Riwaya: Siri

Riwaya: Siri

Poti ni baridi lkn nimejikuta nabana pumzi hadi jasho inapenya ktk uti wa mgongo
 
Hatari sana

Hadi wakati huu bado sijaliona kosa la raisi. .kuamua kumshikilia Olivia na mzee agrey. ..

Hata kama mimi ningekuwa ndiye raisi ninge fanya kama alivyo fanya raisi. ... story nzuri sana

Ila Kuna baadhi ya vipande kwa namna fulani vinahusiana na simulizi ya peniela
 
Jana ilikuwa siku njema sana leo dah, inabidi na mm niiombe pm tu nn?mwenye nayo jamani atupiee arostoooo imetosha wajameni
 
Habar za muda huu wakuu...Huku kwetu leo changamoto ilikuwa umeme....Wacha tushushe vitu
 
SIRI
MTUNZI: PATRICK CK
PART 1 SEASON 7
EPISODE 1
Mathew na Gosu Gosu
waliwasili katika hospitali ya
Dr Philip.Kabla gari
halijasimama vizuri tayari
Mathew alikwisha fungua
mlango akaruka nje na
kumshusha Ruby akambeba
na kuanza kukimbia naye
kuelekea mapokezi
“Please Ruby don’t die!!
Akasema Mathew
Wauguzi walipomuona
Mathew akiwa amembeba
mgonjwa aliyechafuka damu
haraka haraka wakaleta
kitanda na kumtaka Mathew
amlaze mgonjwa kitandani
“Huyu mgonjwa amepata
ajali?akauliza muuguzi
mmoja
“Dr Philip yuko wapi?
Akauliza Mathew
“Dr Philip yuko katika
chumba cha upasuaji
anafanya upasuaji kwa
mgonjwa” akasema mmoja
wa wauguzi .
“Gosu Gosu” Mathew
akasema na kumfanyia
ishara Gosu Gosu asukume
kile kitanda yeye
akatangulia akikimbia
kuelekea katika chumba cha
upasuaji.Hospitali ile
alifahamu vyema kwani
amekuwa akifika pale mara
kwa mara.Wauguzi walibaki
wameduwaa wakishangaa.
Mathew aliufungua
mlango wa chumba cha
upasuaji na Gosu Gosu
akaingiza kitanda kile
alichokuwa amelala
Ruby.Muuguzi aliyekuwa
mezani katika mapokezi ya
chumba cha upasuaji
akastuka na kusimama kwa
hasira
“Nini kimetokea?Nani
karuhusu mgonjwa huyu
aletwe hapa bila kufuata
utaratibu?akauliza yule
mwanamama muuguzi kwa
ukali.
“Dr Philip yuko
wapi?akauliza Mathew
“Kaka samahani
naombeni mumtoe huyo
mgonjwa wenu nje haraka
sana.Hapa si mahali pa
kuingia kila mtu
anavyotaka.Zipo taratibu za
kufuata kabla ya mgonjwa
kuingizwa hapa.!! Yule
mwanamama akaendelea
kuwa mbogo.
“Daktari gani ameruhusu
mgonjwa wenu aletwe hapa?
Akauliza yule mwanamama
kisha akaenda katika simu
iliyokuwa mezani kwake
akapiga na kuanza
kuzungumza kwa ukali
“Rahel nani karuhusu
mgonjwa aletwe chumba cha
upasuaji bila kufuata
utaratibu? Ninataka
kumfahamu yule ambaye
ameruhusu jambo hili
litokee!! Hamjui kuna
upasuaji mkubwa
unaendelea hapa ndani ?
Tafadhali naombeni
tusiharibiane
kaz….”Akasema kwa ukali
na mara mkono wake
uliokuwa umeshika simu
ukashikwa na kushushwa
chini akageuka kwa hasira
na kujikuta akitetemeka
baada ya kujikuta
akitazamana na mdomo wa
bastora.
“Fungua huo mlango
haraka sana mgonjwa
aingizwe ndani akafanyiwe
upasuaji !! akasema Mathew.
“T..tt..taf……” akasema
yule muuguzi akibabaika
“Fungua mlango haraka
sana!! Akafoka Mathew na
yule muuguzi akafungua
mlango Mathew akaingia
ndani ya chumba cha
upasuaji ambako upasuaji
ulikuwa unaendelea kwa
mgonjwa.Gosu Gosu
akasukuma kitanda na
kukiingiza ndani.Madaktari
na wauguzi waliokuwa
wanaendelea na upasuaji
wakastuka .Dr Philip
aliyekuwa anaongoza
upasuaji ule akavua
kitambaa alichokuwa
amekivaa mdomoni
“Mathew !! akasema kwa
mshangao uliochanganyika
na hasira na kumfuata
Mathew
“What are you doing here
Mathew?! Akauliza Dr Philip
kwa hasira
“Tuko kati kati ya
upasuaji kwa nini umefanya
hivi Mathew? Kwa nini
unakosa adabu hata kidogo
tu? akaendelea kuuliza Dr
Philip
“Dr Philip hatuna muda
mrefu wa mazungumzo
nataka kila kitu
kinachoendelea sasa
kisimame na mgonjwa
wangu ashughulikiwe
kwanza ndipo muendelee na
mambo yenu mengine”
akasema Mathew
“Mathew are you
crazy?!!Tumelifumua tumbo
la mgonjwa na hatuwezi
kusimamisha upasuaji kwa
sababu ya mgonjwa
wako.Tuna kitanda kimoja tu
humu ndani cha
upasuaji.Nakushauri kama
mgonjwa wako yuko katika
hali mbaya mpeleke katika
hospitali nyingine kuokoa
maisha yake lakini kwa hapa
hatutaweza kumsaidia kwa
sasa atapoteza
maisha.Tusiendelee
kubishana muwahishe
hospitali nyingine” akasema
Dr Philip
“Dr Philip huyu ni Ruby
amepigwa risasi.Ni mtu
muhimu mno kwangu na
ninahitaji umshughulikie
haraka apone”
“I can’t do that Mathew
!!Please get out of here now !!
akafoka Dr Philip na
kumsukuma Mathew atoke
nje mara kwa hasira Mathew
akamkaba shingoni
akamsukuma na kumbana
ukutani.Madaktari na
wauguzi walipoona tukio lile
wakahamaki na kutaka
kumfuata Mathew
wapambane naye Gosu Gosu
akatoa bastora na
kuwaelekezea
“Kila mtu asimame
mahala alipo asithubutu
hata mtu mmoja kunyanyua
mguu ama nitamfumua kwa
risasi!! Akafoka Gosu Gosu
akiwa amewaelekezea
bastora
“Dr Philip katika watu
wote humu ndani ni wewe
pekee unanifahamu vizuri
mimi ni nani.Naomba
usilifanye suala hili kuwa
gumu.Muhudumie mgonjwa
wangu haraka sana.Ukiacha
akipoteza maisha
nakuhakikishia hakuna
atakayetoka salama humu
ndani.I’ll kill you all!!
akasema Mathew na
kumuachia Dr Philip ambaye
aliinama na kukohoa
mfululizo
“You are a devil Mathew
!! How could you do this to
me?Kwa miaka hii yote
nimekuwa msaada mkubwa
kwako iweje leo unanifanyia
hivi?akauliza Dr Philip
“Dr Philip sitaki maneno
mengi.Are you going to do it
or not?akauliza Mathew
“What if I say no?
‘Dr Philip try to say no
and I swear I’m going to kill
all of you right now !!
akasema Mathew na
kumuelekezea bastora.
Dr Philip alivimba kwa
hasira alimtazama Mathew
kwa jicho kali.
“Arlight ! Weka silaha
yako chini Mathew! Siamini
kama umekuwa na roho ya
kishetani namna hii !!
akasema Dr Philip taratibu
Mathew akashusha chini
mkono wake ulioshika
bastora.Dr Philip akaenda
katika meza ile ambayo
mgonjwa alikuwa amelazwa
akiendelea kufanyiwa
upasuaji
“Jamani hatuna namna
Zaidi ya kusimamisha
upasuaji vinginevyo
yataibuka mambo mazito
humu ndani”
“Dr Phill…….” Daktari
mmoja akafungua mdomo
wake akataka kusema kitu
lakini Mathew aliyekuwa
karibu akamuonya
“Shut up !! Sitaki kusikia
mtu akiongea humu Zaidi ya
Dr Philip.Fanyeni kile
atakachowaelekeza!! Akafoka
Mathew
Mashine kadhaa
alizokuwa amefungwa yule
mgonjwa aliyekuwa
kitandani akifanyiwa
upasuaji zikafunguliwa na
mara mashine ya kuonyesha
mapigo ya moyo ikaanza
kutoa mlio na kusoma
sifuri.Dr Philip akatikisa
kichwa kwa
uchungu.Mgonjwa yule
waliyekuwa wakimfanyia
upasuaji alifariki
dunia.Akashushwa na
kuwekwa katika kitanda cha
wagonjwa kisha Ruby
akalazwa katika kitanda cha
upasuaji haraka haraka
mashine zikaunganishwa
wakaanza kuzitafuta risasi
kwa kutumia mashine
maalum za kupiga picha
wakaziona risasi kisha
upasuaji ukaanza
haraka.Nyuso za madaktari
wale bado zilionyesha
simanzi kubwa kwa kile
kilichokuwa kimetokea kwa
mgonjwa yule kufariki dunia.
“Mathew tumekwisha
kubali tunamshughulikia
mgonjwa wako tafadhali
naomba mtoke nje.Chumba
hiki ni kwa watu maalum
tu.Show some respect !
akasema Dr Philip
“I’m not going
anywhere.Nataka
nihakikishe kila
kinachoendelea humu na
ikitokea mgonjwa wangu
akafariki ninawahakikishia
ninyi nyote hakuna
atakayetoka salama ndani ya
chumba hiki! akasema
Mathew akamfanyia ishara
Gosu Gosu atoke nje
kuhakikisha kunakuwa
shwari.
“Let’s do everything to
save this
woman.Anamaanisha
anachokisema huyu jamaa
he’s going to kill us all
mwanamke huyu
akifa.Tufanyeni kila
kinachowezekana” akasema
Dr Philip taratibu
“Do you know
him?akauliza daktari
mwingine lakini Dr Philip
hakujibu kitu.
“Kwa nini Devotha
amefanya jambo kama hili?
Kwa nini ametaka kumuua
Ruby?Ni kweli alikuwa na
nia ya dhati ya kushirikiana
nasi katika kuutafuta ukweli
au alikuwa na lengo lake
lingine? Mathew akajiuliza
“Nilifanya kosa kubwa
kumuamini Devotha kwa
haraka kiasi kile lakini
sipaswi kujilaumu sana kwa
namna alivyojitolea kuniokoa
na yeye mwenyewe
kuhatarisha maisha yake
mtu yeyote lazima
angemuamini.Nitampata tu
na atanipa majibu kwa nini
alitaka kumuua Ruby mtu
wangu wa muhimu sana”
akawaza Mathew na
kuyaelekeza macho yake
pembeni alikokuwa
amelazwa mgonjwa yule
aliyefariki dunia baada ya
upasuaji kusimama.
“Mungu atanisamehe
kwa hiki nilichokifanya
lakini nimelazimika kufanya
hivi ili kuokoa maisha ya
Ruby.Nchi iko katika hatari
kubwa ya mashambulizi ya
kigaidi na katika kuwatafuta
magaidi hawa ninamuhitaji
mno Ruby” akawaza Mathew
na kumtazama Dr Philip
“Dr Philip ni rafiki yangu
mkubwa na kwa muda mrefu
amekuwa ni msaada
mkubwa kwangu.Kila pale
ninapokuwa katika
operesheni zangu na kuhitaji
msaada wa kitabibu
humkimbilia
yeye.Nimemuumiza sana
kwa hiki nilichokifanya leo
na ninaamini utakuwa ni
mwisho wa urafiki wetu”
akawaza Mathew akiendelea
kushuhudia risasi zikitolewa
katika mwili wa Ruby
Risasi tatu zilitolewa
huku Mathew akishuhudia
zikawekwa katika kisahani
cha bati.Ulikuwa ni upasuaji
uliochukua saa mbili.Baada
ya kuhakikisha hakuna tena
risasi iliyobaki mwilini Dr
Philip akaelekeza sehemu
zilizopasuliwa zianze
kushonwa,akaondoka pale
mezani akiwa amejaa hasira
akamfuata Mathew
“Mathew let’s talk!
Akasema Dr Philip kwa ukali
na kumuongoza Mathew
wakaingia katika chumba
cha kubadilishia mavazi
akamtazama Mathew kwa
hasira
“Tumefanya
ulichokitaka.Tumeua
mgonjwa kwa makusudi
kabisa kwa ajili ya
kumuokoa mgonjwa
wako.Ninakuapia Mathew
damu ya mgonjwa yule
ambaye ameuawa bila hatia
itakuandama kwa maisha
yako yote” akasema Dr Philip
na kuendelea kumtazama
Mathew kwa hasira
“Siamini Mathew kama
kweli ni wewe ndiye
uliyefanya hivi.Mathew
ninayemfahamu mimi
hawezi akafanya kitu kama
hiki ulichokifanya leo.Nani
amekuharibu kichwa chako
namna hiyo Mathew?Hiki
uli…”
“Enough !..akasema
Mathew kwa ukali
“Sijutii nilichokifanya Dr
Philip” akasema Mathew na
kuendelea kumtazama Dr
Philip kwa macho makali
“Sikiliza vyema Dr
Philip.Nchi iko katika kitisho
kikubwa cha mashambulio
ya kigaidi.Usiku huu
kumefanyika shambulio la
kigaidi katika hospitali ya
Mtodora na mpaka sasa
haijulikani watu wangapi
wamepoteza maisha.Magaidi
wamejipanga kufanya
mashambulizi Zaidi na
juhudi za kuwadhibiti
magaidi hao
zinaendelea.Mwanamke yule
aliyepigwa risasi ana
umuhimu mkubwa sana
katika kuwatafuta magaidi
hawa.Kuna mambo
makubwa yanaendelea hapa
nchini huyajui hivyo
nilichokifanya ni kitu sahihi
kabisa.Kwa namna Ruby
alivyo muhimu katika vita
hii ilikuwa lazima nifanye
chochote kile ili aweze
kupona.” akasema Mathew
kwa ukali kisha wakaendelea
kutazamana
“Look Dr Philip.Najua
nilichokifanya
hakijakufurahisha lakini
nimefanya kwa ajili ya
usalama wa taifa.Tuko
katika operesheni nzito sana
hapa nchini na Ruby ana
umuhimu mkubwa katika
opresheni hiyo.N…..”
“Mathew sitaki kusikia
tena kitu chochote kutoka
kwako.Tumekwisha ua
mgonjwa asiyekuwa na hatia
kwa sababu ya mgonjwa
wako.Kitu pekee
ninachokitaka sasa
hivi…………..” akasema Dr
Philip na kunyamaza
akamtazama Mathew
“Wanamalizia kufunga
sehemu zilizopasuliwa na
baada ya kumaliza
utaondoka na mgonjwa wako
sitaki kumuweka hapa
katika hosptali
yangu.Utampeleka kokote
unakojua wewe lakini si
katika hospitali hii.One more
thing Mathew..” akanyamaza
tena na kuvuta pumzi ndefu
na kusema
“Utakapoondoka hapa
iwe ni mwisho wako
kukanyaga tena hapa.Forget
about me,sahau kama
tumewahi kuwa marafiki
kwani urafiki wetu wa muda
mrefu umeishia hapa!!
Akasema Dr Philip
“Dr Philip !!akasema
Mathew
“Usiseme chochote
Mathew.It’s over !! We’re
over !! akasema Dr Philip na
kutoka ndani ya kile chumba
akarejea katika kitanda cha
upasuaji ambako madaktari
walikuwa wanaendelea
kushona sehemu
walizopasua
“Tunampeleka wodi gani
huyu mgonjwa?akauliza
mmoja wa wauguzi
“Hatuna nafasi ya
kumuweka katika hospitali
yetu.Mtu wake aliyemleta
ataondoka naye na
kumpeleka anakojua yeye!
akasema Dr Philip na Ruby
akawekwa katika kitanda
akiwa hana fahamu.Dr
Philip akamfuata tena
Mathew
“Mathew mgonjwa wako
tayari tumekwisha mfanyia
upasuaji na sasa uko huru
kumpeleka mahala
unakotaka lakini siwezi
kumuweka katika hospitali
yangu!! Akasema Dr Philip
“Dr Philip please don’t do
this to me” akasema Mathew
“Mathew nilichokisema
hakitabadlika.Tafadhali
mtoe mgonjwa wako na
umpeleke mahala
unakotaka.Tafadhali
Mathew tunahitaji kuendelea
na shughuli nyingine kuna
wagonjwa wengine
wanahitaji upasuaji”
akasema Dr Philip.Mathew
akamtazama kwa muda
kisha akasema
“Fine.I need an
ambulance.Mgonjwa huyu
siwezi kumuweka katika gari
dogo” akasema Mathew
“Hilda piga simu gari la
wagonjwa lifike hapa haraka
sana” akaelekeza Dr Philip
na Hilda yule mwanamama
wa mapokezi ya chumba cha
upasuaji akapiga simu na
baada ya dakika mbili
likafika gari la wagonjwa
Ruby akaingizwa garini.
“Tunaelekea
wapi?akauliza dereva wa
gari lile la wagonjwa
“Shuka garini” akaamuru
Mathew na yule dereva
akashuka
“Gosu Gosu nifuate na
gari letu nitaendesha hili
gari la wagonjwa” Mathew
akamwambia Gosu Gosu na
kuingia katika gari la
wagonjwa akandoka pale
hospitali akiwaacha watu
wote katika mshangao
mkuwa.Kilichotokea pale
kilikuwa ni kama filamu
lakini ni tukio halisi.
“Let’s get back to work!
Dr Philip akawaambia
madaktari na wauguzi
ambao bado walikuwa katika
taharuki kubwa kufuatia
tukio lile.
“One more thing !
akasema Dr Philip
“Kilichotokea hapa
kitabaki humu
humu.Hakuna mtu mwingine
wa nje kufahamu kwani
itakuwa mbaya Zaidi kwa
upande wetu hasa mimi
hivyo naomba kila mmoja
ajitahidi kuufunga mdomo
wake kama vile hakujatokea
kitu chochote” akaelekeza Dr
Philip na kazi zikaendelea
kama kawaida
Mathew baada ya kutoka
nje ya hospitali ya Dr Philip
akapunguza mwendo wa gari
na kutoa simu yake
akaandika namba na kupiga
simu ikaita na kupokelewa
“Hallow Mathew
Mulumbi”ikasema sauti ya
upande wa pili
“Dr Hiran habari yako”
akasema Mathew
“Mimi mzima kabisa
Mathew.Vipi wewe
mzima?Uko kimya sana siku
hizi Mathew” akasema Dr
Hiran
“Dr Hiran uko wapi sasa
hivi?
“Niko hapa hospitali
ninajiandaa niondoke”
“Usiondoke tafadhali
ninakuja hapo sasa hivi nina
shida nahitaji msaada”
“Karibu sana Mathew
utanikuta hapa” akasema Dr
Hiran
“Mungu aendelee
kumpigania Ruby
apone.Nitafanya kila lililo
ndani ya uwezo wangu
kuhakikisha
anapona.Nitamlilia Mungu
kwa machozi yote
asimchukue Ruby bado
ninamuhitaji sana” akawaza
Mathew
Alifika hospitali
anakofanya kazi Dr Hiran
akampigia simu akamtaka
amfuate.
“Mathew ! akasema kwa
mshangao Dr Hiran baada ya
kumona Mathew katika gari
la wagonjwa.
“Dr Hiran nimekuja
kwako kuomba msaada
wako.Ninaye mgonjwa
wangu amefanyiwa upasuaji
katika hospitali Fulani lakini
nataka akatibiwe nyumbani
kwangu.Nimekufuata
unisaidie kwa hilo ndugu
yangu.Niko tayari kwa
gharama zozote hata mara
mbili Zaidi kwa ajili ya
kumuhudumia mgonjwa
wangu huyu
nyumbani.Tafadhali sana Dr
Hiran” akasema Mathew.Dr
Hiran akafungua mlango wa
gari na kumtazama Ruby
ambaye bado hakuwa na
fahamu
“Nini tatizo lake huyu
mgonjwa hadi akafanyiwa
upasuaji?Kwa nini hutaki
akae hospitali ambako ni
rahisi sana kupatiwa msaada
kila pale hali yake
itakapokuwa mbaya? Kwa
namna alivyofanyiwa
upasuaji anahitaji uangalizi
wa karibu sana na
ninashauri alazwe hapa
hospitali” akasema Dr Hiran
“Dr Hiran sitaki alazwe
hospitali kwa sababu ya
usalama wake.Kama
inawezekana nyumba yangu
inaweza kuwa hospitali ya
muda kwa ajili ya mgonjwa
wangu.Usihofu kuhusu pesa
nitalipa kiasi chochote
kitakachohitajika hata na
Zaidi lakini ninachohitaji ni
uangalizi wa mgonjwa wangu
akiwa nyumbani” akasema
Mathew na Dr Hiran
akazama katika mawazo
“Dr Hiran muda
unakimbia sana naomba jibu
tafadhali”
“Huko walikomfanyia
upasuaji walifanya makosa
makubwa sana kuruhusu
ukaondoka na mgonjwa
akiwa bado kwenye hali
hii.Anahitaji uangalizi wa
karibu sana kwani hali yake
inaweza kubadilika muda
wowote.Ngoja nikaandae
vifaa ambavyo nitavihitaji”
akasema Dr Hiran na
kurejea ndani baada ya
dakika chache akarejea
akiwa na gari ambalo
lilikuwa na vifaa ndani yake
safari ikaanza akilifuata gari
la Mathew hadi walipofika
nyumbani kwa Mathew.Ruby
akashushwa garini na
kuingizwa ndani.Gosu Gosu
akamsaidia Dr Hiran
kushusha vifaa alivyokuja
navyo wakaingiza ndani na
mashine kadhaa zikafungwa
kumsaidia Ruby
“Mashine hizi
tunazifunga tu kusaidia
mifumo ya mwili wake ifanye
kazi lakini hali yake
inaendelea vyema.Nimekuja
na chupa kadhaa za damu ili
kumuongezea damu.”
Akasema Dr Hiran na
kuchukua sampuli ya damu
akapima kujua ni aina gani
ya damu aliyonayo Ruby
kisha akamtundikia chupa
ya damu.
“Kwa sasa kilichobaki ni
kusubiri mgonjwa azinduke”
akasema Dr Hiran
“Nashukuru sana Dr
Hiran.Fanya kila uwezalo
bila kujali suala la fedha”
akasema Mathew
“Mathew suala la fedha
halina kipaumbele sana kitu
kikubwa ni kuokoa
uhai.Lakini nini hasa tatizo
la mgonjwa?Kwa nini
alifanyiwa upasuaji?akauliza
Dr Hiran
“Alipigwa risasi”
“Dah ! Ni nani huyo
mkatili aliyefanya kitendo
hicho kwa mrembo kama
huyu?akauliza Dr Hiran
huku akimtazama Mathew
“Mathew una hakika
hapa tulipo tuko
salama?akauliza tena
“Usihofu Dr Hiran tuko
salama na ndiyo maana
nimemleta mgonjwa wangu
hapa.Endelea kumtazama
mgonjwa mimi na
mwenzangu tuna
mazungumzo kidogo”
akasema Mathew kisha
akamchukua Gosu Gosu
wakaenda katika ofisi yao
“Najaribu kutafakari
sababu ya Devotha kufanya
hivi alivyofanya lakini
sijapata jibu” akasema Gosu
Gosu
“Hata mimi nimetafakari
sana jambo hili.Tulimuamini
Devotha kama mwenzetu na
sijui kwa nini amebadilika
na kutaka kumuua
Ruby.Hatutaweza kupata
jibu kwa nini amefanya hivi
hadi pale tutakapomtia
mikononi.Tumuombee Ruby
aweze kuzinduka na
kutueleza nini kilichotokea
hapa.Wakati tukimsubiri
Ruby azinduke tuendelee
kutafuta namna ya kumpata
Kaiza ambaye ndiye aliye na
Ol……………..” Mathew
akastuka ghafla
“Nini Mathew?akauliza
Gosu Gosu baada ya kuuona
mstuko wa Mathew
“Nimekumbuka komyuta
moja haipo hapa.Ni ile ndogo
aliyokuwa anaitumia Ruby
ambayo ameweka program
zake zote”
“Unadhani Devotha
ameondoka nayo?akauliza
Gosu Gosu
“Hakuna mwingine
anayeweza kuondoka nayo
zaidi yake.Tulimuacha humu
ndani yeye na Ruby na
tuliporejea tumemkuta Ruby
peke yake akiwa amepigwa
risasi.Nashawishika kuamini
lazima Devotha ndiye
aliyeondoka nayo.Vile vile
ameondoka na simu ile
aliyokuwa anaitumia
Ruby.Itakuwa rahisi sana
kufahamu mahala alipo kwa
kufuatilia ile simu
ninazifahamu namba
zake.Kuna vitu hata mimi
ninavifahamu katika
teknolojia ya kompyuta na
mawasiliano.Nimekuwa
karibu sana na Ruby kuna
vitu vingi nimejifunza toka
kwake” akasema Mathew
“Kama unaweza
kufuatilia simu ile na
kufahamu mahala alipo
itakuwa vyema sana.Mimi
ufahamu wangu wa
kompyuta ni mdogo sana na
nimeifahamu kompyuta hivi
karibuni baada ya kuanza
kufanya kazi
kwako.Nimekulia msituni
nikipigana vita.Hatukuwa na
kompyuta kule na hata kama
tungekuwa nayo hakuna
muda wa kujifunza” akasema
Gosu Gosu.Mathew akakaa
katika kompyuta na kuanza
kuitafuta programu ambayo
ingemuwezesha kufuatilia
simu ile aliyoondoka nayo
Devotha.Baada ya muda
akaegemea kiti
“Vipi Mathew?akauliza
Gosu Gosu
“Nimeshindwa kuipata
programu ambayo tunaweza
kuitumia kufuatilia simu ile
aliyoondoka nayo
Devotha.Haya mambo
yanahitaji utaalamu
mkubwa.Mimi utaalamu
wangu ni katika mapambano
na si katika mambo haya ya
teknolojia” akasema Mathew
na kuzama katika tafakari
mara akakumbuka kitu.
“Nisubiri dakika mbili”
akasema na kuelekea
chumbani kwake akafungua
kabati kubwa la nguo na
ndani ya sanduku hilo
kulikuwa na kasiki dogo
akalifungua na kutoa kitabu
Fulani akafunua kurasa
haraka haraka akatabasamu
baada ya kupata kile
alichokuwa anakitafuta
akarejea katika chumba cha
kusomea
“Nina kawaida ya
kuweka kumbu kumbu ya
vifaa vyangu vyote vya
mawasiliano.Kuna namba
Fulani za siri ndani ya simu
ni muhimu sana kuzifahamu
ambazo zinaweza kusaidia
kufahamu mtumiaji wa simu
mahala alipo” akasema
Mathew na kuchukua simu
yake akaandika namba
Fulani kutoka katika kile
kitabu akapiga
“Hallow” ikasema sauti
ya mwanadada upande wa
pili wa simu
“Sasha unazungumza na
Mathew Mulumbi hapa
kutoka Tanzania”akasema
Mathew
“Mathew
Mulumbi?akauliza Sasha
“Ndiyo.Umenisahau?aka
uliza Mathew
“Nikumbushe tafadhali
tumeonana wapi?Najaribu
kukumbuka jina hilo lakini
sikumbuki kama nimewahi
kukutana na mtu kutoka
Tanzania” akasema Sasha
“Tuliwahi kukutana
Mumbai katika klabu
moja.Kuna mtu ulikuwa
unamfuatilia lakini
akagundua Kamba
unamfuatilia akatuma kundi
lake wakakuvamia kukuteka
kwa bahati nzuri nilikuwepo
karibu nikakusaidia
kupambana na wale jamaa
tukawashinda.Tayari
umenikumbuka?
“Ouh ni wewe
kumbe?Sasa
nimekukumbuka
Mathew.Nimelikumbuka na
hili jina.Ni muda wa miaka
kadhaa umepita sasa
hatukuwahi kuwasiliana
ndiyo maana imekuwa rahisi
kusahau jina lako lakini sura
yako bado
naikumbuka.Habari za
Tanzania?akauliza Sasha
“Tanzania salama
kabisa.Vipi wewe
unandeleaje?
“Ninaendelea vyema
Mathew.Uliniahidi utakuja
Marekani lakini mpaka sasa
kimya.Lini utakuja
kutembea huku.Nitafurahi
sana kukuona”
“Nitakuja Sasha kama
nilivyokuahidi”
“Mathew nashukuru
sana kwa
kunikumbuka.Umenikumbus
ha mbali sana” akasema
Sasha
“Bado uko CIA?akauliza
Mathew
“Ndiyo.Kwa sasa
nimerudishwa hapa makao
makuu Langley.Siko tena
katika kazi za nje,kwa nini
umeuliza? Sasha akauliza
“Sasha ninahitaji msaada
wako”
“Sema unahitaji nini
Mathew?
“Nahitaji unisaidie
kufuatilia simu Fulani kujua
mtumiaji wake mahala alipo”
akasema Mathew na Sasha
akaomba ampe namba za siri
za hiyo simu pamoja na
namba za laini ya simu
akamuomba asubiri kwa
dakika chache
“Mathew hujawahi
kuishiwa maarifa.Sikujua
kama unaye mtu ndani ya
CIA anayeweza akatusaidia”
akasema Gosu Gosu
“Ninao marafiki zangu
kutoka katika mashirika
mbalimbali ya kijasusi
duniani ambao huwatumia
kuomba msaada pale
ninapokuwa nimebanwa na
jambo.Huyu Sasha
nilifahamiana naye Mumbai
nilimsaidia kumuokoa
kutoka katika genge la
wahuni.Toka hapo tukawa
marafiki lakini ni muda
mrefu umepita
hatujawasiliana ndiyo maana
imenilazimu kumkumbusha”
akasema Mathew na
kunyamaza baada ya simu
yake kuita alikuwa ni Sasha
“Mathew nimefuatilia
simu hiyo na kuipata mahala
ilipo.Ninakutumia sasa hivi
katika simu yako ramani ya
mahala ilipo simu hiyo
utaendelea kuifuatilia.Kama
kuna msaada Zaidi
utauhitaji utanijulisha”
akasema Sasha
“Ninashukuru sana
Sasha” akasema Mathew na
katika simu yake ukaingia
ujumbe uliotumwa na Sasha
akaufungua.Ilikuwa ni
ramani iliyoonyesha mahala
simu ile aliyoondoka nayo
Devotha ilipo
“Tumempata.Kwa mujibu
wa ramani hii simu
inaonekana ipo katika
bustani ya Kiembe
kavu.Ninahisi kuna mtu
amemfuata mahala
hapo.Nitakwenda
kumfuatilia wewe utabaki
hapa kufuatilia hali ya Ruby
na kulinda
usalama.Hakikisha yule
daktari habanduki mle ndani
na kama kutatokea hatari
yoyote basi utakabiliana
nayo.Bado naamini tuko
katika hatari kwani hatujui
lengo la Devotha kutugeuka
na kukimbia.Umakini
mkubwa sana unahitajika”
akasema Mathew na kuingia
chumbani kwake akabadili
mavazi akachukua bastora
mbili na kuingia garini
akaondoka kuelekea bustani
ya mapumziko ya Kiembe
kavu kumfuata Devotha
“Devotha alifikiri
hataweza
kupatikana.Alikosea
sana,hana sehemu ya
kukimbilia nitamsaka kila
kona hadi nihakikishe
amepatikana na atalipa kwa
hiki alichokifanya.Kama ni
kutusaliti angeondoka kimya
kimya bila kumpiga risasi
Ruby ambaye ni mtu wangu
wa muhimu mno.Nataka
nimuonyeshe kwamba yeye
bado ni mchanga sana katika
hizi kazi”akawaza Mathew
Ilimchukua dakika
ishirini kufika katika bustani
ya Kiembe kavu.Bado simu
ile iliendelea kuonekana
katika ramani aliyotumiwa
na Sasha.
“Devotha anafanya nini
hapa bustanini?Mbona
imekuwa ni muda mrefu
haondoki eneo hili?Kuna mtu
anamsubiri?akajiuliza
Mathew wakati akiegesha
gari akashuka na kuanza
kuifuatilia simu ile kwa
tahadhari kubwa.Alifika hadi
sehemu ambayo ilionyesha
katika ramani kuwa ndipo
ilipo simu.Eneo lile
hakukuwa na mtu.Kulikuwa
na viti vya mbao vya
kupumzikia lakini vilikuwa
tupu.
“Where is she?akajiuliza
Mathew akiangaza kila
upande kwa tahadhari
kubwa lakini hakukuwa na
mtu eneo
lile.Kilichomshangaza bado
aliendelea kuiona simu ile
eneo lile.Akaamua kuipiga ili
kupata majibu na mara
akasikia mlio wa simu katika
maua yaliyokuwa pembeni
ya kiti cha
kupumzikia.Akapekua maua
na kuikuta simu
“Damn you Devotha!!
Akasema Mathew kwa hasira
“Huyu mwanamke ni
mjanja sana na inaonekana
mbinu nyingi za kijasusi
anazifahamu.Alijua
tunaweza kumfuatilia kwa
kutumia simu hii ndiyo
maana akaja akaitupa hapa
ili kutupoteza mwelekeo.Huu
si mwisho Devotha
nitakupata tu.Muda wako
unahesabika” akawaza
Mathew na kumpigia simu
Gosu Gosu akamueleza
kilichotokea
“Huyu mwanamke ni
mjanja sana anafahamu
mbinu za kijasusi hata hivyo
atapatikana tu muda si
mrefu.Vipi hali ya
Ruby?Mathew akauliza
“Bado daktari yuko hapa
anaendelea kumuangalia
anasema maendeleo yake ni
mazuri” akasema Gosu Gosu
“Sawa Gosu Gosu
nitakupigia tena baada ya
muda” akasema Mathew na
kukata simu
“Devotha hakuondoka na
simu hii kwa ajili ya kuja
kuitelekeza hapa.Lazima
kuna mtu aliwasiliana naye”
akawaza Mathew na
kuangalia katika kumbu
kumbu za simu zilizopigwa
lakini hakukuwa na rekodi
zozote.
“Amefuta rekodi zote za
mawasliano na hii
inaonyesha kuna mtu
aliwasiliana naye na ndiyo
maana amefuta kila kitu”
akawaza Mathew na
kumpigia simu Sasha
“Sasha samahani kwa
kukusumbua
tena.Nimefuatilia simu ile na
kuipata lakini nimeikuta
imetelekezwa na
aliyeichukua
hayupo.Ninataka unisaidie
kujua namba ya mwisho
kuwasiliana na simu hii
usiku huu” akasema Mathew
na Sasha akamuomba
asubiri kidogo.
 
SIRI
MTUNZI: PATRICK CK
PART 1 SEASON 7
EPISODE 2
Gari dogo la rangi nyeusi
lilisimama nje ya nyumba
moja ya ghorofa moja
Devotha akashuka na
kumlipa dereva fedha halafu
akatembea kuelekea katika
geti.Akabonyeza kengele ya
getini na baada ya dakika
mbili mlango mdogo wa geti
ukafunguliwa na msichana
ambaye anamfahamu
Devotha
“Karibu sana dada
Devotha” akasema yule
msichana na Devotha
hakujibu kitu akaongoza
moja kwa moja kuelekea
ndani.Aliingia sebuleni na
kumkuta mwanadada mmoja
mweupe sana aliyekuwa
sofani amejilaza akitazama
runinga
“Devotha karibu
sana”akasema yule
mwanadada na kuinuka
akakaa
“Nashukuru sana
Bella”akasema Devotha na
kukaa huku akifumba macho
kwa maumivu
“Devotha are you
okay?akauliza Bella
“I’m okay usihofu”
akasema Devotha
“Utakunywa kinywaji
gani?akauliza Yule msichana
aliyemfungulia geti
“No thank you” akajibu
Devotha
“Devotha kuna tatizo
gani?Si kawaida yako kufika
hapa usinywe hata
maji?akauliza Bella.
“Jane samahani naomba
nizungumze na Bella”
Devotha akamwambia yule
msichana na alipotoka
akamfuata Bella sofani
“Bella watoto wako
wapi?akauliza Devotha
“Wamelala.Kuna nini?
Akauliza Bella kwa wasiwasi
“Sina muda wa kuelezea
kwa sasa lakini naomba
uwaandae watoto
tunandoka”
“Tunaondoka?Tunakwen
da wapi?
“Mko katika hatari
kubwa.Kuna watu
wanajiandaa kuja
kuwachukua watoto
wako.Please Bella sina muda
wa kuelezea tafadhali
jiandae tuondoke” akasema
Devotha
“Devotha sikuelewi.Nani
wanataka kuja kumchukua
mwanangu na kwa
nini?akauliza Bella
“Bella tafadhali
tusiendelee kupoteza
muda.Nitakueleza mbele ya
safari.Jiandae tunaondoka”
akasema Devotha
“Hapana Devotha siwezi
kuondoka hapa hadi
utakaponieleza kuna tatizo
gani” akasema Bella
Devotha akafungua
vifungo vya shati alilokuwa
amevaa na Bella akastuka
“Umefanya nini?
“Nimeshambuliwa na
watu hao ambao wanapanga
kuja kuwachukua
wanao.Tafadhali Bella
naomba uniamini na ufanye
kama ninavyokuelekeza”
akasema Devotha na Bella
akasimama akabaki
anamuangalia Devotha
“Kaiza anafahamu suala
hili?
“Sina mawasiliano
yake.Naomba unipe simu
niwasiliane naye tafadhali”
akasema Devotha na Bella
akazitafuta namba za simu
za mume wake akampigia
lakini simu haikuwa
ikipatikana
“Hapatikani katika
namba zake za
simu”akasema Bella
“Hata mimi nimemtafuta
katika namba zake za simu
hapatikani.Nenda kajiandae
Bella wale jamaa watafika
hapa muda si mrefu
.Tutamjulisha Kaiza jambo
hili” akasema Devotha.Bella
akaenda chumbani kwake
akawatazama watoto wake
mapacha waliolala katika
kitanda pembeni ya kitanda
chao kikubwa.
“Siko tayari mtu yeyote
ahatarishe usalama
wenu.Ninawapenda kuliko
kitu chochote” akasema Bella
na kufungua droo katika
meza yake ya vipodozi akatoa
kitabu akatafuta namba
Fulani ambazo mume wake
Kaiza alimuelekeza azitumie
kumpigia kama kuna
dharura akaziandika katka
simu na kupiga simu
ikapokelewa haraka
“Bella kuna tatizo?
Akauliza Kaiza baada ya
kupokea simu
“Kaiza nimekutafuta
simuni hupatikani”
“Nilikuelekeza utumie
namba hizi kama kuna
dharura kubwa tu.Kuna
tatizo gani? Akauliza Kaiza
kwa ukali kidogo
“Kaiza kuna jambo
limetokea hapa nyumbani
muda huu.Amekuja
Devotha..”
“Devotha?! Kaiza
akastuka sana
“Ndiyo amekuja hapa
muda si mrefu na amenitaka
niwakusanye watoto
tuondoke.Anadai kuna watu
wanapanga kuja kuwateka
watoto”
“Kuwateka
watoto?akauliza Kaiza
“Ndiyo.Anadai hivyo
kwamba kuna watu
wanataka kuja kuwachukua
watoto” akasema Bella
“Bella nisikilize
vizuri.Mwanamke huyo ni
muongo mkubwa”
“Kaiza nini
kimetokea?akauliza Bella
“Bella naomba unisikilize
tafadhali” akasema Kaiza
“Katika kasiki langu
dogo kuna bastora iko
humo.Nilikupeleka katika
mafunzo ya kutumia silaha
nikiamini nyakati kama hizi
zinaweza kujitokeza.Nataka
uichukue hiyo bastora na
ufanye kila unaloweza
kuwalinda watoto
wetu.Jitahidi kuvuta muda
kuna watu ninawatuma hapo
sasa hivi wanakuja
kumdhibiti
Devotha.Mwanamke huyo ni
hatari mno wala usimpe
nafasi ya kuwakaribia watoto
wetu.Umenielewa
Bella?akauliza Kaiza
“Kaiza I’m so
scared.Umeniogopesha sana”
“Usiogope
Bella.Tafadhali kuwa
jasiri.Devotha si mtu mzuri
na ukimpa nafasi ataondoka
na watoto wetu.Tafuta
namna ya kufanya kuvuta
muda wakati timu
ninayoituma inakuja hapo
muda si mrefu” akasema
Kaiza
“Sawa Kaiza ngoja
nijaribu” akasema Bella na
kukata simu akavuta pumzi
ndefu
“Kuna nini
kinaendelea?Devotha
amekuwa kiongozi wa Kaiza
na amekuwa akifika hapa
mara kwa mara amekuwa
rafiki yetu mkubwa,nini
kimetokea leo hadi Kaiza
akatamka maneno
yale?Lazima kuna suala
kubwa limetokea.Ngoja
nifuate ushauri wa mume
wangu yeye ndiye anayejua
kinachoendelea huko katika
shughuli zao.Mtihani
kwangu ni namna ya
kumdhibiti Devotha hadi hao
watu atakaowatuma Kaiza
watakapofika.Sina uwezo
wowote wa kupambana
lakini nitafanya kila
niwezavyo kwa ajili ya
wanangu.Siwezi kukubali
Devotha akawachukua
wanangu.Anataka awafanyie
nini?akajiuliza Bella wakati
akifungua kasiki na kutoa
bastora akaitazama na
kuvua gauni refu alilokuwa
amevaa kisha akavaa suruali
ya jeans na fulana pana
ndefu akaichomeka bastora
ile kiunoni akajitazama
katika kioo bastora haikuwa
inaonekana akashuka
chini.Devotha alipomuona
Bella anashuka akasimama
“Bella tayari
umewaandaa
watoto”akauliza Devotha
“Devotha kuna kitu
naomba ukanisaidie”
akasema Bella na kupanda
ngazi Devotha akimfuata
kwa nyuma.Waliingia katika
chumba ambacho hakikuwa
na kitu kilikuwa kinafanyiwa
ukarabati.
“Nikusaidie nini Bella”
akauliza Devotha mara Bella
akaitoa bastora kiunoni
akamuelekezea Devotha
“Naomba piga magoti
tafadhali !! akasema Bella
kwa ukali
“Bella unataka kufanya
nini?Weka chini bastora
tafadhali !! akasema Devotha
“Devotha piga magoti
chini haraka sana!! Akasema
Bella
“Bella please !! You are
doing a mistake !! akasema
Devotha
“Devotha sitaki utani
katika hili.Piga magoti na
inua mikono juu!! akasema
Bella
“Bella you wont shoot
me..Please put your gun
down !! This is a mistake!!
Akasema Devotha akapiga
hatua moja kutaka
kumsogelea Bella
“Devotha tafadhali
usinisogelee!! Ukijaribu
kupiga hatua moja
nitakupiga risasi ! akasema
Bella.Devotha akamtazama
na kusema
“No Bella you won’t shoot
me.Nimekuja kukuokoa
wewe na familia
yako.Nimekuwa karibu na
familia yenu ndiyo maana
siko tayari watoto wako
malaika wasio na kosa
waingie katika mikono ya
watu wabaya.Tafadhali weka
chini silaha yako Bella”
akasema Devotha
“Devotha piga magoti !!
akafoka Bella
“Bella kwa nini unakuwa
mbishi?Weka silaha yako
chini tafadhali na unisikie
kile ninachokisema.Watu
wabaya wanawatafuta
wanao” akasema Devotha
“Kwa nini wanawatafuta
wanangu?akauliza Bella
“Sikiliza Bella kuna
jambo kubwa linaloendelea
hivi sasa hapa nchini na
linaihusisha idara yetu.Kuna
watu wanataka ku….”
Akasema Devotha akiwa
ameyaelekeza macho yake
kama kinyonga katika
bastora aliyokuwa ameishika
Bella
“Devotha don’t move !!
akasema Bella
“Weka bastora chini
Bella!! Akasema Devotha
akipiga hatua ya pili
“Devotha nitakupiga
risasi tafadhali!! Akasema
Bella
“No Bella you wont shoot
me !! akasema Devotha na
kuinua mguu kabla
hajaweka mguu chini
ukasikika mlio wa
risasi.Jicho la Devotha
lilikuwa katika kidole cha
Bella na alifahamu Bella
anakwenda kupiga risasi
akawahi kujirusha pembeni
kwa wepesi mkubwa.Bella
alipatwa na mstuko mkubwa
baada ya mlio ule wa risasi
kusikika.Aliduwaa kwa
muda na sekunde hizo ndizo
alizozihitaji sana Devotha
akainua ndoo iliyokuwa na
rangi iliyoganda akampiga
nayo Bella mkononi
akapepesuka na kuweka
mkono mmoja ukutani na
kabla hajageuka Devotha
alikwisha fika na
kumtandika teke zito
akaanguka chini na kitu cha
kwanza alichokiwahi
Devotha ni bastora.
“Bella why are you so
stupid? Nimekuja hapa
kukusaidia wewe na familia
yako kwa nini hutaki
kunielewa?akauliza
Devotha.Bella alikuwa chini
akitetemeka.
“Devotha tafadhali
usiwachukue watoto wangu !!
akasema Bella akilia
“You fool !! ninataka
kukusaidia Bella.Sina nia
mbaya na watoto
wako.Ninawapenda kama
watoto wangu ndiyo maana
niko hapa.Tafadhali inuka
twende tukawachukue
watoto tuondoke hapa”
akasema Devotha
“Devotha tafadhali
usiwachukue watoto
wangu.Devotha niko chini ya
miguu yako !! akalia Bella
“Inuka !! akafoka
Devotha
“Devotha kuliko kukuona
ukiwachukua watoto wangu
niko tayari uniue.Niue sasa
hivi Devotha kisha
ukawachukue watoto wangu
uwafanye unachokitaka”
akasema Bella
akilia.Devotha akamtazama
na kuvuta pumzi ndefu na
kumrushia Bella bastora
“Take the gun.Kill me if
you want” akasema Devotha
na Bella akabaki anashangaa
“Simama ! akasema
Devotha na Bella akasimama
“Sina nia mbaya nawe
Bella.Sijaja hapa kukudhuru
wewe na
wanao.Ninawapenda sana na
niko hapa kwa ajili ya
kuwasaidia.Naomba
uniamini Bella ninataka
kuwasaidia lakini kama
hamtaki msaada wangu
fine.Nitaondoka lakini
msinilaumu kwamba
sikuwaonya.Mko tayari
niwasaidie au mnasubiri
watoto waje
wachukuliwe?akauliza
Devotha lakini Bella alikuwa
kimya
“Nijibu Bella kama
mnataka msaada wangu na
kama hamtaki niondoke
zangu” akasema
Devotha.Bado Bella alikuwa
anatetemeka
mikono.Alishindwa aseme
nini.
“Fine.Hamtaki msaada
wangu ninaondoka lakini
kitakachowakuta
msinilaumu” akasema
Devotha na kukishika kitasa
cha mlango akaufungua.
“Wait ! akasema Bella
“Tafadhali niweke wazi
Devotha nini hasa
kinachoendelea?Nani
wanataka kuwachukua
watoto wangu?Nieleze
tafadhali nielewe”
“Bella nimekuwa rafiki
yenu kwa muda mrefu
nimekuwa nikija hapa kwenu
mara kwa mara na watoto
wenu ninawapenda
sana.Kitu gani
kinachokufanya uwe na
wasiwasi na mimi
leo?akauliza Devotha.Bella
akavuta pumzi ndefu na
kusema
“Nilipokwenda chumbani
niliwasiliana na Kaiza
kupitia namba za siri
alizonipatia nimpigie endapo
kuna dharura nikampata
nikamueleza umefika hapa
na unataka kutuchukua
mimi na watoto akanieleza
akanionya nisikupe nafasi ya
kuwachukua watoto.Wewe
na Kaiza mmekuwa watu wa
karibu kwa muda mrefu na
wewe ndiye mkuu wake wa
kazi.Nini kimetokea hadi
Kaiza anipe onyo lile?Nieleze
tafadhali kila kitu.Kama
kweli umekuja kwa lengo la
kutusaidia mimi na wanangu
nieleze kila kitu bila
kunificha” akasema
Bella.Devotha akamtazama
na kusema
“Bella kuna jambo kubwa
linaendelea katika idara yetu
ambalo limezua tofauti
kubwa kati yangu na
Kaiza.Kwa ufupi tu ni
kwamba siko tena katika
idara ile ya siri ya mambo ya
ndani ya nchi na hivi sasa
wananitafuta ndiyo maana
Kaiza amekuonya usinipe
nafasi ya kuwasaidia
akiamini labda lengo langu
ni kuwadhuru.Sina nia hiyo
Bella na ndiyo maana niko
tayari kuwaacha na
kuondoka zangu endapo
hamuhitaji msaada wangu
tena.Kitu ninachotaka
ukifahamu ni kwamba kuna
watu wanapanga mipango ya
kuja kuwachukua hapa wewe
na wanao” akasema Devotha
“Devotha hicho ndicho
ninachotaka
kukifahamu.Watu hao ni
akina nani na kwa nini
wanataka kuwachukua
watoto wangu?akauliza Bella
“Bella hiyo ni hadithi
ndefu na inahitaji muda wa
kutosha
kukuelezea.Tafadhali fanya
maamuzi kama unataka
niwasaidie na kama hutaki
msaada wangu mimi
niondoke zangu” akasema
Devotha Bella alibaki
amesimama akitafakari
“Bella muda unakimbia
fanya maamuzi.Ni wewe
mwenye kufahamu uchungu
wa watoto na si Kaiza hivyo
wewe ndiye unayepaswa
kufanya maamuzi ya
usalama wao.Ninakupa
sekunde kumi za kufanya
maamuzi” akasema
Devotha.Bella alikuwa
anahema haraka haraka
“Sekunde kumi
zimekwisha na umeshindwa
kufanya maamuzi mimi
ninaondoka lakini
kitakachowatokea
msinilaumu kwamba
sikuwaonya” akasema
Devotha na kuanza kupiga
hatua.
“Devotha subiri”
akasema Bella
“Bella please don’t waste
my time.Fanya maamuzi!!
Akafoka Devotha
“Please help us !
akasema Bella
“Are you sure? Akauliza
Devotha
“Tafadhali tusaidie
Devotha.Usiache wanangu
wakatekwa na watu
wabaya.Kama unaweza
kutusaidia tafadhali fanya
hivyo” akasema Bella huku
macho yake yakiwa na
machozi
“Wako wapi
watoto?Haraka sana twende
tukawaandae” akasema
Devotha na kumfuata Bella
wakaingia katika chumba
chao cha kulala
“What a beautifull angels
! akasema Devotha na
kutabasamu alipowaona
watoto wale wakiwa
wamelala katika kitanda
chao.Bella akamuelekeza
mlezi wao awaandae watoto
kwa ajili ya safari.
“Devotha unatupeleka
wapi ukitutoa hapa?akauliza
Bella
“Somewhere safe”
akajibu Devotha
Wakati watoto
wakiendelea kuandaliwa
Devotha akasikia kama
vishindo vya mtu
“Bella kuna watu
wangapi mnaishi
humu?akauliza
“Ni sisi unaotuona hapa
na Kaiza hakuna mwingine”
akajibu Bella
“Fungua mlango
chungulia nje kama kuna
mtu” akasema Devotha na
kuchomoa bastora yake.Bella
akaonyesha wasi wasi
“Bella fungua mlango
angalia kama kuna mtu hapo
nje ya mlango! Akasema
Devotha.Kwa woga Bella
akaenda mlangoni na
kukinyonga kitasa mlango
ukafunguka akajikuta
amesukumwa akaanguka
chini na watu watatu
wakarukia ndani.Devotha
alikuwa mwepesi sana mara
tu Bella aliposukumwa
akaanguka chini tayari
alikwisha rukia katika
kitanda na kumnyakua
mmoja wa watoto
akamuweka kifuani kwake
na kumuelekezea bastora
kichwani.
“Devotha weka silaha
yako chini tafadhali !!
akaamuru mmoja wa wale
jamaa
“Ayoub wewe ni mtu
mdogo sana kunipa mimi
amri! Akasema Devotha
“Devotha ninakuamuru
kwa mara nyingine tena
weka silaha yako chini na
mlaze mtoto kitandani.I have
orders to shoot you !!
akasema Ayoub akiwa
amekunja sura kuonyesha
hana masihara
“C’mon Ayoub you won’t
shoot me.Najua mmetumwa
na Kaiza lakini hata yeye
hatakubali kuona watoto
wake wakiuawa.Kabla
haujaizinga bastora yako na
kunipiga risasi watoto hawa
wawili ambao Kaiza
amehangaika kuwapata
watakuwa wamekufa.Kwa
nini tuwaue malaika
hawa?Niko hapa kuokoa
maisha yao na si kuwadhuru
hivyo wekeni silaha zenu
chini na mniache niendelee
na zoezi langu la kuwaokoa
watoto hawa” akasema
Devotha
“Devotha tafadhali
naomba uweke silaha chini
na umlaze mtoto huyo
kitandani ! akasema Ayoub
“Ayoub ninawapa wewe
na wenzako sekunde kumi
kuweka silaha zenu chini
ama sivyo watoto hawa
watakufa!!
“One ! akaanza kuhesabu
Devotha
“Two !
“Devotha please don’t kill
my children !! akalia Bella
aliyekuwa amesimama
mlangoni
“Three !! akasema
Devotha.Ayoub na wenzake
wakajipanga vyema
“Four !! akasema
Devotha
“five ! Devotha
akaendelea kuhesabu.Bella
akakurupuka na kwenda
kusimama kati kati ya
Devotha na wale jamaa
waliotumwa na Kaiza
“Tafadhalini wekeni
silaha zenu chini.Devotha
hayuko hapa kuidhuru
familia yangu she’s here to
help us.Sikieni
anachokisema na muweke
chini silaha zenu haraka!
Akasema Bella
“Mama tafadhalisogea
pembeni tupe nafasi ya
kutekeleza maagizo!!
Akasema Ayoub
“Ninyi na huyo
aliyewatuma hamfahamu
chochote.Devotha hana tatizo
lolote she’s here to help
us.Tafadhali naombeni
muweke silaha zenu chini na
muondoke hapa haraka
sana!! Akafoka Devotha
“Mama sogea pembeni
tafadhali usitulazimish….”
Akasema Ayoub lakini Bella
akamkatisha kwa ukali
“Kama mnataka kumpiga
risasi Devotha anzeni
kwanza na mimi !! akasema
Bella akimkaribia Devotha
akainyakua simu yake
iliyokuwa mezani na kwa
haraka akampigia Kaiza
“Bella vijana wangu
wamefika hapo nyumbani
tayari?akauliza Kaiza baada
ya kupokea simu
“Kaiza waambie watu
wako waweke silaha zao
chini na waondoke hapa
ndani haraka sana”
“Kwa nini
bella?Nimewatuma waje
wamdhibiti Devotha na
kuwanusuru watoto
wetu”akasema Kaiza
“Devotha hana tatizo
kama unavyodai.She’s here
to help us.She’s here to save
our family!! Akasema Bella
huku akilia
“Bella sikuelewi una
maanisha nini? Nimekueleza
Devotha ni mtu hatari
sana.Tafadhali waache
vijana wangu wafanye kazi
yao niliyowatuma.Nahitaji
sana kumpata Devotha”
“Kaiza hali ya humu
ndani ni mbaya na watoto
wangu ndio wako katika
hatari.Watu
wameelekezeana bastora na
muda wowote wanaweza
wakashambuliana na
waathirika wakubwa
watakuwa watoto
wangu.Tafadhali Kaiza
naomba uwaamuru watu
wako waweke silaha zao
chini.Hivi tuzungumzavyo
kuna bastora katika kichwa
cha mtoto wangu na muda
wowote anaweza akapigwa
risasi.Limalize hili jambo
tafadhali!! Akasema Bella
“Damn !! akasema Kaiza
kwa hasira na kumtaka Bella
ampe simu Ayoub
azungumze naye
“Zungumza na mkuu
wako” akasema Bella na
Ayoub akachukua ile simu
akazungumza na Kaiza kisha
akampa simu Bella na
kuwageukia wenzake
“Stand down ! Ayoub
akawaeleza wenzake na wote
wakashusha silaha zao chini.
“Nyote mtaendelea
kukaa ndani ya chumba hiki
hakuna atakayeruhusiwa
kutoka nje ya chumba
hiki.Yeyote atakayethubutu
atapigwa risasi bila
huruma.Hayo ni maelekezo
kutoka kwa kiongozi wetu!!
Akasema Ayoub
“Kuna watu wanataka
kuja kuwachukua watoto
hawa.Lazima tuwatoe hapa
kwa usalama wao !! akasema
Devotha
“NImesema hakuna
atakayeruhusiwa kutoka
ndani ya chumba hiki bila
sababu.Kwa yeyote
atakayepuuza agizo hili
tutampiga risasi hivyo
endeleeni kukaa humu humu
ndani! Yeyote atakayekuja
hapa kwa lengo hilo la
kuwachukua watoto
atatukuta hapa tutapambana
naye” akasema Ayoub na
kuwaelekeza vijana wake
watoke nje na kufunga
mlango.Watu wawili
wakabaki mlangoni pale
wakilinda kuhakikisha
hakuna mtu anayetoka ndani
ya kile chumba wengine
wakajipanga sehemu mbali
mbali za nyumba ile
kuhakikisha hakuna
anayeingia wala kutoka.
Bella akawachukua
wanae akawakumbatia
machozi yalikuwa
yanamtoka
“Bella kwa nini
hukuniambia kama kuna
watu wametumwa na Kaiza
kuja kunikamata?akauliza
Devotha
“Nisamehe Devotha.Huu
ulikuwa ni mpango wa Kaiza
lakini niliamini tungewahi
kuondoka hapa kabla ya
watu hawa aliowatuma
hawajafika” akasema Bella
“Do you trust
me?akauliza Devotha
“I do” akajibu Bella
“Ulipaswa kunieleza
jambo hili haraka.Chukua
simu na umjulishe mume
wako nahitaji kuonana naye
aje hapa nyumbani haraka”
akasema Devotha.Bella
akachukua simu akampigia
mume wake akamjulisha kile
kilichokuwa kimetokea pale
nyumbani.
“Bella kwa nini
umefanya hivi? Kwa nini
umemuamini Devotha na
kusimama
kumtetea?akauliza Kaiza
kwa ukali
“Kaiza,Devota hana
tatizo lolote.She’s here to
save us!
“Sikiliza Bella
humfahamu Devotha.Huyo
ni mwanamke hatari sana na
sitaki kabisa akae karibu na
familia yangu!!
“Bella naomba nipe simu
nizungumze na Kaiza”
akasema Devotha na Bella
akampa simu
“Hallow Kaiza!! Akasema
Devotha
“Devotha you are a
devil.Kitu gani unakitafuta
kwa familia
yangu?Nakuhakikishia
hautatoka salama humo
ndani! akasema Kaiza
“Sikiliza Kaiza nakutaka
uje hapa nyumbani kwako
haraka sana.Ninakusubiri
hapa.Ninakuonya usijaribu
kutaka kufanya mpango
wowote wa kutuma watu
wako waje wanikamate.Niko
hapa na familia yako na
jaribio lolote la kutaka
kunikamata litaiweka
familia yako katika hatari
kubwa.Njoo haraka sana
nyumbani nataka
kuzungumza nawe” akasema
Devotha na kukata simu.
 
SIRI
MTUNZI: PATRICK CK
PART 1 SEASON 7
EPISODE 3
“Mheshimiwa rais tayari
nimefika hapa kitalu 2
nasubiri maelekezo yako”
Kaiza akamjulisha Rais
baada ya kufika kitalu 2
mahala alikoelekezwa
ampeleke Olivia
“Kuna mtu nimemtuma
hapo anakuja kumchukua
Olivia”
“Anakuja kumchukua
Olivia?Anampeleka wapi?
Mbona bado tunaendelea
kumuhoji? Kaiza akauliza
“Ninamuhitaji mimi”
akajibu Dr Evans kwa ukali
kidogo
“Vipi kuhusu baba yake?
“Agrey Themba endeleeni
kumuhifadhi pale pale
mahala nilipokuelekeza hadi
hapo nitakapowapa
maelekezo
mengine.Umenielewa Kaiza?
“Nimekuelewa mzee”
“Good.Vipi zoezi la
kuwatafuta Devotha na
Mathew Mulumbi limefikia
wapi?akauliza Dr Evans na
Kaiza akastuka akabaki
kimya
“Kaiza !! akaita Dr Evans
baada ya Kaiza kuwa kimya.
“Mheshimiwa rais kuna
muelekeo mzuri sana kuna
taarifa zenye uhakika za
mahala alipo
Devotha.Tunaendelea
kuzifanyia kazi taarifa hizo
ili kujua kama zina ukweli
wowote na kisha tutafika
mahala hapo kumchukua
Olivia.” akasema Kaiza
“Good.Nitafurahi sana
nitakapopata taarifa za
kupatikana kwa Devotha na
wenzake.Kaiza weka uzito
mkuwa sana katika suala
hilo”
“Sawa mheshimiwa Rais
usiku huu hakuna kulala
msako unaendelea hadi
tuhakikishe tunampata
Olivia” akasema Kaiza na Dr
Evans akakata simu
“Mpaka Rais kuamua
kumchukua Olivia
akazungumze naye ni wazi
amekwisha poteza kabisa
imani na sisi.Nahisi ule
usemi wake kwamba
ataifunga idara hii endapo
tutashindwa kupata taarifa
muhimu kutoka kwa Olivia
kuhusu kikundi cha kigaidi
cha IS sasa unaelekea
kutimia.Kitu pekee ambacho
kitamfanya arudishe imani
kwetu ni kwa kumpata
Devotha.Tayari ninafahamu
mahala alipo hivyo sipaswi
kuipoteza nafasi hii ambayo
ni muhimu sana
kwangu.Nataka rais
aniamini ninaweza kazi na
nitaanzia kwa Devotha”
akawaza Kaiza
Baada ya kupita dakika
kumi akawasili mtu
aliyetumwa na rais.Olivia
akatolewa ndani akiwa
amefungwa mfuko kichwani
akaingizwa katika buti la
gari lile kisha yule jamaa
akaondoka naye
“Mzee tayari
nimemchukua yule mtu”
akasema yule jamaa akiwa
garini baada ya kumchukua
Olivia
“Safi sana.Nenda mahala
nilipokuelekeza usubiri
maelekezo yangu” akasema
Dr Evans
Baada ya mjumbe yule
wa rais kuondoka,Kaiza
hakutaka kupoteza muda
akaingia katika gari lake na
kuondoka kuelekea
nyumbani kwake.
“Imekuaje Bella
akamuamini Devotha na
hata kudiriki kumtetea eti
hana tatizo na amekwenda
pale kuwakinga dhidi ya
watu wanaotaka kuiteka
familia yangu?Yule
mwanamke hapaswi
kuaminiwa kabisa ni muongo
na muuaji.Laiti Bella
angefahamu mambo
aliyoyafanya Devotha leo
asingethubutu kusimama na
kumtetea” akawaza Kaiza
“Ninamuamini sana
Bella na lazima iwepo sababu
ya yeye kuamua kuchukua
upande wa
Devotha.Yawezekana
ameamua kujiweka upande
wake ili niweze kupata
nafasi ya kumpata Devotha
bila kutumia nguvu.Sasa
nimeuelewa mchezo
alioucheza Bella.Ana akili
nyingi sana yule mwanamke
hadi akaweza kumuingia
Olivia na kumteka kiakili”
akawaza Kaiza na
kutabasamu kwa mbali
“Mwisho wa Olivia
umefika kwani hataweza
kutoka mle ndani salama na
ataeleza kila kitu.Alifanya
makosa makubwa sana
kuamua kujiunga na akina
Olivia ambao wanatumiwa
na kikundi cha IS.Namuonea
huruma sana Devotha kwa
kile kitakachomkuta lakini
ameyataka yeye mwenyewe
kwa kuchagua kushirikiana
na magaidi na mbaya Zaidi
akadiriki kuua hata watu
wetu ambao hawalali
kuhakikisha nchi inakuwa
salama.” Akaendelea kuwaza
Kaiza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom