SIRI
MTUNZI: PATRICK CK
PART 1 SEASON 5
EPISODE 2
Jengo la ghorofa sita
lililojengwa mita chache kutoka
bahari ya Hindi limekuwa
likizua maswali mengi kutoka
kwa watu wakitaka kumfahamu
mmiliki wake na wengi
wakitaka kufahamu mmiliki
wake alipataje kibali cha
kujenga jengo sehemu
ile.Mjadala kuhusiana na jengo
lile ambalo kwa muonekano
wake ni kama jengo la hoteli ya
kifahari ulimalizika kimya
kimya na ujenzi wa jengo lile
ukaendelea hadi
lilipomalizika.Kitu ambacho
kiliendelea kuzusha maswali
hata baada ya jengo lile kubwa
na zuri sana kumalizika ni
kutokuonekana shughuli yoyote
ikiendelea zaidi ya watuna
magari kuonekana wakiingia na
kutoka pamoja na uwepo wa
ulinzi mkali.Kitu ambacho
wengi hawakukifahamu kuhusu
jengo lile ni kwamba jengo lile
halikuwa jengo la hoteli au ofisi
bali jengo lile lilikuwa chini ya
idara ya siri ya usalama wa
ndani wa nchi na lilijulikana
kama kitalu 1.
Magari matatu ambayo
mojawapo alikuwemo Mathew
Mulumbi yalifunguliwa geti la
jengo lile yakaingia ndani na
kuvuka geti la pili hadi katika
jengo,lango lingine
likafunguliwa yakaingia chini
katika maegesho.Mathew
akafunguliwa pingu za miguu
akashushwa ndani ya lile gari
akaingizwa ndani ya jengo.Bado
aliendelea
kulindwa.Hawakutaka kumpa
hata nafasi ndogo.Waliingia
ndani ya lifti iliyowashusha
chini umbali wa mita mia
moja.Lango la chumba kimoja
likafunguliwa akaingizwa ndani.
Miguu yake ikafungwa na
minyororo mizito halafu
akasikia lango linafungwa watu
wale wakaondoka.Bado
aliendelea kufunikwa mfuko ule
mweusi kichwani.
“Hapa wamenileta wapi?
Akajiuliza Mathew baada ya
wale jamaa kuondoka na
kumuacha mle ndani peke yake
“Nisipofanya juhudi za
kujiokoa kutoka katika mikono
ya hawa jamaa ninaweza
kujikuta katika matatizo
makubwa.Nikipata hata nafasi
ndogo tu lazima niitumie
kikamilifu.Ili kuifahamu siri
iliyojificha nyuma ya sakata hili
lazima nihakikishe ninatoka
humu na kuwaokoa Olivia na
baba yake” akawaza Mathew
Ndani ya chumba kimoja
watu sita wakiongozwa na
Kaiza walikuwa wanamuangalia
Mathew kupitia kamera
zilizomo ndani ya chumba
alimowekwa.
“Tunatakiwa kuanza
kumtesa taratibu wakati
tunamsubiri Devotha.Tuanze na
baridi” akasema Kaiza
aliyekuwa amevaa suti ya rangi
ya kijivu.
Mabomba ya maji
yaliyokuwamo ndani ya
chumba alimowekwa Mathew
yakafunguka na kuanza
kumwaga maji ya baridi
sana.Mathew aliloa chapa chapa
na kuanza kutetemeka kwa
baridi kali.Baada ya dakika
kadhaa maji yale yakaacha
kutoka na ikatokea baridi kali
sana.Mathew alihisi viungo
vyake vyote vinaganda.
“Imetosha tumpe muda wa
mapumziko” akasema Kaiza na
mashine ile yenye kupeleka
ubaridi ndani ya kile chumba
ikazimwa lakini bado Mathew
aliendelea kutetemeka kwa
baridi kali.
“Atolewe mle apelekwe
chumba cheupe” akasema
Kaiza.Baada ya muda mfupi
lango la chumba kile alimo
Mathew likafunguliwa
wakaingia watu sita watatu kati
yao wakiwa na silaha.Mathew
akatolewa ndani ya kile chumba
akavuliwa ule mfuko mweusi
kichwani akavuliwa mavazi
yake akavishwa mavazi meupe
akatolewa ndani ya kile chumba
akapelekwa katika chumba
chenye weupe mkali.Kila kitu
kilichokuwamo mle ni
cheupe.Akafungwa mikono
katika meza wakamuacha mle
ndani peke yake
“Ninahisi baridi kali
mno.Sijawahi kuhisi baridi ya
namna hii toka kuzaliwa
kwangu.Najua hizi ni mbinu zao
za kunitesa lakini
hawatafanikiwa.Nimepitiam
ateso mengi zaidi ya
haya,wanajisumbua bure”
akawaza Mathew
*****************
Jua lilipochomoza lilimkuta
tayari Devotha Adolph
amekwisha wasili kitalu 2
mahala alikohifadhiwa Olivia na
baba yake Agrey.Bado
wataalamu wa mawasiliano wa
idara yake waliendelea na zoezi
la kuhakikisha mtandao mpya
wa mawasiliano
unakamilika.Devotha
akawasalimu na kuelezwa kile
kilichokuwa kinaendelea
akaelekea ofisini kwake.Mara tu
alipoketi kitini akampigia simu
Kaiza
“Hallo Devotha” akasema
Kaiza baada ya kupokea simu
“Kaiza mnaendeleaje huko?
“Huku tunaendelea vyema
kabisa.Tayari tumeanza kumpa
Mathew mateso
taratibu.Tumeanza na baridi
kali,tayari tumemtoa kwenye
baridi na kumpeleka katika
chumba cheupe.”akajibu Kaiza
“Good.Mmefanya kazi nzuri
sana Kaiza.Huyo ni mtu wa
muhimu sana kwetu”
“Unakuja saa ngapi huku
Devotha?akauliza Kaiza
“Niko hapa kitalu 2 nataka
kuendelea na zoezi la
kumfungua Olivia na vile vile
nitazungumza na baba yake
kama kuna kitu chochote
anakifahamu kuhusu
mwanae.Endeleeni kumpa
mateso Mathew na nikitoka
huku nitakuja huko mara
moja.Kwa sasa hatuna tena
hofu,aliyekuwa anatupa hofu ni
huyo Mathew ambaye tayari
tunaye mikononi mwetu”
akasema Devotha
“Sawa Devotha
tunakusubiri” akasema Kaiza na
Devotha akakata simu
“Leo ninajihisi mwenye
amani sana baada ya Mathew
kukamatwa.Nitaifanya kazi
yangu kwa Amani.Nataka
kubadili namna ya kumuhoji
Olivia.Kutumia nguvu
hakutasaidia kumfungua”
akawaza Devotha akachukua
simu akapiga na kuomba
kuunganishwa na chumba cha
Olivia.Baada ya sekunde chache
akaunganishwa na kamera
zilizopo katika chumba
alimolala Olivia.
Olivia alikuwa amelala
katika chumba kizuri na kitanda
safi.Hakuwa amefungwa pingu
mikononi wala
miguuni.Alionekana mwingi wa
mawaz😵livia akampigia simu
Jasmin na kumtaka afike oisini
kwake haraka
“Jasmin leo tunabadili
mbinu za kumuhoji
Olivia.Hatutaendelea na
taratibu zetu za kutumia
mabavu hivyo nataka
tumuonyeshe kwa sisi si watu
wabaya.Nataka tumfanye
aamue mwenyewe kwa hiyari
yake kufunguka na kushirikiana
nasi.Nataka uende chumbani
alimo mpelekee mavazi
mazuri,hakikisha ameoga na
kisha andaa kifungua kinywa
kwa ajili yangu naye” akasema
Devotha na Jasimn akaenda
kutekeleza maagizo
aliyopewa.Olivia alipelekwa
bafuni kuoga,akatibiwa jeraha
alilochomwa kisu pajani,kisha
akapewa mavazi mazuri ya
kuvaa.Wakati yote haya
yanafanyika Devotha alikuwa
akishuhudia kupitia kamera na
kila kitu kilipokamilika
akaelekea katika chumba cha
chakula ambako kuliandaliwa
kifungua kinywa maalum kwa
ajili yake na Olivia.Akampigia
simu Jasmin na kumtaka
ampeleke Olivia katika chumba
cha chakula.Olivia alistuka na
kupandwa na hasira baada ya
kumkuta Devotha akiwa
amekaa katika chumba kile cha
chakula akitabasamu
“Hallo Olivia” akasema
Devotha.Olivia akasimama na
kumtazama Devotha kwa
hasira.Devotha akasimama na
kuvuta kiti
“Karibu Olivia.Karibu
tupate kifungua kinywa”
akasema Devotha
“I’m not hungry!! Akasema
Olivia na kumgeukia Jasmin
“Take me back to my room”
“Olivia come and join me
here, this is an order!! Akasema
Devotha kwa ukali.Mmoja wa
walinzi waliokuwa nyuma ya
Olivia akamshika mkono na
kumkalisha kitini
“Please madam usifanye
mambo yakawa magumu
kwako.Fanya
utakavyoelekezwa” akasema
yule mlinzi na Olivia akaketi
huku akiendelea kumtazama
Devotha kwa macho yaliyojaa
hasira.Dr Olivia na Devotha
wakanywa chai kimya kimya na
baada ya kumaliza Devotha
akasema
“Olivia let’s take a walk”
Olivia akainuka na
kuongozana na Devotha
wakaenda katika bustani ndogo
kulikokuwa na sehemu nzuri ya
kukaa kupumzika.UKimya wa
dakika mbili ukapita kisha
Devotha akasema
“Unaendeleaje
Olivia?akauliza Devotha lakini
Olivia hakumjibu kitu.
“Olivia I’m sorry for what I
did to you yesterday” akasema
Devotha na Olivia akaonekana
kupandisha hasira zaidi
“You are sorry?akauliza
“With my own two eyes I
watched you shot my father
twice .What kind of a woman
are you?akauliza Olivia kwa
ukali
Devotha akamtazama kwa
muda halafu akasimama
“Niangalie vyema” akasema
“I’m a very sexy
woman.Najifahamu mimi ni
mzuri kukushinda hata wewe
lakini umejiuliza kwa nini
mwanamke mwenye uzuri
kama wangu nikawa
mkatili?Ulichokishuhudia jana
si kitu.Bado haujauona ukatili
wangu.Nilikwambia kwamba
wananiita shetani wa
kike.Unadhani ni kwa nini
nimefikia hapo
nilipofika?akauliza Devotha
lakini Olivia hakujibu kitu.
“Uso wangu umejaa
tabasamu kila wakati lakini si
tabasamu la furaha.Do you
think when I smile I’m
happy?akauliza na kuendelea
kumtazama Olivia ambaye bado
alikuwa kimya
“I’m not happy.I’ve never
been happy in my life.Tabasamu
hili ni uumbaji wa Mungu lakini
ndani mwangu hakuna furaha
hata chembe.Ninapata kila
ninachokihitaji katika maisha
yangu,I have
money,jewels,expensive
cars,houses, but I’m not
happy.Umejiuliza kwa nini?
Akauliza Devotha na kuvuta
pumzi ndefu.Akatoa miwani
aliyoivaa na kuiweka mezani
“Nitazame vizuri macho
yangu” akasema Devotha lakini
Olivia hakusumbuka kuinua
kichwa chake kumtazama
“Olivia nitazame machoni
tafadhali!! Akasema Devotha na
Olivia akainua kichwa
akamtazama Devotha
“Kuna kitu umekigundua?
akauliza Devotha lakini Olivia
akabaki kimya
“Umegundua kitu chochote
kisicho cha kawaida?akauliza
lakini Olivia akaendelea kuwa
kimya
“Kama umeshindwa
kugundua nitakueleza” akasema
Devotha
“Nina jicho moja linalofanya
kazi.Jicho la kushoto ni bandia
na halina kazi
yoyote.Ukinitazama ni vigumu
kuamini kwamba ni natumia
jicho moja” akasema Devotha
na kuvaa miwani yake
“Umewahi kujiuliza kwa
nini kila unaponiona ninakuwa
na glovu mkono wangu wa
kushoto? Unadhani ni urembo?
akauliza Devotha na kuvua
glovu yake aliyovaa mkono wa
kushoto
“Unaona mkono wangu
ulivyo?akauliza.Mkono wa
kushoto wa Devotha ulikuwa na
vidole vitatu pekee.
“Nina vidole vitatu katika
mkono wangu wa
kushoto.Ninavaa hii glovu
ambayo imetengenezwa
maalum ili nionekane nina
vidole timilifu lakini sina vidole
viwili” akasema Devotha na
kuvaa glovu yake halafu
akafungua mkoba na kutoa
albamu la picha akampa Olivia
aangalie
“Tazama hizo ni picha
zangu za zamani” akasema
Devotha.
“Picha zako zitanisaidia
nini? akauliza Olivia
“Fungua tazama” akasema
Devotha na Olivia akafungua
ukurasa wa kwanza wa albamu
lile akazitazama picha mbili
kubwa na sura yake ikaonyesha
mshangao kidogo akaendelea
kufunua kurasa kwa kurasa na
alipomaliza akalifunga lile
albamu
“This is stupid!! Akasema
Olivia na kuiweka mezani ile
albamu
“Umegundua nini
Olivia?akauliza Devotha
“Stop wasting my time
Devotha.Unanipima akili
yangu?akauliza Olivia
“Nieleze umeona nini katika
hizo picha?Devotha
akauliza.Olivia akamtazama
kwa muda halafu akasema
“Nimemuona msichana
ambaye hafanani kabisa na
wewe.Naomba usitake kucheza
na akili yangu Devotha”
akasema Olivia
“Huyo unayemuona katika
hizo picha ni mimi”akasema
Devotha
“Nimekwambia usitake
kuijaribu akili yangu
Devotha.Aliyeko katika picha
hizi na wewe ni watu wawili
tofauti kabisa”akasema Olivia
“Uko sahihi Olivia.Kwa
kutazama picha za kwenye
albamu na kunitazama mimi ni
watu wawili tofauti kabisa
lakini ni mtu mmoja ambaye ni
mimi” akasema Devotha na
kunyamaza kimya kwa sekunde
kadhaa halafu akasema
“Olivia umejiuliza kwa nini
nimekueleza haya yote?akauliza
Devotha.Olivia hakujibu kitu
alikuwa anachezea vidole vyake
“Nisikilize vyema” akasema
Devotha
“Picha hizo ulizoziona ni
wakati nikiwa msichana
mdogo.Wazazi wangu walikuwa
masikini.Hatukuwa na
nyumba,tuliishi katika nyumba
za kupanga.Katika harakati za
kutafuta maisha baba alijikuta
akifika hadi nchini Kenya na
kupata kazi katika shamba
moja kubwa la uzalishaji
maua.Ililazimu familia yetu
kuhamia Kenya kumfuata
baba.Katika sehemu tuliyokuwa
tukiishi nchini Kenya nilipata
rafiki aliyeitwa Halima.Huyu
alikuwa msomali.Wazazi wake
walihama kutoka Somalia na
kuishi Kenya.Familia yao na
yetu tulikuwa na ukaribu
mkubwa.Siku moja wakati
tukitoka shule Halima
aliniambia kwamba baba yake
anamtengenezea chombo
ambacho kitampeleka
peponi.Nilikuwa mdogo bado
lakini katika mafundisho
niliyopewa na walimu wa dini
nilifahamu wanaokwenda
peponi pekee ni wale
waliokufa.Nilimtaka
akanionyeshe chombo hicho
ambacho kitampeleka
peponi.Kabla wazazi wake
hawajarejea kutoka katika
mihangaiko yao ya siku Halima
akanipeleka katika chumba
ambacho baba yake alikuwa
anamtengenezea chombo cha
kumpeleka peponi.Alinionyesha
chombo chenyewe kilichokuwa
juu ya meza.Lilikuwa ni bomu
likitengenezwa la kujitoa
mhanga.Toka nikiwa mdogo
nilipenda sana kutazama filamu
mbalimbali hasa za mapambano
na magaidi na niligundua lile
lilikuwa bomu ,niliogopa sana
nikamdanganya kwamba
ninakwenda kuwaita wazazi
wangu ili waje waone kifaa kile
na mimi wanitengenezee
chombo kama kile cha
kunipeleka peponi ili
ikiwezekana tuende pamoja
mimi na yeye.Nilikimbia
nyumbani nikawachukua
wazazi wangu tukaenda hadi
katika chumba kile cha baba
yake Halima na tukamkuta
tayari Halima amekwisha livaa
lile bomu na akasema anataka
kuwaonyesha wazazi wangu
namna kifaa kile kinavyofanya
kazi.Baba alimsihialivue lakini
Halima akagoma,baba
akamfuata ili amvue lile bomu
lakini alichelewa Halima
alibonyeza kilipuzi na moto
mkubwa ukatokea”
akanyamaza Devotha na
kuinamisha kichwa kwa muda
“I’m sorry sipendi
kulikumbuka tukio lile ni moja
ya tukio linaloniumiza mno
katika maisha yangu.Picha ya
moto ule mkubwa haijawahi
kunitoka katika akili yangu”
akanyamaza tena
“Pole sana” akasema Olivia
akionekana kuguswa na taarifa
ile ya Devotha
“Wazazi wa Halima
walikuwa ni wafuasi wa kikundi
cha Alshabaab cha Somalia na
walikuwa wanajiandaa kufanya
shambulio kwa kumtumia
Halima.Wazazi wangu wote
wawili walipoteza maisha pale
pale.Halima naye alifariki akiwa
angali msichana mdogo.Mimi
sikuwa natazamika,niliharibika
vibaya sana.Serikali ya
Marekani waliamua kunichukua
na kugharamia matibabu
yangu.Nilipelekwa Marekani
kwa matibabu ambako
nilifanyiwa operesheni
thelathini na saba hadi kufikia
hali hii niliyonayo leo ndiyo
maana unaona muonekano
wangu wa sasa na ule wa
kwenye picha ni tofauti.Baada
ya kupona niliendelea na
masomo nchini Marekani na
baadae nikasomea masuala ya
kupambana na
ugaidi.Nilisomeshwa na
kufanya kazi katika idara ya
kupambana na ugaidi ya
Marekani.Nikiwa kule
niliendelea kufuatilia taarifa za
nyumbani Tanzania na nilisikia
kuhusu kuanza kuchomoza kwa
vikundi vyenya viashiria ya
ugaidi nchini
Tanzania.Niliwasiliana na Rais
nikampa wazo la kuanzisha
idara ya siri ya usalama wa
ndani wa nchi.Rais Dr Evans
alikubali wazo langu nikarejea
nchini kuanzisha idara hii na
japo imeanzishwa ndani ya
muda mfupi lakini tayari kazi
tuliyoifanya ni
kubwa.Tumefanikiwa
kufyekelea mbali vile vikundi
vyote vyenye muelekeo wa
kigaidi vilivyoanza kuchomoza
na hadi sasa hujasikia tena
tishio lolote la kuibuka kwa
vikundi vya kigaidi.”akatulia
tena na kumtazama Olivia
“Olivia nimekueleza haya
yote kwa sababu nataka
utambue ni namna gani
ninawachukia magaidi.Ni kwa
sababu yao leo hii maisha yangu
hayako sawa.Maisha yangu
hayana furaha hata chembe.Ni
kwa sababu ya magaidi leo hii
niko peke yangu katika hii
dunia sina baba ,mama wala
ndugu yeyote I’m all
alone.Nimeshuhudia unyama
unaofanywa na magaidi toka
nikiwa mdogo.Asubuhi ya
Jumanne ya 11 September 2011
nilikuwepo jijini New York
wakati kikundi cha kigaidi cha
Alqaeda kiliposhambulia
majengo pacha ya kituo cha
kibiashara cha kimataifa na
kusababisha watu wapatao elfu
tatu kupoteza maisha na maelfu
wengine
kujeruhiwa.Yawezekana
unafahamu kupitia mitandao na
vyombo vingine vya habari
lakini mimi nilikuwepo eneo la
tukio na nilishuhudia unyama
ule kwa macho yangu.Ukiacha
tukio hilo nimeshuhudia
matukio mengine mbali mbali
ya kigaidi yanayofanywa na
vikundi mbali mbali vya kigaidi
duniani hivyo sina huruma hata
kidogo na watu hawa” akasema
Olivia
“Baada ya jitihada za muda
mrefu hatimaye serikali ya
Marekani walifanikiwa kumuua
kiongozi mkuu wa kikundi cha
Alqaeda ambacho kilikuwa
kinaongoza mashambilizi ya
kigaidi na kuua watu wengi
duniani.Kuuawa kwa kiongozi
huyo na wengine kadhaaa
kulilifanya kundi la Alqaeda
likose nguvu na kufifia lakini
kwa sasa limeibuka kundi la IS
ambalo limekuwa likifanya
mashambulio mengi sehemu
mbali mbali duniani na kuua
watu wengi wasio na hatia na
wameapa kuendelea kufanya
mashambulio na kuua watu
hadi pale bendera yao
itakapopepea kutoka mashariki
hadi magharibi mwa
dunia.Nilipogundua kuwa una
mawasiliano na watu walio
katika mtandao wa IS nilistuka
sana na kupata hasira
nyingi.Nilijuliza maswali mengi
kuhusu ukaribu wako na hawa
watu.Kama nilivyokueleza awali
kwamba ninawachukia magaidi
na wewe pia uliingia katika
orodha ya maadui zangu lakini
nikikutazama machoni Olivia
hauonekani kama ni
gaidi.Hauna sifa za kuwa
gaidi.Nataka kufahamu kitu gani
kinaendelea kati yako na hawa
watu wa IS? Olivia wewe u
mwanamke mwenye heshima
kubwa hapa Tanzania kutokana
na shughuli yako unayofanya ya
kuokoa maisha ya watu na hata
kesho ukitaka kugombea urais
watanzania hawatakuwa na
sababu ya kutokukuchagua
kutokana na sifa yako
iliyotukuka.Familia yako pia ina
sifa nzuri lakini haya yote
yanaharibiwa na jambo moja tu
nalo ni ushirika wako na watu
wa kikundi cha kigaid cha
IS.Olivia nataka kuwa rafiki
yako badala ya adui.Nataka
nikusaidie sipendi kukutesa
mtu kama wewe lakini
nitakusaidia pale tu
utakapokuwa tayari kunieleza
ukweli wote kuhusu wewe na
IS.Sipendi kuendelea
kukushikilia hapa
kukutesa,kumtesa baba yako
nataka tulimalize suala hili kwa
amani ili maisha yaendelee”
akasema Devotha na kutulia
akaangalia juu kundi la ndege
lilikuwa linapita.Ulipita ukimya
wa dakika mbili
“Olivia please” akasema
Devotha
“Devotha umejitahidi sana
kunishawishi nikueleze kila kitu
lakini kabla sijakueleza
chochote kuna kitu nakihitaji
kujua kutoka kwako” akasema
Olivia
“Sema Olivia unahitaji
nini?Ninakuahidi chochote
ukitakacho kama kiko ndani ya
uwezo wangu nitakupatia”
akasema Devotha.Olivia
akamtazama na kusema
“Nataka kujua mahala aliko
Edger Kaka.Ukinipa taarifa hizo
na ukanisaidia kumpata
ninakuahidi kukueleza kila kitu
unachokitaka” akasema
Olivia.Devotha akavuta pumzi
ndefu na kusema
“Olivia my dear,Edger Kaka
hayuko hai.Amekwisha fariki
miaka mitatu iliyopita na
kilichobaki hivi sasa ni mifupa
yake tu.Labda kama unataka
nikupeleke mahala lilipo kaburi
lake” akasema Devotha
“Devotha ninayasoma
mawazo yako,kila
ninapowaeleza kuhusu suala
hili unaamini nina matatizo ya
akili.Naomba nikutoe wasiwasi
kwamba mimi ni mzima sina
tatizo lolote la
kiakili.Ninachokisema nina
uhakika nacho” akasema Olivia
“Olivia kila atakayesikia
suala hili ataamini una matatizo
ya akili kwa sababu Edger
amekwisha fariki na wewe
mwenyewe ndiye uliyetambua
mwili wake hospitali”akasema
Devotha
“Wote tuliaminishwa hivyo
kwamba Edger amekufa lakini
naomba ufahamu Devotha
kwamba mwili ule uliozikwa
haukuwa mwili wa Edger Kaka”
“That’s not true Olivia”
akasema Devotha
“It’s true and I have proof”
“What proof?
“Nimefanya vipimo kwa
kutumia masalia ya mwili ule
ambao wote tunaamini ni wa
Edger na majibu
yamenionyesha kwamba mwili
ule haukuwa wa Edger”
“That’s a lie Olivia.That’s
not true.Edger Kaka is dead”
akasema Devotha
“Sikudanganyi Devotha
ninachokwambia ni ukweli
mtupu.Wote tumeaminishwa
hivyo kwamba Edger alifariki
katika ile ajali lakini ukweli ni
kwamba Edger yuko hai
anashikiliwa sehemu Fulani”
akasema Dr Olivia
“Olivia do you think I can
believe you?akauliza Devotha
“Believe me or not but
that’s the truth Edger is still
alive.Kama unataka nikueleze
yote unayohitaji kuyajua
kuhusu IS nipe taarifa za alipo
Edger” akasema Olivia na
Devotha akaendelea
kumuangalia
“Najua huniamini Devotha
lakini nitakupa maelekezo
ambayo ukiyafuatilia utagundua
hiki ninachokueleza ni kitu cha
kweli.Katika kaburi la Edger
upande wa kulia ukichunguza
vizuri utagundua
kumechimbwa na ukifukua
eneo hilo utakuta kuna tobo
kubwa lililotobolewa katika
ukuta wa kaburi.Mimi ndiye
niliyetoboa tobo hilo kwa ajili
ya kuingia ndani na kuchukua
sampuli za mabaki ya mwili ule
nikaenda kufanya vipimo na
kugundua mwili ule haukuwa
wa Edger Kaka.Kama ukitaka
unaweza ukachukua sampuli za
mwili ule pia na kwenda
kuufanyia uchunguzi na
ninakuhakikishia majibu
utakayoyapata ni kama haya
ninayokwambia kwamba mwili
ule haukuwa wa Edger
Kaka.Devotha kuna siri kubwa
hapa ambayo huifahamu na
kama ukitaka kuifahamu
nisaidie kujua mahala alipo
Edger Kaka.Nakuhakikishia ni
siri kubwa” akasema Olivia
Baada yatafakari ya muda
Devotha akasema
“Olivia natamani sana
nikuamini lakini nafsi yangu
inasita kabisa”
“C’mon Devotha.Unadhani
ningeibuka tu na kudai Edger
yuko hai kama sina uhakika?
Ninao uhakika mkubwa
kwamba yuko hai ndiyo maana
mtoto wa Rais amechomwa
sindano yenye virusi ili
kumshinikiza Rais aweze
kunipa maelezo ya mahala alipo
Edger.Sijakurupuka Devotha”
akasema Olivia
“Kwa nini umemlenga Rais
moja kwa moja katika suala
hili?Kwa nini unataka
kumchafua rais kwa jambo hili
ambalo halina ukweli
wowote?akauliza Devotha
“Rais ninamuita
baba.Amekuwa ni rafiki
mkubwa wa baba yangu toka
wakiwa wadogo lakini jiulize
kwa nini nikatengeneza virusi
ambavyo vinaweza kumuua
mtoto wake Coletha ambaye
ananiita dada?Nimefanya hivi
kwa kuwa ninafahamu rais
anazo taarifa za jambo hili na
nimefanya hivi ili kumshinikiza
anipe taarifa hizo” akasema
Olivia
“Olivia naomba tuachane na
hilo la Edger.Nataka
tuzungumze masuala
mengine.Nataka unieleze
kuhusu mahusiano yako na
IS.Umeonekana ukiwa na Seif
Almuhsin na vile vile umekuwa
na mawasiliano na Sayid
Omar.Nataka kuf…………..”
“Hakuna haja ya kwenda
mbali Devotha.Sintaweza
kukueleza chochote.Kama
nilivyokueleza kuwa
nitazungumza nawe pale
ambapo utanipa taarifa za
mahala alipo Edger Kaka.Kama
hakuna taarifa hizo hakuna
nitakachoweza
kukwambia.Mmekosea sana
kumteka hata baba yangu ili
kunilazimisha niongee lakini
nawahakikishia hata kama
mtatishia kuua familia yangu
nzima mbele yangu
sintafumbua mdomo wangu
kutamka chochote.Muacheni
baba aende zake muendelee
kunishikilia mimi” akasema
Olivia
“One more thing.Fikisha
salamu zangu kwa Rais kwamba
muda unakwenda na asipofanya
juhudi atampoteza
mwanae.Mimi ndiye
niliyetengeneza virusi hivyo
alivyoambukizwa mwanae na
ndiye mwenye uwezo wa
kumtibu.Asisumbuke kutafuta
tiba hospitali kwani atampoteza
mwanae.Anachotakiwa kufanya
ni kunionyesha mahala alipo
Edger na mimi nitamponya
mwanae.Devotha nadhani
hatuna cha kuzungumza zaidi
hapa nirejeshe chumbani
nataka kupumzika mguu
unaniuma” akasema
Olivia.Devotha akawapa ishara
walinzi watatu waliokuwa
karibu akawataka wampeleke
Olivia chumbani wakamfungie
“Natamani sana kumpuuza
Olivia na kuamini ana matatizo
ya akili lakini kuna kitu
kinanilazimisha intake
kumuamini.Japo tunajaribu
kuamini kwamba ana matatizo
ya akili lakini Olivi ani mzima
hana tatizo lolote.Alizungumza
kwanza na Rais akamueleza
jambo hilo la
Edger,nilipozungumza naye
akaendelea kusisitiza kuwa
Edger yuko hai na leo tena
ameendelea kusisitiza na
amekwenda mbali zaidi akadai
anao ushahidi wa kuthibitisha
hicho anachokisema.Nadhani
Olivia hajakurupuka katika
suala hili.Ninachojiuliza kwa
nini amlenge moja kwa moja
Rais Dr Evans? Kuna kitu
anakifahamu kuhusu jambo
hili?akajiuliza Devotha
“Maneno aliyoyatamka
Olivia yamenishawishi
kulitazama suala hili.Ngoja
nitumie muda mfupi kulitazama
suala hili.Nitaanza kwanza
katika makaburi ya Midizini
alikozikwa Edger.Nataka
nikalichunguze hilo kaburi
kama kweli limechimbwa”
akawaza Devotha na kuelekea
katika gari lake akaondoka.Moja
kwa moja alielekea katika
makaburi ya midizini
alikozikwa Edger
Kaka.Alilitafuta kaburi la Edger
akalipata na kuangalia upande
wa kulia mwa kaburi lile kama
alivyoelekezwa na Olivia ni
kweli kulionekana kama
kumetitia kidogo.Akapiga picha
za kutosha halafu akaondoka
“Olivia anaweza kuwa
sahihi.Alisema upande wa kulia
mwa kaburi la Edger
kumechimbwa na hata
ukitazama panaonekana kweli
pamechimbwa japo si hivi
karibuni.Nashawishika kutaka
kulifanyia suala hili uchunguzi
wa kina.Yawezekasna lina
ukweli ndani yake” akawaza
Devotha akiwa garini
“Devotha kuna siri kubwa
hapa ambayo huifahamu na
kama ukitaka kuifahamu
nisaidie kujua mahala alipo
Edger Kaka.Nakuhakikishia ni
siri kubwa” akayakumbuka
maneno ya Olivia
“Msisitizo huu wa Olivia si
wa bure.Hata mimi kuna kitu
nimeanza kukiona katika
maelezo yake.Michezo kama hii
ya kutengeneza vifo ipo na
inafanyika sana katika nchi za
wenzetu zilizoendelea.Kama
suala hili ni la kweli kwa nini
watengeneze kifo cha Edger?Na
kama ni kweli nani waliofanya
jambo hilo? Devotha
akaendelea kujiuliza maswali
“Najiuliza swali lingine
suala hili la Edger lina maslahi
gani kwa Olivia?Kwa nini
alifuatilie namna hii? Je katika
suala hili yuko peke yake au
kuna watu wako nyuma yake?
Kama wapo ni akina nani?
Kweli hapa kuna siri kubwa
kama alivyosema Olivia.Nitajipa
zoezi la kuchunguza ili niupate
ukweli wa jambo hili hata hivyo
bado nitalazimika kumuhoji
zaidi Olivia kuna mengi
ninaweza kuyapata kwake zaidi
ya hili suala la mahusiano yake
na IS.Natakiwa kujenga naye
urafiki badala ya kuwa adui
yake.Hili halitamfurahisha Dr
Evans lakini nitatafuta namna
ya kufanya ili lisiweze kuleta
mgongano.Dr Evans anataka
majibu ya haraka kutoka kwa
Olivia lakini ukimuangalia
Olivia ana mambo mengi
ambayo ili kuyapata hatupaswi
kufanya haraka wala kutumia
nguvu” akawaza Devotha