SIRI
Episode 25
Mtunzi Patrick CK
kilichokuwa na vifaa mbali
mbali.Ndani ya chumba kile
kulikuwa na mlango mwingine
akaingiza namba ukafunguka
akaingia katika chumba
ambacho kulikuwa na lifti
akaingia na kuelekea chini
akashuka na kuelekeza jicho
lake katika mlango uliokuwa
mbele yake ukafunguka
akaingia ndani ya chumba
kikubwa cha maabara.Kabla ya
kuingia katika maabara
akaingia katika kichumba
kidogo akavaa mavazi maalum
halafu akaanza kazi. **************
Saa moja za jioni Dr Olivia
akatoka ofisini kwake akaingia
garini na kuondoka.Alihisi
uchovu alikuwa amefanya kazi
kwa muda wa siku nzima
“Mwili umechoka natamani
nifike nyumbani haraka
nikapumzike.Zoezi limekwenda
vyema na ninatumai kesho
kupata majibu.Akili yangu
itatulia baada ya kupata majibu
ya kipimo kile na baada ya hapo
nitajua nini kitaendelea”
akawaza Dr Olivia Alipofika nyumbani kwake
akakuta kuna gari la kifahari
limeegeshwa nje akastuka
“Gari la nani hili? Sina miadi
na mtu yeyote kuja kwangu leo
na sipendi kukaribisha wageni
nyumbani kwangu hasa
usiku”akawaza
“Yawezekana ni baba
amekuja lakini baba hii si
kawada yake.Kama angekuwa
na shida na mimi angenijulisha
tuonane na hana mazoea ya
kuja kwangu bila taarifa”
akawaza Dr Olivia akachukua
mkoba na mafaili yake akashuka garini.Mtumishi wake
wa ndani akatoka haraka kwa
ajili ya kumpokea mizigo
“Lucy hili gari la
nani?Nimekwisha wapa
maelekezo msipokee mgeni
yeyote bila ruhusa yangu kwa
nini mmekiuka maelekezo
yangu? akauliza Dr Olivia
akionekana kuwa mkali kidogo
“Samahani dada ni yule
rafiki yako aliyekurudisha jana
hapa nyumbani ndiye yuko
ndani” akajibu Lucy huku
akipokea mizigo “Rafiki yangu gani?akauliza
Dr Olivia
“Yule aliyekurudisha jana
usiku anaitwa Mathew”
“Oh my Gosh
Mathew!!akasema Dr Olivia na
kushusha pumzi
“Ndiyo dada.Alipokuja
alizuiliwa getini akaomba
niitwe nikaenda nikamueleza
kwamba haupo akasema
atakusubiri.Sikuwa na wasi
wasi naye kwa kuwa jana
ulikuwa naye nikajua ni rafiki
yako.Nilitaka nikujulishe
akasema nisifanye hivyo kwani anataka akufanyie
surprise.Samahani sana dada
sintarudia tena” akasema Lucy
na Dr Olivia akatabasamu
“Usijali Lucy huyu hana
tatizo lakini siku nyingine
usirudie kukaribisha mtu bila
ruhusa yangu.Unapaswa
kuniuliza kwanza kabla
hujafanya maamuzi yoyote”
akasema Dr Olivia na kuingia
“Hello Mr Bilionea”
akasema Dr Olivia alipoingia
sebuleni
“Hello Olivia”akasema
Mathew na kusimama wakashikana mikono Dr Olivia
akajitupa sofani
“Pole sana Olivia.Samahani
kwa kuja bila taarifa lakini jana
hatukuachana
vyema.Nilikuacha ukiwa
umelala haujitambui kwa
kinywaji na sikuwa na namba
yako ya simu ndiyo maana
nimekuja leo ili kujua
unaendeleaje.Nisamehe sana
kwa uvamizi huu” akasema
Mathew
“Usijali Mathew lakini
wakati mwingine
kufanya hivi I don’t like
suprises” akasema Dr Olivia
“It wont happen again”
akasema Mathew
“Karibu sana
Mathew.Ninashukuru jana
ulinifikisha nyumbani
salama.Kama ningeendesha gari
mwenyewe nisingefika salama”
akasema Dr Olivia
“Niliona hali uliyokuwa
nayo ndiyo maana nikaamua
kukuleta nyumbani.Olivia
ninashukuru nimekuona na
kuhakikisha uko salama sasa
ninaweza kuondoka” “Acha kunitania
Mathew.Yaani umepoteza muda
wako wote kunisubiri halafu
nimefika tu unaondoka?
Umekuja kwangu wewe ni
mgeni wangu.Tupate chakula na
maongezi kisha utakwenda
kwako.Unakimbilia wapi wakati
mkeo hayupo ?Au una miadi na
mwanamke leo?akauliza Dr
Olivia
“Hapana sina miadi na mtu
yeyote.Ninakuona umechoka
sana ninataka kukupa nafasi ya
kupumzika” “Hayo ni mawazo yako
mimi sijasema kama
nimechoka.Wait for me
ninakuja baada ya muda mfupi”
akasema Dr Olivia na kupanda
chumbani kwake akaingia
bafuni kuoga na kisha oga
akachukua kompyuta yake na
kumpigia simu Habiba
Jawad.Mawasiliano yao
yamekuwa ni katika mtandao
“Olivia” akasema Habiba
Jawad baada ya kupokea simu
“Madam Habiba habari za
huko? “Tunaendelea vyema vipi
wewe unaendeleaje?
“Ninaendelea vyema
pia.Madam nimekupigia
kukujulisha kwamba jana
nimefika salama na usiku wa
jana nikaanza kazi.Nilifanikiwa
kupata baadhi ya sampuli
kutoka katika kaburi lile la
Edger”
“Wow ! kazi nzuri sana
Olivia.Wepesi wako
umenishangaza sana” akasema
Habiba
“Usijali madam” “Nini kinaendelea baada ya
kuzipata sampuli hizo? Lini
tutegemee majibu ya vipimo?
“Tutegemee kesho
madam.Maabara ile ina uwezo
mkubwa sana na inaweza kutoa
majibu ya vipimo vya vinasaba
kwa siku moja hadi mbili hivyo
tutegemee kesho kupata
majibu”
“Olivia sijui niseme
nini.Nina furaha kubwa na vile
vile nina hofu” akasema Habiba
“Madam habiba sote tuna
hofu kubwa kwani majibu
yatakayopatikana yatatupa picha kamili kuhusu Edger
kama kweli ni mzima au
amefariki dunia” akasema Dr
Olivia
“Dr Olivia tafadhali naomba
uhakikishe kipimo hicho
kimefanyika kwa uhakika
mkubwa sana kwani lengo hasa
la kujenga kituo hicho ni kwa
ajili ya kufanya uchunguzi huo
kwa hiyo kesho ndipo tutajua
kama uamuzi wa ujenzi wa
kituo hicho ulikuwa wa
manufaa” akasema Dr Olivia
“Usihofu Madam
Habiba.Niko makini sana na suala hili na majibu
yatakayopatikana yatakuwa na
uhakika.NImeshughulikia suala
hili mimi mwenyewe” akasema
Dr Olivia
“Ahsante sana Olivia.Mimi
na familia yangu tunasubiri
majibu kutoka kwako kwa
hamu kubwa ili tujue nini
kifuate” akasema Habiba
“Tuombe Mungu majibu
yawe mazuri” akasema Dr
Olivia
“Olivia kila la heri vile vile
endelea kuwa makini sana hasa
kwa wakati huu.Usimuamini mtu yeyote yule.Majibu
yatakapotoka kesho tutaangalia
namna ya kufanya ili uwe na
ulinzi.Tafadhali tuwasiliane
tena kesho” akasema Habiba na
kukata simu.Dr Olivia
akashusha pumzi
“Olivia ..Olivia..Olivia..!!
akasema Dr Olivia akiwa
ameweka mikono kichwani.
“Olivia ninakwenda
kupotea hivi hivi nikiona.Kwa
nini lakini nimekubali kufanya
kazi na hawa watu ?akajiuliza
“I’m not with them.I’m
doing this for Edger! Majibu yakipatikana mimi na wao
hatutakuwa na mahusiano tena
na ikiwezekana hata kituo chao
nitawaachia”akawaza na
kuingiwa na woga
“Nikienda kinyume na
matakwa yao wataniua na
familia yangu.Nifanye
nini?akajiuliza
“I’m confused.Nashukuru
Mathew amekuja atanisaidia
kuyaondoa mawazo haya na
kukiweka sawa kichwa changu”
akasema Dr Olivia na kushuka
sebuleni. “Samahani kwa kukuweka
muda mrefu Mathew ”akasema
Olivia
“Usijali Olivia” akajibu
Mathew
“Mathew nakushukuru
umekuja.I real needed someone
to talk to.The house is big and
boring,ninapotoka kazini
nimechoka ninakosa mtu wa
kuongea naye ndiyo maana
ninaamua kwenda klabu
kupoteza mawazo” akasema Dr
Olivia na Mathew akatabasamu
“Tupate chakula kwanza I
feel hungry !! akasema Dr Olivia na kumuongoza Mathew katika
chumba cha chakula.
Baada ya kupata chakula
wakaelekea katika chumba
maalum cha
kupumzikia.Kulikuwa na sofa
nzuri sana na luninga kubwa
ukutani.Katika ukuta mwingine
kulikuwa na kioo kikubwa
ambaco ndanoi yake maji
yalikuwa yanamwagika na
kutoa sauti nzuri huku muziki
wa ala ukisikika kwa
mbali.Kilikuwa ni chumba cha
kipekee kabisa “Ninapotaka kupumzika
huwa ninakuja humu”akasema
Dr OIivia na kumkaribisha
Mathew halafu akafungua
kabati na kutoa chupa zaidi ya
nane za whisky.
“Mathew let’s have some
fun.Hakuna haja ya kwenda
klabu tunaweza kufurahi hata
hapa nyumbani.Kwa ufupi jana
nilifurahi sana kupata kampani
yako.Wewe ni mtu ambaye kila
mtu angependa kutoka
naye.Unajua namna ya
kumfanya mtu afurahi na
asijihisi mpweke.Mathew mkeo ana bahati sana.U wa kipekee
mno” akasema Dr Olivia
“Olivia nashukuru.Kitu
ulichokihisi kwangu nami
ndicho nilichokihisi
kwako.Nilifurahi sana kuwa
nawe jana.Nilikuwa nimeboreka
na nilitaka kuondoka lakini
baada ya kukutana nawe
nilijikuta nikitamani kuendelea
kuwa nawe hadi tukajikuta
tukikaribia kufika
asubuhi”akasema Mathew na
wote wakaangua kicheko
“Let’s have fun Mathew”
akasema Dr Olivia wakaanza kupata kinywaji.Uwepo wa
Mathew ulimpa faraja kubwa
sana Dr Olivia.Walizungumza
mambo mengi na Dr Olivia
alionekana kuzidiwa kwa
kinywaji akainuka na kumfuata
Mathew sofani.
“Mathew why are you
here?akauliza Dr Olivia.Mathew
akatabasamu akamtazama na
kusema
“Nadhani nilikueleza
kwamba nilikuja hapa kwa ajili
kujua maendeleo yako kwani
jana nilikuacha katika hali
ambayo haikuwa nzuri” “Are you sure Mathew?
“Olivia mbona una wasi
wasi na mimi?Nimefanya vibaya
kuja kukujulia hali?akauliza
Mathew
“Hapana Mathew hujafanya
vibaya.Ninataka kujua hasa nini
kimekuleta kwangu hadi
ukaamua kunisubiri? Akauliza
tena Olivia
“Olivia tayari umezidiwa na
kinywaji nadhani ni wakati wa
mimi kuondoka nikuache
ukapumzike” akasema Mathew
“C’mon Mathew you came
here to have fun so let’s have fun” akasema Olivia akimshika
mkono Mathew
“Usihofu leo tuko nyumbani
hata kama ukizidiwa na kilevi
basi utalala hapa hadi
asubuhi.Mathew samahani
kama swali nililokuuliza
limekukera lakini ninataka
niufahamu ukweli.Kama hauko
tayari kunieleza ukweli ngoja
mimi nikueleze ukweli”
akasema Dr Olivia na kunywa
funda moja la kinywaji
“I saw the way you were
looking at me yesterday.I see
love in your eyes.You like me”akasema Dr Olivia na
kumsogelea zaidi Mathew
“Mathew mimi nina tatizo
moja nalo ni kusema
ukweli.Hata kama unakwepa
kunieleza ukweli lakini
ninakuona
machoni,ninaitazama midomo
yako you like me.You came here
for me.You need me”akasema
Dr Olivia
“Olivia nimekuja hapa
kuk……”akasema Mathew
lakinbi Dr Olivia akamzuia
“Tatizo la wanaume wengi
hamtaki kuwa wazi hata pale mnapoelezwa ukweli.Mathew
ulichokifanya si kitu kibaya
kwani hata mimi nilijiuliza sana
ni namna gani ningeweza
kukupata tena.Ninafurahi kuwa
karibu yako.Ninajihisi furaha na
amani nikiwa karibu
yako.Natamani niwe karibu
yako muda wote.Unanifanya
nifurahi,nitabasamu.Mathew
naamini hautanielewa vibaya
kwa hiki nitakachokueleza
lakini mimi na wewe nataka
tujuane zaidi nataka tuwe
karibu zaidi and for tonight I’m
going to …” Dr Olivia hakumalizia sentensi yake
mikono yenye nguvu ya
Mathew ikamvuta na
kumkumbatia kwa nguvu
akaanza kumporomoshea
mabusu mfululizo.Dr Olivia
naye akajibu kwa busu,taa ya
kijani ikawaka na safari
ikaanzia hapo.Chumba cha
mapumziko kiligeuka sayari ya
mahaba.Walihama kutoka sofa
moja hadi lingine.
“Mathew this is not the
right place.Twende chumbani
kwangu” akasema Dr Olivia
wakatoka mle katika chumba cha mapumziko wakapanda
ghorofani chumbani kwa Dr
Olivia.Wote wawili mahaba
yalikwisha wazidi hivyo
walipofika tu chumbani
hakukuwa na maongezi Mathew
akamshika Dr Olivia na
kumuangusha kitandani
ukaanza mtanange wa kukata
na shoka
“Mathew thank you so
much.I needed this.It’s been a
while” akasema Dr Olivia na
Mathew
akatabasamu.Walimaliza
mzunguko mmoja “Ahsante pia nawe.Naomba
nikiri kwamba ni kweli
nilikufuata hapa nyumbani na
na kilichonileta hapa ni
hiki.Olivia nilipokuona jana
ulinisisimua sana.Nilivutiwa
sana nawe na ninaomba tuwe
na ukaribu mkubwa zaidi”
akasema Mathew
“Nilikuona toka jana
nikayasoma mawazo yako na
nilipokuona hapa leo
sikushangaa nilijua
kilichokuleta na mimi nilikuwa
nakihitaji sana.Mathew naomba
tafadhali usinifikirie vibaya kwa sababu imekuwa rahisi mno
kwangu kujiachia kwako na
sijui imenitokeaje.Mimi ni
mwanamke mgumu sana na
ndiyo maana mpaka leo hii
sijabahatika kuwa na rafiki wa
kiume lakini wewe tumekutana
jana tu na leo hii nipo juu ya
kifua chako.Imenitokea hivyo
na nisingejitendea haki kama
ningekuacha
ukaondoka.Ningejilaumu sana
Mathew” akasema Dr
Olivia.Mathew akaupeleka
mkono katika nywele laini za Dr
Olivia akazichezea na kusema “Olivia katu siwezi
nikakuchukulia rahisi
rahisi.Nitakuheshimu sana na
urafiki wetu nitaupa thamani
kubwa,na ningependa urafiki
wetu uendelee zaidi na zaidi
japokuwa nina familia lakini
haiwezi kuwa kigezo cha
kukuumiza wewe”
“Mathew ninakuhitaji sana
hasa kwa wakati huu.Naomba
usimame na mimi.Ninahitaji
mno mtu wa kunishika mkono
naomba uwe karibu nami japo
kwa muda huu ambao
utakuwepo hapa Dar es salaam.Nimejikuta nikipata
nguvu mpya na tumaini toka
jana nilipokutana
nawe.Sifahamu kwa nini
ninajishi namna hii yawezekana
Mathew kuna kizizi unakitumia”
akasema Dr Olivia na wote
wakaangua kicheko.
“Natania Mathew siamini
kabisa katika mambo hayo
japokuwa wapo
wanaoamini”akasema Dr Olivia
“Dr Olivia nadhani ni
wakati wangu wa kuondoka
nikuache upumzike” “Hapana Mathew leo utalala
hapa hapa utaondoka
asubuhi.You are single and I’m
single shida iko wapi?Kuwa na
amani hapa ni sehemu salama
kabisa.Nakuhitaji usiku wa leo
Mathew.Please stay” akasema
Dr Olivia.Mathew akamtazama
machoni na kusema
“Uko sahihi Olivia.Sina
sababu ya kukimbia kwani niko
peke yangu.Tuufanye usiku
wetu uwe wa kipekee” akasema
Mathew
“Thank you Mathew.Thank
you so much.We need champagne to celebrate our
new beginning ” akasema Dr
Olivia na kuvaa nguo akatoka
mle chumbani akaenda
kuchukua vinywaji.
****************
Saa kumi na mbili za
asubuhi Mathew aliamka
akaoga na kuagana na Dr Olivia
akaondoka zake.
“Ninaapa sijawahi kuwa na
usiku mzuri kama jana.Mathew
ni mwanaume wa pekee
kabisa.Sifahamu imenitokeaje lakini kwake nimejikuta nikiwa
mrahisi mno lakini sijakosea
kwani ananisaidia sana kupita
katika kipindi hiki kigumu
ninachopitia.Nikiwa naye
ninakuwa na amani sana na
tabasamu usoni lakini nikiwa
peke yangu ninajiona kama vile
ninaelekea kwenye kitanzi cha
kuninyonga” akawaza Dr Olivia
baada ya Mathew kuondoka
“Ngoja nimuweke kando
Mathew nijielekeze katika
jukumu kubwa nililo nalo.Siku
ya leo ni siku ya kipekee kabisa
kwani ukweli unakwenda
kujulikana kama Edger kaka
alikufa katika ile ajali au bado
mzima.I’m so scared” akawaza
Dr Olivia akakaa kitandani
akionekana kuwa na mawazo
mengi.Akainuka na kuendelea
kujiandaa.
Alifika ofisini kwake saa
nne za asubuhi na kabla ya
kufanya shughuli yoyote
alijiegemeza kitini
“Ninaogopa kuufahamu
ukweli.Nina wasi wasi maisha
yangu yanaweza yakabadilika
kuanzia siku ya leo.Hii ni siku ngumu sana kwangu” akawaza
Dr Olivia
Alikaa kitini kwa zaidi ya
dakika kumi akiwaza halafu
akainuka
“Sipaswi kuogopa.Natakiwa
kuufahamu ukweli” akasema Dr
Olivia na kuvaa koti lake jeupe
akaelekea katika maabara
maalum
Ilipofika saa kumi na moja
jioni Dr Olivia tayari alikuwa na
majibu.Mwili ulimtetemeka
baada ya majibu kuonyesha
kwamba mwili ule haukuwa wa
Edger.Machozi yakamtoka “He’s alive..!He’s not dead !
akasema Dr Olivia.Alikuwa peke
yake ndani ya maabara ile
kubwa.
“Haya mambo nimekuwa
nikiyaona katika filamu na
sikujua kama siku moja
nitayashuhudia kwa maco
yangu.Kila mtu anajua kwamba
Edger amekufa.Oh my God
where is he?akajiuliza
Ni wazi Dr Olivia alikuwa
katika wakati mgumu sana
baada ya kupata majibu yale.
“Habiba alikuwa sahihi
kuamini Edger hajafa.Naniwaliofanya mchezo
ule na kwa nini?Naamini
waliofanya mchezo ule ni watu
wataalamu mno kwani
walifanikiwa kumuaminisha
kila mtu kwamba Edger
amefariki.Kama Habiba
asingeingiwa na shaka ukweli
usingeweza kujulikana lakini
sasa ukweli umejulikana Edger
hajafa na kinachofuata ni
kutafuta mahala alipo” Akawaza
Dr Olivia akatoka mle maabara
akarejea ofisinikwake na
kumpigia simu Habiba Jawad
kupitia kompyuta yake “Dr Olivia naamini simu hii
ina habari njema” akasema
Habiba
“Madam Habiba tayari
ninayo majibu hapa” akasema
Dr Olivia na Habiba Jawad
akavuta pumzi ndefu
“Nimesubiri kwa muda
mrefu kuufahamu ukweli lakini
sasa majibu yamepatikana
ninapata hofu kuyapokea”
akasema Habiba
“Usiogope Madam
Habiba.Kuwa jasiri na uyapokee
majibu” akasema Dr Olivia “Haya nipe majibu Olivia”
akasema Habiba na kufumba
macho.
“Madam niliingia mimi
mwenyewe katika kaburi lile la
Edger na kuchukua sampuli za
mabaki nilizozihitaji na
nimefanya kipimo mimi
mwenyewe kwa usahihi
mkubwa na majibu yaliyotoka
ni …..” akasita kidogo
“Nieleze Olivia unazidi
kuniweka roho juu”akasema
habiba
“Majibu yanaonyesha
kwamba mwili uliozikwa katika lile kaburi si mwili wa Edger ”
akasema Dr Olivia na Habiba
akafunika uso kwa viganja
vyake vya mikono.Akakaa
kimya kwa dakika mbili na
alipotoa viganja vile uso wake
ulikuwa umeloa machozi.
“Ahsante
Mungu.Nimesubiri kwa muda
mrefu sana kuupata ukweli
huu.Imenigharimu muda na
fedha nyingi kuufahamu
ukwelikwamba mwanangu Seif
hajafa bali yuko hai.Olivia sijui
nikushukuruje kwa jambo hili
kubwa ulilolifanya” akasema Habiba akiendelea kumwaga
machozi ya furaha.
“Madam Habiba baada ya
kuufahamu ukweli kwamba
Edger hajafa nini
kinafuata?akauliza Dr Olivia
“Kinachofuata baada ya
kuufahamu ukweli huu ni
kuanza kumtafuta kila kona ya
dunia kwani mpaka sasa bado
hatujui mahala alipo na nani
anamshikilia.Olivia
ninakushukuru mno na
ninaomba nikuache ili nikutane
na watuwangu nizifikishe
taarifa hizi njema kabisa.Nitawasiliana nawe
baadae” akasema Habiba na
kumuaga Olivia
“Mimi mwenyewe sitaki
kuendelea kukaa hapa kichwa
changu kimevurugika
kabisa.Majibuhaya
yaliyopatikana yamezidi
kunichanganya na kuniongezea
hofu.Nani waliofanya jambo lile
la kuidanganya dunia kwamba
Edger amefariki dunia?Edger
yuko wapi?Watu hao
walifahamu kwamba Edger ni
mshirika wa IS ndiyo maana
wakamteka na kutunga kifo chake? Nitaendelea kujuta
kumfahamu Edger kwa ajili
yake nimejikuta nikiingia katika
ulimwengu wa magaidi ambao
wamenibana katika kona na
sijui nifanye nini,sijui
nimweleze nani jambo hili
ambalo linaelekea kunipa
uchizi.Ninayaona maisha yangu
yakielekea shimoni kwani
naamini ikosiku nitajulikana
kuwa ninashirikiana na
magaidi.Kila ninapowaza jambo
hili ninazidi kuchanganyikiwa”
akawaza Dr Olivia. “Ninamshukuru Mungu
ameniona na kuniletea
Mathew.Ni wakati kama huu
ninamuhitaji sana mtu kama
yule ambaye hunipa nguvu ya
kusimama.Ninahisi
amani,furaha na nguvu nikiwa
naye” akawaza Dr Olivia na
mara gari ziliposimama katika
taa za barabarani akachukua
simu akazitafuta namba za
Mathew akampigia
“Dr Olivia” akasema
Mathew
“Mathew uko wapi mida
hii?akauliza “Nimetoka kazini muda si
mrefu ninaelekea
nyumbani.Wewe uko
wapi?akauliza Mathew
“Mathew kama hutajali
tunaweza kukutana nyumbani
kwangu?akauliza Dr Olivia
“Kuna tatizo lolote Dr
Olivia?akauliza Mathew baada
ya kugundua utofauti katika
sauti ya Dr Olivia
“Ninakuhitaji Mathew”
“Usijali Olivia,ninakwenda
nyumbani kwangu kisha
nitakuja kwako,nisubiri hapo
tafadhali”akasema Mathew “Ahsante sana Mathew”
akasema Dr Olivia na kukata
simu
“I real need someone like
Mathew today.Nahitajimtu wa
kunipa nguvu kwa sababu
mambo yanayonikabili ni
mazito” akawaza Dr Olivia
Alifika nyumbani kwake na
kujilaza kitandani kichwa
kilikuwa kizito
“Nimeingia kwenye
ulimwengu wa magaidi na sijui
namna ya
kutoka.Nimeikamilisha kazi yao
na sitaki kuendelea kushirikiana nao tena hawa
jamaa lazima nitafute namna ya
kuwakwepa.Hata hivyo duniahii
ina maajabu sana.Mwili ule
ambao watu wote tuliamini
ulikuwa wa Edger ni wa nani?
Haya aya mambo ni magumu
sana na sitakikuendelea
kuumiza kichwa changu zaidi”
akawaza Dr Olivia na kuingia
bafuni kuoga kisha akajilaza
kitandani akimsubiri Mathew.
Saa moja na nusu Mathew
akafika nyumbani kwa Dr Olivia
ambaye alifurahi sana kumuona
akamkumbatia kwa nguvu “Mathew nimefurahi sana
umekuja.Kila nikuonapo
ninapata nguvu” akasema Dr
Olivia na kumuongoza Mathew
wakaenda kukaa nje sehemu
maalum ya kupumzikia,Olivia
akaleta chupa kadhaa za
mvinyo
“Olivia toka tumefahamiana
juzi umekuwa unatumia sana
kinywaji.Inaonekana kuna
jambo linakusumbua na
unataka kuliondoa kichwani
kwako kwa kutumia
kilevi.Unaweza ukanieleza una
tatizo gani Olivia?You can trust me,Im here for you” akasema
Mathew
“Sina tatizo lolote Mathew
nahitaji tu
kufurahi.Ninaonekana kama
nina tatizo
linanisumbua?akauliza Dr
Olivia
“Ninajua kumsoma mtu
hasa ambaye ana jambo
linamsumbua na japokuwa
hutaki kuniweka wazi lakini
naamini kwamba
unalotatizo.Nataka nikuelekeze
kitu Dr Olivia,siku zote kama
una tatizo usilitatue kwa
kunywa pombe.Njia hiyo
kamwe haitakusaidia kutatua
tatizo lako.Sikulazimishi
unieleze tatizo lako kwanini
muda mfupi tu umepita toka
tumefahamiana lakini kama
hutajali unaweza ukaniamini na
kunieleza kinachokusumbua”
akasema Mathew.
“Mathew hayoni mawazo
yako,sina tatizo lolote
linalonisumbua” akasema Dr
Olivia huku akichukua chupa ya
mvinyo na kutaka kuimimina
katika glasi Mathew akamzuia “Olivia hakuna kutumia
mvinyo leo.Today let’s have fun
without alcohol.Kamauna tatizo
tulitatue bila kutumia kilevi
chochote” akasema Mathew
“Mathew sina tatizo lolote
linanisumbua.Tutumie mvinyo
tafadhali”akasema Dr Olivia
“Hapana Olivia.Leo hakuna
kutumia mvinyo.Si mazoea
mazuri kutumia mvinyo kila
siku.Tuzungumze na kama
kunakitu ambacho kinatufanya
tufurahi basi tufanye lakini si
kugeuza mvinyo sehemu ya
maisha yetu” “C’mon Mathew siwezi
kuwa kawaida kama sintatumia
hata mvinyo kidogo” akasema
Dr Olivia
“Hap…………” Mathew
akanyamaza baada ya simu ya
Dr Olivia kuita.Akatazama
mpigaji na sura yake
ikabadilika.
“Is there any problem
Olivia?akauliza Mathew
“Mathew I have to take this
call” akasema Dr Oliviana
kuelekea ndani.
“Hallow madam Habiba”
akasema Dr Olivia baada ya kuipokea simu ile ambayo
ilipigwa kupitia mtandao wa
skype.
“Dr Olivia nimefikisha
majibu yale kwa wenzangu na
wote wamefurahi sana kwamba
zile hisia zetu kuhusu Edger
kuwa hai ni sahihi
kabisa.Kinachofuata sasa ni
hatua ya tatu ambayo ni
kumtafuta Edger yuko
wapi.Katika hatua hii ya tatu
utakuwa ukiwasiliana na Sayid
Omar yeye ndiye
niliyemkabidhi jukumu lote la
kuhakikisha Edger anajulikana yuko wapi na anapatikana kwa
gharama zozote zile.Olivia
ninakushukuru sanakwa jambo
kubwa ulilolifanya la kuamua
kushirikiana nasi naomba
uendelee kuwa nasi na
ninakuahidi kwamba lazima
Edger atapatikana kwa gharama
zozote.Ninachokusisitiza Olivia
ni usiri.Endelea kuitunza siri
uliyoifahamu hata kama
itakulazimu kuhatarisha maisha
yako lakini siri uliyoifahamu
katu usifumbue mdomo na
kumweleza mtu yeyote”
akasema Habiba “Madam Habiba
tumekwisha wekamakubaliano
na ninaomba makubaliano yetu
muyazingatie na mara tu baada
ya Edger kupatikana utakuwa ni
mwisho wetu mtaniacha
niendelee na maisha yangu”
“Usiogope tutalizingata hilo
Olivia.Mimi ni mtu
ninayeheshimu sana
makubaliano.Naomba sasa
uzungumze na Sayid Omar na
atakupa maelekezo” akasema
Habiba Jawad na katika simu
akatokea mtu mmoja mwenye
kipara na miwani “Hallow Olivia.Naitwa sayid
Omar na kama alivyokuelekeza
Habiba katika awamuhii ya tatu
utakuwa na mimi.Katika awamu
ya kwanza ulikuwa na Abu
dahir,awamu ya pili ukawa na
Habiba na sasa ni awamu ya
tatu ambayo utakuwa na
mimi.Awamu hii imegawanyika
katika sehemu mbili.Sehemu ya
kwanza ni kufahamu nani
waliomchukua Edger na yuko
wapi.Sehemu ya pili itakua ni
kumchukua mahala
alipo.Mpaka sasa hatuna
uhakika ni nani waliofanya mchezo ule na kumchukua
Edger.Nipe muda hadi kesho
asubuhi kwa saa za kwenu
Tanzania nitakupigia simu na
kukueleza ni wapi tunahisi yupo
Edger” akasema Sayid Omar na
kuagana na Dr Olivia ambaye
alihisi miguu inamuisha nguvu
akakaa kitandani
“Ee Mungu kwa nini
umeniacha nikaingia katika
mtihani huu? Nimeingia katika
himaya ya magaidi,himaya ya
watu makatili,wauaji na sioni
mlango wa kutokea.Nionyeshe
njia ee Mungu niweze kujitoa katika mikono ya watu hawa”
akaomba Dr Olivia akilengwa na
machozi
“Kama watafanikiwa
kumpata Edger utakuwa ni
mwisho wa mahusiano yangu
naye.Sitaki kuwa na ukaribu
wowote na hawa magaidi”
akawaza Dr Olivia na
kukumbuka kwamba alimuacha
Mathew peke yake akatoka na
kurejea mahala alipokuwa
Mathew
“Mathew tafadhali naomba
uniruhusu ninywe glasi hata
moja tu ya mvinyo ili kichwa
changu kikae sawa.Bila kupata
mvinyo nahisi kichwa changu
kitapasuka” akasema Dr
Olivia.Mathew akamtazama na
kuchukua chupa akamimina
mvinyo katika glasi.Olivia
akaishika glasi ile na kunywa
pombe yote iliyokuwemo.
“Oh my God !! akasema Dr
Olivia
“Olivia nieleze tatizo lako
tafadhali.You can trust me”
akasema Mathew.Dr Olivia
akainamisha kichwa akazama
mawazoni “Olivia mimi ni rafiki yako
na kama tumeamua kuwa
marafiki hakuna haja ya
kufichana kama una jambo
kubwa nieleze tafadhali
yawezekana nikawa na msaada
kwa tatizo lako” akasema
Mathew.
“Hata kama nikikueleza
Mathew hautaweza
kunielewa”akasema Dr Olivia
“Usiogope Olivia nieleze
nitakuelewa” akasema Mathew
“Nina tatizo kubwa sana
Mathew na ninahitaji msaada wa Mungu pekee kulitatua”
akasema Dr Olivia
“Olivia pole sana kwa tatizo
ulilonalo lakini bado naendelea
kukusisitiza unieleze tatizo lako
kwani yawezekana Mungu
amenituma kwako ili niwe
msaada wa tatizo ulilo
nalo.Usiogope Olivia hata kama
tatizo ni kubwa kiasi gani
nieleze na mimi nitakuelewa”
akasema Mathew.Dr Olivia
akafikiri kidogo na kusema
“Hapana Mathew siwezi
kukueleza.Tatizo nililo nalo nitalikabili mimi mwenyewe na
kulimaliza”akasema Dr Olivia
“Olivia kuna maana gani ya
kuwa marafiki kama hatuwezi
kushirikishana matatizo
tunayopitia?Urafiki maana yake
ni kushirikishana kila tatizo na
kusaidiana.Kama rafiki yako
niko tayari kukusaidia katika
matatizo yote uliyonayo”
akasema Mathew
“Mathew sitaki kukuingiza
katika matatizo.Nitakabiliana
nao mimi mwenyewe” akasema
Dr Olivia “Utakabiliana na akina
nani? Are you in trouble with
some people? akauliza Mathew
“Mathew umenichanganya
hadi nimejikuta nikitamka kitu
ambacho sikupaswa
kukitamka”akasema Dr Olivia
“Niambie ukweli Olivia uko
katika matatizo na watu gani?
Dr Olivia akainamisha
kichwa akafikiri halafu akasema
“Mathew sipendi
kukushirikisha katika tatizo
langu lakini kwa kuwa
umesisitiza nitakueleza kwa ufupi tu.Ni kweli nina tatizo na
watu Fulani”
“Matatizo gani? Ni akina
nani?Mathew akauliza
“Usihofu Mathew ni jambo
ambalo ninaweza kulimaliza na
ninajitahidi kulimaliza.Endapo
nikishindwa kulitatua na
kuhitaji msaada
nitakujulisha.Naomba nisiingie
kwa ndani zaidi” akasema Dr
Olivia
“Nimekuelewa Dr Olivia na
ninakuomba kama ulivyoahidi
kwamba endapo utashindwa kutatua tatizo lako mimi niko
hapa tayari kukusaidia”
“Ahsante
Mathew.Nikishindwa
nitakutafuta” akasema Dr Olivia
“Olivia umeahdi kunitafuta
pale utakapohitaji msaada
wangu lakini mimi ninapenda
kukupa msaada mdogo sana”
“Msaada upi Mathew?
“Nitakupa namba ambazo
unatakiwa uziweke kichwani na
utazitumia pale tu unapokuwa
matatizoni.Ukipiga namba hizo
zitaniwezesha mimi kujua pale
unapokuwa na matatizo.Narudia tena kukupa
angalizo kwamba namba hizi si
za kutumia hovyo hadi pale
utakapokuwa umepata
matatizo.Namba hizo ni kirusi
ambacho kinaweza kuchota
taarifa kwa haraka na
kunijulisha mahala ulipo na
mimi nikatafuta msaada namna
ya kukusaoid” akasema Mathew
“Umewahi kusomea mambo
haya ya teknolojia?Kirusi hicho
kinakusaidia nini
Mathew?akauliza Dr Olivia
“Nina utaalamu kidogo wa
haya masuala.Kirusi hiki
kinanisaidia kwa familia yangu
kujua kama wako katika
hatari.Kuna wakati mwanangu
mmoja aliwahi kutekwa ndipo
nilipoamua kutumia njia hii
kujua kama wako kwenye
matatizo”akasema Mathew na
kumtajia Dr Olivia namba zile
akazihifadhi kisha wakaendelea
na maongezi mengine.walipata
chakula cha usiku na ilipofika
saa tano Mathew akaaga ili
aondoke lakini Dr Olivia akawa
na ombi
“Mathew naomba
usinichoke tafadhali.Ninaomba na usiku wa leo uupitishe hapa
kwangu.Ninakuhitaji sana
Mathew” akasema Dr
Olivia.Haikuwa rahisi kwa
Mathew kukataa.