Mathew na kuanza
kukumbuka alikotoka hadi
alipofika
“Fatma yuko wapi? Yeye
ndiye aliyetuleta hapa
Riyadh kwa nini amepotea
na kutuacha tukihangaika
namna hii?Alihangaika sana
huko njia hadi kuhakikisha
tunafika hapa.Kuna sehemu
nyingine tulisimamishwa
katika vizuizi akalazimika
kutumia fedha na yote haya
aliyafanya ili kuhakikisha
tunafika Riyadh kuonana na
Habiba Jawad.Je naye
ametekwa?akajiuliza
Mathew
“Nitapata jibu
kesho.Siogopi kama niko
katika nchi ya watu lakini
nitauwasha moto hapa
Riyadh na hawataamini.Nina
hasira nyingi na hawa watu
na laiti Abdel Fattah Sarraf
angejua kile kinachokwenda
kumtokea kuanzia kesho
angekimbia.Nina hasira naye
sana”akawaza Mathew na
kuamua kujilaza kitandani
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 5: EPISODE 6
“Abu Zalawi” Sauti ya Dr
Abiha ilipenya katika
masikio ya Mathew na
kumfanya ahisi kama anaota
hadi pale alipotikiswa ndipo
alipofumbua macho na
kumkuta Dr Abiha akiwa
amesimama mbele yake
akitabasamu
“Habari za asubuhi Abu
Zalawi”
“Nzuri Dr Abiha”
“Vipi maendeleo yako?
“Ninaendelea vizuri.Yale
maumivu yamepungua”
“Vizuri amka ujiandae
tuna safari”
“Tunaelekea wapi?
“Usihofu amka uoge
ujiandae” akasema Dr Abiha
na kumuonyesha Mathew
lilipo bafu akaingia
kuoga.Kisha oga akarejea
chumbani kwake akakuta
kuna suti nzuri ya rangi
nyeusi ikiwa
kitandani.Mathew
akatabasamu na mara
mlango wake ukagongwa
akaufungua na kukutana na
Dr Abiha wakatazama kwa
sekunde chache Dr Abia
akatabasamu na kusema
“Utavaa suti hiyo
kitandani” akasema na
kuondoka
Mathew akaivaa suti ile
nzuri ikamtosha
vizuri.Akatabasamu baada
ya kujitazama katika kioo
namna alivyopendeza
“Dr Abiha
amenikumbusha mbali sana
enzi zangu haya ndiyo
yalikuwa mambo
yangu.Nilikuwa nanyuka
suti balaa lakini hivi sasa
nimechakaa sina mvuto tena
na hata suti
hazinipendezi.Hata hivyo
pamoja na kuchakazwa na
mateso na hali ngumu
ninayopitia I’m still
handsome” akawaza na
kutabasamu.
“Abu Zalawi uko
tayari?akauliza Dr Abia
baada ya kuingia mle ndani
bila kubisha hodi
“Niko tayari.Wapi
tunaelekea?akauliza Mathew
“Usiwe na
wasiwasi”akasema Dr Abia
wakatoka mle chumbani
wakaelekea sebuleni ambako
aliwakuta watu
watano.Mathew akahisi
kuna hatari akajiandaa
kukabiliana nao
“Abu Zalawi hawa jamaa
watakupelekea sehemu
fulani” akasema Dr Abia na
mmoja wa wale jamaa
akamshika Mathew mkono
na kumuongoza kuelekea nje
ambako kulikuwa na magari
matatu.Gari mbili ndogo na
kati kati ya gari zile mbili
kulikuwa na gari moja
ambalo hutumika katika
kusafirishia chakula au vitu
vinavyoharibika
haraka.Milango ya nyuma ya
gari lile ikafunguliwa
akaingizwa ndani.Ndani ya
gari lile kulikuwa na viti na
kitanda cha
kupumzikia.Milango
ikafungwa na gari
likawashwa na kuondoka.
“Wananipleka wapi hawa
jamaa?akajiuliza Mathew
Ndaniya gari lile
kulikuwa na hewa nzuri
japokuwa hakukuwa na
dirisha hata moja.Mara
kadhaa gari lile lilisimama
kisha likaendelea na
safari.Hatimaye baada ya
mwendo mrefu gari lile
likasimama na milango
ikafunguliwa.Watu wawili
wakaingia ndani ya lile gari
Mathew akavishwa mfuko
kichwani akashushwa garini
akaingizwa ndani ya nyumba
na mfuko ule ukatolewa
kichwani.Alijikuta katika
sebule nzuri.
“Sebule nzuri
sana.Samani zake
zinaonyesha ni za gharama
kubwa.Nani anaishi
hapa?Lazima atakuwa na
uwezo mkubwa kifedha kwa
sababu vitu ninavyoviona
humu si vya kawaida.Huyu
mtu lazima ni tajiri mkubwa
sana” akawaza Mathew na
kuketi sofani.Muhudumu
akafika akiwa na sinia
akamuandalia Mathew juice
na kumkaribisha.Wakati
akiendelea kupata juice
wakaingia watu watano
waliovalia suti wakazunguka
mle sebuleni.Hakuna
aliyemsemesha kitu chochote
Mathew.
“Maandalizi
yanafanywa,inaonekana
kuna mtu
anakuja.Sintakubali kuteswa
leo na nitakabiliana na
yeyote atakayethubutu
kunigusa” akawaza Mathew
huku akionyesha kutokujali
chochote akaendelea kunywa
juice.Baada ya dakika tatu
toka wale jamaa waingie pale
sebuleni akatokea jamaa
mmoja aliyevaa kanzu nzuri
nyeupe.Alikuwa
ameongozana na walinzi
wengine wanne.
“Abu Zalawi” akasema
Yule jamaa huku
akitabasamu na kumpa
Mathew mkono
“Karibu sana” akasema
na kuwataka walinzi wote
watoke mle ndani na
kuwaacha peke yao
“Naamini hunifahamu
bado.Ninaitwa Sayid
Omar.Ni moja wa
wafanyabiashara wakubwa
hapa Riyadh” akasema Yule
jamaa na Mathew
akakumbuka mbali wakati
akishughulikia suala la
Olivia aliwahi kusama barua
pepe kati ya Olivia na Sayid
Omar.
“Huyu ndiye Yule
ambaye alishirikiana na
Olivia kutengeneza kirusi”
akawaza Mathew
“Abu Zalawi nakupa pole
sana kwa yote yaliyokupata
kwanza kuanzia kufungwa
gerezani,mateso yote
uliyopitia na hadi
uliponusurika katika
shambulio na vikosi vya
Israel.Ninamfahamu Ammar
Nazari na niliposikia
ametoka gerezani nilifurahi
sana.Siku alipotoka gerezani
alinipigia simu
nikampongeza na
akaniambia namna
alivyofanikiwa kutoroka
gerezani.Kilikuwa ni kitendo
cha hatari lakini cha
kishujaa.Nilipopata taarifa
za kifo chake nilistuka na
kuumia sana.Tumempoteza
mtu mmoja muhimu katika
mapambano ya kudai haki”
akasema Sayid
Omar.Mathew hakusema
chochote aliendelea
kumsikiliza
“Tulipata taarifa kutoka
kwa Fatma kwamba mjane
wa Ammar anaitwa Nawal
amekwenda kwake akiwa
ameongozana na Abu Zalawi
na wanahitaji msaada na
kubwa walilohitaji ni
kuonana na Habiba
Jawad.Nilimtaka awaulize
sababu kuu ya kutaka
kuonana na Habiba na
akasema ni Abu anazo
taarifa kuhusiana na mtu
anayeitwa Edger
Kaka.Nilimtuma Fatma
aulize mara mbili kuhusu
hicho alichoambiwa kwamba
wana uhakika wanazo
taarifa za kumuhusu Edger
Kaka na baada ya
kunithibitishia kwamba Abu
Zalawi anazo taarifa muhimu
za Edger Kaka nilimtaka
Fatma afanye taratibu na
kuhakikisha anawaleta
Riyadh yeye
mwenyewe.Japokuwa
umekuwa na Ammar kwa
muda na hata umefanikiwa
kutekeleza shambulio la
Jerusalem lakini bado
ilitulazimu kujiridhisha
kuhusu wewe.Je kweli wewe
ni Abu Zalawi? Tulifanya
hivyo kwa sababu Habiba
Jawad ni mtu anayetafutwa
sana na Israel na tulihofu
wanaweza wakatumia mbinu
ya kumpandikiza mtu katika
mtandao wa kigaidi ili aweze
kufahamu mahala alipo
Habiba.Kuuawa kwa Ammar
Nazari kulitupa wasi wasi
kwani kwa miaka mingi
Israel hawakuwahi
kufahamu mahala anapoishi
Ammar.Lakini baada ya ujio
wako katika kundi la Ammar
Nazari brigades Ammar
amejulikana mahala alipo na
akauawa.Tulitafuta katika
mitandao na kuzipata taarifa
zako kwamba unatafutwa na
Israel lakini tukataka
tujiridhishe
zaidi.Tulitengeneza taarifa
za mtu ambaye tulimfanya ni
Abu Zalawi ili wewe
uonekane
unadanganya.Abdel Fattah
alipewa kazi ya kukuhoji na
ndipo alipoanza
kukutesa.Wewe na
mwenzako Nawal mlipatiwa
mateso kwa wakati
mmoja.Wakati mkiteswa
tulikuwa tunafuatilia kila
kitu.Pamoja na mateso yale
yote hukutetereka na
hukulikana jina lako.Kwa
mateso yale makali hakuna
ambaye angeweza kuvumilia
na kama ungekuwa si Abu
Zalawi ungeweza kukiri.Japo
ulivuka mtihani wa kwanza
tulikupeleka hospitali
ambako tulimtumia Dr Abiha
kuendelea kukuchunguza na
kujiridhisha kama kweli
wewe ni Abu Zalawi na una
nia ya dhati ya kuonana na
Habiba jawad.Kama
utakumbuka Dr Abiha
amekuwa akikuuliza mswali
mengi lengo likiwa ni kutaka
kukufahamu
zaidi.Tumefuatilia maongezi
yako yote na Dr Abiha na
mwisho tukajiridhisha
kwamba kweli wewe ni Abu
Zalawi.Baada ya kuridhika
nawe ndipo nikaelekeza
nikutane nawe.Pole sana
kwa yote uliyokutana
nayo.Ilikuwa lazima upitie
mateso yale ili
tujiridhishe.Tunafanya hivi
kwa ajili ya kumlinda Habiba
Jawad ambaye anatafutwa
sana na Israel.Mtu yeyote
ambaye anataka kuonana
naye hawezi kwenda moja
kwa moja lazima kwanza
apitie mitihani kama ile na
ashinde ndipo anapoweza
kupata nafasi ya kuonana na
Habiba Jawad.Wewe
umefanikiwa kushinda
mtihani huo na ndiyo maana
uko hapa.Mimi ni mshirika
mkubwa wa Habiba Jawad
na huwezi kuonana na
Habiba jawad bila kupitia
kwangu” akasema Sayid
Omar na Mathew akalengwa
machozi
“Kumbe ujasiri wangu
wa kuvumilia mateso na
kushikilia msimamo kwamba
mimi ni Abu Zalawi
umenisaidia.Endapo
ningekata tamaa mapema
ningepoteza kila kitu”
akawaza Mathew
“Vipi maendeleo yako
Abu Zalawi?akauliza Sayid
Omar
“Ninaendelea vizuri.Dr
Abiha amenihudumia vizuri
sana”
“Abu Zalawi nakuomba
uwe na amani na usiwe na
hasira na mtu yeyote kwa
yale uliyoyapitia.Ilikuwa
lazima uyapitie.Wale wote
waliokupitisha katika
mtihani ule hawana ubaya
nawe bali walikuwa
wanafuata maelekezo
waliyopewa.Tusameheane
kwa yote yaliyotokea”
akasema Sayid Omar
“Mwenyezi Mungu
Subhanahu wa ta’ala
ametusisitiza tusameheane
na siwezi kwenda kinyume
na maelekezo yake hivyo
nimesamehe yote
yaliyonitokea na moyo wangu
una amani”akasema Mathew
“Ahsante sana Abu
Zalawi.Kwa kuwa tayari
umeshinda mtihani basi
wewe ni mwenzetu na
nitakupeleka kuonana na
Habiba Jawad uzungumze
naye umueleze kile ambacho
unatataka kumueleza lakini
kuna taratibu ambazo lazima
uzipitie” akasema Sayid
Omar na kuinuka akawaita
walinzi wake na kuwapa
maelekezo Mathew
akafunikwa mfuko kichwani
na kutolewa mle ndani
akaingizwa katika helkopta
na baada ya dakika chache
ikapaa na kuondoka.
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Melanie Davis aliamka
mapema sana na kujiandaa
kwa ajili ya kuikabili
siku.Alipokuwa tayari
hakusubri kifungua kinywa
kilichokuwa kinaandaliwa na
wale watumishi wake wa
ndani akamtaka Joyce
dereva wake waondoke.Moja
kwa moja wakaelekea kwa
Gosu Gosu.Hakuwa
amemtaarifu kama
atakwenda asubuhi ile
“Sikukujulisha kama
ninakuja nilitaka kuja
kufumania” akasema
Melanie na wote wakacheka
“Karibu sana” akasema
Gosu wakaelekea chumbani
na kumuacha Joyce sebuleni
“GosuGosu nimeshindwa
kulala usiku wa leo
nikikuwaza ndiyo maana
nilipoamka asubuhi ya leo
hata kifungua kinywa
nimeshindwa kupata
nimeharakisha nije nikuone”
akasema Melanie huku
akiwa amekumbatiana na
Gosu Gosu wakipeana
mabusu
“Melanie hapa ni kwako
na unaweza ukaja muda
wowote unaotaka.Usihofu
kama ninaweza kukusaliti
siwezi katu kufanya
hivyo.Ninakupenda mno”
“Nashukuru sana Gosu
Gosu” akasema Melanie
“Kuhusu lile suala la
jana” akasema Gosu Gosu
“Ehee”
“I made some phone
calls.Nitapata jibu baadae
lakini muelekeo wa
kufanikiwa kuonana na
James Kasai ni mkubwa”
akasema Gosu Gosu
“Ahsante sana Gosu Gosu
kwa kusimama nami katika
hili”
“Usijali mpenzi wangu
mimi nitasimama nawe
katika kila jambo.Kama
nilivyokuahidi kwamba
nitatangulia mbele na kuwa
ngao yako kukulinda na kitu
chochote kibaya” akasema
Gosu Gosu
“Sikufanya kosa
kukupenda Gosu Gosu.Wewe
ni wa kipekee kabisa
kwangu” akasema Melanie
“Melanie mpenzi wangu
naomba nikuweke
wazi.James Kasai si mtu wa
mchezo.Ni mtu hatari
sana.Nchi za Congo na
Uganda
wanamfahamu.Kitendo cha
kutaka kuonana naye
kinatuweka katika hatari
kubwa.Hata hivyo
ninakuahidi tutakuwa
salama.Nitakulinda
usijali.Lakini kuna kitu
nahitaji kufahamu kama
hutajali” akasema Gosu Gosu
“Uliza chochote Gosu
Gosu nitakujibu”
“Nini dhumuni la kutaka
kuonana na James
Kasai?akauliza Gosu Gosu
“Nataka kumuua Rebeca
Eyenga mke wa Patrice
Eyenga.Nataka kumuumiza
Patrice Eyenga”
“Kama ni hilo hakuna
haja ya kuhatarisha maisha
kwenda Uganda kuonana na
James Kasai.Ninaweza
kuifanya hiyo kazi.I’m a
soldier and I can kill for you”
akasema Gosu Gosu.Melanie
akatabasamu akambusu
GosuGosu
“My love ninakupenda
sana na ninajua unanipenda
na unaweza ukaifanya hiyo
kazi lakini sitaki nikuingize
katika hayo mambo ndiyo
maana ninataka kumtumia
adui wa Patrice Eyenga
kufanya kazi hiyo.Naomba
uwe na amani mpenzi
wangu”
akasema Melanie na
kumbusu tena Gosu Gosu
“Usiwe na haraka ya
kutaka kuua kwa ajili yangu
iko siku utafanya mauaji
ambayo hata shetani
asingeweza kuyafanya.Siku
hiyo yaja GosuGosu kaa
tayari” akawaza Melanie.
Walipata kifungua
kinywa kisha wakatoka
kwenda kutembelea baadhi
ya miradi ambayo Melanie
alikuwa ameinunua kutoka
kwa Peniela
RIYADH – SAUDI RABIA
Helkopta aliyopanda
Mathew ilitua bila Mathew
kuelewa mahala
alikopelekwa.Muda wote
ilipokuwa angani alikuwa
amevalishwa mfuko mweusi
kichwani na kuwekewa vifaa
maalum masikioni ili asiweze
kusikia wala kuona
chochote.Mara tu helkopta
ailipotua Mathew
akashushwa na kukimbizwa
ndani bado aliendelea
kufunikwa
kichwani.Alipandishwa ngazi
na kuingizwa katika chumba
kimoja chenye ubaridi mzuri
uliotokana na kiyoyozi
akakalishwa katika
sofa.Hakuweza kuona
chochote kutokana na ule
mfuko aliovishwa kichwani
lakini aliweza kuhisi kuna
watu mle sebuleni ambao
aliamini walikuwa
wanamlinda.Baada ya
dakika kumi akasikia hatua
za mtu akiingia mle
chumbani na harufu ya uturi
mzuri sana ikajaa mle
sebuleni.Mfuko aliovishwa
kichwani ukatolewa na
Mathew akajikuta
akitazamana na Nawal
ambaye alikuwa amerembwa
vilivyo.Alikuwa amevaa
mavazi ya gharama kubwa
na vito vya thamani.Mathew
akabaki mdomo
wazi.Ulikuwa ni mshangao
mkubwa kwake.
“Nawal ! akasema
Mathew kwa mshangao
“Hallow Abu Al Zalawi”
akasema Nawal
“Siamini macho
yangu.Nilikuwa na mawazo
mengi sana kuhusu
wewe.Sikujua umepelekwa
wapi na nitakupataje”
akasema Mathew
“Ahsante kwa kunijali
Abu Zalawi lakini mimi niko
salama usihofu” akasema
Nawal
“Nini
kilitokea?Ulipelekwa
wapi?Umefikaje
hapa?akauliza Mathew
“Nilipitia hatua ulizopitia
wewe.Siku ile
ulipochukuliwa kutoka
katika ile nyumba
tulimofikia mimi pia
nilichukuliwa na kupelekwa
sehemu ambako niliteswa
sana.Nilipitia mateso
makali” akasema Nawal
huku akilengwa na machozi
“Pole sana Nawal”
akasema Mathew na Nawal
akatabasamu
“Ahsante.Yameshapita.B
aada ya kuteswa sana
nikaingizwa katika helkopta
na kuletwa hapa.Niliuliza
kuhusu wewew
nikahakikishiwa kwamba
uko salama na wewe pia
utaletwa hapa.Nimefurahi
nimekuona tena Abu”
akasema Nawal
“Pole Nawal.Nilikuwa na
wasiwasi mwingi sana
kuhusu usalama wako”
“Waliniambia umekuwa
unaniulizia kila mara na
uliahidi kwamba huwezi
kuondoka Riyadh bila
mimi.Ahsante sana kwa
kunijali Abu Zalawi.Pole vile
vile kwa yote uliyoyapitia”
akasema Nawal
“Haikuwa
rahisi.Nimepitia mateso
mengi lakini nashukuru jana
nimeonana na Sayid Omar
akanieleza kwamba mateso
yale yote niliyopitia ulikuwa
ni mchakato wa kunipima
kabla sijaonana na Habiba
Jawad.Mahala hapa ni wapi?
Akauliza Mathew
“Hapa ni makazi ya
bilionea Abu Dahir”
“Abu Dahir ni
nani?akauliza Mathew
“Ni mfanya biashara
tajiri sana na mtoto wa
Habiba Jawad”
“Sayid aliniambia
kwamba ninakuja kuonana
na Habiba Jawad je naye
anaishi hapa?Mathew
akauliza
“Sina hakika kama naye
anaishi hapa kwani toka
nimefika hapa sijafanikiwa
kuonana naye.Niliyeonana
naye ni mtoto wake Abu
Dahir”
“Kwa nini tumeletwa
hapa?akauliza Mathew
“Mathew kuna jambo
ambalo unapaswa
kulifahamu” Akasema Nawal
“Jambo gani
Nawal?akauliza Mathew
akionekana kuwa na
wasiwasi.
“Nieleze Nawal kuna
tatizo gani?
“Abu dahir anataka
kunioa”
“Abu anataka kukuoa?!
Mathew akashangaa
“Ndiyo anataka
kunioa.Aliponiona alinipenda
na akaagiza niletwe
hapa.Nimepewa jumba
kubwa la kuishi wakati
tukisubiri taratibu nyingine
zikamilike kabla ya kufunga
ndoa”akasema Nawal
“Wewe umekubali
kuolewa na huyo Abu
Dahir?akauliza Mathew
“Ndiyo niko tayari
kuolewa naye.Kwa sasa sina
mume hivyo sioni sababu ya
kukataa kuolewa naye”
akasema Nawal
Mathew alizisoma alama
za mwili alizoonyeshwa na
Nawal na akazielewa.
“Mimi sina kipingamizi
chochote katika suala
hilo.Kama umempenda Abu
Dahir unaweza kuolewa naye
hakuna tatizo” akasema
Mathew na ukimya ukapita
na mwanamke mmoja mnene
akaingia mle ndani na
kumjulisha Nawal kwamba
anahitajika katika chumba
cha marembo
“Abu Zalawi tutaonana
baadae.Nimefurahi kukuona”
akasema Nawal na kuondoka
akiwa na walinzi na
wasichana wawili wasaidizi
wake.Mathew akabaki peke
yake pale sebuleni
“Nimefurahi kuonana
tena na Nawal.Nilikuwa
naumiza kichwa ningempata
wapi kumbe naye alipelekwa
kuteswa.Nashukuru kwa
hatua hii tuliyofikia kwani
tuko karibu sana kuonana na
Habiba Jawad.Jambo lingine
la kufurahisha ni Nawal
kutakiwa kuolewa na Abu
Dahir mtoto wa Habiba
Jawad.Hili ni fanikio kubwa
kwani tutafahamu mambo
mengi kuhusiana na ufadhili
wa ugaidi duniani.Naomba
mipango hii iende kama
ilivyopangwa kusitokee
mambo yoyote yakavurugika
hapo kati kati na kama kila
kitu kikienda namna hii basi
Habiba Jawad siku zake
zinahesabika” akawaza
Mathew na mtu mmoja
akaingia mle sebuleni
akamtaka Mathew amfuate
akampeleka katika chumba
kimoja kizuri akamtaka
apumzike.
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Akiwa ameambatana na
Gosu Gosu.Melanie
alizungukia baadhi ya
makampuni aliyoyanunua
kutoka kwa Peniela yaliyo
chini ya MAPEN GROUP
akajitambulisha na
kufahamiana na
wafanyakazi.Mzunguko ule
uliwapeleka hadi saa kumi
za jioni ndipo Melanie
aliporejea nyumbani kwake
kupumzika.
“Makampuni yote
yanaendelea vizuri na
nimefurahi kukutana na
wafanyakazi hata hivyo akili
yangu mimi haipo katika
biashara.Kikubwa
kinachonila akili yangu hivi
sasa ni kulipiza kisasi”
Simu yake ikaita
akaichukua akatazama
alikuwa ni Devotha
“Hallow Devotha
“Melanie habari
yako?Habari za Dar es
salaam?
“Huku kwema
ninaendelea vizuri”
“Nashukuru kulifahamu
hilo.Melanie nimejulishwa na
Edwin kwamba umempiga
marufuku asikanyage hapo
kwako na vile vile umesema
hutaki tena timu maalum ya
walinzi waliowekwa
kukulinda.Hizi ni taarifa za
kweli?akauliza Devotha
“Ni kweli kabisa
Devotha.Nilifanya hivyo”
“Kwa nini
Melanie?Edwin ndiye
ambaye anasimamia kila
kitu kukuwezesha wewe
uweze kufanikisha mambo
yako kwa wepesi.Bila yeye
hautaweza kufanikiwa
katika kitu chochote.Kuhusu
ulinzi kwa nini hutaki tena
walinzi?akauliza Devotha
“Yule mtu wako hana
adabu hata
kidogo.Alithubutu kufungua
milango na kuingia ndani
wakati sipo.Kitendo kile
kilinikasirisha sana ndiyo
maana nikampiga marufuku
asiingie humu ndani kama
sipo.Hata yeye mwenyewe
alikiri kwamba alifanya kosa
na akaomba
msamaha.Kuhusu walinzi ni
kweli sihitaji walinzi kwa
sasa hadi hapo
nitakapomjulisha”
“Kwa nini Melanie?
“I can manage on my own
!
“Sikiliza Melanie walinzi
wale ni muhimu sana.Kwa
namna yoyote ile unahitaji
walinzi na wataendelea
kukulinda hata kama
hutaki”
“Devotha nimekwisha
sema sitaki ulinzi
wowote.Mmekwisha nipa
mlinzi mmoja Joyce inatosha
sana hao wengine sitaki
kuwasikia”
“Melanie nini
kimekutokea?Kwa nini
umebadilika namna
hii?akauliza Devotha
Melanie akawa kimya
“Nisikilize vizuri
Melanie.Mimi ndiye mkubwa
wako,ndiye kiongozi wako na
utafuata kile
ninachokuelekeza.Nakuonya
usithubutu kwenda nje ya
mstari utajuta.Utamsikiliza
Edwin ndiye atakayekuwa
akikuongoza.Chochote
atakachokuelekeza ufanye
bila kusita.Umenielewa
Melanie?akauliza Devotha
kwa ukali
“Devotha naomba na
mimi unisikilize.Mmenituma
kuja huku Tanzania kufanya
kazi zenu chafu.Mmenitumia
mimi kwa sababu mnajua
ninaweza hivyo basi kuanzia
sasa mtanisikiliza mimi kile
nikitakacho na operesheni hii
itafanyika vile nitakavyo
mimi.Sitaki kupangiwa au
kuamrishwa chochote.Nyote
kaeni kimya nisikilizeni
mimi.Mmenipa kazi ya
kufanya basi niacheni
nifanye kazi.Tumeelewana
Devotha? Akauliza Melanie
“Jambo lingine naomba
usithubutu tena kunitisha
Devotha” akasema Melanie
na kukata simu akaitupa
pembeni.
“This is my war,this is
my revenge and I’m going to
do it my way.Hakuna
atakayenieleza chochote.Si
Devotha wala nani.Wote
watakaa kimya waangalie
kile nitakachokifanya.Najua
maneno niliyomweleza
yatamuudhi sana Devotha na
hata Rais Michael lakini
potelea mbali kwani ni
wazazi wangu ndio
waliouawa hapa na lazima
niwalipie kisasi” akawaza
Melanie na kuichukua simu
yake nyingine iliyokuwa
inaita.Alikuwa ni GosuGosu
“Mfalme wangu”
akasema Melanie baada ya
kuipokea
“Melanie mpenzi wangu
habari za muda huu?
“Nzuri kabisa GosuGosu”
“Melanie kuna jambo
nataka tuzungumze hapa
nyumbani kama hutajali”
“Ninakuja hapo kwako
Gosu Gosu.Nisubiri
tafadhali” akasema Melanie
na kukata simu
“Ngoja niende kwa Gosu
Gosu nikasikie
alichoniitia.Lazima kitakuwa
ni kitu muhimu sana.Halafu
Devotha tayari amenitibua
na dawa yangu pekee
ninapotibuliwa ni kufanya
mapenzi” akawaza Melanie
na kumpigia simu Joyce
akamtaka ajiandae
waondoke
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 5: EPISODE 7
“Gosu Gosu nadhani
unafahamu utaratibu wangu
kila nikija hapa” akasema
Melanie baada ya kufika
nyumbani kwa Gosu
Gosu.Hakujibiwa kwa
maneno bali kwa
vitendo.Gosu Gosu ambaye
alikuwa na nguvu kama
tembo akamuinua Melanie
na kumuweka juu ya meza
ambayo huitumia kwa ajili
ya kusomea akiwa mle
chumbani,akamtoa nguo ya
ndani na mtanange ukaanzia
hapo.Mzunguko mmoja wa
haraka haraka ulimalizika
kisha wakahamia kitandani
kwa ajili ya mzunguko wa
pili.Kama kawaida kila
wakutanapo wawili hawa ni
Melanie ambaye huomba
apewe muda wa kupumzika.
“Daaah ! Gosu Gosu sijui
nikueleze nini lakini ninazidi
kukupenda zaidi na zaidi kila
uchao.Unanipa raha ya ajabu
mno unanifanya niyafurahie
maisha.Ahsante sana”
akasema Melanie baada ya
mzunguko wa pili kumalizika
“Nakupenda pia
Melanie.Unanipa furaha
kubwa katika maisha yangu”
akasema Gosu Gosu
“Haya nieleze kile
ambacho ulitaka kunieleza”
akasema Melanie
“Ulinipa kazi ya kutafuta
namna utakavyoweza
kukutana na James
Kasai.Sijafanikiwa
kuwasiliana naye yeye
mwenyewe bali nimefanikiwa
kumpata mtu mmoja
anaitwa Edie.Huyu ni rafiki
na James.Mimi na Edie
tunafahamiana tuliwahi
kushiriki wote katika vita ya
msituni.Kwa sasa yeye
anajishughulisha na
biashara ya
silaha.Nimemueleza nia
yangu ya kutaka kukutana
na James Kasai na ameahidi
kunisaidia”
“Good.Umemueleza
sababu za kutaka kuonana
na James Kasai?
“Hapana sijamueleza
chochote” akajibu Gosu Gosu
“Ni vipi tutaonana na
huyo Edie?Melanie akauliza
“Kesho tunakwenda
Uganda na tutakutana na
Edie ambaye atatupeleka
kwa James Kasai”
“Ahsante sana Gosu
Gosu.Nakushukuru kwa
kunisaidia”
“Usijali Melanie.Niko
tayari kufanya chochote kwa
ajili yako”akasema Gosu
Gosu na Melanie hakutaka
kupoteza muda kwa furaha
aliyokuwa nayo wakaingia
katika mzunguko mwingine
wa tatu
RIYADH –SAUDI ARABIA
Kiza kimekwisha ingia
pale mlango wa chumba
alimopumzika Mathew
ulipogongwa na jamaa
mmoja aliyevalia nadhifu
akamsalimu,kisha
akampatia nguo zilizokuwa
katika mfuko akamtaka
avae.Mathew akaufungua
mfuko ule na kukuta ndani
yake kuna kanzu nzuri
nyeupe akavaa kisha
akatoka na kuongozana na
Yule jamaa.Alipelekwa
katika ukumbi mkubwa
uliokuwa na meza kubwa ya
chakula iliyosheheni vyakula
vya aina mbali
mbali.Wahudumu waliovalia
nadhifu walikuwa
wamejipanga tayari
kuhudumia.Mathew
akakaribishwa mezani
akishangaa kwa uwingi ule
wa chakula.
Akiwa amekaa pale
mezani mara akatokea
Nawal akiwa ameongozana
na wanadada wawili
wakasalimiana na wakati
wakiendelea kuzungumza
likatokea kundi la watu kumi
hivi na meza
ikazungukwa.Katika watu
wale Mathew aliweza
kumtambua Sayid Omar.Bila
kupoteza muda Sayid Omar
akasimama
“Ndugu zangu
tuliokusanyika hapa,chakula
hiki jioni ya leo ni maalum
kabisa kwa ajili ya
kuwakaribisha ndugu zetu
wawili
waliotutembelea.Tunaye Abu
Zalawi” akasema Sayid huku
akitabasamu na
kumnyooshea mkono
Mathew akasimama huku
akitabasamu
“Abu Zalawi amekuwa
mstari wa mbele katika
mapambano ya kudai haki
na kupambana na wale
maadui zetu Israel na
washirika wake.Akiwa jijini
Nairobi aliweza kumuua
mkuu wa Mossad Afrika
mashariki pamoja ma
majasusi wengine wa
Mossad.Abu Zalawi
alikamatwa akafungwa
katika gereza kwa miaka
mitatu nchini Israel na huko
akakutana na shujaa Ammar
Nazari na kwa ushujaa
alifanikiwa kuandaa mpango
wa kutoroka gerezani na
kufanikiwa.Huyu ndiye
aliyemtorosha Ammar
Nazari gerezani.Baada ya
kutoka gerezani alijiunga na
Ammar Nazari brigades na
mlipuko uliotokea Jerusalem
katika kituo cha treni hivi
majuzi huyu ndiye
aliyetekeleza shambulio
lile.Abu Zalawi tuna furaha
kuwa nawe hapa.Karibu
jisikie nyumbani” akasema
Sayid Omar.
“Ahsante sana Sayid”
akasema Mathew
“Tunaye mgeni mwingine
pia.Huyu amekuwa nasi
hapa kwa siku mbili
sasa.Anaitwa Nawal.Huyu
alikuwa mke mdogo wa
Ammar Nazari hadi pale
majeshi ya Israel
yalipokatisha uhai wake”
akasema Sayid na Nawal
akatabasamu
“Wageni wetu karibuni
sana.Mimi naitwa Sayid
Omar ambaye tayari
mnanifahamu” akasema
Sayid na kufanya
utambulisho kwa watu
waliokuwepo mezani na
mwisho akamtambulisha
mtu muhimu
“Mwisho kabisa
ninamtambulisha kwenu
mtu muhimu sana ambaye
mmepitia safari ndefu
mkimtafuta.Habiba Jawad”
akasema Sayid Omar na
Habiba akanyoosha mkono
huku akitabasamu.Habiba
alikuwa na unene wa kadiri
na mweupe wa sura.Umri
wake japo ulionekana
mkubwa lakini bado sura
yake ilivutia kutokana na
kutunzwa vyema.Usiku huu
alivaa gauni zuri la rangi ya
kijani na kujitanda ushungi
mwepesi wa rangi ya
gauni.Masikioni alivaa
hereni za gharama
kubwa,vidole vyake vilijaa
pete za thamani.
Baada ya utambulisho
ule wakajumuika wote
kupata chakula kile kizuri
kilichoandaliwa kwa ajili ya
wageni wale wawili Mathew
na Nawal.Kisha maliza kula
Habiba akamuelekeza Sayid
awapeleke wageni katika
chumba cha mazungumzo
kisha naye akaenda
kuungana nao
“Abu Zalawi na Nawal
karibuni sana.Nimefurahi
kuwaoneni hapa” akaanzisha
mazungumzo Habiba
“Hata sisi tumefurahi
mama kukutana nawe”
akasema Mathew
“Poleni kwa yote
mliyopitia najua haikuwa
rahisi hadi mmefika hapa
lakini tunafanya vile ili
kujilinda.Mimi na wenzangu
tunasakwa sana na serikali
ya Israel na washirika wake
hivyo lazima tuchukue
tahadhari kubwa kwa mtu
yeyote anayetaka kuonana
nami.Najua Sayid Omar
amekwiha kueleza kila kitu
lakini nachukua nafasi hii
kwa mara nyingine tena
kukuthibitishia kwamba
hatuna tatizo nawe wala
Nawal.Yale yaliyofanyika ni
kwa mujibu wa taratbu
zetu.Tusameheni na
tuufungue ukurasa mpya
hivyo amani itawale”
akasema Habiba Jawad
“Tunashukuru sana
mama” akasema Mathew
“Mimi ndiye Habiba
Jawad ambaye mmekuwa
mkinisikia lakini leo hii mko
nami ana kwa ana” akasema
Habiba huku akitabasamu
halafu akamtazama Nawal
“Nawal,wewe nenda
kapumzike nitakuwa na
mazungumzo nawe kesho leo
nataka nizungumze kwanza
na Abu Zalawi” akasema
Habiba na Nawal akatoka
ndani ya kile chumba
akawaacha Mathew na
Habiba
“Abu Zalawi naomba
tufanye matembezi
kidogo.Mimi hupenda
kuwatembeza wageni katika
himaya yangu” akasema
Habiba kisha wakatoka
ndani ya kile chumba
wakatembea kuelekea katika
bustani nzuri.
“Vipi hali yako Abu
Zalawi”Habiba akauliza
“Ninajisikia vyema
mama Habiba.Maendeleo
yangu ni mazuri.Baada ya
kuonana nawe nahisi
majeraha yangu yote
yamepona” akajibu Mathew
kisha wakatembea kimya
kimya na kwenda kukaa
mahala ambako
kumetengenezwa maalum
kabisa kwa ajili ya
kupumzika.Habiba
akamtazama Mathew na
kusema
“Yapata miaka minne au
zaidi kidogo niliwahi kukaa
mahala hapa na binti mmoja
aliitwa Olivia Themba
akitokea Tanzania na leo hii
niko nawe tena Mathew
Mulumbi kutoka huko huko
Tanzania” akasema Habiba
huku akitabasamu lakini
Mathew alipatwa na mstuko
mkubwa sana kusikia
Habiba Jawad akilitamka
jina lake.Akahisi baridi ya
ghafla.
Mathew Mulumbi
alihisi tumbo likivurugika kwa
ndani akamtazama Habiba
Jawad kama mtu aliyeona
mzimu.Alitamani apae apotee
zake lakini
haikuwezekana.Habiba hakuwa
na wasiwasi alikuwa
anatabasamu
“Huku ndiko kuruga jivu
unakanyaka moto.Natamani
nigeuke upepo nipotee lakini
sina nguvu hiyo.Kama
ningekuwa na ugonjwa wa
moyo ningeanguka nakufa hapa
hapa kwa mstuko
nilioupata.Sikutegemea kabisa
kwa habiba kutamka jina
langu.Au labda
ananifananisha?Ngoja
nimjaribu” akawaza Mathew
akitazamana na Habiba
“Mama umekosea kutamka
jina langu.Mimi ni Abu Al Zalawi
na si Mathew Mulumbi kama
ulivyotamka” akasema Mathew
akijilazimisha
kutabasamu.Habiba
akatabasamu na kusema
“Relax son.Usiwe na
hofu.Hakuna kilichoharibika”
akasema Habiba Jawad kwa
sauti yake ya upole.Mathew
alibaki anamtazama Habiba
kwa hofu.Alikosa neno la
kusema
“Mathew Mulumbi huna
haja ya kuendelea kukana jina
lako kama ulivyofanya kwa
Abdel Fattah Sarraf wakati
anakufanyia mahojiano.Mimi
sikufanyii mahojiano kwani
ninakufahamu wewe ni nani na
kwa nini uko hapa.Taarifa zako
zote ninazo.Nina mtandao
mrefu sana katika nchi mbali
mbali duniani hivyo ninapata
taarifa nyingi.Nina watu wangu
Tanzania unakotoka,nina watu
wangu Israel ndani ya
Mossad,nina watu wangu ndani
ya CIA na mashirika mengine
makubwa ya ujasusi
duniani.Ninafahamu mipango
yao yote kuhusu mimi.Umewahi
kujuliza swali Israel pamoja na
ukubwa wa shirika lao la
ujasusi lakini mpaka leo hii
wameshindwa kunikamata kwa
nini? Yamebaki ni maneno tu
kwamba tunamsaka Habiba
Jawad lakini hawawezi
kunifikia.Umejiuliza pia
Marekani kwa kupitia shirika
lao la ujasusi CIA mpaka leo
wameshindwa kuwasaidia
Israel kufahamu mahala nilipo
kwa nini?Unadhani CIA hawajui
nilipo? Wanafahamu mahala
nilipo lakini hawawezi kuwapa
Israel taarifa zangu.Mimi ndiye
Habiba Jawad” akasema Habiba
na kutoa kicheko kidogo kisha
akamtazama Mathew
“Mathew ninakufahamu
wewe ni jasusi kutoka Tanzania
japo haufanyi tena kazi katika
shirika la ujasusi Tanzania
lakini umekuwa ukishirikishwa
katika operesheni mbali mbali
kubwa kubwa.Nafahamu hivi
sasa wewe ni mfanyabiashara
una mke anaishi Ufaransa
anaitwa Peniela na una watoto
wanne.Wawili ukiwa umezaa na
Peniela na wawili ukiwa
umezaa na mwanamke
mwingine lakini wote wako
Paris.Ukiwa Tanzania uliingia
katika mahusiano ya kimapenzi
na daktari Olivia Themba
ambaye kama nilivyokueleza
awali kwamba niliwahi kukaa
naye mahala hapa hapa
tukazungumza miaka kadhaa
iliyopita.Dr Olivia alikuwa ni
mpenzi wa Edger Kaka na
alitekwa na idara ya serikali ya
Tanzania baada ya kubainika
ana mawasiliano na watu wa IS
na hapo ndipo ulipojitokeza
wewe na sitaki kuelezea kile
kilichoendelea kwani
unafahamu kila kitu lakini
mwisho wa sakata lile ni pale
ambapo ulitekwa na vikosi vya
Israel wakati mkibadilishana
mateka.Tanzania mkiwahitaji
Olivia na mtoto wa Rais na IS
wakimuhitaji Edger
Kaka.Mabadilishano hayo ya
matea hayakufanikiwa kwani
mlivamiwa na wewe ukatekwa
pamoja na Edger kaka.Nadhani
tayari unafahamu kwamba
waliokuvamieni wakati wa
mabadilishano yale walikuwa ni
vikosi vya Israel lakini je
umejiuliza walipataje taarifa za
kufanyika kwa mabadilishano
yale?Nani aliwapa taarifa hizo?
Unataka kumfahamu?akauliza
Habiba na Mathew Mulumbi
akatikisa kichwa kukubaliana
na Habiba
“Nitakueleza siku nyingine
lakini kukamatwa kwako
ulikuwa ni mpango
maalum.Ulipelekwa Israel
ambako ulifungwa na kupatiwa
mateso mengi kwa miaka
mitatu na uliyavumilia mateso
hayo bila hata kutamka neno
lolote na ndipo Mossad
walipomtuma mtu wao ambaye
alianzisha mahusiano na mkeo
Peniela na wakakuonyesha
picha wawili hao wakifanya
mapenzi,lengo likiwa ni
kukuumiza.Walifanikiwa lengo
lao kwani ulikubali kushirikiana
nao na ndipo mlipoandaa
mpango kabambe wa kunitafuta
mahala nilipo.Ulijenga
mahusiano na Ammar Nazari
ukamtorosha gerezani na
ukajiunga na kundi
lake.Hakujua kama wewe
ulikuwa nipandikizi la
Israel.Ulijenga uaminifu
mkubwa kwa Ammar ili siku
moja aweze kukuleta kwangu
unipe taarifa za Edger Kaka
lakini lengo lako likiwa ni
kuniua kama ulivyotumwa na
Mossad.Niliwapa maelekezo
wakupe mateso kidogo
kukupima na kweli umeiva
katika ujasusi kwani pamoja na
kuteswa kote lakini uliendelea
kushikilia wewe ni Abu
Zalawi.Wengine wote waliamini
kwamba wewe ni Abu Zalawi
lakini mimi kwa kuwa tayari
ninakufahamu niliwaelekeza
wakulete moja kwa moja
kwangu hivyo karibu sana
jisikie nyumbani.Mimi ndiye
Habiba Jawad yule ambaye
uliweka kiapo cha kuhakikisha
unampata na kumuua” akasema
Habiba na kumtazama Mathew
aliyekuwa kimya
akimsikiliza.Alikuwa mpole
kama vile amemwagiwa barafu.
“Nawal aliyekuwa mke wa
Ammar naye ni pandikizi la
CIA.Aliolewa na Ammar lakini
alikuwa katika misheni maalum
ya kumtafuta gaidi mmoja
aliyeitwa Abdul Yasin Al Nasser
ambaye anatafutwa na
Marekani kwa kuhusika katika
matukio kadhaa ya milipuko ya
mabomu.Jana Abdul Yasin
amekamatwa na makachero wa
CIA.Unajua wamemkamata
vipi?Ni kwa sababu mimi ndiye
niliyetaka akamatwe.Nilimpa
Nawal taarifa za mahala alipo
Abdul,akawapa watu wake na
Abdul Yasin akakamatwa.Hivi
sasa tayari amekwisha fikishwa
Marekani.Kama nisingeamua
Abdul akamatwe
asingekamatwa.Nimekueleza
haya ili ujue Habiba Jawad ni
mtu wa namna gani.Nina nguvu
kubwa na si mtu ambaye
unaweza ukapanga kuniua
kirahisi rahisi namna hiyo”
akasema Habiba na kucheka
kidogo.
“Mathew Mulumbi mtandao
wote wa kigadi duniani uko
hapa katika kiganja changu
ninafahamu kila kitu kuhusu
ugaidi duniani kwa sababu wote
hawa mimi ndiye mfadhili
wao.Wote mimi ndiye mlezi
wao.Ninawasaidia kupata
silaha,fedha za kugharamia
operesheni zao na wakati
mwingine hadi fedha za
kujikimu.Mezani kwangu kuna
maandiko kutoka katika
makundi kadhaa yakihitaji
ufadhili katika operesheni zao”
akanyamaza kwa muda halafu
akaendelea.
“Edger kaka” akasema
Habiba Jawad kwa hisia kali na
kunyamaza kwa muda
“Jina lake halisi si Edger
Kaka.Jina lake halisi anaitwa
Seif Jawad”
“Seif Jawad?! Mathew
akashangaa
“Ndiyo.Anaitwa Seif
Jawad.Ngoja nikupe historia
kidogo Mathew Mulumbi”
akasema Habiba na kunyamaza
kidogo kwa sekunde chache
akasema
“Mimi asili yangu ni
Somalia lakini nilizaliwa na
kukulia nchini Kenya.Baada ya
kumaliza shule niliolewa na
tajiri mmoja aliitwa Nasser
jawad.Alikuwa ni tajiri mkubwa
sana pale Kenya.Mimi na Nasser
tulipata mtoto mmoja Seif
Jawad ambaye ninyi
mnamfahamu kama Edger
Kaka.Seif alipofikisha umri wa
miaka mitano tulimuhamishia
nchini Tanzania.Kuhamia kwa
Seif Tanzania kulikuwa na
sababu maalum.Niliichukia
Tanzania na nilitaka kulipiza
kisasi kwa kumtumia
Seif.Wazazi wangu waliokuwa
wakizunguka sehemu mbali
mbali Afrika Mashariki
wakifanya mihadhara ya kidini
waliuawa nchini Tanzania
wakidaiwa kwamba walikuwa
wanahamasisha ugaidi.Jambo
hili liliniumiza sana kwani
nawafahamu wazazi wangu
hawakuwa magaidi na
mihadhara aliyoifanya baba
haikuwa na mlengo wowote wa
chuki wala kuhimiza ugaidi.
Japo serikali ya Tanzania
walidai kwamba wazazi wangu
waliuawa na majambazi lakini
taarifa nilizozipata ulikuwa ni
mpango wa viongozi wa Afrika
mashariki kuwaua wakidai
kwamba walikuwa
wanahamasisha watu kujiunga
na vikundi vya kigaidi hivyo
nilimuingiza Seif Tanzania kwa
lengo la kumtumia katika
kulipiza kisasi.Toka akiwa
mdogo Seif alianza kuandaliwa
kuwa mwanasiasa na lengo kuu
ni siku moja aweze kushika
madaraka makubwa na
kuiongoza
Tanzania.Nilimkabidhi Seif kwa
familia ya watanzania
waliomlea na kumbadili jina
akaitwa Edger Kaka na
kutambuliwa kama
mtanzania.Watu hao walikuwa
wakiishi nchini Kenya na
walikuwa na mtoto wa kiume
mwenye umri sawa na Seif
lakini alifariki hivyo Seif
alitumia jina la huyo mtoto
ambaye alikuwa amefariki
nchini Kenya.Niliwarejesha
watuhao Tanzania na kuendelea
kugharamia maisha yao.Baba
yake Seif alifariki kwa ugonjwa
wa saratani nikaolewa na
mwanaume mwingine Abdul
Dahir.Huyu nilizaa naye mtoto
mmoja anaitwa Abu
Dahir.Abdul alikuwa mpalestina
na alikuwa tajiri sana.Alitumia
utajiri wake kufadhili makundi
mbali mbali ya wanamgambo
waliokuwa wakipambana na
serikali ya Israel wakidai haki
ya ardhi yao.Kwa bahati mbaya
Abdul naye alifariki dunia kwa
kuuawa na vikosi vya
Israel.Baada ya kifo cha Abdul
nilishika hatamu na kuendeleza
kile alichokuwa
anakifanya.Niliendelea kufadhili
makundi ya wanamgambo na
baadae nikaendelea kufuatwa
na makundi mengine ya kigaidi
sehemu mbali mbali duniani
wakiomba msaada nikalazimika
kuwasaidia na ndipo
nilipojikuta nikiwa mfadhili
mkubwa wa ugaidi duniani”
akanyamaza na kumtazama
Mathew
“Nchini Tanzania bado Seif
aliendelea kuandaliwa.Aliingia
katika siasa kwa kugombea
ubunge na akashinda.Baada ya
kuingia bungeni Seif au Edger
alianza kutengeneza jina kwa
kuibua kashfa mbalimbali za
ufisadi.Ulifanya uchunguzi
wako na unafahamu kila
kilichokuwa kinaendelea namna
alivyokuwa anapewa taarifa
mbalimbali za
mafisadi.Mtandao wote
unaufahamu” akasema Habiba
“Mathew Mulumbi kuna
mengi ya kukueleza lakini kwa
hayo machache naamini tayari
umepata picha kubwa kuhusu
mimi na harakati zangu.Narudia
tena kukukumbusha kwamba
nafahamu kwa nini uko
hapa,umetumwa na Israel uje
uchunguze na kuwapa taarifa
mahala nilipo au ikiwezekana
uniue.Nafahamu Ammar Nazari
hakuuawa na mabomu ya Israel
bali wewe na Nawal
mlimuua.Ninazo picha za
namna mlivyomuua ambazo
Nawal aliwatumia CIA” akasema
Habiba na Mathew akazidi
kuchoka.
“Lakini Mathew usiwe na
hofu yoyote.Ninayefahamu
kuhusu ninyi wawili kuwa ni
majasusi ni mimi peke
yangu.Hakuna yeyote kati ya
wasaidizi wangu anayefahamu
ninyi ni akina nani na
sintawaeleza chochote.Mimi ni
mama na ninyi ni kama watoto
wangu sitaki muuawe.Sitaki
mingie katika matatizo.Mateso
mliyoyapitia yametosha na
hapa mmekuja kupata
pumziko.Ninataka kuwasaidia
Mathew wewe na mwenzako
Nawal.Nataka kuwaondoa
katika maisha haya ya mateso
makubwa mnayoyapitia na
kuwaingiza katika maisha
mapya yaliyojaa amani na
furaha tele ndiyo maana
sijataka mtu wangu yoyote
afahamu kuhusu ninyi ni akina
nani” akanyamaza tena na
kumtazama Mathew
“Nawal amepitia mateso
makubwa kwa Ammar Nazari
na kama angejulikana
angeuawa.Wewe vile vile
umepitia mateso makali nchini
Israel kwa miaka mitatu.Nini
mnakipata katika mateso hayo
yote mnayoyapitia?Je nchi zenu
zinazowatuma mfanye
operesheni hizo za hatari
zinawapa thamani gani? Kwa
mambo uliyoyafanya nchini
kwako mtu kama wewe
ulitakiwa kupewa tuzo kubwa
ya heshima lakini hakuna
chochote unachokipata badala
yake maisha yako yamekuwa
kama ya ndege.Hivi sasa hakuna
anayesumbuka kukutafuta
wakiamini tayari umefariki
dunia.Hii si sawa hata kidogo
walipaswa kutumia kila aina ya
uwezo kukutafuta na
kukurejesha
nyumbani.Kikubwa
ninachotaka ukifahamu hapa ni
kwamba mambo unayoyafanya
ni makubwa lakini thamani
yako bado ni ndogo mno.Baada
ya kupitia hayo yote hatimaye
mmefika nyumbani.Hapa
ninawajali na
kuwathamini.Mlikuwa ni
maadui zangu lakini ninataka
kuwafanya kuwa watoto na
watu wangu wa karibu.Nataka
kubadili maisha yenu muishi
kwa amani na furaha” akasema
Habiba na kuendelea
kumtazama Mathew
“Nadhani tayari Nawal
amekwisha kueleza kwamba
mipango inaandaliwa ili aweze
kuolewa na mwanangu Abu
Dahir.Abu alipomuona Nawal
alitokea kumpenda na
akaniomba kama anaweza
akamuoa mimi sikuwa na
kipingamizi chochote na hapo
ndipo nilipopata wazo la
kuwatoa kuwa maadui zangu na
kuwafanya watoto
wangu.Kinachoendelea hivi sasa
ni taratibu za kidini zikamilike
ili Nawal na Abu waweze
kuoana.Najua wewe si
muislamu lakini unaufahamu
uislamu na unazifahamu
taratibu za kiislamu zilivyo kwa
mwanamke ambaye amefiwa na
mumewe kutaka kuolewa
tena.Nawal hana tatizo
amekubali kuolewa na hii ndiyo
sababu umemuona Nawal
amebadilika tofauti na
ulivyomfahamu alipokuwa kwa
Ammar Nazari.Naamini
utajiuliza siogopi kwamba
Nawal kuolewa na mwanangu
Abu Dahir nitakuwa nimejiweka
katika hatari zaidi kwamba
Nawal atapeleka taarifa zangu
CIA? La hasha siogopi chochote
na jambo hilo haliwezi katu
kutokea.Ninajiamini na kile
ninachokifanya” akasema
Habiba.Ulipita ukimya mfupi
halafu Habiba akaendelea
“Baada ya kifo cha Abdul
Dahir nilikuwa na mahusiano ya
kimapenzi na tajiri mmoja
lakini hatukufunga ndoa.Katika
mahusiano hayo tulifanikiwa
kupata mtoto mmoja wa kike
anaitwa Najma.Baba yake ni
Raia wa Iran na kwa muda
mrefu Najma alikuwa akiishi na
baba yake.Kwa sasa ni
daktari,amesomea nchini Urusi
na ninaishi naye hapa
Riyadh.Kwa bahati mbaya
hakuweza kujumuika nasi kwa
chakula cha usiku lakini utapata
nafasi ya kukutana naye.Kama
nilivyokueleza Mathew kwamba
ninataka kuwafanya wewe na
Nawal muwe watoto
wangu.Nataka nihitimishe
maisha yenu ya shida na
mahangaiko mliyoyapitia kwa
miaka mingi.Kama ilivyokuwa
kwa Nawal nataka nawe
Mathew Mulumbi umuoe
mwanangu Najma” akasema
Habiba na Mathew akahisi
kama nyundo imegonga kichwa
chake.Habiba akamtazama
Mathew na kutabasamu
“Nauona mstuko mkubwa
katika uso wako baada ya
kukueleza umuoe mwanangu
Najma.Kitu gani kimekustua
Mathew?akauliza
Habiba.Mathew akakohoa
kidogo na kusema
“Mama Habiba nimestuka
kwa kuwa hilo jambo
ulilolisema haliwezekani.Mimi
nina mke na watoto wanne na
siwezi tena kuoa mke
mwingine” akasema Mathew na
Habiba akatoa kicheko kidogo
“Hauna mke Mathew
Mulumbi,unaye mjane.Peniela si
mkeo tena.Huko aliko anaamini
tayari umekwisha fariki dunia
na ameamua kuendelea na
maisha yake.Labda nikupe siri
ya kitu ambacho
hukifahamu.Mali zako zote
zilizoko Dar es salaam tayari
zimeuzwa”
“Zimeuzwa?Mathew
akashangaa
“Ndiyo.Peniela ameuza mali
zote zilizoko
Tanzania.Unadhani kwa nini
ameamua kufanya hivyo?Ni
kwa sababu anajua hutarudi
tena,umekwisha kufa.Maisha
yako Tanzania yamekwisha
ndiyo maana nataka
kukuanzishia maisha mengine
hapa.Ningekuwa sina nia nzuri
kwako ningeweza kuelekeza
uuawe lakini sijafanya
hivyo.Sioni sababu yoyote ya
kukuangamiza Mathew
Mulumbi.Bado unayo nafasi ya
kuendelea kufurahia maisha
yako.Familia yako wamekwisha
kubaliana na ukweli kwamba
umeondoka na hautarudi tena
hivyo hakuna haja ya kwenda
kuwasumbua na kuvuruga
maisha waliyonayo sasa.Nakupa
nafasi ya kuanza maisha mapya
ukiwa na Najma.Ninao utajiri
mkubwa sana na utakuwa
mmoja wa watoto wangu
ambao nitawaingiza katika
orodha ya warithi wangu.Mali
zako zote ulizopoteza Tanzania
utazipata hapa hata mara kumi
zaidi” akasema Habiba na
Mathew akainamisha kichwa
“Mathew najua yote
niliyokueleza yamekustua
sana.Hukutegemea kama
ninafahamu wewe ni Mathew
Mulumbi,hukutegemea kama
ninafahamu mipango yako
yote.Umepatwa na mshangao
mkubwa sana kwa uliyoyasikia
lakini naamini ni kwa sababu
hukuwa ukimfahamu Habiba
Jawad ni nani.Habiba Jawad ni
zaidi ya mnavyoelezwa katika
mashirika yenu ya
kijasusi.Habiba Jawad
anaelezewa kijuu juu tu kwa
sababu hafahamiki lakini kwa
wanaomfahamu Habiba
wanamuogopa sana.Sitaki
kukuogopesha lakini nataka
umfahamu Habiba ni nani na
ukishamjua utajilaumu sana
kwa kupoteza muda wako
kumfuatila mtu ambaye
hapaswi kufuatiliwa.Tuyaweke
hayo pembeni nataka unieleze
kuhusu Edger Kaka.Ulisema
unafahamu mahala
alipo?akauliza Habiba.Mathew
akameza mate kuloanisha koo
kisha akasema
“Ndiyo ninafahamu mahala
alipo” akasema Mathew
“Nieleze ukweli kuhusu
Edger” akasema Habiba
“Kwanza kabisa naomba
ufahamu kwamba Edger
hakuwa anashikiliwa na serikali
ya Tanzania bali alikuwa
ametekwa na Israel na alikuwa
akishikiliwa katika ubalozi wao
jijini Nairobi.Mimi ndiye
niliyeongoza timu iliyovamia
ubalozi huo wa Israel jijini
Nairobi na kumchukua Edger
Kaka.Alikuwa amefungwa
katika chumba chenye giza
akipatiwa mateso makali.Edger
alikuwa katika hali mbaya
alikuwa amekonda na hakuwa
na uwezo hata wa
kutembea.Baada ya kumuokoa
tulimpeleka Dar es salaam
ambako ilitulazimu kufanya
mabadilishano na IS kwa ajili ya
kuwapata mtoto wa Rais
pamoja na Olivia Themba
ambao walikuwa wanashikiliwa
na IS.Niliongoza mabadilishano
hayo na katikati ya
mabadilishano ndipo
tukavamiwa na vikosi vya Israel
na mabadilishano
hayakufanyika tena.Mimi
nikachukuliwa mateka na Edger
pia akachukuliwa.Kwa bahati
mbaya wakati wa purukushani
zile Edger alianguka na
kugonga kichwa katika jiwe
kwa kuwa hakuwa na uwezo wa
kukimbia.Alipoteza fahamu na
toka wakati huo hajawahi
kuzinduka tena.Alipofikishwa
Israel hali yake ilizidi kuwa
mbaya na akalazimika
kuwekwa katika mashine ya
kumsaidia kuishi lakini kwa
taarifa ya daktari ni kwamba
ubongo wa Edger umekufa na
hakuna uwezekano wa
kuzinduka tena.Kwa ufupi ni
kwamba Edger amekwisha
fariki na kinachomuweka hai
hadi sasa ni mashine” akasema
Mathew na Habiba akainama
akafuta machozi.
“Mwanangu nilikuwa na
mipango naye mikubwa sana
lakini mipango yote
haijafanikiwa imeishia
njiani.Inaniuma sana” akasema
Habiba na kuendelea kufuta
machozi.
“Mathew nakuomba
ukaniletee mwanangu walau
niweze kumzika kwa heshima
zote.Naamini akiendelea kukaa
huko aliko watamfukia kama
mzoga kwa chuki walizonazo
kwetu.Naomba fanya kila lililo
ndani ya uwezo wako uniletee
mwili wa mwanangu.Nakuomba
sana” akasema Habiba
akiendelea kufuta machozi
“Sawa mama nitakuletea
mwili wa mwanao” akasema
Mathew
“Utafanyaje kuupata mwili
huo?akauliza Habiba
“Nitaondoka hapa na
kurejea Israel.Nitaonana na
wakuu wa Mossad nitawaeleza
kwamba nimewasiliana nawe
kwa simu na umenitaka
nikupelekee mwili wa
Edger.Nina uhakika mkubwa
watakubaliana nami na
watanipa mwili wa Edger”
“Mathew ninakutuma
nenda kaniletee mwili wa
mwanangu lakini ninakuonya
usijaribu kufanya jambo lolote
la kipuuzi kwani nitajua na
utakuwa umefanya jambo baya
sana”
“Mama usiwe na wasi wasi
nami.Nakutaka uniamini na
nitamrejesha Edger nyumbani”
akasema Mathew
“Mathew ahsante.Nini
utakihitaji katika zoezi hilo?
“Ninahitaji kufikishwa
katika mpaka wa Israel na
Jordan”
“Sawa.Nitakukabidhi kwa
Sayid Omar na atashughulikia
kila kitu” akasema Habiba na
kisha akainuka wakaondoka
wakarejea ndani akampigia
simu sayid Omar akafika mara
moja na kumchukua Mathew
wakaenda kupanga mipango ya
kwenda kuondoka kuelekea
Israel kuchukua mwili wa Edger
Kaka
MPENZI MSOMAJI TUKUTANE
SEHEMU IJAYO…………………
 
Maadui wanapatana kuwa marafiki... Mathew + Habiba
Shukrani mbududa ukipata nafasi weka muendelezo
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 5: EPISODE 7
“Gosu Gosu nadhani
unafahamu utaratibu wangu
kila nikija hapa” akasema
Melanie baada ya kufika
nyumbani kwa Gosu
Gosu.Hakujibiwa kwa
maneno bali kwa
vitendo.Gosu Gosu ambaye
alikuwa na nguvu kama
tembo akamuinua Melanie
na kumuweka juu ya meza
ambayo huitumia kwa ajili
ya kusomea akiwa mle
chumbani,akamtoa nguo ya
ndani na mtanange ukaanzia
hapo.Mzunguko mmoja wa
haraka haraka ulimalizika
kisha wakahamia kitandani
kwa ajili ya mzunguko wa
pili.Kama kawaida kila
wakutanapo wawili hawa ni
Melanie ambaye huomba
apewe muda wa kupumzika.
“Daaah ! Gosu Gosu sijui
nikueleze nini lakini ninazidi
kukupenda zaidi na zaidi kila
uchao.Unanipa raha ya ajabu
mno unanifanya niyafurahie
maisha.Ahsante sana”
akasema Melanie baada ya
mzunguko wa pili kumalizika
“Nakupenda pia
Melanie.Unanipa furaha
kubwa katika maisha yangu”
akasema Gosu Gosu
“Haya nieleze kile
ambacho ulitaka kunieleza”
akasema Melanie
“Ulinipa kazi ya kutafuta
namna utakavyoweza
kukutana na James
Kasai.Sijafanikiwa
kuwasiliana naye yeye
mwenyewe bali nimefanikiwa
kumpata mtu mmoja
anaitwa Edie.Huyu ni rafiki
na James.Mimi na Edie
tunafahamiana tuliwahi
kushiriki wote katika vita ya
msituni.Kwa sasa yeye
anajishughulisha na
biashara ya
silaha.Nimemueleza nia
yangu ya kutaka kukutana
na James Kasai na ameahidi
kunisaidia”
“Good.Umemueleza
sababu za kutaka kuonana
na James Kasai?
“Hapana sijamueleza
chochote” akajibu Gosu Gosu
“Ni vipi tutaonana na
huyo Edie?Melanie akauliza
“Kesho tunakwenda
Uganda na tutakutana na
Edie ambaye atatupeleka
kwa James Kasai”
“Ahsante sana Gosu
Gosu.Nakushukuru kwa
kunisaidia”
“Usijali Melanie.Niko
tayari kufanya chochote kwa
ajili yako”akasema Gosu
Gosu na Melanie hakutaka
kupoteza muda kwa furaha
aliyokuwa nayo wakaingia
katika mzunguko mwingine
wa tatu
RIYADH –SAUDI ARABIA
Kiza kimekwisha ingia
pale mlango wa chumba
alimopumzika Mathew
ulipogongwa na jamaa
mmoja aliyevalia nadhifu
akamsalimu,kisha
akampatia nguo zilizokuwa
katika mfuko akamtaka
avae.Mathew akaufungua
mfuko ule na kukuta ndani
yake kuna kanzu nzuri
nyeupe akavaa kisha
akatoka na kuongozana na
Yule jamaa.Alipelekwa
katika ukumbi mkubwa
uliokuwa na meza kubwa ya
chakula iliyosheheni vyakula
vya aina mbali
mbali.Wahudumu waliovalia
nadhifu walikuwa
wamejipanga tayari
kuhudumia.Mathew
akakaribishwa mezani
akishangaa kwa uwingi ule
wa chakula.
Akiwa amekaa pale
mezani mara akatokea
Nawal akiwa ameongozana
na wanadada wawili
wakasalimiana na wakati
wakiendelea kuzungumza
likatokea kundi la watu kumi
hivi na meza
ikazungukwa.Katika watu
wale Mathew aliweza
kumtambua Sayid Omar.Bila
kupoteza muda Sayid Omar
akasimama
“Ndugu zangu
tuliokusanyika hapa,chakula
hiki jioni ya leo ni maalum
kabisa kwa ajili ya
kuwakaribisha ndugu zetu
wawili
waliotutembelea.Tunaye Abu
Zalawi” akasema Sayid huku
akitabasamu na
kumnyooshea mkono
Mathew akasimama huku
akitabasamu
“Abu Zalawi amekuwa
mstari wa mbele katika
mapambano ya kudai haki
na kupambana na wale
maadui zetu Israel na
washirika wake.Akiwa jijini
Nairobi aliweza kumuua
mkuu wa Mossad Afrika
mashariki pamoja ma
majasusi wengine wa
Mossad.Abu Zalawi
alikamatwa akafungwa
katika gereza kwa miaka
mitatu nchini Israel na huko
akakutana na shujaa Ammar
Nazari na kwa ushujaa
alifanikiwa kuandaa mpango
wa kutoroka gerezani na
kufanikiwa.Huyu ndiye
aliyemtorosha Ammar
Nazari gerezani.Baada ya
kutoka gerezani alijiunga na
Ammar Nazari brigades na
mlipuko uliotokea Jerusalem
katika kituo cha treni hivi
majuzi huyu ndiye
aliyetekeleza shambulio
lile.Abu Zalawi tuna furaha
kuwa nawe hapa.Karibu
jisikie nyumbani” akasema
Sayid Omar.
“Ahsante sana Sayid”
akasema Mathew
“Tunaye mgeni mwingine
pia.Huyu amekuwa nasi
hapa kwa siku mbili
sasa.Anaitwa Nawal.Huyu
alikuwa mke mdogo wa
Ammar Nazari hadi pale
majeshi ya Israel
yalipokatisha uhai wake”
akasema Sayid na Nawal
akatabasamu
“Wageni wetu karibuni
sana.Mimi naitwa Sayid
Omar ambaye tayari
mnanifahamu” akasema
Sayid na kufanya
utambulisho kwa watu
waliokuwepo mezani na
mwisho akamtambulisha
mtu muhimu
“Mwisho kabisa
ninamtambulisha kwenu
mtu muhimu sana ambaye
mmepitia safari ndefu
mkimtafuta.Habiba Jawad”
akasema Sayid Omar na
Habiba akanyoosha mkono
huku akitabasamu.Habiba
alikuwa na unene wa kadiri
na mweupe wa sura.Umri
wake japo ulionekana
mkubwa lakini bado sura
yake ilivutia kutokana na
kutunzwa vyema.Usiku huu
alivaa gauni zuri la rangi ya
kijani na kujitanda ushungi
mwepesi wa rangi ya
gauni.Masikioni alivaa
hereni za gharama
kubwa,vidole vyake vilijaa
pete za thamani.
Baada ya utambulisho
ule wakajumuika wote
kupata chakula kile kizuri
kilichoandaliwa kwa ajili ya
wageni wale wawili Mathew
na Nawal.Kisha maliza kula
Habiba akamuelekeza Sayid
awapeleke wageni katika
chumba cha mazungumzo
kisha naye akaenda
kuungana nao
“Abu Zalawi na Nawal
karibuni sana.Nimefurahi
kuwaoneni hapa” akaanzisha
mazungumzo Habiba
“Hata sisi tumefurahi
mama kukutana nawe”
akasema Mathew
“Poleni kwa yote
mliyopitia najua haikuwa
rahisi hadi mmefika hapa
lakini tunafanya vile ili
kujilinda.Mimi na wenzangu
tunasakwa sana na serikali
ya Israel na washirika wake
hivyo lazima tuchukue
tahadhari kubwa kwa mtu
yeyote anayetaka kuonana
nami.Najua Sayid Omar
amekwiha kueleza kila kitu
lakini nachukua nafasi hii
kwa mara nyingine tena
kukuthibitishia kwamba
hatuna tatizo nawe wala
Nawal.Yale yaliyofanyika ni
kwa mujibu wa taratbu
zetu.Tusameheni na
tuufungue ukurasa mpya
hivyo amani itawale”
akasema Habiba Jawad
“Tunashukuru sana
mama” akasema Mathew
“Mimi ndiye Habiba
Jawad ambaye mmekuwa
mkinisikia lakini leo hii mko
nami ana kwa ana” akasema
Habiba huku akitabasamu
halafu akamtazama Nawal
“Nawal,wewe nenda
kapumzike nitakuwa na
mazungumzo nawe kesho leo
nataka nizungumze kwanza
na Abu Zalawi” akasema
Habiba na Nawal akatoka
ndani ya kile chumba
akawaacha Mathew na
Habiba
“Abu Zalawi naomba
tufanye matembezi
kidogo.Mimi hupenda
kuwatembeza wageni katika
himaya yangu” akasema
Habiba kisha wakatoka
ndani ya kile chumba
wakatembea kuelekea katika
bustani nzuri.
“Vipi hali yako Abu
Zalawi”Habiba akauliza
“Ninajisikia vyema
mama Habiba.Maendeleo
yangu ni mazuri.Baada ya
kuonana nawe nahisi
majeraha yangu yote
yamepona” akajibu Mathew
kisha wakatembea kimya
kimya na kwenda kukaa
mahala ambako
kumetengenezwa maalum
kabisa kwa ajili ya
kupumzika.Habiba
akamtazama Mathew na
kusema
“Yapata miaka minne au
zaidi kidogo niliwahi kukaa
mahala hapa na binti mmoja
aliitwa Olivia Themba
akitokea Tanzania na leo hii
niko nawe tena Mathew
Mulumbi kutoka huko huko
Tanzania” akasema Habiba
huku akitabasamu lakini
Mathew alipatwa na mstuko
mkubwa sana kusikia
Habiba Jawad akilitamka
jina lake.Akahisi baridi ya
ghafla.
Mathew Mulumbi
alihisi tumbo likivurugika kwa
ndani akamtazama Habiba
Jawad kama mtu aliyeona
mzimu.Alitamani apae apotee
zake lakini
haikuwezekana.Habiba hakuwa
na wasiwasi alikuwa
anatabasamu
“Huku ndiko kuruga jivu
unakanyaka moto.Natamani
nigeuke upepo nipotee lakini
sina nguvu hiyo.Kama
ningekuwa na ugonjwa wa
moyo ningeanguka nakufa hapa
hapa kwa mstuko
nilioupata.Sikutegemea kabisa
kwa habiba kutamka jina
langu.Au labda
ananifananisha?Ngoja
nimjaribu” akawaza Mathew
akitazamana na Habiba
“Mama umekosea kutamka
jina langu.Mimi ni Abu Al Zalawi
na si Mathew Mulumbi kama
ulivyotamka” akasema Mathew
akijilazimisha
kutabasamu.Habiba
akatabasamu na kusema
“Relax son.Usiwe na
hofu.Hakuna kilichoharibika”
akasema Habiba Jawad kwa
sauti yake ya upole.Mathew
alibaki anamtazama Habiba
kwa hofu.Alikosa neno la
kusema
“Mathew Mulumbi huna
haja ya kuendelea kukana jina
lako kama ulivyofanya kwa
Abdel Fattah Sarraf wakati
anakufanyia mahojiano.Mimi
sikufanyii mahojiano kwani
ninakufahamu wewe ni nani na
kwa nini uko hapa.Taarifa zako
zote ninazo.Nina mtandao
mrefu sana katika nchi mbali
mbali duniani hivyo ninapata
taarifa nyingi.Nina watu wangu
Tanzania unakotoka,nina watu
wangu Israel ndani ya
Mossad,nina watu wangu ndani
ya CIA na mashirika mengine
makubwa ya ujasusi
duniani.Ninafahamu mipango
yao yote kuhusu mimi.Umewahi
kujuliza swali Israel pamoja na
ukubwa wa shirika lao la
ujasusi lakini mpaka leo hii
wameshindwa kunikamata kwa
nini? Yamebaki ni maneno tu
kwamba tunamsaka Habiba
Jawad lakini hawawezi
kunifikia.Umejiuliza pia
Marekani kwa kupitia shirika
lao la ujasusi CIA mpaka leo
wameshindwa kuwasaidia
Israel kufahamu mahala nilipo
kwa nini?Unadhani CIA hawajui
nilipo? Wanafahamu mahala
nilipo lakini hawawezi kuwapa
Israel taarifa zangu.Mimi ndiye
Habiba Jawad” akasema Habiba
na kutoa kicheko kidogo kisha
akamtazama Mathew
“Mathew ninakufahamu
wewe ni jasusi kutoka Tanzania
japo haufanyi tena kazi katika
shirika la ujasusi Tanzania
lakini umekuwa ukishirikishwa
katika operesheni mbali mbali
kubwa kubwa.Nafahamu hivi
sasa wewe ni mfanyabiashara
una mke anaishi Ufaransa
anaitwa Peniela na una watoto
wanne.Wawili ukiwa umezaa na
Peniela na wawili ukiwa
umezaa na mwanamke
mwingine lakini wote wako
Paris.Ukiwa Tanzania uliingia
katika mahusiano ya kimapenzi
na daktari Olivia Themba
ambaye kama nilivyokueleza
awali kwamba niliwahi kukaa
naye mahala hapa hapa
tukazungumza miaka kadhaa
iliyopita.Dr Olivia alikuwa ni
mpenzi wa Edger Kaka na
alitekwa na idara ya serikali ya
Tanzania baada ya kubainika
ana mawasiliano na watu wa IS
na hapo ndipo ulipojitokeza
wewe na sitaki kuelezea kile
kilichoendelea kwani
unafahamu kila kitu lakini
mwisho wa sakata lile ni pale
ambapo ulitekwa na vikosi vya
Israel wakati mkibadilishana
mateka.Tanzania mkiwahitaji
Olivia na mtoto wa Rais na IS
wakimuhitaji Edger
Kaka.Mabadilishano hayo ya
matea hayakufanikiwa kwani
mlivamiwa na wewe ukatekwa
pamoja na Edger kaka.Nadhani
tayari unafahamu kwamba
waliokuvamieni wakati wa
mabadilishano yale walikuwa ni
vikosi vya Israel lakini je
umejiuliza walipataje taarifa za
kufanyika kwa mabadilishano
yale?Nani aliwapa taarifa hizo?
Unataka kumfahamu?akauliza
Habiba na Mathew Mulumbi
akatikisa kichwa kukubaliana
na Habiba
“Nitakueleza siku nyingine
lakini kukamatwa kwako
ulikuwa ni mpango
maalum.Ulipelekwa Israel
ambako ulifungwa na kupatiwa
mateso mengi kwa miaka
mitatu na uliyavumilia mateso
hayo bila hata kutamka neno
lolote na ndipo Mossad
walipomtuma mtu wao ambaye
alianzisha mahusiano na mkeo
Peniela na wakakuonyesha
picha wawili hao wakifanya
mapenzi,lengo likiwa ni
kukuumiza.Walifanikiwa lengo
lao kwani ulikubali kushirikiana
nao na ndipo mlipoandaa
mpango kabambe wa kunitafuta
mahala nilipo.Ulijenga
mahusiano na Ammar Nazari
ukamtorosha gerezani na
ukajiunga na kundi
lake.Hakujua kama wewe
ulikuwa nipandikizi la
Israel.Ulijenga uaminifu
mkubwa kwa Ammar ili siku
moja aweze kukuleta kwangu
unipe taarifa za Edger Kaka
lakini lengo lako likiwa ni
kuniua kama ulivyotumwa na
Mossad.Niliwapa maelekezo
wakupe mateso kidogo
kukupima na kweli umeiva
katika ujasusi kwani pamoja na
kuteswa kote lakini uliendelea
kushikilia wewe ni Abu
Zalawi.Wengine wote waliamini
kwamba wewe ni Abu Zalawi
lakini mimi kwa kuwa tayari
ninakufahamu niliwaelekeza
wakulete moja kwa moja
kwangu hivyo karibu sana
jisikie nyumbani.Mimi ndiye
Habiba Jawad yule ambaye
uliweka kiapo cha kuhakikisha
unampata na kumuua” akasema
Habiba na kumtazama Mathew
aliyekuwa kimya
akimsikiliza.Alikuwa mpole
kama vile amemwagiwa barafu.
“Nawal aliyekuwa mke wa
Ammar naye ni pandikizi la
CIA.Aliolewa na Ammar lakini
alikuwa katika misheni maalum
ya kumtafuta gaidi mmoja
aliyeitwa Abdul Yasin Al Nasser
ambaye anatafutwa na
Marekani kwa kuhusika katika
matukio kadhaa ya milipuko ya
mabomu.Jana Abdul Yasin
amekamatwa na makachero wa
CIA.Unajua wamemkamata
vipi?Ni kwa sababu mimi ndiye
niliyetaka akamatwe.Nilimpa
Nawal taarifa za mahala alipo
Abdul,akawapa watu wake na
Abdul Yasin akakamatwa.Hivi
sasa tayari amekwisha fikishwa
Marekani.Kama nisingeamua
Abdul akamatwe
asingekamatwa.Nimekueleza
haya ili ujue Habiba Jawad ni
mtu wa namna gani.Nina nguvu
kubwa na si mtu ambaye
unaweza ukapanga kuniua
kirahisi rahisi namna hiyo”
akasema Habiba na kucheka
kidogo.
“Mathew Mulumbi mtandao
wote wa kigadi duniani uko
hapa katika kiganja changu
ninafahamu kila kitu kuhusu
ugaidi duniani kwa sababu wote
hawa mimi ndiye mfadhili
wao.Wote mimi ndiye mlezi
wao.Ninawasaidia kupata
silaha,fedha za kugharamia
operesheni zao na wakati
mwingine hadi fedha za
kujikimu.Mezani kwangu kuna
maandiko kutoka katika
makundi kadhaa yakihitaji
ufadhili katika operesheni zao”
akanyamaza kwa muda halafu
akaendelea.
“Edger kaka” akasema
Habiba Jawad kwa hisia kali na
kunyamaza kwa muda
“Jina lake halisi si Edger
Kaka.Jina lake halisi anaitwa
Seif Jawad”
“Seif Jawad?! Mathew
akashangaa
“Ndiyo.Anaitwa Seif
Jawad.Ngoja nikupe historia
kidogo Mathew Mulumbi”
akasema Habiba na kunyamaza
kidogo kwa sekunde chache
akasema
“Mimi asili yangu ni
Somalia lakini nilizaliwa na
kukulia nchini Kenya.Baada ya
kumaliza shule niliolewa na
tajiri mmoja aliitwa Nasser
jawad.Alikuwa ni tajiri mkubwa
sana pale Kenya.Mimi na Nasser
tulipata mtoto mmoja Seif
Jawad ambaye ninyi
mnamfahamu kama Edger
Kaka.Seif alipofikisha umri wa
miaka mitano tulimuhamishia
nchini Tanzania.Kuhamia kwa
Seif Tanzania kulikuwa na
sababu maalum.Niliichukia
Tanzania na nilitaka kulipiza
kisasi kwa kumtumia
Seif.Wazazi wangu waliokuwa
wakizunguka sehemu mbali
mbali Afrika Mashariki
wakifanya mihadhara ya kidini
waliuawa nchini Tanzania
wakidaiwa kwamba walikuwa
wanahamasisha ugaidi.Jambo
hili liliniumiza sana kwani
nawafahamu wazazi wangu
hawakuwa magaidi na
mihadhara aliyoifanya baba
haikuwa na mlengo wowote wa
chuki wala kuhimiza ugaidi.
Japo serikali ya Tanzania
walidai kwamba wazazi wangu
waliuawa na majambazi lakini
taarifa nilizozipata ulikuwa ni
mpango wa viongozi wa Afrika
mashariki kuwaua wakidai
kwamba walikuwa
wanahamasisha watu kujiunga
na vikundi vya kigaidi hivyo
nilimuingiza Seif Tanzania kwa
lengo la kumtumia katika
kulipiza kisasi.Toka akiwa
mdogo Seif alianza kuandaliwa
kuwa mwanasiasa na lengo kuu
ni siku moja aweze kushika
madaraka makubwa na
kuiongoza
Tanzania.Nilimkabidhi Seif kwa
familia ya watanzania
waliomlea na kumbadili jina
akaitwa Edger Kaka na
kutambuliwa kama
mtanzania.Watu hao walikuwa
wakiishi nchini Kenya na
walikuwa na mtoto wa kiume
mwenye umri sawa na Seif
lakini alifariki hivyo Seif
alitumia jina la huyo mtoto
ambaye alikuwa amefariki
nchini Kenya.Niliwarejesha
watuhao Tanzania na kuendelea
kugharamia maisha yao.Baba
yake Seif alifariki kwa ugonjwa
wa saratani nikaolewa na
mwanaume mwingine Abdul
Dahir.Huyu nilizaa naye mtoto
mmoja anaitwa Abu
Dahir.Abdul alikuwa mpalestina
na alikuwa tajiri sana.Alitumia
utajiri wake kufadhili makundi
mbali mbali ya wanamgambo
waliokuwa wakipambana na
serikali ya Israel wakidai haki
ya ardhi yao.Kwa bahati mbaya
Abdul naye alifariki dunia kwa
kuuawa na vikosi vya
Israel.Baada ya kifo cha Abdul
nilishika hatamu na kuendeleza
kile alichokuwa
anakifanya.Niliendelea kufadhili
makundi ya wanamgambo na
baadae nikaendelea kufuatwa
na makundi mengine ya kigaidi
sehemu mbali mbali duniani
wakiomba msaada nikalazimika
kuwasaidia na ndipo
nilipojikuta nikiwa mfadhili
mkubwa wa ugaidi duniani”
akanyamaza na kumtazama
Mathew
“Nchini Tanzania bado Seif
aliendelea kuandaliwa.Aliingia
katika siasa kwa kugombea
ubunge na akashinda.Baada ya
kuingia bungeni Seif au Edger
alianza kutengeneza jina kwa
kuibua kashfa mbalimbali za
ufisadi.Ulifanya uchunguzi
wako na unafahamu kila
kilichokuwa kinaendelea namna
alivyokuwa anapewa taarifa
mbalimbali za
mafisadi.Mtandao wote
unaufahamu” akasema Habiba
“Mathew Mulumbi kuna
mengi ya kukueleza lakini kwa
hayo machache naamini tayari
umepata picha kubwa kuhusu
mimi na harakati zangu.Narudia
tena kukukumbusha kwamba
nafahamu kwa nini uko
hapa,umetumwa na Israel uje
uchunguze na kuwapa taarifa
mahala nilipo au ikiwezekana
uniue.Nafahamu Ammar Nazari
hakuuawa na mabomu ya Israel
bali wewe na Nawal
mlimuua.Ninazo picha za
namna mlivyomuua ambazo
Nawal aliwatumia CIA” akasema
Habiba na Mathew akazidi
kuchoka.
“Lakini Mathew usiwe na
hofu yoyote.Ninayefahamu
kuhusu ninyi wawili kuwa ni
majasusi ni mimi peke
yangu.Hakuna yeyote kati ya
wasaidizi wangu anayefahamu
ninyi ni akina nani na
sintawaeleza chochote.Mimi ni
mama na ninyi ni kama watoto
wangu sitaki muuawe.Sitaki
mingie katika matatizo.Mateso
mliyoyapitia yametosha na
hapa mmekuja kupata
pumziko.Ninataka kuwasaidia
Mathew wewe na mwenzako
Nawal.Nataka kuwaondoa
katika maisha haya ya mateso
makubwa mnayoyapitia na
kuwaingiza katika maisha
mapya yaliyojaa amani na
furaha tele ndiyo maana
sijataka mtu wangu yoyote
afahamu kuhusu ninyi ni akina
nani” akanyamaza tena na
kumtazama Mathew
“Nawal amepitia mateso
makubwa kwa Ammar Nazari
na kama angejulikana
angeuawa.Wewe vile vile
umepitia mateso makali nchini
Israel kwa miaka mitatu.Nini
mnakipata katika mateso hayo
yote mnayoyapitia?Je nchi zenu
zinazowatuma mfanye
operesheni hizo za hatari
zinawapa thamani gani? Kwa
mambo uliyoyafanya nchini
kwako mtu kama wewe
ulitakiwa kupewa tuzo kubwa
ya heshima lakini hakuna
chochote unachokipata badala
yake maisha yako yamekuwa
kama ya ndege.Hivi sasa hakuna
anayesumbuka kukutafuta
wakiamini tayari umefariki
dunia.Hii si sawa hata kidogo
walipaswa kutumia kila aina ya
uwezo kukutafuta na
kukurejesha
nyumbani.Kikubwa
ninachotaka ukifahamu hapa ni
kwamba mambo unayoyafanya
ni makubwa lakini thamani
yako bado ni ndogo mno.Baada
ya kupitia hayo yote hatimaye
mmefika nyumbani.Hapa
ninawajali na
kuwathamini.Mlikuwa ni
maadui zangu lakini ninataka
kuwafanya kuwa watoto na
watu wangu wa karibu.Nataka
kubadili maisha yenu muishi
kwa amani na furaha” akasema
Habiba na kuendelea
kumtazama Mathew
“Nadhani tayari Nawal
amekwisha kueleza kwamba
mipango inaandaliwa ili aweze
kuolewa na mwanangu Abu
Dahir.Abu alipomuona Nawal
alitokea kumpenda na
akaniomba kama anaweza
akamuoa mimi sikuwa na
kipingamizi chochote na hapo
ndipo nilipopata wazo la
kuwatoa kuwa maadui zangu na
kuwafanya watoto
wangu.Kinachoendelea hivi sasa
ni taratibu za kidini zikamilike
ili Nawal na Abu waweze
kuoana.Najua wewe si
muislamu lakini unaufahamu
uislamu na unazifahamu
taratibu za kiislamu zilivyo kwa
mwanamke ambaye amefiwa na
mumewe kutaka kuolewa
tena.Nawal hana tatizo
amekubali kuolewa na hii ndiyo
sababu umemuona Nawal
amebadilika tofauti na
ulivyomfahamu alipokuwa kwa
Ammar Nazari.Naamini
utajiuliza siogopi kwamba
Nawal kuolewa na mwanangu
Abu Dahir nitakuwa nimejiweka
katika hatari zaidi kwamba
Nawal atapeleka taarifa zangu
CIA? La hasha siogopi chochote
na jambo hilo haliwezi katu
kutokea.Ninajiamini na kile
ninachokifanya” akasema
Habiba.Ulipita ukimya mfupi
halafu Habiba akaendelea
“Baada ya kifo cha Abdul
Dahir nilikuwa na mahusiano ya
kimapenzi na tajiri mmoja
lakini hatukufunga ndoa.Katika
mahusiano hayo tulifanikiwa
kupata mtoto mmoja wa kike
anaitwa Najma.Baba yake ni
Raia wa Iran na kwa muda
mrefu Najma alikuwa akiishi na
baba yake.Kwa sasa ni
daktari,amesomea nchini Urusi
na ninaishi naye hapa
Riyadh.Kwa bahati mbaya
hakuweza kujumuika nasi kwa
chakula cha usiku lakini utapata
nafasi ya kukutana naye.Kama
nilivyokueleza Mathew kwamba
ninataka kuwafanya wewe na
Nawal muwe watoto
wangu.Nataka nihitimishe
maisha yenu ya shida na
mahangaiko mliyoyapitia kwa
miaka mingi.Kama ilivyokuwa
kwa Nawal nataka nawe
Mathew Mulumbi umuoe
mwanangu Najma” akasema
Habiba na Mathew akahisi
kama nyundo imegonga kichwa
chake.Habiba akamtazama
Mathew na kutabasamu
“Nauona mstuko mkubwa
katika uso wako baada ya
kukueleza umuoe mwanangu
Najma.Kitu gani kimekustua
Mathew?akauliza
Habiba.Mathew akakohoa
kidogo na kusema
“Mama Habiba nimestuka
kwa kuwa hilo jambo
ulilolisema haliwezekani.Mimi
nina mke na watoto wanne na
siwezi tena kuoa mke
mwingine” akasema Mathew na
Habiba akatoa kicheko kidogo
“Hauna mke Mathew
Mulumbi,unaye mjane.Peniela si
mkeo tena.Huko aliko anaamini
tayari umekwisha fariki dunia
na ameamua kuendelea na
maisha yake.Labda nikupe siri
ya kitu ambacho
hukifahamu.Mali zako zote
zilizoko Dar es salaam tayari
zimeuzwa”
“Zimeuzwa?Mathew
akashangaa
“Ndiyo.Peniela ameuza mali
zote zilizoko
Tanzania.Unadhani kwa nini
ameamua kufanya hivyo?Ni
kwa sababu anajua hutarudi
tena,umekwisha kufa.Maisha
yako Tanzania yamekwisha
ndiyo maana nataka
kukuanzishia maisha mengine
hapa.Ningekuwa sina nia nzuri
kwako ningeweza kuelekeza
uuawe lakini sijafanya
hivyo.Sioni sababu yoyote ya
kukuangamiza Mathew
Mulumbi.Bado unayo nafasi ya
kuendelea kufurahia maisha
yako.Familia yako wamekwisha
kubaliana na ukweli kwamba
umeondoka na hautarudi tena
hivyo hakuna haja ya kwenda
kuwasumbua na kuvuruga
maisha waliyonayo sasa.Nakupa
nafasi ya kuanza maisha mapya
ukiwa na Najma.Ninao utajiri
mkubwa sana na utakuwa
mmoja wa watoto wangu
ambao nitawaingiza katika
orodha ya warithi wangu.Mali
zako zote ulizopoteza Tanzania
utazipata hapa hata mara kumi
zaidi” akasema Habiba na
Mathew akainamisha kichwa
“Mathew najua yote
niliyokueleza yamekustua
sana.Hukutegemea kama
ninafahamu wewe ni Mathew
Mulumbi,hukutegemea kama
ninafahamu mipango yako
yote.Umepatwa na mshangao
mkubwa sana kwa uliyoyasikia
lakini naamini ni kwa sababu
hukuwa ukimfahamu Habiba
Jawad ni nani.Habiba Jawad ni
zaidi ya mnavyoelezwa katika
mashirika yenu ya
kijasusi.Habiba Jawad
anaelezewa kijuu juu tu kwa
sababu hafahamiki lakini kwa
wanaomfahamu Habiba
wanamuogopa sana.Sitaki
kukuogopesha lakini nataka
umfahamu Habiba ni nani na
ukishamjua utajilaumu sana
kwa kupoteza muda wako
kumfuatila mtu ambaye
hapaswi kufuatiliwa.Tuyaweke
hayo pembeni nataka unieleze
kuhusu Edger Kaka.Ulisema
unafahamu mahala
alipo?akauliza Habiba.Mathew
akameza mate kuloanisha koo
kisha akasema
“Ndiyo ninafahamu mahala
alipo” akasema Mathew
“Nieleze ukweli kuhusu
Edger” akasema Habiba
“Kwanza kabisa naomba
ufahamu kwamba Edger
hakuwa anashikiliwa na serikali
ya Tanzania bali alikuwa
ametekwa na Israel na alikuwa
akishikiliwa katika ubalozi wao
jijini Nairobi.Mimi ndiye
niliyeongoza timu iliyovamia
ubalozi huo wa Israel jijini
Nairobi na kumchukua Edger
Kaka.Alikuwa amefungwa
katika chumba chenye giza
akipatiwa mateso makali.Edger
alikuwa katika hali mbaya
alikuwa amekonda na hakuwa
na uwezo hata wa
kutembea.Baada ya kumuokoa
tulimpeleka Dar es salaam
ambako ilitulazimu kufanya
mabadilishano na IS kwa ajili ya
kuwapata mtoto wa Rais
pamoja na Olivia Themba
ambao walikuwa wanashikiliwa
na IS.Niliongoza mabadilishano
hayo na katikati ya
mabadilishano ndipo
tukavamiwa na vikosi vya Israel
na mabadilishano
hayakufanyika tena.Mimi
nikachukuliwa mateka na Edger
pia akachukuliwa.Kwa bahati
mbaya wakati wa purukushani
zile Edger alianguka na
kugonga kichwa katika jiwe
kwa kuwa hakuwa na uwezo wa
kukimbia.Alipoteza fahamu na
toka wakati huo hajawahi
kuzinduka tena.Alipofikishwa
Israel hali yake ilizidi kuwa
mbaya na akalazimika
kuwekwa katika mashine ya
kumsaidia kuishi lakini kwa
taarifa ya daktari ni kwamba
ubongo wa Edger umekufa na
hakuna uwezekano wa
kuzinduka tena.Kwa ufupi ni
kwamba Edger amekwisha
fariki na kinachomuweka hai
hadi sasa ni mashine” akasema
Mathew na Habiba akainama
akafuta machozi.
“Mwanangu nilikuwa na
mipango naye mikubwa sana
lakini mipango yote
haijafanikiwa imeishia
njiani.Inaniuma sana” akasema
Habiba na kuendelea kufuta
machozi.
“Mathew nakuomba
ukaniletee mwanangu walau
niweze kumzika kwa heshima
zote.Naamini akiendelea kukaa
huko aliko watamfukia kama
mzoga kwa chuki walizonazo
kwetu.Naomba fanya kila lililo
ndani ya uwezo wako uniletee
mwili wa mwanangu.Nakuomba
sana” akasema Habiba
akiendelea kufuta machozi
“Sawa mama nitakuletea
mwili wa mwanao” akasema
Mathew
“Utafanyaje kuupata mwili
huo?akauliza Habiba
“Nitaondoka hapa na
kurejea Israel.Nitaonana na
wakuu wa Mossad nitawaeleza
kwamba nimewasiliana nawe
kwa simu na umenitaka
nikupelekee mwili wa
Edger.Nina uhakika mkubwa
watakubaliana nami na
watanipa mwili wa Edger”
“Mathew ninakutuma
nenda kaniletee mwili wa
mwanangu lakini ninakuonya
usijaribu kufanya jambo lolote
la kipuuzi kwani nitajua na
utakuwa umefanya jambo baya
sana”
“Mama usiwe na wasi wasi
nami.Nakutaka uniamini na
nitamrejesha Edger nyumbani”
akasema Mathew
“Mathew ahsante.Nini
utakihitaji katika zoezi hilo?
“Ninahitaji kufikishwa
katika mpaka wa Israel na
Jordan”
“Sawa.Nitakukabidhi kwa
Sayid Omar na atashughulikia
kila kitu” akasema Habiba na
kisha akainuka wakaondoka
wakarejea ndani akampigia
simu sayid Omar akafika mara
moja na kumchukua Mathew
wakaenda kupanga mipango ya
kwenda kuondoka kuelekea
Israel kuchukua mwili wa Edger
Kaka
MPENZI MSOMAJI TUKUTANE
SEHEMU IJAYO…………………
Mzee muendelezo lini tena?
 
Vagkojo estory eje jekholye lweli lweli. Big up sana kwa uliyetudondoshea huu mzigo. Nmejifunza mambo mengi sana juu ya uongozi na ujasusi.
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 6: EPISODE 1
UGANDA
Ndege ya shirika la ndege la
Tanzania ilitua katika uwanja
wa ndege wa kimataifa wa
Entebe nchini Uganda.Miongoni
mwa abiria waliokuwemo ndani
ya ndege hii iliyotokea Dar es
salaam Tanzania ni Melanie
Davis na Gosu Gosu.Kisha
kamilisha taratibu za uwanjani
hapo waliruhusiwa kuingia
nchini Uganda na nje ya wanja
walipokewa na mwenyeji wao
aliyeitwa Eddie Okello.Huyu
alikuwa ni rafiki wa muda
mrefu wa Gosu Gosu waliwahi
kupigana wote vita ya
msituni.Eddie na Gosu Gosu
walikumbatiana kwa furaha
kubwa baada ya kuonana baada
ya muda mrefu
“Papii siamini macho yangu
ni wewe kweli?akasema Eddie
na kumkumbatia tena Gosu
Gosu.Ilikuwa ni furaha
iliyopitiliza kwa marafiki hawa
wa muda mrefu kuonana tena.
“Eddie kutana na Melanie
Davis ni mchumba wangu”
akasema Gosu Gosu na Eddie
akabaki mwenye mshangao
akiushangaa uzuri wa Melanie.
“Hallow Eddie” akasema
Melanie baada ya kumuona
Eddie amepigwa na butwaa.
“Hallow Melanie.karibu
sana Uganda” akasema Eddie na
kupeana mkono na Melanie
kisha akawaongoza hadi katika
gari lake wakaingia na
kuondoka pale uwanjani
“Papii uliponiambia
kwamba unakuja Uganda
sikuamini ndiyo maana furaha
niliyonayo leo
haielezeki.Umebadilika sana
Papii,si yule niliyekufahamu
msituni” akasema Eddie na
Gosu Gosu akatabasamu
“Sote tuna mabadiliko
makubwa baada ya kuachana
na mambo yale ya msituni.Kila
mmoja ana maisha mapya hivi
sasa” akasema Gosu Gosu na
kukumbushana mengi kuhusu
maisha yao ya msituni.Muda
huo wote Melanie alikuwa
kimya alikuwa mbali kimawazo.
Hatimaye walifika katika
jumba moja kubwa Eddie
akawakaribisha ndani
“Hapa ndipo
ninapoishi.Karibuni jisikieni
nyumbani” akasema Eddie na
kumuita muhudumu
akawahuduia wageni vinywaji
“Eddie kama nilivyokueleza
kwamba hatutakuwa na muda
mrefu hapa Uganda tunataka
tumalize kilichotuleta hapa leo
na kurudi nyumbani hivyo
ingekuwa vyema kama
ungetupa mwongozo kuhusu
safari yetu” akasema Gosu Gosu
“Usihofu Gosu Gosu
maandalizi yamefanyika na
mtaonana na James Kasai lakini
naomba ninaweke wazi
kwamba si safari
nyepesi.Mahala alipo James ni
ndani sana msituni hivyo
tutakuwa na safari ndefu
kidogo.Tutakwenda na helkopta
na tutafika sehemu tutachukua
gari kuelekea huko msituni
anakoishi” akasema Eddie
“Hakuna tatizo sisi tuko
tayari” akasema Gosu Gosu na
hawakupoteza muda wakaingia
garini na kuondoka hadi katika
jumba moja kubwa
lililoonekana kama hoteli.Eddie
akashuka garini akaingia ndani
ya jumba lile akatumia kama
dakika kumi hivi kisha akatoka
akiwa ameongozana na mtu
mmoja mnene aliyevaa suti
nyeusi.Eddie akamtambulisha
Yule jamaa kwa akina Melanie
kama rafiki yake na ndiye
mmiliki wa jumba
lile,wakasalimiana kisha Eddie
akawataka washuke garini
wakatembea katika njia nzuri
kuelekea nyuma ya jumba lile
ambako kulikuwa na helkopta
ya rangi nyeusi.Gosu Gosu na
Melanie wakatakiwa kuingia
ndani ya helkopta,Eddie
akabaki akizungumza na yule
rafiki yake halafu naye akaingia
katika helkopta
wakaondoka.Walituia zaidi ya
dakika arobaini angani kisha
wakatua ndani ya uwanja
mkubwa uliopandwa nyasi
nzuri uliokuwa pembeni ya
jumba moja la ghorofa.Eddie
akawataka akina Gosu Gosu
washuke
“Kutokea hapa tutaendelea
na safari yetu kwa kutumia
gari” akasema Eddie na
kuwaongoza hadi katika magari
mawili yaliyokuwa
yameandaliwa kwa ajili ya
safari ile wakaingia katika gari
mojawapo na safari ikaanza
“Kutokea hapa tutachukua
muda gani kufika tuendako?
akauliza Gosu Gosu
“Itatuchukua muda wa saa
tatu hadi nne.Miundo mbinu
hasa barabara huko tuendako ni
mibovu sana na endapo
tutakuta mvua imenyesha basi
inaweza kutuchukua hata masa
matano hadi sita.Kuna sehemu
nyingine itatulazimu kushuka
na kutembea kwa miguu.Ni
safari ndefu itawalazimu
kuvumilia.”akasema Eddie
“Hakuna tatizo
tunachokihitaji ni kuonana na
James” akasema Gosu Gosu
Hakukuwa na mazungumzo
mengi garini,walipita katika
barabara za vumbi zenye
mashimo mengi na kuna
sehemu ambazo barabara
ilikuwa mbaya zaidi na
kuwalazimu kushuka
wakatembea kwa miguu ndipo
wakaendelea na safari.Ulikuwa
ni mwendo wa zaidi ya masaa
manne.Melanie alichoka
sana.Hatimaye baada ya
mwendo wa takribani saa tano
wakafika sehemu Fulani
ambako walikuta kuna kizuizi
na watu zaidi ya kumi wakiwa
na sare za kijeshi
wakawasimamisha na
kuwashusha garini.Eddie
akazungumza nao na kiongozi
wa kikosi kile akafanya
mawasiliano kisha akawaamuru
waingie katika gari lao na
wakaanza kusindikizwa na gari
mbili za wanajeshi wale wa
kikundi cha James Kasai.Baada
ya mwendo wa dakika
thelathini wakaukuta mto na
hapo ulikuwa mwisho wa
kutumia gari kwani hakukuwa
na daraja kwa ajili ya kuvusha
magari.Walishuka garini na
kuanza kuvuka daraja la kamba
kuelekea ng’ambo ya
pili.Haikuwa rahisi kwa Melanie
kuvuka katika daraja lile la
kamba ikamlazimu Gosu Gosu
kumshika mkono na kumsaidia
kuvuka katika daraja lile
ambalo Mamba walionekana
wakizunguka zunguka.Baada ya
kuvuka katika lile daraja
wakaanza kutembea kwa miguu
kama dakika ishirini.Melanie
alichoka mno na wakati
mwingine ikamlazimu Gosu
Gosu kumbeba.
Baada ya kumaliza kuvuka
daraja walitembea kilometa
chache kisha wakaanza
kukutana na mahema ya
wanajeshi.Kila mwanajeshi
waliyekutana naye alikuwa na
sura ya kutisha na amebeba
bunduki ya vita.Ilikuwa ni
sehemu ya kutisha
sana.Hatimaye wakafika katika
nyumba ya ghorofa iliyojengwa
kwa mbao na miti.Ilikuwa
imezungukwa na walinzi kila
kona na mizinga kadhaa ya
kutungulia ndege ilionekana
kuzunguka nyumba ile.Pembeni
yake kulikuwa na nyumba
nyingine za mbao kama nane
hivi.Kambi hii ilikuwa katikati
ya msitu mnene.Yule kamanda
aliyewapokea katika kizuizi
akawaongoza wakaingia katika
ile nyumba ya ghorofa
akawakaribisha katika sebule
ambayo haikuwa na vitu vya
thamani akawaacha pale
akapanda juu ghorofani
“Hapa ndipo anapoishi
james Kasai” akasema Eddie
“Dah ! nimewaona wale
wanajeshi nimekumbuka mbali
sana maisha tuliyoishi msituni”
akasema Gosu Gosu
“Tumetoka mbali sana.Yale
si maisha ya kutamani
kuyarudia hata kidogo.Ni
maisha magumu sana yaliyojaa
hatari kila sekunde” akasema
Eddie
Wakiwa pale sebuleni kila
mmoja akiwaza lake mara
akatokea Yule mwanajeshi
aliyewapokea kizuizini akiwa
ameongozana na jamaa mmoja
mrefu aliyevaa suruali ya kijeshi
na fulana nyeusi iliyokatwa
mikono.Mabega yake yote
yalikuwa yamechafuliwa na
michoro mbali mbali.Kichwani
alivaa kofia ya mduara na
macho yake aliyafunika kwa
miwani myeusi.Nyuma yake
alikuwa na watu sita wakiwa na
bunduki wakimlinda.Eddie
alipomuona akishuka
akawataka akina Gosu Gosu
wasimame
“Karibuni sana wageni
wangu.Poleni kwa safari ndefu
hadi kufika hapa” akasema Yule
jamaa huku akiwapa mikono
akina Gosu Gosu halafu
akawataka wapande ghorofani
ambako kulikuwa na sebule
nzuri sana yenye samani za
kuvutia.
“Wageni wetu
tunawashukuru mmefika
salama Poleni sana kwa safari
ndefu ya kufika hapa.Si safari
nyepesi kufika hapa lakini haya
ndiyo maisha yetu
tumekwishayazoea.Naamini
mmechoka kwa safari mtaenda
kupumzika na baadae
tutakutana kwa mazungumzo”
akasema James na mmoja wa
makamanda wake akasogea
karibu akapiga saluti kali mbele
yake.
“Wapeleke wageni
wakapumzike” akasema James
na akina Gosu Gosu
wakachukuliwa wakapelekwa
katika nyumba moja
iliyojengwa kwa mbao lakini
ukiwa ndani huwezi amini
kama imejengwa kwa mbao
kutokana na uzuri
wake.Walikaribishwa katika
chumba kizuri sana
kilichoandaliwa kwa ajili
yao.Melanie alikuwa amechoka
kupita maelezo.Ilikuwa ni mara
yake ya kwanza kufanya safari
ngumu kama ile.
“Pole sana mpenzi wangu
kwa safari hii ndefu” akasema
Gosu Gosu wakiwa wamejilaza
kitandani baada ya kuoga.
“Sijawahi kuchoka kiasi
hiki.Ni mara yangu ya kwanza
kufanya safari ndefu na ngumu
kama hii” akasema Melanie
“Pole sana.Hata hivyo lengo
letu limetimia na tumefanikiwa
kukutana na James
Kasai”akasema Gosu Gosu
“Yule jamaa hapatikani
kirahisi.Kwanza anaishi katika
msitu mnene na kufika hapa si
kazi nyepesi”
“Maisha haya ya msituni
ndiyo niliyokuwa nikiishi”
akasema Gosu Gosu
“Ilikuaje hadi ukaingia
msituni na kujiunga na makundi
ya waasi?akauliza Melanie
“Niliingia msituni angali
nikiwa mdogo sana.Nilikuwa na
miaka nane nilipotekwa na
makundi ya waasi waliovamia
kijiji chetu usiku na kuua
watu,wakabaka wanawake na
kisha wakateka watoto na
kutupeleka msituni.Tulikuwa
jumla yetu ishirini na nane na
tukaanza kutunzwa na
waasi.Tulianza kwa kutumwa
na wakubwa zetu baadae
tukaanza kupewa mazoezi
mbali mbali na kufundishwa
silaha.Nilipokuwa na umri wa
miaka kumi na tatu tayari
nilikuwa na uwezo wa kupigana
vita.Mara yangu ya kwanza
kuua mtu nilikuwa na miaka
kumi na tatu.Baada ya hapo
nikawa mpiganaji na mtu katili
sana.Sehemu kubwa ya maisha
yangu yote nimekuwa nikiishi
msituni” akasema Gosu Gosu
“Ilikuaje ukatoka msituni
na kuja kuishi hapa
Tanzania?akauliza Melanie na
Gosu Gosu akampa historia
yake namna alivyotoka msituni
akaja kuishi hapa Tanzania na
hadi alipokutana na Mathew
Mulumbi ambaye amemfikisha
hapa alipofika
“Ninatamani sana
kumfahamu huyo mtu Mathew
Mulumbi.Alikuwa mtu wa aina
gani hasa?akauliza Melanie
“Mathew alikuwa jasusi
ambaye aliifanya kazi yake kwa
mafanikio makubwa
sana.Nashindwa namna ya
kumuelezea ana sifa nyingi.Siku
zote atabaki kuwa mtu wa
pekee kwangu na kwa nchi pia
japo mchango wake
hauthaminiwi”akasema Gosu
Gosu
“Alifariki vipi?akauliza
Melanie
“Alifariki akiwa katika
misheni ya kuwakomboa
mateka waliokuwa wametekwa
na kundi la IS.Ilikuwa ni
misheni ya hatari sana”
akasema Gosu Gosu na kisha
wakaendelea kupumzika.
Saa moja za jioni
walitakiwa kujiandaa kwa ajili
ya kukutana na James Kasai.
“Unajisikiaje hivi sasa
mpenzi?Gosu Gosu akamuuliza
Melanie
“Kwa sasa baada ya
kupumzika najisikia vyema”
akasema Melanie wakatoka na
kwenda kukutana na James
Kasai.Eneo lote lilikuwa
linawaka taa walikuwa
wanatumia umeme
unaozalishwa kwa
maporomoko ya maji.
Walikaribishwa katika
sehemu maalum ambako James
alikuwa anawasubiri wageni
wake
“Natumai mmepumzika
kidogo.Ni wakati wa kupata
chakula kisha tuendelee na
mazungumzo”akasema James
Kasai na kuwaongoza akina
Melanie katika meza iliyokuwa
imeandaliwa vyakula mbali
mbali wakaketi na kupata
chakula kisha wakaenda
sehemu ya maongezi
“Natumai kwa sasa tuko
tayari kwa mazungumzo”
akasema James
“James tunashukuru sana
kwa makaribisho mazuri
tuliyoyapata hapa na sasa tuko
tayari kwa mazungumzo”
akasema Gosu Gosu
“Mimi kama
nilivyojitambulisha awali
ninaitwa James Kasai ndiye
kiongozi wa kikundi
hiki.Historia yangu si nzuri sana
lakini ninapigana kwa ajili ya
maslahi ya nchi yangu.Ninataka
kuikomboa Kongo kutoka
katika makucha ya wanyonyaji”
akasema James Kasai na kuinua
chupa ya mvinyo iliyokuwa
mezani akamimina katika glasi
akanywa na kusema
“Nilipata taarifa kwamba
kuna watu wanataka kuniona
kuna jambo muhimu sana
wanataka kuzungumza
nami.Taarifa hiyo niliipata toka
kwa Eddy ambaye
nimefahamiana naye kwa miaka
mingi na ni mshirika wangu wa
karibu sana ndiyo maana
nikakubali kuonana nanyi.Eddie
alinijulisha kwamba mmoja wa
watu wanaohitaji kuonana nami
amewahi kupigana vita ya
msituni nikafurahi kukutana na
mwanajeshi huyo ambaye
naamini ni wewe” akasema
James Kasai na kumtazama
Gosu Gosu
“Ni mimi” akasema Gosu
Gosu
“Kwa nusu ya maisha yangu
nimeishi msituni nikipigana
vita” akasema Gosu Gosu na
kumtajia James majina ya watu
ambao walikuwa pamoja katika
mapambano yale ya
msituni.James Kasai alifurahi
sana kumsikia Gosu Gosu
akiwataja watu wale.
“Nimefurahi sana kukutana
nawe Gosu
Gosu.Umenikumbusha mbali
sana.Tukipata nafasi
tutazugumza mengi lakini kwa
sasa tujielekeze katika kile
kilichotukutanisha hapa”
akasema James Kasai
“Nimeambatana na mpenzi
wangu anaitwa Melanie
Davis.Yeye ndiye ambaye ana
jambo la kuzungumza
nawe”akasema Gosu Gosu
“Melanie karibu
sana.Nimekutana na Gosu Gosu
nikajkuta nikikumbuka mbali
sana na kukusahau
kabisa.Jisikie
nyumbani”akasema James
Kasai.
“Ahsante nashukuru”
akasema Melanie na
kumtazama Gosu Gosu
akamfanyia ishara Fulani na
Gosu Gosu akasimama
“Nitawaacha mzungumze
nitarejea baadae mkisha
maliza” akasema Gosu Gosu na
James akamuita mmoja wa
walinzi wake akamtaka
ampeleke Gosu Gosu katika
sehemu ya kupumzika maofisa
“Melanie karibu sana.Haya
ndiyo makazi yetu tuko kati kati
ya msitu”akasema James baada
ya Gosu Gosu kuondoka
“Nashukuru sana.Japo ni
mbali na kufika kwake si kazi
nyepesi lakini nimependa
mazingira yake ya utulivu na
hewa safi” akasema Melanie na
James akatabasamu
“Melanie
umenifahamuje?akauliza James
“Mimi nina asili ya Congo
nilikuwa naishi Ufaransa lakini
kwa sasa nimehamia
Tanzania.Nina makampuni
kadhaa Tanzania”
“Hongera sana.Nafurahi
kukufahamu Melanie kumbe
wewe ni mtu wa nyumbani
kabisa” akasema James na
kunywa funda la mvinyo
“Nimekuwa nikisoma sana
historia ya Congo ndiyo maana
nikakufahamu” akasema
Melanie
“Historia yangu ni mbaya
na hadi sasa ninatafutwa na
mahakama ya uhalifu wa kivita
nikajibu mashtaka
ninayotuhumiwa
nayo.Nimejiuliza pamoja na
historia yangu hiyo kuwa
mbaya lakini bado umetaka
kuonana nami.Kitu gani hasa
kilichokufanya upande milima
na mabonde kutaka kuonana
nami?akauliza James na Melanie
akavuta pumzi ndefu akasema
“Nina jambo kubwa ambalo
nimekuja kuzungumza nawe na
ninaamini nimekuja sehemu
muafaka kabisa” akasema
Melanie
“Usihofu Melanie nieleze
chochote kama ni siri
nitaitunza” akasema
James.Baada ya sekunde kadhaa
Melanie akasema
“Naamini umewahi
kumsikia Lucy Muganza”
akasema Melanie
“Lucy Muganza
ninamfahamu.Ni Yule
mwanamke tajiri sana ambaye
aliuawa yeye na mumewe
nchini Tanzania.Alikuwa
amechaguliwa na chama kikuu
cha upinzani ili agombee urais
katika uchaguzi mkuu uliopita”
akasema
“Wale walikuwa wazazi
wangu”
“Wazazi wako?! James
akashangaa
“Ndiyo ni wazazi
wangu.Jina langu halisi ni
Theresia Muganza.Nilikuwa
pamoja na wazazi wangu Dar es
salaam siku walipouawa na
mimi nilinusurika kwa kupigwa
risasi ya kifua.Nilipelekwa
hospitali nikapatiwa matibabu
ya haraka,baadae serikali ya
Ufaransa ikanitaka nihamishiwe
Paris kwa matibabu zaidi na
nimekuwa Paris kwa muda
wote hadi hivi juzi nilipokuja
tena Tanzania.Baada ya kupona
ilinilazimu kufanyiwa upasuaji
wa kubadili mwonekano wangu
kwa ajili ya usalama kwani bado
ninaamini wale watu ambao
walitaka kuiteketeza familia
yetu bado wapo na kama
wakijua mimi ni Theresia
Muganza lazima wataniua.Kwa
sasa nina sura mpya na jina
jipya la Melanie Davis” akasema
Melanie na James akavua kofia
akaiweka pembeni
“Pole sana
Melanie.Umepitia mambo
makubwa.Nani lakini
waliofanya mauaji yale?Nini
malengo yao?akauliza James
“Yalikuwa ni mauaji ya
kisiasa.Inatajwa kwamba tukio
lile lilikuwa na kijambazi na
siku ile ile ya tukio waliuawa
majambazi kadhaa lakini kuna
tarifa zenye kuaminika kwamba
halikuwa tukio la kijambazi bali
yalikuwa ni mauaji
yaliyopangwa na majambazi
wale waliangushiwa mzigo.Miili
ilipofanyiwa uchunguzi
imekutwa na risasi za bunduki
kubwa za wadunguaji ambazo
majambazi wale hawakuwa
nazo na bunduki hizo
zinamilikiwa na serikali.Hii
inatupa picha ya wazi kwamba
mauaji yale yalifanywa na
serikali ya Tanzania
wakishirikiana na serikali ya
Congo”akasema Melanie
“Hata mimi niliamini lazima
kuna jambo nyuma ya mauaji
yale” akasema James
“Ipo sababu kwa nini
wazazi wangu waliuawa”
akasema Melanie na kunyamaza
kidogo baada ya muhudumu
kuleta sinia lililojaa nyama za
kuchoma
“Karibu nyama Melanie.Hii
ni nyama ya Swala ambayo
humuandalia kila mgeni
anayetutembelea.Usihofu iko
salama.Japo tuko msituni lakini
tuko vizuri katika suala la
afya.Tunao madaktari wetu
ambao hupima kila chakula
kabla hakijaliwa.” akasema
James .Melanie akachukua
finyango chache akaweka katika
sahani
“Ipo sababu ya wazazi
wangu kuuawa” akasema
Melanie na kutafuna nyama
moja halafu akaendelea
“Baada ya kushinda
uchaguzi,Rais Patrice Eyenga
alikutana na makundi vya waasi
waliokuwa wakipigana na
serikali ya Congo kwa muda
mrefu na wakakubaliana
kuweka silaha zao chini na huo
ukawa ni mwisho wa mapigano
ya Congo amani ikarejea tena.Ni
wewe pekee ambaye hukutaka
kukubaliana na mkataba ule wa
amani” akasema Melanie
“Ni kweli kabisa” akasema
James na Melanie akaendelea
“Patrice alifumua kila
alichokikuta kimefanywa na
watangulizi wake.Alifukuza
wawekezaji wakubwa katika
sekta mbali mbali na kutafuta
wawekezaji wapya.Lakini
baadae ikaja kugundulika
kwamba viongozi wa makundi
ya waasi walikubaliana kuweka
silaha zao chini kwa kupata
asilimia kadhaa ya fedha
iliyotokana na mauzo ya madini
hivyo kufanya kuwe na kundi
dogo linalofaidika na rasilimali
za nchi.Serikali ya Ufaransa
baada ya kuligundua hilo
walitafuta njia ya kuweza
kuliondoa genge hilo la walafi
wanaohujumu rasilimali za nchi
wakiongozwa na Patrice Eyenga
na ndipo walipoamua kutumia
uchaguzi mkuu uliopita ili
kumuondoa Patrice na genge
lake.Walimchagua mama yangu
agombee urais kupitia chama
kikuu cha
upinzani.Walimchagua mama
yangu kwa vile alikuwa ni mtu
mwenye jina kubwa nchini
Congo na alitegemewa kushinda
ndiyo maana akauwa kabla ya
chaguzi kufanyika.Serikali za
Tanzania na Congo
zilishirikiana katika mauaji yale
ya wazazi wangu” akanyamaza
na kutafuna nyama kisha
akaendelea
“Nilipatiwa matibabu
nchini Ufaransa na baada ya
kupona Rais Michael weren
alikuja kuzungumza nami
akanieleza kila kitu kuhusiana
na mauaji yale ya wazazi wangu
na akanitaka nivae viatu vya
mama niendeleze kile ambacho
alikusudia kukifanya yaani
kulisafisha genge la walafi
wanaomaliza rasilimali za
Congo.Haikuwa rahisi mimi
kukubali lakini baada ya
kutafakari sana nikakubali
kuifanya kazi hiyo aliyotakiwa
kuifanya mama na ndipo
nilipofanyiwa upasuaji wa
kubadili mwonekano wangu ili
watu wasinitambue kama
Theresia Muganza, nikapewa
jina jipya Melanie Davis ama
bilionea Melanie Davis”
akasema Melanie na James
akatoa tabasamu kubwa
“Nimekuja Afrika Mashariki
kwa malengo mawili
makubwa.Kwanza ni
kuisambaratisha jumuiya ya
afrika Mashariki na pili ni
kumuondoa madarakani Rais
Patrice Eyenga na kuliondoa
genge la mafisadi wanaopora
mali za nchi.Nimeisoma historia
yako na Rais Patrice ndiyo
maana nikaamua kukufuata ili
tuunganishe nguvu katika
mapambano dhidi ya kuung’oa
utawala wake” akasema
Melanie na James Kasai akatoa
pakiti la sigara akawasha moja
na kuvuta akapuliza moshi
halafu akasema
“Kwa muda wote ambao
nimekaa msituni hapa sijawahi
kupata mgeni muhimu kama
wewe Melanie.Ahsante sana
kwa kuja na ninakuhakikishia
kwamba hujakosea kuja
kwangu”
“Ahsante sana James kwa
kunipokea na ninaamini mimi
nawe tutatengeneza timu nzuri
sana” akasema Melanie
“Baada ya kunieleza kuhusu
wewe na historia yako nataka
sasa kusikia sababu hasa ya
kuja kuniona” akasema James
“Kama nilivyokueleza
kwamba nimekuja Afrika
Mashariki kwa malengo mawili
kwanza kuisambaratisha
jumuiya ya Afrika Mashariki na
pili kumuondoa Rais Patrice
Eyenga madarakani”
“Ninataka uniambie kuhusu
mpango wako namna
ulivyojipanga kutekeleza hayo
malengo yako mawili.Unao
mpango wowote umeuandaa?
Akauliza James
“Ndiyo ninao mpango
ambao ndio ulionileta hapa
kwako” akasema Melanie
“Nieleze tafadhali”
“Mkutano mkubwa wa
wake za marais kutoka nchi
zote duniani unatarajiwa
kufanyika jijini Dar es salaam
wiki ijayo.Ninataka kuitumia
nafasi hiyo kuwaua wake za
marais wa Congo na
Rwanda.Kama ujuavyo nchi ya
Congo na Rwanda hazina
mahusiano
mazuri.Halikadhalika nchi ya
Congo na Uganda hazina
mahusiano mazuri.Nataka
Uganda ibebe lawama za
kuhusika na mauaji hayo ya
wake za marais wa Congo na
Rwanda.Baada ya mauaji hayo
wewe utajitokeza na kudai
kwamba kundi lako ndilo
lililotekeleza mauaji hayo.Nchi
za Congo na Rwanda zitaipigia
kelele Uganda kwa kukuhifadhi
wewe na kundi lako na
msuguano utaibuka katika
jumuiya ya Afrika
Mashariki.Hakutakuwa na
maelewano baina ya nchi
wanachama.Nchi za Rwanda na
Congo lazima zitataka kutuma
majeshi yao msituni kukutafuta
lakini serikali ya Uganda
haitakuwa tayari kwa hilo na
huo utakuwa ni mwanzo wa
mzozo mkubwa sana na
taratibu jumuiya ya Afrika
Mashariki itaanza kutengeneza
ufa na baadae kusambaratika
kabisa.Kwa upande wangu
nitakuwa nimeua ndege wawili
kwa jiwe moja kwanza mpango
wa kuisambaratisha jumuiya ya
Afrika mashariki utakuwa
umefanyika na vile vile
nitakuwa nimelipiza kisasi kwa
Patrice Eyenga kwa
alichokifanya kwa familia
yangu.Kwa upande wako na
kundi lako mtakuwa
mmejiongezea nguvu zaidi na
baada ya jumuiya ya Afrika
Mashariki kusambaratika
mtarejea kupambana na serikali
ya Congo” akasema
Melanie.Kwa muda wote ambao
Melanie alikuwa anaelezea
mpango wake,James alikuwa
anavuta sigara wa fujo huku
akimsikiliza.Zilipita dakika
mbili za ukimya kisha James
akasema
“Baba yangu alikuwa
jenerali katika jeshi la serikali
ya Congo lakini hakuridhika
namna mambo yalivyokuwa
yakiendeshwa na watawala
akaamua kuasi na kuanzisha
kikundi chake.Kwa wakati huo
nilikuwa mwanajeshi wa
kawaida katika jeshi na
nikalazimika kuacha jeshi
kumfuata baba yangu msituni
na kuanza harakati za kuindoa
serikali madarakani.Harakati
hizo za kuiondoa serikali
madarakani zilipelekea wazazi
wangu wote wawili kuuawa
kwa bomu na majeshi ya
serikali na baada ya hapo mimi
ndiye niliyeshika usukani na
kuvaa viatu vya
baba.Niliendeleza mapambano
dhidi ya serikali na nilifanikiwa
kudhibiti miji miwili yenye
utajiri mkubwa wa
madini.Kundi langu liliogopwa
sana na ilihofiwa siku moja
ningeweza kuiondoa serikali
madarakani.Baada ya Patrice
Eyenga kushinda uchaguzi wa
Rais aliwaita makundi yote ya
waasi na wakakubaliana
kusitisha vita lakini ni mimi
pekee na kundi langu ndio
tuliosema hapana.Patrice
Eyenga alianzisha mashirikiano
na nchi ya Marekani ambao
walimsaidia kupata zana za
kisasa za jeshi na kutuondoa
mimi na kundi langu kutoka
katika miji tuliyokuwa
tunaishikilia tukakimbilia hapa
Uganda.Kutokuelewana kati ya
Congo na Uganda ni kwa sababu
yangu mimi.Serikali ya Congo
inailaumu Uganda kunipa
hifadhi.Siri ya mimi kupewa
hifadhi na Uganda ni kwa
sababu nimemuoa mdogo wake
na mke wa Rais wa Uganda.Mke
wangu na watoto wanaishi nje
ya nchi” akanyamaza na
kumsisitiza Melanie aendelee
kula nyama.
“Jeshi la Congo kwa
kushirikiana na vikosi vya
Marekani waliua wanajeshi
wangu wengi hivyo kunirudisha
nyuma sana.Kwa muda mrefu
tangu nimehamia katika misitu
hii nimekuwa na kazi moja
kubwa ya kusuka upya jeshi
langu.Ninataka kuwa na kikosi
kidogo lakini chenye nguvu
kubwa katika vita.Kuunda jeshi
jipya haijawa kazi nyepesi
kwangu.Kama unavyojua
nimekuwa ninatafutwa na
mahakama ya kimataifa ya
uhalifu wa kivita hivyo siwezi
kusafiri kwenda nchi yoyote
kutafuta msaada.Ninahitaji
silaha na zana nyingine za
vita,ninahitaji mahitaji
mbalimbali kwa ajili ya
wanajeshi wangu na haya yote
yanahitaji fedha.Nilikuwa na
akiba kubwa ya madini ambayo
nimeitumia katika
kujiimarisha.Pamoja na
changamoto zote hizo lakini
ninaendelea vizuri na kikosi
changu kimeendelea
kujiimarisha.Ninafanya
maandalizi haya yote kwa ajili
ya kurejea tena nchini
Congo.Ndoto yangu itatimia
pale nitakapofanikiwa kuingia
ikulu” akasema James na
kuwasha sigara nyingine
akaanza kuvuta
“Ndiyo maana nikachagua
kuja kwako James kwani mimi
nawe ndoto zetu
zinafanana.Sote tunataka
kuikomboa Congo.Pamoja na
nia zetu zinazofanana za
kuikomboa Congo lakini kila
mmoja wetu anayo ajenda yake
binafsi.Wewe unataka kutawala
Congo na mimi ninataka
kulipiza kisasi kwa wale wote
waliowaua wazazi wangu.Hivyo
basi ili kutimiza malengo yetu
lazima tusaidiane.Nisaidie
kulipiza kisasi na mimi
nitakusaidia katika mpango
wako wa kuitawala Congo”
akasema Melanie na James
akamimina mvinyo katika glasi
akanywa na kuuliza
“Endapo nitakubali
kushirikiana nawe na
kukusaidia katika mpango wako
wa kulipiza kisasi wewe
utanisaidia vipi katika mpango
wangu?
“Ninaungwa mkono na
Ufaransa na mataifa mengine
makubwa ya Ulaya hivyo basi
ninayo nguvu ya kuwashawishi
waweze kukuunga mkono
katika harakati zao na vile vile
kukusaidia vifaa na zana za
kivita” akasema Melanie
“Melanie mimi nina kanuni
moja”akasema James
“Sitaki kuwa na taifa lolote
nyuma yangu.Mataifa haya
yametutumia vya
kutosha.Yametukandamiza kwa
kiwango kikubwa.Kwa miaka
mingi yametutumia kama
chanzo cha machafuko katika
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo.Tumekuwa tukipigana
wenyewe kwa wenyewe lakini
nyuma ya mapigano hayo yapo
mataifa ambayo yalikuwa
yananeemeka.Sitaki tena
kuungwa mkono na taifa lolote
la kigeni katika harakati
zangu.Ninataka nifanye
mapinduzi ya kweli ambayo
yatawanufaisha watu wa
Congo.Nataka niirudishe nchi
na rasilimali zake kwa
wakongomani.Nikikubali
msaada kutoka mataifa hayo
unyonyaji hautakwisha.Yapo
mataifa ambayo yako tayari
kunisaidia lakini kwa masharti
kwamba nitakaposhika
madaraka nao lazima wafaidike
jambo ambalo siko tayari.Hata
wewe ninakushauri uwe makini
na hao uliowataja kuwa
wanakuunga mkono
wanakutumia na mwisho
watakuacha au
kukuua”akanyamaza akanywa
mvinyo na kusema
“Kwa miezi kadhaa sasa
nimekuwa na mazungumzo na
watu wa kikundi cha IS”
“Islamic State?akauliza
Melanie akionekana kushangaa
“Ndiyo.Nimekuwa na
mazungumzo nao.Kikubwa
wanachokitaka ni mashirikiano
kati yangu nao”
“Kile ni kikundi cha
kigaidi.Unawezaje kushirikiana
nao?Unataka kubadili harakati
zako kuwa za kigaidi?akauliza
Melanie
“Hapana Melanie sitaki
kukigeuza kikundi changu kuwa
cha kigaidi.Kwa miaka ya hivi
karibuni IS wamekuwa
wakijiimarisha sana katika bara
la Afrika.Wanataka kujiimarisha
zaidi katika eneo la Afrika
Mashariki na kati.Wanataka
kuungana nami lakini
wanachokihiaji ni kupata fursa
ya kujificha katika misitu
minene ya Congo ambako
watajenga kambi za mafunzo
kwa ajili ya watu
wao.Watanisaidia na
kuniwezesha kurejea tena
msituni kupambana na serikali
ya Congo na kudhibiti eneo
kubwa kisha wao wataingia na
kuimarisha kambi yao ya
mafunzo.Wanapata ugumu
kupata sehemu ya kuweka
kambi ya mafunzo ndiyo maana
wakanifuata na wazo hilo la
kutaka tushirikiane.Bado
majadiliano yanaendelea lakini
sina sababu ya kusema
hapana.Ninahitaji kuendeleza
operesheni zangu,ninahitaji
kupata fedha za kugharamia
jeshi langu ninahitaji vifaa na
zana za kisasa kwa ajili ya
kuanzisha tena vita na serikali
ya Congo na IS wanao uwezo wa
kunipatia silaha na zana za
kivita ninazozihitaji hivyo basi
sioni sababu ya kusema hapana
kuhusu ombi lao la kuanzisha
mashirikiano” akasema James
“Pamoja na sababu
ulizoeleza James lakini hawa
watu ni magaidi na hupaswi
kushirikiana nao kwa namna
yoyote ile kwani nawe
utaonekana kama gaidi na
utaanza kusakwa” akasema
Melanie
“Melanie usiwe na hofu
yoyote.Hawa watu
wanachohitaji ni kupata
sehemu ya kuweka kambi yao
ya mafunzo na wao
wataniwezesha mimi kuweza
kupata kile ninachokihitaji sana
yaani fedha na zana za
vita.Nakuhakikishia Melanie
kwamba watu hawa
ninawahitaji sana.Tutawatumia
pia katika mashambulio mbali
mbali.Kwa mfano ninafikiria
kuwatumia katika shambulio
hilo unalolipanga la kuwaua
wake za marais wa Rwanda na
Congo endapo
tutakubaliana.Hawana kitu
kikubwa wanachokihitaji zaidi
ya kupata hifadhi msituni ili
waendeshe kambi zao za
mafunzo.Watu wao
watakaofundishwa katika
kambi hizo za mafunzo si kwa
ajili ya kushambulia Congo bali
watapelekwa katika nchi mbali
mbali duniani kutekeleza kazi
zao za kigaidi”akasema James
Kasai
“James nimekuja safari hii
ndefu kuomba kushirikiana
nawe lakini baada ya kusikia
kwamba una mashirikiano na
kikundi cha kigaidi cha IS
nimeanza kusita kama
tunaweza kuendelea na
mashirikiano haya” akasema
Melanie
“Melanie unachokihitaji
wewe ni kulipiza kisasi kwa
walioua wazazi wako na ndiyo
maana uko hapa.Umekuja
kuhitaji msaada wangu na mimi
niko tayari kukusaidia lakini
nimekueleza ukweli kwamba
kuna watu ambao niko katika
mazungumzo ya mashirikiano
na watu hao ni kikundi cha IS.Ni
kweli IS ni kikundi cha kigaidi
lakini mimi nao tuna sehemu
ambazo
tutashirikiana.Ninahitaji fedha
na silaha na hivi vitu vyote
wameahidi kunipatia na kutoka
kwangu wanachohitaji ni
sehemu ambayo wataweza
kuweka kambi yao ya
mafunzo.Sioni tatizo kama
nikishirikiana nao.Ni fedha na
silaha pekee ndicho ninahitaji
kutoka kwao” akasema James
akapuiza moshi na kusema
“Melanie tafadhali usisite
wala kuhofia kushirikiana
nami.Nina mahitaji makubwa ya
fedha kama nilivyokwambia”
“Ninao utajri mkubwa na
kama unahitaji fedha
nitakupatia lakini achana na
mpango wa kushirikiana na
magaidi” akasema
Melanie.James akavuta mkupuo
mkubwa na kupuliza moshi
mwingi akamtazama Melanie na
kusema
“Melanie naomba
tuelewane jambo moja.Umekuja
kwangu ukihitaji msaada hivyo
kama unataka nikusaidie
utafuata kile ninachokielekeza
mimi.Endapo hutaridhika na
masharti yangu basi
sikulazimishi ushirikiane nami
unaweza ukatafuta mwingine
wa kushirikiana naye” akasema
James na kuwasha tena sigara
nyingine alionekana kuanza
kukasirika
“James bado tuna mengi
ambayo tunaweza kushirikiana
mimi na w….” akasema Melanie
na James akamkatisha
“Nataka sana kukusaidia
Melanie lakini sitaki uniwekee
masharti yoyote.Nimekueleza
ukweli kwa kuwa nawe pia
umenieleza ukweli wako wote
hivyo kama ukiamua
kushirikiana nami tambua
kwamba lazima ushirikiane pia
na IS” akasema James na
kumtazama Melanie kwa
sekunde kadhaa
“Melanie nakupa muda
ukalitafakari tena suala hili na
pale utakapokuwa tayari
utanijulisha maamuzi yako”
akasema James.Melanie
akaimaisha kichwa akazama
mawazoni na James akasimama
“Melanie nadhani
tumemaliza mazungumzo
yetu.Nenda ukalale utafakari na
Gosu Go…………” akasema James
na kunyamaza akamtazama
Melanie
“Melanie wewe na Gosu
Gosu ni wapenzi?akauliza na
Melanie akainua kichwa
“Ndiyo sisi ni wapenzi”
“Nilikuwa najiuliza kwa nini
hujataka kumshirikisha Gosu
Gosu katika suala hili?Kwa nini
hutaki aifahamu mipango yako?
Humuamini?Akauliza James
“Gosu Gosu hafahamu
chochote kuhusu mimi”
“Hafahamu kama wewe ni
Theresia Muganza?
“Hapana hafahamu
chochote na sitaki afahamu”
“Kwa nini hutaki
kumueleza ukweli kuhusu
wewe?Naamini angekuwa na
msaada mkubwa sana kwako”
akasema James
“Siwezi kumueleza ukweli
kuhusu mimi na hatakiwi
kufahamu chochote” akasema
Melanie
“Kwa nini Melanie?
“Nina sababu zangu
binafsi.James tuachane na suala
hilo,bado hatujamaliza suala
letu” akasema Melanie
“Nini unataka kukisema
Melanie? Nimekwisha kwambia
kwamba nenda katafakari kisha
utanijulisha maamuzi
utakayoyachukua kama
utakuwa tayari kushirikiana
nami” akasema James Kasai
“James nimekuja umbali
huu mrefu kwa ajili ya kutafuta
msaada na siwezi kuondoka
hapa bila ya kuwa na uhakika
kwamba mipango yangu
itafanikiwa.Nimekuja kwako
kwa kuwa ninakutegemea sana
unisaidie”
“Melanie niko tayari
kukusaidia lakini lazima ufuate
kile ninachokitaka mimi na si
kunipangia nini cha
kufanya.Kama uko tayari kwa
hilo tuendelee na
mazungumzo”akasema James
“James nahitaji msaada
wako na samahani kwa
kukukwaza.Naomba
tushirikiane”
“Nataka tukubaliane
endapo utahitaji msaada wangu
basi utakubaliana na masharti
yangu.Uko tayari kwa
hilo?akauliza James
“Niko tayari”
“Vizuri sana.Sasa tunaweza
kuendelea kuzungumza”
akasema James
“Umeniambia mpango
wako ni kuwaua wake za
marais wa Randa na
Congo.Kuna mpango wowote
tayari umekwisha uandaa?
“Mpango nilioufikiria ni
huu.Nitazungumza na balozi wa
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo nchini Tanzania na
nitamshawishi aandae chakula
cha usiku na kuwakaribisha
wake za marais hao katika
makazi yake na hapo ndipo
watakapouawa wote”akasema
Melanie
“Ni mpango
mzuri.Mshawishi balozi
kwamba wewe utagharamia
kila kitu katika chakula hicho
cha pamoja cha wake za marais
wa Rwanda na Congo.Ninao
wanajeshi wangu hapa ambao n
I wapishi wazuri wana ubora
wa kimataifa.Wao ndio
wanaotakiwa kuwa wapishi
siku hiyo. Watawahi kuingia na
silaha zilizofichwa na baadae
wakati watu wakianza kula
chakula ndipo mauaji
yatakapofanyika.Kuna jambo
moja ambalo nataka ulifanyie
kazi” akasema James
“Jambo gani James?akauliza
Melanie
‘Nataka utafute namna
wapishi hao watakavyoweza
kuingia na kutoka Tanzania”
“Usihofu hilo ni jambo dogo
sana kwangu.Nitalifanyia kazi”
akasema Melanie
“Basi hakuna tatizo.Mimi
nitakusaidia katika suala
hilo.Kitu cha msingi ni
kuhakikisha unanikiwa
kuwakutanisha wanawake hao
sehemu moja na vijana wangu
watafanya kazi moja tu ya
kuwamaliza wote” akasema
James
“James ahsante kwa
kukubali kunisaidia.Huu ni
mwanzo mzuri wa mashirikiano
yetu makubwa na nina hakika
yapo mambo mengi huko
mbeleni
tutashirikiana”akasema Melanie
“Melanie mimi nimekubali
kukusaidia katika mipango yako
ya kulipiza kisasi lakini na mimi
kuna mambo ambayo nitajitaji
msaada wako.Kila mmoja
lazima afaidike na mwenzake”
akasema James
“Unahitaji nini
James?akauliza Melanie
“Nilikueleza awali kwamba
bado tunaendelea na
majadiliano na kikundi cha IS
kuhusu mashirikiano yetu.Yapo
mambo kadhaa ambayo
tumekwisha kukubaliana lakini
lipo suala ambalo mpaka sasa
bado hatujaweza kulipatia
ufumbuzi nalo ni kuhusu fedha”
“Nini kinaleta
ugumu?Hawajakubali kiwango
unachokihitaji?
“Hapana si hivyo bali
namna nitakavyokuwa
nikipokea fedha kutoka
kwao.Kwa ujio wako tayari
nimepata ufumbuzi” akasema
James
“Ufumbuzi upi James?
“Wewe ni mfanya biashara
unamiliki makampuni
makubwa na biashara nyingine
kubwa kubwa.Nataka pesa
kutoka IS zipitie kwako.Hakuna
ambaye anaweza akakutilia
shaka kwa kuwa u mfanya
biashara mkubwa”
“Pesa za magaidi zipitie
kwangu?! Melanie akauliza kwa
hamaki
“Nakukumbusha tena si
magaidi bali ni washirika.Kama
umekubali kushirikiana nami
basi ukubali kushirikiana pia na
IS ndiyo maana nilikuuliza
kama utakuwa tayari na
ukakubali hivyo basi kama
kweli una nia ya dhati ya
kushirikiana nami sitaki kusikia
ukitamka neno ugaidi katika
kinywa chako.Tumeelewana
Melanie?
“Tumeelewana.Samahani”
akasema Melanie
“Vizuri” akasema James
“Ninahitaji fedha kutoka
kwa hawa jamaa na wao wako
tayari kunipatia hiyo fedha
lakini tatizo lilikuwa ni namna
ya fedha hizo
kunifikia.Kumekuwa na ugumu
sana katika usafarishaji wa
fedha duniani.Serikali nyingi
duniani zimekuwa macho sana
katika suala hilo la usafirishaji
wa fedha kwa hofu ya ufadhili
wa ugaidi.Wewe ukiwa kama
mfanya biashara fedha hii
itapitia kwako na hakuna
ambaye atakuwa na wasiwasi
nawe hata kidogo.Utasimama
kati yangu na IS na kila kitu
kitapitia kwako.Si kazi nyepesi
na wala si ngumu kwako”
akasema James
“Sawa James mimi niko
tayari kufanya hivyo na
nitakusaidia kwa kila kitu ili
mrad tu unihakikishie kwamba
kile ninachokihitaji kitatimia”
akasema Melanie
“Nakuhakikishia kwamba
kila unachokihitaji
kitatimia.Unataka
kuisambaratisha jumuiya ya
Afrika mashariki hilo
litatimia,jumuiya hii
itasambaratika.Kuna jambo
unahitaji lifanyike lakini hutaki
kuliweka wazi.Unahitaji
machafuko yatokee nchini
Congo.Hicho ndicho walio
nyuma yako
wanakihitaji.Nakuhakikishia
machafuko yatatokea kama
wanavyotaka.Lakini Melanie
naomba nikuweke wazi kitu
kimoja” akanyamaza kidogo
halafu akaendelea
“Hawa watu walio nyuma
yako hawana uchungu na nchi
yetu.Kwa miaka mingi
wamekuwa wakifadhili
makundi mbali mbali ya waasi
damu nyingi imemwagika lakini
si kwa maslahi ya Congo bali
kwa maslahi yao.Tani na tani za
madini zinatoroshwa kutoka
nchini kwetu na yanabaki
mashimo.Sitaki tena kumwaga
damu ya wakongomani kwa ajili
ya hawa jamaa.Nchi yetu
inaendelea kuogelea katika
umasikini huku nchi zao
zikiendelea kutajirika.Nitaenda
tena msituni kupigana na
serikali ya Congo kwa ajili ya
maslahi ya wakongo na si kwa
ajili ya nchi tajiri.Melanie mimi
nawe tunaweza kuunganisha
nguvu na kuwa wakombozi wa
nchi yetu ya Congo.Nakushauri
achana na hao mabeberu ambao
hawana lengo lolote zuri na
nchi zetu” akasema James.
“James ninachokihitaji
mimi ni kukamilisha misheni
zangu na sijali kama kuna
mabeberu watafaidika ama
vipi.Naomba tuendelee na
mipango yetu” akasema
Melanie
“Sawa Melanie mimi
nitakaa na watu wangu na
nitawaeleza haya
tuliyokubaliana na kisha
nitakujulisha kila kitu
kitakavyokuwa.Wewe nenda
kaanze maandalizi ya mpango
huo wa mauaji ya wake za
marais na utanijulisha kila
kinachoendelea” akasema
James kisha ukapita ukimya
“Melanie nakukumbusha
kuwa makini na Gosu Gosu.Ni
mtu hatari sana na akifahamu
kama wewe ni Theresia
Muganza atakasirika kwa
kumficha na anaweza
akakufanyia kitu kibaya
sana.Nimeelezwa sifa zake si
mtu mzuri” akasema James
“Usihofu James,Gosu Gosu
hawezi kuwa na hatari yoyote
kwangu” akasema
Melanie.Majadiliano yaliendelea
hadi ilipofika saa sita za usiku
na Gosu Gosu akaitwa kisha
James Kasai akawapeleka katika
chumba chao cha kulala
“Mambo yamekwendaje
katika maongezi yenu? akauliza
Gosu Gosu
“Haikuwa rahisi lakini
tumekubaliana mambo kadhaa”
akasema Melanie
“James amekubali
kukusaidia katika mpango
wao?akauliza Gosu Gosu
“Ndiyo amekubali
kusaidiana nami” akasema
Melanie ambaye alionekana
mwingi wa mawazo.Hakutaka
mazungumzo mengi
akamkumbatia Gosu Gosu
ambaye alifahamu kile
alichokitaka Melanie na
kuuanzisha mtanange.
“Nimehangaika hadi
kumfikisha Melanie sehemu
hatari kama hii lakini kwa nini
hajataka nishiriki katika
mazungumzo yake na
James?Kuna kitu gani hakutaka
nikifahamu?akajiuliza
GosuGosu akiwa amejilaza
pembeni baada ya mtanange
kumalizika.
“Jambo hili limezidi kuwa
kubwa.Itanilazimu kushirikiana
pia na magaidi wa IS.Sifahamu
nini kitatokea endapo Devotha
akigundua hiki ninachotaka
kukifanya.Lakini potelea mbali
ninachokitaka mimi ni mipango
yangu ikamilike na wale
walowaua wazazi wangu nao
pia walipe uovu wao” akawaza
Melanie
TEL AVIV – ISRAEL
Moshe Levine mkurugenzi
wa shirika la ujasusi la Israel
Mossad alistuliwa kutoka
usingizini na mke wake baada
ya simu yake kuita mfululizo.
“Nani huyo asubuhi yote
hii? akauliza Moshe kwa sauti
iliyoonyesha bado alikuwa na
usingizi na alihitaji kuendelea
kulala.Simu ilikatika na kuanza
kuita tena akainuka na
kuichukua akatazama mpigaji
akastuka kidogo.Alizifahamu
zile namba za simu
zilizompigia,akaipokea
“Hallow Nawal” akasema
Moshe
“Ni mimi Abu Zalawi na si
Nawal” ikasema sauti ya kiume
“Mathew Mulumbi ! Moshe
akashangaa
“Mathew ni wewe? Akauliza
bado alikuwa katika mshangao
“Ndiyo ni mimi
mkurugenzi.Habari za asubuhi”
akasema Mathew na Moshe
akainuka akatoka mle
chumbani
“Mathew uko wapi? Uko
salama?akauliza
“Niko salama mkurugenzi
usihofu.Nimefika Jerusalem
alfajiri hii.Nahitaji kukuona”
akasema Mathew
“Nielekeze mahala ulipo
tafadhali hapo Jerusalem”
akasema Moshe.Mathew
akamuelekeza mahala alipo na
Moshe akamtaka asubiri kwa
dakika chache pale pale alipo.
“Katika jiji hili nilimwaga
damu ya watu wasio na
hatia.Inaniuma sana lakini
nilifanya vile kwa lengo la
kumfanya Ammar Nazari
aniamini na mwishowe nifike
kwa Habiba Jawad na baada ya
safari ndefu hatimaye
nimeonana na Habiba jawad”
akawaza Mathew na kuanza
kukumbuka mara ya kwanza
alipomtia machoni Habiba
“Nilijiapiza kumtoa uhai
Habiba Jawad nitakapomtia
machoni lakini imekuwa
tofauti.Mambo hayajakwenda
kama nilivyotegemea.Habiba
Jawad is no t who we think she
is.Wengi wanaomtafuta Habiba
hawajawahi kumuona na
hawana taarifa zake sahihi.Moto
wote niliokuwa nao nikiamini
ndani ya muda mfupi nitakuwa
nimekamilisha kazi yangu ya
kumuua Habiba Jawad
umezimika na nimejikuta
nikiwa mtumwa ndani ya
himaya yake.Mathew Mulumbi
kutoka ujasusi hadi ugaidi.Ni
vigumu kuamini lakini ni kweli
tayari nimeingia katika dunia ya
ugaidi” akawaza Mathew na
kutazama watu wakiwa katika
pilika pilika zao za siku
“Lazima nikubali kwamba
maisha yangu tayari
yamebadilika.Safari yangu
haitakuwa nyepesi kama
nilivyotegemea,bado nina safari
ndefu.Habiba ananifahamu
vyema mimi ni
nani,anayafahamu maisha
yangu na anafahamu kama
nimetumwa kumuua lakini
haogopi chochote.Sijawahi
kukutana na mtu wa aina yake
katika maisha yangu ndani ya
ujasusi. Amenifanya akili yangu
ishindwe kuwaza mengine
nimebaki nikimtafakari yeye tu
ni mtu wa namna gani.Hata
hivyo mimi si mtu wa kukata
tamaa.Ninao mlima mrefu wa
kupanda lakini misheni yangu
kwa namna yoyote ile lazima
niikamilishe.Kwa sasa misheni
yangu imekuwa kubwa tofauti
na nilivyotegemea hivyo hata
mbinu zangu lazima zibadilike
na ziwe kubwa kulingana na
misheni yenyewe” akawaza
Mathew huku akiwa makini
kuhakikisha usalama wake
“Nimeingia katika kitovu
cha ugaidi duniani.Habiba
Jawad ndiye nguvu ya ugaidi
duniani kwani karibu makundi
mengi ya kigaidi duniani
yanamtegemea yeye ili
kujiendesha.Kuna mengi ya
kujifunza kuhusu Habiba
Jawad,kuna mengi pia ya
kujifunza kuhusu ugaidi duniani
na ili niweze kulikamilisha hilo
kwa namna yoyote ile lazima
nifanye maamuzi magumu sana
nayo ni kuachana na kila kitu na
kujiunga na Habiba
Jawad.Kujiunga na Habiba
Jawad ina maana kwamba
nitakuwa nimejiunga na ugaidi”
akaendelea kuwaza
“Habiba Jawad angeweza
kuelekeza tuuawe haraka sana
lakini hakufanya hivyo.Pamoja
na kufahamu sisi ni majasusi na
mpango wetu ni kwenda
kumuua hajamjulisha mtu wake
yeyote jambo hilo.Kwa nini
amewaficha siri hii na hataki
wajue? Watu wake wote
wanafahamu mimi na Nawal ni
magaidi tuliotoka katika kundi
la Ammar Nazari.Kitu gani
anakitafuta kwetu? Akawaza
Mathew na kukumbuka kitu
“Sijapata nafasi nzuri ya
kukaa na kuzungumza na Nawal
kujua mambo aliyopitia lakini
nitajitahidi kutafuta muda
nizungumze naye.Kuna mambo
yananipa ukakasi kidogo kwani
nimemkuta kwa Habiba Jawad
tayari amekwisha zoea na
amekubali kuolewa na Abu
Dahir mtoto wa Habiba.Kuna
kitu hakikai vizuri akilini,kwa
nini amekubali haraka hivyo
kuolewa na huyo Abu? Kuna
mambo ambayo nahitaji
kuyafahamu vizuri.Halafu dah
!!..Mathew akainamisha kichwa
chini
“Habiba anataka nimuoe
mwanae Najma” akawaza
Mathew na kuyakumbuka
maneno ya Habiba.
“Hauna mke Mathew
Mulumbi,unaye mjane.Peniela
si mkeo tena.Huko aliko
anaamini tayari umekwisha
fariki dunia na ameamua
kuendelea na maisha
yake.Labda nikupe siri ya kitu
ambacho hukifahamu.Mali
zako zote zilizoko Dar es
salaam tayari zimeuzwa”
“Habiba anafahamu kila
kinachoendelea katika maisha
yangu.Nilistushwa na taarifa ya
Peniela kuuza mali zetu
zilizokuwa Dar es salaam”
“Unadhani kwa nini
ameamua kufanya hivyo?Ni
kwa sababu anajua hutarudi
tena,umekwisha kufa.Maisha
yako Tanzania yamekwisha
ndiyo maana nataka
kukuanzishia maisha mengine
hapa.Ningekuwa sina nia
nzuri kwako ningeweza
kuelekeza uuawe lakini
sijafanya hivyo.Sioni sababu
yoyote ya kukuangamiza
Mathew Mulumbi.Bado unayo
nafasi ya kuendelea kufurahia
maisha yako.Familia yako
wamekwisha kubaliana na
ukweli kwamba umeondoka
na hautarudi tena hivyo
hakuna haja ya kwenda
kuwasumbua na kuvuruga
maisha waliyonayo
sasa.Nakupa nafasi ya
kuanza maisha mapya ukiwa
na Najma” Maneno ya Habiba
bado yaliendelea kumjia
Mathew kichwani
“Yawezekana kweli familia
yangu wamekwisha
kubalianana na matokeo
kwamba nimekwisha fariki na
sintarejea tena,wameamua
kusonga mbele na maisha yao
ndiyo maana Peniela ameamua
kufanya maamuzi hayo ya
kuuza mali kwani hana tena
mpango wa kurejea kuishi
Tanzania.Habiba amenieleza
kwamba maisha yangu
Tanzania yamekwisha,anaweza
akawa anasema kweli kwa
upande mmoja lakini maisha
yangu Tanzania bado
yapo.Nilizaliwa Tanzania na
nitazikwa Tanzania.Haya yote
ninayoyapitia ni kwa sababu ya
mapenzi makubwa niliyonayo
kwa Tanzania.Amenitaka
nimuoe mwanae Najma na
nianzishe maisha mapya.Huu ni
mtihani mgumu sana lakini
kama ninataka kukamilisha
misheni yangu sina budi
kukubaliana na Habiba kumuoa
huyo Najma.Sifahamu
kitakachotokea huko mbeleni
lakini ninachokihitaji mimi ni
m…..” Mathew akatolewa
mawazoni baada ya gari moja
ndogo rangi nyeusi kusimama
karibu na aliposimama mlango
ukafunguliwa akashuka mtu
mmoja akamfuata
“Abu Zalawi?akauliza Yule
jamaa na Mathew akaitika kwa
kichwa.Yule jamaa akamtaka
amfuate wakaingia ndani ya lile
gari ambamo alikuta kuna watu
wengine wawili na kuondoka
mahala pale.Hakukuwa na
mazungumzo
yoyote.Walikwenda hadi katika
ofisi za Mossad jijini Jerusalem
na kuingia katika helkopta
ikapaa na kuondoka.
Hakukuwa na mazungumzo
yoyote ndani ya helkopta hadi
walipofika jijini Tel
Aviv.Helkopta ikatua katika
makao makuu ya Mossad na
Mathew akashushwa.Mara tu
aliposhuka akakutana na Moshe
Levine akimsubiri.
Wakasalimiana kisha akamtaka
Mathew waeelekee ofisini
kwake.
“Mathew karibu
sana.Sikuamini uliposema
kwamba ni wewe” akasema
Moshe,Mathew hakujibu kitu
“Mathew Mulumbi
sifahamu nianzie wapi lakini
kama idara tumepitia kipindi
kigumu sana kwa maamuzi
tuliyoyafanya ya kumtorosha
Ammar Nazari.Tulipata wakati
mgumu kwa vile
tulichokitegemea hakikufanyika
kama tulivyotarajia.Tulikubali
kumuacha Ammar Nazari
atoroke gerezani kwa
kutegemea kwamba
tunatengeneza njia ya kuelekea
kwa Habiba Jawad.Ulituahidi
kutafuta namna ya kutupa
mrejesho mara utakapokuwa
umefika kwa Ammar Nazari
brigades lakini hukutupa taarifa
zozote.Tulihitaji sana kupata
mrejesho kutoka kwako ili
tuweze kuendelea na mipango
yetu lakini muda ulipokuwa
mrefu bila kupata taarifa zako
zozote tulilazimika kuamini
yawezekana umeuawa hivyo
tukakuondoa katika mipango
yetu” akasema Moshe na
Mathew akamtazama kwa muda
na kusema
“Mlifanikiwa kupata mahala
alipo Ammar nazari na
mkalipua mabomu bila kujali
uwepo wangu pale.Kama
isingekuwa Nawal ningekwisha
fariki dunia” akasema Mathew
“Naomba ufahamu kwamba
hatukuwa na namna nyingine
ya kufanya.Hatukuwa na
mawasiliano yako na tulihitaji
kumuua Ammar hivyo baada ya
kufanikiwa kupata mahala alipo
kazi yetu ilikuwa moja tu
kumsambaratisha yeye na
wafuasi wake.Halikuwa kosa
letu kama ungefariki katika
mashambulio yale kwa sababu
hatukuwa na taarifa zako”
akasema Moshe na Mathew
akamtazama kwa hasira
“Mlifanikiwa kumuua
Ammari Nazari katika
mashambulio yale?akauliza
Mathew
“Ndiyo tulimuua Ammar
Nazari.” Akasema Moshe na
Mathew akacheka kidogo
“Pamoja na kufahamu
mahala alipo Ammar Nazari
lakini msingeweza
kumuua.Ammar alikuwa
amejiandaaa vilivyo” akasema
Mathew
“Lakini tulifanikiwa
kumuua na hicho ndicho
kikubwa tulichokuwa
tunakitafuta.Ammari Nazari
brigades halipo tena na tuna
uhakika wa watu wetu kuwa
salama” akasema Moshe
“Nilimuua Ammari Nazari
kabla hamjaangusha mabomu
yenu” akasema Mathew
“Ulimuua Ammar?
“Ndiyo” akasema Mathew
na kuchukua simu ya Nawal
akamuonyesha Moshe picha
“Hivi ndivyo Ammar Nazari
alivyouawa.Mliisambaratisha
ngome yake kwa mabomu lakini
tayari alikwisha uawa.Mimi na
Nawal tulimuua”
“Nawal?
“Ndiyo.Mlimpigia simu
Nawal na kumtaka aondoke
mara moja eneo lile kwani
mlipanga kulipua mabomu
ndipo tulipomuua Ammar
kwani angeweza kutoroka”
“Ulikuwa na ukaribu na
Nawal?
“Ndiyo.Nilikuwa na ukaribu
naye mkubwa”
“Kwa nini usingetumia
simu yake kuwasiliana nasi
kutujulisha kwamba uko
salama?
“Nawal alikuwa katika
misheni nyingine na hakutaka
simu yake itumike katika
mawasiliano na Mossad kwa
ajili ya usalama wake” akasema
Mathew
“Pole sana Mathew kwa
yaliyotokea lakini yote haya
yamesababishwa na ukosefu wa
mawasiliano baina yetu.Kama
kungekuwa na mawasiliano
mazuri baina yetu yote haya
yasingetokea.Nashukuru
kwamba u mzima” akasema
Moshe
“Naamini katika mawazo
yenu mliamini nimetoroka na
kutokomea zangu lakini
nisingeweza kufanya hivyo
kabla ya kukamilisha misheni
yangu ya kumpata Habiba
Jawad.Hamkupaswa kuondoa
imani kwangu.Mimi si mtu
mwenye ndimi mbili.Nikiamini
kitu lazima nikitekeleze.Sjawahi
kupewa misheni nikaishia njiani
hivyo mlikosea sana kupoteza
imani kwangu.Habiba Jawad si
muhimu kwenu tu bali kwa nchi
yangu Tanzania na ulimwengu
mzima hivyo sintaweza kuishia
njiani katika misheni hii hadi
pale nitakapohakikisha Habiba
Jawad aidha ameuawa au
ametiwa nguvuni” akasema
Mathew
“Nakubali Mathew tulifanya
kosa lakini tulikuwa katika
shinikizo kubwa baada ya
Ammar Nazari kutekeleza
shambulio lile katika kituo cha
treni na kuua
watu.Utatusamehe sana kwa
lililotokea.Mambo kama haya
katika kazi zetu hizi huwa
yanatokea” akasema Moshe
“Ninaelewa Moshe lakini
ningefurahi sana kama
kungekuwa na kuaminiana
baina yetu.Hakuna
tunachoweza kukifanya
kufanikisha misheni hii kama
hakutakuwa na kuaminiana
baina yetu” akasema Mathew
“Mathew tunakuamini
sana.Kama tusingekuwa
tunakuamini tusingeweza
kukubali wazo lako la kumtoa
Ammar Nazari gerezani.Yule
alikuwa mtu hatari kwa taifa
lakini tulikubali kumtorosha
gerezani kwa sababu
tulikuamini.Kilichotokea baina
yetu ni ukosefu wa
mawasiliano.Kama tungekuwa
tunawasiliana vizuri basi haya
yote yasingetokea.Tuachane na
hayo karibu tena.Nataka kujua
kila kitu toka ulipoondoka na
Ammar” akasema Moshe na
Mathew akamuelezea kila
kilichotokea.Namna alivyoingia
katika kundi la Ammar Nazari
na kila kilichoendelea.Katika
maelezo aliyoyatoa Mathew
hakuweka wazi kama yeye
ndiye aliyetekeleza shambulio
lile la bomu katika kituo cha
treni jijini Jerusalem.
“Nilikuwepo katika kikao
kile cha kupanga shambulio la
Jerusalem lakini nisingeweza
kuwajulisha kwani kama
shambulio lile lingeshindwa
kufanikiwa Ammar na kundi
lake wangejiuliza sababu ya
kushindwa kufanikiwa na
wangeanza uchunguzi”
akadanganya Mathew zikapita
sekunde kadhaa za ukimya
halafu akaendelea
“Baada ya kumuua Ammar
Nazari mimi na Nawal
tuliondoka kuelekea Ramallah
ambako tulionana na
mwanamama mmoja anaitwa
Fatma ambaye alikuwa ni rafiki
wa Ammar.Tukiwa pale Nawal
ambaye alikuwa na kitabu
ambacho Ammar amekuwa
akiandika mambo yake muhimu
aliwasiliana na mtu mmoja
akamueleza kilichotokea na
akamtaka atukutanishe na
Habiba Jawad.Jamaa huyo
alitutaka tuelekee Amman
Jordan.Tulifanikiwa kupata hati
za kusafiria na kuvuka mpaka
hadi Jordan ambako tulipokewa
na mtu mmoja akatupeleka
katika nyumba Fulani ambayo
siikumbuki kwani ilikuwa ni
usiku.Alfajiri tulichukuliwa
tukiwa tumevishwa mifuko
kichwani tukapelekwa sehemu
Fulani na huko tulianza
kupatiwa mateso”
Mathew akamuonyesha
Moshe vidonda alivyovipata
katika mateso
“Pole sana.Nini hasa
ilikuwa sababu ya
kuteswa?Walitaka nini?
“Walitaka kuthibitisha
kama kweli mimi ni Abu Al
zalawi.Niliteswa sana lakini
baadae waliridhika kwamba
mimi ni Abu Zalawi” akasema
Mathew
“Nini kilifuata baada ya
hapo?
“Tulikutanishwa na mtu
aliyejitambulisha kwetu
anaitwa Sayid Omar.Kwa
mujibu wa maelezo yake ni mtu
wa karibu sana na
Habiba.Aliniuliza sababu ya
kutaka kuonana na Habiba
Jawad nikamweleza kwamba
ninazo taarifa za mahala alipo
Edger Kaka.Kwa kutumia
kompyuta yake niliweza
kuwasiliana na Habiba Jawad
kwa kupitia simu ya mtandaoni
tukazungumza”akasema
Mathew na Moshe akashusha
pumzi wakatazamana
“Ulizungumza na habiba
Jawad?akauliza Moshe
“Ndiyo.Baada ya mateso
makali nilifanikiwa
kuzungumza na Habiba Jawad”
akasema Mathew
“Nini mlizungumza?
“Nilijitambulisha kwake
kama Abu Zalawi kutoka kwa
Ammari Nazari brigades na
nikamweleza kwamba
ninafahamu mahala alipo Edger
Kaka.Nilimwambia ukweli
kwamba hali yake si nzuri na
anaishi kwa kutumia
mashine.Habiba alinitaka
nithibitishe ninachokisema kwa
kumpelekea mwili wa Edger
ambaye anaonekana kweli ni
mtu muhimu sana kwake”
“Hii ni hatua kubwa
ambayo sikuwa
nimeitegemea.Umezungumza
na Habiba Jawad na
akakuamini!
“Bado hajaniamini kama
ninachomweleza ni kitu cha
kweli na ndiyo maana akanitaka
nilithibitishe ninalolisema kwa
kumpelekea mwili wa Edger
kaka akiwa mzima au
amekufa.Moshe japo
sijafanikiwa kuonana ana kwa
ana na Habiba Jawad lakini
kuzungumza naye tu kwenye
simu na kutaka nimpelekee
mwili wa Edger Kaka ni hatua
kubwa sana.Kwa asilimia
hamsini naweza kusema tuko
karibu kumfikia Habiba Jawad”
akasema Mathew
“Nakubali haya ni
mafanikio makubwa sana.Toka
tumeanza kumsaka Habiba
Jawad hatujawahi kufikia hatua
hii kubwa.Hongera sana
Mathew kwa mafanikio haya”
akasema Moshe
“Ahsante”
“Nawal yuko wapi?
“Nawal anashikiliwa hadi
pale nitakapoupeleka mwili wa
Edger”
“Unaweza ukapakumbuka
mahala ulikofikia na sehemu
mlizokuwa mkipelekwa kwa ajli
ya kuteswa?Moshe akauliza
“Hapana sikumbuki
chochote.Kila mahala
nilikokuwa ninapelekwa
nilikuwa nimefunikwa mfuko
kichwani”
“Nataka kujua.Ulimweleza
Habiba mwili wa Edger uko
sehemu gani?
“Nilimweleza kwamba
Edger amewekwa kwenye
mashine ya kumsaidia kuishi
katika hospitali moja hapa Tel
Aviv.Walitaka kunipa kikosi
lakini nilikataa nikawahakikisha
kwamba mahala hapo
hapahitaji kikosi.Ninao uwezo
wa kuingia na kumchukua
Edger Kaka” akasema Mathew
“Mathew narejea tena
kukupa pole na kukupongeza
kwa hatua hii kubwa uliyopiga
katika kumtafuta Habiba
Jawad.Hatua lilipofika suala hili
tunahitaji umakini mkubwa
sana.Hatupaswi kufanya
makosa hata
kidogo.Nitawashirikisha
wenzangu suala hili ili tuone
namna tutakavyoweza
kujipanga kwa jambo hili
kubwa.Kwa sasa utakwenda
kupumzika baada ya safari
ndefu yenye misuko suko
mingi”akasema Moshe na
kupiga simu akaingia jamaa
mmoja akampa maelekezo ya
kumpeleka Mathew kupumzika.
******************
Saa tano za asubuhi
Mathew akaletewa simu na
moja wa walinzi wa nyumba ile
alimokuwa amepelekwa
kupumzika.Moshe Levine ndiye
aliyempigia simu na kumtaka
ajiandae kwani anahitajika
katika kikao.
“Mambo yameiva.Naamini
hivi sasa watakuwa tayari
wamekwisha jadiliana na
kufikia muafaka.Lazima
niwasaliti Israel ili kujenga
imani kwa Habiba
Jawad.Nitakachowafanyia
kitawapa hasira lakini kitakuwa
na manufaa makubwa kwa siku
za usoni si kwa Israel pekee bali
kwa dunia nzima” akawaza
Mathew huku akijiandaa.Nusu
saa baadae lilifika gari na
kumchukua kumpeleka katika
ofisi kuu za Mossad.Alipelekwa
moja kwa moja katika ofisi ya
Moshe Levine na kupokewa na
katibu muhtasi ambaye
alimjulisha mkuu wake kwamba
Mathew tayari amefika pale
ofisini.Moshe akatoa maelekezo
apelekwe katika chumba cha
mikutano.Katibu muhtasi wa
Moshe akampa maelekezo
mlinzi Yule aliyekuwa
ameongozana na Mathew
ambaye alimpeleka katika
chuma kile cha mikutano
maalum.Mlango ukafunguliwa
Mathew akakaribishwa ndani
ya kile chumba.Aliangaza
macho haraka haraka kulikuwa
na watu nane.Alioweza
kuwatambua ni Moshe Levine
na Efraim Dagan.Akaelekezwa
kiti akaketi.
“Mathew karibu sana na
ninatuma umepata muda mzuri
wa kupumzika” akasema Moshe
na Mathew akaitika kwa kichwa
“Walioko mbele yako
naamini unawafahamu.Si mara
yako ya kwanza kukutana
nao.Umeshakutana nao katika
vikao kadhaa” akasema Moshe
na Mathew akaitika kwa kichwa
“Kwa muda wa saa kadhaa
sasa tumekuwa tukijadiliana
kuhusu suala lako
ulilonieleza.Tumekuwa na
mjadala mpana sana na
ninapenda kukujulisha kwamba
kila mmoja ndani ya chumba
hiki anakupongeza sana kwa
ushujaa wako kwanza kwa
kumuua Ammar Nazari.Ni
jambo kubwa sana umelifanya
kwetu.Jambo la pili ni ushujaa
wako wa kuvumilia mateso
makali na hatimaye umeweza
kupiga hatua kubwa katika
kumfikia Habiba
jawad.Tulikuwa tumepoteza
matumaini ya wewe kuwa hai
lakini umeibuka ukiwa na
jambo kubwa na la
muhimu.Nimejitahidi
kuwaeleza wenzangu kwa
upana kila ulichonieleza na
wameelewa” akanyamaza
kidogo
“Tumekuita hapa ili wewe
uweze kutueleza mpango wako
namna mlivyokubaliana kuweza
kuufikisha mwili wa Edger Kaka
kwa Habiba Jawad” akasema
Moshe na Mathew akakohoa
kidogo kuweka sawa koo lake
na kusema
“Habiba Jawad alinitaka
niupeleke mwili wa Edger Kaka
lakini mipango yote tulifanya
mimi na Sayid Omar.Huyu ni
mtu muhimu sana na wa karibu
kwa Habiba.Tulikubaliana
kwamba nikiupata mwili wa
Edger nijitahidi nifike mpakani
mwa Israel na Jordan na
nitakuta kuna watu pale
wananisubiri kisha baada ya
hapo nitawakabidhi mwili wa
Edger na wao watajua wapi pa
kuelekea.Naamini itakuwa ni
safari ya kuelekea kwa Habiba
Jawad” akasema Mathew
“Ni vipi kama baada ya
kuupata mwili wa Edger kaka
watakuua na kutokomea
zao?akauliza mmoja wa
wajumbe wa kikao kile
“Hilo lina asilimia hamsini
kutokea.Wanaweza wakaniua
na mimi niko tayari kwa hilo
lakini ushauri wangu mwili wa
Edger uwekewe kifaa ambacho
kitawawezesha kuufuatilia kwa
kutumia satelaiti.Endapo
ikitokea nikauawa njiani basi
zoezi litaendelea na mwili huo
utakakopelekwa ndiko
atakuwepo Habiba Jawad”
akasema Mathew
“Wazo la kuweka kifaa
katika mwili wa Edger ni zuri
lakini ni vipi kama wakikuua na
halafu wakauchunguza mwili
huo kama una kifaa chochote na
wakagundua kifaa hicho na
kukitoa? Tutakuwa tumekosa
kila kitu”akauliza Efraim Dagan
“Naombeni niwatoe
wasiwasi wakuu
wangu.Haikuwa rahisi kufika
hatua hii hata kuweza kukutana
na Sayid Omar na vile vile
kuzungumza na Habiba
Jawad.Nimepitia mateso
makali” akasema Mathew na
kusimama akavua shati
akawaonyesha viongozi wale
vidonda alivyokuwa navyo
ambavyo havijapona bado
alivyovipata kufuatia mateso
aliyoteswa.
“Mateso niliyopitia ni
makubwa na siwezi kuyaelezea
lakini niliendelea kushikilia
msimamo wangu kwamba mimi
ni Abu Zalawi.Baada ya kunitesa
sana wakaridhika kwamba
mimi ndiye Abu Zalawi na
ndipo waliponikutanisha na
Sayid Omar nikazungumza naye
na akaniunganisha na
Habiba.Tayari wananiamini na
kitendo cha kumpeleka Edger
Kaka kitawafanya waniamini
zaidi.Mlinikabidhi suala hili na
ninawaomba muendelee
kuniamini kwamba nitafika
mahala alipo Habiba jawad”
akasema Mathew
“Mathew Mulumbi una
uhakika kwamba watu hawa
wanakuamini na unaweza
ukafika alipo Habiba
Jawad?akauliza Moshe Levine
“Siwezi kusema kwamba
nina uhakika asilimia mia moja
kwamba nitafanikiwa kufika
kwa Habiba jawad kwani
sifahamu upande wao nini
wanakipanga lakini kitu kimoja
ambacho kinanipa matumaini ni
kwamba hawa jamaa tayari
wananiamini na imani hiyo
inaweza ikanifikisha
mbali.Tulipoanza misheni hii
hakuna aliyetegemea kama
ningeweza kufika hapa
nilipofika hivyo naomba
muendelee kuwa na imani
kwangu.Ninawaahidi kwamba
nitafanya kila lililo ndani ya
uwezo wangu kuhakikisha
ninafahamu mahala alipo
Habiba Jawad.Lazima tukubali
kucheza kamari,kupata au
kukosa.Tukikosa tutajipanga
tena upya na hautakuwa
mwisho wa kumsaka Habiba
Jawad.Mapambano yataendelea
na mwisho Habiba atapatikana
kama alivyopatikana Osama Bin
Laden” akasema Mathew na
chumba kile kikawa
kimya.Moshe akavua miwani
akafuta vioo vyake halafu
akavaa tena na kusema
“Mathew ameeleza vyema
nadhani tufuate ushauri
wake.Tuweke kifaa katika mwili
wa Edger Kaka ambacho
kitatuwezesha kufuatilia na
kujua mahala ambako mwili ule
utapelekwa.Ninakubaliana na
Mathew kwamba watu hawa
wamekwisha onyesha
kumuamini hasa baada ya
kumpitisha katika mateso hivyo
suala la kumuua lina asilimia
ndogo sana” akasema Moshe
Levine
“Kuongezea hapo
mkurugenzi” akasema Efraim
Dagan ambaye toka awali
alionyesha kumuamini sana
Mathew Mulumbi.
“Tuitumie vyema fursa hii
ya Mathew kuaminiwa na kundi
la Habiba.Kuonana na Sayid
Omar ni hatua kubwa hivyo
nina hakika kwa imani hiyo
waliyonayo kwa Mathew
hawana tena sababu ya
kumchunguza.Nashauri Mathew
naye awekewe kifaa ambacho
kinaweza kutusaidia kufuatilia
na kujua mahala alipo”akasema
Efraim
“Mathew unasemaje
kuhusu hilo wazo la Efraim?
akauliza Moshe
“Si wazo baya ingawa wale
jamaa wakigundua kwamba
nina kifaa mwilini nitakuwa
nimeharibu kila kitu lakini
niwekeeni kifaa hicho” akasema
Mathew
“Vizuri.Kwa mujibu wa
daktari ni kwamba Edger Kaka
amekwisha fariki kitambo sana
na kinachomuweka hai mpaka
sasa ni mashine hivyo pale
mashine zitakapozimwa
utakuwa ndiyo mwisho wa
Edger Kaka hivyo
utakachoondoka nacho ni maiti
yake.Mathew utapewa nafasi ya
kipekee ya kuzima mashine
kuashiria mwisho wa Edger na
baada ya hapo mwili wake
utaanza kuandaliwa.Kila kitu
kikikamilika utaondoka kwa
usafiri wa helkopta hadi karibu
na mpakani ambako utapewa
gari na ukifika mahala
mlipokubaliana utawasiliana na
watu hao.Sisi hatutaingilia
chochote tutakuwa mbali lakini
tutakuwa tunakufuatilia
kuhakikisha kwanza unakuwa
salama na pili tunajua mahala
mwili huo unakopelekwa”
akasema Moshe
“Hakuna tatizo Moshe”
akasema Mathew
“Kabla hatujahitimisha
kikao hiki nataka kuuliza
swali.Unahisi Habiba Jawad
anaishi nchini Jordan?akauliza
mmoja wao
“Siwezi kusema moja kwa
moja kama anaishi Jordan kwa
sababu sijabahatika kukutana
naye ana kwa ana.Hiki
tunachokwenda kukifanya leo
kinaweza kutupa picha ya
mahala alipo Habiba Jawad
kama yuko nchini Jordan au
yuko wapi” akajibu Mathew.
Baada ya kikao kile
kumalizika,wote waliingia
katika magari na kuelekea
katika hospitali alikolazwa
Edger Kaka.
“Mathew kama
nilivyokueleza tunakupa
heshima ya kuzima mashine hii
inayomsaidia Edger kuishi
kama ishara ya kuhitimisha
safari yake hapa duniani”
akasema Moshe na Mathew
akaelekezwa sehemu ya kuzima
“Ninakuita kwa jina lako
halisi Seif Jawad.Ulikuwa na
malengo mabaya sana kwa nchi
yangu Tanzania lakini kwa
nguvu ya mwenyezi Mungu
wewe na wenzako hamkuweza
kufanikiwa na sasa ninakwenda
kuhitimisha safari ya maisha
yako hapa duniani.Kabla ya
kuzima mashine hii ninakuahidi
kwamba kama ninavyomaliza
safari yako leo ndivyo
nitakavyommaliza mama yako
Habiba jawad” Mathew
aliyatamka maneno haya
kimoyo moyo na kisha akazima
mashine ile na baada ya
sekunde chache mashine
inayoonyesha mwenendo wa
mapigo ya moyo ikabadili mlio
na grafu yake ikabadilika pia
“Tayari amekwisha kufa”
akasema daktari na kila kitu
kikazimwa
“Safari ya Edger imefika
mwisho.Sasa yanaanza
maandalizi” akasema Moshe na
mwili wa Edger ukachukuliwa
na kupelekwa katika chumba
maalum kwa ajili ya kuuandaa
kwa safari.Mathew naye kama
walivyokuwa wamekubaliana
aliwekewa kifaa kidogo katika
mkono wake wa kushoto
ambacho kingewawezesha
Mossad kuweza kumfuatilia na
kujua mahala alipo
Zoezi la maandalizi ya
mwili wa Edger Kaka
lilikamilika mida ya saa kumi na
moja za jioni na Mathew akawa
tayari kwa safari.
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Saa kumi na mbili za jioni
ndege ya shirika la ndege la
Tanzania ilitua katika uwanja
wa ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere Dar es salaam
ikitokea Uganda.Miongoni mwa
waliokuwamo katika ndege
hiyo ni Melanie Davis na Papii
Gosu Gosu.Joyce Dereva wa
Melanie alikuwepo uwanjani
kuwasubiri.Waliingia garini na
kuelekea nyumbani kwa Gosu
Gosu wakaagana na Melanie
akaelekea katika makazi
yake.Hakuhitaji mazungumzo
yoyote alikuwa amechoka mno
kwa safari ndefu akaenda
kujifungia chumbani
kwake.Kitu cha kwanza
alichokifanya ni kuingia katika
bafu lake zuri akaoga na
kwenda kujilaza kitandani
“Safari ilikuwa ndefu na
ngumu lakini nashukuru
nimefanikiwa kuonana na
James Kasai.Mafanikio ya safari
yangu ni makubwa japo
yamejitokeza mambo mengine
ambayo sikuwa nimeyafikiria
lakini hakuna
kitakachoharibika.Nitafanya
kama alivyoelekeza James yaani
kushirikiana na magaidi wa IS
ambao watakuwa wakipitishia
fedha kwangu.Si jambo jepesi
kushirikiana na magaidi lakini
kwa vile niliweka ahadi ya
kufanya kila niwezalo
kuhakikisha ninalipa kisasi kwa
watu walioua wazazi wangu
nitashirikiana nao” akawaza
Melanie na simu yake ambayo
aliiweka maalum kwa ajili ya
watu wake wa muhimu ikaita
jina lilionyesha James
“James Kasai.Nadhani
anataka kujua kama
tumekwisha fika salama”
akawaza Melanie na kuipokea
simu
“Hallow James” akasema
Melanie
“Melanie mmefika salama?
Akauliza James
“Ndiyo james tumefika
salama.Ninashukuru sana kwa
mapokezi na huduma nzuri
mlizotupa”
“Usijali Melanie.Nashukuru
kama mmefika salama”
“Tuko salama usihofu”
“Melanie kuna jambo
lingine ambalo nataka
kukujulisha.Kesho kutwa
utakuwa na safari ya kwenda
Dubai”
“Dubai?
“Ndiyo.Utakwenda
kukutana na wajumbe maalum
ambao mtajadiliana nao kuhusu
masuala yale ya fedha namna
zitakavyopita kwako” akasema
James
“James kwa nini
umenistukiza hivyo? Hata mimi
nina ratiba zangu”
“Sikuwa nimetegemea hata
mimi kama ingetokea safari ya
ghafla namna hii lakini baada ya
kuwajulisha jamaa kuhusiana
na makubaliano yetu
wameomba wakutane nawe
haraka hivyo jiandae kesho
kutwa unatakiwa Dubai”
akasema James Kasai
“Sawa james nitajiandaa
kwa hiyo safari” akasema
Melanie
“Ahsante Melanie.Nitakupa
maelekezo yote kuhusiana na
safari hiyo kesho”akasema
James kasai na kuagana na
Melanie akaitupa simu pembeni
kitandani
“Sitaki ufike wakati
nijilaumu kwa maamuzi
niliyoyafanya kwa kukubali
kujiunga na James
Kasai”akawaza Melanie
“Kuna nyakati ninakuwa na
wasi wasi sana na suala hili la
kushirikiana na IS.Kinachonipa
hofu ni pale ambapo akina
Devotha
watagundua.Hawatafurahi
kwani nitakuwa nimeenda
kinyume na maelekezo na
mipango yao.Rais wa Ufaransa
Michael Weren ambaye
amejitahidi sana kuhakikisha
ninafika hapa nilipofika
hatafurahi lakini potelea mbali
ninataka kuendesha
mapambano haya kwa namna
ninavyotaka mimi.Mpango wao
umelenga zaidi katika maslahi
ya nchi zao huku wakilipa
umuhimu mdogo sana suala la
kuhakikisha wale waliotekeleza
mauaji ya wazazi wangu
wanalipa uovu wao.Devotha
ana ndoto za urais wa Tanzania
na ameahidiwa hivyo na umoja
wa Ulaya.Rais Michael Weren
na wenzake ndoto yao ni
kurejesha machafuko nchini
Kongo ndiyo maana wanataka
Afrika Mashariki isambaratike
na machafuko yaanze ili wapate
nafasi nzuri ya kuweza kupenya
na kuendelea kuchota
rasilimali.Mimi si mtoto mdogo
ambaye siwezi kushindwa
kung’amua malengo
yao.Niliwakubalia kufanya kazi
yao kwa lengo la kupata nafasi
ya kutimiza mpango wangu”
akawaza Melanie na sura yake
ikabadilika
“Kama si wao na tamaa zao
za rasilimali za Congo hivi sasa
wazazi wangu wangekuwa
hai.Walimrubuni mama yangu
agombee urais na mwisho wake
akauawa.Kama
wasingemuingiza katika
masuala yao ya siasa mpaka
sasa mama
angekuwepo.Hakuwa na shida
na fedha lakini wao
walimrubuni kwa madaraka
makubwa na aliyetumwa
kufanya hivyo ni
Devotha.Anadhani mimi
sifahamu kama yeye ndiye
aliyetumiwa na serikali ya
Ufaransa kumshawishi mama
yangu akubali kuwania
urais?Yeye na wenzake
ninaweka pembeni kwanza
nitawashughulikia
mwisho.Hakuna aliyeshiriki
atakayepona.” akaendelea
kuwaza Melanie.
ISRAEL
Mathew Mulumbi aliwasili
mahala alikopanga kukutana na
timu iliyoandaliwa kwa ajili ya
kuupokea mwili wa Edger
Kaka.Ilikuwa ni katika mpaka
wa Israel na Jordan.Alipelekwa
na helkopta hadi karibu na
mahala hapo kisha akaingia
katika gari na kuelekea upande
wa Jordan mahala ambako
alipanga kukutana na watu wale
waliowekwa maalum kwa ajili
ya kuupokea mwili wa Edger
Kaka
Aliwasiliana na mtu
aliyeelekezwa awasiliane naye
kisha baada ya dakika tano
zikatokea gari mbili.Mwili wa
Edger kaka ukashushwa kutoka
katika gari la Mathew na
kuingizwa katika mojawapo ya
gari walizokuja nazo wale
jamaa kisha wakaondoka.
Mara tu walipoanza safari
gari lililokuwa na majasusi wa
Mossad waliokuwa
wakimfuatilia Mathew
wakawasiliana na majasusi
wenzao waliokuwa upande wa
Jordan wakawajulisha kwamba
tayari safari imeanza na
Mathew yumo katika moja
wapo ya magari yale yaliyovuka
mpaka.Majasusi wale
waliokuwa upande wa Jordan
walishika usukani wa
kuendelea kumfuatilia Mathew
ambaye alikuwa amewekewa
kifaa maalum mkononi
klichowawezesha kujua mahala
alipo
Akiwa ndani ya gari
Mathew akamtaka Yule jamaa
kiongozi wa ile timu iliyokuja
kuupokea mwili wa Edger ampe
simu yake.Alipopewa
akaifungua akatoa laini na
kuivunja vunja.
“Kwa nini unafanya
hivyo?akahamaki Yule jamaa
aliyejulikana kwa jina la Bashar
“Kwa sababu za
kiusalama”akasema Mathew na
kuchukua simu aliyokuwa nayo
akaikanyaga ikavunjika kisha
akatoa laini yake akaivunja
vunja na kuvitupa vipande
vyote nje.Hakuwa na simu
tena.Katika kompyuta za
Mossad simu ile aliyokuwa
anaitumia Mathew iliyokuwa
imeunganishwa ili kufuatilia
mawasiliano yote
atakayoyafanya ikapotea ghafla
“Lazima nihakikishe
ninawapoteza Mossad wasijue
ninaelekea wapi” akawaza
Mathew.
Saa nne za usiku waliwasili
katika jiji la Amman.
“Tunaelekea wapi? Mathew
akamuuliza Bashar ambaye
bado alikuwa amekasirika kwa
kitendo cha Mathew kuivunja
simu yake
“Hutakiwi kuuliza
chochote.Utatufuata sisi
tunakoelekea” akasema Mathew
na kutaka gari lile lisimame ili
wazungumze.Bashar akaamuru
gari lisimame wakashuka
“Unasemaje?akauliza
Bashar kwa ukali
“Ninafahamu wewe ni
kiongozi na umepewa
maelekezo hata hivyo nataka
kukuweka wazi kwamba tuko
katika hatari kubwa na endapo
hamtakuwa tayari kunisikiliza
mimi basi hatutaweza kufika
huko tunakoelekea” akasema
Mathew
“Hupaswi kunifundisha kazi
yangu ! akasema Bashar kwa
hasira na kuanza
kuondoka.Mathew akamfuata
akamvuta mkono,Bashar
akageuka kwa hasira akarusha
ngumi na Mathew akaiona
akamtandika ngumi nzito
iliyompeleka chini.Mathew
akamuwahi na kuichukua
bastora yake na mara watu
waliokuwa katika magari
wakashuka na kumuelekezea
Mathew bunduki
“Sikilizeni ndugu
zangu.Mimi ndiye
niliyepambana vya kutosha
hadi kufanikiwa kuupata mwili
huu wa Seif Jawad.Hapa tulipo
hatuko salama majasusi wa
Mossad wanaendelea
kutufuatilia.Endapo hamtafuata
maelekezo yangu hatutaweza
kufika salama huko
tuendako.Mwili huu wa Seif
Jawad umewekewa vifaa
maalum vya kuwawezesha
Mossad kufuatilia na kujua
mahala unakopelekwa kwani
wanaamini mtu huyu ana
ukaribu na Habiba
Jawad.Mkipuuza maelekezo
yangu mtakuwa mmemuweka
mama Habiba na Sayid Omar
katika hatari kubwa.Mimi siko
tayari kuwaweka watu hawa
muhimu katika hatari ya
Mossad.Niko tayari mniue hapa
hapa endapo hamtakubaliana
na ushauri wangu” akasema
Mathew na watu wale wakabaki
kimya
“Ninawahakikishia ndugu
zangu hiki ninachowaeleza ni
kitu cha kweli na kama
hamuamini mimi sintakuwa
tayari kuendelea na safari.Niko
tayari mniue hapahapa”
akasema Mathew na kuitupa
bastora ya Bashar chini na
kuinua mikono juu
“Nipigeni risasi sasa
hivi.Siko tayari kuendelea na
safari hii kama hamtakuwa
tayari kusikiliza kile
ninachowaelekeza” akasema
Mathew kwa ukali.Wale jamaa
wakatazamana kisha Bashar
akauliza
“Unataka tufanye nini?
“Tunahitaji kupata hospitali
yenye mashine ya MRI ambayo
itatuwezesha kupata picha za
ndani ya mwili wa Seif na kujua
vifaa hivyo vimewekwa sehemu
gani” akasema Mathew na wale
jamaa wakajadiliana halafu
Bashar akachukua simu ya
mmoja wa wale jamaa akataka
kupiga Mathew akamzuia
“Usipige simu yoyote.Hapa
tulipo wanatufuatilia na ukipiga
simu yoyote watajua na
kumfuatilia huyo mtu
unayetaka kumpigia ndiyo
maana niliiharibu simu yako
kwa vile nilikupigia.Bila
kufanya vile wangekutafuta
hadi wahakikishe wamekutia
mikononi mwao” akasema
Mathew
“Ndugu zangu tusitafute
msaada wowote kutoka nje kwa
sasa.Tunatakiwa kupambana
sisi wenyewe.Ninyi
mnalifahamu vyema jiji hili na
mnazifahamu hospitali zote
kubwa na nzuri.Nielekezeni
hospitali moja mnayodhani
kutakuwa na mashine hiyo ya
MRI” akasema Mathew.Bashar
na wenzake wakajadiliana kwa
sekunde chache kisha akasema
“Advaclinic.Iko mtaa wa
Suleiman Al Hadidi lakini muda
huu itakuwa imefungwa.Kwa
kawaida hufunguliwa saa mbili
asubuhi na kufungwa saa moja
za jioni”akasema Bashar
“Sawa tunaelekea huko na
mtafuata maelekezo yangu”
akasema Mathew wakaingia
ndani ya magari na safari ya
kuelekea AdvaClinic
ikaanza.Wakiwa ndani ya gari
kuelekea Adva clinic mvua
kubwa ikaanza
kunyesha.Bashar akamjulisha
Mathew kwamba wamekaribia
kufika katika jengo la
kliniki.Mathew akaomba apewe
bastora,Bashar akampa bastora
yake iliyofungwa kiwambo cha
sauti.Magari yaliwasha taa
kuashiria kuingia Advaclinic
“Wanaelekea Advaclinic”
mmoja wa majasusi wa Mossad
waliokuwa garini
wakiwafuatilia akina
Mathew,akawajulisha Mossad
ofisi kuu Tel Aviv
“Wanakwenda kufanya nini
hapo hospitali usiku huu?
Akauliza Efraim Dagan
aliyekuwa katika chumba
kikubwa wakiendelea
kuwafuatilia akina Mathew
“Wamesimamishwa na
walinzi getini” Majasusi wale
wakaendelea kutoa taarifa
“Nataka kujua Advaclinic
inahusika kutibu magonjwa
gani? Akauliza Efraim na
kuwataka watu wake wafuatilie
baada ya dakika mbili
mwanadada mmoja akasema
“Inahusika na huduma ya
vipimo mbali mbali kwa njia ya
mionzi.MRI,CT Scan,X-ray,Ultra
sound na vingine kadhaa”
akasema Yule mwanadada na
Efraim akashika kichwa.
“Kuna kitu hakiko sawa
hapa.Sielewi sababu ya kwenda
katika kliniki hiyo” akasema
Efraim na kuwataka wale
majasusi waliokuwa
wakiwafuatilia akina Mathew
waendelee kuwafuatilia kwa
karibu kujua nini wanakwenda
kukifanya katika kliniki ile.
Geti la kuingilia hospitali
lilikuwa limefungwa na walinzi
walikuwa ndani kufuatia mvua
kubwa iliyokuwa
ikinyesha.Mathew akaichukua
bastora yeye kiwambo cha
kuzuia sauti akashuka garini na
kwenda mlangoni akagonga geti
lakini walinzi hawakusikia
kutokana mvua ile
kubwa.Mathew akajaribu
kufungua mlango mdogo wa
pembeni haukua umefungwa
akaingia ndani na kuwaona
walinzi wakiwa wamesimama
katika chumba chao pembeni ya
geti.Mlinzi mmoja akachukua
mwavuli akamfuata.
“As salaam Alaikum”
akasema Mathew akimsalimu
Yule mlinzi
“Wa alaikum salaam”
akajibu Yule mlinzi
“Nikusaidie nini?akauliza
“Ninahitaji huduma.Nina
mgonjwa ana hali mbaya sana”
akasema Mathew
“Kwa sasa hakuna huduma
yoyote inayotolewa hapa.Kliniki
imefungwa.Hufunguliwa saa
mbili asubuhi na kufungwa saa
moja za jioni.Nawashauri
mumkimbize katika hospitali
nyingine ambazo zinafanya kazi
kwa saa ishirini na nne” akajibu
Yule mlinzi na Mathew akatoa
bastora akamuonyeshea Yule
mlinzi na kumtaka afungue
geti.Mlinzi Yule akatupa
mwavuli na kupiga kelele
akikimbilia katika nyumba ya
walinzi lakini kabla hajaingia
ndani ya ile nyumba yao
iliyokuwa pembeni ya geti
Mathew aliyekuwa mwepesi
kama unyoya akaizinga bastora
yake na kumtandika risasi mbili
akaanguka.Wenzake wawili
waliokuwa ndani ya ile nyumba
wakatoka kwa haraka lakini
walikutana na risasi kutoka
katika bastora iliyoshikwa na
mkono mwepesi wa Mathew
Mulumbi na wote wawili
wakaanguka chini.Kwa
tahadhari akaenda kutazama
ndani ya kile chumba hakukuwa
na mlinzi mwingine.Akawasachi
wale walinzi na kupata funguo
ya geti akaenda kulifungua na
kuwataka wenzake waingize
gari ndani.Haraka haraka gari
zikangizwa ndani.
“Geti limefunguliwa na gari
zao zinaingia ndani” Majasusi
wale waliokuwa wakiwafuata
akina Mathew wakatoa taarifa
“Nini kimewapeleka hapo
kliniki usiku huu? Efraim Dagan
akauliza
“Mkuu kuna kitu
nimekipata kuhusiana na
Advaclinic” akasema Bayla
Brahm
“Umepata nini
Bayla?akauliza Efraim
“Kliniki hii hufunguliwa saa
mbili asubuhi na kufungwa saa
moja za jioni hivyo muda huu
hakuna huduma yoyote
inayotolewa pale” akasema
Bayla
“Kama hakuna huduma
yoyote inayotolewa muda huu
wamekwenda kutafuta
nini?akauliza Efraim na
kuwataka majasusi wale
wafuatilie kile kinachoendelea
mle ndani.
“Wavuteni hao walinzi
muwafiche katika maua”
akaelekeza Mathew baada ya
kufunga geti.Mlango mkubwa
wa kioo wa kingilia mapokezi
ulikuwa umefungwa Mathew
akapiga teke kioo kikavunjika
akapenya akaingia ndani,Bashar
naye akamfuata.Ndani ya jengo
kulikuwa kimya kabisa.Mathew
akatafuta sehemu ya kuwashia
taa akaipata na kuiwasha.Watu
wengine wote walibaki nje
ndani ya magari wakisubiri
maelekezo.
“Tunahitaji kukipata
chumba chenye mashine ya
MRI” akasema Mathew na mara
Bashar akamuita.Alikuwa
amesimama katika ramani
iliyoelekeza sehemu mbali
mbali za jengo lile
“Ghorofa ya tatu ndimo
kilimo chumba cha MRI”
akasema na Mathew
akajiridhisha kwamba kweli ni
ghorofa ya tatu kama ramani
ilivyoelekeza wakapanda ngazi
haraka haraka kuelekea ghorofa
ya tatu wakakuta kuna kibao
kinachoelekeza kilipo chumba
cha MRI.Wakakifuata kibao kile
na kukikuta chumba ambacho
juu ya mlango kulikuwa na
kibao Chumba cha MRI.Mathew
akajaribu kukiminya kitasa
kuufungua mlango lakini
haukufunguka.Akarudi nyuma
na kuruka teke zito mlango
ukaachia wakaingia
ndani.Akatafuta ukutani
akapata sehemu ya kuwashia
taa na chumba kikawa na
mwanga.Kulikuwa na vyumba
viwili.Chumba cha kwanza
kilikuwa na mashine na chumba
cha pili kulikuwa na kompyuta
ambayo imeunganishwa na ile
mashine na ambayo ndiyo
husoma mwili wa
mgonjwa.Mathew
akamuelekeza Bashar kwenda
kuuleta mwili wa Edger Kaka.
“Tutafanyaje bila
daktari?akauliza Bashar
“Usihofu nitafanya
mimi.Ninafahamu mambo haya”
akasema Mathew na Bashar
akataka kusema kitu lakini
Mathew akamtaka akaulete
mwili wa Edger.Nje bado mvua
kubwa iliendelea
kunyesha.Bashar kwa kutumia
bastora yenye kiwambo cha
sauti akailenga taa kubwa
iliyokuwa ikimulika eneo la nje
na kukawa na giza kisha
akaelekeza magari yale yasogee
karibu na mlango mwili wa
Edger ukashushwa na
kuingizwa ndani.
“Joseph kuna chochote
unakiona kinachoendelea hapo
ndani?Efraim akamuuliza Jasusi
Yule ambaye alikuwa katika
harakati za kutaka kujua
kinachoendelea ndani ya kliniki
walimoingia akina Mathew
“Nashindwa kuona
chochote wamezima taa ya nje
na kuna mvua kubwa sana
inanyesha huku”akajibu Joseph
na Efraim akakasirika akavua
spika zile za masikioni
alizokuwa amevaa kwa ajili ya
mawasiliano akazitupa chini
“Katika maisha yangu ya
ujasusi nimejifunza mambo
mengi sana na niliwahi
kufundishwa namna ya kutumia
mashine kama hizi lakini ni
muda mrefu sana umepita
sijawahi kutumia
mashine.Mungu nisadie tuweze
kufanikisha malengo yetu”
akawaza Mathew
Bashar na watu wake
wakasaidiana kuubeba mwili
wa Edger na kuuingiza ndani ya
kile chumba cha MRI.Mathew
akauandaa mwili ule kwa ajili
ya kuuingiza katika mashine ile
ambayo alikwisha
iwasha.Akampa Bashar
maelekezo halafu akaingia
katika chumba cha pili na
taratibu mwili wa Edger
ukaanza kuingia katika mashine
ile huku Mathew akiangalia
katika kompyuta.
“Mossad bado
hawajanifahamu vizuri mimi ni
nani” akawaza Mathew na
kutabasamu baada ya
kufanikiwa kukiona kifaa
kidogo ambacho kilikuwa
kimewekwa kitaalamu sana
sehemu ya kifua.Baada ya
kuhakikisha ni kifaa kimoja tu
kilichokuwa kimewekwa
mwilini mwa Edger akatoka na
kuingia katika chumba kile
ilimo mashine akaomba
kupewa kisu na kupasua
sehemu ile ambayo alikiona kile
kifaa kidogo akakitoa huku
wote wakibaki
wanashangaa.Akafungua
dirisha na kukitupa kifaa kile
nje.Mwili wa Edger ukatolewa
mle ndani ya chumba Mathew
akabaki nyuma na walipotoka
watu wote akapasua sehemu ya
mkono wake alikowekewa kile
kifaa kidogo cha kuwawezesha
Mossad kumfuatilia kujua
mahala alipo akakitupa kile
kifaa nje ya jengo na kuzima
kila kitu kisha naye akatoka.
“Kwa hapa naweza kusema
tuko salama lakini wanafahamu
kama tuko hapa hivyo lazima
kutafuta namna ya kuwapoteza”
akasema Mathew
“Tuelekee barabara ya
Zaharani.Kuna handaki la
Suhaib.Pale ndipo
tutakapowapoteza.Gari moja
litarejea tulikotoka na lingine
litaendelea.Tutakuwa
tumewapoteza wale
wanaotufuatilia hawatajua
wafuatilie gari lipi” akasema
Bashar
“Huo ni mpango
mzuri.Haraka tuondokeni
mahala hapa” akasema Mathew
na magari yale mawili
yakaondoka
“Magari yanaondoka
hospitali” Joseph akawajulisha
Mossad Tel Aviv
“Joseph haraka sana wewe
na wenzako ingieni hapo
ndani.Kompyuta yetu
inatuonyesha Mathew Mulumbi
yuko hapo ndani ya hospitali
pamoja na mwili wa Edger
Kaka.Tunataka mkahakikishe
kama Mathew ni mzima.Yumo
humo ndani na tuna wasiwasi
na usalama wake” akaelekeza
Efraim.Bila kupoteza muda
Joseph na wenzake wakaingia
ndani.Hakukuwa na mlinzi
yeyote na baada ya kupekua
katika kuchunguza wakakuta
miili mtatu ya walinzi
“Walinzi watatu wameuawa
kwa risasi” Joseph akatoa
taarifa kisha wakaingia
ndani.Walizunguka mle ndani
ya hospitali na hakukuwa na
dalili zozote za kuwepo mtu.
“Hakuna dalili zozote za
kuwepo mtu humu ndani”
akasema Joseph
“Tumempoteza
Mathew.Tumepoteza kila kitu”
akawaza Efraim Dagan.
“Tunasubiri maelekezo
mkuu” akasema Joseph
“Ondokeni sehemu hiyo
haraka sana.Tutawasiliana
wenzetu wa Jordan kuomba
msaada katika suala hili na
tutafahamu ukweli”akasema
Efraim
Kama walivyokuwa
wamepanga.Baada ya kufika
katika handaki la Suhaib gari
moja likageuza kurejea
lilikotoka na lingine likaendelea
na safari kwa lengo la
kuwapoteza wale waliokuwa
wakiwafuatilia.
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 6: EPISODE 2
Pembezoni mwa jiji la
Amman nchini Jordan kulikuwa
na kijiji cha bilionea Rayan
Jaber.Huyu alikuwa mmoja wa
matajiri wakubwa sana na
walioheshimika nchini
Jordan.Alimiliki visima vya
mafuta katika nchi kadhaa za
kiarabu na vile vile
kilichomuongezea umaarufu ni
kumuoa mpwa wa mfalme wa
Jordan.Rayan alikuwa na wake
wawili hivyo alijenga kijiji
chake ambako aliishi yeye na
ukoo wake na baadhi ya watu
wachache aliopenda waishi
karibu yake.Katika kijiji hicho
cha kifahari kulikuwa na
huduma zote muhimu.
Gari walilokuwamo akina
Mathew Mulumbi lilifika katika
geti la kuingilia kijiji cha Jaber
.Bashar alipewa maelekezo ya
kufika hapa na taarifa zao
zilikuwepo kwa walinzi hivyo
mmoja wa walinzi akaongozana
nao kuelekea katika nyumba
Fulani akawataka akina Mathew
wabaki garini akaenda kugonga
mlango na jamaa mmoja
akaufungua wakazungumza
kwa dakika chache Yule jamaa
akaenda kuwasalimu akina
Mathew garini halafu akarejea
tena ndani na baada ya dakika
chache akatoka akiwa na gari
aina ya jeep akawataka
wamfuate.Walimfuata hadi
katika hospitali.Wakazunguka
nyuma ya jengo lile la hospitali
ambako kulikuwa na jengo zuri
kwa ajili ya kuhifadhia
maiti.Mwili wa Edger
ukashushwa na kuingizwa
katika friji ukahifadhiwa
hapo.Yule jamaa ambaye
hakujitambulisha jina lake
akamtaka Mathew aingie katika
gari lake akaagana na akina
Bashar kisha wakaondoka na
Yule jamaa akaendesha gari
hadi walipofika katika kasri
kubwa lililojengwa kati kati ya
kijiji kile cha kifahari.Geti
likafunguliwa wakaingia ndani
na kwenda kusimamisha gari
katika sehemu maalum ya
maegesho wakashuka.Walinzi
wakafika wakiwa na silaha na
mbwa wawili ambao
walimkagua Mathew kila
sehemu na bastora yake
ikachukuliwa.Kisha kaguliwa
wakaelekea ndani.Ilikuwa ni
mara ya kwanza kwa Mathew
kuingia katika jumba la kifahari
namna ile.
“Kuna watu ndani ya dunia
hii wanaishi kama vile
hawataondoka hapa
duniani.Maisha ya namna hii ni
kufuru.Huu ufahari
umepitiliza”akawaza wakati
wakipita ndani ya jumba lile
wakielekea katka sebule.Katika
sehemu mbali mbali walizopita
kulikuwa na walinzi
wamesimama kwa adabu
Waliingia katika sebule
kubwa na kukaribishwa na
mwanadada mrembo.Ilikuwa ni
mara ya kwanza kwa Mathew
kukalia kiti cha dhahabu .Baada
ya dakika chache akaingia
jamaa mmoja na kuzungumza
na Yule jamaa aliyekuwa
ameongozana na Mathew.Wote
wawili wakamfuata Yule jamaa
wakatoka nje na kuelekea
katika bwawa la
kuogelea.Sakafu ilikuwa
imetengenezwa kwa madini
yenye kung’aa
Katika bwawa kubwa la
kuogelea jamaa mmoja alikuwa
amekaa katika kiti
kizuri.Alikuwa kipande cha mtu
na alionekana alikuwa ametoka
kuogelea.Walisimama umbali
wa hatua kadhaa kisha Yule
jamaa aliyekwenda
kuwachukua akina Mathew kule
sebuleni akamfuata Yule jamaa
akamjulisha kwamba wale watu
tayari wamekwisha fika Yule
jamaa akaelekeza wapelekwe
sehemu ya kupumzika.Yule
jamaa aliyekuwa na Mathew
alionekana ni mwenyeji wa
nyumba ile kwani
alipoelekezwa akamtaka
Mathew waondoke.Walikwenda
katika sehemu moja yenye uzuri
wa kipekee.Pembeni ya mahala
pale walipokuwa wamekaa
kulikuwa na banda kubwa
ambalo ndani yake kulikuwa na
chui wawili ambao usiku huu
walionekana wakizunguka
zunguka katika banda lao
kubwa.
“Wanyama hawa lazima
wanatoka Afrika.Nani anaishi
hapa?Je hapa ni moja ya makazi
ya Habiba Jawad? akajiuliza
Mathew na kutamani kumuuliza
Yule jamaa kuhusiana na
mahala pale walipokuwa lakini
Yule jamaa hakuonekana kutaka
mazungumzo yoyote.
“Nimezunguka sehemu
mbali mbali nimefika katika
makazi mengi ya matajiri lakini
kwa utajiri huu niliouona hapa
katika hii nyumba ni kufuru.Ni
mara yangu ya kwanza
ninakalia kiti cha dhahabu
katika maisha yangu.Pesa
iliyotumika kununua samani za
ile sebule kama zingetolewa
msaada kwa nchi za Afrika
zingesaidia sana” akatolewa
mawazoni baada ya Yule jamaa
waliyemkuta akiogelea kuingia
mahala pale .Alikuwa amevaa
koti refu lenye nakshi za
kupendeza.Akaketi kitini na
kuwasalimu akina Mathew
“As salaam Alaikum”
akasema Yule jamaa aliyekuwa
ameongozana na walinzi
kadhaa ambao walisimama
mbali kidogo na alipokuwa
amekaa.
“Wa alaikum salaam”
Mathew na yule jamaa
aliyekuwa naye wakajibu
“Mkuu nimemleta mgeni na
kila kitu kimefanyika kwa
mujibu wa maelekezo” akasema
Yule jamaa aliyekuwa na
Mathew
“Ahsante sana Majid”
akasema Yule jamaa tajiri na
Majid akasimama akamuaga
akaondoka.
“Abu Zalawi karibu sana
katika himaya yangu.Naamini
hunifahamu mimi ninaitwa
Rayan Jaber.Ni mfanya biashara
mkubwa hapa Jordan.Ninamiliki
visima vya mafuta katika nchi
mbali mbali.Habiba Jawad ni
rafiki yangu sana.Urafiki wetu
umeanza muda mrefu toka
wakati akiwa na mumewe na
baada ya kufariki mumewe
tumeendelea kuwa marafiki wa
karibu sana.Alinieleza kuhusu
wewe na ndiye aliyetaka uje
ufikie hapa kwangu baada ya
kutoka Israel.Pole sana kwa
misukosuko yote.Vipi safari
yako ilikuaje huko ulikotoka?
Akauliza Rayan
“Rayan nashukuru sana
kwa kunikaribisha hapa katika
himaya yako,safari yangu
haikuwa rahisi.Haikuwa rahisi
kuupata mwili wa Edger kaka
kwani ulikuwa umefichwa
mahala pa siri na Mossad lakini
nashukuru Mungu
nimefanikiwa kuupata na
nitakwenda kuukabidhi kwa
Habiba Jawad” akasema
Mathew na Rayan alionyesha
mstuko kidogo Mathew
alipotamka kuhusu Mossad
“Una hakika wale jamaa
hawajakufuatilia na kujua
umekuja hapa?akauliza Rayan
“Hapana hawajui kama niko
hapa ndiyo maana nikasema
kwamba haikuwa rahisi kuweza
kufika hapa.Nimechukua kila
aina ya tahadhari”
“Vizuri sana.Narudia tena
kukupa pole nyingi na
kukushukuru pia kwa
kufanikiwa kuupata mwili wa
Seif. Habiba amekwisha lia
machozi mengi sana kwa ajili ya
Seif.Mimi kama mtu wake wa
karibu huwa hanifichi
jambo.Ninafahamu uchungu
alioupata kuhusu mwanae huyu
na hatimaye amefanikiwa
kuupata mwili wake na atauzika
kwa heshima.Kwa hili
ulilolifanya,umemfanyia Habiba
kitu kikubwa sana ambacho
hatakisahau katika maisha
yake” akasema Rayan
akanyamaza kidogo na kusema
“Utalala hapa usiku wa leo
na kesho tutaongozana
kuupeleka mwili wa Seif kwa
mama yake” akasema Rayan na
kumuita mmoja wa walinzi
wake akamuelekeza jambo
kisha mlinzi Yule akamtaka
Mathew amfuate
“Rayan nashukuru sana na
usiku mwema” akasema
Mathew na kuondoka
akamfuata Yule
mlinzi.Alipelekwa katika
nyumba moja iliyokuwa na
chumba cha kulala,sebule
kubwa na nzuri na sehemu ya
kulia chakula.Ilionekana ni
nyumba maalum kwa ajli ya
wageni kwani hakukuwa na
dalli zozote za kuishi mtu ndani
ya nyumba ile.Mathew akaingia
ndani ya chumba cha kulala na
kuustaajabia uzuri
wake.Akatabasamu kwa uzuri
wa chumba kile kisha akakaa
juu ya kitanda kikubwa.
“Dunia hii wapo watu
wanaishi kama wako
peponi.Hawana mawazo kama
siku moja wataondoka katika
hii dunia.Tazama chumba hiki
cha wageni namna kilivyo kizuri
ni vipi katika chumba chake cha
kulala? Akajiuliza
“Lakini haya mambo
hayanihusu kikubwa ambacho
natakiwa kujielekeza ni
kuhakikisha mwili wa Edger
kaka unafika salama kwa
Habiba Jawad.Naamini Mossad
hivi sasa watakuwa
wananitafuta sana baada ya
kuwapoteza pale
Advaclinic.Wataamini kwamba
wale jamaa niliokuwa nao
wamegundua kwamba mimi na
Edger tumewekewa vifaa
mwilini na wakavitoa.Sitaki
wafahamu chochote kuhusu
Habiba Jawad kwa sasa.Nataka
nipate nafasi nzuri ya
kumfahamu mwanamama huyu
wa aina yake.Tayari nimeanza
kuufahamu mtandao
wake.Kama huyu jamaa Rayan
ana utajiri mkubwa kiasi hiki ni
vipi kuhusu Habiba
Jawad?Naamini utajiri wake ni
mkubwa mno na ndiyo maana
haoni hasara kufadhii makundi
ya kigaidi” akawaza Mathew na
kuingia bafuni kuoga.Alipotoka
akajilaza kitandani mara
mlango wake
ukagongwa.Alikuwa ni jamaa
mmoja aliyejitambulisha kama
daktari.Akalitibu jeraha la
Mathew mkononi pale mahala
alipokuwa amewekewa kile
kifaa akampima na kila kitu
kilikuwa kinakwenda
vizuri.Baada ya daktari
kuondoka mlinzi akamfuata na
kumjulisha kwamba chakula
tayari kimeandaliwa akaenda
katika chumba cha chakula
akala na kurejea chumbani
kwake akajilaza kitandani.
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Saa kumi na moja za alfajiri
simu ya Melanie ikaita.Alikuwa
amechoka sana akaiacha ikaita
na kukatika ikaanza kuita tena.
“Nani huyu alfajiri
yote?akasema na kuinuka
akaichukua simu akatazama
mpigaji alikuwa ni Devotha
“Asubuhi yote hii anatafuta
nini?akajiuliza Melanie na
kuipokea ile simu.
“Hallow Devotha” akasema
Melanie kwa sauti ya uchovu
“Melanie habari yako?
“Nzuri kabisa.Habari za
huko?
“Huku kwema.Vipi
maendeleo yako?
“Ninaendelea vizuri”
“Juzi na jana ulikuwa wapi
Melanie? Akauliza Devotha na
Melanie akawa kimya
“Nilikutafuta nilikuwa na
jambo la msingi sana la
kuzungumza nawe lakini
hukuwa ukipatikana
simuni.Ulikuwa wapi?akauliza
Devotha
“Ni kweli nilikuwa
sipatikani kuna masuala
nilikuwa nayafuatilia”
“Melanie nimekwisha
kuelekeza kwamba usifanye
kitu chochote bila ya Edwin
kujua.Yeye ndiye kiongozi wako
hapo Dar es salaam.Masuala
yote kuhusiana na usalama
wako yeye ndiye
tumemkabidhi.Ulionekana
ukiondoka na sanduku
ulikwenda wapi?akauliza
Devotha
“Devotha nimekwisha
kwambia kwamba kuna suala
muhimu nilikuwa nalifuatilia”
“Ni suala gani hilo?
“Usihofu Devotha
litakapokamilika nitakujulisha”
akasema Melanie
“Melanie unafahamu
umuhimu wa suala
lililokupeleka Tanzania lakini
unaonyesha kupuuzia.Suala
unalokwenda kulifanya ni
zito.Kusambaratisha jumuiya
kubwa kama ya Afrika
Mashariki si suala dogo ndiyo
maana imetuchukua miaka
kuliandaa jambo hili na sasa
tumeanza utekelezaji wake
lakini unaanza kwenda katika
mwelekeo usio sahihi.Suala hili
huwezi ukalifanya peke yako
ndiyo maana tumetengeneza
mtandao mpana ambao
utakusaidia wewe uweze
kutimiza misheni yako.Kwa
sasa macho yote yameelekezwa
kwako hivyo tafadhali
nakuomba ufanye kile
ulichoelekezwa kwenda
kukifanya.Ukienda kinyume na
maelekezo utasababisha
mambo kushindwa kufanikiwa
hivyo shirikiana na mtandao
mkubwa ulioko hapo Tanzania”
akasema Devotha
“Devotha huna haja ya
kunikumbusha majukumu
yangu.Ninafahamu kilichonileta
hapa na ndicho
ninachokifanya.Pamoja na
mtandao mliouandaa kwa ajili
ya kunisaidia lakini lazima mimi
mwenyewe niwe na mipango
ambayo itanisaidia katika
kutimiza malengo yangu hivyo
unaponitafuta katika simu na
kuikosa fahamu kwamba niko
katika kutimiza majukumu
yangu” akasema Devotha
“Ninalielewa hilo Melanie
lakini naomba sana shirikiana
na Edwin.Kila unachotaka
kukifanya mshirikishe”
“Nitafanya hivyo”
“Vipi maandalizi yamefikia
wapi?
“Ninaendelea kufanya
maandalizi na ndani ya siku
chache nitakupa mrejesho”
akasema Melanie
“Jitahidi sana Melanie
kukamilisha maandalizi haraka
kwani zimebaki siku chache
kwa mkutano kufanyika”
akasema Devotha.Baada ya
mazungumzo kidogo
wakaagana na Devotha akakata
simu Melanie akairusha simu
pembeni na kuendelea kulala.
Saa tatu za asubuhi,mlango
wa chumba cha Melanie
uligongwa akainuka na kwenda
kuufungua alikuwa ni Joyce.
“Madam nimepigiwa simu
na Frimina anasema saa nne na
nusu leo utakuwa na kikao
muhimu na watu kutoka
mamlaka ya mapato.Hivi sasa ni
saa tatu na dakika ishirini”
akasema Joyce
“Mwambie Mina avunje
ratiba yangu nzima ya siku ya
leo.Ninahitaji
kupumzika.Kuhusu hao watu
wa mamlaka ya mapato
amuelekeze GosuGosu
atalishughulikia hilo suala”
akasema Melanie
“Kila kitu kinakwenda sawa
Melanie?akauliza Joyce
“Nimechoka sana nahitaji
kupumzika” akasema Melanie
na Joyce akatoka.
“Mwili wote
umechoka.Safari ya Uganda
ilikuwa ndefu na ngumu.Siku ya
leo natakiwa kushughulikia
safari ya kesho Dubai.Halafu
natakiwa kuonana na balozi
Mapupu ili kuanza maandalizi
ya mpango wangu” akawaza
Melanie na kumpigia simu Joyce
ambaye alifika haraka
“Joyce kesho nina safari ya
kuelekea Dubai.Tafadhali
naomba ushughulikie suala hilo
na asifahamu mtu mwingine
yeyote kama nimekwenda
Dubai.Kuwa makini sana hasa
na hawa wanawake wawili
humu ndani.Usiwaeleze
chochote kuhusu safari
zangu”akasema Melanie
“Sawa Melanie” akasema
Joyce na kutoka ndani Melanie
akaitafuta namba ya simu ya
balozi Mapupu akampigia
“Hallo Melanie” akasema
balozi Mapupu
“Mheshimiwa balozi habari
yako?
“Nzuri
Melanie.Unaendeleaje?Umekwis
ha rejea safari yako ya
Kinshasa?akauliza balozi
Mapupu
“Tayari nimekwisha rejea
nilibanwa na majukumu ndiyo
maana nikashindwa
kuwasiliana nawe”
“Pole sana na
majukumu.Safari yako ilikuwa
na mafanikio?akauliza balozi
Mapupu
“Ndiyo ilikuwa na
mafanikio makubwa sana”
‘Ninafurahi kusikia hivyo”
akasema balozi Mapupu
“Mheshimiwa balozi
nahitaji kukutana nawe kwa
chakula na mazungumzo kama
hutajali” akasema Melanie
“Hakuna tatizo
Melanie.Unataka tukutane lini
na wapi?akauliza balozi
Mapupu
“Nitakukaribisha nyumbani
kwangu leo kama hutajali”
“Ahsante sana Melanie
lakini nyumbani kwako
sipafahamu”
“Usijali balozi utanielekeza
mahala ulipo nitamtuma dereva
wangu atakuja kukuchukua na
kukuleta mahala nilipo”
akasema Melanie
“Sawa tutawasiliana hapo
baadae”akasema balozi Mapupu
na kukata simu
“Uzuri huu nilio nao
umekuwa ni kama sumaku
ambayo inavuta kila
mwanaume
ninayemuhitaji.Tayari ninaye
GosuGosu,na sasa ni balozi
Mapupu.Kumkaribisha
nyumbani kwangu ameona ni
nafasi ya dhahabu hakuwa
ametegemea kabisa bila kujua
kwamba taratibu anajipeleka
katika mdomo wa Mamba”
akawaza Melanie na kuendelea
kulala
AMMAN – JORDAN
Mathew Mulumbi aliwahi
kuamka asubuhi na kuoga
akajiweka tayari kwa kile
kitakachojiri siku hii.Daktari
alifika mapema na kulitibu
jeraha lake mkononi na ilipofika
saa mbili za asubuhi
muhudumu akafika akiwa na
kanzu nzuri nyeupe Mathew
akavaa na kuchukuliwa
akapelekwa katika jumba
kubwa la Rayan Jaber
akakaribishwa katika chumba
maalum kwa ajili ya kifungua
kinywa.Kulikuwa na meza ya
duara ambayo iliwekwa vyakula
mbali mbali kwa ajili ya mlo wa
asubuhi.Muda mfupi baadae
Rayan Jaber akaingia.Siku hii
alikuwa amevaa kanzu nyeupe
“As salaam Alaikum Abu
Zalawi” akasema Rayan.
“Wa alaikum salaam”
Akajibu Mathew
“Vipi maendeleo yako?
“Ninaendelea vizuri
Rayan.Nashukuru sana kwa
kunikaribisha na nimepata
huduma nzuri” akasema
Mathew
“Nimepata heshima kubwa
kwa uwepo wako hapa kwangu
na mimi nashukuru sana”
akasema Rayan huku
wakiendelea kupata kifungua
kinywa
“Mwili wa Seif unaandaliwa
hivi sasa kwa ajli ya
kusafirishwa.Tukimaliza hapa
tutaelekea moja kwa moja
uwanja wa ndege tayari kwa
safari.Tungeweza kuuandaa
hapa kwa kila kitu lakini
hatuwezi kufanya hivyo hadi
pale Habiba atakapouona mwili
wa mwanae ndipo taratibu
nyingine za mazishi
zitaendelea” akasema
Walipomaliza kifungua
kinywa Rayan akamchukua
Mathew na kumpeleka katika
chumba cha mapumziko
akamtaka apumzike na atarejea
baada ya muda mfupi.Dakika
kumi baadae Rayan akarejea na
kumtaarifu Mathew kwamba
kila kitu tayari na wanaweza
kuondoka.Waliingia katika gari
la kifahari la Rayan na kuelekea
katika uwanja wa ndege uliopo
kwenye kijiji cha Rayan.Ndege
tatu za bilionea Rayan
zilikuwepo pale
kiwanjani.Mwili wa Edger
ambao uliwekwa katika jeneza
maalum ukaingizwa katika
mojawapo ya ndege kisha
Rayan na Mathew pamoja na
walinzi wa Rayan wakaingia
ndegeni na baada ya muda
mfupi ikapaa na kuondoka.
TEL AVIV – ISRAEL
Efraim Dagan aliingia
katika ofisi ya mkurugenzi
mkuu wa Mossad Moshe
Levine.Uso wake ulionyesha
alikuwa na mzigo wa
mawazo.Akaketi katika kiti
kilichokuwa mbele ya meza ya
Moshe
“Efraim kuna taarifa gani
mpya? Akauliza Moshe
“Tumempotezaje Mathew
Mulumbi” Akasema Efraim
“Nini
kimetokea?Tumempotezaje?aka
uliza Moshe
“Tulimfikisha Mathew
mpakani kama tulivyokuwa
tumekubaliana na akakutana na
watu wale kama alivyokuwa
ameeleza na safari ya kuelekea
Amman ikaanza.Majasusi wetu
walioko upande wa Jordan
walishika usukani na kuendelea
kumfuatilia na sisi tukiendelea
kumfuatilia kwa kutumia kile
kifaa tulichomuwekea
mkononi.Baada ya kuingia
Amman gari la akina Mathew
likaelekea Advaclinic ambayo
inajishughulisha na vipimo
mbalimbali.Watu wetu
walishindwa kuona kilichokuwa
kinafanyika kutokana na hiyo
mvua kubwa.Baada ya gari za
akina Mathew kuondoka
waliingia ndani ya hospitali
lakini hawakuweza kumpata
Mathew wala mwili wa Edger
Kaka japo vile vifaa viliendelea
kutuonyesha kuwa walikuwa
katika maeneo hayo ya
hospitali.Ililazimu kuomba
msaada kwa wenzetu wa Jordan
na asubuhi ya leo nimepata
majibu.” Efraim akanyamaza
kisha akaendelea
“Uchunguzi umefanyika na
ndani ya kliniki hiyo hakuna
mwili wowote uliopatikana wa
Mathew au Edger.Taarifa
inasema kwamba waliua
walinzi watatu ndipo
walipoweza kuingia ndani ya
hospitali.Walichokifanya ndani
ya hospitali walikwenda hadi
katika chumba chenye mashine
ya MRI na rekodi zinaonyesha
kwamba waliitumia mashine
hiyo.Nadhani umekwisha
fahamu ni kitu gani walikusudia
kukifanya”
“Walitaka kuona kama kuna
vifaa vyovyote tumeviweka
katika mwili wa Edger Kaka na
walipogundua wakakiondoa
pamoja na kile cha Mathew
ndiyo maana tukaendelea
kuviona vifaa vile vile pale
hospitali.Mathew ametoweka
na hatujui mahala alipo”
akasema Efraim.Moshe
akainamisha kichwa
“Kama wameweza
kugundua Mathew alikuwa na
kifaa mwilini hawatamuacha
salama lazima watakwenda
kumuua.Tuombe msaada kwa
vyombo vya Jordan watusaidie
kutupa taarifa kama kuna mtu
yeyote ataripotiwa kuuawa.
Jambo lingine,siku zote
tumekuwa tukiamini kwamba
Habiba anaishi Saudi Arabia
lakini ukifuatilia taarifa ya
Mathew alidai kukutana na
Sayid Omar ambaye ni mtu wa
karibu sana na Habiba nchini
Jordan na nina uhakika hata
Habiba alikuwa Jordan
alipozungumza naye ndiyo
maana nashawishika kuamini
kwamba tukiwekeza nguvu
nchini Jordan tunaweza
kumpata Habiba Jawad au hata
kuufahamu mtandao
wake.Hatua aliyopiga Mathew
ni kubwa sana ametufungulia
dirisha ambalo tukilitumia
vyema basi tutapiga hatua
kubwa” akasema Moshe Levine.
“Ulichokisema hata mimi
nilikuwa nakiwaza kuna
uwezekano mkubwa Habiba
Jawad akawa na makazi yake
nchini Jordan lakini inabidi
suala hilo tulichunguze
wenyewe bila kuwashirikisha
Jordan kwani Habiba mtandao
wake unaweza kuwa
mkubwa.Kuhusu Mathew
Mulumbi bado nina imani
naye.Kuna kitu ndani yangu
kinanifanya niendelee kuamini
kwamba yawezekana akawa
hai.Tusikate tamaa
mapema.Hata wakati ule
tulikata tamaa lakini amekuja
kuibuka na kumbe yeye ndiye
aliyemuua Ammar Nazari.Japo
mazingira yanaonyesha kuna
uwezekano mkubwa wa
Mathew akaenda kuuawa lakini
tusikate tamaa” akasema Efraim
RIYADH – SAUDI ARABIA
Ndege waliyopanda akina
Mathew ilitua katika uwanja
mdogo wa ndege unaomilikiwa
na familia ya Habiba
Jawad.Rayan akamtangulia
Mathew kushuka ndegeni.Nje
kulikuwa na watu zaidi ya
ishirini na magari saba yote
yakiwa na rangi nyeusi.Watu
kadhaa wakaingia ndegeni na
mwili wa Mathew Mulumbi
ukashushwa na kuingizwa
katika gari maalum kisha
magari yale yakaondoka pale
uwanjani.Katika watu wale
wote waliowakuta pale
uwanjani hakuna hata mtu
mmoja ambaye Mathew
alimfahamu.Mathew alikuwa
mgeni katika jiji la Riyadh hivyo
hakujua walikuwa wanaelekea
wapi.
“Hawa jamaa utajiri wao ni
wa kufuru.Wana ndege zao
binafsi na wana viwanja vyao
vya ndege.Bado nina safari
ndefu na ngumu ya kumfahamu
vyema Habiba Jawad ni mtu wa
aina gani na ninapoendelea
kumfahamu Habiba Jawad
siwezi kuwaacha watu wake wa
karibu.Mmoja ni huu Rayan
Jaber.Utajiri wake
unatisha.Mambo niliyoyaona
nyumbani kwake hatujazoea
kuyaona nchini kwetu.Mimi ni
tajiri….Oh my God nimejisahau
sipaswi kujiita
bilionea.Nilikuwa bilionea na
ninawafahamu mabilionea
wengi nchini kwetu hawana
maisha ya kufuru kama ya
Rayan.Hadi vikombe vya
kunywea chai ni vya dhahabu !
akawaza Mathew na kutazama
nje
“Kwa hiki nilichokifanya
cha kuuleta mwili wa Edger
Kaka kitaniweka karibu zaidi na
Habiba Jawad.Kingine
kitakachoniweka karibu yake
zaidi ni pale nitakapokubali
kumuoa mwanae Najma kama
alivyokuwa amenitaka.Lakini ni
vipi kama nitajikuta
nikimpenda huyo Najma na
kujikuta nikianza maisha mapya
huku na kusahau misheni
yangu? Ni hiki ndicho
anachokitaka Habiba Jawad?
Nini hasa malengo yake kwangu
na kwa Nawal? Akajiuliza huku
msafara ule ukienda kwa kasi
Dakika zipatazo ishirini
wakawasili katika geti moja
kubwa lililokuwa linalindwa na
walinzi wanne.Geti lilikuwa
limefunguliwa na msafara ule
wa magari ukaingia
ndani.Kulikuwa na majumba
kadhaa makubwa na mengine
madogo na yote yakiwa
yamepakwa rangi
nyeupe.Barabara zote za
kuelekea katika majumba yale
zilijengwa vizuri kwa
lami.Kulipandwa miti ya maua
mazuri bila kusahau taa za
barabarani.Kilionekana kama
kijiji kidogo lakini si kama kile
cha Rayan Jaber.Mathew
aliyekuwa amepanda gari moja
na Rayan wakashuka.Kulikuwa
na watu wamejipanga kwa ajili
ya kuwapokea.Mtu wa kwanza
kukutana naye alikuwa ni Abu
Dahir mtoto wa Habiba
“Abu Zalawi ahsante sana
kwa kumrejesha nyumbani
ndugu yangu” akasema Abu
Dahir.Kisha Mathew
akasalimiana na Sayid Omar na
watu wengine waliopata
ishirini.Mwili ukashushwa
garini na kubebwa ukapelekwa
katika jumba moja kubwa jeupe
ukawekwa katika chumba
maalum na baada ya muda
mfupi Habiba Jawad akaingizwa
akiwa ameshikwa na akina
mama wawili.Hakuwa na
nguvu.Macho yake yalikuwa
mekundu.Akasogezwa karibu
na jeneza likafunguliwa
akamuona mwanae Edger au
Seif Jawad.Habiba alimwaga
machozi mengi akiwa ameweka
mikono yake katika kichwa cha
mwanae.Aliporidhika akatoa
ruhusa taratibu nyingine za
mazishi ziendelee.
Mathew na watu wengine
waliokuwamo ndani ya jumba
lile kubwa wakatoka na kwenda
katika sehemu kulikoandaliwa
hema kubwa na ambako
kulikuwa na watu wasiozidi mia
mbili.Sayid Omar aliyekaa
pembeni mwa Mathew
akamshika mkono na kumtaka
amfuate wakaenda sehemu
Fulani kwa ajili ya
mazungumzo.
“Abu Zalawi wakati
maandalizi yakiendelea
nimeona tuzungumze
kidogo.Kwanza kabisa pole sana
kwa safari ndefu hadi
kuufikisha mwili hapa.Najua
haikuwa rahisi”
“Ni kweli Sayid.Haikuwa
kazi nyepesi”
“Nimejulishwa na Bashar
kuhusu mlichokifanya pale
Amman.Nakupongeza ulikuwa
ni ujasiri mkubwa
sana.Umefanya kitu kikubwa
mno na hata Habiba Jawad
amekushukuru mno” akasema
Sayid
“Habiba tayari anajua
kilichotokea Amman?akauliza
Mathew
“Ndiyo.Utaratibu wetu hapa
lazima ajulishwe kila
kinachotokea.Tayari anajua na
akipata muda wa kuonana nawe
baadae atakupa shukrani
zake.Ulifahamuje kama mwili
wa Edger umewekewa kifaa
maalum? Akauliza Sayid Omar
“Mossad wanamtafuta sana
Habiba Jawad na wanajua Edger
Kaka ni mtu wake wa muhimu
hivyo kwa namna yoyote ile
wasingeweza kumuacha hivi
hivi lazima wangemuwekea
kifaa maalum.Nimekuwa
nikipambana na Mossad kwa
muda mrefu hivyo
ninawafahamu vyema” akasema
Mathew na mara vin’gora
vikasikika na msafara wa
magari ya kifahari ukaingia
“Huyo ni mwana mfalme
wa Saudi Arabia amekuja
kuungana nasi.Mfalme wa
Saudia ni rafiki sana na Habiba
hivyo amemtuma mwanae kuja
kumuwakilisha.Vile vile
mwanamfalme huyu ni rafiki
mkubwa wa Abu
Dahir.Tutazungumza baadae
ngoja nikampokee” akasema
Sayid Omar na kwenda
kumpokea mwana
mfalme,Mathew akarejea
kuungana na waombolezaji
wengine.Mwana mfalme
alipokelewa na Sayid Omar na
Abu Dahir na moja kwa moja
akapelekwa katika chumba
alimokuwamo Habiba Jawad
akampa pole na salamu za
mfalme kisha akapelekwa
sehemu waliko waombolezaji
wengine akaungana nao.Wengi
wa waliokuwepo katika msiba
ule walionekana ni watu wenye
uwezo mkubwa
kifedha.Walikaa kimakundi
wakizungumza wakati
wakisubiri mwili wa Edger
uandaliwe kwa ajili ya
mazishi.Ni Mathew pekee
ambaye hakuwa na mtu wa
kuzungumza naye alikuwa peke
yake.Alionekana tofauti na
wengine wote kwanza kwa
rangi na hata kwa
muonekano.Mabilionea wale
hawakujua kama walikuwa
wamekaa na mtu hatari
sana.Wakati wengine
wakiendelea na mazungumzo
yao huku wahudumu wakipita
na kugawa sahani za vitafunwa
mbali mbali Mathew alikuwa
mbali sana kimawazo.Aliwaza
mambo mengi sana kuhusu
mustakabali mzima wa maisha
yake.
Mwili wa Edger uliandaliwa
na kuletwa kwa waombolezaji
kwa ajili ya taratibu za
ibada.Imamu aliongoza swala
na taratibu nyingine kisha
mwili ukachukuliwa kupelekwa
katika makaburi.Taratibu mwili
ukaingizwa kaburini na
kuzikwa.
“Mwisho wa Edger Kaka
ndio mwanzo wa Habiba
Jawad.Haijalishi nitatumia
miaka mingapi lakini lazima
kwa namna yoyote ile Habiba
Jawad na mtandao wake
wapotee.Yawezekana
nikashindwa kutimiza malengo
yangu ya kuwaangamiza
wafadhili hawa wa ugaidi
duniani lakini
nitajaribu.Nitakufa nikijaribu”
akawaza Mathew wakati kaburi
la Edger Kaka likifukiwa.
Baada ya shughuli ya
mazishi kumalizika
waombolezaji wakarejea katika
sehemu zao.Mwana mfalme
hakukaa sana akawaaga
waombolezaji akaondoka
zake.Chakula kiliandaliwa
waombolezaji wakala na kisha
wakaanza kuondoka mmoja
mmoja.Abu Dahir akamchukua
Mathew na kumpeleka katika
nyumba Fulani ndogo
“Abu Zalawi natumai
tutapata nafasi ya kuzungumza
zaidi lakini kwa sasa ninapenda
nikushukuru kwa mara
nyingine tena kwa kitendo hiki
ulichokifanya cha kuuleta
nyumbani mwili wa kaka yangu
Seif.Tumehangaika kwa muda
mrefu sana kumtafuta.Hadi
tunampumzisha leo Seif
amepitia magumu mengi
sana.Kwa ufupi tu ni kwamba
Seif alikuwa akiishi nchini
Tanzania na alikuwa ni
mbunge.Alikuwa na maadui
wengi hivyo aliwekewa sumu
kwa lengo la kumuua lakini kwa
bahati nzuri akapona katika
jaribio hilo.Baada ya kupona
ikatokea ajali ambayo
tulitangaziwa kwamba
amefariki dunia lakini baadae
tukagundua kwamba yuko hai
na tukaanza harakati za
kumtafuta.Niliwahi kufika hadi
Tanzania kukutana na
mwanadada mmoja anaitwa
Olivia Themba nikiwa katika
harakati za kumtafuta
Seif.Mambo mengi yalitokea
hadi usiku ule ambao Seif
alitakiwa kukabidhiwa kwetu
na serikali ya Tanzania lakini
akatekwa na majasusi wa
Israel.Binafsi japokuwa nina
majonzi lakini nina furaha sana
ya kumuona kaka yangu japo
hatukuweza kuzungumza lakini
nimemzika kwa
heshima.Ahsante sana Abu
Zalawi” akasema Abu Dahir
Mathew hakujibu chochote
alikuwa kimya kabisa
“Ninakushukuru vile vile
kwa kumuokoa Nawal kutoka
katika mashambulio ya
Israel.Nadhani
umekwishadokezwa kwamba
ninataka kumuoa Nawal”
akasema Abu Dahir
“Ndiyo.Mama Habiba
amekwisha nijulisha suala hilo”
akasema Mathew
“Kuna tatizo lolote?akauliza
Abu Dahir
“Hakuna tatizo lolote.Nawal
alikuwa ni mke wa kiongozi
wangu Ammar Nazari na mimi
sina tatizo lolote kwa wewe
kumuoa kwani kwa sasa hana
mume”
“Nashukuru sana Abu
Zalawi.Tutaendelea
kufahamiana zaidi kwani kwa
mujibu wa taarifa aliyonipa
mama ni kwamba utaendelea
kukaa nasi hapa.Karibu sana na
jisikie nyumbani”akasema Abu
Dahiri na kuagana na Mathew
baada ya kupigiwa
simu.Mathew naye akatoka na
kurejea mahala walikokuwepo
waombolezaji wengine
akaungana nao.
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Mlio Fulani ulisikika
chumbani kwa Melanie
Davis,akayaelekeza macho yake
katika runinga iliyokuwa
ukutani ambayo iliunganishwa
na kamera zilizokuwa getini na
kuliona gari la Joyce likivuka
geti.Joyce alikuwa ametumwa
kwenda kumchukua balozi
Germinus Mapupu ambaye
Melanie alikuwa amemualika
kwa chakula cha jioni.Melanie
akajitazama na kutabasamu
“Sihitaji kujifanyia
maandalizi makubwa kwani bila
hata kujiremba mimi ni mzuri
na balozi Mapupu tayari
alikwisha onyesha
kuchanganyikiwa mara ya
kwanza tu aliponiona.Wanaume
Mungu aliwapa udhaifu
mkubwa kwa mwanamke”
akawaza huku akikoleza rangi
ya mdomo.
Mlango ukagongwa
akaingia Joyce.
“Tayari mheshimiwa balozi
amekwisha fika” akasema Joyce
“Ahsante Joyce.Mpeleke
katika sebule yangu nitakuja
hapo muda si
mrefu.Msimuhudumie chochote
kwanza hadi nitakapofika
mwenyewe” akasema Melanie
Balozi Mapupu alipelekwa
katika sebule maalum ya
Melanie.Baada ya dakika chache
Melanie akaingia pale
sebuleni.Usiku huu alikuwa
amevaa sketi fupi nyeusi alivaa
pia fulana ya rangi nyeupe
ambayo ilimpwaya iliyokuwa na
shingo pana na kuonyesha kifua
chake kizuri.
“Mr Mapupu” akasema
Melanie kwa sauti yake laini na
kumfuata balozi Mapupu
ambaye alisimama na
kumkumbatia
“Karibu sana mheshimiwa
balozi.Nimefurahi sana
kunitembelea hapa kwangu”
akasema Melanie.Balozi
Mapupu mapigo ya moyo
yalimbadilika baada ya
kukumbatiwa na kimwana Yule.
“Ahsante sana Melanie kwa
kunikaribisha nyumbani
kwako.Siwezi kuelezea furaha
yangu” akasema balozi Mapupu
“Mheshimiwa balozi
unatumia kinywaji gani usiku
wa leo? Akauliza Melanie
“Nitakuomba unichagulie
kinywaji chochote
nitatumia.Kwako siwezi kusema
hapana kwa chochote
utakachonikirimu” akasema
balozi Mapupu na Melanie
akaachia tabasamu pana sana
akainuka na kutoka baada ya
dakika chache akarejea akiwa
na sinia lililokuwa na chupa
kadhaa za mvinyo.
“Mr Mapupu naomba usiku
huu uchague kinywaji
tutakachokitumia” akasema
Melanie na balozi Mapupu
huku akitabasamu akachagua
chupa moja Melanie akamimina
katika glasi mbili na
kumkaribisha
“Kwa ajili ya urafiki wetu”
akasema Melanie huku akiinua
glasi wakagonganisha na kila
mmoja akanywa funda moja
“Balozi naomba kwa mara
nyingine tena nikushukuru kwa
kukubali mwaliko
wangu.Nafahamu una shughuli
nyingi lakini umeacha shughuli
zako zote umekuja kuungana
nami hapa.Ahsante sana”
akasema Melanie
“Melanie ningewezaje
kukataa mwaliko kutoka kwa
mtu muhimu kama wewe? U
mtu muhimu sana kwa nchi
yetu ya Congo.Binafsi ninajihisi
fahari kubwa kuwepo hapa
pamoja nawe usiku huu”
akasema balozi Mapupu
“Vipi kuhusu safari yako
ilikuwa na mafanikio?akauliza
balozi Mapupu na Melanie
akamueleza kwa upana kuhusu
lengo lake la kuwekeza nchini
Congo.Balozi Mapupu alifurahi
sana kwa maelezo hayo
aliyoyatoa Melanie.Baada ya
mazungumzo Melanie
akamkaribisha balozi Mapupu
kwa chakula kizuri
kilichoandaliwa.Baada ya
chakula kile wakaelekea katika
chumba cha mapumziko
“Melanie ninashukuru sana
kwa chakula kizuri
sana”akasema balozi Mapupu
“Ahsante balozi” akasema
Melanie kisha akainuka na
kwenda kuketi karibu na balozi
“Usihofu balozi hapa tuko
peke yetu hakuna mtu
atakayefika hapa”
“Mumeo yuko wapi
Melanie?akauliza balozi
Mapupu
“Mume? Akauliza Melanie
na kutoa kicheko.
“Sina mume”
“Huna mume? Balozi
Mapupu akashangaa
“Ndiyo sina mume.Ni ajabu
kukosa mume?akauliza
“Si ajabu lakini kwa
mrembo kama wewe kwa nini
ukose mume?
“Nimeamua nikae hivi
kwanza hadi hapo baadae”
akasema Melanie huku
akitabasamu
“Lakini mara moja moja
nimekuwa nikitoka na
wanaume mbali mbali lakini
sitaki ule urafiki wa kudumu”
akasema Melanie na balozi
Mapupu akawa kimya
‘Balozi Mapupu kuna jambo
nataka kulileta kwako kama
utaona inafaa”
“Omba Melanie chochote”
“Si ombi bali ni pendekezo”
“Nitalipokea kwa mikono
miwili” akasema balozi Mapupu
“Mkutano mkubwa wa
wake za marais unatarajiwa
kufanyika hapa Tanzania wiki
ijayo.Nchi ya Congo na Rwanda
kwa sasa hazina mahusiano
mazuri.Kama Tanzania
wameweza kuandaa mkutano
huu mkubwa na kuwakaribisha
wake za maraisi kutoka duniani
kote kwa nini wewe na balozi
mwenzako wa Rwanda
msiitumie fursa hii kuwaweka
karibu wake za marais wa
Rwanda na Congo? Mnaweza
kuandaa chakula cha jioni
mkawaalika wote wakakutana
na kuzungumza.Huo utakuwa ni
mwanzo mzuri wa kuleta amani
katika nchi zao.Kama akina
mama hawa wakielewana na
kuzungumza lugha moja basi
watakwenda kuzungumza na
waume zao na mambo yatakaa
sawa”akasema Melanie
“Melanie una akili sana.Hilo
ni wazo zuri mno na sikuwa
nimelifikiria kabisa.Ahsante
kwa kunipa wazo kama hilo
ambalo kama likifanikiwa ni
kweli linaweza kuwa chanzo
cha amani kwa nchi zetu hizi
mbili.Ni kweli nchi ya Congo na
Rwanda kwa sasa hazina
mahusiano mazuri.Maraisi
hawa wawili wamekuwa katika
vita ya maneno nadhani
mkutano huu unaweza ukawa
ni chachu ya kuondoa vita ya
maneno ya marais hawa
wawili.Jambo hilo
linawezekana.Kumpata Rebeca
Eyenga mke wa Rais wa Congo
si kazi ngumu na nina uhakika
lazima atakubali mwaliko
wangu lakini kazi itakuwa
katika kumpata mke wa Rais wa
Rwanda.Kama unavyofahamu
msuguano uliopo umepelekea
hata sisi mabalozi ambao
tunaziwakilisha nchi zetu hapa
tusiwe na mahusiano
mazuri.Mimi na mwenzangu wa
Rwanda hatuna maelewano
mazuri” akasema balozi
Mapupu
“Nalifahamu hilo ndiyo
maana nikashauri kwamba
mkutano huu utumike katika
kuleta amani.Wewe na
mwenzako wa Rwanda
mtaanzisha maelewano,wake za
marais wataelewana na
kitakachozaliwa hapo ni marais
wa Rwanda na Congo
kuelewana.Mimi nitagharamia
kuandaa chakula hicho kwa kila
kitu wewe kazi yako itakuwa ni
kutafuta namna ya
kuwakutanisha wake hawa za
marais” akasema Melanie
“Ahsante sana Melanie kwa
kulileta wazo hili na hata
kujitolea kugharamia jambo hili
kubwa.Ubalozi wangu
hautakuwa na maana kama
nitashindwa kuitumia nafasi hii
kusaidia kuleta amani katika
nchi zetu.Ninakuahidi nitafanya
kila kitu kwa ajili ya
kuhakikisha ninawaleta mezani
wanawake hawa.Hata hivyo
kuna wazo nimelipata” akasema
balozi Mapupu na kunyamaza
kidogo
“Umepata wazo gani
mheshimiwa balozi?akauliza
Melanie kwa sauti laini na
kuupeleka mkono wake katika
tai ya balozi Mapupu
“Ili jambo hili lifanikiwe
anahitajika mtu wa tatu ambaye
anaweza akawaleta wanawake
hawa katika meza moja na
kuwaunganisha”
“Unadhani nani anayeweza
kuifanya kazi hiyo ya
kuwaweka wanawake hawa
mezani na wakazungumza?
Akauliza Melanie
“Millen Kelelo mke wa Rais
wa Tanzania.Yeye ndiye
muandaaji wa mkutano na
ndiye anayeweza kuwaalika
wanawake hawa kwa pamoja na
wakajikuta sehemu
moja.Hawataweza kukataa
mwaliko wake”akasema balozi
Mapupu
“Hilo ni wazo zuri sana
mheshimiwa balozi”
“Melanie mambo ya
mheshimiwa ni pale
tunapokuwa kazini lakini nje ya
hapo niite Mr Mapupu inatosha”
“Mr Mapupu hilo ni wazo
zuri sana kumshirikisha mke
wa Rais wa Tanzania.Pamoja na
kumshirikisha huko lakini iwe
ni katika kuwaleta mezani
wanawake hao tu.Hatuwezi
kumbebesha mzigo wa kuandaa
chakula hicho kwani
amekwisha tumia fedha nyingi
kuandaa mkutano mkubwa”
akasema Melanie
“Usijali kuhusu hilo
Melanie.Sisi tutaandaa kila kitu”
“Maandalizi yaanze mara
moja.Kutana na bi Millen
uzungumze naye kuhusu nia
yako hiyo na nina uhakika
hawezi kukataa na baada ya
hapo utatafuta ni sehemu gani
ambako unadhani panaweza
pakafaa kwa kufanyia jambo
hilo pamoja na gharama
nyingine zote.Mimi
nitagharamia kila
kitu,nitawaleta wapishi wa
kimataifa wenye uwezo wa
kupika kila aina ya
chakula,tutaandaa pia burudani
kadhaa ili kunogesha usiku
huo.Utakuwa ni usiku wa aina
yake na mambo makubwa
lazima yafanyike usiku
huo.Naipenda sana nchi yangu
na ninapenda kuiona ikiwa na
amani bila mikwaruzano na
majirani zake hivyo ni jukumu
letu mimi na wewe kuhakikisha
kwamba tunalifanikisha jambo
hili na baada ya hapo hakuna
ajuaye pengine mimi nawe
tunaweza kupata nafasi nzuri
zaidi ya kujipongeza kwa kazi
kubwa tuliyoifanya” akasema
Melanie huku akiuchukua
mkono wa Mr Mapupu
akaushika na kuuweka katika
paja lake.
“Melanie
tutafanikiwa.Kesho asubuhi
kazi yangu ya kwanza ni
kwenda katika ofisi ya mke wa
Rais na kuzungumza naye juu
ya jambo hili na halafu
nitakujulisha majibu yake.Nina
uhakika hawezi kukataa jambo
jema kama hili.Nakuhakikishia
Melanie hata kama mke wa Rais
wa Tanzania hatatuunga mkono
katika jambo hilo mimi binafsi
nitafanya kila njia ili wanawake
hawa waweze kukaa meza
moja”
“Nitashukuru sana balozi
kama utalifanikisha hilo na
kama nilivyokuahidi kwamba
baada ya kufanikisha jambo hilo
mimi nawe tutapata nafasi
nzuri ya kupongezana” akasema
Melanie
“Tunaweza kuanza
kupongezana kwani jambo hili
hesabu limekwisha na
limefanikiwa” akasema balozi
Mapupu na Melanie
akatabasamu
“Kwa leo haitawezekana
mheshimiwa balozi.Vuta subira
hadi hapo tutakapofanikisha
jambo hili kubwa”
“Kuna mtu yeyote anakuja
hapa kwako usiku huu?
“Hakuna yeyote anayekuja”
“Kwa nini basi
tusipongezane kwa kuanzisha
urafiki huu mkubwa? Niruhusu
mimi nikupongeze kwa kunipa
wazo zuri kabisa ambalo hata
mimi sikuwa nalo” akasema
balozi Mapupu
“Usijali Mr
Mapupu.Tutapata wasaa mzuri
zaidi wa kupongezana baada ya
kumaliza shughuli hiyo
muhimu.Isitoshe kwa siku ya
leo sitaki kuchoka kwani kesho
nina safari ya Dubai”
“Unakwenda Dubai?
“Ndiyo.Ninakwenda
kuhudhuria kikao cha biashara”
“Utatumia siku ngapi huko?
“Siku mbili nitakuwa
nimerejea nyumbani”
“Utakaporudi uwasiliane
nami ili nikupe mrejesho”
“Nitafanya hivyo
balozi”akasema Melanie
“Hata hivyo kuna kitu
nataka kukuomba Mr Mapupu”
“Omba chochote Melanie”
“Sitaki kujulikana kama
nimejitolea kugharamia jambo
hili.Naomba uhusika wangu
uwe wa siri.Nitagharamia kila
kitu lakini nataka ionekane
wewe ndiye uliyegharamia kwa
fedha zako” akasema Melanie
“Kwa nini hutaki
kutambulika kama sehemu ya
mafanikio makubwa
yatakayopatikana?
‘Sipendi sana kujulikana na
isitoshe nataka sifa zote zije
kwako Mr Mapupu” akasema
Melanie
“Basi usihofu.Nitalizingatia
ombi lako.Hakuna atakayejua
kama wewe ndiye
uliyefanikisha kila kitu”
Waliendelea na
mazungumzo hadi ilipofika saa
tano za usiku balozi Mapupu
akaondoka..
“Ameongozeka Millen
Kelelo.Balozi yuko sahihi
kumtumia Millen
kuwakutanisha wanawake hao
wawili.Naamini Millen
akiwaalika katika chakula usiku
huo hakuna anayeweza
kukataa.Kama Millen
atahudhuria sherehe hiyo
lazima naye awe miongoni mwa
watakaouawa.Yatakuwa ni
mauaji makubwa yatakayoibua
mzozo mkubwa ndanio ya
jumuiya ya Afrika
Mashariki.Taratibu itaanza
kumeguka.Marais Fabian Kelelo
na Patrice Eyenga watapata
uchungu usioelezeka.Machozi
yangu ninayomwaga kila siku
kuwalilia wazazi wangu
yataondoka na wengi” akawaza
Melanie
RIYADH – SAUDI ARABIA
Karibu watu wote
waliohuduhuria mazishi ya
Edger Kaka walikwisha ondoka
na waliobaki ni familia ya
Habiba Jawad.Sayid Omar
ambaye alikuwa na pilika pilika
sana siku hii akamfuata Mathew
aliyekuwa amekaa na watu
wengine wakicheza karata
akamtaka amfuate
“Samahani sana Abu Zalawi
usione kama tumekuacha peke
yako ni kutokana na heka heka
nyingi siku ya leo.Kama
unavyoona wageni wanakuja na
kuondoka na mimi ndiye
ninayewapokea wote”
“Usijali Sayid Omar
ninaelewa.Pole sana kwa
jukumu hilo gumu” akasema
Mathew
“Habiba anataka
kuzungumza nawe.Hakuweza
kupata nafasi ya kuzungumza
nawe mchana kutokana na
kutingwa sana” akasema Sayid
Omar na kumpeleka Mathew
katika nyumba alimo Habiba
Jawad.Alikuwa katika chumba
kimoja cha ukubwa wa wastani
akiwa na akina mama wengine
watano waliokuwa
wakimsaidia.Sayid Omar na
Mathew walipoingia Habiba
akawataka wale akina mama
waliokuwa naye watoke
anataka kufanya mazungumzo
“Karibu sana Abu Zalawi”
akasema Habiba Jawad
“Ahsante mama.Pole sana”
akasema Mathew na kupiga
magoti akamsalimu Habiba kwa
adabu.
“Sayid waambie
watuandalie bustanini.Mimi
hupenda sana kufanya
mazungumzo bustanini”
akaelekeza Habiba na Sayid
akatoka
“Sikupata muda wa
kuzungumza nawe kutokana na
wageni wengi waliokuwa
wakija na kuondoka.Uliowaona
leo ni watu wachache tu
waliofahamu na wengine sijui
wamefahamu vipi,suala hili
niliwaeleza watu wachache
sana nashangaa taarifa
zilivyosambaa lakini
nawashukuru wote waliofika
kwa mapenzi mema na
kunisaidia kumhifadhi
mwanangu kwa heshima
zote.Mfalme wa Saudi Arabia
alitaka kuja mwenyewe lakini
nilimwambia anaweza akatuma
mwakilishi akamtuma
mwanae.Mfalme wa Jordan
naye ananilaumu sana kwa
kutomjulisha jambo hili.Kwa
ufupi ….” Habiba akanyamaza
baada ya mtu mmoja kuingia
mle ndani akamjulisha kwamba
tayari bustanini kumeandaliwa.
“Abu twende tukakae
bustanini tuzungumze mimi
hupenda sana kuzungumzia
bustanini” akasema Habiba
wakatoka na kuelekea bustanini
kulikokuwa na sehemu maalum
ambayo Habiba hupenda
kupumzika kila jioni.
“Mathew Mulumbi”
akasema Habiba
“Naam mama” akaitika
Mathew
“Nitakuita kwa jina lako
pale tukapokuwa wawili tu tena
sehemu kama hii ambako
hakuna ambaye anasikiliza
maongezi yetu.Ukiacha Nawal
ni mimi pekee ambaye
ninafahamu wewe ni
nani.Tukiwa katika maisha ya
kawaida utaendelea na jina lako
la Abu Zalawi na ndilo
utakalotumia katika maisha
yako yote utakayoishi hapa”
akasema Habiba na ukimya
ukapita
“Mathew kwanza kabisa
napenda nikushukuru sana kwa
kazi kubwa uliyoifanya ya
kuniletea mwanangu.Nimelia
sana lakini nimefurahi kuweza
kumzika mwanangu mimi
mwenyewe kwani kule Israel
angezikwa kama
mzoga.Ahsante sana kwa
hilo.Mimi na familia yangu yote
tumefurahi sana na kwa niaba
yao nakushukuru sana.”
Akasema Habiba
“Naamini haikuwa rahisi
kuuleta mwili wa Seif lakini
umepambana na ukafanikiwa
kuufikisha hapa
nyumbani.Mossad waliuwekea
mwili ule kifaa maalum cha
kuwawezesha kuufuatilia na
kujua unaelekea wapi.Wewe pia
uliwekewa kifaa katika mkono
wako wa kushoto hapo mahala
penye jeraha.Nilikuwa na
taarifa hizi kabla hata
hujaondoka Israel.Nilifahamu
kila ulichowaeleza Mossad
katika kikao mlichojadili
kuhusu kuutumia mwili wa
Edger Kaka kufahamu mahala
nilipo” akasema Habiba na
kucheka kidogo.
“Nimefurahishwa sana na
kile ulichokifanya.Ngoja
nikuweke wazi Mathew
kwamba huu ulikuwa ni
mtihani wako wa kwanza na
umefaulu.Kwanza kwa namna
ulivyowashawishi viongozi wa
Mossad na wakakuelewa
wakakupa mwili wa Seif,pili ni
namna ulivyoweza kupambana
hadi ukafanikiwa kuondoa kifaa
kile katika mwili wa
Seif.Nimekwambia kwamba
nilifahamu kuhusu kifaa
kilichowekwa katika mwili wa
Seif na nilitaka kuona
ungefanya nini.Je ungekubali
mwili ule wa Edger uje na kifaa
kile na kuwapa nafasi Mossad
ya kufahamu mahala nilipo?
Hukuacha hilo litokee na
ukapambana kuhakikisha
unakiondoa kile kifaa.Endapo
ungechagua kushirikiana na
Mossad basi ungekuwa ni
mwisho wako kwani usingefika
kokote.Umewasaliti wenzako
waliokuamini kwa ajili
yangu.Hili ni jambo kubwa sana
umelifanya.Umeweka mbele
maisha yako kwa ajili yangu na
kuhakikisha mwili wa Seif
unafika nyumbani ukiwa safi na
salama.Ahsante sana kwa hilo.
Wewe ni mtu mahiri
sana.Umeiva katika kazi yako.Ni
majasusi wachache sana
wanaofikia uwezo wako”
akasema Habiba na Mathew
alihisi fulana yake aliyoivaa
ndani ikiloa jasho.
“Huyu mama anazidi
kunichosha.Kama ameweza
kufahamu kila nilichozungumza
na Mossad ni mtu wa namna
gani huyu?Ni binadamu wa
kawaida kweli huyu? Ninajiuliza
kwa sababu mambo yake
yananishangaza sana.Au
anatumia nguvu za
giza?Mathew akajiuliza maswali
“Mathew nataka kufahamu
kwa nini uliamua kufanya vile
ulivyofanya? Nakuuliza hivyo
kwa sababu umepita njia
ngumu sana hadi
kunifikia.Ulikubali kufanya
jambo la hatari sana la
kumtorosha Ammar Nazari
gerezani na ukajiunga na kundi
lake yote hiyo ikiwa ni kwa ajili
ya kutafuta njia ya kufika
kwangu.Nafahamu maisha
ndani ya Ammar Nazari
brigades hayakuwa rahisi na
kama hitoshi bado ukaenda
kulipua lile bomu kule Israel na
kuua watu.Yote hii ni katika
kuhakikisha unatengeneza
mazingira ya kuweza kufika
mahala nilipo.Umelipa gharama
kubwa sana kufika hapa
ulipofika.Ulikuwa na uwezo wa
kuwaeleza Mossad kila kitu
kuhusu mimi na namna
wanavyoweza kunifikia lakini
hukufanya hivyo.Ilikuwa ni
nafasi yako ya dhahabu
kuhitimisha misheni yako lakini
hukufanya hivyo badala yake
ukawapa taarifa za uongo
kuhusu mimi na
wakakuamini.Kwa nini ulifanya
hivyo? Akauliza
Habiba.Ilimchukua Mathew
muda kidogo kutafakari kisha
akasema
“Hata mimi sielewi kwa nini
nilifanya vile” akasema Mathew
na Habiba akatabasamu kwa
mbali.Kimya kifupi kikapita
halafu Habiba akasema
“Mathew ngoja
nikufahamishe kitu kimoja cha
muhimu.Hukuweza kufanya
hivyo kwa sababu hapa ndipo
mahala unapotakiwa
kuwepo.You belong here !
akasema Habiba na Mathew
akatoa kicheko.
“Unanifurahisha
mama.Hapa ndipo sehemu
ninapotakiwa kuwa? This is not
my place.I don’t belong to
terrorists” akasema Mathew
“Mathew bado una mengi
ya kujifunza” akasema Habiba.
“Nini hasa unakitafuta
kwangu mama Habiba?akauliza
Mathew
“Ninachokitafuta kwako?
Habiba akauliza
“Ndiyo.Umenieleza namna
nilivyopita njia ngumu kwa ajili
ya kutaka kufika kwako na
lengo langu likiwa moja tu
kukuua.Kama ulilifahamu lengo
langu na ulikuwa na uwezo wa
kuniua kwa nini hukuniua?Kwa
nini ukanikaribisha mimi adui
yako katika makazi yako?Una
uhakika gani kwamba
sintabadilika kesho na kukuua?
Akauliza Mathew na Habiba
akacheka kidogo
“Sikuelekeza uuawe kwa
sababu ninafahamu hapa ndipo
mahala unapotakiwa
uwe.Kuhusu kuniua huwezi
kufanya hivyo si leo,kesho wala
kesho kutwa.Sikiliza Mathew
nimempoteza mtoto wangu wa
kwanza and I need you as my
son”
“Me ?
“Yes you” akajibu Habiba
“Hilo haliwezekani.Siwezi
katu kuwa mtoto wako.Mimi
siko katika dunia ya ugaidi”
akasema Mathew
“Unasema hivyo kwa
sababu bado mambo mengi
huyafahamu Mathew.Nataka
nikufumbue macho yako na
kukuonyesha dunia ambayo
huifahamu.Kuna mambo
makubwa ambayo huyajui na
siku ukiyajua utashangaa
hutaamini macho
yako.Nitakupeleka
huko.Nitayabadili maisha yako
na utakuwa mtu mkubwa”
“Sihitaji kuwa mtu
mkubwa.Maisha niliyonayo sasa
yananitosha” akasema Mathew
“Haya si maisha yako
Mathew.Maisha yako ni
makubwa zaidi ya
unavyofikiri.Kwa kuanzia…..”
Habiba akanyamaza kidogo
kupisha helkopta iliyopita
maeneo yale na kusababisha
kelele
“Helkopta hii hufanya doria
katika eneo hili kila siku
kuhakikisha hakuna hatari
yoyote.Hii pia ni salamu kutoka
kwa mfalme” akasema Habiba
na helkopta ilipopita
akaendelea
“Nilikuwa nakueleza
kwamba utajiri wangu
niliugawa katika sehemu
nne.Kila mtoto wangu alikuwa
na sehemu yake ya utajiri na
sehemu moja ilikuwa ya
kwangu.Seif ameondoka na
sehemu yake ya utajiri haina
mtu.Wewe utachukua sehemu
yake.Utajiri wako wote
uliopotea nakurejeshea”
akasema Habiba
“Mama najua nia yako ni
nzuri sana lakini siwezi
kulikubali jambo hilo.Siwezi
kukubali kupata utajiri ambao
sijui chanzo chake.Nina nguvu
bado na nitaendelea
kupambana kuhakikisha
ninapata tena mali kutokana na
jasho langu.Kukubali utajiri huo
ni sawa na kukubali kuwa
gaidi.Siwezi” akasema Mathew.
“Watch your tongue son!
Akasema Habiba kwa sauti ya
ukali akachukua kichupa kidogo
cha dawa ya mafua akakifugua
akanusa halafu akasema
“Nimejishusha kwako isiwe
sababu ya kuzungumza nami
vile utakavyo.Who do you think
you are? Wakubwa wa dunia hii
wananyenyekea
wanapozungumza nami na
wanaitafuta nafasi ya kukaa
nami namna hii wanaikosa,kwa
nini wewe umeipata halafu
unakosa adabu? Akafoka
Habiba
“Samahani mama” akasema
Mathew
“Na iwe ni mara ya mwisho
kuzungumza nami kama uko na
vijana wenzio.Mtu
unayezungumza naye laiti
ungemfahamu hata kidogo tu
ungezugumza naye ukiwa
umelala chini kwa adabu !
“Nisamehe mama” akasema
Mathew
“Ninakupenda ndiyo maana
ninazungumza nawe namna
hii.Hata watoto wangu wa
kuzaa mwenyewe sijawahi
kukaa nao tukazungumza
namna hii.Wananiogopa na
kuzungmza nami kwa adabu
kubwa” akasema Habiba tayari
uso wake ulionyesha kukasirika
“Nataka ubadilike.Jifunze
kuwa na adabu.Niheshimu sana
kwani mimi ndiye ambaye
nitayabadili maisha
yako.Habiba Jawad hajui jibu
hapana.Neno langu ni amri !
Umenisikia?akauliza Habiba
kwa ukali
“Ndiyo mama” akajibu
Mathew na ukimywa wa dakika
mbili ukapita
“I’m sorry sikutarajia kuwa
mkali na si tabia yangu kuwa
mkali hadi pale
ninapokorofishwa.Mathew
hukuzaliwa hapa lakini wewe ni
wa hapa.You belong here.This is
your home.I’m not your
biological mother but from now
on I’m going to be your
mother.Hili si ombi hii ni amri
.Umenielewa Mathew?akauliza
Habiba jawad
“Nimekuelewa mama”
“Ahsante” akajibu Habiba
na ukimya ukatawala.Baada ya
muda akasema
“Kesho unakwenda Dubai”
akasema na kunyamaza kidogo
halafu akaendelea
“Utaambatana na
Najma.Anakwenda
kuniwakilisha katika
mazungumzo
muhimu.Utahudhuria
mazungumzo hayo lakini
hupaswi kuchangia
chochote.Tazama jifunze hadi
wakati wako utakapofika.Najma
atazungumza badala
yangu.Bado tuna majonzi lakini
kazi haziwezi kusimama.Maisha
lazima yaendelee kwani hata
tukisimamisha kila kitu Seif
hatarejea” akasema Habiba na
kunyamaza baada ya dakika
mbili akasema
“Tayari kila kitu
kimekwisha andaliwa kwa ajili
ya safari kesho
asubuhi.Mtaondoka na ndege
binafsi kuelekea
Dubai.Mtapumzika kwa muda
wa wiki moja ndipo
mtarejea.Nimefanya hivi ili
wewe na Najma muweze kupata
muda mzuri wa kufahamiana”
akasema Habiba na kukaa tena
kimya
“Mathew ninayafanya haya
kwa faida yako mwenyewe.Siku
moja utanishukuru kwa haya
ninayoyafanya hivyo nakuomba
usikasirike wala kuniona
mkatili.Kitu kikubwa ambacho
ninaendelea kukusisitiza ni
kuwa mwangalifu.Mimi nina
macho mawili lakini
yanatazama kila sehemu.Nina
masikio mawili lakini yanasikia
mambo mengi hivyo usijaribu
kufanya jambo lolote la
kipuuzi.Nadhani umenielewa
vizuri” akasema Habiba
“Nimekuelewa mama”
akasema Mathew
“Vizuri.Kuhusu Nawal bado
ataendelea kusubiri taratibu za
dini zikamilike kwani
mwanamke ambaye amefiwa na
mumewe kwa taratibu za dini
yetu atakaa eda kwa miezi
minne na siku kumi ndipo
atakapoolewa tena” akasema
Habiba
“Mama Habiba samahani
sana kwa hiki ninachotaka
kuuliza lakini sina nina mbaya”
akasema Mathew
“Uliza usihofu”
“Mimi na Nawal
unatufahamu vyema.Sisi si
waislamu lakini tumejiingiza
huku katika uislamu kutokana
na hizi kazi zetu
lak…………”akasema Mathew na
Habiba akamkatisha
“Nalifahamu hilo na hiyo ni
siri yetu mimi na ninyi hadi
kuingia kaburini.Sijali kuhusu
imani zenu kwani Mungu
tunayemuabudu ni Yule Yule
mmoja lakini kwa kuwa
mmekwisha ingia kwenye
uislamu basi mtaendelea kuwa
waislamu.Ninakachokueleza
hapa ndicho nitakachomueleza
Nawal. Umenielewa Mathew?
Akauliza Habiba
“Nimekuelewa mama”
akajibu Mathew
“Vizuri sana.Sasa nenda
kapumzike tutazunguza
utakaporejea kutoka Dubai”
akasema Habiba huku
akiinuka.Mathew naye akainuka
wakaanza kuondoka pale
bustanini
“Mathew usiwe na wasi
wasi kuhusu Najma.Ninaamini
utampenda” akasema Habiba
huku akitabasamu
Walirejea ndani na kupata
chakula kisha Habiba
akampeleka Mathew
kupumzika katika nyumba moja
ya ghorofa mbili.Ilikuwa ni
nyumba nzuri sana yenye
samani za kuvutia mno
iliyojengwa juu ya kilima.
“Hii ni nyumba ambayo
niliijenga maalum kwa ajili ya
Seif kwa bahati mbaya hajawahi
kuingia hata ndani.Kuanzia sasa
nyumba hii ni yako kama
nilivyokwambia kwamba kila
kilichokuwa cha Seif kitakuwa
chako” akasema Habiba
“Nashukuru sana mama”
akasema Mathew na Habiba
akamuonyesha sehemu mbali
mbali za nyumba ile kisha
akamuacha apumzike.Mathew
akaenda katika kioo
akajitazama.
“Huyu ninayemuona katika
kioo ndiye Yule Mathew
Mulumbi ambaye alikula kiapo
cha kumuua Habiba Jawad? Nini
kimemtokea? Akajiuliza na
kwenda kukaa kitandani
“Nini kimenitokea?
Nimepitia mchakato mgumu
hadi kumfikia Habiba lakini
baada ya kumuona mipango
yangu yote imeyeyuka kama
mshumaa.Nimekutana ana kwa
ana na mfahdili mkuu wa ugaidi
duniani.Nimekosa ujasiri
nimejikuta nikikubali kila
anachonieleza.Nimepewa
sehemu ya utajiri wa Edger
Kaka na hii inanihalalisha
kwamba mimi tayari nimeingia
katika mtandao wa
kigaidi.Sifahamu Yule
mwanamke ana nguvu gani
kwani ukiwa karibu yake
unajikuta ukikubali kila
unachoelezwa” akaendelea
kuwaza kisha akasimama
“No ! This is not me.This is
not Mathew Mulumbi I know.
Mathew Mulumbi katu hawezi
kuwa gaidi.This isn’t
over.Natakiwa kuendelea na
misheni yangu ya kumuua
Habiba Jawad.I m ust kill her !
akawaza na kugonganisha
mikono kwa hasira
“Lazima nikiri nimeteleza
baada ya kuonana na Habiba
lakini siwezi kuanguka na
kulala hapo hapo lazima
niinuke na niendelee na
misheni yangu.Hata kama
itanichukua miaka kutimiza
misheni yangu lakini lazima
nihakikishe nimeitimiza.Kwa
sasa suala hili limekwisha
kuwa kubwa tofauti na
nilivyotegemea.Natakiwa
kutumia akili kubwa sana
kujipanga.Nitaendelea kujifanya
mjinga huku nikiendelea
kujipanga taratibu.Bado
hawajamfahamu vizuri Mathew
Mulumbi”akaendelea kuwaza.
“Siku ilikuwa ndefu
sana.Napaswa kupumzisha
kichwa changu.Bado nina safari
ndefu” akawaza na kujilaza
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 6: EPISODE 3
Mathew aliamshwa saa
moja za asubuhi na mtumishi
aliyekuwa ameambatana na
watu wengine wawili ambao
walijitambulisha kama
wataalamu wa mitindo na
waliokwenda kumuandaa
Mathew kwa ajili ya safari ya
Dubai.Bila kupoteza muda
wataalamu wale wakaanza kazi
yao ya kumuandaa
Mathew.Kwanza walianza kwa
kumpima halafu mmoja
akaondoka na mwingine
akaendelea na kazi.Baada ya
nusu saa Yule jamaa
aliyeondoka akarejea akiwa na
masanduku mawili makubwa
yaliyokuwa yamesheheni
nguo.Zilikuwa ni suti za
gharama kubwa na nguo
nyingine pamoja na viatu.
Saa moja ilimalizika na
Mathew akawa
tayari.Alipojitazama kwenye
kioo akatabasamu.
“Hii dunia ina maajabu
sana.Jana nilikuwa mtu
niliyechakaa nisiye na
mwonekano wowote lakini
tazama leo hii mwonekano
wangu umebadilika kabisa
nimerudia mwonekano wangu
wa awali na hata zaidi.Dah !
wamenikumbusha mbali sana
hawa jamaa” akawaza Mathew
na mmoja wa wale jamaa
akamuuliza kama ameridhika
na mwonekano wake na
Mathew hakuwa na tatizo
lolote.
“Kwa mujibu wa maelekezo
niliyopewa nitaambatana nawe
Dubai kwa ajili ya kuhakikisha
kila siku unakuwa katika
mwonekano nadhifu kabisa”
akasema mmoja wa wale
wanamitindo
Muhudumu akamchukua
Mathew na kumpeleka kwa
Habiba Jawad ambaye naye
alipatwa na mshangao baada ya
kumuona Mathew
“Abu Zalawi umebadlika
kiasi hata mimi nimetaka
kukupotea” akasema Habiba na
kusalimiana na Mathew kisha
wakajumuika katika kifungua
kinywa.Sayid Omar naye
akafika na kujiunga nao kila
mmoja aliustaajabia
muonekano mzuri wa
Mathew.Wakati wakiendelea
kupata kifungu akinywa
akaingia mwanamke mmoja
mrefu kidogo aliyejitanda nguo
ndefu hadi miguuni na ushungi
uliofunika nywele zake.Macho
yake aliyafunika kwa miwani
kubwa myeusi.
“Huyu lazima atakuwa
ndiye Najma.Amefanana na
Habiba Jawad.Pamoja na
mavazi haya aliyoyavaa ya
kufunika mwili wote lakini ni
mzuri.Huyu ndiye ninayetakiwa
kumuoa.” Akawaza Mathew na
kugonganisha macho na
Habiba,Mathew
akatabasamu.Habiba akatoa
salamu kwa wote waliokuwepo
pale mezani kisha akavuta kiti
akaketi
“Kila kitu tayari? Akauliza
Habiba
“Ndiyo mama kila kitu
tayari” akajibu Yule msichana.
“Abu Zalawi kutana na
Najma” akasema Habiba
“Najma huyu ndiye Abu
Zalawi” Habiba akaendelea na
utambulisho
“Karibu sana Abu Zalawi
nafurahi kukufahamu”akasema
Najma
“Mtapata nafasi nzuri ya
kuzungumza na kufahamiana
pale mtakapokuwa Dubai”
akasema Habiba.Nadya
akamuomba mama yake
wakazungumze pembeni pale
mezani wakabaki Mathew na
Sayid Omar
“Abu Zalawi itumie vyema
nafasi ya Dubai kuwa karibu
sana na Najma.Ni mwanamke
mwenye sifa zote na mpaka
sasa hana mwanaume yeyote”
akasema Sayid Omar huku
akitabasamu.Mathew hakujibu
kitu akatabasamu
Najma alimaliza
mazungumzo na mama yake
wakarejea katika chumba cha
chakula.
“Abu Zalawi muda umefika
twende tuondoke” akasema
Najma.Mathew akaagana na
Habiba na Sayid akaungana na
Najma wakaelekea nje
kulikokuwa na gari
wakaondoka kuelekea katika
uwanja wa ndege.Najma
alikuwa ameongozana pia na
wanawake wengine wawili
katika safari ile.Uwanja wa
ndege waliokuwa wanaelekea
ni ule ambao walitua na ndege
ya Rayan Jaber wakati
wakiurejesha mwili wa Edger
Kaka kutoka Israel.
Habiba Jawad na familia
yake walimiliki ndege kadhaa
kubwa na ndogo na asubuhi hii
zilikuwepo uwanjani ndege
tatu.Baada ya kushuka katika
magari Najma akasalimiana na
jamaa wengine wanne
waliokuwa wamevalia kanzu
zao nzuri na baada ya maongezi
mafupi yaliyochukua kama
dakika kumi hivi Najma
akawaongoza watu wale
wakapanda ndege ile ya kifahari
ya Habiba Jawad na safari ya
Dubai ikaanza.Kutoka Riyadh
hadi Dubai walitegemea
kutumia saa mbili na nusu
kutokana na mwendo mkali wa
ile ndege.Ndani ya ndege Najma
alikuwa na mazungumzo na
wale jamaa wanne waliowakuta
uwanja wa ndege.Mathew
alikuwa peke yake katika
sehemu maalum ambako hukaa
Habiba Jawad kama akisafiri
kwa kutumia ndege hii.
“Mathew ngoja
nikufahamishe kitu kimoja
cha muhimu.Hukuweza
kufanya hivyo kwa sababu
hapa ndipo mahala
unapotakiwa kuwepo.You
belong here ! Mathew
akayakumbuka maneno ya
Habiba Jawad wakati
wakizungumza jana usiku.
“Je ni kweli hapa ndipo
mahala ninapotakiwa kuwepo?
Akajiuliza huku akipata juisi ya
matunda
“Sifahamu alimaanisha nini
lakini yawezekana labda
ninatakiwa kuwepo hapa katika
ulimwengu huu wa magaidi ili
niweze kuufahamu mtandao
wao wote na namna
wanavyoendesha shughuli
zao.Yawezekana mimi ndiye
nikasaidia dunia kupambana na
ugaidi kwani hapa nilipo ndipo
kitovu chake.Sasa nimeanza
kupata picha kamili ni kweli
ninatakiwa kuwepo mahali
hapa.It’s true I belong here”
akawaza Mathew na kuinua
glasi yake ya kinywaji akanywa.
“Wakubwa wa dunia hii
wananyenyekea
wanapoizungumza nami na
wanaitafuta nafasi ya kukaa
nami namna hii
wanaikosa,kwa nini wewe
umeipata halafu unakosa
adabu? Akaendelea
kukumbuka mazungumzo yao
usiku uliopita
“Alimaanisha nini kwa kauli
yake hii kwamba wakubwa wa
dunia hii wananyenyekea
wanapozungumza naye?Ni
wakubwa gani
aliowamaanisha?Ni viogozi wa
mitandao ya kigaidi au akina
nani?akaendelea kujiuliza
maswali
“Kuna mengi ya kufahamu
kwa Habiba Jawad.Kuna kauli
moja alisema ”Nataka
nikufumbue macho yako na
kukuonyesha dunia ambayo
huifahamu.Kuna mambo
makubwa ambayo huyajui na
siku ukiyajua utashangaa
hutaamini macho
yako.Nitakupeleka
huko.Nitayabadili maisha
yako na utakuwa mtu
mkubwa”
“Kitu ninachotakiwa
kukifanya ni kuwa mvumilivu
na nitafahamu mambo mengi
kutoka kwa Habiba.Natakiwa
kufaham…………….”
“Hallo Abu” Sauti nzuri ya
Najma ikamtoa Mathew
Mawazoni
“Samahani Abu Zalawi kwa
kukuacha peke yako.Nilikuwa
nawapa maelekezo wale
wajumbe wangu” akasema
Najma na kujimiminia kinywaji
katika glasi kisha akaketi sofani
akanywa funda moja na
kutazama saa yake ya dhahabu
mkononi
“Tumebakiza dakika chache
kutua Dubai.Naamini mama
amekwisha kufahamisha
kwamba tutakuwa hapo kwa
muda wa wiki moja” akasema
Najma
“Ndiyo amekwisha nijulisha
suala hilo”
“Vizuri” akasema Najma na
kabla hawajaendelea na
maongezi akaja mtu mmoja
akamuita Najma akatoka
“Ni mwanamke mzuri
sana.Ana umbo zuri,ana adabu
na anaonekana ni mchapa kazi
mzuri sana kiasi cha mama yake
kumuamini kumtuma
akamuwakilishe katika kikao
hicho muhimu. Hapa ndipo
ninapochanganyikiwa kwani
yawezekana nikajikuta
nikimpenda Najma na kusahau
misheni yangu.” Akawaza
Mathew na kutabasamu
“Kwa namna yoyote ile
lazima niikamilishe misheni
yangu na ili kuikamilisha sina
budi kumuoa Najma”
akaendelea kuwaza Mathew
huku akiyatafakari maisha yake
alikotoka na alipo sasa.
DUBAI
Ndege ya akina Mathew
ilitua jijini Dubai na baada ya
kukamilisha taratibu wakatoka
na kuingia katika magari
maalum yaliyokuwa
yakiwasubiri.
“Jiji hili nilikuwa nikifika
mara kwa mara kwa ajili ya
biashara zangu” akawaza
Mathew wakiwa garini.Walifikia
katika hoteli moja yenye
gharama za juu mno yenye
hadhi ya kifalme.
“Hoteli hii ninaifahamu ni
hoteli yeye gharama za juu mno
kuliko zote Dubai na wageni
wake wengi ni wafanyabiashara
mabilionea au viongozi wakuu
wa nchi.Mimi na utajiri wangu
niiokuwa nao sikuwahi
kuthubutu kufikia hoteli kama
hii” akawaza Mathew wakaingia
katika chumba chao.Wahudumu
wakapanga mabegi na Najma
akatoa maelekezo kadhaa ya
kufanyika mle chumbani.Kuna
baadhi ya maua akaagiza
yaletwe na alihitaji mwonekano
Fulani ndani ya kile chumba.
“Abu Zalawi hiki ndicho
chumba ambacho tutakitumia
kwa muda wa wiki nzima
tutakayokuwa hapa
Dubai.Nilikichagua
mwenyewe,Unakionaje?Umekip
enda? akauliza Najma
“Ni chumba kizuri sana
nimekipenda”
“Kitu gani hasa unakipenda
kiwepo katika chumba chako
cha kulala?akauliza Najma
“Kuwe na kitanda kizuri na
godoro” akasema Mathew na
Najma akacheka kidogo
“Kitanda pekee?
“Najma hutajali nikikuita
Naj badala ya Najma?akauliza
Mathew na Najma akatabasamu
“Huyu mtoto anapenda
kutabasamu kama mama yake”
akawaza Mathew
“Hakuna tatizo Abu niite
upendavyo”akasema Najma
“Ahsante.Naj naamini
mama amekupa taarifa zangu
kwamba ninatokea katika kundi
la Ammari Nazari brigades
ambalo limekuwa likiendesha
mapigano na serikali ya
Israel.Sehemu kubwa ya maisha
yangu nimekuwa katika ugaidi
hivyo maisha yetu sisi ni ya
shida ndiyo maana usishangae
nikikwambia ninahitaji kitanda
na godoro tu katika chumba
changu cha kulala” akasema
Mathew
“Nalifahamu hilo Abu lakini
maisha yale yamekwisha.Tayari
umetoka huko na hautarudi
tena.Hapa unaanza maisha
mapya na utaishi kama mfalme
ndiyo maana nimechagua hoteli
hii kubwa na nzuri kwa ajili
yako Abu.Nataka usahau tabu
zote ulizowahi kupitia huko
nyuma.Nitafanya kila lililo
ndani ya uwezo wangu
kuhakikisha unasahau yote na
kuanza maisha mengine”
“Nashukuru sana Naj”
“Tutazungumza mengi
lakini kwa sasa nataka twende
tukafanye manunuzi ya vitu
mbali mbali” akasema Najma
“Naj ahsante sana lakini
ninahitaji kupumzika.Nenda
kafanye manunuzi utanikuta
mimi hapa
ninapumzika”akasema Mathw
“Basi hakuna
tatzo.Chochote ukihitaji
utawajulisha hotelini
watakuhudumia.Usihofu
kuhusu usalama ni mkubwa
sana mahala hapa” akasema
Najma na kuondoka
“Natamani ningekwenda na
Najma kufanya manunuzi lakini
ninaogopa.Watanzania ni wengi
hapa Dubai na ninaweza
kukutana na wanaonifahamu
hasa Gosu Gosu ambaye huwa
anakuja hapa Dubai mara kwa
mara” Mathew alipomkumbuka
Gosu Gosu akajikuta
akitabasamu
“Nimemkumbuka sana
Gosu Gosu.Sijui kwa sasa
atakuwa wapi.Je Peniela bado
anaendelea kumtumia katika
biashara au tayari naye
ameendelea na maisha yake?
Yawezekana naye tayari
amekwisha nisahau na
anaamini nimefariki dunia.Yule
jamaa siwezi kumsahau katika
maisha yangu.Alikuwa ni
msaidizi wangu
mkubwa.Ninashukuru sana
kumfahamu.Kwa kule kwetu
anaitwa Jembe.Ni mchapakazi
mzuri,haogopi chochote lakini
ni mtu hatari sana.Ni mwepesi
mno kutoa uhai wa mtu
nadhani ni kwa sababu ya
maisha aliyopitia kwani kwa
mujibu wa maelezo yake
alichukuliwa na kundi la waasi
angali akiwa mdogo
akapelekwa msituni akaanza
kufundishwa kupigana.Kuna
nyakati hata mimi huwa
ninamuogopa ninapokuwa naye
katika misheni lakini
ninachoshukuru ni kwamba
kwangu mimi ana adabu
sana.Ananiheshimu mno na
hajawahi katu kunidharau au
kupuuza chochote
nilichomuelekeza.Gosu Gosu
kwangu ni zaidi ya
rafiki.Natamani sana kama
ningekuwa naye huku kwa
Habiba lakini angeweza
kuharibu misheni Yule ana
hasira za karibu sana.Ngoja tu
niendelee mwenyewe naamini
kama tunaendelea kuwa hai
tutaonana siku moja”akawaza
Mathew na kutabasamu
“Siwezi kumkumbuka Gosu
Gosu nikacha kumkumbuka
Ruby.Sifahamu yuko wapi hivi
sasa na anafanya nini.Sjui ni
machozi kiasi gani alilia baada
ya kupata taarifa kwamba
nimefariki dunia.Ruby
alinipenda mno na alinieleza
wazi wazi namna
anavyonipenda na anavyotaka
kuwa na mimi katika
mahusiano ya
kimapenzi.Nimekuwa naye
karibu kwa miaka mingi na
amenisaidia sana katika
misheni mbali mbali za hatari
lakini mara zote nilipomuita
hata katika misheni za hatari
hakuwahi kusema hapa.Muda
wowote nilipomuta aliitika
ndiyo.Ruby ni mtu wa pekee
kabisa kwangu. Kama
nisingeingia katika matatizo
haya na kufika huku niliko hivi
sasa ningekuwa naye katika
mahusiano.Tayari nilikwisha
fanya maamuzi ya kuwa naye
katika mahusiano ya siri kwani
alikuwa tayari kuishi mahala
kokote nitakakoishi kitu
ambacho mke wangu Peniela
hakuwa tayari
kukifanya.Hakuwa tayari kuishi
Tanzania lakini Ruby alikuwa
tayari” akawaza na mwili
ukamsisimka baada ya
kukumbuka tukio la Ruby
kupigwa risasi na Devotha
“Nimekumbana na matukio
mengi mabaya lakini lile la
Ruby kupigwa risasi na Devotha
ni tukio lililoniumiza sana na
ninakumbuka nilifanya tukio
moja baya ili kuokoa maisha ya
Ruby.Sasa ndipo ninaamini
kweli Ruby yuko moyoni
mwangu.Maumivu niliyoyapata
yalikuwa makubwa.Nilipanga
baada ya sakata lile kumalizika
ningekwenda naye sehemu
tukatulie tupumzike na
nilikuwa na mipango ya kuzaa
naye mtoto mmoja au hata
zaidi.Kwa bahati mbaya sana
mpango huo
haukufanikiwa.Sijui kama
atakuwa ameolewa kwa sasa au
bado? Daah ! sikutegemea
kabisa maisha yangu kubadilika
namna hii” akawaza Mathew
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Saa tatu za asubuhi balozi
wa jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo nchini Tanzania
Germinus Mapupu aliwasili
katika jengo zilimo ofisi za mke
wa Rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Millen
Kelelo.Alipokewa na wahudumu
wa mapokezi na akaeleza shida
yake ya kuonana na mke wa
Rais.Kwa kuwa Millen hakuwa
amefika bado akapigiwa simu
na wale wahudumu na
kujulishwa kwamba balozi
Mapupu alikuwepo pale ofisini
akihitaji kuonana naye.Millen
akamtaka balozi Mapupu
aendelee kusubiri atafika pale
ndani ya kipindi kifupi.
Saa nne na dakika ishirini
mke wa Rais wa Tanzania
Millen Kelelo akawasili katika
ofisi zake.Siku hii alikuwa
amevaa suti nzuri ya suruali ya
rangi nyekundu.Alipendeza
sana.Kisha shuka garini
akaelekea ofisini akapita
kuwasalimu watu wa mapokezi
halafu akaelekea katika ofisi
yake ambako alimkuta balozi
Mapupu akimsubiri
“Balozi Germinus” akasema
Millen huku akitabasamu
“Madam first lady” akasema
balozi Mapupu wakasalimiana
na kumkaribisha ofisini kwake
“Karibu sana mheshimiwa
balozi.Ungenijulisha kama
unakuja ofisini kwangu leo
ningewahi zaidi”
“Usijali mama
Kelelo.Nilikuwa na haki ya
kusubiri kwa kuwa nimevamia
bila taarifa”
“Karibu sana” akasema
“Madam first lady sitaki
kuchukua muda wako mwingi
lakini kuna suala la muhimu
sana lililonileta hapa kwako”
Akasema balozi Mapupu
“Usijali mheshimiwa balozi
tunao muda wa kutosha”
akasema Millen
“Kwanza kabisa napenda
nikupongeze sana kwa kuandaa
mkutano mkubwa
utakaowakutanisha wake za
marais wa dunia nzima.Rebeca
Eyenga mke wa rais wa Congo
naye tayari amekwisha
thibitsha kushiriki.Kama
unavyofahamu kwa muda wa
miaka kadhaa hivi sasa
mahusiano ya nchi yangu na
Rwanda yamekuwa si mazuri
sana.Nimefikiria kuutumia
mkutano huo kama chanzo cha
kutafuta amani kwa nchi zetu
hizi mbili.Nimepanga kuandaa
chakula maalum na
kuwakaribisha mke wa Rais wa
Congo na mke wa Rais wa
Rwanda na huo utakuwa ni
mwanzo wa kupatikana
amani.Wanawake hawa wawili
wakiweza kukaa meza moja
wakazungumza nina uhakika
mkubwa watawashawishi
waume zao kuweka kando
tofauti zao na amani
itapatikana”
“Hilo ni wazo zuri sana
mheshimiwa balozi.Kama
ukianza kuwakutanisha
wanawake hawa wawili
wakaelewana na wakaondoa
tofauti zao basi uhakika wa
marais wa Rwanda na Congo
kumaliza vita yao ya maneno ni
mkubwa sana.Nakupongeza
sana mheshimiwa balozi kwa
wazo hili zuri” akasema Millen
“Madam Millen,ahsante
kwa kulikubali ombi langu
lakini nitahitaji msaada wako”
akasema balozi Mapupu
“Nikusaidie nini
mheshimiwa balozi?
“Kutokana na msuguano
uliopo baina ya waume zao,upo
ugumu wa kuwaleta wanawake
hawa katika meza
moja.Kumpata mke wa Rais wa
Rwanda itakuwa ni kazi ngumu
ndiyo maana nahitaji msaada
wako”
“Ni kweli hilo unalolisema
mheshimiwa balozi.Nini
unataka nikifanye? Akauliza
Millen
“Ninachokiomba kwako ni
hiki.Mimi nitaandaa kila kitu
lakini nitakukaribisha wewe na
wewe ndiye
utakayewakaribisha wanawake
hao katika chakula.Utakaa nao
meza moja na watajikuta
wakizungumza na kuweka
kando tofauti zao.Ninakuomba
sana mama ukubali kunisaidia
kwa hilo” akasema balozi
Mapupu
“Mimi sina tatizo kabisa na
suala hilo.Ni suala jema sana
ambalo lazima tuliunge
mkono.Siwezi kukataa kusaidia
katika suala hili.Hawa wote ni
wageni wangu na ninakubali
kuwaleta wote
mezani.Nitakusaidia kwa
hilo.Utanieleza namna
ulivyopanga kulifanya hilo
jambo ili na mimi nifanye
maandalizi”
“Nashukuru sana madam
first lady.Nitakuja tena kukupa
mrejesho wa namna
ninavyoliandaa jambo hilo
lakini narudia tena
kukushukuru kwa kulikubali
ombi langu.Hili ni jambo kubwa
sana umelifanya kwa nchi
yangu” akasema Balozi mapupu
kisha akaagana na Millen
akaondoka kwa miadi ya
kurejea tena kumpa Millen
mrejesho wa namna
anavyoandaa chakula hicho cha
pamoja cha wake za marais wa
Congo na Rwanda
DUBAI
Saa kumi na mbili za jioni
iliwakuta Najma na Mathew
tayari wamekwishajiandaa
kwenda kukutana na wageni
wao ambao Mathew hakuwa
amejulishwa wanatoka wapi na
hakutaka kuuliza.Kikao
kilipangwa kufanyika ndani ya
hoteli ile ile waliyokuwa
wamefikia.Wakiwa
wameongozana na watu
wengine wanne pamoja na
walinzi wawili wakaingia katika
ukumbi maalum wa mikutano
unaoweza kuchukua watu kumi
na tano.Wageni waliokuwa
wanawasubiri hawakuwa
wamefika na Najma akaomba
wasubiri kidogo ndani ya
dakika tano mlango ukagongwa
mlinzi akaufungua na
mwanamke mmoja mwenye
umbo na uzuri wa kipekee
kabisa akaingia.Wote mle ndani
walikuwa kama wamepigwa na
butwaa kwa sekunde
chache.Ilikuwa ni kama waliona
kitu cha kuwashangaza.
“Huyu ndiye tunayemsubiri
au amepotea njia?akajiuliza
Mathew
“Naamini sijakosea
chumba” akasema Yule mgeni
baada ya kuona namna watu
wote mle chumbani
walivyopigwa na butwaa
wakimuangalia.
“Hapana hujakosea
chumba” akasema Najma
ambaye jioni hii alikuwa
amevaa suti nzuri nyeusi
iliyomkaa vyema na
kulionyesha umbo lake zuri
“Karibu sana” akasema
Najma na kusalimiana na Yule
mwanamke mzuri
akamkaribisha kiti
“Karibu sana.Uko
mwenyewe au kuna wengine
wanakuja? Najma akauliza
“Hakuna mwingine ni mimi
mwenyewe”akasema Yule
mwanamke mwenye uzuri wa
kimalaika
“Basi hakuna haja ya
kupoteza muda tunaweza
kuanza kikao chetu” akasema
Najma
“Sawa tunaweza
kuendelea” akasema yule
mwanamama
“Kwanza tuanze kwa
utambulisho.Mimi naitwa
Najma Hanifnejad ndiye
kiongozi wa jopo hili lililokuja
kukutana nawe.Pembeni yangu
anaitwa Abu Al Zalawi”
akasema Najma na kuendelea
kutambulisha watu wote
alioongozana nao.
“Ninashukuru sana
kuwafahamu” akasema Yule
mwanamke mrembo
“Mimi ninaitwa Melanie
Davis ninatokea Tanzania.Ni
mwekezaji ambaye ninamiliki
makampuni kadhaa
makubwa.Nimefurahi sana
kukutana nanyi” akasema
Melanie
“Hata sisi tumefurahi sana
kukutana nawe
Melanie.Naamini huu ni
mwanzo mzuri wa mashirikiano
makubwa baina yetu” akasema
Najma.Mathew alihisi mwili
wake ukitetemeka aliposikia
Melanie akitaja kwamba
ametokea Tanzania.
“Abdallatif Al Hashimi
naomba utufungulie kikao hiki
kwa kutupa maelezo ya
utangulizi” akasema Najma
“Bismillahir Rahmnair
Raheem” akasema Abdallatif
“Jina langu ni Abdalatif Al
Hashimi bin Abdul
Aleem.Ninatoka IS kitengo cha
fedha” akanyamaza kidogo
halafu akaendelea
“Kikundi cha IS kina
mpango mkubwa wa
kujiimarisha katika bara la
Afrika na tumechagua eneo la
Afrika Mashariki na kati kama
sehemu muhimu kwa ajili ya
kujenga kambi maalum ya
kuandaa watu wetu na
kuwapeleka katika mapambano
sehemu mbali mbali duniani.
Katika utafiti wetu tuligundua
kwamba sehemu nzuri ambayo
tunaweza kujenga kambi kubwa
ya mafunzo ni katika misitu
mikubwa ya jamhuri ya
kidemokrasia ya watu wa
Congo.Ili suala hilo liweze
kufanikiwa ilitulazimu kuingia
makubaliano ya mashirikiano
na mtu anaitwa James Kasai
ambaye anaongoza kundi la
waasi waliotimuliwa huko Kivu
ya Kaskazini nchini jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo na
kukimbilia Kaskazini mwa
Uganda ambako yeye na kundi
lake wamejificha msituni.Kwa
sasa James na kikundi chake cha
waasi wako katika hali mbaya
ya kiuchumi kwani chanzo
pekee cha fedha walichokuwa
wanakitegemea ni biashara ya
madini ambayo kwa sasa
yanadhibitiwa na
serikali.Tumekuwa na
majadiliano na James na
amekubali kushirikiana nasi na
mambo yote ambayo
tunayahitaji ameyakubali lakini
ombi lake kubwa ni kupatiwa
msaada wa fedha na vifaa vya
kijeshi.James anataka kurejea
tena msituni kupambana na
serikali ya Jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo hivyo
anahitaji silaha na zana za
kisasa za kivita.Sisi
tumemuahidi kumsaidia kwa
kila kitu kumpatia fedha na
vifaa vya kijeshi kwa ajili ya
kupambana na serikali ya DR
Congo.Ugumu ulikuwepo njia
yakuweza kumfikishia fedha
kwani serikali nyingi hivi sasa
ziko macho sana katika suala la
usafirishaji wa fedha wakiogopa
fedha za dawa za kulevya na
fedha za kufadhili ugaidi.Hilo
limetukwamisha kwa muda
mrefu hadi pale James
alipotufahamisha kwamba
amekwisha pata mshirika
ambaye tutapitishia kwake
fedha ambaye ni wewe”
akasema Abdallatif
“Ni kweli mimi ndiye
mshirika wa James Kasai na
nimekuja hapa kama
alivyowaeleza kuanza mchakato
huo wa kifedha”akasema
Melanie Davis na majadiliano
yakaanza.Saa tatu za usiku
kikao kilisimama kwa wajumbe
kupata chakula cha usiku kisha
kikao kikaendelea hadi saa tisa
za usiku.Kila kitu kilitakiwa
kumalizika usiku ule kwani
asubuhi siku iliyofuata Melanie
alitakiwa kuondoka kurejea
Tanzania
Kikao kilimalizika kwa
mafanikio makubwa wakaagana
na Melanie akaondoka kurejea
hotelini alikofikia.Najma
akampeleka Mathew chumbani
kupumzika yeye akarejea
kuendelea na kikao na wale
wajumbe wa IS.
“Chumba kilikuwa na
ubaridi wa kutosha wa kiyoyozi
lakini mwili wote umeloa jasho
baada ya kushuhudia kwa
macho yangu namna Habiba
anavyofadhili ugaidi.IS
wanataka kujiimarisha Afrika
Mashariki na kati na wana
mikakati mizito ya kuanzisha
kambi kubwa ya mafunzo
itakayokuwa ikifundsha
ugaidi.Nimesisimkwa mwili
kwa vile jambo hili
linalofanyika ni lile ambalo
nimekuwa nikipambana nalo
kwa miaka mingi lakini leo hii
nimekuwa mjumbe
nikishuhudia kwa macho yangu
kundi la kigaidi la IS likipokea
ufadhili wa fedha nyingi kutoka
kwa Habiba Jawad katika
harakati zake za kujitanua na
kujiimarisha katika eneo la
Afrika Mashariki na
kati.Magaidi ambao
wanakwenda kuzalishwa katika
kambi hiyo ya mafunzo wataua
idadi kubwa ya watu
duniani.Kama magaidi wakiwa
na kambi yao ya mafunzo nchini
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo basi eneo zima la Afrika
Mashariki halitakuwa
salama.Nimeshuhudia mikataba
ya fedha na silaha ikifanyika
ambayo inakwenda
kumuimarisha huyo mtu
anayeitwa James Kasai ambaye
ndiye atakayewasaidia IS
waweze kupata eneo la kujenga
kambi ya mafunzo”Akawaza
Mathew akiwa amevua shati
akipata ubaridi
“Kwa nini Habiba Jawad
ametaka niyashuhudie haya?
Nini anakitafuta kwangu?Huyu
mwan…….” Mathew akastuka
baada ya mlango kufunguliwa
Najma akaingia.Haraka haraka
Mathew akataka kuvaa fulana
yake lakini Nadya akamzuia
“Abu usivae kwanza hiyo
fulana yako” akasema Najma na
kumsogelea Mathew.Alipatwa
na mshangao mkubwa
alipouona mwili wa Mathew
ukiwa na makovu mengi ya
vidonda.
“Nini kimekutokea Abu
hadi ukawa katika hali hii?
Akauliza
“Usijali Naj haya ndiyo
maisha yetu” akasema Mathew
“Hapana hili si jambo la
kawaida.Huu ni ukatili mkubwa
uliopitiliza.Mwili wa binadamu
hauwezi kuharibiwa namna hii
na likaonekana jambo la
kawaida” akasema Nadya huku
akiukagua mwili wa Mathew
“Nilifungwa Israel miaka
mitatu nikiteswa kila uchao na
makovu haya unayoyaona
niliyapata huko.Haya majeraha
mengine ambayo yameanza
kupona niliyapata katika
mchakato wa kufika kwa mama
yako Habiba.Haikuwa rahisi
kufika kwake ilinilazimu kupitia
mateso makali”
“Sikulifahamu hilo.Kwa nini
umepitia mateso haya? Kwa
nini uliteswa na Israel kwa
muda huo wote wa miaka
mitatu? Akauliza Najma
“Nilimuua mkuu wa Mossad
ukanda wa Afrika Mashariki na
ndipo nilipokamatwa na Israel
na kufungwa kwa miaka mitatu
nikiteswa na baadae nikiwa
gerezani nikafahamiana na
Ammar nazazi mkuu wa
kikundi cha Ammar Nazari
brigades,tukafanya mpango na
tukatoroka gerezani nikaenda
kujiunga naye na kuendelea
mapambano dhidi ya Israel.Hivi
majuzi Israel walifahamu
maficho ya Ammar
wakatuvamia.Kwa bahati nzuri
niliwahi kumtorosha Nawal
lakini wengine wote
waliuawa.Baada ya kunusurika
katika mashambulio yale
nilihitaji kumuona Habiba ili
kumpa taarifa za mwanae Seif
ambaye nilikuwa nafahamu
mahala alipo na ndipo
iliponilazimu kuyapitia haya
niliyoyapitia ili kufika kwake”
“Pole sana Abu Zalawi kwa
haya uliyoyapitia.Hukupaswa
kupitia mateso haya lakini
kuanzia sasa hutapitia tena
mateso kama haya” akasema
Najma na kuanza kulia.
“Nyamaza kulia
Najma.Haya ni maisha yangu ya
kawaida nimeyazoea” akasema
Mathew akimbembeleza
“Sikujua kama umepitia
haya kufika kwetu” akasema
Najma akiendelea kulia
“Haya ni maigizo au
nini?.Analia kwa kuona vidonda
mwilini mwangu kwa nini halii
kwa watu wanaopoteza maisha
kwa kuuawa na makundi ya
ugaidi wanayoyafadhili? Muda
mfupi uliopita ameweka sahihi
kiasi kikubwa cha fedha kilipwe
kwa James Kasai ambaye
atazitumia fedha hizi kwa
mauaji,haya ni maigizo tu”
akawaza Mathew akimtazama
Najma akilia
“Naj nyamza usiendelee
kulia.Haya yamekwisha pita na
itabaki ni kumbu kumbu yangu
hivyo yasikuumize
sana”akasema Mathew na
kuchukua kitambaa akamfuta
machozi
“Abu Zalawi nikufanyie kitu
gani uwe na furaha katika
maisha yako na usahau mambo
hayo magumu
uliyoyapitia?Niambie chochote
unachokitaka nitakufanyia ili
uwe na furaha.Naamini kwa
haya uliyoyapitia hutakuwa na
furaha kamwe katika maisha
yako” akasema Najma.Mathew
akamfuta machozi na kushika
mikono akamtaka ainuke
wakaenda sofani.Mathew
akamtazama Najma usoni na
kusema
“Naj sihitaji kitu
chochote.Pole uliyonipa
inatosha sana” akajibu Mathew
na ukimya ukapita halafu Najma
akasema
“Sijawahi kuwa na
mwanaume katika maisha
yangu nina maanisha
mpenzi.Hilo limewafanya watu
wajiulize maswali mengi sana
kuhusu mimi kwa nini sitaki
kuwa na mpenzi?Hata mimi
sifahamu ni kwa nini hali ile
imenitokea lakini nimejikuta tu
sitaki kuwa na mwanaume
yeyote katika mahusiano ya
kimapenzi.Mama amewahi
kuniuliza mara kadhaa kwamba
kwa nini sitaki kuwa na
mwanaume nikamjibu hata
mimi sifahamu kwa nini.Moyoni
niliamini kwamba maisha
yangu nitakuwa mwenyewe na
sintahitaji mwanaume yeyote”
akanyamaza na kufuta machozi
“Kwa nini mwanamke
mzuri kama wewe Naj hutaki
kuwa na mpenzi? U mzuri wa
sura na umbo na ninaamini
wapo wanaume wengi
wanakupenda na huko waliko
wanaomba siku moja wapate
bahati ya kuwa nawe”akauliza
Mathew
“Hata mimi sifahamu Abu
nini kimenitokea lakini
nimejikuta nikiwa hivyo”
akajibu Najma na kukaa kimya
kidogo halafu akaendelea
“Baba yangu anatokea
nchini Iran” akasema na
kunyamaza kidogo
“Nimeishi naye kwa muda
mrefu hadi nilipomaliza
masomo yangu ya udaktari
nchini Urusi ndipo nilipoamua
kuhamia Saudi Arabia kwa
mama.Kilichoniondoa Iran ni
kijana mmoja ambaye alikuwa
ananifuatilia mno akinitaka
tuwe wapenzi kitu ambacho
sikuwa tayari.Hata baba yangu
alikuwa akimfahamu kwani ni
mtoto wa tajiri
mwenzake.Niliamua kuja huku
kujiepusha na kero za kijana
huyo.Nashukuru kwa hapa
Saudi kidogo wananielewa
kwamba sipendi mahusiano ya
kimapenzi” akasema Najma na
kunyamaza kwa sekunde
chache hakutaka kumtazama
Mathew usoni.
“Hivi majuzi mama aliniita
na kunieleza kwamba
anafahamu sihitaji mahusiano
ya kimapenzi lakini kuna mtu
mmoja atakuja ambaye
anaamini anaweza
akanifaa.Alinieleza kila kitu
kuhusu Abu Zalawi na
nikajikuta nikimfahamu kabla
hata sijamtia machoni.Mama
alikiri kwamba yeye binafsi
anampenda na angependa awe
sehemu ya familia
yetu.Alinitaka nijaribu japo kwa
mara ya kwanza kuingia katika
mahusiano na kama
nikishindwa basi
hatanishawishi tena kuingia
katika mahusiano
yoyote.Sifahamu nini kilinitokea
lakini nilijikuta nikimkubalia
mama kwamba nitajaribu.Hata
yeye binafsi hakuamini
nilipompa jibu lile kwamba
nitajaribu kuingia katika
mahusiano na Abu
Zalawi.Sifahamu kama kuna
nguvu yoyote ambayo mama
aliitumia kunishawishi lakini
nilijikuta nikikubali kuingia
katika mahusiano na mtu
ambaye sijawahi kumtia
machoni pangu.Inashangaza
sana” akasema Najma na kutoa
kicheko kidogo halafu
akaendelea.
“Mara ya kwanza kukuona
kwa macho yangu mawili ni leo
asubuhi kabla ya kuondoka kuja
huku.Nilistuka
nilipokuona.Sifahamu sababu
ya mstuko ule lakini nilistuka
sana.Nilihsi kitu cha tofauti
kinanitokea.Kwa mara ya
kwanza nilihisi mwili
unanisisimka baada ya
kumuona mwanaume.Abu
Zalawi umekuwa ni mwanaume
wa kwanza kunisisimua na kwa
mara ya kwanza najihisi
kupenda na kutaka kuingia
katika mahusiano” akasema
Najma na kunyamaza kidogo
akatazama chini kama vile
anaona aibu
“Nilipoona mgongo wako
nilistuka kwa namna
ulivyochafuliwa na makovu na
vidonda.Toka ndani ya moyo
wangu nimeumia sana kukuona
ukiwa katika hali hii.Naamini
haya uliyoyapitia yataendelea
kukutesa ndani ya moyo wako
kwa miaka mingi ndiyo maana
ninataka nifanye kila lililo ndani
ya uwezo wangu kukufanya
uwe na furaha.Abu Zalawi
naomba nikiri kwako kwamba
toka ndani kabisa ya moyo
wangu niko tayari kuwa na
mahusiano nawe.Umenigusa
moyo wangu kwa namna ya
ajabu” akasema Najma na
kunyamaza akatazama chini
kwa muda halafu akainua
kichwa akamtazama Mathew
“Abu yawezekana ikawa
vigumu kwako kuufungua moyo
wako kwangu na nitalipokea
hilo lakini niruhusu japo niwe
sehemu ya maisha
yako.Niruhusu nikupe furaha ya
maisha.Niruhusu
nikusahaulishe maisha yako ya
nyuma uliyopitia mateso
mengi.Nataka nikupe pumziko”
akasema Najma kwa hisia kali
sana
“Dah ! huyu mtoto
anaongea kwa hisia kali mpaka
ninasisimka mwili” akawaza
Mathew
“Abu Zalawi sisi ni matajiri
wakubwa.Tuna fedha nyingi
mno lakini nakuhakikishia
kwamba sintatumia utajiri
tulionao kukunyanyasa.Siku
zote nitakuwa chini
yako,nitakuwa mnyenyekevu
kwako,nitaitika haraka kila pale
utakaponiita,nitakuwa mwepesi
kuomba msamaha kila pale
nitakapokosea,katu
sintasimama kujibizana nawe
na neno lako ni amri kwangu
kwani wewe utakuwa ni
mfalme nami kijakazi wako”
akasema Najma
“Maneno mazito sana haya
ameyatamka Naj na
anaonekana anamaanisha
anachokisema” akawaza
Mathew
“Najma huna sababu ya
kuendelea kulia.Maneno
uliyoyatamka ni mazito na
yamenigusa hadi ndani ya moyo
wangu.Ni nadra sana kwa dunia
ya sasa kumpata mwanamke wa
aina yako ambaye anaogelea
katika utajiri na akatamka
maneno mazito kama hayo
uliyonitamkia.Naweza kusema
nina bahati ya kipekee kwanza
kuwa mwanaume wa kwanza
ambaye nimeugusa moyo wako
hadi ukaamua kubadili
msimamo wako na kujikuta
ukitamani kuingia katika
mahusiano.Pili ninajiona
mwenye bahati sana kutamkiwa
maneno kama hayo ya
unyenyekevu mkubwa mimi
ambaye sina mbele wala
nyuma” akasema Mathew
“Usiseme hivyo Abu.Moyo
wangu unaumia sana kwa
maisha magumu uliyopitia”
akasema Najma
“Huo ndio ukweli Naj
ambao siwezi kuona haya
kuusema.Mimi ni masikini
hohehahe na ninamshukuru
sana mama Habiba kwa
kuguswa na maisha yangu na
kuamua kunisaidia kuyaanza
maisha mapya.Kama
alivyokushauri wewe kufikiria
kama unaweza ukaanzisha
mahusiano nami ndivyo
alivyonishauri na mimi kufikiria
kama ninaweza kuanzisha
mahusiano nawe na hatimaye
tukafunga ndoa na kuishi kwa
furaha na amani.Sifahamu kitu
gani mama amekiona kwetu na
kuhisi tunaweza tukaendana
hadi akatushauri tuanzishe
mahusiano.Naamini kuna kitu
amekiona kwetu na mimi ni
nani wa kumpinga? Siwezi
kukataa japo itatuchukua muda
kwa kila mmoja kumfahamu
vyema mwenzake yukoje kwani
mimi nina mapugufu yangu
nawe pia unayo yako lakini
kama kweli tukiamua tuwe na
furaha na amani basi hakuna
kitakachoshindikana” akasema
Mathew
“Abu Zalawi ni hicho tu
ambacho nilitaka kukisikia
kutoka kwako.Kuhusu madhaifu
hayo ni ya kawaida nitayabeba
yote na kuyavumilia.Nataka
unihakikishie je lile ombi la
mama la kutaka mimi na wewe
tuoane unalikubali?Usikubali tu
kwa vile mama amekushauri
lakini usikie moyo wako
unakuambia nini.Usishinikizwe
na mtu yeyote.Kama hauko
tayari kwa hilo
nitaelewa.Niambie ukweli
tafadhali” akasema
Najma.Mathew akamtazama na
kutabasamu kidogo halafu
akasema
“Mama alitoa ushauri na
kunitaka nifikirie kama ushauri
alioutoa utafaa na ndiyo maana
akaniruhusu niambatane nawe
huku Dubai kwa lengo la
kufahamiana na kila mmoja
ajitafakari kama mwenzake
anaweza akamfaa.Mimi kwa
upande wangu ninamshukuru
sana mama kwa kuwa na
maono makubwa na mtazamo
wa mbali.Ameyaona maisha
yangu na yalivyokuwa na
ameyaona yatakavyokuwa na
akajua mtu pekee ambaye
anaweza akanifaa ambaye
atanipa furaha katika maisha
yangu ni wewe Najma.Kwa hili
nitaendelea kumshukuru mama
Habiba siku zote.Kujibu swali
lako ndiyo nimelikubali ombi
lake.Nitawezaje kusema hapana
kwa malaika kama wewe?
Akasema Mathew na tabasamu
likajengeka katika sura ya
Najma
“Ahsante Abu Zalawi.Kama
nilivyokuahidi kwamba
nitakuwa mke mwema na
muaminifu
kwako,nitakuheshimu kwa
maisha yangu yote lakini kuna
jambo moja ambalo nataka
unihakikishie” akasema
Najmana kunyamaza
“Naj sema chochote”
“Nataka unihakikishie
kwamba katika mahusiano haya
yetu sintatoa machozi na
kujutia maamuzi yangu”
akasema Najma na Mathew
akatabasamu
“Najma mimi ni mgumu
sana kutoa ahadi ambayo siwezi
kuitekeleza lakini kwa hili
ninakuahidi kwamba hutatoa
machozi.Nitakulinda kama
mboni ya jicho langu na
hutajutia maamuzi
yako”akasema Mathew
“Abu kila nionapo midomo
yako ikitamka maneno ninazidi
kusisimkwa mwili.Nimevumilia
kwa muda mrefu nadhani
siwezi tena kuendelea
kuvumilia.Tafadhali nao…..”
Najma hakumaliza alichotaka
kukisema kwani tayari Mathew
alikwisha muelewa naye
hakupoteza wakati
akamnyanyua na kumpeleka
kitandani.Kila mmoja
alionekana kuwa na kiu kubwa
na mtanange ule hivyo
hakukuwa na kupoteza muda
kipute kikaanza mara moja.
WIKI MOJA BAADAE
RIYAD – SAUDI ARABIA
Ndege ya kifahari ilitua
katika uwanja wa ndege
unaomilikiwa na familia ya
Habiba Jawad.Ndege hii ilitokea
Dubai na ndani yake alikuwepo
Mathew Mulumbi akiwa na
Najma.Kwa muda wa wiki moja
waliyokaa na kustarehe Dubai
mapenzi mazito yaliibuka kati
yao na wazo la Habiba Jawad la
kuwataka wafunge ndoa lilipita
bila kupingwa.Wawili hawa
walionekana ni wenye nyuso za
furaha sana walipowasili
Riyadh Saudi Arabia
Walishuka ndegeni na
kuingia katika gari safari ya
kuelekea nyumbani kwa Habiba
ikaanza.
“Nina hakika mama
atafurahi sana pale atakaposikia
kuhusu maamuzi yetu ya
kufunga ndoa” akasema Najma
“Lazima afurahi kwa kuwa
yeye ndiye mwasisi wa jambo
hili” akajibu Mathew
“Abu Zalawi sikuuliza swali
hili.Ungependa lini ndoa yetu
ifungwe?akauliza Najma akiwa
amemuegemea Mathew
“Hakuna chochote cha
kutuzuia hivyo ningependa iwe
mapema iwezekanavyo” akajbu
Mathew
“Hata leo hii?
“Hata sasa tukishuka
kwenye gari mimi niko tayari”
akajibu Mathew na kumuacha
Najma akiwa na tabasamu
kubwa sana
Waliwasili katika makazi ya
Habiba Jawad na kupokewa na
Sayid Omar akawakaribisha
ndani ambako walikutana na
Habiba Jawad ambaye alitoa
tabasamu kubwa baada ya
kuwaona
“Karibuni wageni” akasema
Habiba.Baada ya mazugumzo ya
dakika kumi na tano Habiba
akasema
“Nimefurahi kuwaoneni
mmerejea salama
wanangu.Najma wewe nenda
kaendelee na shughuli zako
tutazungumza baadae kwa sasa
nataka kwanza kuzungumza na
Abu Zalawi” akasema Habiba na
Najma akatoka Habiba
akamgeukia Sayid Omar
“Na wewe pia Sayid
naomba utupishe kwanza nina
mazungumzo muhimu na Abu”
akasema Habiba na Sayid
akaaga akaondoka wakabaki
Habiba na Mathew
“Abu habari za huko Dubai?
Sikumpigia simu Najma
sikutaka kumsumbua lakini
kwa nyuso zenu namna
ninavyoziona mlivyoondoka na
mlivyorejea nadhani mambo si
mabaya” akasema Habiba huku
akitabasamu
“Mambo yamekwenda
vizuri mama.Ilikuwa ni safari
nzuri ambayo naweza kusema
ilikuwa na mafanikio.Mimi na
Najma tulipata nafasi nzuri sana
ya kufahamiana na kwa bahati
nzuri tumejikuta wote kila
mmoja akimuhitaji
mwenzake.Binafsi nimekubali
kumuoa Najma” akasema
Mathew na uso wa Habiba
ukachanua kwa tabasamu pana
“Utanifanya nipasuke kwa
furaha Abu Zalawi. Ni kweli
umefanya maamuzi hayo ya
kumuoa Najma?
“Ndiyo mama.Nimeamua
nitamuoa Najma” akasema
Mathew
“Abu kauli hiyo ni nzito
sana ninakuomba ujipe muda
ujitafakari tena na ujiridhishe
kama kweli uko tayari kumuoa
Najma.Sitaki nikushinikize
kwani unayekwenda kumuoa ni
mwanangu na sitaki apatwe
matatizo” akasema Habiba
“Usiwe na hofu
mama.Nimekwisha jitafakari
vya kutosha na kujiridhisha
kwamba ninamuhitaji
Najma.Mama wewe mwenyewe
unayafahamu maisha yangu….”
“Shhhh…” akasema Habiba
na kumzuia Mathew asiendelee
“Tukiwa hapa ndani
hatuzungumzi masuala yale
kwani anaweza akaingia mtu
yeyote na kusikia hivyo chunga
sana.Tutazungumza masuala
yale tukiwa sehemu salama
kama kule
bustanini.Umenielewa Abu”
“Nimekuelewa mama”
akasema Mathew
“Abu naomba nikuweke
wazi kwamba kuna siku chache
sana katika maisha yangu
ambazo nimewahi kufurahi na
siku ya leo ni
mojawapo.Nimefurahi sana kwa
maamuzi yako ya kumuoa
Najma.Sina hakika kama
amekueleza historia yake”
“Amenieleza mama”
akasema Mathew
“Vizuri kama
amekueleza.Alichokueleza ni
kitu cha kweli kabisa.Najma
hakuwahi kuwa na mpenzi na
hakutaka kuwa na mpenzi.Hiki
ni kitu kilichomshangaza kila
mtu kwa nini hataki kuwa na
mpenzi? Nimezungumza naye
mara kadhaa lakini hata yeye
pia alikiri kwamba hafahamu
kwa nini amekuwa
hivyo.Nimejaribu kumkutanisha
na wanaume mbalimbali wenye
sura nzuri na uwezo mkubwa
kifedha lakini
imeshindikana.Mwana mfalme
wa Saudia anampenda mno
Najma lakini hata naye
ameshindwa kupata
nafasi.Sifahamu nilipata wapi
wazo la kumgusia kuhusu
wewe.Nilishangaa
nilipomueleza kuhusu wewe
alionyesha mabadiliko na
akataka kuonana nawe.Ni mara
ya kwanza Najma alinipa jibu
hilo na ndipo nilipokuomba
umuoe mwanangu kwani
alionekana kukupenda kabla
hata hajakutia machoni.Jibu
ulilonipa kwamba uko tayari
kumuoa ni jibu ambalo limenipa
furaha kubwa ambayo siwezi
kuielezea na ndiyo maana
ninakuomba ulitafakari kwa
kna suala hilo na kujiridhisha
kama kweli uko tayari kumuoa
Najma.Nataka Najma awe na
furaha katika maisha
yake.Nataka awe na familia
yenye furaha.Sitaki aje
kumwaga machozi na kujutia
maamuzi yake” akasema Habiba
“Mama sina sababu ya
kukudanganya,nimeamua kwa
dhati ya moyo wangu kumuoa
Najma.Ninamuhitaji katika
maisha yangu na ninakuahidi
kwamba hata mara moja
hataangusha chozi na kujutia
maamuzi yake ya kuolewa
nami” akasema Mathew.Ukapita
muda kidogo na Habiba
akasema
“Ninashukuru kwa
kunihakikishia hilo.Sifahamu
kwa nini nimekuamini namna
hii hadi nikaamua kukuomba
umuoe mwanangu.Yawezekana
ni kwa sababu ninakuchukulia
kama mwanangu na ndiyo
maana nina mipango mikubwa
ya kuyabadili maisha
yako.Nataka nikutoe katika yale
maisha yako ya awali ya mateso
na mahangaiko na kukuingiza
katika maisha mapya yaliyojaa
amani na furaha tele ndiyo
maana nimekupitisha katika
mitihani kadhaa ambayo
umefanikiwa kuishinda”
akasema Habiba na kukaa
kimya kidogo halafu akaendelea
“Utakumbuka kabla ya
kwenda Dubai nilikueleza
kwamba nitakupatia sehemu ya
utajiri wa Seif .Ni utajiri
mkubwa sana ambao naweza
kusema ni mara kumi zaidi ya
ule utajiri wako uliokuwa
nao.Hautakuwa na ulazima wa
kufanya kazi kwani pesa
inaingia tu na huku wewe mkeo
na watoto mtakaojaliwa
kuwapata mkiishi maisha ya
starehe” akasema Habiba na
kunyamaza akamtazama
Mathew
“Mama mimi
ninakushukuru sana kwa
kuniamini hadi kufanya
maamuzi hayo ya kunipa utajiri
kubwa uliokuwa wa Seif
Jawad.Najiuliza mimi ambaye
unafahamu kabisa kwamba nia
yangu ilikuwa ni kukuua kwa
nini ukanifanyia haya? Kwa nini
ukanipokea na kunifanya
mwanao?akauliza Mathew
“Kuna jambo moja ambao
sikuwa nimetaka kukuweka
wazi bado lakini kwa kuwa
umeuliza nitakueleza.Ninataka
uwe msaidizi wangu”
“Nini?Mathew akauliza kwa
mshangao
“Ninataka uwe msaidizi
wangu.Kama unavyoniona umri
wangu unazidi kusogea hivyo
utafika wakati ambao itanibidi
na mimi nipumzike.Nataka pale
nitakapoamua kupumzika basi
wewe usimame badala yangu”
akasema Habiba
“Kwa nini mimi?akauliza
Mathew
“Kwa sababu unafaa na una
sifa za kuwa mrithi wangu”
akasema Habiba
“Mama una watu wengi
wanaokuzunguka.Sayid Omar
na hata mwanao Abu Dahir kwa
nini umewaacha hao wote na
ukanichagua mimi?
“Hao wote na wengine
ambao hukuwataja hawana sifa
za kushika nafasi yangu pale
nitakapokuwa nimeamua
kupumzika.Ni wewe pekee na
msaidizi wako atakuwa Nawal”
akasema Habiba
“Mama utanisamehe kama
nitakuwa nimekukosea lakini
wewe una fadhili ugaidi duniani
na juzi Dubai nimeshuhudia
ukifadhili kundi la IS katika
harakati zake za kuanzisha
kambi yake ya mafunzo nchini
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo.Je unataka mimi nije
kurithi kazi hiyo ya kufadhili
ugaidi na kusababisha watu
wasio na hatia kuuawa?
Akauliza Mathew na Habiba
akacheka kidogo
“Bado una mengi
huyafahamu kijana wangu.Bado
una safari ndefu ya kujifunza
kuhusu hayo unayoyasema
hivyo kaa tayari
kujifunza.Usiwe na haraka ya
kutoa majibu na maamuzi,kuwa
na subira.Kule Dubai nilifanya
makusudi kabisa ili uweze
kushuhudia tukio lile na bado
utaendelea kushuhudia
mengine mengi ila nakuomba
uwe mvumilivu.Endelea
kujifunza.Kuna mengi bado
utatakiwa
kuyafahamu.Tuachane na hayo”
akasema Habiba na kunyamaza
kidogo halafu akasema
“Lini mnataka kufunga
ndoa?Mmekwisha lijadili
hilo?akauliza Habiba.
“Mapema
iwezekanavyo.Hakuna sababu
ya kuchelewa” akasema
Mathew na Habiba akatoa
kicheko kikubwa
“Kweli Abu Zalawi
umenifanya niwe na furaha
kubwa.Kwa nini umeamua iwe
mapema hivyo?Hamuhitaji
kupata muda wa kufahamiana
zaidi kabla ya kuingia katika
ndoa?
“Hakuna kitu cha kutuzia
tusifunge ndoa.Mimi na Najma
kila mmoja anamuhitaji
mwenzake,kila mmoja
amekwisha ridhika na
mwenzake hivyo hatuhitaji
kuvuta muda.Jambo la heri
kama hili halihitaji kuvuta
muda.Labda kama una
kipingamizi kinachoweza
kutufanya tusifunge ndoa”
akasema Mathew
“Mimi sina kipingamizi
chochote cha kuwafanya
mkachelewa kufunga ndoa
yenu.Kama maamuzi yenu ni
hayo mimi sina kipingamizi
nitazungumza na wenzangu na
maandalizi yaanze mara moja”
“Ahsante mama lakini kuna
kitu kinaniumiza kichwa
kidogo” akasema Mathew
“Kitu gani Abu?
“Najma hajui chochote
kuhusu historia yangu ya
nyuma.Najiuliza ni vipi endapo
akija kufahamu ukweli kuhusu
mimi? Kwamba huko nitokako
nina mke na watoto?
“Kwa nini umeuliza Abu?
“Nimeuliza kwa sabau
dunia imekuwa ndogo sana hivi
sasa”
“Hatalifahamu hilo na hata
akilifahamu italazimu aufahamu
ukweli hivyo jambo hilo
lisikuumize kichwa” akasema
Habiba
BAADA YA SIKU TATU
Nyumbani kwa Habiba
Jawadi kulikuwa na heka heka
za maandalizi ya harusi ya
Najma na Mathew.Ni siku ya
tatu tu toka waliporejea kutoka
Dubai na Mathew kutamka
kwamba anataka kumuoa
Najma.Maandalizi makubwa
yalifanywa katika bustani nzuri
ambako ndiko sherehe
zingefanyika.
Mathew Mulumbi
alisimama dirishani katika
nyumba yake akichungulia
namna maandalizi yalivyokuwa
yakindelea bustanini
“Nimefanya maamuzi
magumu ya kuamua kumuoa
Najma.Nasikia kuna sauti mbili
ndani mwangu zinakinzana
kuhusu maamuzi haya lakini
naamini nimefanya maamuzi
sahihi kwa wakati muafaka
kabisa.Sikuwa na namna
nyingine ya kuendelea na
misheni yangu zaidi ya kumuoa
Najma.Hii ni misheni nzito na
kubwa zaidi ya nilivyotegemea
na inahitaji maamuzi kama
haya.Lakini bado kuna mambo
ambayo bado najiuliza kuhusu
Habiba Jawad.Anafahamu mimi
ni nani anafahamu kwa nini
niko hapa,lakini juzi aliniambia
kwamba anataka mimi niwe
mrithi wake kwa nini hanioni
mimi kama mtu hatari kwake?
Inanibidi niwe makini sana na
nifikiri mara mbili zaidi yake
kwani vinginevyo nitashindwa
kutimiza misheni yangu.Niko
kwenye uti wa mgongo wa
ugaidi na lazima niuvunje ili
ugaidi ukose nguvu.Lakini kama
alivyosema Habiba kwamba
nina mengi ya kujifunza
bado.Alisema kuna mengi bado
siyafahamu na ili niyafahamu
hayo yote,maamuzi haya
niliyoyafanya ya kumuoa Najma
ni sahihi”akawaza na sura ya
Najma ikamjia akatabasamu
“Ni mwanamke mzuri
mwenye adabu na
mnyenyekevu.Wanawake wa
aina yake ni nadra sana
kupatikana zama
hizi.Nitajitahidi kufanya kila
niwezalo ili kumlinda siku moja
asijitie uamuzi wake wa
kuolewa nami japokuwa nina
uhakika siku moja lazima
ataufahamu ukweli na utaumia
sana.Lakini ni vipi kama
nitajikuta nimezama mapenzini
na kuamua kusahau kila kitu
kuhusu misheni yangu? Kwa
mwanamke kama Najma hilo
linawezekana kabisa”akawaza
na kutabasamu
“Kama hilo likitokea na
nikajikuta nimeamua
kukubaliana na ile kauli ya
Habiba kwamba hapa ndipo
mahala ninapotakiwa niwepo
basi nitakuwa nimekubali kuwa
mrithi wa Habiba na kuendelea
kufadhili makundi ya kigaidi’
akawaza na kucheka kidogo.
“Hiki ni kichekesho.Mathew
Mulumbi kutoka ujasusi hadi
kuwa mfadhili wa
ugaidi”akawaza na kucheka
tena
“Wengi hawatanielewa
lakini iko siku nitakuwa shujaa
wa dunia” akawaza Mathew
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Nyumbani kwa Germinus
Mapupu balozi wa jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo nchini
Tanzania maandalizi ya chakula
cha jioni kwa ajili ya wake za
marais wa Congo na Rwanda
yalikuwa yanaendelea.Asubuhi
na mapema gari maalum
lililowabeba wapishi wa
kimataifa walioletwa na nchini
na Melanie Davis liliwasili na
bila kupoteza muda wakaanza
maandalizi.Wapambaji nao
walifika na kuanza kuandaa
sehemu watakapokutana akina
mama hao.Ulinzi uliimarishwa
sana toka asubuhi na kila
aliyeingia mahala hapa
alipekuliwa.Kwa bahati nzuri
gari la wapishi liliwahi sana
kufika kabla ya askari
hawajawasili hivyo
hawakukaguliwa.
Wake za marais kutoka nchi
mbali mbali tayari walikwisha
anza kuwasili jijini Dar es
salaam kwa ajili ya mkutano
mkubwa wa wake za marais na
miongoni mwa wageni wa
mwanzo kabisa kuwasili ni
wake za maraisi wa Congo na
Rwanda.Kwa siku nzima mke
wa Rais wa Tanzani Millen
Kelelo alikuwa na kazi ya
kuwapokea wake za marais
walioendelea kuwasili jijini Dar
es salaam kwa ajili ya mkutano
ambao ungefunguliwa siku ya
jumapili na Rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Dr
Fabian Kelelo.Ulinzi
uliimarishwa mno katika jiji la
Dar es salaam na hasa katika
mahotel ambako wageni
walifikia.Hadi wageni
walipoanza kuwasili hakukuwa
na taarifa yoyote ya
kiintelijensia iliyoonyesha
kuwapo kwa kitisho cha
usalama.
Hadi ilipofika saa kumi na
moja za jioni tayari wake za
marais hamsini na nne
walikwisha wasili.Millen Kelelo
alirejea ikulu kujiandaa kwa
ajili ya kuhudhuria katika
chakula cha usiku nyumbani
kwa balozi Germinus Mapupu
kwani kwa jioni ile hakukuwa
tena na mgeni mwingine
aliyetarajiwa kuwasili
Akiwa katika maandalizi ya
kuelekea katika chakula hicho
cha jioni akaingia mumewe Dr
Fabian Kelelo
“Mambo yamekwendaje?
“Siku imekuwa fupi sana
mambo ni mengi.Wageni
hamsini na nne wamekwisha
wasili hadi hivi sasa na wengine
watawasili kesho.Katika hao
waliokwisha wasili wengi
wanatoka nchi za Afrika”
“Vipi kuhusu nchi za
Ulaya,Asia na Amerika?akauliza
Dr Kelelo
“Nadhani wengi watawasili
kesho.Usiwe na hofu Fabian
watakuja.Wengi wamekwisha
nihakikishia kwamba watafika
na nina uhakika watakuja”
akasema Millen
“Hakuna tatizo hata
wasipofika lakini hao waliofika
wanatosha kabisa kufikisha
ujumbe kwa dunia” akasema Dr
Fabian na kumshika mkewe
mikono
“Millen nakuhakikishia
mkutano huu
utafanikiwa.Ahsante sana kwa
kulileta wazo hili.Dunia nzima
kwa sasa macho yao
yameelekezwa Tanzania.Dunia
nzima inajua kuna kitu
kinaendelea Tanzania” akasema
Dr Fabian na kumbusu mkewe
“Ahsante sana Millen”
“Fabian umekwisha
nishukuru zaidi ya mara
hamsini kwa siku hii ya leo”
akasema Millen huku akicheka
“Hata nikisema ahsante
mara elfu kumi bado
haitoshi.Jambo hili unalolifanya
ni jambo kubwa kwa
nchi.Umepambana kuhakikisha
jina la Tanzania kisiwa cha
amani linarejea kutamkwa na
dunia nzima na katika
kulithibitisha hilo wake za
marais wa jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo na
Rwanda wanakwenda
kuufungua ukurasa mpya usiku
wa leo na nina uhakika huu
utakuwa ni mwanzo mzuri wa
kumaliza msuguano
unaoendelea hivi sasa baina ya
nchi zao.Hongera sana Millen
kwa kulifanikisha hilo” akasema
Dr Fabian na kumbusu tena
mke wake kisha akamuacha
amalizie kujiandaa.Baada ya
kumaliza kujiandaa akamuaga
mumewe na kuondoka kuelekea
nyumbani kwa balozi wa Congo
nchini Tanzania
Ulinzi ulikuwa kali na
walioruhusiwa kuingia mle
ndani ni watu maalum tu
waliopewa mwaliko.Jeshi la
polisi liliimarisha ulinzi eneo
lote la kuzunguka makazi yale
ya balozi Mapupu.Saa moja na
nusu Millen Kelelo mke wa Rais
wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania akawasili katika
makazi ya balozi
Mapupu.Alipokelewa na balozi
Mapupu na mke wake
akakaribishwa na burudani
nzuri ya ngoma za asili.Dakika
kumi na tano baadae Rebeca
Eyenga mke wa Rais wa jamhuri
ya kidemokrasia ya Congo
akawasili akapokewa na Millen
na balozi Mapupu na
kukaribishwa ndani.Dakika
chache baadae mke wa Rais wa
Rwanda akawasili naye kama
ilivyokuwa kwa wengine
akapokewa na Millen na
kukaribishwa ndani.Alistuka
sana alipomkuta Rebeca mle
ndani.Hakuwa ametegemea
“Kwa nini hukuniambia
kama huyu naye
umemulika?Mke wa Rais wa
Rwanda akamnong’oneza
Millen
“Usiwe na hofu.Kuwa na
amani” akasema Millen.
Burudani ya ngoma za asili
ikatolewa kisha balozi Mapupu
akazungumza machache na
kumkaribisha mgeni rasmi
ambaye ni Millen Kelelo ambaye
alianza kwa kumshukuru balozi
Mapupu kwa kumkaribisha
jioni ile vile vile akawashukuru
wote waliohudhuria chakula
kile
“Balozi Germinus
aliponialika nyumbani kwake
kwa chakula aliniambia
kwamba utakuwa ni usiku wa
kipekee kabisa na nilikuwa
najiuliza ameandaa kitu gani
cha kuufanya usiku huo kuwa
wa kipekee? Mimi alinipa kazi
moja tu ya kuhakikisha
ninamualika mke wa Rais wa
Rwanda na nilifanya hivyo naye
kwa heshima kubwa
amehudhuria.Baada ya kuingia
hapa ndani ndipo nikagundua
kitu kikubwa alichokifanya
balozi Mapupu.Ukiangalia
mahala hapa kuna
wakongomani,wapo
wanyarwanda na watanzania
pia.Naamini wapo
wakristu,waislamu pia wa dini
nyingine.Ujumbe ambao
tunaupata kwa hiki
alichokifanya balozi Mapupu ni
kwamba mipaka ya kijiografia
haiwezi kututenganisha.Sisi ni
ndugu
moja.Wakongo,wanyarwanda,w
arundi ,watanzania nakadhalika
sote tu ndugu moja.Mipaka yetu
isitugawe na kujenga hasama
baina ya nchi zetu.Kuanzia
usiku huu tunakwenda
kuidhihirishia dunia kwamba
Afrika Mashariki ni moja na
watu wake ni wamoja” akasema
Millen na kuwainua wake za
marais wa jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo na
Rwanda akawashika mikono na
kusimama kati kati
yao.Akamuita balozi wa
Rwanda na kumtaka akae
upande ule wa Rebeca Eyenga
na balozi wa Congo akamtaka
akae pembeni ya mke wa Rais
wa Rwanda.
“Usiku wa leo tunaufungua
ukurasa mpya wa kutafuta
amani katika nchi zetu.Kwa
muda sasa nchi ya Rwanda na
nchi ya jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo hazina
maelewano mazuri lakini usiku
wa leo tunataka kuanzisha
vuguvugu la kutafuta
amani.Nitawaomba kwanza
wanawake hawa wawili kutoka
ndani ya mioyo yao washikane
mikono wasalimiane na
kumaliza tofauti zao.Nataka
watakaporejea nchini kwao
wakawe chachu ya kutafuta
amani katika nchi zao.”
akasema Millen .Rebeca Eyenga
na mke wa Rais wa Rwanda
huku wote wakitabasamu na
makofi mengi yakipigwa
wakashikana mikono na
kukumbatiana.Watu
wakashangilia.Wakazungumza
na kukumbatiana tena.Mabalozi
wa Congo na Rwanda nao
wakasalimiana na
kukumbatiana kwa
furaha.Wageni waliokuwa
wamealikwa nao wakaanza
kusalimiana kwa
furaha.Lilikuwa ni tukio la aina
yake.
Baada ya tukio lile watu
wakaa mezani kwa ajili ya
kupata chakula.Wageni
wakajipanga mstari na kuanza
kupata chakula.Baada ya
wageni wote kupata chakula
wahudumu wakaanza kupita na
meza kubwa za magurudumu
zilizosheheni vinywaji mbali
mbali na baada ya meza zote za
wageni kusheheni vinywaji
meza tatu za magurudumu
zikapangwa vinywaji mbali
mbali kwa ajili ya wageni
waalikwa kujihudumia
wenyewe pale
watakapohitaji.Ni meza ambazo
zilikuwa zimefunikwa kwa
vitambaa safi na hakuna
ambaye angeweza kuhisi
chochote kibaya.Wakati wageni
wakiendelea kupata chakula
wapishi na wahudumu
wakakusanyika mahala
walikokuwa wametengeneza
jiko lao la muda
“Kazi tumeimaliza.Mabomu
yote yamekwisha tegwa ndani
ya zile meza na kilichobaki ni
kuyalipua.Kinachofuata kwa
sasa ni kuanza kutoka humu
ndani.Hakikisheni wote
mnatoka.Mnafahamu lile gari
letu lilikoegeshwa hivyo kila
mmoja akaingie humo.Nataka
ndani ya dakika kumi kila mtu
awe nje na tuondoke mahala
hapa” akaelekeza Yule mkubwa
wao kisha wapishi na
wahudumu wakaanza
kupungua taratibu mle
ndani.Hakuna aliyeweza
kuligundua hilo kwa
haraka.Ndani ya dakika kumi
tayari wote walikwisha toweka
mle ndani na kuingia katika gari
lao lililokuwa nje.Kiongozi wao
akahakikisha wote wako
salama.Gari lao likawashwa na
kuondoka. taratibu
“Sasa ni ule wakati wa
kuibadili historia” akasema
kiongozi wa kundi lile na
kuchukua kifaa Fulani mithili ya
simu akabonyeza namba
kadhaa halafu akabonyeza
kitufe chekundu na mara
mlipuko mkubwa ukatokea na
kulitingisha lile eneo.
Wakiwa ndani ya gari Yule
kiongozi wao akachukua simu
na kumpigia James Kasai
akamjulisha kwamba
wamemaliza kazi.James
akawapongeza halafu naye
akampigia simu Melanie Davis
akamjulisha kwamba kazi
imemalizika.Melanie Davis
akampigia simu Edwin Mbeko
akamuelekeza kwamba wale
watu wake wamemaliza kazi
hivyo anatakiwa ahakikishe
wameondoka nchini salama
kuelekea Uganda.
“Kazi ndiyo kwanza
imeanza.Afrika Mashariki
itawaka moto” akawaza Melanie
na kuwasha runinga ambako
kulikuwa habari mpasuko
kuhusiana na tukio lile.Kikosi
cha uokoaji na zimamoto
kilikuwa cha kwanza kufika
eneo lile la tukio na kufuatiwa
na vikosi vingine vya
usalama.Hali ya mahala pale
ilitisha.Maiti zilisambaa kila
kona.
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 6: EPISODE 4
Dakika arobaini baada ya
mlipuko ule kutokea,ilianza
kusambaa video ikimuonyesha
kiongozi wa kundi pekee la
waasi lililosalia kutoka jamhuri
ya kidemokrasia ya Congo
James Kasai akijitapa kuhusika
katika shambulio lile kwa
kushirikiana na kikundi cha
kigaidi cha IS huku akieleza
kwamba mashambulio mengine
zaidi yatafuata.Mwisho James
akaahidi kwamba anajiandaa
kurejea Congo kwenda
kuikomboa nchi hiyo.
Dr Fabian Kelelo akiwa
katika makazi yake ikulu
alichanganyikiwa akiwataka
wasaidizi wake wampeleke
eneo la tukio ili akahakiki kama
mke wake yuko hai ama
amekufa.Rais hakuruhusiwa
kutoka mle ndani kwa ajili ya
usalama wake na hakuruhusiwa
hata kushika simu.Kila kitu
kilifanywa na wasaidizi wake.
Akiwa amekaa sofani
ameinamisha kichwa huku
machozi yakimdondoka mmoja
wa wasaidizi wake akamsogelea
akiwa ameshika simu.
“Mzee kuna simu kutoka
kwa Rais Patrice Eyenga”
akasema Yule msaidizi na
kumuibua Dr Fabian Kelelo
kutoka katika dimbwi la
mawazo.Dr Fabian akaichukua
simu ile na kusogea pembeni
huku wasaidizi wake wakiwa
makini sana
“Hallo Patrice”
“Dr Fabian tafadhali
nihakikishie kama Rebecca
yuko salama” akasema Patrice
Eyenga
“Sifahamu Patrice.Sifahamu
kama yuko hai ama vipi.Hapa
nilipo nimechanganyikiwa
ninasubiri taarifa kutoka kwa
watu wangu walioko eneo la
tukio kujua kama kuna mtu
amenusurika” akasema
DrFabian
“Dr Fabian hili jambo
limetokeaje? Uliihakikishia
dunia kwamba usalama ni
mkubwa sana nini
kimetokea?Nataka
kusik…………”Dr Fabian akaitoa
simu sikioni baada ya mmoja
wa wasaidizi wake aliyekuwa
ameshika kompyuta mpakato
kumfanyia ishara kwamba kuna
suala la muhimu sana
analotakiwa kulitazama.
“Patrice naomba dakika
moja nitakupigia” akasema na
kukata simu
“Kuna nini? Akauliza na
kuonyeshwa video ile ya James
Kasai akijitapa kufanya
shambulio lile.
“Aaaaghhh !! akasema kwa
hasira Dr Fabian na kupiga
ngumi meza.Wasaidizi wake
wakamshika na kumsihi atulie
“Tafadhali niacheni.Huyu
muuaji ndiye ame….oh my God !
akasema kwa hasira na kushika
kichwa.Baada ya dakika kadhaa
mmoja wa wasaidizi wake
akamsogelea akiwa na simu
“Mzee kuna simu kutoka
kwa mkuu wa jeshi la polisi
nchini” akasema Yule jamaa na
Rais akaichukua haraka
“Hallo” akasema
“Mheshimiwa Rais”
akasema mkuu wa jeshi la polisi
nchini
“IGP tafadhali niambie mke
wangu yuko salama ! akasema
Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais niko
hapa eneo la tukio na vikosi vya
uokoaji.Hali ni mbaya na
yaliyolipuka ni mabomu matatu
yaliyokuwa yamefichwa katika
meza za vinywaji.Miili yote ya
waliofariki imekwisha
ondolewa hapa kupelekwa
hospitali na tumepata jumla ya
maiti arobaini na sita na
majer………..”
“Kamanda unazidi
kunichanganya kwa taarifa
ndefu.Nataka kujua mke wangu
yuko salama?akauliza Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais
nasikitika kutamka kwamba
mkeo ni mmoja wa waliofariki
dunia katika tukio hilo pamoja
na wake za marais wa Congo na
Rwanda bila kusahau mabalozi
wa Congo na Rwan……”
“Oh Millen..!! akasema Dr
Fabian na kuanguka chini
akapoteza fahamu.Haraka
haraka akachukuliwa na
kukimbizwa katika chumba cha
huduma ya kwanza.
 
SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 6: EPISODE 5
Melanie Davis akiwa katika
chumba chake akifuatilia habari
za kuhusiana na tukio lile huku
mezani akiwa na chupa ya
shampeni simu yake ikaita
alikuwa ni Edwin Mbeko
“Hello Edwin” akasema
Melanie
“Madam wale watu tayari
wamekwisha ondoka na ndege
inayoelekea Nairobi Kenya”
“Ahsante sana Edwin.Kazi
nzuri.Endelea kufuatilia kwa
karibu sana taarifa zote za
usalama na unijulishe kama
kutakuwa na tatizo lolote kwa
upande wetu” akasema Melanie
na kukata simu
“Damu ya wazazi wangu
haitamwagika bure.Lazima
itaondoka na watu wengi na
kama nilivyoahidi huu ni
mwanzo tu” akawaza na
kuchukua glasi ya shampeni
akanywa
“Sikutegemea kama siku
moja ninaweza nikawa mkatili
namna hii lakini ni wao
wenyewe ndio walionifanya
mimi niwe mkatili kiasi hiki
kwa kuwaondoa wazazi wangu
kikatili.Walifanya makosa
makubwa sana kushindwa
kuniua na sasa nitawawinda
usiku na mchana na wote
walioshiriki suala hili watalipa
uovu wao” akawaza Melanie na
simu yake ikaita alikuwa ni
Devotha.
“Hallo Devotha” akasema
Melanie
“Melanie nini
umekifanya?akauliza Devotha
kwa ukali
“Devotha kwa nini badala
ya kunipongeza unaanza
kunifokea?Melanie akahamaki
“Ninakufokea kwa kitendo
ulichokifanya ! akaendelea
kufoka Devotha
“Kwa kitendo
nilichokifanya ! Melanie
akashagaa
“Nilichokifanya si ndicho
nilitumwa kukifanya? Sasa
nimekosea wapi?akauliza
Melanie
“Umekosea sana
Melanie.Kwa nini
umewashirikisha IS? Kwa nini
umeshirikiana na magaidi?
Akauliza Devotha kwa ukali
“Devotha mlinituma Afrika
Mashariki kwa ajili ya misheni
maalum hivyo basi ni jukumu
langu kuhakikisha misheni
inafanikiwa bila kujali
ninashirikiana na
nani.Ninaomba msianze
kunivuruga niacheni nitekeleze
kazi mliyonituma niitekeleze”
akasema Melanie kwa ukali
“Melanie hujui kwamba
kwa kushirikiana na magaidi wa
IS unalifanya suala hili kuwa
kubwa zaidi tofauti na
tulivyokuwa tumelipanga?
“Nimekwisha kueleza
Devotha na ninarudia tena
kukueleza kwamba hii ni
misheni yangu na ninaitekeleza
vile nitakavyo.Naomba kama
huna lingine la kunieleza
tafadhali kata simu ! akasema
Melanie kwa ukali
“Nisikilize Melanie.Kuanzia
sasa hakuna tena mashirikiano
baina yako na hao magaidi wala
kikundi kingine
chochote.Unafanya kitu cha
hatari sana Melanie.Mpango
huu ni wa siri kubwa lakini kwa
hiki ulichokifanya cha
kuwashirikisha waasi na
magaidi kitaufanya mpango
wetu huu
kufahamika.Ninakuelekeza
kuanzia sasa vunja kabisa
mahusiano yoyote uliyo nayo na
hao watu.Umenielewa
Melanie?! Akauliza Devotha
“Devotha kwa mara ya
mwisho ninarudia kukusisitiza
kwamba mmenituma kufanya
kazi na nitaifanya kwa jinsi
nitakavyo mimi.Naomba iwe ni
mara ya mwisho kunifokea bila
kujua ni magumu gani nimepitia
hadi kufanikisha tukio lile
kubwa ! akasema Melanie na
kukata simu
“Huyu Devotha kwa nini
ananilazimisha nimuondoe
kabla ya wakati wake?Yeye pia
yumo katika orodha ya watu
ambao lazima damu yao
imwagike kwani ni yeye
aliyemfuata mama yangu na
kumshawishi ajiunge katika
siasa.Kwa kuwa anaonekana
kutaka kunipanda kichwani
dawa yake ni ndogo tu.Lazima
nimuondoe na kazi hii ataifanya
Gosu Gosu.Nitamtuma kwenda
Ufaransa kumuua Devotha”
akawaza Melanie na kuinua
glasi yake ya shampeni
akanywa.
NDUGU MSOMAJI TUKUTANE
SEHEMU IJAYO……………..
 
asante sana tena sana tunaomba mwendelezo wa hii kitu mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom