Riwaya: Siri

Riwaya: Siri

SIRI
MTUNZI: PATRICK CK
PART 1 SEASON 6
EPISODE 5
Kaiza alikaa katika
iliyokuwa ofisi ya Devotha
akakiegemeza kichwa
kitini.Alizama katika lindi la
mawazo akiitazama picha ya
Devotha iliyokuwa mezani
akitabasamu
“Devotha ndiye
aliyeniingiza katika idara
hii.Siku zote nimekuwa
nikimuheshimu kama dada
yangu na siamini kama
tumefikia hapa.Kwa nini lakini
akafanya maamuzi haya
ambayo nayaita ya kijinga
kujiunga na watu
wanaoshirikiana na
magaidi?Kwa nini amechagua
kuwa adui yetu? Rais ametoa
ruhusa ya kumpiga risasi
kokote
atakapoonekana,inaniumiza
kwa amri hii lakini yote haya
ameyataka yeye
mwenyewe.Kitendo cha kuua
watu ambao amekuwa akiishi
na kufanya nao kazi kama
ndugu kimeniumiza sana na
kuna wakati inaniwia ugumu
kuamini kama kweli aliyefanya
unyama huu ni Devotha huyu
ninayemfahamu mimi ambaye
amekuwa ni kama dada
yangu.Amenisaidia katika
mengi lakini sintaweza
kumsaidia katika hili
alilolifanya.Rais amekwisha toa
maelekezo lazima yafuatwe.”
akawaza Kaiza na kuifunika
picha ile ya Devotha
“Lakini amri hii ya rais ni
kubwa mno.Naamini ametoa
amri hii kwa hasira.Tulipaswa
kumkamata Devotha akahojiwa
na kufahamu sababu
iliyompekekea akafanya hivi
alivyofanya.Hata hivyo
hatuwezi kumpinga,maagizo
yke ni amri kwetu na lazima
yatekelezwe.Kikubwa
ninachopaswa kuumiza kichwa
kwa sasa ni namna ya
kumpata.Devotha anaifahamu
idara hii kama nyuma ya
kiganja chake cha mkono na
anafahamu mbinu zetu zote
hivyo kumpata inaweza kuwa
ngumu sana kwetu
lakini…”Kaiza akatabasamu kwa
mbali baada ya kukumbuka kitu
“Asubuhi baada ya
kumuhoji Mathew
Mulumbi,Devotha aliondoka
hapa bila kuaga anakwenda
wapi na ninakumbuka
aliondoka akiwa na Saada.Sasa
nimepata picha.Yawezekana
alimtumia Saada katika
kudukua simu ya rais kwani
Saada ni mmoja wa wadukuzi
tunaowategemea hapa katika
idara yetu.Nina uhakika
mkubwa tukimpata Saada
tutakuwa tumempata pia
Devotha au tutafahamu mahala
alipo Devotha.Kwa nini sikuwa
na wazo hili toka
mapema?Tusingesumbuka
namna hii na pengine mida hii
tungekwisha mpata Devotha”
akawaza Kaiza akainua simu na
kupiga akauliza kama Saada
alikuwepo wakati Devotha
aliovamia akajibiwa hakuwepo.
“Tayari nimepata jibu.Saada
anatumiwa na Devotha.Ipo
namna rahisi ya kumpata
Saada.Kuna kifaa kidogo sana
huwa tunawawekea mwilini
watu wote wa idara yetu bila
wao kuna na tunaofahamu siri
hii ni mimi na Devotha
pekee.Kila mtu anayejiunga
huchomwa sindano ya usingizi
na huwekewa kifaa Fulani
kidogo mithili ya punje ya
mchele ambacho hutuwezesha
sisi kufahamu mahala alipo kwa
siri bila wao kuwa na
taarifa.Sijui kwa nini sikuwa na
wazo kama hili toka mapema”
akawaza Kaiza na kuufunga
kabisa mlango wa ofisi ile
halafu akaingiza namba za siri
katika kompyuta yake na
kuanza kutafuta kitu Fulani na
baada ya muda akakipata
alichokuwa anakitafuta
“Sasa amepatikana.Tayari
nimekwisha ona mahala alipo”
akawaza Kaiza na kutoka
akaelekea control room.Hali ya
simanzi kubwa ilikuwa
imetanda.Watu walikuwa
wameketi vitini wengine
wakilia
“Naombeni tusikilizane
jamani” akasema Kaiza na kila
mmoja akakaa sawa kumsikiliza
“Poleni sana kwa kile
kilichotokea.Tumeumizwa mno
kwa wenzetu tuliowapenda
kuuawa.Kibaya na
kinachoumiza Zaidi ni kwamba
aliyefanya jambo hili ni
mwenzetu,ndugu yetu ambaye
kwa muda wote amekuwa
akituongoza lakini leo
amebadilika na kufanya hivi
alivyofanya.Hili halivumiliki na
lazima tuhakikishe wale wote
waliofanya hivi wanapatikana
wakiwa hai au wamekufa!
Akasema Kaiza na kunyamaza
akawatazama watu wale
waliokuwa wameyaelekeza
macho yao kwake kisha
akaendelea.
“Nimekuwa ofisini
nikijaribu kutafakari kama
aliyefanya jambo hili ni Devotha
huyu ninayemfahamu mimi au
ni mwingine anayefanana naye
lakini jibu ni jepesi kwamba ni
Devotha huyu huyu ambaye
amekuwa kiongozi wetu ndiye
aliyebadilika na kufanya haya
yaliyotokea.Nimemjulisha rais
kilichotokea naye pia
amestushwa mno na hiki
alichokifanya Devotha ambaye
alimuamini sana.Kwa hiyo basi
Rais ameelekeza kwamba
Devotha ni mtu hatari sana
ambaye amekuwa adui yetu na
adui yetu ni adui wa Tanzania
hivyo basi kokote
atakapoonekana anatakiwa
kuuawa.Si yeye peke yake bali
na wale wote anaoshirkiana nao
akiwemo Mathew Mulumbi
ambaye yeye na Olivia
wanashirikiana na kikundi cha
IS.Mkumbuke watu hawa wana
mafunzo makubwa hivyo
yawezekana kuwakamata
ingawa ngumu kwetu ndiyo
maana rais ametoa maelekezo
hayo kwamba kokote
wakatakoonekana wapigwe
risasi na kufa.Nafahamu wengi
hapa mtashangaa kwa amri hii
ya rais kwa sababu tumekuwa
na Devotha na tunampenda
lakini kwa hili alilolifanya
hatuna namna Zaidi ya
kutekeleza amri ya
rais.Anastahili adhabu ya kifo
kama alivyoua wenzetu”
akasema Kaiza na kunyamaza
akawatazama wale watu mle
ndani ambao nyuso zao zilijaa
simanzi kubwa.
“Asubuhi ya leo Devotha
alipoondoka hapa alikuwa
ameongozana na Saada ambaye
wote tunamfahamu uwezo
wake mkubwa katika
udukuzi.Devotha alimchukua
Saada ili akamsaidie kazi zake
za udukuzi na nina uhakika
mkubwa kwamba ni yeye
aliyemsaidia Devotha kuingia
hapa ndani na haya yote
yakatokea.Ili kumpata Devotha
tunatakiwa kumpata
Saada.Ninaamini aidha wako
pamoja au anafahamu mahala
alipo.Kuanzia sasa Saada naye
anaingia katika orodha ya wale
tunaowatafuta.Ninawahakikishi
a kwamba tukimpata Saada
tutakuwa tumempata
Devota.Ninafahamu mahala
tunakoweza kumpata Saada
hivyo nitaongozana na timu ya
watu tutakwenda huko
kumchukua na akipatikana
atatupa ukweli wote mahala
alipo Devotha.Wakati sisi
tunakwenda kumtafuta Saada
wengine mtaendelea na kazi
kama kawaida.Hiki ni kipindi
kigumu sana kwetu hivyo
lazima na sisi tusimame imara
kuhakikisha kwamba tunaibuka
washindi.Siku zote kushindwa
kwetu ni mwiko.Lazima
tuhakikishe tunashinda na
kuwatia mikononi Devotha na
mtandao wake wote.Rais
anatutegemea sana
sisi,Tanzania inatutegemea pia
hivyo basi lazima tuhakikishe
tunakiondoa kitisho cha
usalama kinachoikabili nchi
yetu kwa sasa kutoka kwa IS”
akasema Kaiza na kuchagua
watu wanne akawataka
waongozane kwenda kumtafuta
Saada.Hakumueleza mtu yeyote
wapi wanaelekea au
amefahamuje mahala alipo
Saada.Safari ilikuwa ya
kimyakimya na Kaiza ndiye
aliyekuwa anatoa maelekezo
wapi waelekee.Macho yake
hayakubanduka katika simu
yake.
 
SIRI
MTUNZI: PATRICK CK
PART 1 SEASON 6
EPISODE 6
Saada baada ya kutoka
Lupai hotel,alifikiria sehemu ya
kwenda akaogopa kwenda
nyumbani kwake kwani alihisi
anaweza akafuatiliwa
huko.Hakutaka tena kurejea
nyumbani kwa Mathew kwani
aliyempeleka pale alikuwa
Devotha ambaye alipoteza
mawasiliano naye na hakujua
angempata wapi.Sehemu pekee
ambako aliamini ni salama
kwake kwa muda ule ni kwa
mpenzi wake Aziz Mubarak
anayeishi katika maghorofa ya
Kaumbe.
Toka Lupai hotel Saada
akamuelekeza dereva wa ile
taksi aliyopanda ampeleke
katika maghorofa ya
Kaumbe.Alikuwa na ufunguo
mmoja wa kuingia katika
nyumba ya mchumba wake
Aziz.Alimlipa dereva pesa yake
akapanda lifti hadi ghorofa ya
saba anakoishi mpenzi
wake.Akaingia ndani ya
nyumba ya mpenzi wake
akafunga mlango.Hakutaka
kuwasha simu yake kwa kuwa
aliogopa anafuatiliwa.Mle ndani
ilikuwemo kompyuta ya Aziz
akawasha na kumpigia simu
kupitia mtandao akamjulisha
kuwa amekwenda pale
kwake.Aziz akamjulisha kuwa
atafika pale muda si
mrefu.Baada ya dakika kumi na
tano Aziz akawasili kama
alivyoahidi.Saada hakumueleza
kitu chochote kilichotokea na
hata Aziz alipomtaka wafanye
mapenzi hakutaka kwani
hakutaka kuonyesha kama kuna
jambo limemtokea.
Kaiza na vijana wake
waliwasili katika maghorofa ya
Kaumbe.Kaiza akiwa na simu
yake ambayo ilimuelekeza
mahala aliko Saada aliwaongoza
vijana wake wakafika hadi
katika mlango wa kuingia katika
nyumba ya Aziz akagonga
mlango na Aziz akainuka
akaenda kuufungua.Alistuka
sana alipowaona wale
jamaa.Hakuwahi kuwaona
maeneo yale
“Karibuni” akasema kwa
wasiwasi
“Samahani kaka.Namuulizia
dada mmoja anaitwa Saada
Amiri” akasema Kaiza na Aziz
akastuka
“Aliwalekeza anaishi
hapa?akauliza
“Hajatuelekeza hivyo lakini
tunafahamu yuko humu ndani
hivyo tunaomba tuzungumze
naye” akasema Kaiza
“Ninyi ni akina nani?Ni
polisi?akauliza Aziz
“Hapana sisi si polisi ni
wafanyakazi wenza na
Saada.Tunamuomba
tuzungumze naye tafadhali ni
mambo ya kiofisi usiwe na
hofu” akasema Kaiza.Aziz
akageuka na kurejea ndani
“Darling kuna mtu yeyote
ulimjulisha kuwa unakuja
hapa?akauliza Aziz
“Hapana darling
sijamjulisha mtu yeyote Zaidi
yako.Kuna nini kwani?akauliza
Saada
“Una hakika?Azizi akauliza
“Ndiyo nina uhakika hata
simu yangu nimeizima ndiyo
maana nikawasiliana nawe kwa
kutumia mtandao.Kwani kuna
nini Aziz?
“Kuna watu
wanakuulizia.Wanadai ni
wafanyakazi wenzako.Twende
ukawasikilize wanadai
wamekufuata kwa mambo ya
kiofisi.Kama hujawaeleza uko
hapa nashangaa
wamefahamuje?akauliza Aziz.
Saada alipatwa na mstuko
mkubwa sana aliposikia kuna
watu wanamtafuta.
“Darling mbona umestuka
sana?akauliza Aziz
“Devotha ameniingiza
katika matatizo makubwa”
akawaza huku akiinuka na
kuvaa nguo zake
“Darling kuna tatizo
lolote?akauliza Aziz
“Hakuna tatizo Darling”
akasema Saada na kisha
akafungua mlango wa
chumbani na kutoka.Wakiwa
sebuleni Saada akasimama
akawaza.Aziz aliendelea
kumtazama.Saada akamfuata
akamkumbatia na kumbusu
“Nakupenda sana Aziz”
akasema kisha akatembea
hatua tatu kama kuna kitu
anakifuata ukutani ghafla
akachomoka hadi dirishani
akajirusha nje.Aziz akapiga
ukelele mkubwa uliowafanya
Kaiza na vijana wake kuingia
ndani ndipo wakashuhudia kile
kilichokuwa kimetokea.Wote
walibaki na mshangao
mkubwa.Aziz alitoka mbio
kushuka chini huku akipiga
kelele kama chizi.Kaiza
akawaelekeza watu wake
wafanye upekuzi wa haraka mle
ndani wakakuta mkoba wa
Saada uliokuwa na vifaa
vichache wakachukua
kompyuta mbili walizozikuta
mle ndani wakaondoka haraka.
“Damn you
Devotha.Umesababisha binti wa
watu akaamua kujitoa uhai kwa
woga.Damu yake na wale wote
uliowatoa uhai itaendelea
kukulilia siku zote za maisha
yako.Nitahakikisha
ninakukamata” akawaza Kaiza
akiwa garini.Kaiza akawataka
vijana wake kuchukua taksi
warejee kitalu 1 yeye akabaki
na gari lake akaelekea mahala
aliko Olivia
 
SIRI
MTUNZI: PATRICK CK
PART 1 SEASON 6
EPISODE 7
Saada baada ya kutoka
Lupai hotel,alifikiria sehemu ya
kwenda akaogopa kwenda
nyumbani kwake kwani alihisi
anaweza akafuatiliwa
huko.Hakutaka tena kurejea
nyumbani kwa Mathew kwani
aliyempeleka pale alikuwa
Devotha ambaye alipoteza
mawasiliano naye na hakujua
angempata wapi.Sehemu pekee
ambako aliamini ni salama
kwake kwa muda ule ni kwa
mpenzi wake Aziz Mubarak
anayeishi katika maghorofa ya
Kaumbe.
Toka Lupai hotel Saada
akamuelekeza dereva wa ile
taksi aliyopanda ampeleke
katika maghorofa ya
Kaumbe.Alikuwa na ufunguo
mmoja wa kuingia katika
nyumba ya mchumba wake
Aziz.Alimlipa dereva pesa yake
akapanda lifti hadi ghorofa ya
saba anakoishi mpenzi
wake.Akaingia ndani ya
nyumba ya mpenzi wake
akafunga mlango.Hakutaka
kuwasha simu yake kwa kuwa
aliogopa anafuatiliwa.Mle ndani
ilikuwemo kompyuta ya Aziz
akawasha na kumpigia simu
kupitia mtandao akamjulisha
kuwa amekwenda pale
kwake.Aziz akamjulisha kuwa
atafika pale muda si
mrefu.Baada ya dakika kumi na
tano Aziz akawasili kama
alivyoahidi.Saada hakumueleza
kitu chochote kilichotokea na
hata Aziz alipomtaka wafanye
mapenzi hakutaka kwani
hakutaka kuonyesha kama kuna
jambo limemtokea.
Kaiza na vijana wake
waliwasili katika maghorofa ya
Kaumbe.Kaiza akiwa na simu
yake ambayo ilimuelekeza
mahala aliko Saada aliwaongoza
vijana wake wakafika hadi
katika mlango wa kuingia katika
nyumba ya Aziz akagonga
mlango na Aziz akainuka
akaenda kuufungua.Alistuka
sana alipowaona wale
jamaa.Hakuwahi kuwaona
maeneo yale
“Karibuni” akasema kwa
wasiwasi
“Samahani kaka.Namuulizia
dada mmoja anaitwa Saada
Amiri” akasema Kaiza na Aziz
akastuka
“Aliwalekeza anaishi
hapa?akauliza
“Hajatuelekeza hivyo lakini
tunafahamu yuko humu ndani
hivyo tunaomba tuzungumze
naye” akasema Kaiza
“Ninyi ni akina nani?Ni
polisi?akauliza Aziz
“Hapana sisi si polisi ni
wafanyakazi wenza na
Saada.Tunamuomba
tuzungumze naye tafadhali ni
mambo ya kiofisi usiwe na
hofu” akasema Kaiza.Aziz
akageuka na kurejea ndani
“Darling kuna mtu yeyote
ulimjulisha kuwa unakuja
hapa?akauliza Aziz
“Hapana darling
sijamjulisha mtu yeyote Zaidi
yako.Kuna nini kwani?akauliza
Saada
“Una hakika?Azizi akauliza
“Ndiyo nina uhakika hata
simu yangu nimeizima ndiyo
maana nikawasiliana nawe kwa
kutumia mtandao.Kwani kuna
nini Aziz?
“Kuna watu
wanakuulizia.Wanadai ni
wafanyakazi wenzako.Twende
ukawasikilize wanadai
wamekufuata kwa mambo ya
kiofisi.Kama hujawaeleza uko
hapa nashangaa
wamefahamuje?akauliza Aziz.
Saada alipatwa na mstuko
mkubwa sana aliposikia kuna
watu wanamtafuta.
“Darling mbona umestuka
sana?akauliza Aziz
“Devotha ameniingiza
katika matatizo makubwa”
akawaza huku akiinuka na
kuvaa nguo zake
“Darling kuna tatizo
lolote?akauliza Aziz
“Hakuna tatizo Darling”
akasema Saada na kisha
akafungua mlango wa
chumbani na kutoka.Wakiwa
sebuleni Saada akasimama
akawaza.Aziz aliendelea
kumtazama.Saada akamfuata
akamkumbatia na kumbusu
“Nakupenda sana Aziz”
akasema kisha akatembea
hatua tatu kama kuna kitu
anakifuata ukutani ghafla
akachomoka hadi dirishani
akajirusha nje.Aziz akapiga
ukelele mkubwa uliowafanya
Kaiza na vijana wake kuingia
ndani ndipo wakashuhudia kile
kilichokuwa kimetokea.Wote
walibaki na mshangao
mkubwa.Aziz alitoka mbio
kushuka chini huku akipiga
kelele kama chizi.Kaiza
akawaelekeza watu wake
wafanye upekuzi wa haraka mle
ndani wakakuta mkoba wa
Saada uliokuwa na vifaa
vichache wakachukua
kompyuta mbili walizozikuta
mle ndani wakaondoka haraka.
“Damn you
Devotha.Umesababisha binti wa
watu akaamua kujitoa uhai kwa
woga.Damu yake na wale wote
uliowatoa uhai itaendelea
kukulilia siku zote za maisha
yako.Nitahakikisha
ninakukamata” akawaza Kaiza
akiwa garini.Kaiza akawataka
vijana wake kuchukua taksi
warejee kitalu 1 yeye akabaki
na gari lake akaelekea mahala
aliko Olivia
 
SIRI
MTUNZI: PATRICK CK
PART 1 SEASON 6
EPISODE 8
Mathew na Gosu Gosu
waliwasili katika makazi ya
bilionea Agrey
Themba.Aliwakuta walinzi
wawili nje ya geti.Walikuwa ni
walinzi wa kampuni binafsi ya
ulinzi na mmoja wao alikuwa na
bunduki.Akawasalimu na
kuwaeleza shida yake ya kutaka
kuonana na Lucy
Themba.Walinzi wale
wakamueleza kwamba hakuna
mgeni yeyote anayeruhusiwa
kuingia ndani bila ruhusa ya
Lucy Themba hivyo
wakawataka akina Mathew
wasubiri ili wamuulize
Lucy.Mmoja wa wale walinzi
akaingia ndani na kumuacha nje
yule mwenye bunduki.Mathew
akampa ishara Fulani Gosu
Gosu halafu akamuita yule
mlinzi
“Samahani kaka nataka
kuuliza” akasema Mathew yule
mlinzi ambaye bunduki yake
ilikuwa begani akasogelea gari
la akina Mathew.
“Unasemaje? akauliza
“Wewe uko hapa mara kwa
mara kuna tetesi zozote za
kupatikana kwa Olivia na baba
yake Agrey?akauliza
Mathew.Gosu Gosu akafungua
mlango wa gari akashuka na
kuzunguka nyuma ya gari
akajifanya anatazama matairi
huku akimsogelea yule jamaa
“Swali hilo muwaulize watu
wa familia mimi kazi yangu ni
kulinda.Sina muda wa kufuatilia
mambo ya ndani” akasema yule
jamaa na kutaka kugeuka
aondoke ghafla akajikuta
akizuiliwa na GosuGosu
aliyemuwekea bastora tumboni
“Ingia garini haraka sana
ama sivyo nitausambaza
utumbo wako sasa hivi”
akasema Gosu Gosu.Mathew
aliyekuwa ndani ya gari naye
akatoa bastora akamnyooshea
yule jamaa halafu akafungua
mlango kwa ndani Gosu Gosu
akamuingiza garini yule
mlinzi.Kabla hajakaa sawa yule
mlinzi akajikuta amepigwa
vichwa viwili mfululizo kutoka
kwa Gosu Gosu akaanguka kitini
hakuwa na fahamu.Akaichukua
silaha yake akaitupa nyuma ya
gari.
Mathew akashuka garini
haraka na kwenda katika ule
mlango mdogo akausukuma
taratibu akachungulia na
kumuona yule mlinzi akiwa
ndani ya nyumba ndogo ya
walinzi akiinua mkono wa simu
Mathew hakutaka kumpa nafasi
akaingia ndani na kwa kutumia
bastora yenye kiwambo cha
sauti akakipiga risasi kiganja
cha mkono wa yule jamaa
akaanguka chini.Kufumba na
kufumbua tayari Mathew
alikwisha ingia mle katika
nyumba ya walinzi.
“Usithubutu kupiga kelele
nitakumaliza.Nataka uniambie
Lucy Themba yuko ndani?
“Ndiyo yuko ndani”
akasema yule jamaa
“Kuna watu wangapi mle
ndani?Mathew akauliza
“Yupo Lucy na Teddy
mtumishi wa ndani” akajibu
yule mlinzi.Mathew akampiga
pigo zito akalala sakafuni
hakuwa na fahamu.Bila
kupoteza muda Mathew
akafungua geti Gosu Gosu
akaingiza gari ndani Mathew
akamuelekeza amshughulikie
yule jamaa aliyepigwa risasi
mkononi ili damu isiendele
kumwagika yeye akapiga hatua
ndefu kuelekea mlango mkuu
wa kuingilia
sebuleni,akakinyonga kitasa
mlango ukafunguka akaingia
sebuleni hakukuwa na mtu
yeyote.Akanyata taratibu
kuelekea katika chumba cha
chakula.Akasikia sauti ya
mwanamke akiimba.Sauti ile
ilitokea jikoni akanyata taratibu
na kumuona msichana mmoja
akiosha vyombo huku
akiimba.Mathew akakohoa
kidogo msichana yule akastuka
na kugeuka sahani aliyoishika
ikamponyoka na kuanguka
chini baada ya kujikuta
akitazamana na bastora.Mwili
wote ulimtetemeka.
“Shhhhhh !! Mathew
akamfanyia ishara asipige
kelele.
“Nionyeshe alipo Lucy!
“Yuko chumbani kwake”
akajibu yule msichana huku
akitetemeka Mathew akamtaka
amuongoze kuelekea chumbani
kwa Lucy.Alimuonyesha mlango
wa chumba cha Lucy na
Mathew akamtaka agonge
mlango naye akafanya kama
alivyoelekezwa akagonga
mlango
“Nani? Ikauliza sauti
kutokea ndani
“Mama ni mimi” akajibu
yule mtumishi
“Unasemaje Teddy?akauliza
Lucy Themba akiwa chumbani
kwake.
“Mwambie kuna kitu
unataka kuuliza”akasema
Mathew kwa sauti ya chini sana
“Mama kuna kitu nataka
kukuuliza” akasema Teddy na
baada ya sekunde kadhaa
mlango ukafunguliwa.Lucy
Themba alipatwa mstuko
mkubwa mno kama vile
ameona jitu la kutisha baada ya
kumuona Mathew Mulumbi
akiwa na bastora.Alitaka
kuufunga mlango Mathew
akawahi akaupiga teke mlango
ukambamiza Lucy akaanguka
chini Mathew akachumpa ndani
na kumuelekezea bastora
“Simama tafadhali !!
akasema Mathew
“Niue tu shetani
wewe.Siendi kokote!akasema
Lucy
“Lucy nakupa sekunde tano
uwe umeinuka mwenyewe !!
“Nimesema niue siendi
kokote” akasema Lucy
Mathew akailenga taa
kubwa iliyokuwa juu
ikasambaratika na kutoa
mlio.Lucy alikuwa anatetemeka
mwili kwa woga.Mathew
akamuinua
“Lucy tafadhali fanya kile
ninachokuelekeza ili uwe
salama” akasema Mathew na
kumuamuru Lucy atoke
wakaenda sebuleni
“Ninakuhakikishia Mathew
hautafika mbali na huu mchezo
unaoufanya.Kwa taarifa yako
unatafutwa kila kona.Tayari
serikali inafahamu kila kitu
kuhusu wewe”akasema Lucy
lakini Mathew hakumjibu kitu.
“Mathew tumekukosea kitu
gani hadi ututese namna hii?Ni
kitu gani unakitafuta
kwetu?Unahitaji fedha?Sema ni
kiasi gani unataka tukupatie
utuache salama kuliko
kuendelea kututesa kiasi hiki !
Akasema Devotha.Mathew
hakujibu kitu aliendelea
kumtazama Lucy halafu
akaweka bastora mezani na
kusema
“Mama kwanza kabisa
nakuomba samahani kwa hiki
kilichotokea.Imenilazimu
kutumia njia hii ya nguvu kwani
isingekuwa rahisi wewe
kukubali kuzungumza nami
kwa kuwa tayari unafahamu
mimi ni mtu mbaya na nina
malengo mabaya na familia
yako.Mama nimekuja hapa kwa
mazungumzo muhimu
nawe.Naomba unipe dakika
kadhaa na unisikilize kwa
makini” akasema Mathew Lucy
Themba akaendelea kumtazama
kwa hasira
“Mama naomba niende
moja kwa moja katika jambo la
msingi lililonileta
hapa.Ulinipigia simu asubuhi
leo ukanitaka nifike nyumbani
kwako kuna jambo unataka
kuniambia nikafika kwako na
kumbe ulikuwa ni mtego
umeandaliwa
nikatekwa.Nimekuja kukueleza
kile ambacho nimekigundua
huko mahala nilikokuwa
nimepelekwa baada ya
kutekwa.Naomba unisikilize
kwa makini sana” akasema
Mathew na kumtazama Lucy
Themba
“Waliponitoa hapa
walinilipeleka mahala kunaitwa
Kitalu 1 nikafungiwa ndani ya
chumba kilicho zaidi ya mita
mia chini ya ardhi.Nilihojiwa na
mwanamama anaitwa Devotha
ambaye ndiye mkurugenzi wa
idara hiyo na kikubwa alitaka
kufahamu kuhusu mahusiano
yangu na Olivia.Nilimweleza
kila kitu bila kumficha akataka
kufahamu kwa nini ninamlinda
Olivia hadi nikampa namba
maalum za kunijulisha mahala
alipo pindi anapokuwa katika
hatari.Nilimueleza Devotha kila
kitu na ndipo alipoamua
kufunguka ukweli kwamba
sababu iliyowafanya
wanishikilie ni ukaribu wangu
na Olivia.Mama kuna kitu
ambacho nadhani hamkifahamu
kuhusu Olivia na hata mimi
sikuwa nikikifahamu hadi
asubuhi ya leo” Mathew
akanyamaza tena kidogo halafu
akaendelea
“Olivia anashirikiana na
magaidi wa kikundi cha IS”
akasema Mathew na
kunyamaza baada ya kuuona
mstuko mkubwa katika uso wa
Lucy Themba.
“Hapana ! Hilo jambo si
kweli !! akasema Lucy na
kusimama
“Mama naomba kaa chini
tafadhali ! akasema Mathew
“Hakuna utakachoniambia
kuhusu huo uongo wako
nikaukubali.Olivia ni mwanangu
nimemzaa na kumlea
mwenyewe.Ninamfahamu
alivyo kulio mtu
yeyote.Ninazifahamu tabia zake
ninafahamu kila kitu kuhusu
Olivia na ninadiriki kusema
katu hawezi akafanya kitu kama
hicho.Katu hawezi akajihusisha
na magaidi!! Akasema Lucy
Themba kwa ukali
“Mama naomba unisikilize
bado ninaendelea” akasema
Mathew.Lucy Themba
akaonekana kutulia kusikiliza
“Olivia ametekwa na idara
ya siri ya usalama wa ndani wa
nchi” akasema Mathew na Lucy
akastuka tena
“Unasema mwanangu
ametekwa na idara ya
serikali?akauliza
“Mama naomba tafadhali
endelea kunisikiliza” akasema
Mathew
“Idara ya usalama wa taifa
ya nchini jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo
walipata taarifa za kiintelijensia
kwamba kuna mtu kutoka
kikundi cha Islamic States
anaitwa Seif Almuhsin
anaelekea nchini kwao hivyo
wakaanza kumfuatilia toka
alipoingia Congo na katika
kumfuatilia wakagundua
kwamba Seif alikutana na
kufanya mazungumzo na
mtanzania.Kwa bahati mbaya
sina picha zake hapa lakini
alipigwa picha na zikaletwa Dar
es salaam kwa rais.Mtanzania
huyo aliyekutana na Seif
Almuhsin akatambulika kuwa ni
mwanao Olivia
Themba”akasema Mathew na
Lucy akahamaki
“No ! No ! That’s impossible
!! akasema Lucy kwa ukali
“Nisikilize mama” akasema
Mathew
“Idara ya siri ya usalama wa
ndani ya nchi walitaka kujua
sababu ya Olivia kukutana na
kufanya mazungumzo na Seif
mtu ambaye kazi yake kubwa ni
kukusanya vijana kutoka nchi
za ukanda wa afrika mashariki
na kati na kuwapeleka katika
makambi ya IS ambako
hufundishwa ugaidi hivyo
wakaandaa mpango wa
kumteka mara tu atakapotua
nchini akitokea Kinshasa”
“Mathew naomba usicheze
na akili yangu baba.Unaniambia
mwanangu ametekwa na idara
ya serikali?akauliza Lucy
“Baada ya kutekwa Olivia
alihojiwa na katika kumpekua
wakakuta mawasiliano ya barua
pepe kati yake na mtu anaitwa
Sayid Omar ambaye anatajwa
kuwa mfadhili mkubwa sana wa
kikundi cha IS.Walimtaka Olivia
awaeleze kwa kina kuhusu
kinachoendelea kati yake na
IS.Katika mahojiano akawapa
namba ambazo nilimpa mimi
apige pindi atakapokuwa katika
hatari ili kunijulisha akidai
zinaweza kuwasaidia kufahamu
alipo Sayid Omar.Namba zile ni
kirusi na ambacho kiliufunga
kabisa mfumo wote wa
mawasiliano wa idara hiyo ya
siri ya serikali.Baada ya kila kitu
kusimama Olivia aliombwa
aufungue mfumo huo lakini
akagoma kuufungua hadi
atakapozungumza na Rais hivyo
ikawalazimu viongozi wa idara
hiyo kufanya mpango na
kumuita Rais akakutana na
Olivia”Mathew akanyamza
baada ya Lucy kusimama na
kuweka mikono kichwani
“Mathew unataka
kuniambia Rais alionana na
Olivia? Rais anafahamu kuhusu
jambo hili la kutekwa
Olivia?akauliza Lucy huku
akihema haraka haraka
“Ndiyo mama.Rais
nafahamu na alikwenda
kuonana na Olivia.Katika
mazungumzo yao Olivia
alimueleza kusudi la kutaka
kuonana naye.Alimweleza Rais
kwamba mwanae anayeitwa
Coletha ameambukizwa virusi
ambavyo amevitengeneza yeye
mwenyewe Olivia na Coletha
anaweza kupoteza maisha kama
rais hatatekeleza kile
atakachomuelekeza.Naomba
nikurudishe nyuma kidogo
mama.Nilikueleza kwamba
Olivia alikuwa anawasiliana na
Sayid Omar na nilibahatika
kuzisoma barua pepe
walizokuwa wanatumiana
ambazo zilikuwa katika lugha
ya kiarabu na katika
mawasiliano yao walikuwa
wanawasiliana kuhusiana na
mradi wa kutengeneza kirusi
ambacho ndicho hicho
ameambukizwa Coletha mtoto
wa rais”akasema
“Mathew unataka kuupasua
moyo wangu.Olivia mwanangu
huyu anaweza akafanya kitu
kama hicho?Anaweza
akatengeneza kirusi kwa lengo
la kumuua mtoto wa
rais?Hapana si kweli”akasema
Lucy Themba
“Lengo la Olivia si kumuua
Coletha bali ni kumshinikiza
Rais aweze kutimiza matakwa
yake na ili kumfanya rais
amsikilize ndiyo maana
akamuambukiza mwanae virusi
hivyo na ni yeye pekee mwenye
tiba yake.Hivi sasa Coletha yuko
hospitali akiendelea kufanyiwa
uchunguzi na hali yake
inaendelea kuwa mbaya”
“Jesus Christ !! akasema
Lucy.Mathew akamtazama na
kuendelea
“Kuna jambo ambalo Olivia
analitaka kutoka kwa
rais.Nadhani unamkumbuka
mtu anaitwa Edger
Kaka.Aliwahi kuwa mbunge na
akapata ajali akafariki miaka
mitatu iliyopita”
“Ninamkumbuka.Olivia
ndiye aliyeokoa maisha yake
kwa kumpeleka hospitali Israel
na alipata ajali na kufariki dunia
wakati akielekea nyumbani
kwake baada ya kurejea nchini
akitokea Israel” akasema
Lucy.Mathew akaendelea
“Olivia anadai kwamba
Edger Kaka hajafariki yuko hai”
“Edger Kaka
hajafariki?Kivipi?Lucy Themba
akashangaa
“Hakuna anayefahamu hadi
sasa kwa nini ametoa madai
hayo lakini hicho ndicho
anachoendelea kukisisitiza
kwamba Edger kaka hakufariki
katika ile ajali na anadai kuwa
amefanya uchunguzi wake
akagundua mwili ule uliozikwa
katika kaburi la Edger haukuwa
wa Edger bali ni wa mtu
mwingine kabisa hivyo Edger
yuko hai”
“Nashindwa kukuelewa
Mathew.Tulikuwa tumetoka
kumpokea Olivia uwanja wa
ndege akirejea nchini yeye na
Edger Kaka wakitokea
Israel.Wakati wa kuondoka
uwanja wa ndege Edger na
msafara wake wakatangulia sisi
tukaondoka dakika chache
baade.Tukiwa njiani tulipitwa
na magari mawili ya zimamoto
na mbele kidogo tukakuta ajali
kubwa na magari yakiwaka
moto,tukajulishwa kuwa
imetokea ajali na miongoni
mwa magari yaliyopata ajali ni
gari la mbunge Edger
Kaka.Baada ya moto kuzimwa
miili iliyokuwa imeungua
ikatolewa na kupelekwa
hospitali.Olivia alitaka
kuhakikisha ni kweli Edger
amefariki katika ajali ile
tukampeleka hospitali. Ni mimi
niliyemshika mkono Olivia
katika chumba cha maiti na
akautambua mwili wa Edger
Kaka uliokuwa umeungua na
hautambuliki lakini aliugundua
kutoka na mkufu wa shingoni
pamoja na pete za
vidoleni.Iweje leo aibuke na
kudai kuwa Edger hajafa?
Yawezekana mwanangu
amepatwa na matatizo ya akili!!
Akasema Lucy
“Olivia hana tatizo lolote la
kiakili mama.Amesimama
katika kauli yake na anachodai
ni kuwa ajali ile ni ya
kutengeneza na kwamba Edger
yuko mahala
amefichwa.Amekwenda mbali
Zaidi kwa kumtaja muhusika
mkuu wa mchezo huo kuwa ni
rais Dr Evans na kitendo cha
kumuambukiza mwanae virusi
ni ili kumshinikiza aweze
kumuonyesha mahala aliko
Edger Kaka.Olivia ameendelea
kulisisitiza jambo hili na amedai
kama rais hatamuonyesha
mahala alipo Edger basi
mwanae atakufa.Ili
kumshinikiza Olivia aweze
kufunguka na kueleza ukweli
wote kuhusu mashirikiano yake
na IS iliwalazimu kumteka pia
baba yake Agrey Themba ili
kusaidia kumfungua Olivia
lakini bado haikusaidia kitu
Olivia hajafunguka na bado
anaendelea kusisitiza kuwa
Edger hajafa na anamtaka rais
amuonyeshe mahala alipo.Dr
Evans ameulizwa kuhusu suala
hilo akakiri hajui chochote
kuhusu Edger Kaka kuwa
hai.Baada ya kuendelea
kusisitiza jambo hilo mkuu wa
idara ya usalama wa ndani ya
nchi anaitwa Devotha akaamua
kuanza kulichuguza hili jambo
ili kuubaini ukweli.Alianza kwa
kudukua simu ya rais ili
afahamu kama Rais
analifahamu jambo hilo lakini
hakufanikiwa na akagundulika
kuwa amedukua simu ya rais
hivyo akaanza
kutafutwa.Ilimlazimu kufanya
kila juhudi kunitoa mahala
nilikokuwa nimefungiwa
akisaidiwa na mwenzangu yuko
nje anaitwa Gosu Gosu na katika
harakati za kuniokoa Devotha
amepigwa risasi na hivi sasa
yuko hospitali anayapigania
maisha yake.Mimi na
mwenzangu tunaendelea na
suala ili kuutafuta ukweli wa
jambo hili analosema Olivia
kuwa Edger yuko hai na vile vile
kujua kwa nini Olivia
anashirikiana na magaidi.Kwa
hiyo mama nimekuja hapa ili
kukupa taarifa hizo ujue
kinachoendelea hivi sasa
kuhusu mwanao” akasema
Mathew.Lucy Themba akafuta
machozi.
“Nataka kufahamu jambo
moja tu je rais anafahamu pia
kuhusu kutekwa kwa mume
wangu Agrey?akauliza Lucy
Themba
“Kila kinachofanyika katika
idara hiyo ya siri ya mambo ya
ndani ya nchi,Rais anakifahamu
hivyo naamini hata kutekwa
kwa Agrey Themba anafahamu
pia” akasema Mathew
“Nihakikishie mume wangu
na Olivia wako salama”
akasema Lucy akiendelea
kufuta machozi
“Mama hakuna
anayefahamu hadi sasa mahala
walipo Olivia na baba yake
Agrey Themba lakini naamini
wako salama.Mimi na
mwenzangu Gosu Gosu jukumu
letu ni kuwatafuta na kufahamu
mahala walipo na kuufahamu
ukweli wa hili
jambo.Nimekuleta hapa mama
kukueleza suala hili na
kukuthibitishia kuwa uko
salama.Ninachokuomba toka
kwako ni kuniamini.Nilikuja
kwenu nikawaomba ruhusa
niweze kusaidia kumtafuta
Olivia ukaniruhusu lakini
baadae ukabadilika
ukashirikiana na wale jamaa
waliomteka mwanao mkaweka
mtego nikatekwa.Mimi si mtu
mbaya.Olivia ni rafiki yangu na
mimi nina nia ya dhati ya
kumtafuta.Nina uzoefu mkubwa
wa mambo haya ya kiuchunguzi
na ninakuhakikishia kwamba
Olivia na baba yake
watapatikana lakini ni pale tu
utakapokuwa tayari
kushirikiana nami” akasema
Mathew.Lucy Themba
alimuangalia Mathew kwa
macho ya huruma
“Mama haya yote
niliyokueleza ni ukweli mtupu
naomba uniamini.Bila
kuunganisha nguvu hatutaweza
kuwapata Olivia wala baba
yake.Agrey Themba hana kosa
lolote na hajui kama mwanae
anashirikiana na magaidi hivyo
lazima tuhakikishe tunamuokoa
lakini kwa Olivia tunataka
kumpata ili kufahamu kwanza
kuhusu mashirikiano yake na
magaidi na pili kupata uhakika
wa hicho anachokisisitiza kuwa
Edger Kaka you hai.Yawezekana
ni kweli Edger Kaka yuko hai na
yawezekana ni kweli Rais
anahusika katika suala hili na
kama hayo yote ni kweli basi
Olivia atakuwa katika wakati
mgumu sana na kuna hatari
anaweza akapotezwa ili jambo
hili liendelee kubaki siri.Jukumu
letu ni kumuokoa Olivia na
kuufahamu ukweli”akasema
Mathew
“Mathew nashindwa
niseme nini.Ulichonieleza
kimenistua mno na ulimi wangu
unakuwa mzito hata kutamka
chochote.Kwanza ni kuhusu
mwanangu Olivia kushirikiana
na magaidi na pili ni kuhusu
hicho anachodai eti Edger Kaka
yuko hai lakini kubwa Zaidi ni
Rais kulifahamu suala hili la
kutekwa Olivia.Ninatamani sana
kuyaamini hayo unayoyasema
Mathew lakini
ninashindwa”akasema Lucy
“Kitu gani kinakuwia
ugumu kuniamini mama?
“Yote uliyonieleza.Kwanza
kuhusu Olivia kushirikiana na
magaidi.Ninamfahamu vyema
Olivia hawezi katu kufanya kitu
kama hicho.Nimemlea katika
maadili mazuri na ninarudia
tena kwamba hana sababu
yoyote ile ya kujiunga na
magaidi kama mnavyodai.Pili ni
kuhusu rais Dr Evans.Huyu ni
rafiki mkubwa sana wa familia
yetu na amekuwa anasaidiana
nasi kwa hali na mali kumtafuta
Olivia toka tukio hili
lilipotokea.Anatumia uwezo
wake wote katika kuhakikisha
Olivia na baba yake
wanapatikana.Dr Evans hawezi
katu akafanya jambo kama hilo
kwa familia yetu.Jambo
lingine,Olivia hawezi kabisa
kumfanyia Coletha jambo lolote
baya.Wanapendana na wanaishi
kama ndugu hivyo hawezi
kabisa akamtengenezea virusi
vinavyoweza kumdhuru.Olivia
hana roho mbaya ya namna
hiyo” akasema Lucy
“Hivi sasa Coletha yuko
hospitali amelazwa
anaumwa.Unaweza
ukalithibitisha hilo kwa muda
wako lakin..” Mathew akataka
kusema kitu Lucy akainuka
Mathew akamtaka aketi
“Ninataka kuwasiliana na
rais ili kuthibitisa hilo
unalolisema lakini simu yangu
iko chumbani” akasema Lucy.
“Mtume mtumishi wako wa
ndani akuletee nataka
uzungumze hapa mbele yangu”
akasema Mathew na Lucy
akamuita Teddy akamtuma
amletee simu yake na ilipoletwa
akazitafuta namba za simu za
rais akampigia.
“Weka sauti kubwa nataka
kusikia kile
mnachokizungumza” akasema
Mathew
“Hallow Lucy” akasema Dr
Evans baada ya kupokea simu
“Dr Evans samahani kwa
usumbufu nimekupigia kutaka
kujua maendeleo.Sijapata
mrejesho wowote kutoka
kwako toka asubuhi Mathew
alipochukuliwa.Kuna taarifa
zozote hadi hivi sasa za kuhusu
Olivia na baba yake? Mathew
amesema chochote?akauliza
Lucy
“Samahani Lucy sikuwa
nimekujulisha kile kilichokuwa
kinaendelea.Vijana wangu bado
wanaendelea kumuhoji Mathew
Mulumbi ili aweze kufunguka
na kueleza kila kitu.Yule jamaa
aliwahi kufanya kazi katika
idara ya ujasusi na ni mtu
anayefahamu mbinu zote za
mateso hivyo si rahisi
kumfungua na kumfanya asema
kila kitu lakini usihofu Lucy
nitakujulisha kila pale
nitakapopata taarifa kutoka
kwa watu wangu.Bado juhudi za
kuwatafuta Olivia na baba yake
zinaendelea.Ninaendelea
kuwasiliana na jeshi la polisi
wamenihakikishia kwamba
wamefika sehemu nzuri katika
kufahamu mahala walipo Olivia
na baba yake na kwa kuwa ni
mapema bado siwezi kuweka
wazi taarifa za kiuchunguzi
ninachokuomba niamini na
tuliamini jeshi la polisi
wanafanya kazi nzuri sana
kuhakikisha Olivia na Agrey
wanapatikana wakiwa salama
salimini” akasema Dr Evans
“Ninashukuru sana Dr
Evans kwa namna ulivyojitoa
katika jambo hili.Kabla
sijasahau nimepata taarifa
kuwa Coletha amelazwa
hospitali.Hizi ni taarifa za
kweli?akauliza Lucy na swali
lile likaonekana kumstua Dr
Evans
“Dr Evans” akaita Lucy
baada ya Dr Evans kuwa kimya
“Lucy ni kweli Coletha
amelazwa hospitali.Samahani
sikukueleza jambo hili”
“Nimeshangaa sana kwa
mtoto kulazwa hospitali bila
kutujulisha.Nimepata taarifa
hizo kutoka kwa watu wengine
kabisa”
“Nisamehe sana Lucy kwa
kutokufahamisha”
“Nini kinamsumbua
Coletha?akauliza Lucy
“Kulitokea tukio la moto
chuoni kwao na katika harakati
za kujiokoa akapoteza fahamu
na toka wakati huo hajisikii
vizuri ndiyo maana
nikamchukua na kumpeleka
hospitali kwa ajili ya uchunguzi
kufahamu nini
kinachomsumbua.Lakini
maendeleo yake ni mazuri”
akasema Dr Evans
“Nashukuru Dr
Evans.Nitakwenda kumjulia hali
nikipata nafasi”
“Sawa Luvy lakini kesho
anaweza akatoka hospitali kwa
mujibu wa madaktari” akasema
Dr Evans
“Mpe pole sana.Usiache
kunijulisha maendeleo yake vile
vile kile kinachoendelea katika
utafutaji wa familia yangu”
akasema Lucy
“Nitakujulisha Lucy”
akasema Dr Evans wakaagana
na kukata simu.Lucy
akamtazama Mathew
“Nadhani sasa
umejihakikishia mwenyewe
kwamba ninachokueleza ni kitu
cha kweli kabisa.Coletha
anaumwa yuko hospitali na
kinachomsumbua ni virusi
alivyoambukizwa na Olivia
akishirikiana na watu wa
IS.Mama ninayokueleza yote
haya ni ukweli mtupu”akasema
Mathew
“Kidogo ninaanza
kukuamini Mathew.Dr Evans
amekuwa na ukaribu mkubwa
sana kwetu na toka jambo hili
lilipotokea amekuwa karibu
kutufariji na kutuhakikishia
kuwa Olivia
atapatikana.Itaniumiza sana
kama nikihakikisha ni yeye
aliye..”akasema Lucy na
kukatishwa na Mathew
“Ninakuhakikishia mama
rais Dr Evans anafahamu kila
kitu kuhusu suala hili na
anafahamu mahala walipo
Olivia na baba yake.Hayo
maneno ya kwamba jeshi la
polisi wako karibu kuwapata ni
uongo mkubwa anakupa moyo
wakati anafahamu fika kuwa
hawatajua mahala
alipo”akasema Mathew.Lucy
akafikiri kidogo na kusema
“Kwa haya uliyonieleza
kuna picha Fulani ninaanza
kuipata.Jana usiku ulipoondoka
hapa nikampigia simu rais na
kumfahamisha kuwa Agrey
amepotea.Nilimueleza kila kitu
namna alivyotoweka na
aliposikia jina lako likitajwa
akasema moja kwa moja kuwa
wewe unahusika katika suala
hilo na kwamba lazima
ukamatwe ili ueleze mahala
walipo Olivia na Agrey.Ni yeye
aliyewatuma watu wake wakaja
kuweka mtego na kukuchukua
nikiamini maneno yake kuwa
unahusika na utekaji ule wa
Olivia na baba yake.Maneno
unayonieleza kuwa anafahamu
kila kinachoendelea yameukata
kabisa moyo
wangu.Nimechanganyikiwa
niambie nifanye nini
Mathew?akauliza Lucy
“Kwa sasa usifanye
chochote.Nimekuja kukueleza
mambo haya ili kukuweka sawa
ufahamu kile
kinachoendelea.Usimweleze
chochote Dr Evans kwamba
umefahamu yeye yuko nyuma
ya haya matukio ya utekaji wa
familia yako.Msikilize kila
atakachokueleza.Mimi na timu
yangu tunaendelea na zoezi la
kuwatafuta Olivia na baba yake
na tayari tuna chanzo kizuri cha
kujua mahala alipo
Olivia.Tukimpata Olivia itakuwa
rahisi kufahamu ukweli wa kile
kinachoendelea.Kama nitahitaji
msaada wako wowote nitakuja
kukuomba lakini nakuomba
usimweleze mtu yeyote haya
tuliyoyazungumza.Dr Evans
akifahamu kuwa umeifahamu
siri yake utakuwa katika hatari
kubwa hivyo jizuie kuzungumza
lolote.Narudia tena
kukuhakikishia mama kuwa
mimi na wenzangu tutafanya
kila linalowezekana
kuhakikisha tunafahamu
mahala waliko Olivia na mzee
Agrey” akasema Mathew
“Mathew sijui nikwambie
nini baba lakini naomba
samahani sana kwa kile
nilichokufanyia kijana
wangu.Niliaminishwa na Dr
Evans kwamba wewe ni mtu
mbaya na kwamba ndiye
unayehusika na matukio yote ya
kutekwa kwa Olivia na
Agrey.Nilifanya makosa
makubwa sana kuamini taarifa
hizi.Nisamehe sana.Bila wewe
nisingeyafahamu haya
yote.Ahsante kwa kuja
kunieleza siri hii uliyoifahamu”
akasema Lucy
“Mama usijali.Kila kitu
huongozwa na Mungu.Kama
nisingetekwa tusingeifahamu
siri hii.Narudia tena kukuomba
mama usimueleze mtu yeyote
hili jambo hadi hapo
tutakapokuwa tumewapata
Olivia na Agrey”akasema
Mathew
“Mathew nawaombea
Mungu awatangulie muweze
kuwapata Olivia na mume
wangu Agrey.Chochote
mnachokihitaji nielezeni
nitawapatia” akasema Lucy
“Ninashukuru mama kama
kuna msaada nitahitaji kutoka
kwako nitakujulisha.Narudia
kukuomba mama Jambo hili ni
siri kubwa asifahamu mtu
mwingine yeyote.Hata
unapotaka kuwasiliana name
usitumie simu yako ya kawaida
naamini watakuwa wanafuatilia
simu zako.Tafuta simu nyingine
na utawasiliana nami kupitia
namba hizi za simu” akasema
Mathew na kumpatia Lucy
namba za simu anazotumia
kisha akainuka kwa ajili ya
kuondoka
“Mama kabla sijasahau
kuna mlinzi wako mmoja
amejeruhiwa mkononi katika
harakati za kutaka kuingia hapa
ndani naomba atibiwe na
uwaonye wasiseme chochote
kwa mtu yeyote kuhusu mimi
kuja hapa” Mathew
akamuelekeza Lucy
“Nitafanya hivyo Mathew”
akasema Lucy akaongozana na
Mathew hadi lilipo gari lao
wakaagana na kuondoka zao.
“Maneno ya Mathew
kuhusu Dr Evans kufahamu
kutekwa kwa Olivia na Agrey
ninaweza kuyakubali.Amekuwa
mstari wa mbele sana kutupa
moyo na kutuhakikishia kuwa
Olivia atapatikana tusihofu hata
alipopotea Agrey amekuwa
karibu nami sana kunifariji na
kunihakikishia kuwa
watapatikana.Sikutegemea
kama Dr Evans anaweza
akatufanyia hivi.Sisi tumekuwa
ni kama n dugu zake iweje
atutese namna hii?
Nimemchukia ghafla kwa hili
alilotufanyia.Natamani hata
sasa nimpigie simu nimjulishe
tayari ninafahamu kila kitu
anachotufanyia lakini Mathew
ameniomba sana nisimueleze
chochote Rais ili nimpe nafasi
ya kuweza kuwatafuta Olivia na
Agrey” akawaza Lucy na kuhisi
baridi pale alipoyakumbuka
maneno ya Dr Evans namna
alivyokuwa akiwapa moyo
“Nilifanya makosa
makubwa kumuamini Dr Evans
aliponidanganya kuhusu
Mathew.Alisisitiza Mathew
lazima akamatwe kwa sababu
alijua tayari anafahamu nani
waliomteka Olivia na angeweza
kuvuruga mipango yao.Ninahisi
yawezekana Agrey aliwasiliana
naye akamjulisha kuhusu
Mathew kufahamu mahala alipo
Olivia na ndiyo maana Olivia
akahamishwa mahala
alipokuwa amefichwa.Evans
ametufanyia kitu kibaya mno
ambacho sikukitegemea
kabisa..”Lucy akastuka kama
mtu aliyekuwa ndotoni baada
ya kukumbuka kitu
“Mathew anadai Olivia
anashirikiana na magaidi wa
IS.Hii taarifa bado kidogo
inipasue moyo
wangu.Mwanangu Olivia
anashirikiana na magaidi?!!
Kama ni kweli kitu gani
kimemuingia na kumfanya
aamue kufanya kitu kama
hiki?Amekosa nini Olivia hadi
akaamua kujiunga na
magaidi?Balaa gani hili
anatuletea katika familia
yetu?akajiuliza Lucy na
kumtafakari Olivia kiundani.
“Hapana siamini kama
Olivia wangu amebadilika na
kuwa gaidi.Nakubaliana na
Mathew kwamba uchunguzi
ufanyike ili tuufahamu ukweli
wa hili jambo” Lucy alihisi
kuchanganyikiwa akaenda
chumbani kwake
 
SIRI
MTUNZI: PATRICK CK
PART 1 SEASON 6
EPISODE 9
“Nilikueleza kilichotokea
jana nilipokwenda kumuokoa
Olivia” Mathew akamwambia
Gosu Gosu walipoondoka
nyumbani kwa Lucy
“Ndiyo ulinieleza” akasema
Gosu Gosu
“Baada ya kumkosa Olivia
na kutekwa kwa Agrey Themba
niliamini kuna mtu mwenye
ukaribu na familia ya akina
Olivia ambaye anashirikiana na
watekaji na leo nimepata jibu
kuwa ni rais Dr Evans.Yeye na
Agrey Themba ni marafiki
wakubwa na walikuwa
wanamshirikisha kila
kinachoendelea.Jana usiku
walimjulisha kuhusu mimi
kufahamu mahala alipo Olivia
na mipango yangu ya kwenda
kumuokoa bila kujua kama
anafahamu kila kitu.Rais
aliwasiliana na watu wake wa
idara ya usalama wa ndani ya
nchi waliokuwa wamemteka
Olivia na wakamuondoa Olivia
haraka sana kabla sijafika na
nilipofika nikaambulia
patupu.Ninaanza kuyaamini
maneno aliyosema Olivia kuwa
Edger kaka hajafa na kwamba
Dr Evans anahusika katika suala
hili na anafahamu mahala alipo”
Akasema Mathew na kumueleza
Gosu Gosu kila kitu
alichozungumza na Lucy
Themba
“Tuliweke pembeni hilo la
Edger Kaka na tushughulikie
kwanza kumpata Olivia ambaye
ndiye mwenye ukweli
wote.Kwa kuwa tunao muda
mchache kabla Ruby hajawasili
tupite madukani tununue vifaa
alivyoelekeza nimuandalie kwa
ajili ya kufanyia kazi yake”
akasema Mathew
“Inaumiza sana kwa familia
ya Olivia kugundua kwamba
rais ambaye ni mtu wao wa
karibu analifahamu suala hili la
utekaji na amekuwa
akiwadanganya”akasema Gosu
Gosu
“Inaumiza sana.Nilimuona
namna Lucy alivyostuka
alipofahamu kuwa rais
anafahamu kila kitu kuhusu
kutekwa kwa Olivia na baba
yake”
“Una hakika hawezi
akaharibu mambo yule
mama?akauliza Gosu Gosu
“Hapana hataweza
kuharibu kitu kwani tumani
pekee la kuwapata Olivia na
mume wake liko kwangu hivyo
atafuata maelekezo yote
nitakayompa” akasema Mathew
 
SIRI
MTUNZI: PATRICK CK
PART 1 SEASON 6
EPISODE 10
Baada ya kumaliza
kuzungumza na Lucy Themba
simuni,Dr Evans akasimama na
kushika kiuno
“Mambo yanazidi kuwa
magumu.Nilitegemea hadi
muda huu Mathew awe
amekwisha funguka na tujue
kila kitu kinachoendelea
kuhusu mipango ya IS lakini
ametoroshwa na hajulikani
alipo.Alikuwa ni mtu muhimu
sana kwetu.Devotha amefanya
kitu kibaya mno kuamua
kumtorosha Mathew.Nguvu
kubwa kwa sasa ni kuielekeza
kwa Olivia.Kama bado
ataendelea kuwa mgumu
nitaagiza hata mama yake naye
achukuliwe aunganishwe na
baba yake.Akiwaona wazazi
wake wanavyopata mateso
atafunguka” akawaza Dr Evans
akachukua simu na kumpigia Dr
Mbeula ikiwa ni mara ya tatu
kumpigia toka asubuhi
“Mheshimia rais” akasema
Dr Mbeula
“Dr Mbeula nataka
kufahamu maendeleo ya
mwanangu.Kuna hatua yoyote
mmepiga hadi hivi
sasa?akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa rais
tumeendelea na zoezi la
kuvifahamu kwa undani virusi
hivi ili tuone namna ya
kuvikabili lakini kadiri muda
unavyokwenda ndivyo
tunavyozidi kugundua mambo
mengine Zaidi kuhusu virusi
hivi.Kwanza kabisa virusi hivi
vina tabia ya kujibadili
umbo.Kila vinapokutana na
dawa au kemikali aina Fulani
hujibadili umbo lake. Hivyo
inatupa ugumu kupata dawa ya
kupambana navyo.Pili virusi
hawa wakiingia katika mwili wa
binadamu wanatengeneza
kemikali ambayo inaua kinga ya
mwili.Mhes….”
“Dr Mbeula samahani kwa
kukukatisha” Rais akasema
“Endelea mheshimiwa rais”
“Ninachotaka kusikia
kutoka kwako ni kama uwezo
wa kupambana na virusi hivyo
mnao.Kama unadhani hamna
uwezo nijulishe haraka ili
nimpeleke mwanangu nje ya
nchi kwa matibabu Zaidi kabla
hali yake haijawa mbaya”
akasema Dr Evans
“Mheshimiwa rais kwa
namna tunavyoendelea na zoezi
letu nina uhakika mkubwa
tutafanikiwa kuwafahamu
vyema virusi hawa na
kupambana nao lakini
haitakuwa kwa haraka”
“Una uhakika mtafanikiwa
Dr Mbeula?
“Ndiyo mheshimiwa rais
ninao uhakika.Naomba
uniamini”akajibu Dr Mbeula
“Vipi hali ya Coletha hivi
sasa anaendeleaje?akauliza Dr
Evans
“Hali yake inandelea vyema
mheshimiwa rais”
“Sawa Dr Mbeula.Nitakuja
baadae jioni kumjulia hali
mgonjwa.Naombeni mjitahidi
sana” akasema Dr Evans
“Tunajitahidi mheshimiwa
rais lakini bado kuna kitu
nataka kukifahamu” akasema
Dr Mbeula.
“Kitu gani Dr Mbeula?
akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa rais ninataka
kujua kama unafahamu kitu
chochote kuhusiana na virusi
hivi.Ninataka kufahamu chanzo
chake na kama kuna wagonjwa
wengine ambao
wameambukizwa virusi hivi”
akasema Dr Mbeula.
“Dr Mbeula kwa sasa
jielekezeni katika kutafuta
ufumbuzi wa kupambana na
virusi hao.Hayo masuala
mengine achana nayo
kwanza”akasema Dr Evans
wakaagana
“Olivia ! Olivia !! akasema
Dr Evans kwa hasira
“Ni Olivia aliyesababisa
haya yote.Kwa nini lakini
akanifanyia kitendo cha kikatili
namna hii?Kwa nini anataka
kumuangamiza mwanangu?
Nimemkosea nini hadi akaamua
kunifanyia hivi?Atapata faida
gani kama Coletha akipoteza
maisha? Ninaapa kama
mwanangu Coletha akifariki
dunia nitaiteketeza familia yake
yote bila kujali kama ni marafiki
zangu.Mwanangu hawezi
kupoteza maisha bila hatia
halafu nikae kimya!! Akawaza
Dr Evans na kumpigia simu
Kaiza
“Mheshimiwa rais”akasema
Kaiza
“Kaiza nipe habari.Nini
kinaendelea mpaka
sasa?akauliza Dr Evans kwa
ukali
“Mheshimiwa rais
tunaendelea kumtafuta Devotha
na tulifanikiwa kumfahamu mtu
ambaye angetupa taarifa
muhimu za kuweza kumpata
Devotha lakini kwa bahati
mbaya tumempoteza”
“Mmempoteza?! Dr Evans
akashangaa
“Tumempoteza
mheshimiwa rais.Aliwahi
kujirusha ghorofani kabla
hatujamkamata akafariki
dunia.Hivi sasa vijana
wanaendelea kupitia kompyuta
yake na ili kufahamu kama
wanaweza wakapata kitu
chochote kitakachopelekea
kumpata Devotha.Kwa sasa
nimefika hapa mahala alipo
Olivia ninataka kuendelea na
mahojiano naye”akasema Kaiza
“Kaiza tafadhali hakikisha
Olivia anafunguka na anasema
kila kitu.Ninakupa huu ni
mtihani wako wa mwisho
ukishindwa kumfungua
nitatafuta watu wengine
wanaoweza kuifanya hiyo kazi”
akasema Dr Evans
“Nitajitahidi kufanya kila
niwezalo kuhakikisha tunapata
kila taarifa kutoka kwa Olivia”
akasema Kaiza na rais akakata
simu kwa hasira
“Rais amepoteza kabisa
Imani na sisi kwa sababu ya
Olivia.Nikishindwa katika hili
hataniamini tena na aligusia
hata kuifutilia mbali idara
yetu.Natakiwa kumfanya
atuamini tena na hii
itawezekana kama tukimfungua
Olivia” akawaza Kaiza wakati
akishuka ndani ya gari.
NAIROBI KENYA
Ndege ya shirika la ndege la
Ethiopia iliwasili katika uwanja
wa ndeje wa Jomo Kenyatta
jijini Nairobi ikitokea Tel aviv
Israel kupitia Adis Abbaba
Ethiopia.Miongoni mwa abiria
wawili waliokuja na ndege hii ni
majasusi wawili wa shirika la
ujasusi la Israel Mossad,Fishel
na Ehud ambao walitumwa
nchini Kenya kwa kazi maalum.
Siku tatu zilizopita roketi
lililorushwa na wanamgambo
wa kipalestina wakishirikiana
na kikundi cha Islamic state
lilitua katika shule ya chekechea
na kusababisha vifo vya watoto
kumi na mbili.Shambulio hilo
lililolaaniwa kila kona ya dunia
lilimpelekea waziri mkuu wa
Israel aitishe kikao cha dharura
na wakuu wa shirika la ujasusi
la Israel Mossad.Katika kikao
hicho waziri mkuu alitaka
kufahamu namna Mossad
walivyojipanga kuwamakata
viongozi wakuu wa kikundi cha
IS ambacho kinashirikiana na
vikundi vingine vya
wanamgambo wa kipalestimna
kuendesha mashambulizi katika
ardhi ya Israel na kuua watu.
Mkurugenzi mkuu wa
Mossad alimueleza waziri mkuu
mikakati ya Mossad kuwa ni
kuwapata wafadhili wakuu wa
vikundi vile ambao ni Habiba
Jawad na Sayid Omar.Alimpa
taarifa za kuwepo kwa mtu
wanayemshikilia katika sehemu
ya siri nchini Kenya anaitwa
Edger Kaka ambaye ana
mahusiano na watu hao wawili
wanaowatafuta
sana.Alimkumbusha kuhusu
operesheni iliyofanyika nchini
Tanzania na Edger akatekwa.
“Baada ya kumteka nchini
Tanzania tulimpeleka Kenya
ambako tumemuhifadhi kwa
miaka mitatu sasa.Aliwahi
kuhojiwa na kutoa taarifa
chache lakini hazikusaidia
kuwapata Habiba Jawad na
Sayid Omar ambao
wameendelea kufadhili vikundi
vya kigaidi vinavyoendeleza
mauaji dhidi ya
waisrael.Tuliamua kumuacha
kwa muda mrefu bila kumuhoji
huku akiishi katika mateso na
upweke mkubwa ndani ya
chumba chenye giza na mateso
mengine ya kumuumiza kiakili
ili kumfanya awe tayari kutupa
taarifa zote za kuwahusu
Habiba na Sayid pale
tutakapoamua
kumuhoji.Naamini sasa ni muda
muafaka wa kumuhoji.Kwa
mateso aliyoyapata kwa miaka
mitatu atakuwa tayari
kuzungumza.”akasema mkuu
wa Mossad
Baada ya kikao kile ndipo
Fishel na Ehud wakatumwa
nchini Kenya kumfanyia
mahojiano Edger Kaka na
kuhakikisha anaeleza kila kitu.
Katika uwanja wa ndege wa
Jomo Kenyatta majasusi hao
walipokewa na afisa kutoka
ubalozi wa Israel nchini Kenya
wakaelekea moja kwa moja
katika hoteli walikoandaliwa
kufikia.Kutoka hotelini
wakachukuliwa na kupelekwa
hadi katika ubalozi wa Israel
nchini Kenya ambako Mossad
walikuwa na ofisi zao.
“Karibuni sana
Nairobi,karibuni sana
Afrika”akasema Avi mkuu wa
Mossad Afrika mashariki
“Tunashukuru sana
tumekaribia” akasema Ehud
“Nini kinachoendelea hapa
kuhusu Edger Kaka?akauliza
Fishel
“Edger yuko hapa ubalozini
kwa muda wa miaka mitatu
sasa na kwa muda huo
ameendelea kuishi katika
mateso bila kufanyiwa
mahojiano yoyote.Tumekuwa
tunamtesa kisaikolojia ili pale
tutakapoanza kumuhoji awe
ameteseka vya kutosha na
aeleze kila kitu.Watu kama
hawa wenye mahusiano na
magaidi kwa kawaida
wanakuwa wagumu mno
kufunguka na kutoa siri hivyo
mateso kama haya huwafanya
wawe tayari kusema kila kitu”
akasema Avi na kuwasha
runinga na mtu mmoja
aliyekuwa mtupu akiwa
amefungwa minyororo
mikononi na miguuni amelala
katika sakafu yenye baridi
akaonekana.
“Yule ndiye Edger
Kaka”Akasema Avi
“Haya ndiyo mateso
ambayo amekuwa akipewa kwa
miaka mitatu sasa.Amekuwa
akipewa chakula mara moja
kwa siku.Chumba alimo kuna
baridi na amekuwa akiishi
hivyo bila mavazi
yoyote.Kikubwa ambacho
tumekuwa tunakiwekea mkazo
mkubwa ni kuhakikisha hapati
magonjwa yoyote.Kila siku
daktari humkagua kujiridhisha
na maendeleo yake.Anaonekana
dhaifu lakini hana tatizo lolote
la kiafya” akasema Avi
Edger kaka alikuwa
amejikunyata katika pembe
akiwa amefungwa minyororo
mikononi na miguuni.Alikuwa
mtupu kabisa Alitia huruma
sana.Alikuwa ameota ndevu
nyingi na haikuwa rahisi
kutambulika kwa haraka.Ehud
akamtazama kwa makini na
kusema
“Kwa namna
anavyoonekana tayari
amekwisha kata tamaa”
“Hatua ya kwanza
tunayoanza nayo ni kumtoa
katika mateso aliyonayo sasa na
kumuweka katika maisha
mazuri.Anatakiwa anyolewe
nywele na ndevu aogeshwe na
avishwe mavazi mengine
mapya.Baada ya hapo
tutaendelea na hatua
inayofuata.Kitu kingine kabla ya
kuanza kumuhoji Edger
tunatakiwa kuifahamu historia
yake alikokotoka hadi hapa
alipofika.Naamini kwa muda
huu mrefu mtakuwa
mmekusanya taarifa za kutosha
za kumuhusu” akasema Ehud na
Avi akapiga simu akaomba
kutumiwa faili la Edger Kaka
katika ile ofisi
alimokuwemo.Baada ya
sekunde chache faili likatumwa
akatoka akawaacha akina Ehud
wakiendelea kupitia taarifa
zilizokuwa zimekusanywa
kuhusu Edger.
“Taarifa yake ni nzuri haina
hata chembe ya mashaka.Ni
mbunge aliyependwa
sana,amekuwa mstari wa mbele
kupambana na mafisadi.Ni
mbunge aliyejizoea umaarufu
mkubwa sana na ni mmoja wa
wanasiasa vijana waliokuwa
wanatajwa kufaa kushika nafasi
ya urais.Imetokeaje mtu kama
huyu akajiunga na kikundi cha
ugaidi?akauliza Fishel
“Hata mimi
inanishangaza.Sikujua kama
alikuwa mtu maarufu nchini
mwao kiasi cha watu kumtaja
hata kushika nafasi ya urais”
akasema Ehud
Edger Kaka alifunguliwa
minyororo akatolewa katika
kile chumba,hakuweza
kutembea akabebwa na
kupelekwa bafuni akaogeshwa
akanyolewa nywele na ndevu
halafu akavishwa mavazi
mengine mapya.Ngozi yake
ambao haikuonja hata tone la
mafuta kwa muda wa miaka
mitatu ilikuwa imekakamaa
hakuwa Edger yule
mtanashati.Alibadilika
mno.Hakuweza kutembea
akawekwa katika kiti cha
magurudumu akasukumwa
hadi katika chumba kimoja
kulikoandaliwa chakula
kizuri.Harufu nzuri ya vyakula
vilivyoandalia ilimsisimua sana
Edger ambaye hakuwa
ameisikia harufu nzuri kama ile
kwa muda mrefu.Alihisi njaa
kali alitamani akivamie chakula
kile akimalize chote lakini mwili
wake haukuwa na nguvu.Baada
ya dakika tatu wakaingia watu
wawili wakakaa mezani na
Edger akasogezwa karibu na
meza akashushwa kutoka
katika kiti kile cha
magurudumu na kuweka katika
kiti cha kulia chakula.Mikono
ilikuwa inamtetemeka alipoona
chakula kile kizuri.
“Edger karibu
chakula,tumia kadiri uwezavyo”
akasema Fishel na kumsogezea
Edger sahani na kumpakulia uji
mzuri katika bakuli.Edger
akajaribu kushika kijiko
akashindwa.Mikono haikuwa na
nguvu.Fishel akasohgeza kiti
akakaa karibu yake
akamnywesha uji ule hadi
bakuli lilipomalizika.Taratibu
Edger akaanza kuhisi mikono
inapata nguvu akaomba tena
chakula kingine.Fishel
akampakulia chakula
akaendelea kumlisha
sambamba na kumnywesha
kinywaji.Edger hakuamini kama
amekula tena chakula kile kizuri
ambacho hakuwa na matumaini
ya kukiweka tena katika ulimi
wake.Hakutaka kuacha alitaka
aendelee kula lakini Fishel
akamzuia akamtaka apumzike
kwanza.Edger akatolewa katika
kile chumba cha chakula
akapelekwa katika chumba
kingine kizuri chenye kitanda
kikubwa na godoro
zuri.Machozi yalimtoka
alipobebwa kutoka kwenye kiti
na kukalishwa kitandani.
“Siamini kama nimeweza
tena kulala katika godoro zuri
kubwa na laini.Sifahamu ni kwa
muda gani nimekaa katika kile
chumba chenye giza lakini
naamini ni muda
mrefu.Nimeteseka na kulala
mtupu katika sakafu yenye
baridi nikiteseka kwa njaa na
kiu.Nini kimetokea leo hadi
wakanitendea hivi?akajiuliza
Edger akiendelea kutiririkwa na
machozi.Taratibu akahisi
macho mazito na haukupita
muda akapitiwa na usingizi
akalala
“Nimemtazama machoni
anaonekana wazi amechoka na
mateso aliyoyapata.Hakuamini
alipoweka tena mdomoni
chakula kizuri.Naamini
tutakapoanza kumuhoji
atakuwa tayari kusema kila
kitu” akasema Ehud
“Ni mateso makubwa sana
miaka mitatu kukaa ndani ya
chumba chenye giza huoni
mwangaza wa jua.Naamini
hatakubali tena kurejea katika
mateso yale” akasema Fishel.
Edger aliachwa apumzike
katika kitanda kile kikubwa
akaamshwa na kupelekwa
katika chumba kingine ambamo
walikuwemo Fishel na Ehud
“Edger Karibu.Tumekutana
tena.Unajisikiaje?akauliza
Fishel
“Kwa sasa ninahisi nguvu
kidogo” akasema Edger kwa
sauti dhaifu ambayo haikuwa
inasikika vyema.
“Edger mimi na
mwenzangu tuna mazungumzo
kidogo nawe lakini kabla ya
kuzungumza nataka upumzike
kwa dakika kumi.Wakati
ukipumzika tunataka uangalie
filamu hii halafu tutarudi
kuzungumza” akasema
Fishel.Edger akashushwa
kutoka katika kile kiti cha
magurudumu akakalishwa
sofani.Fishel na Ehud wakatoka
wakamuacha peke yake.Baada
ya dakika tano toka Fishel na
Ehud watoke mle chumbani
akaingia mtu mmoja akamfunga
Edger kifaa Fulani mkononi
halafu akawasha runinga kisha
akatoka akamuacha Edger peke
yake ndani ya chumba.
“Ifuatayo ni historia fupi ya
mbunge Edger Kaka aliyefariki
katika ajali ya gari siku mbili
zilizopita” Ndivyo ilivyoanza
taarifa ile na kumstua mno
Edger.Alitamani kunyanyuka
lakini miguu haikuwa na
nguvu.Akabaki anashuhudia
picha zake mbali mbali
zikionyeshwa zilizoambatana
na historia yake.Mdomo ulibaki
wazi akishangaa
Wakati Edger akiendelea
kutazama taarifa ile
iliyohusiana na kifo na mazishi
yake Fishel na Ehud walikuwa
katika ofisi yao wakimfuatilia
Edger kwa makini kupitia
kamera.Pamoja nao alikuwepo
mtu mwingine aliyekuwa katika
kompyuta akiangalia grafu
iliyokuwa inapanda na kushuka
“Ameonyesha mstuko
mkubwa sana baada ya taarifa
kuanza.Inaonyesha hafahamu
chochote kilichotokea.Hajui
kama alikwisha fariki na
kuzikwa” akasema yule jamaa
aliyekuwa anafuatilia chati ile
katika kompyuta.Wakati Edger
akiendelea kutazama rekodi ile
runingani akionekana
kuchanganyikiwa mara
akapatwa na mstuko mkubwa
baada ya kumuona mwanadada
mmoja akiwa amevaa gauni
refu jeusi na kilemba cheusi
kichwani na macho yake
aliyafunika kwa miwani
mikubwa akiwa amesimama
katika mimbari akisoma
historia ya Edger
Kaka.Alishindwa kumalizia aya
ya mwisho akaangua kilio
akatokea mwanamke mmoja na
kwenda kumshika mkono
akamrejesha kitini kuketi.
“Olivia !! akasema Edger
Kaka akiwa ameyatumbua
macho.Alipatwa na mstuko
mkubwa sana
“Huyu mwanamke ni
nani?akauliza Fishel
“Huyu ni daktari wake
anaitwa Olivia Themba.Ndiye
aliyekuwa naye nchini
Israel”akajibu yule jamaa
aliyekuwa anafuatilia grafu
“Edger amestuka mno
baada ya kumuona Olivia.Grafu
imepanda hadi kupita kile
kiwango chake cha
kawaida.Kwa mstuko huu
lazima Olivia ni mtu muhimu
sana kwake”akasema yule
jamaa.Ehud na Fishel
waliendelea kumtazama Edger
mara wakastuka baada ya
Edger kuanguka
chini.Walisubiri kwa dakika
mbili kama atainuka lakini
aliendelea kulala pale
chini.Haraka haraka wakatoka
mbio na kwenda katika chumba
alimo Edger na kumkuta
amepoteza fahamu.Wakamtoa
ndani ya kile chumba na
kumuingiza katika chumba
kingine daktari akaitwa akafika
haraka na kumpima na
akawatoa wasiwasi kwamba
Edger hakuwa na tatizo bali
alipoteza fahamu kutokana na
mstuko.
“Ni mstuko uliopelekea
akapoteza fahamu lakini hana
tatizo lolote”akasema daktari.
Edger aliachwa katika
chumba chenye hewa ya
kutosha hadi
alipozinduka.Baada ya
kuzinduka akaachwa kwa muda
wa robo saa halafu akapelekwa
tena katika chumba kingine
walimo Fishel na Ehud
“Edger pole sana kwa
kilichotokea” akasema Fishel
aliyezungumza kwa upole
mkubwa
“Ninyi ni watu wakatili
sana.Kwa nini mmenifanyia
hivi? Kwa nini mmenionyesha
video ile?akauliza Edger
machozi yakimtoka.Bado sauti
yake ilikuwa dhaifu sana
“Jina lako nani?akauliza
Fishel
“Naitwa Edger Kaka”
“Edger unatokea wapi?
“Mimi ni mtanzania”
“Hapa ulipo unafahamu ni
wapi?
“Sifahamu niko
wapi.Maisha yangu yamekuwa
katika chumba chenye giza
nikisubiri Mungu aichukue roho
yangu lakini naye ameniacha
nikiteseka hataki kunichukua”
akasema Edger akionekana
kukata tamaa kabisa na maisha
yake
“Siku 1095,saa 26280 ndizo
ulizokaa humu ndani ambazo ni
sawa na miaka mitatu.Najua
hufahamu muda ambao umekaa
ndani ya kile chumba lakini ni
miaka mitatu sasa.Hiki ni
kipindi kirefu,mambo mengi
yamefanyika duniani.Binadamu
wa kwanza ametua katika
sayari ya Mars.Chaguzi nyingi
zimefanyika katika nchi mbali
mbali ikiwemo
Tanzania.Kikubwa kuliko yote
ulifariki ukazikwa na tayari jina
lako limesahaulika limebaki
katika kumbu kumbu kwamba
aliwahi kutokea mtu anaitwa
Edger Kaka” akasema Ehud
“Mimi sijafariki bado niko
hai.Kilichoonekana katika
filamu ile ni uongo
mkubwa.Mimi niko hai”
akasema Edger
“Video ile uliyoitazama
muda mfupi uliopita ambayo
imesababisha ukapoteza
fahamu imekuonyesha kila kitu
kwamba tayari umefariki dunia
na tayari umezikwa.Umeyaona
mazishi yako namna watu
walivyohuzunika kwa kifo
chako.Wengi walivaa fulana
zenye jina lako
wakikulilia,wakipita mbele ya
jeneza lako wakitoa salamu za
mwisho.Edger wewe tayari
umekwisha fariki”akasisitiza
Ehud
“Nashindwa
kuwaelewa.Kwa nini
mnanisisitiza kwamba
nimekufa wakati niko hai? Mimi
niko hai sijafa ! Mimi ni
binadamu si mzimu.Nini
kimefanyika hadi nionekane
nimekufa?akauliza Edger
“Edger tayari
umekufa.Naomba
nikukumbushe namna
ulivyopoteza maisha.Ulikuwa
unaelekea nyumbani kwako
ukitokea uwanja wa ndege wa
Julius Nyerere jijini Dar es
salaam.Ulikuwa umerejea
nchini kwako kutokea Israel
ulikoenda kwa matibabu.Muda
mfupi baada ya kuondoka
uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere msafara wako ulipata
ajali.Tayari umepata picha ya
kilichotokea?akauliza
Fishel.Edger akabaki kimya
“Edger unakumbuka
chochote kuhusiana na ajali
ile?akauliza Ehud
“Ndiyo nimekumbuka kila
kitu na kitu cha mwisho
ninachokumbuka ni kishindo
kikubwa na kukawa kiza
kinene.Sifahamu kama ilikuwa
ni ajali au nini lakini nilipokuja
kupata fahamu nilijikuta katika
chumba chenye giza nikiwa
nimefungwa minyororo na watu
wakaanza kunihoji kuhusu
kikundi cha IS.Nimeshangaa
kuona video ile watu wakinililia
eti nimekufa.Nimestuka sana
sikutegemea kitu kama hiki
ndiyo maana nikapoteza
fahamu.Nini kiliwekwa ndani ya
lile sanduku ili kuwaaminisha
watu kuwa nimekufa”akauliza
Edger
“Edger ulifariki usiku ule na
tayari umekwisha zikwa na hili
hapa ni kaburi lako” akasema
Ehud akatoa picha katika faili
akamuonyesha Edger
akaitazama huku mikono
ikimtetemeka
“Haya mambo nashindwa
kuyaelewa.Kwa nini
nimefanyiwa hivi?kwa nini
mmeniteka na kunizushia kifo
wakati niko hai?Mwili ule
ambao ulizikwa ndani ya jeneza
linalodaiwa ni la kwangui ni
mwili wa nani?akauliza Edger
“Sikiliza Edger.Katika siku
1095 waisrael 59 wamepoteza
maisha.Kumekuwa na
urushwaji wa maroketi kutokea
upande wa Palestina
kunakofanywa na vikundi vya
wanamgambo wa kipalestina
wakisaidiwa na kikundi cha
kigaidi cha IS.Siku tatu
zilizopita roketi limerushwa na
kutua katika shule ya watoto
wadogo na kuua idadi kubwa ya
watoto.Matendo kama haya ya
kikatili yanayofanywa na
wanamgambo wa kipalestina
wakisaidiwa na kikundi cha
kigaidi cha IS yameendelea
kushika kasi kutokana vikundi
hivi kuwezeshwa kwa fedha na
silaha hivyo kuwa na uwezo wa
kujipanga na kufanya
mashambulio katika ardhi ya
Israel.Baada ya uchunguzi wa
kina imebainika kwamba
mfadhili mkubwa wa vikundi
hivi anaitwa Habiba
Jawad.Huyu ni mwanamke
tajiri.Aliwahi kuolewa na
mwanaume tajiri ambaye
alikuwa na asili ya Palestina na
aliutumia utajiri wake kufadhili
makundi ya wanamgambo kuua
waisrael na ndipo vikosi vya
Israel vilipompiga risasi
akafariki.Habiba Jawad alirithi
utajiri wa mumewe na
akaendelea kufadhili vikundi
vya kigaidi.Ili asigundulike
kuwa ni yeye anayefadhili
vikundi hivi anamtumia mtu
anaitwa Sayid Omar.Kwa muda
mrefu Habiba na Sayid
wamekuwa wakitafutwa sana
na serikali ya Israel lakini
hawajapatikana hadi
sasa.Wamekuwa wakisaidiwa
na serikali ya Saudi Arabia
kujificha” Fishel akasema na
kumtazama Edger kwa muda
halafu akaendelea
“Ukiwa hospitalini nchini
Israel ulitembelewa na watu
wawili ambao ni Habiba Jawad
na Sayid Omar ukaonana nao
mkazungumza.Kitendo cha
Habiba Jawad na Sayid Omar
kuhatarisha maisha yao kwa
kuingia katika ardhi ya Israel
wanakotafutwa sana kwa lengo
moja tu la kuja kuonana nawe ni
kiashiria tosha kuwa wewe ni
mtu muhimu sana
kwao.Ukaribu wako na Habiba
na Sayid unakufanya uwe mtu
wetu muhimu sana ndiyo
maana uko hapa kwa miaka
mitatu sasa na yawezekana
ukaendelea kuishi hapa kwa
miaka mingi Zaidi yawezekana
hadi mwisho wa uhai wako
kwani katika ulimwengu wa
kawaida tayari
umefariki,umezikwa na
umesahaulika.Jina lako limebaki
historia.Hakuna anayekutafuta
tena.Tumekuacha kwa miaka
mitatu bila kukuuliza chochote
ili kukuonyesha kwamba
tunaweza kukuacha ukateseka
hadi siku utakapopoteza maisha
yako.Siku ya leo tumekutoa
katika chumba cha giza na
tumekurejesha katika maisha ya
kawaida japo kwa muda mfupi
kukumbusha kwamba unayo
nafasi ya kurejea katika maisha
yako ya kawaida.Bado unayo
nafasi Edger ni juu yako
kuitumia”Fishel akanyamaza
tena akamtazama na kusema
“Edger historia yako
inaonyesha wewe uliwahi kuwa
mbunge wa bunge la jamhuri ya
muungano wa Tanzania ukiwa
ni mbunge mwenye umaarufu
mkubwa.Ulikuwa kinara wa
kupambana na ufisadi na
kutokana na juhudi zako katika
kuwapigania na kuwasemea
wanyonge walianza kukutaja
kuwa ni mmoja wa watu
wanaofaa hata kupewa nafasi
ya kuongoza nchi.Nyota yako
tayari ilikwisha anza kung’ara
lakini hukuweza kutimiza
malengo yako na ukajikuta
mahala hapa ambako kumezima
ndoto zako zote.Edger
tumekufungulia dirisha dogo
ambalo unaweza ukalitumia
kutoka na kurejea katika
maisha yako ya awali.Uchaguzi
ni wako mwenyewe kama utoke
kupitia nafasi hii uliyoipata au
uendelee kubaki hapa kwa
maisha yako yote ukiendelea
kuteseka hadi pale roho yako
itakapokutoka.Kipi
unakichagua?Kutoka au
kuendelea kukaa katika chumba
kile cha giza?Kumbuka hakuna
mtu yeyote anayefahamu kuwa
uko hai au uko hapa hivyo
mwenye kuamua hatima ya
maisha yako ni wewe
mwenyewe” akasema
Fishel.Edger akainamisha
kichwa akatafakari kwa muda
halafu akasema
“Nimechoka na mateso
haya.Mmenitesa vya kutosha
sitaki kurejea tena katika kile
chumba.Niambieni nini
mnakitaka ili kuniondoa katika
mateso haya na kunirejeshea
maisha yangu ya
uhuru?akauliza Edger
“Umefanya uchaguzi
mzuri.Huo ni uamuzi wa busara
sana.Nataka unijibu
unawafahamu Habiba Jawad na
Sayid Omar? Akauliza Ehud
“Ndiyo ninawafahamu”
akajibu Edger
“Tunataka utupe taarifa
ambazo zitatusaidia kuwapata
watu hawa wawili.Habiba
Jawad na Sayid Omar
wanaendelea kufadhili vikundi
vya wanamgambo wa
kipalestina ambao wanafanya
mauaji dhidi ya waisrael.Ni hilo
tu ambalo tunalihitaji na kama
ukitusaidia tukawapata watu
hao nakuhakikishia kwamba
tutakurejeshea maisha
yako.Tutakuachia huru na
tutakupa pia ulinzi mkubwa
pamoja na kukupeleka ukaishi
mahala ambako utakuwa
salama salimini na utaendesha
maisha yako kimya kimya.Uko
tayari kutueleza
ukweli?akauliza Fishel.Edger
akavuta pumzi ndefu
akainamisha kichwa akazama
mawazoni.Fishel na Ehud
wakamuacha atafakari.Zilipita
dakika tatu Edger akainua
kichwa na kusema
“Nimekaa katika chumba
cha giza kwa miaka mitatu na
sielewi chochote
kinachoendelea huko duniani
hivyo ni ngumu sana kwangu
kujua mahala waliko Habiba
Jawad au Sayid” akasema Edger
“Wote wawili walikuja
kukutembelea hospitali nchini
Israel.Una mahusiano gani
nao?akauliza Ehud
“Sina mahusiano yoyote
nao” akajibu Edger
“Kama huna mhusiano nao
kwa nini walikuja
kukutembelea hospitali mara
mbili?akauliza Fishel
“Sikuwa nikifahamiana na
Habiba au Sayid Omar hadi
walipokuja kunitembelea
hospitali.Kilichowaleta hospitali
walitaka niwasaidie kufanikisha
mradi wao wa kuanzisha
kampuni ya mafuta nchini
Tanzania”
“Habiba Jawad na Sayid ni
watu ambao wanatafutwa na
serikali ya Israel lakini
hawakuhofia usalama wao na
wakaingia Israel kwa sababu
moja tu ya kuja kukuona
hospitali.kwa nini wewe na
asiwe mtu mwingine?akauliza
Fishel
“Walipataje taarifa za wewe
kulazwa hospitali Israel?
akauliza Ehud
“Sifahamu walipataje
taarifa zangu na sielewi kwa
nini walinichagua mimi” akajibu
Edger
“Edger hiki unachokieleza
tunajua ni uongo
mtupu.Tunajua unawafahamu
vyema Habiba na Sayid na
hospitali pale haikuwa mara ya
kwanza kuonana.Edger tambua
hapa tunazungumzia maisha ya
waisrael wanaoendelea kuuawa
kila siku,maisha ya wapalestina
ambao wanaendelea kuuawa
kutokana na vurugu
zinazosababishwa na
wanamgambo wa kipalestina
wanaofadhiliwa na akina
Habiba.Vile vile tunazungumzia
hatima ya maisha yako.Najua
unafahamu kila kitu kuhusu
Habiba na Sayid lakini
unaogopa
kusema.Nakuhakikishia Edger
unakosea sana kwani hao
unaojaribu kuwaficha hawana
msaada tena kwako.Tayari
wanajua umefariki na
wamekwisha kusahau.Hakuna
ambaye atakusaidia kukuondoa
mahala hapa.Hatima ya maisha
yako utaiamua wewe
mwenyewe.Tupe kile
tunachokitaka tuokoe maisha
ya watu wetu na sisi
tukurejeshee maisha yako
mazuri.Tunajua kile
utakachotueleza kina gharama
hivyo tuko tayari kutoa malipo
ambayo ni kukusaidia kuanza
maisha mapya.Hii ni nafasi
pekee umeipata na hautaipata
tena nafasi nyingine kama hii
hivyo ukishindwa kuamua leo
utarudishwa tena katika kile
chumba na huo utakuwa ni
mwisho wako” akasema Fishel
“Sipendi kukaa katika
chumba kile nimechoka na
mateso haya ninayoyapata
lakini sina chochote cha
kuwaeleza kuhusu Habiba au
Sayid Omar.Nilichowaeleza ni
ukweli mtupu siwafahamu watu
hawa na mara yangu ya kwanza
kukutana nao ilikuwa ni
hospitali kabla ya hapo
sikuwahi kuonana
nao.Tulipanga kuwasiliana nao
baada ya kufika Tanzania ili
kuwasaidia kwa taratibu za
kuanzisha kampuni ya
mafuta.Habiba alinieleza
kwamba ana visima vya
mafuta.Hakuwahi kunipa
maelezo yoyote kuhusu yeye
wala mahala anakoishi hivyo
sifahamu chochote.Naombeni
mniamini ndugu
zangu.Mnanitesa bure bila kosa
mkinihusisha na watu
nisiowafahamu” akasema Edger
na kwa mbali macho yake
yakalengwa na machozi
“Edger macho yako ingawa
yanalengwa machozi lakini
yanaonyesha wazi
unadanganya.Kwa nini
unakubali kuteseka kwa ajili ya
watu ambao hawatakuwa na
msaada kwako? Kwa nini
unawaficha watu ambao
wanajua umekwisha fariki?
Hakuna yeyote katika dunia hii
ambaye atakusaidia.Uko peke
yako hivyo jiokoe
mwenyewe.Sahau kuhusu
Habiba,Sayid au IS hakuna
ambaye atakuja hapa
kukuokoa.Edger narudia tena
kukuhakikishia kwamba
endapo ukiamua kushirikiana
nasi tutakulinda dhidi ya
IS.Serikali ya Israel itakusaidia
uweze kupata sehemu salama
ya kuishi ambako utaanza upya
maisha yako.Taarifa
utakazotupa ni muhimu sana na
ambazo zitasaidia kuokoa
maisha ya watu wengi hivyo
lazima na sisi tuhakikishe
unakuwa na maisha mazuri
wewe na wale uwapendao”
akasema Ehud.Walimpa tena
Edger nafasi ya kutafakari kisha
akasema
“Natamani sana kupata
nafasi nyingine ya kuishi
maisha mazuri yenye furaha na
amani lakini sintaweza
kuyapata maisha hayo kwa
kuwa sifahamu chochote
kuhusu Habiba Jawad au
mtandao wa IS.Laiti
ningefahamu kitu chochote hata
kidogo cha kuweza kusaidia
kuwapata watu hao
ningewaeleza lakini sina
chochote cha kuwasaidia”
“Uko tayari kurejea tena
katika kile chumba cha giza
kuendelea na mateso? akauliza
Fishel lakini Edger hakujibu
akabaki kimya
“Edger nimekuuliza hivyo
kwa sababu hii ni mara yako ya
mwisho utaipata nafasi kama
hii,kama hautaitumia vyema
hakuna tena dirisha lolote
litakalofunguliwa kukuruhusu
upite.Itumie vyema nafasi hii
kujiondoa kutoka katika mateso
haya.Narudia tena
kukuhakikishia kwamba watu
hao ambao unawaficha na
hutaki kutupa taarifa zao
hawana msaada wowote
kwako.Wakati wewe unateseka
kwa miaka mitatu ndani ya
chumba cha giza wao
wanaendelea na maisha yao
mazuri ya kifahari,wanakula
vizuri wanalala sehemu nzuri
wanasafiri kwa magari ya
kifahari na wanapata kila
wanachokihitaji kwenye maisha
yao.Wewe uko katika chumba
ambacho hakina mwangaza
ukilala katika sakafu yenye
baridi tena ukiwa
mtupu,ukipata chakula kidogo
mara moja kwa siku huku
ukinateseka kwa kiu.Si
Habiba,Sayid au IS wanafahamu
ni mateso gani unayapitia.Edger
nakukumbusha tena uko peke
yako hivyo jisaidie wewe
mwenyewe” akasema Ehud
“Naridia tena
kukuhakikishia kwamba
utakuwa na maisha mazuri
ukitoka hapa,utaishi katika
nyumba nzuri,gari zuri la
kifahari na utapata kila
unachokihitaji.Kama kuna kitu
kingine chochote unataka
tukupatie ili utupe taarifa za
Habiba na Sayid tueleze.Sisi
tukohapa kwa niaba ya serikali
hivyo chochote utakachokitaka
utakipata” akasema
Fishel.Edger akafikiri na
kusema
“Ninataka kurejea tena
katika kile chumba changu cha
giza nikaendelee na
mateso,sihitaji kitu kingine
chochote” akasema Edger
.Fishel na Ehud
wakatazamana.Hawakutegemea
jibu lile
“Edger unalifunga dirisha
ambalo halitafunguliwa
tena.Tumekupa nafasi ya
kuchagua wewe mwenyewe
aina ya maisha unayotaka
kuishi na kama ukichagua
kurudi katika kile chumba cha
giza sisi hatuna kipingamizi
tutakurejesha lakini fahamu
kuwa hakuna tena nafasi
nyingine itakayofunguliwa
kwako” akasema Ehud
“Nirejesheni nikaendelee
kuteseka” akasema Edger.
“Edger kabla ya
kukurejesha tena katika
chumba kile kuna kitu nataka
ukifahamu” akasema Fishel na
kufungua faili akatoa picha
akamuonyesha Edger ambaye
sura yake ilibadilika baada ya
kuiona picha ile.
“Unamfahamu
huyu?akauliza
“Ndiyo.Huyu ni Olivia
Themba daktari wangu ambaye
aliyaokoa maisha yangu
nilipotaka kuuawa kwa sumu”
akajibu Edger
“Kila unapoiona picha yake
unastuka sana.Kuna nini
kinaendelea kati yenu?akauliza
Ehud
“Huyu mtu mwenye
umuhimu mkubwa kwangu.Bila
yeye hivi sasa tayari
ningekwisha fariki na hata ninyi
msingep[ata nafasi ya
kunitesa.Watu walitaka nifariki
dunia lakini yeye alipambana
akayaokoa maisha yangu hivyo
nitaendelea kumshukuru hadi
mwisho wa maisha yangu”
akasema Edger
“Kwa namna
unavyomuangalia Olivia
inaonyesha wazi kuna jambo
linaendelea zaidi ya urafiki wa
kawaida.Unampenda
Olivia?Fishel akauliza
“Olivia ni rafiki
yangu”akajibu Edger
“Jibu swali
unampenda?akauliza Ehud
Edger akawa kimya
“Naomba nikupe taarifa
kwamba Olivia ametekwa na
watu wasiojulikana siku mbili
zilizopita na mpaka leo hii
hajulikani mahala alipo”
akasema Fishel
Mstuko mkubwa
ulionekana usoni kwa Edger.
“Mstuko mkubwa ulioupata
unaonyesha jinsi gani Olivia
alivyo muhimu kwako”
akasema Fishel na
kumuonyehsa Edger taarifa
mbali mbali za kuhusiana na
tukio la kutekwa Olivia kupitia
kompyuta yake.
“Nani wamemteka
Olivia?akauliza Edger
“Edger ni vipi kama
tukikusaidia ukakutana tena na
Olivia na ikiwezekana
mkaanzisha maisha yenu
sehemu tulivu ambako hakuna
atakayewasumbua?akauliza
Fishel.Edger akaitazama tena ile
picha
Ya Olivia.
“Mnao uhakika wa
kumuokoa Olivia kutoka kwa
watekaji?akauliza Edger
“Sisi tuna mtandao mkubwa
na tunaweza kukusaidia
kumpata Olivia na
tukakukutanisha naye tena”
akasema Fishel
“Tafadhali kama mnao
uwezo wa kumuokoa Olivia
fanyeni hivyo.Ni mwanamke wa
kipekee kabisa ambaye huwezi
kumfananisha na wengine na
hastahili kufanyiwa kitendo hiki
alichofanyiwa” akasema Edger
“Edger tunaweza
kumuokoa Olivia kwa vile wewe
umetutuma tufanye hivyo lakini
kabla ya kuandaa operesheni ya
kumtafuta Olivia tunataka
kufahamu kwa nini unataka
tumuokoe?Ni kwa sababu
alikusaidia kuokoa maisha yako
au kuna sababu nyingine?Tupe
sababu ya msingi ili tuone uzito
wake”Akauliza Ehud
“Olivia ni mwanamke
nimpendaye kuliko
wote.Sijawahi kupenda
mwanamke kama
ninavyompenda Olivia”
akasema Edger
“Ulipotoweka tayari
mlikuwa wapenzi?
“Sikuwa nikimfahamu
Olivia hadi nilipofumbua macho
na kujikuta hospitali nchini
Israel na ndipo nilipomuona
Olivia kwa mara ya
kwanza.Nilimpenda sekunde ya
kwanza nilipomtia
machoni.Nilimueleza hisia
zangu na tulikubaliana kulipa
suala hilo nafasi ya kutosha
tutakaporejea nyumbani kwa
bahati mbaya hilo halikutokea
tena mlinichukua na kunileta
hapa sikumuona tena Olivia
hadi nilipomuona leo katika ile
filamu.Ninampenda Olivia
tafadhali muokoeni kama
uwezo mnao”
“Ahsante kwa kutueleza
ukweli.Tutakusaidia katika
hilo.Tutakwenda Tanzania
kumtafuta Oliviana lakini kabla
ya kufanya hivyo na sisi
tutaomba utueleze kuhusiana
na Habiba Jawad na Sayid
Omar” akasema Fishel
“Nitawaeleza kila kitu pale
nitakapomuona Olivia mbele ya
macho yangu”akasema Edger
“Usihofu Edger sisi
tunakwenda kumtafuta Olivia
na tuna uhakika wa kumpata
lakini kabla hatujaingia katika
operesheni hiyo nataka kwanza
utupe maelezo kuhusu Habiba
na Sayid Omar ni jinsi gani
tutaweza kuwapata?
“Nimewaambia nitawaeleza
kila kitu lakini hadi hapo
nitakapomuona Olivia mbele ya
macho yangu niishike mikono
yake na kuhakikisha kweli ni
yeye mwanamke nimpendaye”
akasema Edger
“Sawa Edger tunakwenda
kufanya operesheni katika nchi
ya watu na kumchukua raia wa
nchi nyingine bila ruhusa au
kibali cha mamlaka husika,hili
ni jambo kubwa sana hivyo
kabla hatujafanya hivyo
tunataka kupata uhakika kuwa
hiki tunachokwenda kukifanya
kina manufaa kwetu”
“Awali uliniambia kwamba
nichague kitu chochote
ninachokitaka kutoka kwenu ili
niweze kuwapa taarifa
mnazozihitaji.Ninachokihitaji ni
kumpata OIlivia Themba na
nitawaeleza kila kitu
mnachokihitaji.Kingine nataka
mniandalie nyumba mahala
ambako nitaishi na Olivia kwa
amani” akasema Edger
“Sawa Edger.Tutafanya
kama unavyotaka.Tutamleta
Olivia mbele ya macho yako
lakini kama hautakuwa tayari
kutueleza kile tunachokitaka
utakuwa umemuweka Olivia
katika matatizo makubwa
kwani hautamuona tena na kwa
kuwa atakuwa ameifahamu siri
hii na yeye pia atafungwa katika
chumba cha giza kwa maisha
yake yote.Nataka uwe na
uhakika kuwa utatupa taarifa
zote za kuwahusu Habiba Jawad
na Sayid Omar kabla
hayujamleta Olivia” akasema
Fishel
“Naombeni mniamni
nitawaeleza kila kitu pale
nitakapomuona Olivia mbele
yangu.Kwa ajili yake niko tayari
kuweka kila kitu bayana hivyo
hakikisheni mnafanya kila
mnaloweza kumpata
Olivia.Aliyaokoa maisha yangu
na sasa ni zamu yangu
kuyaokoa maisha yake”
akasema Edger
“Sawa Edger nimeyapokea
maneno yako na sisi tutafanya
kila lililo ndani ya uwezo wetu
kuhakikisha tunampata Olivia
lakini ukumbuke
nilivyokueleza.Kama ukienda
kinyume na makubaliano yetu
utakuwa umempoteza pia Olivia
kwani hautamuona tena na
utakuwa umemsababishia
mateso makubwa” akasema
Fishel
“Msiwe na wasiwasi na
mimi.Nitawaeleza kila kitu
nikimuona Olivia” akasema
Edger.
“Vizuri.Kwa kuwa
umetuhakikishia kwamba uko
tayari kuzungumza na
kutueleza ukweli wote
hatutakurejesha tena katika kile
chumba cha giza utaendelea
kuishi maisha mazuri katika
chumba kipya ukipata kila
unachokihitaji” akasema Ehud
kisha wakamuita Avi na kumpa
maelekezo kwamba Edger
aendelee kuishi maisha mazuri
katika kile chumba kipya
asiendelee tena na mateso
Fishel na Ehud wakarejea
katika ofisi yao kujadiliana
kuhusiana na kile walichokipata
kutoka kwa Edger
“Hatimaye Edger amekubali
kueleza ukweli wote kama
akimuona Olivia.Ninaiona
nguvu ya mwanamke.Kikubwa
sasa ni namna ya kumpata huyo
Olivia.Nani kamteka na kwa
nini? Akauliza Fishel
“Fishel japo tumemuahidi
Edger kwamba tunao uwezo wa
kumpata Olivia lakini si jambo
rahisi hata kidogo.Hatujui hata
tuanzie wapi” akasema Ehud
“Ehud hilo lisikupe
shida.Tulichokuwa tunakitafuta
ni kupata taarifa kutoka kwa
Edger ambaye amekubali
kueleza kila kitu lakini hadi
atakapomuona Olivia hivyo ni
jukumu letu kuhakikisha
tunampata Olivia.Tunakwenda
Tanzania na tutahakikisha
tunampata Olivia” akasema
Fishel
“Fishel kwa mtazamo
wangu tumetengeneza
operesheni mpya ambayo
haikuwa na
ulazima.Tungetumia nguvu
tungeweza kupata taarifa zote
kutoka kwa Edger bila
kulazimika kuingia tena katika
operesheni nyingine.Tayari
amekwisha choshwa na mateso
yale na lazima angefunguka”
akasema Ehud
“Kuna siri kubwa ambayo
Edger anaificha hapa na ndiyo
maana alikubali kurejea tena
katika kile chumba akaendelea
kuteseka kuliko kuisema na
hata kama tungetumia nguvu ya
kiasi gani asingeweza kusema
chochote.Ameteseka kwa miaka
mitatu lakini ameona ni bora
arudi tena katika mateso
akaendelee kuteseka kuliko
kusema chochote hadi
tulipomgusia Olivia ndipo
akawa tayari kufunguka.Nina
uhakika mkubwa sana
tukimleta Olivia atafunguka na
atatueleza kila kitu” akasema
Fishel
“Una uhakika atatueleza au
atakuwa anacheza na akili zetu?
“Atafunguka.Niamini mimi”
akasema Fishel
“Fishel bado moyo wangu
unakuwa mgumu sana katika
suala hili kwani litatuingiza
tena gharama za kufanya
operesheni katika nchi nyingine
na hatuna uhakika kama
tutampata Olivia kama
ulivyomuahidi Edger” akasema
Ehud
“Ehud kwa ajili ya taifa
teule la Israel kila kitu
kinawezekana.Lazima tufanye
kila linalowezekana
kuhakikisha taifa teule
linakuwa salama.Tutaingia
Tanzania na kumtafuta Olivia
tutamleta hapa ili Edger aweze
kutueleza mahala alipo Habiba
Jawad na Sayid Omar ambao
kwa kutumia fedha zao
wanaendelea kufadhili vikundi
vya wana mgambo ambavyo
vinaendesha mauaji dhidi ya
waisrael” akasema Fishel na
kutazama na Ehud kwa muda
halafu akasema
“Tuwasiliane na makao
makuu tuwajulishe kuhusu
suala hili” akasema Fishel na
kuomba waunganishwe na
makao makuu baada ya muda
mkurugenzi mkuu wa Mossad
akawa hewani
“Fishel habari za
Nairobi?Nimeambiwa mnataka
kuzungumza nami.Kuna kitu
gani kinaendelea huko?Kuna
chochote mmeshakipata kutoka
kwa yule jamaa?akauliza
mkurugenzi
“Mkurugenzi tumefika
salama kabisa Nairobi na bila
kuchelewa tumeanza kazi
iliyotuleta hapa.Tumemtoa
Edger katika chumba cha giza
na kumrejesha katika maisha
mazuri kisha tukaanza
kuhojiana naye.Alikana
kuwafahamu Habiba Jawad na
Sayid Omar na akatuomba
tumrejeshe katika chumba cha
giza akaendelee
kuteseka.Hakuwa tayari
kusema lolote hadi
tulipomuonyesha picha ya
mwanamke mmoja anaitwa
Olivia.Huyo mwanamke ni
daktari ambaye ndiye
aliyeyaokoa maisha yake kwa
kumpeleka Israel baada ya
kupewa sumu.Edger amekiri
kumpenda Olivia na ameahidi
kutueleza kila kitu tunachohitaji
kama tukimkutanisha tena na
Olivia” akasema Fishel
“Hiyo ni hatua nzuri
sana.Kama amekubali kueleza
kila kitu endapo atampata huyo
mwanamke ni jambo zuri
sana.Huyo mwanamke
anapatikana wapi?akauliza
mkurugenzi
“Mkurugenzi hapa kuna
tatizo kidogo.Huyo mwanamke
anapatikana nchini Tanzania”
“Tanzania ni karibu sana na
Kenya na tuna ubalozi wetu
pale hivyo kumpata huyo
mwanamke itakuwa kazi
nyepesi.Tutatuma timu ya watu
kwenda kumtafuta na kumleta
Nairobi.Mossad tunao utajiri
mkubwa wa majasusi mahiri”
akasema mkurugenzi
“Tatizo lililopo mkurugenzi
ni kwamba mwanamke huyo
ametekwa nyara siku mbili
zilizopita na watu wasiojulikana
na hadi leo hii bado
hajapatikana”
“Ametekwa?!!
“Ndiyo
mkurugenzi.Ametekwa nyara
na watu wasiojulikana”akajibu
Fishel
“Pamoja na kutekwa nyara
lakini bado ni mtu wa muhimu
kwetu.Edger anazo taarifa nyeti
sana tunazozihitaji hivyo ni
jukumu letu kuhakikisha
tunampata huyo
Olivia.Tutatuma majasusi
wetukwenda Tanzania
kumtafuta Olivia lakini kabla ya
kutuma kikosi cha majasusi
Tanzania ninataka wewe na
Ehud mtangulie
Tanzania.Nitatoa maelekezo
kwa balozi wetu ili muweze
kupatiwa kila msaada
mnaouhitaji mkiwa
Tanzania.Nataka mkafanye
uchunguzi wa tukio hilo la
kutekwa kwa Olivia na kisha
mnipe taarifa haraka namna
gani tunaweza kufanya yetu ya
kumtafuta na kumpata
Olivia.Naombeni mlipe uzito
suala hili muhimu
mno.Maroketi yanaendelea
kurushwa katika ardhi ya Israel
na ili kuwadhibiti wanamgambo
hao wanaofanya mashambulio
haya lazima tukate mrija
unaowaunganisha na kisima
cha fedha kwa kuwakamata
Habiba na Sayid.Tuwasiliane
mtakapofika Tanzania”
akasema mkurugenzi na kukata
simu.Fishel na Ehud
wakatazamana
“Fishel tumenunua kazi
nyingine ambayo haikuwa na
ulazima wowote.” akasema
Ehud
“Ehud nini hasa tatizo
lako?Unaonekana hujafurahia
kabisa suala la kumtafuta Olivia
ili Edger aweze kutupa taarifa
muhimu” akasema Fishel
“Ni kweli sijafurahishwa na
jambo hili.Tulikuja hapa
kumfanya Edger afunguke na
atupe taarifa zile muhimu sana
tunazozihitaji lakini
mwenzangu umekuwa mwepesi
sana kukubali matakwa
yake”akasema Ehud
“Ehud hakuna ambacho
tungekipata kwa Edger,yuko
tayari kuendelea kuteseka
kuliko kueleza chochote.Hata
kama tungetumia nguvu
kumtesa tungeweza kumuua
kabla ya kupata chochote toka
kwake kwani afya yake ni
dhaifu mno.Lakini baada ya
kumgusia kuhusu Olivia
amekubali kutueleza kila kitu
kama tukimleta Olivia,huoni
kama hayo ni mafanikio
makubwa Ehud” akasema
Fishel.
“Japokuwa mkurugenzi
ameridhia lakini binafsi
sijapendezwa na hili jambo”
akasema Ehud
“Ehud nakufahamu wewe
unapenda matumizi ya nguvu
lakini kwa hali aliyonayo Edger
hatuwezi kutumia
nguvu.Tutatumia nguvu
kumsaka Olivia na kisha
tutapata taarifa nyeti toka kwa
Edger.Haya tayari ni maelekezo
tumepewa hatuna haja ya
kuendeleza mjadala
kinachotakiwa kwa sasa ni
kuanza kujiandaa kuelekea
Tanzania.Twende tukaonane na
balozi kwa ajili ya maandalizi ya
kuelekea Tanzania” akasema
Fishel.
TANZANIA..
Hali ya Olivia Themba
iliendelea kuwa mbaya kadiri
muda ulivyozidi
kusonga.Hakuwa na fahamu.Hii
ilitokana na mateso makali
aliyopewa na Kaiza akiwa na
watu wake.Dr Alex alikuwa
amefungwa katika kiti pembeni
akishuhudia Olivia alivyokuwa
akiteswa baada ya kutokea
mzozo kati yake na Kaiza
kuhusiana na mateso aliyokuwa
akimpa Olivia.Pamoja na
jitihada zote za Kaiza lakini
hakuweza kupata chochote
kutoka kwa
Olivia.Alichanganyikiwa kwani
tayari kiza kiliingia na hakuwa
amekamilisha kazi aliyopewa
na rais.Akamgeukia Dr Alex
“Dr Alex unatakiwa ufanye
kila linalowezekana
kumuamsha Olivia.Lazima
afunguke.lazima aseme kila kitu
leo!! Akasema Kaiza kwa ukali
“Siwezi Kaiza.Siwezi
kufanya chochote
tena.Umekataa kusikia ushauri
wangu na hayo ndiyo matokeo
yake.Olivia is going to die and
you’ll get nothing !! Ungenisikia
ushauri wangu usingefika hapa
ulipofika.Sina chochote cha
kukusaidia kwa sasa.Let her
die!! Akasema Dr Alex maneno
yaliyompandisha hasira Kaiza
akamrukia Dr Alex teke zito la
kifua lililompeleka
chini.Akaenda ukutani na
kupiga ukuta kwa mikono yake
alipandwa na hasira.Akageuka
kumtazama Olivia hali yake
bado haikuwa nzuri.
“Dah ! nitafanya nini?Hali
ya Olivia ni mbaya na huyu
daktari amegoma kufanya
chochote.Lazima nitafute
msaada siwezi kumuacha Olivia
akafariki kwani ni my muhimu
sana kwetu” akawaza Kaiza
akatoka ndani ya kile chumba
na kumpigia simu Dr Evans
“Kaiza naamini tayari zoezi
limekamilika” akasema Dr Alex
mara tu alipopokea simu
“Mheshimiwa rais”akasema
Kaiza
“Nini Kaiza?akauliza Dr
Evans
“Zoezi halijafanikiwa
mheshimiwa rais.Mpaka sasa
hatujafanikiwa kupata chochote
kutoka kwa Olivia.Nimetumia
kila aina ya mateso lakini
hajafungua mdomo wake
kusema chochote na kwa bahati
mbaya hali yake imebadilika
ghafla hana fahamu nina
wasiwasi anaweza akapoteza
maisha muda wowote”
“What?! Akauliza Dr Evans
kwa mstuko
“Ndiyo mheshimiwa
rais,hali yake si nzuri hata
kidogo”
“Kaiza don’t let her die !!
Umenisikia?
“Mheshimiwa rais..”
“Sikiliza Kaiza,nimetoka
hospitali kumtazama
mwanangu Coletha na hali yake
si nzuri hata kidogo.Madaktari
wanahangaika kutafuta tiba
lakini mpaka sasa
hawajafanikiwa.Mwenye
kuifahamu tiba ya mwanangu ni
Olivia pekee ambaye ndiye
aliyetengeneza virusi
vinavyomtesa mwanangu.Kwa
namna yoyote ile Olivia
hatakiwi kufa bado namuhitaji
sana” akasema Dr Evans
“Mheshimiwa rais….”
“Kaiza sihitaji maelezo
nataka kusikia Olivia
anazinduka na anakuwa salama
tena asiendelee kupatiwa
mateso yoyote.Namuhitaji sana
kwa ajili ya uhai wa
mwanangu.Olivia akifa utakufa
naye!!
“Mheshimiwa rais
ninahitaji msaada natakiwa
kumpeleka Olivia hospitali kwa
matibabu” akasema Kaiza
“Dr Alex yuko hapo mtumie
kuhakikisha Olivia anakuwa
salama” akasema Dr Evans
“Mheshimiwa rais hata Dr
Alex mwenyewe amekiri hawezi
kufanya kitu.Olivia anatakiwa
kupelekwa
hospitali.Mheshimiwa rais kuna
kitu ambacho nadhani itakuwa
vyema ukakifahamu kuhusu Dr
Alex.Sifahamu kwa nini lakini
amekuwa mgumu sana kutoa
ushirikiano kwetu na kuna
wakati nilimkamata
akizungumza na mtu kwenye
simu kuhusu Olivia na
nilipomuhoji akadai
anamzungumzia Olivia
mwanae.Mheshimiwa rais sina
imani na huyu mtu kabisa kuna
mchezo anatuchezea” akasema
Kaiza na ukimya mfupi ukapita
halafu Dr Evans akasema
“Sikiliza Kaiza,Olivia
hatakiwi kupelekwa
hospitali.Kila mtu anafahamu
Olivia amepotea hivyo
akionekana tayari kila kitu
kitakuwa kimeharibika na
tutashindwa kupata taarifa za
muhimu.Nitakuelekeza
shambani kwangu,mtoe Olivia
hapo na utampeleka shambani
kwangu kuna nyumba kubwa
pale.Ninamtuma daktari wangu
anakwenda kule akiwa na vifaa
vyote vinavyotakiwa mtamkuta
kule na yeye ndiye atakayebeba
jukumu la kuhakikisha Olivia
anazinduka.Inaniuma kusema
hivi lakini wakati mnaondoka
hapo muue Dr Alex na watu
wake wote.Sehemu hiyo
itakuwa chini yenu.Umenielewa
Kaiza? Akauliza Dr Evans
“Nimekuelewa mheshimiwa
rais” akasema Kaiza na Dr
Evans akamueleza mahala lilipo
shamba lake na bila kupoteza
muda maandalizi ya kuondoka
mahala pale yakaanza.Dr Alex
akafunguliwa na kusaidiana na
akina Kaiza kumtoa Olivia mle
ndani na kumpakia garini.Kabla
hawajaondoka Kaiza
akamuomba Dr Alex warejee
ndani wakazungumze.
“Dr Alex imelazimu
kumuhamisha Olivia
tunampeleka hospitali.Ahsante
sana kwa msaada wako
mkubwa uliotupatia na
ninakuomba samahani kwa yale
yaliyotokea.Kuna uwezekano
tukarejea tena hapa kuendelea
na zoezi letu pale Olivia
atakapokuwa tayari”akasema
Kaiza
“Hata mimi ninashukuru
sana Kaiza.Tusahau yaliyopita
tuangalie ya mbele.Kabla
haujaondoka ninaweza kuipata
simu yangu tafadhali?akauliza
Dr Alex.Kaiza akaingiza mkono
mfukoni kama vile anaitoa simu
yake lakini kwa kasi ya ajabu
mkono wake ukaenda katika
bastora aliyokuwa
ameichomeka nyuma kiunoni
akaichomoa na kuachia risasi
mfululizo Dr Alex akaanguka
chini na hakuwa na uhai tena
Kaiza akamtazama halafu
akamtemea mate na kutoka mle
ndani.Wakati Kaiza akiwa ndani
ya ofisi vijana wake ambao
tayari alikwisha wapa
maelekezo waliwavamia wale
watu wa Dr Alex na kuwamaliza
wote Kaiza alipotoka alikuta
kazi imemalizika.
“Kila kitu tayari?akauliza
Kaiza
“Ndiyo mkuu kila kitu
tayari”
“Good.Let us go” akasema
Kaiza wakaingia katika magari
na kuondoka eneo lile kuelekea
mahala walikoelekezwa na rais
shambani kwake.
 
SIRI
MTUNZI: PATRICK CK
PART 1 SEASON 6
EPISODE 11
Tayari Kiza kimekwisha
tanda angani ndege ya shirika la
ndege la Misri ilipotua katika
uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere.Miongoni mwa abiria
waliokuja na ndege hii ni Ruby
ambaye baada ya kukamilisha
taratibu akatoka na kupokewa
na Mathew na Gosu Gosu
wakaingia garini na kuondoka
haraka eneo lile
“Ruby karibu tena
Tanzania.Nimefurahi sana
kukuona tena” akasema
Mathew wakiwa garini
“Sikuwa na mpango wa kuja
Tanzania hivi karibuni lakini
imenilazimu kuja kwa ajili ya
hili suala muhimu sana.Nini
kinaendelea hivi sasa?akauliza
Ruby na Mathew akamsimulia
kila kitu kilichotokea hadi
mahala walikofika
“Poleni sana kwa kila
kilichotokea.Suala lolote ambalo
ndani yake kuna mkuu wa nchi
lazima liwe zito sana.Suala hili
lina mkusanyiko wa mambo
kadhaa ndani yake.Kuna suala
la Olivia kujihusisha na
mtandao wa IS,suala la Edger
Kaka ambalo rais amehusishwa
nalo na ninaamini kadiri
tunavyoendelea kulichimba hili
suala kuna mengi zaidi
yatajitokeza” akasema Ruby
baada ya kupata picha nzima ya
namna jambo lile
linavyokwenda
Baada ya kutoka uwanja wa
ndege walielekea moja kwa
moja katika hospitali ya Dr
Philip kujua maendeleo ya
Devotha waliyemuacha pale.
“Devotha anaendelea
vyema.Tulifanikiwa kutoa risasi
mbili alizokuwa amepigwa
begani.Anaendelea vyema yuko
katika chumba maalum
anapumzika” DrPhilip
akamwambia Mathew kisha
akawaongoza kuelekea katika
chumba alimokuwa amelazwa
Devotha ambaye alikuwa
amekaa kitandani akitazama
runinga.Dr Philip akakinyonga
kitasa na kuufungua mlango
wakaingia.Sura ya Devotha
ikapatwa na mstuko halafu
akatabasamu
“Hello Devotha” akasema
Dr Philip
“Oh thank you Lord !
akasema Devotha
“Nilikuwa na wasiwasi sana
kama mlifanikiwa kutoka
salama” akasema Devotha
“Usihofu tulitoka
salama.Unaendeleaje?akauliza
Mathew
“Ninaendelea
vyema.Nawashukuru madaktari
wamenihudumia.Ahsanteni
sana kwa kuokoa maisha
yangu” akasema Devotha
“Devotha mimi ndiye
ninayepaswa kukushukuru kwa
kuyaokoa maisha yangu.Bila
wewe hivi sasa bado
ningeendelea kuwapo ndani ya
lile shimo”akasema Mathew
“Nini kinaendelea hivi sasa
Mathew?akauliza Devotha
“Devotha nitakuja
kukujulisha kila kinachoendelea
lakini kwa sasa usiwaze
chochote endelea kupumzika”
akasema Mathew.Devotha
akarusha shuka pembeni
“Dr Philip I’m okay
now.Tafadhali nahitaji
kuondoka”
“Devotha pumzika
tafadhali.Tutakujulisha kila
kinachoendelea” akasema
Mathew
“Hapana Mathew.I need to
get out of here.Kuna mambo
mengi yanayoendelea na siwezi
kuendelea kulala hapa na
kuwaacha mfanye kazi peke
yenu” akasema Devotha
“Devot…….” Dr Philip
akataka kusema kitu Devotha
akamzuia
“Dr Philip unakwenda
kutoa huu mrija wa maji au
niuondoe mwenyewe?akauliza
Devotha
“Let her go” akasema
Mathew na Dr Philip
akauchomoa mrija wa maji
aliyokuwa ametundikiwa
Devotha
“Utanisamehe Dr Philip
najua ulipenda niendelee kukaa
hapa lakini baada ya kuwaona
wenzangu hawa nimepata
nguvu ya ghafla na siwezi
kuendelea kukaa tena hapa
hospitali”akasema Devotha na
kulivua lile gauni la wagonjwa
alilokuwa amevaa akavaa nguo
zake
“Wow ! she’s so hot !
akawaza Gosu Gosu
akimshuhudia Devotha akivaa
mbele yao
“Tunaweza kuondoka”
akasema Devotha Dr Philip
akamuomba asubiri amletee
dawa za kutumia kisha
wakaondoka
“Pole sana Devotha”
akasema Gosu Gosu
“Ahsanteni sana” akasema
Devotha
“Mathew unaweza
ukanieleza nini hasa kilitokea
pale kitalu 1?Mliwezaje
kuufungua mlango wa kutokea
nje?akauliza Devotha
“Devotha tujielekeze katika
masuala mengine ya muhimu ya
kumtafuta Olivia.Unahisi
anaweza kuwa wapi?akauliza
Mathew
“Olivia alihamishwa kutoka
kitalu 2 na sifahamu mahala
alikopelekwa.Niligundulika
nimedukua simu ya Rais
nikaanza kutafutwa na
nikafungiwa kila kitu.Sikuwa na
sehemu nyingine salama ya
kukimbilia Zaidi ya nyumbani
kwako ambako nilipokelewa
vyema na Theresa mtumishi
wako mimi na Saada msichana
ambaye alinisaidia kudukua
simu ya rais.Niliamua kumfuata
Olivia kitalu 2 nikaonane naye
sikumkuta tayari alikwisha
hamishwa na sikuweza kujua
mahala aliko kwani sikuweza
tena kuingia katika mfumo wa
idara yetu. Nilirejea nyumbani
kwako ndipo nikakutana na
Gosu Gosu ambaye naye
alikuwa amefika muda huo
tukazungumza na kuanza
mikakati ya kukuokoa .Mathew
sifahamu alipo Olivia.Naamini
watakuwa wamempeleka
mafichoni mahala ambako
sipafahamu kwa kuhofia
ninaweza kumtorosha”
akasema Devotha na safari
ikaendelea kimya kimya
“Gosu Gosu umewasiliana
na Saada?Yuko salama?akauliza
Devotha
“Nimepiga simu hotelini
nikaunganishwa na chumba
chake ili nizungumze naye
lakini simu ya chumbani kwake
inaita bila kupokelewa”
akasema Gosu Gosu
“Au atakuwa amekamatwa
na akina Kaiza baada ya
kugundua kuwa anacheza na
kamera za kitalu 1?” akauliza
Devotha.
“Tumuombee awe salama”
akasema Gosu Gosu
Safari iliendelea hadi
walipofika katika nyumba ya
Mathew wanayoitumia kama
ofisi yao.Wakashuka garini na
kuingia ndani
“Karibuni ndani
jamani,hapa ni nyumbani
kwangu ni sehemu ambayo
naamini itakuwa salama kwetu
na kila kitu kitafanyika kutokea
hapa” akasema Mathew na
kuwakaribisha Devotha na
Ruby
“Mathew una nyumba ngapi
hapa Dar es salaam?akauliza
Ruby
“Ninazo nyumba zaidi ya
ishirini hapa Dar es
salaam.Ninawekeza katika
majengo kwani thamani yake
inapanda kila wakati tofauti na
magari ambayo kila mwaka
thamani yake hushuka hivyo
msiwe na hofu kama
tukigundulika tuko hapa
tutahama na kwenda sehemu
nyingine bado ninazo nyumba
za kutosha” akasema Mathew
na kuwaonyesha Ruby na
Devotha chumba chao
“Devotha ingekuwa vyema
kama ungepumzika.Mimi na
wenzangu tutaendelea na
utakapokuwa tayari utajiunga
nasi”akasema Mathew.
“Hapana Mathew huu si
muda wa kupumzika ni muda
wa kupambana.Siwezi kulala
kitandani wakati wenzangu
mnaendelea kupambana hili ni
jeraha dogo ambalo haliwezi
kunizuia kupambana.Count me
in Mathew” akasema Devotha
kisha Mathew akawataka wote
waelekee chumba cha kusomea
ambacho kilikuwa kikubwa
kidogo.
“Awali ya yote
nawashukuru sana nyote kwa
kufika kwenu hasa wale
mliotoka mbali Gosu Gosu na
Ruby.Najua niliwapa taarifa
ndani ya muda mfupi na
mkasitisha shughuli zenu kuja
kunisaidia nawashukuru sana
kwa upendo wenu huo.Kabla
sijaendelea Zaidi naomba
nifanye utambulisho
mdogo.Gosu Gosu n Ruby
kutaneni na Devotha ambaye
alikuwa mkurugenzi wa idara
ya siri ya usalama wa ndani ya
nchi.Devotha tayari umekwisha
kutana na Gosu Gosu na
ninaomba usiku huu ukutane
pia na Ruby ambaye anatokea
nchini Uingereza huyu
ninamuita mtu
mashine.Anaifahamu kompyuta
kuliko hata aliyeigundua.Kuna
nyakati humuita jini kutokana
na uwezo wake wa ajabu wa
kucheza na kompoyuta.Huyu
ndiye aliyetengeneza ile
programu ambayo ilifunga
mfumo wenu.Ni mtu ambaye
ananisaidia sana kila pale
ninapokuwa na kazi na amekuja
kushirikiana nasi katika
kumtafuta Olivia” Akasema
Mathew
“Nimefurahi sana
kukufahamu Olivia” akasema
Devotha
“Mimi pia nimefurahi
kukutana nawe” akasema Ruby
“Baada ya utambulisho sasa
tunaendelea.Ndugu zangu
mbele yetu tunalo jambo kubwa
linatukabili.Ni jambo ambalo
ndani yake kuna mambo
mengine kadhaa yamejitokeza
ambayo yanaongeza utata.Kwa
ufupi ni kwamba nina urafiki na
mrembo mmoja anaitwa Olivia
Themba.Siku mbili zilizopita
alitekwa na watu wasiojulikana
na lengo la kuwaita Gosu Gosu
na Ruby ni ili mnisaidie
kumtafuta lakini katika suala
hilo yameibuka mambo
mengine makubwa.Devotha
idara yako inahusika kwa kiasi
kikubwa sana na suala
hili,nataka uwe wa kwanza
kutueleza kwa kina kila kitu
kuhusiana na Olivia,Karibu”
akasema Mathew.
“Idara ya usalama wa taifa
ya jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo walipata taarifa kwamba
kuna mtu anaitwa Seif
Almuhsin ambaye kazi yake
kubwa ni kukusanya vijana
kutoka katika nchi za Afrika
mashariki na kati na
kuwapeleka katika kambi za
mafunzo za IS anaelekea nchini
kwao.Akiwa jijini Kinshasa Seif
alikutana na mtu ambaye baada
ya kumchunguza waligundua ni
mtanzania anaitwa Olivia
Themba.Rais wa Congo
alimtuma mjumbe maalum
kuleta ujumbe kwa rais wa
Tanzania kumjulisha kuhusu
Olivia kukutana na mtu wa
kikundi cha IS,Rais naye
akatukabidhi sisi jukumu hilo
tukaandaa mpango wa kumteka
Olivia mara tu alipotua nchini
akitokea Congo.Tulimpeleka
mafichoni na kuanza kumfanyia
mahojiano.Tukagundua alikuwa
na mawasiliano pia na mtu
anaitwa Sayid Omar ambaye
baada ya kumchunguza
tukagundua ni mfadhili wa
kikundi cha IS.Tulimbana Olivia
atueleze kuhusiana na
mahusiano yake na watu wale
wa IS na akatupa namba Fulani
akatutaka tuzitumie zitatusaidia
kujua mahala alipo nabaada ya
kuziingiza namba zile mtandao
wote wa idara yetu
ukajifunga.Olivia akadai kuwa
ili kuufungua tena mtandao
wetu anataka kuzugumza na
rais.Niliwasiliana na rais
akafika akazungumza naye
lakini hawakuelewana.Olivia
alimueleza rais kwamba
mwanae Coletha
ameambukizwa virusi ambavyo
kama hatatibiwa kwa muda wa
siku kumi na mbili atapoteza
maisha.lengo la kumuambukiza
Coletha virusi hivyo ambavyo
alivitengeneza yeye mwenyewe
ni kumtaka rais amuelekeze
mahala alipo Edger Kaka.Huyu
Edger aliwahi kuwa mbunge wa
bunge la jamhuri ya muungano
wa Tanzania na alifariki dunia
katika ajali iliyotokea siku
aliporejea nchini akitokea Israel
alikoenda kwa matibabu.Olivia
anadai kuwa Edger hajafa na
kwamba rais Dr Evans
anafahamu mahala alipo.Anadai
ajali ile iliyotokea ni ya
kutengenezwa na kwamba
serikali ndio waliofanya tukio
lile na Rais anafahamu mahala
Edger alipo.Tumemtesa Olivia
ili atupe taarifa za kuhusu yeye
na IS lakini bado ameendelea
kushikilia msimamo wake kuwa
Edger hajafa na rais anafahamu
mahala alipo.Nilimuuliza rais
kuhusu tuhuma zile akakana
kufahamu chochote kuhusu
Edger Kaka.Baadae nilitaarifiwa
na rais kuwa kuna mtu anaitwa
Mathew Mulumbi aliwahi
kufanya kazi katika idara ya
ujasusi ya taifa tayari
anafahamu mahala alipo Olivia
na alikuwa katika mikakati ya
kwenda
kumuokoa.Tulimuhamisha
Olivia haraka kutoka mahala
alipokuwa amehifadhiwa na
tukaweka kikosi cha kulinda
mahala pale na ili Mathew
atakapofika atiwe nguvuni kwa
bahati mbaya karibu kikosi
chote kiliuawa.Mathew naye
akaingia katika orodha ya watu
tunaowatafuta na tuliamini
naye pia ni mmoja wa watu wa
IS na kazi yake kubwa ni
kumlinda Olivia.Ili
kumshinikiza Olivia aweze
kutueleza kila kitu tulimteka
baba yake mzee Agrey
Themba.Tulimtesa sana Agrey
huku Olivia akishuhudia lakini
hakufunguka.Usiku huo huo
nikapokea maelekezo kutoka
kwa rais ya kutuma timu
nyumbani kwa Lucy Themba
alfajiri kwa ajili ya kumkamata
Mathew na mtego huo
ukafanikiwa tukishirikiana na
Lucy Themba mama yake
Olivia.Asubuhi ya leo nilianza
kwa kumuhoji tena Olivia na
akanieleza kuwa ni kweli Edger
yuko hai na kama nikitaka
kupata uhakika nifanye
uchunguzi nitajua.Nililazimika
kumuamini na kuamua
kulichunguza hilo
suala.Nilikwenda kuonana pia
na Mathew nikamuhoji na
katika mahojiano hayo
akanisaidia kuzisoma barua
pepe ambazo Olivia alikuwa
anawasiliana na Sayid Omar na
ndipo nikagundua kwamba
Olivia na Sayid Omar walikuwa
wanashirikiana kuandaa kirusi
ambacho amemuambikiza
mtoto wa rais kushinikiza
kupewa taarifa za mahala alipo
Edger kaka.Nilikata tamaa
baada ya kugundua IS wako pia
katika mpango ule wa
kushinikiza rais aeleze mahala
alipo Edger Kaka.Mathew
alinishauri nisiache kuchunguza
na akanishauri nianze kwa
kumchunguza rais.Nilimtumia
Saada tukadukua simu ya rais
lakini hatukupata chochote
kwani tuligundulika
mapema.Baada ya kugundulika
nilifungiwa mawasiliano yote
siwezi kupiga simu wala kuingia
katika mtandao wetu na ndipo
nilipoamua kukimbilia kwa
Mathew kuomba msaada kwani
alinieleza anao watu wake
wawili wanaoweza kunisaidia
ambao ndio nyie Gosu Gosu na
Ruby.Nilimueleza Gosu Gosu
kila kitu nashukuru akanielewa
na tukaanza mikakati ya
kumuokoa kwanza Mathew na
katika harakati hizo nikapoteza
fahamu hadi nilipozinduka na
kujikuta nikiwa hospitali.Kwa
ufupi hayo ndiyo yaliyojiri kwa
upande wa idara yangu”
akasema Devotha
“Ahsante Devotha kwa
maelezo hayo ambayo naamini
kila mmoja wetu
ameyaelewa.Kufuatia maelezo
hayo tunaweza kuichora chati
yetu namna hii.Kwanza kabisa
tunaye Olivia Themba.Huyu ana
mawasiliano na Seif Almusin na
Sayid Omar ambao hawa wote
ni watu wa kundi la IS.Hapa
lazima tufahamu Olivia ana
mahusiano gani na hawa watu
wa IS?Ni mwenzao au
wanamtumia tu kufanikisha
mipango yao?Olivia nimekuwa
naye karibu ni mtu mwenye kila
kitu na binafsi sioni sababu ya
yeye kujiunga na kikundi cha
IS.Olivia na IS wanamleta mtu
anaitwa Edger
Kaka.Tunatakiwa kumfahamu
huyu Edger Kaka ni nani?Ana
mahusiano gani na Olivia na
hawa watu wa IS?Huyu Edger
aliwahi kuwa mbunge wa bunge
la jamhuri ya muungano wa
Tanzania je anahusianaje na IS?
Hawawezi kupoteza nguvu
kubwa na fedha kama suala hili
halina maslahi kwao.Baada ya
kumfahamu Edger Kaka na
mahusiano yake na Olivia na IS
linakuja swali je ni kweli yuko
hai kama wanavyodai?Kama
bado yuko hai yuko wapi? Kama
yuko hai Rais anafahamu
mahala alipo? Ili kupata baadhi
ya majibu ya maswali yetu
tunatakiwa kumpata Olivia
ambaye ametekwa na hajulikani
yuko wapi.Tunayo sehemu ya
kuanzia kufahamu mahala alipo
Olivia.Kuna mtu alipiga simu
nyumbani kwangu
akazungumza na GosuGosu
naamini hata wewe Devotha
ulikuwepo,mtu huyo alikuwa
ananitafuta mimi na Gosu Gosu
akajifanya ni mimi
akazungumza naye mtu huyo
akamueleza kwamba anataka
kumpa taarifa za kuhusiana na
Olivia.Kwa bahati mbaya
hakueleza chochote cha msingi
kwani simu ilikatika.Ruby ni
wewe tuliyekuwa tunakusubiri
uje ili uifanye kazi hii.Tunataka
kujua huyo jamaa alipiga simu
hii kutoka wapi? Hii ndiyo
sehemu ya kwanza kuanzia kazi
yetu.Kuna yeyote mwenye swali
la kuuliza kabla hatuaendelea
mbele?Akauliza Mathew
“Olivia anashirikiana na
magaidi na ndiyo sababu
anashikiliwa na idara ya
serikali.Nataka kufahamu kwa
nini sisi tunamtafuta?Kwa nini
tunataka kumtoa kutoka katika
mikono ya idara ambayo
wanaweza wanao mtandao
mpana Zaidi wa kupambana na
magaidi?Endapo tutafanikiwa
kumpata Olivia hamuoni
kwamba tutakuwa tunafifisha
juhudi za idara ya serikali
kupambana na magaidi?
Akauliza Ruby
“Ruby umeuliza swali zuri
kwa nini tunamtafuta Olivia na
Kutaka kumtoa katika mikono
ya serikali?Kikubwa
kinachotufanya tumtafute Olivia
ni kutaka kuufahamu ukweli
kuhusiana na suala la Edger
Kaka.Tunataka kupata uhakika
kama kweli yuko hai au
amekufa.Kama kweli Edger
yuko hai na Rais anahusika na
suala hilo basi Olivia hataachwa
salama hivyo basi tunatakiwa
kumuokoa na kujua kuhusu
suala hili kwa upana wake na
vile vile kujua IS wameingiaje
katika suala hili na wana
maslahi gani nalo?Majibu ya
maswali haya tutayapata kwa
Olivia pekee.Nadhani
umenielewa Ruby” akasema
Mathew
“Nimekuelewa Mathew”
akasema Ruby
“Good.Endelea kufanya
mambo yako kila kitu
ulichoelekeza nikuandalie kipo
tayari” akasema Mathew na
kumuonyesha Ruby vifaa mbali
mbali alivyokuwa
amemuandalia akaanza
kuvifunga tayari kuanza
kazi.Wakati Ruby akiendelea
kufanya maandalizi ya kuanza
kazi akisaidiwa na Gosu
Gosu,Mathew akatoka nje
Devotha akamfuata
“Unajisikiaje
Devotha?akauliza Mathew
“Mathew nina wasiwasi
sana na Saada.Sijui atakuwa
katika hali gani.Ninatamani
kwenda kumtafuta kujua hali
yake” akasema Devotha
“Devotha sahau kuhusu
Saada kwa sasa.Elekeza akili
yako katika suala kubwa lililo
mbele yetu la kumpata Olivia.”
akasema Mathew
“Mathew huyo Saada
ninayemzungumzia ndiye
aliyefanikisha sisi tukakufikia
mahala ulikokuwa
umefungwa.Bila yeye kucheza
na mtandao wetu kuzima na
kuwasha kamera tusingekufikia
kwa urahisi na
kukukomboa”akasema Devotha
“Nalifahamu hilo Devotha
na ninashukuru lakini kwa sasa
tuna kazi kubwa ya kufanya
kumtafuta Olivia.Naamini huyo
mtu wako anafahamu namna ya
kuchukua tahadhari na atakuwa
salama.Baadae kama tukipata
nafasi ya kutosha tutaangalia
namna ya kumtafuta” akasema
Mathew na ukimya mfupi
ukapita
“Naamini sikufanya kosa
kuchagua kusaliti idara yangu
na kujiunga nawe Mathew”
akasema Devotha
“Ulifanya uamuzi sahihi na
hautajutia uamuzi huo” akajibu
Mathew na kurejea ndani
akamuacha Devotha pale nje.
 
SIRI
MTUNZI: PATRICK CK
PART 1 SEASON 6
EPISODE 12
Ving’ora vya magari ya
wagonjwa vilisikika na magari
matatu ya wagonjwa
yaliyokuwa katika mwendo
mkali yakawasili katika
hospitali kuu ya taifa ya
Mtodora.Geti likafunguliwa na
magari yale yakapita.Ving’ora
vile viliwafanya wauguzi na
madaktari kutoka kwa haraka
kujua ni aina gani ya wagonjwa
walioletwa na magari yake
“Kuna ajali imetokea watu
kadhaa wamefariki dunia na
majeruhi tumewakimbiza hapa”
akasema mmoja wa wauguzi wa
gari la wagonjwa.Haraka haraka
majeruhi wale wa ajali
wakashushwa katika yale
magari wakapelekwa katika
chumba cha upasuaji kwani
wengi walikuwa wamechafuka
damu na haikujulikana ni
sehemu zipi walizokuwa
wameumia.Walikuwa jumla
majeruhi nane.Wanaume saba
na mwanamke mmoja.
Dakika mbili toka magari
yale ya wagonjwa yawasili pale
hospitali,gari mbili aina ya Noah
zenye rangi nyeusi zikawasili
pale hospitali akashuka
mwanaume moja
akajitambulisha kuwa
wamefika pale kujua hali za
ndugu zao ambao wamepata
ajali ya gari.Waliruhusiwa
kuingia ndani na kuegesha
magari yao maegesho
wakashuka wanaume watatu na
wanawake saba ambao
walikuwa wamevaa mavazi
marefu ya kufunika uso na
kuacha macho tu.Walikwenda
mapokezi na kujulishwa kuwa
wagonjwa waliopata ajali
wamepelekwa katika chumba
cha upasuaji na wakawataka
watu wale wakasubiri nje ya
chumba cha upasuaji
kulikokuwa na sehemu ya
kupumzika.Baada ya muda
mfupi zikawasili gari nyingine
mbili nao wakadai pia ni ndugu
wa majeruhi wa ajali ya gari
walioletwa pale.Waliruhusiwa
kupita na mara tu
walipofunguliwa geti kuingia
ndani vioo vya gari la nyuma
vikafunguliwa na mitutu ya
bunduki zilizofungwa viwambo
vya sauti ikajitokeza na walinzi
wote waliokuwa getini
wakamiminiwa risasi.Magari
yale yakasimama wakashuka
watu wanne na kuwamalizia
kwa risasi walinzi wawili
waliokuwa ndani ya chumba
cha walinzi kisha
wakawakusanya wale walinzi
wote waliouawa kwa risasi na
kuwafungia katika kile
chumba.Mmoja wao akachukua
simu na kupiga
“We have control of the
main gate”akasema
Nje ya chumba cha upasuaji
jamaa mmoja aliyevaa kanzu ya
kijivu alimaliza kuzungumza na
mtu simuni akaiweka mfukoni
halafu akamsogelea jamaa
mmoja akampa maelekezo na
bila kupoteza muda akaelekea
katika mlango wa chumba cha
upasuaji akakinyonga kitasa
lakini ulikuwa umefungwa kwa
ndani akagonga kwa nguvu na
baada ya dakika mbili
ukafunguliwa na muuguzi
ambaye alingiwa na baridi ya
ghafla baada ya kujikuta
akitazamana na mtutu wa
bunduki uliofungwa kiwambo
cha kuzuia sauti.Haraka haraka
watu sita waliovaa mavazi ya
kufunika nyuso zao
wakionekana kama wanawake
wakaingia ndani ya chumba cha
upasuaji na kutoka ndani ya
mavazi yao wakachomoa
bunduki walizokuwa
wameshika.Yule kiongozi wao
akaachia risasi na
kuisambaratisha taa kubwa
inayotumika katika upasuaji
kisha akawaamuru watu wote
mle ndani kukaa pembeni ya
meza zile za upasuaji.Madaktari
na wauguzi waliokuwa ndani ya
chumba kile walipatwa na
mstuko mkubwa baada ya
kuwaona wale majeruhi wa ajali
waliokuwa wamelala vitandani
wakiinuka baada ya wenzao
kuingia mle ndani.
Haraka haraka madaktari
wakavuliwa mavazi na
vitambaa walivyokuwa
wamevaa midomoni
vikaingizwa ndani ya midomo
yao kuwazuia kupiga kelele
kisha wote wakafungiwa katika
chumba kimoja.Jamaa wawili
wakavaa mavazi ya madaktari
na wanawake wawili wkavaa
sare za wauguzi.Mtu mmoja
akalala katika kitanda cha
wagonjwa kisha wakatoka
wakikisukuma kitanda
kile.Pembeni ya mtu yule
aliyelala kitandani kama
mgonjwa zilipangwa silaha na
kufunokwa na shuka ili watu
wasizione.Ndani ya chumba kile
cha upasuaji walibaki watu
wawili wakilinda ili asitokee
mtu yeyote akaharibu
operesheni kabla haijakamilika.
Yeyote aliyewaona watu
wale aliamini ni madaktari
wakiwa na mgonjwa.Nyuma yao
walifuatwa na watu wengine
sita waliokuwa wamevaa
mavazi marefu kama wanawake
na kuficha nyuso zao
wakionekana kama ndugu wa
mgonjwa aliyekuwa
anasukumwa katika
kitanda.Walikuwa wanaelekea
katika jengo kubwa maarufu
kama jengo la wagonjwa binafsi
ambako kuna wodi
wanakolazwa watu wenye
uwezo mkubwa kifedha pamoja
na viongozi.Ni katika jengo hili
ndiko alikolazwa Coletha mtoto
wa rais.Kiongozi wa kundi lile
akachukua simu na kupiga
“Kila mtu akae katika nafasi
yake tunakaribia kufika katika
jengo” akasema yule jamaa na
kukata simu.Jamaa aliyepewa
maelekezo naye akatoa
maelekezo kwa wenzake
waliokuwa nje ya chumba cha
upasuaji na taratibu wakaanza
kutawanyika wakielekea katika
jengo lile aliko mtoto wa rais.
Lango la kuingilia jengola
wagonjwa binafsi lilikuwa wazi
na kitanda kile kikaingizwa
ndani.Kulikuwa na meza ya
mapokezi na wauguzi
waliokuwepo pale wakastuka
baada ya kuona kitanda
kikiingizwa bila wao kupewa
taarifa kama kuna mgonjwa
anapelekwa ili waandae
chumba.Kulitokea mabishano
kidogo kati ya wauguzi wa ile
wodi na wale jamaa mmoja wa
wale wauguzi akataka kupiga
simu lakini lilikuwa ni kosa
kubwa kwani risasi kama mvua
zilitoka kwa mmoja wa wale
watu waliokuwa wamejitanda
mavazi marefu akionekana
kama mwanamke na ndani ya
vazi lile alikuwa ameshika
bunduki ndogo.Wakati wauguzi
wakishughulikiwa,nje ya jengo
walinzi wawili waliovaa sare za
kampuni ya ulinzi walijikuta
wakiminiwa risasi bila maelezo
na watu waliovalia mavazi yale
marefu.Haraka haraka wauguzi
wale wakafichwa nyuma ya
meza yao kubwa.Kiongozi wa
magaidi wale akatoa simu na
kupiga
“Tunaelekea ghorofa ya
juu”akasema
Waliingia katika lifti na
kuelekea ghorofa ya
sita.Milango ya lifti ilipofunguka
kulikuwa na watu watatu
waliokuwa nje ya lifti wakiwa
na kazi maalum ya kuwakagua
watu waliokuwa wakiingia
ghorofa ya sita kuhakikisha
hakuna anayeingia na
silaha.Hakukuwa na muda wa
kuulizana kwani tayari ramani
nzima tayari waliifahamu hivyo
kabla wale walinzi hawajafanya
chochote wakamiminiwa risasi
za kustukiza halafu
wakaingizwa na kufungiwa
katika chumba cha
pembeni.Safari ikaendelea
wakisukuma kitanda kile na
mara wakakutana na madaktari
watatu
waliostuka.Wakawasimamisha
na kutaka kupata maelezo
kuhusiana na mgonjwa yule
aliyekuwa kitandani.Miongoni
mwa madaktari wale
alikuwemo Dr Stanslaus Mbeula
ambaye ndiye anayeongoza
jopo la madaktari
wanaochunguza virusi
alivyoambukizwa Coletha.
“Mgonjwa huyu anakwenda
wapi?Nani katoa ruhusa aletwe
huku? Utaratibu wa hapa
hamuufahamu?akauliza Dr
Mbeula baada ya kuona
maelezo ya wale jamaa
yanajichanganya.Kitendo kile
cha Dr Mbeula kuwafokea wale
madaktari kwa kupeleka
mgonjwa katika wodi ile bila
kufuata utaratibu kikawavuta
walinzi waliokuwa wakimlinda
Coletha waliokuwa wamezagaa
katika ghorofa ile ya sita.Ghafla
wale magaidi waliovaa sare za
madaktarina wauguzi
wakabonyea chini ya kitanda na
risasi zikaanza kuvuma kutoka
kwa watu waliokuwa nyuma
yao waliokuwa wamevaa
mavazi marefu meusi,Dr
Mbeula na wenzake
wakaanguka chini.Kitendo kile
kiliwastua walinzi wa Coletha
ambao walianza kurusha risasi
kuwaelekea wale jamaa.Yule
mgonjwa aliyekuwa amelala
kitandani akalitupa shuka
pembeni na kuwapa nafasi
wenzake waliokuwa chini ya
kitanda kuchukua silaha.Wakati
akijiandaa kushuka kitandani
akapigwa risasi za kifua
akaanguka juu ya kitanda na
kufa hapo hapo.Mapambano
makali yakaanza kati ya walinzi
wa Coletha na wale magaidi.
“Red six ! Red six
!!..akasema mmoja wa walinzi
wa Coletha akiwajulisha
wenzake kuwa wamevamiwa.
Bastora za walinzi wa
Coletha hazikuwa na viwambo
vya sauti hivyo milio ya risasi
ilisikika na kuzua taharuki
kubwa.Magaidi zaidi
walikimbilia ndani ya jengo lile
kuwasaidia wenzao wakiwa na
bunduki nzito.Walinzi wa
Coletha wakazidiwa nguvu na
kuuawa.Kiongozi wa magaidi
wale akaingia ndani ya chumba
alimolazwa Coletha na kumkuta
akiwa amekumbatiwa na
msaidizi wake
“Tafadhali naomba
msituue!! Akalia yule msaidizi
wa Coletha na bila huruma yule
kiongozi wa magaidi
akamchapa risasi na
kumuua.Coletha akayafunika
macho kwa mikono yake
aliogopa sana
“Usihofu Coletha
hatutakuua.Tunakupeleka
sehemu salama” akasema yule
jamaa na kitanda kikaingizwa
Coletha akapandishwa
wakatoka haraka mle chumbani
hadi kwenye lifti tayari kwa
kushushwa chini.Hawakuiacha
maiti ya mwenzao aliyeuawa
kwa risasi.Baada ya kushuka
chini kitanda alichopanda
Coletha kikaanza kusukumwa
kwa kasi kubwa kuelekea
mahala yalikoegeshwa
magari.Magaidi wale walikuwa
wamejipanga vyema
kukabiliana na hatari yoyote
ambayo ingetokea.Baada ya
kukamilisha kazi yao
wakakimbilia katika magari yao
na kuondoka.Mara tu
walipovuka geti kuu la kuingilia
hospitali mlipuko mkubwa
ukatokea katika jengo la
wagonjwa binafsi.Bomu
lililipuka
 
SIRI
MTUNZI: PATRICK CK
PART 1 SEASON 6
EPISODE 13
Kwa maelekezo
waliyopewa na Ruby,Mathew
na Gosu Gosu walifanikiwa
kufika katika jengo ambalo
ndimo mtu aliyepiga simu
akitaka kumjulisha Mathew
kuhusu Olivia alikuwemo
wakati akipiga simu.Nyumba
ilikuwa giza na haikuwa
ikiwaka hata taa moja.Geti
halikuwa limefungwa,Mathew
akalisukuma taratibu na kuingia
ndani wakiwa katika tahadhari
kubwa.Ndani ya ile nyumba
kulikuwa na magari mengi
mabovu
“Mathew unadhani tuko
sehemu sahihi?Mbona hapa
panaonekana kama
gereji?akauliza Gosu Gosu
“Ninamuamini sana Ruby
hawezi akatuelekeza sehemu
ambayo si sahihi.Tuchunguze
mahala hapa vizuri.Mara nyingi
sehemu kama hizi hutumika
kama maficho kwani si rahisi
mtu kutilia shaka kama kuna
kitu kinaendelea” akasema
Mathew
Walinyata kwa tahadhari
wakipita gari baada ya jingine
wakichungulia na walipokaribia
kufika katika mlango wa
kuingia ndani ile nyumba
waligundua kuna miili ya watu
ndani ya gari wakiwa
wamekufa.Mathew akawasha
tochi akawamulika walikuwa
wamekufa.Akamgeukia Gosu
Gosu
“Tuko sehemu sahihi
kabisa.Kuna kitu kimetokea
hapa tumekikosa !! akasema
Mathew huku Gosu Gosu akiwa
makini kujihami na hatari
yoyote ambayo ingetokea.
Mlango wa kuingilia ndani
ulikuwa wazi wakaingia kwa
tahadhari.Haikuwa nyumba
kubwa.Ilikuwa na vyumba
vichache wakakagua vyumba
vyote hakukuwa na kitu
chochote cha maana zaidi ya
vifaa vya magari .
“Nini kinachofanyika katika
nyumba hii? Ukiangalia kwa
haraka haraka shughuli kubwa
inayofanyika mahala hapa ni
ufundi wa magari lakini kitendo
cha watu wale kuuawa
kinawasha taa nyekundu
kutuonyesha kuwa
kinachofanyika hapa ni zaidi ya
kutengeneza magari.Yule mtu
aliyepiga simu akinitafuta
ukazungumza naye alipiga simu
kutokea hapa”
“Mathew unadhani Olivia
alikuwepo hapa? Nyumba yote
imejaa vifaa vya magari hakuna
sehemu ambako Olivia anaweza
akafichwa” akasema Gosu Gosu
“Gosu Gosu naamini lazima
kuna kitu hapa.Tujiulize nani
kawaua watu wale? Lazima ipo
sababu ya kuuawa kwao na si
bahati mbaya” akasema
Mathew na kwenda tena katika
gari ilimowekwa miili ya wale
jamaa waliouawa.Wakaitoa
miili ile na kuanza
kuichunguza.Walikuta vitu
mbalimbali kutoka kwa wale
jamaa lakini wote waliwakuta
wakiwa na kadi maalum za
kufungulia mlango.
“Wote wana kadi hizi
ambazo ni maalum kwa ajili ya
kufungulia milango.Mlango upi
hapa ndani unafunguliwa kwa
kadi?akauliza Mathew kisha
wakaelekea tena ndani ya
nyumba wakaanza kuchunguza
milango yote kupata mlango
ambao kadi zile walizokutwa
nazo wale jamaa hutumika
kuufungua.Wakati wakiendelea
kuchunguza Gosu Gosu
akamuita Mathew
“Kuna kitu nimekiona
katika chumba hiki” akasema
Gosu Gosu na kumuonyesha
Mathew kitu Fulani Mathew
akajaribu kupitisha moja ya
kadi waliyoipata kutoka kwa
wale jamaa na mlango
ukajifungua kukaonekana ngazi
za kushuka chini.
“Nilijua tu lazima kuna kitu
kinaendelea katika nyumba hii”
akasema Mathew na kumtaka
Gosu Gosu aendelee kubaki pale
pale juu kulinda usalama
endapo kungetokea hatari
yoyote.Taratibu akashuka chini
akiwa katika tahadhari
kubwa.Mara tu baada ya
kushuka ngazi kitu cha kwanza
alichokishuhudia ulikuwa ni
mwili wa mtu aliyelala chini
akiwa amekufa kwa kupigwa
risasi.Alikuwa amevaa koti la
kidaktari.Mathew
akamchunguza kwa makini
akampekua lakini hakumkuta
na kitu chochote.Alimuacha
yule jamaa akaanza kupitia
chumba kimoja baada ya
kingine akikagua na mwisho
akakifikia chumba kikubwa
kilichokuwa na mitambo
kadhaa ambayo aliigundua ni
mitambo maalum ya kutesea
watu.
“Hii sehemu inaonekana ni
maalum kwa ajili ya
mateso,naamini Olivia aliletwa
hapa kuteswa .Devotha alieleza
kuwa Olivia alihamishwa kwa
siri na hajui alipelekwa wapi
naamini aliletwa hapa.Hawa
waliouawa ni akina nani?Je ni
wale waliokuwa wanamshikilia
Olivia? Kama ndiyo nani
kawaua?Ninaanza kuwa na
wasiwasi yawezekana labda
wamevamiwa wakauawa na
kisha wavamizi wakaondoka na
Olivia” akawaza Mathew na
kwenda kumpiga picha yule
jamaa aliyeuawa akiwa na koti
la kidaktari halafu akamtumia
Ruby na kumpigia simu
“Ruby tumefika mahala
hapa ulipoelekeza,tumekuta
shughuli kubwa inayoendelea ni
ufundi wa magari” akasema
Mathew na kumuelezea Ruby
namna eneo lilivyo
“Lakini tumegundua kuna
nyumba ya siri iko chini ya
nyumba hii ndogo iliyo juu
ambako ndiko shughuli mbali
mbali za utesaji
zinaendelea.Kuta zina damu na
inaonekana unyama mkubwa
sana hufanyika hapa katika hii
nyumba.Kuna vyumba kadhaa
na kimoja kina mitambo na
zana mbali mbali za kutesea
watu.Hakuna mtu yeyote
tuliyemkuta eneo hili bali
tumekuta kuna watu
wameuawa na kufichwa ndani
ya gari na huku chini nimekuta
ameuawa mtu
mmoja.Nimekutumia picha ya
huyo mtu nataka umuonyeshe
Devotha kama
anamfahamu.Nataka kujua
kama anamfahamu” akasema
Mathew na Ruby
akamuonyesha Devotha ile
picha aliyotumiwa na Mathew
baada ya muda mfupi Devotha
akasema
“Mathew huyu mtu
simfahamu kabisa.Hayuko
katika idara yangu”
“Devotha hiyo ndiyo hali
tuliyoikuta hapa.Yamefanyika
mauaji na huyo mtu ni mmoja
wa wale walioua….”
“Mathew..!! akaita Devotha
“Kuna nini Devotha?
“Mathew ninatazama
runinga sasa hivi kuna habari
mpasuko.Umetokea mlipuko
mkubwa katika jengo la
wagonjwa binafsi katika
hospitali kuu ya Mtodora.Jengo
hilo linalodaiwa kulipuliwa
ndimo alimokuwa amelazwa
Coletha mtoto wa rais.Chanzo
cha mlipuko huo inasadikiwa ni
bomu la kutegwa.Taarifa za
awali zinaeleza kwamba
kikundi cha watu
wasiofahamika walifika
hospitali hapo wakiwa na
magari ya kubebea wagonjwa
wakidai kupeleka majeruhi wa
ajali ya gari.Waliwateka
madaktari wakawavua mavazi
yao wakavaa na inasemekana
walielekea katika jengo
alimokuwa amelazwa mtoto wa
rais.Mpaka sasa hakuna idadi
kamili ya vifo au majeruhi
iliyotolewa” akasema Devotha
“Oh my God !! akasema
Mathew na kukuna kichwa.
“Kuna taarifa zozote hadi
hivi sasa kuhusiana na Coletha
kama ni mzima?
“Hakuna taarifa yoyote hadi
hivi sasa iliyotolewa” akasema
Devotha.Mathew akafikiri
kidogo na kusema
“Hakuna shaka wavamizi
hao walikuwa na shida na
Coletha.Naamini lazima
watakuwa ni watu wa IS
wakiendelea na mpango wao
wa kumtaka rais awaeleze
mahala alipo Edger
Kaka.Devotha naomba umpatie
simu Ruby” akasema Mathew
“Hallo Mathew” akasema
Ruby
“Ruby kama nilivyokueleza
awali kwamba ninaamini Olivia
alikuwepo mahala
hapa.Nimegundua nyumba hii
imezungukwa na kamera za
siri,kuna chumba ambacho kina
runinga kubwa
zilizounganishwa na kamera
zinazoizunguka nyumba
hii.Kamera hizi zinaweza
kutusaidia kufahamu
kilichotokea na kinachofanyika
mahala hapa.Ninataka tupitie
kumbu kumbu zote
zilizohifadhiwa kuanzia asubuhi
ya leo”akasema Mathew na
Ruby akamtaka aende katika
chumba hicho chenye
kuonyesha picha zote za
kamera.Akaketi na kuanza
kufuata maelekezo yote ambayo
Ruby alimpa.Baada ya dakika
tano Ruby akaweza kudukua
kamera zile na kuanza kupitia
kumbu kumbu za kamera
akianzia na kamera iliyokuwa
katika geti la kuingilia
ndani.Aliipeleka mbele kamera
hadi pale aliposhuhudia geti
likifunguliwa na magari matatu
yenye rangi nyeusi yakiingia
“There stop ! ..Devotha
aliyekuwa pembeni ya Ruby
akasema
“Hizi ni gari zetu”
akazitazama kwa makini halafu
akamtaka Ruby apeleke
mbele.Milango ya magari
ikafunguliwa na watu kadhaa
wakashuka
“Kaiza !! akasema Devotha
kwa hasira
“Unamfahamu?Ruby
akauliza
“Ndiyo.Alikuwa msaidizi
wangu” akajibu Devotha
Kaiza alisalimiana na mtu
aliyevaa koti jeupe.Baada ya
muda lango kubwa la moja
wapo ya chumba likafunguliwa
na gari moja kati yay ale
waliyokuwa nayo akina Kaiza
likaingia.Ruby akahamisha
kamera baada ya watu wote
kuonekana wakiingia ndani.
Katika kamera nyingine
walimshuhudia Olivia akiwa
amefungwa kitandani.
Walifuatilia kila
kilichokuwa kimetokea katika
kile chumba alimokuwa
amefungwa Olivia akiteswa.
“Nimekuwa mkurugenzi wa
idara ya siri ya mambo ya ndani
ya nchi lakini sipafahamu
mahala hapa ni
wapi.Nakubaliana na Mathew
kwamba mahala hapa ni
maalum kwa ajili ya kutesea
watu.Kaiza amepafahamuje
mahala hapa? akawaza Devotha
Walifuatilia kila kitu hadi
pale Olivia alipondolewa katika
kile chumba akapakiwa garini
na kuondoka.
“Ahsante sana Ruby kwa
msaada huu mkubwa na sasa
tumepata uhakika kuwa Olivia
alikuwa hapa na amehamishwa
na kupelekwa mahala
kusikojulikana.Tunao uhakika
bado yuko mikononi mwa idara
ya usalama wa ndani ya
nchi.Swali linaloibuka
wamempeleka wapi?akauliza
Mathew
“Kwa kuwa tumepata
uhakika kuwa Olivia yuko
katika mikono ya Kaiza njia
nyepesi ya kufahamu mahala
alipo ni kwa kumpigia simu
Kaiza na kufahamu mahala
alipo.” akasema Devotha
“Hilo ni wazo zuri.Fanyeni
hivyo kisha mtatujulisha,sisi
tunaondoka hapa” akasema
Mathew kisha akatoka kule
chini akakutana na Gosu Gosu
wakaelekea garini na kuondoka
mahala pale.Mathew
akamueleza kila kitu
kilichotokea akiwa kule chini.
“Ukiacha hilo la Olivia
kuwepo hapa kuna lingine
kubwa limetokea” akasema
Mathew
“Kumetokea nini tena?
“Hospitali kuu ya Mtodora
imevamiwa na watu
wasiofahamika wamefanya
mauaji na kulipua jengo la
wagonjwa binafsi alimokuwa
amelazwa mtoto wa rais”
Mathew akasema
“Nani waliofanya kitendo
hicho? akauliza Gosu Gosu
“Naamini waliofanya
kitendo hiki ni magaidi wa IS
ambao wanataka kumshinikiza
rais awaeleze mahala alipo
Edger Kaka na japo haijawekwa
wazi bado lakini nina uhakika
mtoto wa rais ndiye sababu ya
wao kuvamia hospitali
hapo.Ninazidi kujiuliza
umuhimu wa Edger Kaka kwa
kikundi cha IS.Mtu pekee
ambaye anaweza akatusaidia
kutuondoa katika wingu hili
lililotanda ni Olivia ambaye
mpaka sasa hatujui mahala
alipo” akasema Mathew na simu
yake ikaita alikuwa ni Ruby
“Hallow Ruby” akasema
Mathew
“Mathew tumejaribu
kumpigia simu Kaiza lakini
hapatikani kwa namba zile
anazozifahamu Devotha”
akasema Ruby
“Hakuna namna nyingine ya
kumpata Kaiza? Ninaomba
kuzungumza na Devotha”
akasema Mathew
“Hallow Mathew”
“Devotha nataka unielekeze
mahala anakoishi Kaiza”
“Kwa nini Mathew?
Unataka kumfuata kwake?
“Nataka kuichukua familia
yake”
“Mathew hapana hilo si
jambo zuri”
“Kwa nini Devotha?
“Kaiza ana watoto wadogo
mapacha wana miezi miwili
hawastahili kuingizwa katika
jambo hili.Tutafute namna
nyingine ya kumtafuta Olivia na
si kuwaumiza familia ya Kaiza
ambao hawana kosa lolote”
akasema Devotha
“Devotha ninaomba usiwe
kikwazo cha kukwamisha
mambo yetu.Sijali kama ana
watoto mapacha hata kama
angekuwa na watoto hamsini
lakini tayari Kaiza ni mtu
muhimu sana kwetu hivyo kila
njia inapaswa kutumika
kuhakikisha tunampata Olivia”
akasema Mathew
“Hapana Mathew tutafute
namna nyingine lakini binafsi
siko tayari kuwaingiza malaika
wale katika hatari.Hawana kosa
lolote” akasema Devotha
“Listen to me lady.This is
my mission and we’re going to
do it my way.Wewe ni nani wa
kunizuia nisitekeleze mipango
yangu? Akauliza Mathew kwa
ukali
“Mathew this is my mission
too” akasema Devotha kwa
ukali
“Devotha you don’t know
me well.Naomba tusibishane
tafadhali nieleze anakoishi
Kaiza” akasema Mathew
akionekana kukasirishwa sana
na maneno yale ya Devotha
“Usinitishe Mathew”
akasema Devotha na kukata
simu
“Damn it !! akasema
Mathew kwa hasira
“Simuelewi huyu
mwanamke.Kwa nini amegoma
kunielekeza anakoishi
Kaiza?Tumekwama Gosu Gosu
turejee nyumbani
nikamuonyeshe huyu
mwanamke mimi sipendi
mzaha” akasema Mathew.
 
SIRI
MTUNZI: PATRICK CK
PART 1 SEASON 6
EPISODE 14
Taarifa ya kuvamiwa kwa
hospitali ya Mtodora na kutokea
kwa mlipuko katika jengo
alimokuwa amelazwa Coletha
mtoto wake zilimstua mno Dr
Evans.Alitaka kuelekea huko
haraka kujua hali ya mwanae
lakini walinzi wake wakamzuia
kwani eneo lile tayari ni hatari
kwa usalama wake.
“Kwa nini mnanizuia
wakati jengo lililolipuliwa
amelazwa mwanangu?akauliza
kwa ukali
“Mheshimiwa rais jukumu
letu ni kukulinda wewe na
kuhakikisha unakuwa salama
hivyo hatuko tayari kukuacha
ukaenda mahala ambako si
salama.Tunaomba utulie hapa
na tutafuatilia kujua kama
mwanao ni mzima” akasema
Hassan kiongozi wa kikosi cha
kumlinda rais.Dr Evans alikuwa
anatokwa na jasho usoni kama
amemaliza mbio ndefu.
“Hassan my pills please”
akaomba apewe dawa zake
akameza na kutulia sofani
“Hassan tafadhali nataka
haraka taarifa za kilichotokea
hospitali.Nataka kujua kama
mwanangu ni mzima” akasema
Dr Evans.
“Mzee tayari vikosi mbali
mbali viko eneo la tukio na
jitihada za uokozi
zinaendelea.Watu wetu pia
wameelekea huko na muda si
mrefu tutapata jibu” akasema
Hassan
“Nani hawa waliofanya
jambo hili? Huu ni unyama
mkubwa sana kuvamia hospitali
na kuua watu! Wanyama hawa
lazima wapatikane !! akasema
Dr Evans na kumpigia simu
mkurugenzi wa idara ya
kudhibiti na kupambana na
ugaidi.
“Mheshimiwa rais”
akasema mkurugenzi wa idara
ya kupambana na ugaidi
“Mkurugenzi nataka kupata
taarifa za hiki kilichotokea
hospitali ya Mtodora” akasema
Dr Evans kwa ukali
“Mheshimiwa rais tayari
timu yetu imekwisha fika eneo
la tukio na uchunguzi
unaendelea ila kwa taarifa
ambazo zimepatikana hadi sasa
ni kwamba usiku huu zilifika
gari tatu za wagonjwa zikiwa na
majeruhi wa iliyodaiwa ni ajali
ya gari.Haraka haraka majeruhi
wale walichukuliwa na
kukimbizwa katika chumba cha
upasuaji kwa ajili ya kupatiwa
huduma kwani walikuwa
wamechafuka damu na
walionekana kuumia
mno.Wakati madaktari
wakiendelea kuwachunguza
majeruhi wale ili kujua sehemu
walizoumia walifika tena watu
wengine ambao walidai ndugu
zao wamepata ajali na
kukimbizwa pale hospitali.Kwa
mujibu wa madaktari
waliokuwemo katika chumba
cha upasuaji wanadai kwamba
wakati wakiendelea na zoezi la
kuwahudumia majeruhi wale
mara wakajikuta wakivamiwa
na watu wenye silaha na kitu
cha kushangaza wale majeruhi
waliokuwa katika vitanda
wakihudumiwa wakainuka
wote kumbe hawakuwa
wameumia kokote ulikuwa ni
mpango wa kuwawezesha
kuingia pale hospitali.Magaidi
wale waliwavua nguo
madaktari wakavaa wao kisha
wakasukuma kitanda kuelekea
katika jengo
lililolipuliwa.Haijajulikana bado
kitu gani walikwenda kukifanya
katika jengo hilo.Timu yetu
wakishirikiana na idara
nyingine wanaendelea na
uchunguzi na pale tutakapopata
taarifa Zaidi tutakujulisha
mheshimiwa rais” akasema
mkurugenzi wa idara ya
kupambana na ugaidi
“Mkurugenzi idara yako
imepewa jukumu la
kuhakikisha inang’amua
kuwepo kwa mashambulio ya
kigaidi.Hamkupata viashiria
vyovyote vya kutokea kwa
shambulio hili?akauliza Dr
Evans
“Mheshimiwa rais
hatukuwa tumepata viashiria
vyovyote vya kufanyika kwa
shambulio kama hili la kigaidi”
“Nataka muhakikishe
mnawafahamu waliofanya tukio
hilo ni akina nani na kuwatia
nguvuni haraka sana.Vile vile
hakikisheni mnafahamu kama
kuna mashambulio mengine
Zaidi yamepangwa kufanyika na
muhakikishe mnazuia
kufanyika kwa shambulio
lingine tena la kigaidi hapa
nchini.Nataka taarifa za kila
mtakachokuwa mnakigundua
kuhusiana na tukio hili”
akasema Dr Evans
“Nitakujulisha mheshimiwa
rais” akajibu mkurugenzi na
rais akakata simu
“Mwili wote unatetemeka
kila nikimuwaza mwanangu
Coletha.Je atakuwa
mzima?akajiuliza Dr Evans na
mara simu yake ikaita.Zilikuwa
ni namba ngeni katika simu
yake akaipokea.
“Hallow” akasema Dr Evans
“Mheshimiwa rais habari za
usiku huu.Mimi ni kiongozi wa
kikundi kilichofanya shambulio
usiku huu katika hospitali kuu
ya Mtodora.Kama uko na watu
karibu usionyeshe mstuko
wowote sogea pembeni
ninataka kuzungumza
nawe,usijaribu kutaka
kuifuatilia simu hii nitagundua”
akasema mtu wa upande wa pili
wa simu aliyekuwa
anazungumza Kiswahili safi.Dr
Evans akawafanyia walinzi
wake ishara kwamba anaingia
chumbani kwake kuzungumza
na simu.Mwili ulikuwa
unamtetemeka
“Hallow” akasema Dr Evans
kwa woga
“Mheshimiwa rais
nilikueleza kwamba mimi ni
kiongozi wa kikundi
kilichofanya shambulio usiku
huu katika hospitali kuu ya
Mtodora.Napenda kukujulisha
usihangaike kumtafuta mwanao
tumemchukua tunaye sisi.Hali
yake si nzuri anaumwa sana na
anaweza akapoteza maisha
hivyo ili kuokoa uhai wake
unapaswa kusikiliza na
kutekeleza kila kile
tutakachokuelekeza” akasema
yule jamaa na kumfanya Dr
Evans ashushe pumzi
“Kwa nini mmemteka
mwanangu?Amewakosea nini?
Ninawaonya kuwa mmekosea
kuanzisha vita na
mimi.Matokeo yake ni mabaya
mno kwenu !! akasema Dr
Evans kwa ukali
“Mheshimiwa Rais
tunafahamu nguvu kubwa
uliyonayo lakini kwa usalama
wa mwanao utafuata kila
tutakachokuelekeza ukifanye na
kama ukipuuzia utamkosa
mwanao na mashambulio Zaidi
yataendelea katika sehemu
mbali mbali hapa Dar es
salaam.Tumejipanga vizuri
katika sehemu mbali mbali
zenye mikusanyiko ya watu na
pindi utakapokataa
kutekekeleza matakwa yetu
basi Tanzania itageuka
nyekundu.Hatutanii.Tukio la
usiku huu katika hospitali ya
Mtodora ni ishara kwamba
tunaweza kuingia sehemu
yoyote tukiamua” akasema yule
jamaa
“Punguani wewe !! akasema
Dr Evans kwa hasira
“Mheshimiwa rais hivi sasa
kisu kiko shingoni kwa mtoto
wako Coletha na unayeweza
kuzuia kifo chake ni wewe kwa
kutekeleza maagizo yetu”
“Mnataka nini kutoka
kwangu?akauliza Dr Evans
“Tunataka mambo kadhaa
na jambo la kwanza tunataka
utupatie mtu anaitwa Olivia
Themba ambaye anashikiliwa
na serikali.Nataka tumpate
Olivia ndani ya nusu saa
kuanzia sasa na kama
hautatekeleza hilo basi tegemea
kusikia mambo mengine
makubwa sana usiku wa
leo.Usiku huu utakuwa ni usiku
wa damu.Tekeleza hicho
nilichokueleza na utaokoa
maisha ya maelfu ya
watanzania ambao watapoteza
maisha yao usiku wa leo kama
hautakuwa tayari kutekeleza
kile tulichokuelekeza.Dakika
ishirini kutoka sasa nitakupigia
simu na ninataka hadi muda
huo Olivia awe ameandaliwa
tayari kupelekwa mahala
nitakapokuelekeza.Tekeleza
hilo nililokuelekeza na mwanao
atakuwa salama.Ninaanza
kuhesabu muda kuanzia
sasa”akasema yule jamaa na
kukata simu.Dr Evans akabaki
ameshikilia simu sikioni
“Haya ni majaribu
makubwa sana kuwahi
kuyapata katika uongozi
wangu.Nilikuwa sahihi
nilipohisi waliofanya shambulio
hilo lengo lao lilikuwa ni
kumpata mwanangu
Coletha.Lazima hili ni kundi la
IS na ndiyo maana wametaka
kwanza wampate mtu wao
kabla ya kitu kingine
chochote.Watu hawa hatari
natamani nitumie nguvu yangu
kubwa kuwasaka lakini
ninahofia usalama wa
mwanangu Coletha.Kwanza ni
mgonjwa na pili hawa jamaa
wanaweza wakamuua.Ni watu
wakatili mno.Kwa nini Olivia
akajiunga na watu
hawa?Anapata nini kutoka kwa
magaidi?akajiuliza Dr Evans
“Ninafikiria nivishirikishe
vyombo vya usalama
kuwatafuta hawa jamaa lakini
linapokuja suala la mwanangu
ninaingiwa na hofu.Sitaki
kuhatarisha usalama wa
mwanangu.Magaidi hawatanii
wanaweza wakautoa uhai wa
mwanangu.Wamenibana
kwenye kona na sina namna
nyingine ya kufanya Zaidi ya
kuwasikiliza kwa ajili ya
usalama wa mwanangu.Hiki ni
kitendo cha ukatili mkubwa
sana na
hakivumiliki.Nitawaonyesha
mimi ni nani pale nitakapokuwa
nimempata mwanangu”
akawaza Dr Evans na kumpigia
simu Kaiza
“Kaiza anaendeleaje Olivia?
“Kwa sasa hali yake
inaendelea vyema.Daktari
uliyemtuma amemuhudumia na
hali yake inaridhisha” akajibu
Kaiza
“Kaiza nataka umchukue
Olivia na uende naye kitalu
2.Nataka ndani ya dakika
ishirini uwe umefika pale”
akasema Dr Evans na Kaiza
akashangaa
“Kuna nini mheshimiwa
rais?akauliz
“Kaiza fanya kama
nilivyokuelekeza.Ndani ya
dakika ishirini uwe umefika
kitalu 2 ukiwa na Olivia.Anza
safari sasa hivi” akasema Dr
Evans na kukata simu.
“I’m doing this for Coletha
but you’ll pay for this you
bastards.Lazima watalipa kwa
gharama kubwa sana kitendo
hiki walichokifanya cha
kumwaga damu za watu na
kumteka mwanangu.Kwa nini
wananiandama kiasi
hiki?Wameanza kwa
kumuambukiza mwanangu
virusi na kama haitoshi
wakaona wamteke kabisa.Je ni
hili suala la Edger Kaka ndilo
linasababisha haya yote?Kwa
nini hawataki kunielewa
nikiwaeleza kuwa sifahamu
chochote kuhusu suala
hilo?Safari hii wamevuka mstari
na lazima nitawaonyesha mimi
ni nani”akawaza Dr Evans
akiwa amekunja uso kwa
hasira.
 
SIRI
MTUNZI: PATRICK CK
PART 1 SEASON 6
EPISODE 15
Mathew na Gosu Gosu
walirejea katika makazi yao
“Nataka nimuonyeshe
Devotha sihitaji mzaha
ninapokuwa kazini” akawaza
Mathew baada ya kushuka
garini akipiga hatua ndefu
kuingia ndani Gosu Gosu akiwa
nyuma yake.Mara tu
alipofungua mlango wa
sebuleni akakutana na kitu
ambacho hakuwa
amekitarajia.Akasimama pale
mlangoni kwa sekunde kadhaa
asiamini kile alichokishuhudia
kwa macho yake
“Jesus Christ !! akasema
Mathew kwa sauti ndogo
“Kuna nini
Mathew?akauliza Gosu Gosu
aliyekuwa nyuma yake.
Mathew akatoka mbio na
kumfuata Ruby ambaye alikuwa
amelala sakafuni katika dimbwi
la damu.
“Ruby !! Ruby !! akaita
Mathew na kumgeuza Ruby
“Ruby !! akaita Mathew na
Ruby akafungua macho.Hakuwa
na nguvu.Alikuwa amepigwa
risasi haikujulikana ni risasi
ngapi kwani mwili wake wote
ulikuwa umechafuka kwa damu
“My God !! akasema Gosu
Gosu
“Please don’t die Ruby!!
Akasema Mathew na kumuinua
“Gosu Gosu tunatakiwa
kumuwahisha Ruby hospitali”
akasema Mathew akambeba
Ruby hadi garini kisha
wakaondoka kwa kasi
kubwa.Gosu Gosu akiwa katika
usukani na Mathew akiwa
amemshikilia Ruby
“De…dev..D..dd…” Ruby
akalalama
“Ruby !! akaita Mathew
“Devot….” Akasema na
kukohoa akatema damu
“Ruby usiseme
chochote..You’ll be fine.!!
Akasema Mathew
“De…Devoth….aaaa…sh..o..o
t..m..m..eee!! akasema Ruby kwa
taabu.Mathew akahisi kama
nyundo kubwa imetua kichwani
kwake
“Devotha ?!! Mathew
akasema kwa mshangao.
“Dd…” Ruby akataka
kusema lakini akashindwa
fahamu zikampotea.
“Ee Mungu baba nakuomba
mponye Ruby.Bado namuhitaji
sana katika operesheni hii.Nchi
iko katika vitisho vya
mashambulio ya magaidi,watu
wengi watapoteza maisha na
huyu ana msaada mkubwa
katika mapambano haya”
Mathew akaomba kimya kimya
“Kwa nini Devotha ametaka
kumuua Ruby?Japo sijajua
sababu ya kutaka kumuua Ruby
lakini Devotha amekosea
sana.Ruby ni mtu wangu wa
muhimu na yeyote anayemgusa
ananigusa mimi moja kwa
moja.Nitamsaka katika kila
pembe ya dunia na
nitahakikisha ninampata.”
akawaza Mathew na kumsisitiza
Gosu Gosu aongeze mwendo wa
gari kuwahi hospitali.
MPENZI MSOMAJI
- RUBY ATAPONA?NINI
SABABU YA
KUSHAMBULIWA?
DEVOTHA YUKO WAPI?
- MAGAIDI
WATAFANIKIWA
KUMPATA OLIVIA?
- FISHEL NA EHUD
WANAKUJA TANZANIA
KUMTAFUTA OLIVIA
WATAMPATA?
- MPENZI MSOMAJI
USIKOSE SEHEMU IJAYO
 
Kimbembe, aliyekuwa mkurugenz wa idara ya siri ya usalama tyar amekuwa adui
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom